Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Nape Nauye Asema TBC Haitarusha 'Live' Matukio Ya Bunge Kuanzia Leo ili Kubana Matumizi

$
0
0

MWENYEKITI wa Bunge, Andrew Chenge leo ameahirisha bunge mara mbili kutokana na mvutano ulioibuka baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuomba bunge liahirishe kujadili hotuba ya rais na badala yake wajadili kuzuiwa kwa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) kurusha matangazo ya moja kwa moja.
 
Kabla ya kuahirishwa kwa bunge, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye aliwasilisha taarifa ya serikali kulieleza bunge kwamba, serikali imesitisha huduma ya matangazo ya moja kwa moja kupitia TBC.

Kutokana na taarifa hiyo, Zitto alisimama na kuliomba bunge kusitisha shughuli za kuendelea kujadili hotuba ya rais ambayo ilianza kujadiliwa jana ili kutoa fursa kujadiliwa hatua ya serikali kuzuia haki ya wananchi kupata matangazao ya moja kwa moja kupitia televisheni hiyo.

Hata hivyo, Chenge alianza kuonesha nia ya kutaka kuzima hoja ya Zitto lakini wabunge wa upinzani kwa umoja wao waliungana na Zitto katika kushikilia msimamo wa kujadiliwa suala la TBC kabla ya kuendelea na mjadala wa hotuba ya rais.

Yalisikika maneno kama ‘usituburuze, mtemi, hapa hakuna kuburuzana’ huku wabunge wengine wakipiga kelele kuashiria kuunga mkono hoja ya Zitto.

Kutokana na mvutano huo, Chenge alilazimika kuagiza kamati ya uongozi kukutana ili kujadili taarifa hiyo na baadaye kuwasilisha kulichojadiliwa na kamati hiyo.

“Naipa kamati saa moja,” alisema Chenge jambo ambalo lilipokelewa kwa mikono miwili na upinzani. Baada ya kauli hiyo mwenyekiti huyo aliahirisha bunge kwa saa moja.

Hata hivyo, baada ya bunge hilo kurejea tena baada ya kupita saa moja , Chenge aliahirisha tena bunge kwa kuwa, kamati ilikuwa haijamaliza kujadili.

Wakati akizungumza bungeni wakati wa kuwasilisha kauli ya serikali Nape alisema,“naomba kutoa kauli ya serikali kuhusu TBC kutangaza moja kwa moja vikao vya majadiliano ya bunge.”

TBC ilianza kurusha moja kwa moja matangazo ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005. Kabla ya kuanza kurusha moja kwa moja, TBC wakati huo televisheni ya taifa ilikuwa inarekodi matukio yote ya bunge na kurusha usiku katika vipindi maalumu vilivyojulikana kama bungeni leo kwa maana ya yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika.

Hata hivyo Nape alisema “baada ya kuanza kwa utaratibu wa kuanza kurusha matangazo moja kwa moja mwaka 2005, gharama za kufanya kazi hio zimekua zikipanda kwa kasi hadi kufikia Sh. 4.2 bilioni kwa mwaka kwa maana ya mikutano minne ya bunge.

“Shirika limekuwa likigharamia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo madogo ya biashara, ifahamike kuwa asilimia 75 ni vipindi vingi vinavyolenga kutoa elimu kwa umma na asilimia 25 ni burudani.”

Nape amesema, kutokana na hali hii, TBC imeona ni busara kubadilisha mfumo wa utangazaji wa shughuli za bunge ili kukabiliana na kupanda kwa gharama za uendeshaji.

Amesema TBC imeona ni busara kuanzia mkutano huu wa bunge iwe inarusha baadhi ya matangazo ya bunge moja kwa moja yaani ‘live’ ikiwa ni njia ya kubana matumizi.

Amefafanua kuwa,“chini ya utaratibu huu, TBC itahakikisha kuwa, baadhi ya matukio ya matukio ya bunge yatarushwa moja kwa moja na mengine kurekodiwa na kuandaliwa kipindi maalum kitakachoitwa leo katika bunge.

“Kipindi hiki kitakua na mambo yote muhimu yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika. Kipindi hichi kitakuwa kinarushwa kuanzia saa nne usiku hadi saa tano usiku.”

Serikali Yasema Mawaziri Wakuu Waliokihama Chama cha Mapinduzi (LOWASSA na SUMAYE ) Wataendelea Kulipwa Pensheni Zao Kama Kawaida

$
0
0

Serikali imesema leo kuwa mawaziri wakuu waliokihama Chama cha Mapinduzi (CCM) wataendelea kulipwa pensheni zao kwa mujibu wa sheria ya nchi.

Mawaziri wakuu hao; Fredrick Sumaye na Edward Lowassa walihama CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema)na badaye Lowassa aligombea urais chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akijibu maswali ya baadhi ya wabunge waliohoji endapo watu waliokuwa katika nyadhifa hizo wanaweza kuzuiwa kuchukua pensheni zao kwa kuhamia upinzani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma, Angellah Kairuki amesema sheria haizuii kwa kuwa kuhama chama ni haki ya kikatiba.

Akinukuu Sheria ya mwaka 1999 pamoja na ile ya mwaka 2005 ya Utumishi wa Umma, Kairuki amesema waliokuwa viongozi katika nyadhifa hizo wana haki ya kuendelea kupata stahiki hizo kisheria.

Hata hivyo ameonya kuwa, wanapaswa kuheshimu sheria ya nchi inayowazuia kutoa siri za nchi wakati wakiwa katika nyadhifa zao.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, amesema uchumi ukiimarika utaisaidia serikali kuwalipa wastaafu pensheni itakayokidhi mahitaji yao.

Serikali Yaahidi Kuendelea Kushusha Kodi kwa Wafanyakazi

$
0
0

Serikali imesema imeadhimia mwaka wa fedha wa 2016/2017 kushusha kiwango cha tozo la kodi kwa mfanyakazi kutoka asilimia 11 ya hivi sasa hadi kufikia asilimia 10 kwa mwaka huo wa fedha.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo bungeni ambapo amesema kuwa lengo la serikali ni kushusha zaidi hadi kufikia digiti moja.

Waziri Kijaji ameongeza kuwa baada ya kufikia asilimia 10 ya tozo la kodi hiyo serikali itakaa na wadau ikiwemo vyama vya wafanyakazi ili kutafuta ufumbuzi wa ni namna gani wanaweza kushusha zaidi kutokana na ukuaji wa uchumi siku hadi siku.

Katika hatua nyingine waziri Kijaji amesema kuwa serikali imedhamiria kupandisha kiwango cha pensheni kwa wazee wastaafu hadi kufikia shilingi laki mbili na nusu kadri ya uchumi utakavyoimarika na mikakati tayari imeshaanza kuandaliwa.

Serikali Kuanzisha Vyuo vya vya Uvuvi Kuongeza Ujuzi kwa vijana

$
0
0

Serikali imekusudia kuanzisha Vyuo vya Uvuvi katika maeneo yote yanayozungukwa na bahari ili kuwafundisha vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kuwawezesha kukuza vipato vyao kwa kujiajiri.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma  na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.William Tate  Ole Nasha akijibu swali la Mhe. Hamidu Hassan Bolali Mbunge wa Mchinga (CUF) kuhusu umuhimu wa kujenga chuo cha uvuvi mkoani Lindi ili kuwaongezea vijana ujuzi wa kazi hiyo.

Ameongeza kuwa wizara inatambua umuhimu wa kuwafundisha vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za uvuvi kilimo na ufugaji  na kwa sasa wizara kupitia Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvivu (Fisheries Education and Training Agency (FETA) imeanzisha Chuo cha Uvuvi Mikindani Mtwara kwa lengo la kusogeza huduma ya mafunzo ya uvuvi kwa wananchi hususani vijana walioko ukanda wa kusini mwa Tanzania ukiwamo mkoa wa Lindi.

Mhe.William Tate Ole Nasha amesema uanzishwaji wa Vyuo vya Uvuvi sio kwa maeneo yanayozungukwa na bahari ila kwa maeneo mengine pia ili kuwezesha vijana kupata ujuzi zaidi sio katika uvuvi pekee bali pia katika kilimo na ufugaji

Mbali na Chuo cha Uvuvi Mikindani  Mtwara pia kuna vyuo vingine kama vile Chuo cha Mbegani Mtwara  chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 , Chuo cha Kibilizi Kigoma na  Chuo cha Nyegezi Mwanza.

Mbali za Vyuo hivyo serikali imehaidi kujenga vyuo Tanzania nzima ili kuwawezesha vijana  wengi zaidi kupata kupata ujuzi zaidi katika Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ili kuendeleza ukuaji wa sekta hiyo na kuwezesha vijana kujiajiri wenyewe kupitia mafunzo wanayapata.

Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) itaanza kutoa mafunzo ya uvuvi katika Chuo cha Uvuvi Mikindani ya muda mfupi kwa mwaka 2016/2017 na yale ya Astashahada na Stashahada yataanza mwaka 20017/2018.

Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi Yakanusha Kujihusisha na Biashara ya Kusafirisha Wahamiaji Haramu

$
0
0

Idadi ya Raia wa kigeni kutoka nchini Ephiopia waliokuwa wakisafirishwa na Gari la magazeti la kampuni ya Mwananchi Communication Ltd imefikia 12 baada ya wengine 4 kukamatwa Jioni wakiwa Eneo la Kibwabwa  mjini Iringa wakiwa wamefichwa porini.
 
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Peter Kakamba amesema kuwa tayari ametuma usafiri kwenda kuwabeba Raia hao ambao wanadai walishushwa katika gari hilo aina ya Hiace ili kuvuka eneo la ukaguzi wa Magari ( check pointi)  kijiji cha Igumbilo nje kidogo ya mji wa Iringa.

Wakati huo huo Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL)  imetoa ufafanuzi kuhusiana na kuhusishwa na kadhia hiyo. Soma zaidi:

Vurugu zaibuka, Wabunge wa Upinzani watimuliwa Bungeni

$
0
0
Hali ya Sintofahamu imetawala Bungeni jioni hii kufuatia wabunge wa Upinzani kupinga TBC kusitisha kurusha live matangazo ya moja kwa moja kuanzia jana kwa kigezo cha kubana matumizi.

Kutokana na vurugu hizo, Polisi wamelazimika kuingia Bungeni na kuwatoa nje wabunge wa Upinzani kufuatia kugoma kutokana na maagizo ya Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge, Andrew Chenge.

Chanzo cha vurugu hizo  ni  Wabunge wa Upinzani kupinga kuendelea kwa mjadala wa Bunge wakitaka kauli ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuhusu TBC kusitisha kurusha matangazo ya moja kwa moja toka Bungeni  ijadiliwe kwanza.

Sakata hilo liliibuka tangu asubuhi ambapo Mwenyeki wa Bunge, Andrew Chenge aliahirisha Kikao cha Bunge mara mbili huku akiitaka kamati ya uongozi kukutana  ili kutoa majibu.
 
Maamuzi ya kamati ya uongozi  
Baada ya Bunge kurejea jioni hii mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge ameliambia Bunge kuwa maamuzi ya kamati ya uongozi baada ya kuketi mchana wa leo ni kama ifuatavyo.

(a) Mwenyekiti wa Bunge alikuwa sahihi kutaka hoja iliyokuwa mbele ya Bunge kuhusu hotuba ya Rais iendelee.

(b) Hakuna haki yoyote ya Bunge iliyovunjwa kwa Bunge kuendelea na kazi yake baada ya hoja ya Waziri

(c) Hoja ya Bunge iliyo mbele ya Bunge ni hotuba ya Rais na kamati ya uongozi imeagiza shughuli ziendelee kama kawaida.

(d) Endapo kuna Mbunge yoyote ambaye hataridhika atumie kanuni ya 5 (4) kuomba kibali kwa katibu wa bunge ili apate nafasi maalumu.

Aidha kwa mujibu wa ratiba ya kikao cha Bunge ni kwamba Bunge litajadili hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 Novemba 20, 2015 kwa muda wa siku 3. Baada ya kauli hii, vurugu ziliibuka Bungeni
 
Wabunge  wa  Upinzani walianza kupiga mayowe, ikiwemo kuimba nyimbo mbalimbali suala lililomlazimu Mwenyekiti kuwaondoa Wabunge wa Ukawa wote watoke nje ili wabunge wengine waendelee na kikao cha kujadili hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Wabunge wa CCM wako Bungeni wanaendelea na kikao cha Bunge 

Dr. Saleh Kutoka Kisiwani Lamu… Bingwa Wa Kisomo, Anaye Fanya Miujiza Mikubwa Kwa Kutumia Vitabu Kutoka Misri Na India.

$
0
0

MWANDISHI :  MUNGWA  KABILI……………………… SIMU NAMBA 0744  000  473
Kila  mwanadamu  anaye kuja  duniani, huja  akiwa  na  karama  aliyo tunukiwa na  Mwenyezi  Mungu.

Mungu ametuleta  duniani  ili  tuweze  kushirikiana, kusaidiana  na  kutegemeana.
 
Jambo  hili  lisingewezekana  kama  watu  wote  tungekuwa  na  karama  zinazo  fanana  ama  kulingana.
 
Ili  kufanikisha  lengo  lake  hilo  TUKUFU, Mwenyezi  Mungu  ametoa  karama  tofauti  tofauti  kwa  watu  tofauti  tofauti.
 
Katika  karama  zote  zitolewazo  na  Mwenyezi  Mungu  kwa  wanadamu,   KARAMA  iliyo  KUU  kuliko  karama  zote  ni   KARAMA  YA  KUTATUA  MATATIZO  YA  WANADAMU.. Hasa  hasa  yale  yaliyo  nje  ya  uwezo  wa  kibinadamu.
 
Karama  hii  ni  karama  kuu  kuliko  zote  kwa  sababu  ni  karama  inayo  muhusisha  Mwenyezi  Mungu  moja  kwa  moja.
 
Kazi  ya  kutatua  matatizo  ya  wanadamu  ni  kazi  ambayo  ilitakiwa  kufanywa  na  Mungu  mwenyewe  moja  kwa  moja.
Lakini  kwa  kuwa  Mungu  anataka  wanadamu  tushirikiane  na  kutegemeana,  ametunuku  karama  hii  kwa  wanadamu  wachache ili  wapate  kufanya  kazi  hiyo  ya  Mungu. Kazi  ya  kutatua  matatizo  ya  wanadamu  yaliyo  nje  ya  uwezo  wao.
 
Kwa  lugha  nyingine  ni  sawa  na  kusema,  Mungu  mwenyewe  anatatua  matatizo  ya  wanadamu kwa  kuwatumia  wanadamu  wengine…

Dr. Saleh  kutoka   visiwa  vya  Lamu, vilivyopo  katika  pwani  ya  nchi  jirani  ya  Kenya,  ni  miongoni mwa  wanadamu  walio  tunukiwa  na  kujaaliwa  karama  kuu  ya  utatuzi  wa  matatizo  mbalimbali  ya  wanadamu.
 
Dr. Saleh  ambaye  pia  hujulikana  kama  KUN FAYA  KUN  yaani  KUWA  NA  IWE,  ni  chotara  wa  KIARABU  na  KIAJEMI  (  Waajemi  ni  watu  kutoka  nchi  ya  Iran  ) ambae  amerithishwa  UGANGA na  babu  yake  kizaa  baba  yake…
 
Upande  wa  baba  yake  ni  waarabu  wakaazi  wa  Lamu na Malindi  nchini  Kenya, ambao  wana  asili  ya  Omani, wakati  kwa  upande  wa  mama  yake  ni  wapemba  kutoka  jamii  ya washiraz  wenye  asili  ya  Irani.
 
Dr. Saleh  amesoma  na  kubobea  kwenye   ELIMU  YA  KORAN.  Alianza  kujifunza  elimu  ya  Koran  akiwa  kisiwani  Unguja  wakati  huo  baba  yake  akiwa  anafanya  kazi ya  kufundisha  Koran kwenye  madrasa.
 
Baadaye  aliendelea  na  elimu  ya  juu  ya  Koran  kisiwani  Lamu  Kenya, kisha  Khartoum  Sudani, Timbuktu Mali  na  hatimaye  nchini  Misri  ambako  alipata  elimu  ya  juu  kabisa  katika  Koran.
 
Dr. Saleh  amerithi  uganga  kutoka  kwa  babu  yake  kizaa  baba  yake.
 
Dr. Saleh   amebobea  katika  elimu  ya  majini  na  mashetani wa  ardhini, angani  na  baharini.
 
Anatumia  uganga  kutoka   Misri, India, Irani   katika  kutatua  matatizo  mbalimbali  ya  wanadamu.
 
Anatumia  uganga  wa  KISUMERIA  katika  kutatua  matatizo  mbalimbali  ya wanadamu.
 
Amebobea  katika  UGANGA  na  UGANGUZI   kutoka  katika  makabila  yote  ya  kiarabu kuanzia Wa  Banu Abas  hadi   WaBanu  Zayd.

MAMBO   ANAYO   YAFANYA  SHEIKH  SALEH.
i. Anatoa  PETE  ZA  MAJINI  na  PETE  ZA  BAHATI  kwa  watu  wenye  matatizo  na  mahitaji  mbalimbali.
ii.Anasaidia  katika  masuala  ya  uongozi
iii.Anafanya  matambiko  maalumu  kwa  wachimbaji  wa  madini.
iv. Anatoa  dawa  na  pete  za  biashara
v. Anasaidia  kumrudisha  mke  au  mume  aliye  kimbia  pamoja  na  masuala  yote  yanayo  husu mapenzi  na  mahusiano.
vi.Anasaidia  kutoa  pete  za  utajiri  kwa  wanao  taka  utajiri.
vii.Kama  unataka  kuuza  nyumba, gari, shamba, kiwanja  au  mali  yako  yoyote, atakusaidia  kupata  mteja  wa  uhakika  kwa  haraka  sana.
viii.Kama  una  shida  ya  kuto  kupata  ujauzito, atakusaidia  kushika  mimba.
ix.Kama  umerogwa  au  umetupiwa  jinni  , Sheikh  Saleh  atakusaidia
x. Kutoa  nuksi,mikosi  na  uchawi  tumboni.
xi. Anatoa  kinga  ya  nyumba, gari  na  mashamba.
xii. Anatoa  dawa  ya  kuwakinga  watu  na  ajari
xiii. Anatoa  kinga  dhidi  ya  wachawi
xiv. Kurudisha  mali  iliyo  potea
xv. Kumuita  ndugu  aliyepotea
xvi.Kama  umedhulumiwa, Sheikh  Saleh  atakusaidia kurudisha  mali  yako.
xvii.Kama  umesingiziwa  kesi, Sheikh  Saleh  atakusaidia  na  kesi  yako  itafutwa  mara  moja.
xviii.Kama  umebambikiwa  kesi  kazini, Sheikh  Saleh, atakusaidia  na  kesi  yako  itafutwa  mara  moja.
xix. Anatoa  pete  za  kukukinga  dhidi  ya  adui  zako.
xx.  Anatoa  hirizi  ya  simba
xxi. Anaendesha  kituo  maalumu  cha  dua, ambapo  watu  wenye  shida, tabu  na  matatizo  mbalimbali  hufika  kwa  ajili  ya  kuombewa  dua.
Pamoja  na  na  matatizo  mengine  mengi  yanayo  muhusu  mwanadamu
 
MAHALI   ANAKO  PATIKANA  SHEIKH  SALEH
Shughuli  zake  nyingi  anazifanyia  Nairobi  na  Mombasa  nchini  Kenya. Lakini  kutokana  na uwezo  wake  mkubwa  wa  kutatua  shida  za  watu amekuwa  akisafiri  mara  kwa  mara  katika  nchi  tofauti  tofauti. 

Nchi  anazo  safiri  kwa  ajili  ya  kazi  zake ni  pamoja  na  Msumbiji, Jamhuri  ya  Kidemokrasia  ya Kongo, Gabon, Oman,  Tanzania  Bara  na  Visiwani, United  Arabs  Emirates, Visiwa  vya  Comoro, Misri, Afrika  Kusini, Algeria, Uingereza  na  Marekani  kwa  kutaja  nchi chache.
 
Kwa  sasa  yupo  jijini  Dar  Es  Salaam, ambapo atakaa  kwa  muda  wa  wiki  mbili  kwa  ajili  ya kuwasaidia  watu  mbalimbali  wenye  shida  na  matatizo  mbalimbali.Baada  ya  hapo, Sheikh  Saleh  ataelekea  nchini  Msumbiji, kwa  mwaliko  wa  wachimba  madini.

MAKALA  HAYA  YAMEANDIKWA  NA   NDUGU. MUNGWA  KABILI. MUNGWA  KABILI. NI  MWANDISHI  NA  MTAFITI   KUHUSU  MASUALA  YA    ULIMWENGU  USIO  ONEKANA.  ANAPATIKANA  JIJINI  DAR  ES  SALAAM, KWA  NAMBA   0744  000  473

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Januari 28


Serikali ya Zanzibar Yasema Uchaguzi wa Marudio Utakuwa Huru na Wa Haki

$
0
0
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema imejipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa marudio utakaofanyika Machi 20, mwaka huu unakuwa huru na haki kwa kupambana na makundi ya aina ya watu mbalimbali wanaokusudia kufanya fujo ikiwemo kuwazuia wenye sifa wasipige kura.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud wakati alipozungumza na watendaji wa Serikali wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa na baadhi ya vikosi vya ulinzi mjini Chake Chake, Pemba.

Alisema zipo taarifa kwamba kipo kikundi cha watu kimeandaliwa kwa ajili ya kufanya vurugu katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu, ikiwemo kuwazuia watu washindwe kwenda kupiga kura kwa malengo ya kisiasa zaidi.

Aboud alisema, Serikali haiwezi kuvumilia watu wa aina hiyo pamoja na vitendo hivyo ambavyo vinakwenda kinyume cha demokrasia ya mfumo wa vyama vingi inayotoa fursa zaidi kwa watu kushiriki katika Uchaguzi Mkuu kwa kuwachagua viongozi wanaowataka.

“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejizatiti kuhakikisha kwamba wananchi wote wenye sifa ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa marudio wanatimiza azma ya kidemokrasia ya kupiga kura na vitendo vya kihuni vyenye lengo la kusababisha fujo na vurugu kamwe havina nafasi,” alisema Aboud.

Alifafanua zaidi kuwa chama ambacho hakipo tayari kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa marudio hakina sababu ya kuanza kuweka mikakati ambayo itasababisha watu wengine kushindwa kutekeleza malengo ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wanaotawaka kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Alisema, vipo viashiria vya vitendo vya vurugu na fujo vimeanza kujitokeza hivi sasa kwa baadhi ya watu kuandika vikaratasi vyenye muelekeo wa kuleta uchochezi wa kisiasa pamoja na mtizamo wa kuwagawa wananchi wa visiwa viwili vya Unguja na Pemba.

Aboud alisema msimamo wa serikali tayari umetangazwa kupitia Tume ya Uchaguzi ya kufanya uchaguzi wa marudio Machi 20, baada ya ule wa Oktoba 25, mwaka jana kufutwa baada ya kujitokeza kwa kasoro mbalimbali.

Alisema ni wajibu wa vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi wa Oktoba 25 kushiriki tena katika mchakato huo ambao ndio halali utakaowafanya wananchi kupata viongozi wao kwa njia ya kidemokrasia ya uchaguzi.

“Msimamo wa Serikali ya Mapinduzi upo wazi kwamba vyama vya siasa vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu uliofutwa wa Oktoba mwaka jana vinapaswa kujiandaa na uchaguzi wa marudio,” alisema.

Watuhumiwa 7 wa Makontena Ambao ni Wafanyakazi wa Bandari Waliokuwa Wametoroka Wakamatwa

$
0
0

Wafanyakazi saba kati ya wanane wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) waliotuhumiwa kuhusika kutorosha makontena 11,019 na magari 2,019 kutoka bandarini ambao walitoroka, wamepatikana na tayari wanaendelea kuhojiwa na polisi juu ya tuhuma hizo.

Watumishi hao ni kati ya watuhumiwa 15 wa TPA waliotangazwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuwa wameshiriki kuondosha makontena na magari hayo kutoka katika bandari kavu saba bila kulipa ushuru wa Bandari.

Meneja Mawasiliano wa TPA, Janet Ruzangi alisema jana kuwa mfanyakazi mmoja kati ya hao wanane, hajapatikana; na anaendelea kusakwa na polisi ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

“Wote walishapatikana kasoro mtumishi mmoja, Happygod Naftali, ambaye huyu alishaacha kazi siku nyingi baada ya viongozi kuanza kufuatilia suala hilo; lakini bado polisi wanaendelea kumsaka,” alisema Ruzangi.

Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alithibitisha watuhumiwa hao, kukamatwa na kwamba bado wanaendelea kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo.

“Ni kwamba tunaendelea na upelelezi wetu,” alisema Sirro licha ya kuwa hakutaka kutaja idadi ya wafanyakazi wa TPA ambao wamepatikana. “Kwa kweli idadi nitaitoa siku nitakapozungumza na waandishi wa habari wiki hii,” alifafanua.

Watumishi waliokuwa wanasakwa na polisi waliopatikana kwa mujibu wa Ruzangi ni Aron Lusingu, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Bonasweet Kimaina, Zainab Bwijo na Nathan Edward.

Watumishi hao wanaungana na watumishi wengine saba John Elisante, Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Adnan Ally, Masoud Seleman na Benadeta Sangawe waliokamatwa na kuhojiwa kuhusu sakata hilo. Watumishi hao saba, kwa mujibu wa Sirro, tayari walishapelekwa mahakamani.

“Ukiacha wale saba ambao tumeshawafikisha mahakamani, hawa wengine bado tuko nao tunaendelea kufanya upelelezi,” alieleza.

Wafanyakazi hao wanatuhumiwa kuhusika kutorosha makontena 11,884 na magari 2,019 ambayo yalitoroshwa kutoka katika Bandari Kavu (ICD) saba bila kulipiwa ushuru wa bandari na hivyo kuipotezea Serikali mapato ya Sh bilioni 48.55.

Kuhusu mawakala 280 waliopewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo yao makao makuu ya TPA namna ya walivyohusika kulipia makontena hayo, Ruzangi alisema mamlaka yake inajipanga kutoa taarifa kamili juu ya suala hilo.

“Tunaendelea kuandaa taarifa ya kilichotokea na kilichobainika kuhusu mawakala hao, tutatoa taarifa hivi karibuni,” alisema Meneja Mawasiliano huyo.

Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani, uongozi wake umeibua ufisadi wa kutisha ambao ulikuwa unafanywa Bandari ya Dar es Salaama kwa kuwashirikisha wafanyakazi wa TPA na mawakala pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Kwa mara ya kwanza upotevu wa makontena 349 uligundulika baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutinga bandarini na kubaini makontena hayo kutolewa bandari kavu bila kulipiwa kodi. 

Upotevu huo ulifanya vigogo wa TRA, akiwemo Kamishna Mkuu Rished Bade na makamishna wengine kusimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani.

Baadaye Majaliwa alibaini upotevu wa makontena 2,431 yaliyoondolewa bandari kavu bila kulipiwa ushuru wa Bandari.

Katika sakata hilo, baadhi ya mawakala wa forodha walifungiwa kufanya biashara na TPA Sakata la mwisho ni la kupotea kwa makontena 11,019 na magari 2,019, ambayo yaliondolewa kwenye ICD saba bila kulipiwa ushuru wa bandari na kuipotezea serikali mapato ya Sh bilioni 48.

Kesi Ya Askofu Gwajima Kuendelea Kusikilizwa Februari 24

$
0
0

Mahama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imesema itaendelea kusikiliza ushahidi wa Jamhuri katika kesi inayomkabili  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Gwajima anakabiliwa na tuhuma za kutoa lugha ya matusi dhidi ya  Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, kwamba ni mtoto, hana akili na mpuuzi. Anadaiwa kutoa maneno hayo.

Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa ushahidi huo jana lakini iliahirishwa baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro, anayeendesha kesi hiyo kuwa mgonjwa.

Kimaro alitoa madai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Cyprian Mkeha, anayesikiliza kesi hiyo.

Wakili wa utetezi Peter Kibatala, alidai kuwa hana pingamizi na maombi ya Jamhuri.

Hakimu Mkeha alisema kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Februari 24, mwaka huu na dhamana ya mshtakiwa inaendelea.

Katika kesi ya msingi, Askofu Gwajima anadaiwa kuwa kati ya Machi 16 na 25, mwaka jana, katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam, alitoa lugha ya matusi kwamba “mimi Askofu Gwajima nasema Askofu Pengo ni mpuuzi mmoja yule, mjinga mmoja, amekula nini yule, sijui amekula nini yule mtoto hana akili yule”.

Alidai kuwa Askofu Gwajima alitoa maneno hayo ya kufadhaisha dhidi ya Kardinali Pengo na kwamba yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

CUF Kutoa Tamko Zito Leo Kuhusu Suala la Zanzibar

$
0
0

Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF), leo linatarajia kutangaza uamuzi mzito kutokana na kikao cha Kamati ya Utendaji, kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam chini ya Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad.

Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji kilifanyika kwa saa tatu kujadili suala la tarehe iliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ya kurudia uchaguzi wa Zanzibar, uliofutwa Oktoba 28, mwaka jana.

Kamati hiyo ambayo ilikuwa na ajenda moja pekee, ilijadili na  kutoa uamuzi mzito ambayo yatawasilishwa kwenye Baraza Kuu leo na kutolewa kwa umma.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji, ambaye hakutaka kutajwa jina , alisema kuwa maazimio yaliyotolewa na kikao hicho kilichoanza saa nne asubuhi, yataishangaza dunia.

Alisema uchaguzi uliotangazwa na ZEC kuwa utafanyika  Machi 20, mwaka huu, ni batili kwa kuwa tayari mshindi wa uchaguzi huo anafahamika ni Maalim  Seif.

“Jukumu kubwa la kikao cha Kamati Tendaji kwa mujibu wa Katiba (ya CUF) ni kuandaa ajenda kwa ajili ya kikao cha Baraza Kuu litakaloanza kesho (leo) na baada ya hapo tutatangaza msimamo wetu juu ya uchaguzi huo,” kilieleza chanzo hicho.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa CUF, Silas Bwire, Kamati ya Utendaji ilikuwa na wajumbe 18 kutoka Tanzania Bara na  Zanzibar, ambao ni viongozi waandamizi wa chama.

Baraza kuu ambalo linatarajia kufanya kikao chake leo, litakalopokea ajenda zilizojadiliwa jana, lina wajumbe 60.

Kikao cha Baraza ambacho kitaongozwa na Mwenyekiti wake, Dk. Twaha Tasilima, kitajadili kwa kina ajenda zitakazowasilishwa pamoja na kuzitolea uamuzi.


==>Wakati hatima ya CUF kushiriki au kutoshiriki uchaguzi wa marudio inatarajia kufahamika leo, mgawanyiko mkubwa umeibuka miongoni mwa wajumbe wake wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa.

Katika mgawanyiko huo, wamo wanaopinga kushiriki huku wengine wakitaka chama kuangalia upya msimamo wa kususia uchaguzi huo.

==>Akizungumzia mgawanyiko huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano  wa  CUF, Ismail Jussa Ladhu, alisema kutokana na ukubwa na uzito wa mgogoro wa uchaguzi, mgawanyiko ni jambo ambalo halikwepeki kwa chama kikubwa kama hicho.

Alisema uongozi wa chama uko makini katika kujadili ajenda ya mgogoro wa uchaguzi na kuwataka viongozi na wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa na moyo wa subira wakati Baraza Kuu la Uongozi la Chama linajiandaa kutoa kauli ya mwisho juu ya hatima ya uchaguzi huo.

Jussa alisema uamuzi utakaotolewa na Baraza Kuu ndio utakuwa mwongozo kwa wagombea wote wa chama pamoja na wanachama na watu wanaokiunga mkono chama.

Alisema mchezo aliyoufanya Jecha wa kufuta matokeo ya uchaguzi kwa manufaa ya CCM, haukubaliki katika misingi ya demokrasia na utawala bora.

Profesa Muhongo Ataka Nyaya Za Umeme Zipite Chini Ya Ardhi

$
0
0

Wataalam kutoka Shirika la Umeme (Tanesco) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), wanaendelea kupiga hesabu kabla ya kuja na majawabu ya kushusha bei ya umeme.

Aidha, Profesa Muhongo alisema, kwa mara ya kwanza, wanataka nyaya zote za umeme jijini Dar es Salaam hususan katikati ya jiji, zipite chini ya ardhi.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema jana bungeni kwamba bei hiyo itashuka kwa mchakato huo (wa kupiga hesabu) na si kwenye majukwaa.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) aliyetaka kufahamu hatua ambazo serikali imefikia katika uzalishaji, usambazaji na umeme kwa ubia.

“Kuhusu bei ya umeme, wengine wanasema nilisema ishuke haijashuka…nilisema tunapiga hesabu. Bei huwezi kuongea kwenye majukwaa. Tanesco na Ewura wanapiga hesabu tunataka kushusha bei na si kwenye majukwaa,” alisema.

Kwa upande wa nyaya za umeme, alisema mkandarasi ameelekezwa ifikapo Aprili mwaka huu, serikali iachane na kesi za nyaya kuanguka kwa kuwa zitakuwa zimepitishwa chini ya ardhi.

“Kwa mara ya kwanza, Serikali inataka nyaya zote za umeme zipite chini ya ardhi,” alisema na kufahamisha bunge kwamba, maeneo ya Mbagala na Temeke, inajengwa transfoma kubwa.

Pia kwa upande wa Jimbo la Kibamba, inaondolewa transfoma yenye kilovolti 100 a kuwa na yenye kilovolti 2000.

Alisema Tanzania ijayo itakuwa ya umeme mwingi na wa bei nafuu ambapo inatarajia kuwa na umeme wa megawati 10,000. Profesa Muhongo alisema serikali inaendelea kukaribisha wawekezaji na kwamba Tanzania ijayo itakuwa ya umeme mwingi na wa bei nafuu.

Akizungumzia suala la usambazaji umeme, alisema kuna miradi kadhaa inaendelea kutekelezwa na serikali kwenye maeneo mbalimbali nchini. Profesa Muhongo alisema umeme uliopo hivi sasa hauvuki megawati 1,500 na ili kufikia lengo wanahitaji kufikia megawati 10,000.

Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (CHADEMA), Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani, alisema ukarabati wa miundombinu katika jimbo hilo, unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia mwanzoni mwa mwezi ujao na kukamilika Juni, mwaka huu.

Waziri Mkuu Asisitiza Bungeni Leo Kuwa TBC Hawatarusha Live Matangazo ya Bunge

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba matangazo ya bunge hayatarushwa yote live kama serikali ilivyosema jana na tayari hatua hiyo imekwisha kuanza.

Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Hai ambaye pia ni msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe aliyetaka kujua kwanini serikali imefanya maamuzi ya kuzuia wananchi wasione matangazo ya Bunge moja kwa moja.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema kwamba uamuzi wa kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja uliombwa na chombo cha umma chenyewe kwamba hakina uwezo kujiendesha na uamuzi wao huo umeungwa mkono na serikali.

''Maamuzi ya chombo hiki yameungwa mkono na serikali na waziri Nape Nnauye amefanya kipindi maalum kuhusiana na jambo hilo na wananchi wameelewa vizuri na wameiunga mkono serikali kwamba matangazo yatarekodiwa na yatarushwa kama kipindi maalum usiku'' Amesema Waziri Majaliwa.

Aidha chombo cha umma kitakuwa kinarusha matangazo ya moja kwa moja kwa muda wa maswali na majibu kwa serikali na baada ya hapo matangazo yatarekodiwa na kurushwa katika kipindi kiitwacho leo katika Bunge.

Shirika la Fedha Duniani Lavutiwa na Hatua za Ukuaji Uchumi Tanzania

$
0
0

Mkuu wa Ujumbe wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, Hervé Joly amesema Matarajio ya kiuchumi ya Tanzania yanatia matumaini sana, huku serikali ya awamu ya tano ikiwa imeahidi kulipa malimbikizo kwa wanaotoa huduma.

Bw.Joly amesema IMF imekamilisha tathmini ya tatu ya uchumi wa Tanzania kupitia mfumo wa PSI,ambao mapendekezo yake yanategemewa na wahisani.

Mkuu huyo wa IMF,amesema hali ya kiuchumi nchini Tanzania ni nzuri, na uchumi ukiwa umekuwa kwa asilimia 7 mwaka 2015 na ongezekeo la bei za bidhaa likiwa ni asilimia 5.6 tu.

Licha ya hayo, amesema IMF imekuwa na wasiwasi kuhusu bajeti ya serikali lakini amesema harakati zilizochukuliwa na serikali mpya zimetia matumaini.

Amesema matarajio ya ukuaji wa uchumi ni mazuri kwa mwaka 2016,huku IMF ikipendekeza kuendelea kuleta mabadiliko katika matumizi ya serikali na hasa kupunguza madeni ya TANESCO.

Watu 30 Wameokolewa Baada ya Kivuko cha Kilombero Kupinduka Jana Usiku.....Mtu Mmoja Hajapatikana Hadi sasa

$
0
0

Watu wapatao 30 wameokolewa mpaka sasa baada ya kivuko cha mto Kilombero kushindwa kuhimili upepo mkali ulioambatana na mvua ya radi  na  kukifanya kigonge nguzo za pembeni ya mto na kukosa mwelekeo hivyo kupinduka ndani ya maji jana usiku.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa leo Bungeni na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu) Jenista Mhagama, kivuko hicho kilikuwa  na  watu 31, magari na mizigo mbalimbali  ambapo  mpaka sasa  mtu  mmoja bado hajapatikana.

Tukio la kivuko hicho cha mto Kilombero kushindwa kumudu upepo sio mara ya kwanza kujitokeza katika eneo hilo la mpakani mwa wilaya za Kilombero na Ulanga, ambapo juzi hali kama hiyo ilijitokeza.

Kweli Kwenye Siasa Hakuna Adui wa Kudumu.....Watazame Mbowe na Zitto Kabwe Wakicheka na Kufurahi Pamoja

$
0
0

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (kulia) akipeana mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari wakipinga kitendo cha kutolewa kwa nguvu katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana. 

March 10 2015, Zitto Kabwe alivuliwa uanachama wa CHADEMA  kwa tuhuma za kukihujumu na kikisaliti chama hicho.

Hata hivyo, baada ya muda mfupi, Zitto alijiunga na chama cha ACT-Wazalendo na kuteuliwa kuwa kiongozi mkuu wa chama hicho huku mwenyekiti wake akiwa Anna Mghwira

Wabunge wa Upinzani Watoka Bungeni tena.......Ni Baada ya Naibu Spika Tulia Ackson Kuwanyima Muongozo ili Waongee

$
0
0
Hali ya sintofahamu imeendelea ndani ya bunge baada ya wabunge wote wa Upinzani kutoka ndani ya bunge.

Hali hiyo imetokea baada ya Naibu Spika Tulia Mwansasu kumtaka katibu wa Bunge kuarifu bunge ratiba inayoendelea, ambapo katibu wa Bunge alibainisha kwamba kazi ya ratiba ya leo inaonyesha kwamba ni kuchangia hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge.

Baada ya hapo wabunge wa upinzani waliomba miongozo kutoka kwa Naibu Spika, ambapo Naibu spika alimruhusu Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko.


Mbunge huyo aliuliza swali kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa elimu bure kwa wanafunzi kutozwa michango katika jimbo lake.

Naibu wa spika akitoa majibu ya muongozo huo alisema kwamba serikali inatambua matatizo yanayojitokeza na inayafanyia kazi

Jambo hilo liliwakasirisha wabunge wa upinzani na kuzidi kuomba miongozo ambapo Naibu Spika aliwakataza na kuruhusu ratiba iliyo mbele ya bunge kuendelea,hali ambayo iliwafanya wabunge wa upinzani wasuse na  kutoka nje.

==>Wabunge wa CCM wanaendelea  kujadili Hotuba ya Rais.

Wizara Ya Ujenzi, Uchukuzi Na Mawasiliano : Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kufungwa Kwa Muda Barabara Ya Mpanda – Koga – Tabora

$
0
0

Tunapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa, Barabara ya Mpanda – Koga – Tabora imefungwa kwa muda kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini zilizosababisha kufurika kwa mto Koga na kufanya daraja la Koga, lililopo mpakani mwa Mikoa ya Katavi na Tabora kutopitika na hivyo kukata mawasiliano ya barabara katika mikoa hiyo

Kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara kupitia daraja hilo, tunaomba wananchi kusitisha safari kwa kutumia barabara hiyo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza hadi hapo barabara hiyo itakapofunguliwa mara tu baada ya maji kupungua katika eneo hilo.

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kifungu cha 41 (1) cha Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni ya 8 (1) ya Kanuni za Usimamizi za Barabara za Mwaka 2009.

Wizara, inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote.

Imetolewa na:
Eng. Joseph Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)
28/01/2016

Tusimruhusu Rais Magufuli Kusimika Utawala Wa Kidikteta Nchini- ACT Wazalendo

$
0
0
JANA limetokea tukio la aibu katika nchi yetu pale serikali ilipofanya jaribio la hatari la kuzuia wananchi kuona na kusikia kinachoendelea bungeni.

Kitendo cha serikali ya CCM kuzuia kuonyeshwa moja kwa moja vipindi vya bunge katika televisheni ya taifa ni cha kijima na sisi chama cha ACT-Wazalendo tunakilaani kwa nguvu zetu zote.
 
Tunakitafsiri kitendo hiki cha serikali kama mwendelezo wa hatua na juhudi za Rais Magufuli za kuminya demokrasia na kusimika utawala wa kiimla.

Tunawasihi wananchi kusimama imara na kuzipinga jitihada zozote ovu za kuminya demokrasia nchini.
 
Tunawapongeza wabunge wazalendo wa upinzani kwa kusimama pamoja na kupinga nia ovu ya serikali ya kuua demokrasia katika nchi yetu.

Tunawatia shime wabunge wote wazalendo kuendelea kupigania maslahi mapana ya taifa letu.

ACT-Wazalendo! Taifa kwanza leo na kesho!

Imetolewa na;
Samson Mwigamba,
KATIBU MKUU.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images