Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

MSD Yajiandaa Kuanza Kuzalisha Dawa Nchini

0
0
BOHARI Kuu ya Dawa (MSD), imesema iko kwenye hatua nzuri za kuanzisha mradi wa uzalishaji dawa na vifaa tiba nchini kwa ubia na sekta binafsi, lengo likiwa kupunguza tatizo la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini. Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Mwanakunu alisema zabuni ya kumpata mtaalamu mshauri imekwishatangazwa na inategemea kukamilika mwezi huu. Alisema, kwa sasa Bohari

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Apewa Masaa 48 Ya Kujieleza

0
0
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Mazingira na Muungano) Luhaga Mpina amempatia saa 48 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kujieleza sababu za Jiji la Mwanza kuwa chafu. Mpina alisema hayo jana jijini hapa wakati akieleza mambo aliyoyabaini wakati wa ziara yake ya siku mbili jijini Mwanza. Alisema licha ya serikali kutangaza suala la usafi kuwa ni hoja ya kitaifa, Jiji la Mwanza

Taarifa ya Uteuzi wa Wabunge Kwenye Kamati za Kudumu Za Bunge

0
0
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA WABUNGE KWENYE KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE. Katibu wa Bunge anatoa taarifa kwa umma kwamba: (a) Kwa mujibu wa Kanuni ya 116 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano amepewa mamlaka ya kuteua Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa namna ambayo itawezesha kila Mbunge kuwekwa kwenye Kamati mojawapo.

Wazanzibari Kusherehekea Miaka 52 ya Mapinduzi LEO

0
0
WAZANZIBARI leo wanasherehekea miaka 52 ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964, ambayo yaling’oa utawala wa Sultani kutoka Oman na kuwezesha wazalendo wengi kushika hatamu ya kuongoza nchi. Katika kilele cha sherehe hizo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein atahutubia taifa katika uwanja wa Amaan. Atapokea maandamano ya wananchi wa mikoa mitano ya

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya January 12

CCM Wajibu Mapigo Zanzibar.......Wasema Uchaguzi Lazima Urudiwe

0
0
Muda mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kasoro na athari za kurudia Uchaguzi uliofutwa kinyume cha sheria na Jecha Salim Jecha, viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametangaza kuwa uchaguzi  huo lazima urudiwe. Wakizungumza jana na vijana wa chama cha Mapinduzi katika viwanja vya Maisara waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya

UVCCM yataka Rais mstaafu wa Zanzibar Dr Aman Abeid Karume Afukuzwe CCM

0
0
UMOJA wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umekitaka chama hicho kumvua uanachama Rais mstaafu wa Zanzibar Dk  Aman Abeid Karume. Kauli hiyo ilitolewa jana katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Khamis wakati wa kilele cha matembezi ya vijana wa umoja huo kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi. Alimshushia tuhuma nzito mstaafu huyo kuwa

Serikali yakusudia kuanza kuzalisha drip za maji za IV katika hospitali zake zote kubwa nchini

0
0
SERIKALI inakusudia kuanza kuzalisha drip za maji za IV (Intravenous Fluids) katika hospitali zake zote kubwa nchini. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipotembelea mtambo wa kutengenezea drip hizo za majimaji katika hospitali ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho, Mkoani Ruvuma. Amesema haoni kwa nini hospitali hizo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Afika Muhimbili Kumjulia Hali Waziri Mkuu Staafu Fredrick Sumaye

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri Mkuu, Mstaafu Frederick Sumaye  ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu Januari 12, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amnaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa Matibabu Januari 12, 2016. Kushoto ni Mke wa

CCM Yaomba Radhi Kutokana na Maneno ya Kibaguzi Kwenye Bango Katika Sherehe za Mapinduzi

0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi. Ujumbe huo

DPP Akata Rufaa Kupinga Kuachiwa Huru Kwa Shehe Ponda

0
0
MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) ameamua kukata rufaa Mahakama Kuu dhidi ya kesi ya uchochezi inayomkabili mwanaharakati wa Kiislamu Shehe Ponda Issa Ponda. Mwanasheria Mwandamizi katika ofisi ya DPP, Bernard Kongola amesema kuwa Serikali inapinga kuachiwa kwa Shehe Ponda ambaye alishitakiwa kwa makosa ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro. “Tayari tumeomba tupatiwe nakala

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya January 13

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete Wampa pole Mama Maria Nyerere kwa msiba wa Marehemu Leticia Nyerere

0
0
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongea na Mama Maria Nyerere, mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, walipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumpa pole kwa kufiwa na mkwewe Marehemu Leticia Nyerere Jana Jumanne Januari 12, 2016 Mama Salma Kikwete akimfariji  Mama Maria Nyerere, mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, walipomtembelea

Mwanafunzi wa Miaka 13 Aozeshwa kwa Ng’ombe 13

0
0
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Mika Nyange Mtoto mwenye umri wa miaka 13 anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Wishiteleja wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga, ameozeshwa kwa nguvu na wazazi wake baada ya kupokea mahari ya ng’ombe 13. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga juzi, Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE, John Myola alisema mwanafunzi huyo

Chadema Yatuma Salamu Za Rambirambi Kufuatia kifo cha Aliyekuwa Mbunge Wake Leticia Nyerere

0
0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wake wa Viti Maalum, Leticia Nyerere kilichotokea juzi nchini Marekani. Leticia alifariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lan ham, Maryland Jumapili saa 2 usiku wa saa za Afrika Mashariki alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Taarifa ya Chadema iliyotolewa na Mkuu

Jecha wa ZEC Atoka Mafichoni.....Dk. Shein Asisitiza Uchaguzi Lazima Urudiwe Zanzibar

0
0
Hatimaye  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, jana ameonekana hadharani katika maadhimisho ya sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja. Jecha ambaye inaaminika alikuwa mafichoni tangu alipotangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Oktoba 28, mwaka jana, alionekana ameketi kwenye jukwaa kuu la viongozi,

Rais Mstaafu, Dk Ali Hassani Mwinyi atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA)

0
0
Rais Mstaafu wa Tanzania, MzeeAli Hassani Mwinyi (katikati) akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA) na Rais wa Sudani ambaye pia ni mkuu wa chuo hicho, Omar al-Bashir (wa pili kulia) mjini Khartoum, Sudani  hivi karibuni.  Rais Mstaafu, Ali Hassani Mwinyi (wa pili kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa zamani wa

Waziri Muhongo aahidi kuongeza matumizi ya umeme wa makaa ya mawe

0
0
Serikali imesema itahakikisha makaa ya mawe yanakua chanzo kingine kikubwa cha uzalishaji wa umeme nchini ili kupunguza gharama za umeme zilizopo hivi sasa. Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameyasema hayo  alipotembelea mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka uliopo wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma na kuongeza kuwa serikali itahakikisha inafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na

Naibu Waziri wizara ya fedha aibana TRA Mbeya

0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji ameitaka Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Mbeya kuhakikisha inaanda mpango maalumu kwa ajili kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kushamiri kwa biashara ya ubadilishaji wa fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma na Zambia.   Dk. Kijaji ametoa kauli hiyo Mkoani Mbeya baada ya kutembelea TRA mkoani humo na kusema serikali imekuwa

Waziri Mkuu Ampa Pole Mama Maria Nyerere

0
0
WAZIRI MKUU,Kassim Majaliwa amemtembelea na kuampa pole  mke wa Baba wa Taifa,  Mama Maria Maria Nyerere kwa kufiwa na mkwewe  Leticia Nyerere. Akizungumza na mama Maria alipomtembelea nyumbani kwake jana(Jumanne, Januari 12,2016), Msasani jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu ametoa pole kwa  Mama Maria Nyerere pamoja na familia  na kuwaomba waendelee kuwa  wavumilivu katika kipindi hiki
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images