Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TRL Yasitisha Kwa Muda Safari Za Treni Ya Bara Kutokana Na Mafuriko Kati Ya Morogoro Na Dodoma

$
0
0
KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE) Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL umetangaza kusitisha kwa muda kuanzia  Januari 01, 2016, huduma zake baada ya eneo la reli ya kati ya Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma tuta la reli kukumbwa na Mafuriko. Kwa mujibu wa taarifa za kifundi eneo lililoathiriwa na mafuriko ni kubwa hivyo

Bajeti ya Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar Yatengwa.......Kinachosubiriwa ni ZEC Kutangaza Tarehe Ya Uchaguzi

$
0
0
Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema bajeti ya uchaguzi wa marudio imeshatengwa na wanachosubiri ni Mwenyekiti wa Tume ya  Uhaguzi Zanzibar (ZEC) atangaze tarehe hiyo ya kufanya uchaguzi. Amesema bajeti hiyo haitatofautiana na ile iliyotumika katika uchaguzi wa Novemba 2015 iliyofikia karibu ya shilingi bilioni saba. Amekanusha kauli kuwa uchaguzi huo

Dkt. Kigwangala Amtembelea na Kumjulia hali Mwadhama Kardinali Pengo.

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala jana alimtembelea na kumjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Akiongelea kuhusu hali ya Kadinali Pengo, Mhe. Kigwangala

Waziri Mkuu Majaliwa Kutikisa Mkoa wa Ruvuma Kwa Siku 3 Kuanzia Leo

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo ataanza ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma, kuhimiza na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa, Said Mwambungu alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Songea jana. Alisema, Waziri Mkuu atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Songea saa 6 mchana, ambapo atapokelewa na viongozi wa serikali na vyama vya siasa.

Basi lenye abiria 42 latumbukia mtoni

$
0
0
WATU sita wamekufa papo hapo na wengine 25 kujeruhiwa na kulazwa hospitalini kutokana na ajali mbili tofauti.  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema mjini hapa jana kuwa ajali ya kwanza, ilihusisha basi la abiria lililokuwa na abiria 42, ambalo liligonga kingo za daraja, likaparamia miti miwili kisha kutumbukia ndani ya mto Lukosi, Iyovi eneo la Msosa huko Mikumi

Ikulu Yaagiza Mtumishi Atakayefanya Kosa Aadhibiwe Hapohapo Alipo Badala Ya Kuhamishiwa Sehemu Nyingine ya Kazi

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.   MAKATIBU Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu walioteuliwa na kuapishwa juzi wamekutana katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya semina elekezi iliyoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. Akizungumza kabla ya kuanza kwa mada zilizoandaliwa katika semina hiyo  jana, Katibu Mkuu Kiongozi Sefue, alisema semina

Dk Makongoro Mahanga Amvaa Rais Magufuli Kwa Kuunda Serikali Kubwa Tofauti Na Ahadi Yake Aliyoitoa wakati wa Kampeni

$
0
0
Wakati watu mbalimbali wakimminia sifa Rais John Magufuli kwa kubana matumizi, aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga amesema uwingi wa makatibu wakuu unakinzana na dhana ya yake ya kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri. Dk Mahanga alikuwa Naibu Waziri wa Lazi na Ajira tangu mwaka 2008 na hakuwahi kuhamishwa wala kupandishwa hadi ngazi ya uwaziri hadi Serikali ya

Wananchi Wavamia Shamba la Sumaye na Kugawana

$
0
0
Wananchi zaidi ya 100, wakiwemo waliobomolewa maeneo ya mabondeni jijini Dar es Salaam, wamevamia shamba la Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye lenye ukubwa wa heka 33, lililopo Mji Mpya eneo la Mabwepande na kujikatia viwanja. Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tano kati ya mwaka 1995 hadi 2005, amekiri wananchi kuvamia shamba hilo lakini alisema hana wasiwasi

Kingunge Ngombare Mwiru Kumpima Rais Magufuli Baada ya Siku 100

$
0
0
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru, amesema atampima na kuzungumzia utendaji wa Rais wa tano, John Magufuli atakapotimiza siku 100 Ikulu. Dk. Magufuli leo ametimiza siku 59 tangu kuapishwa kushika madaraka hayo Novemba 5, mwaka jana na ameshafanya mambo makubwa yaliyompa sifa kem kem kitaifa na kimataifa. Kingunge ambaye mwishoni mwa mwaka jana alikihama chama

Misaada Ya Mbunge Lwakatare (Chadema ) Yakataliwa Hospitalini

$
0
0
Baadhi ya wakuu wa vituo vya afya na zahanati katika Manispaa ya Bukoba, wamegoma kupokea misaada kwa ajili ya wajawazito uliotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare kwa madai ya kupewa maelekezo na Serikali. Mbunge huyo mwishoni mwa wiki alikuwa akisambaza vifaa tiba katika vituo vya afya na zahanati, lakini wasimamizi walikataa kuvipokea, huku wengine wakikimbia

Waziri Maghembe Afichua Siri Ya Uteuzi Wa Jenerali Gaudence Milanzi Wizara Ya Maliasili.

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amefichua sababu za Rais John Magufuli, kumteua Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo. Profesa Maghembe alisema lengo ni kuwa na kamanda atakayeongoza mapambano dhidi ya ujangili na kutoa onyo kwa majangili kujisalimisha na silaha zao, vinginevyo watakiona cha mtema kuni. “Yale maneno maneno kuwa

Dkt. Shein Afanya Uzinduzi wa Sherehe za Mapinduzi kwa Usafi wa Mazingira Kitaifa

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizoa taka katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akibeba taka katika zoezi la

Mchungaji Lwakatare Apinga Nyumba yake Kubomolewa....Mwanasheria Wake Aitaka Serikali Kuheshimu Hukumu ya Mahakama

$
0
0
Mchungaji  a  Kanisa  la  Assemblies of God,Mikocheni, Dr Getrude Lwakatare amepinga  nyumba  yake  kubomolewa  ikiwa  ni  siku chache  baada ya wizara  ya  maliasili  na  utalii kupitia  wakala  wa  misitu  Tanzania (TFS ), kuweka alama  ya X wakidai imo katika hifadhi  ya  bahari. Mwishoni mwa mwaka jana, Serikali ilianza ubomoaji wa nyumba zote zilizojengwa mabondeni, kama Bonde la Mto

Sakata la Upotevu wa Makontena Bandari Lachukua Sura Mpya Baada ya Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa) Kufungua Kesi Mahakama Kuu

$
0
0
Sakata la utoaji makontena bila kulipia tozo ya bandari, limechukua sura mpya baada ya Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa) kufungua kesi Mahakama Kuu, kupinga kitendo cha Mamlaka ya Bandari (TPA) kuwadai fedha za tozo hiyo ambazo wamesema wameshalipia.   Taffa imefungua kesi hiyo kwa hati ya dharura, ikipinga TPA kutaka kufungia kampuni zinazojihusisha na masuala ya forodha, kuwakamata

Ole Sendeka Amjibu Dk Makongoro Mahanga ....Asema Makatibu Wakuu na Manaibu wao Sio Wajumbe Wa Baraza La Mawaziri

$
0
0
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na mbunge wa zamani wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka amewataka watanzania kuwa makini na kuzipuuza kauli zinazoenezwa na baadhi ya watu  kwenye mitandao kuwa serikali ya Dk John Magufuli imekuwa na baraza kubwa la mawaziri kuliko alivyo ahidi na kwamba serikali inaweza kuwa nagharama zaidi kwakuwa kauli hizo zinalengo la kufifisha juhudi za serikali ya

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Jaunuari 4

Waziri Mbarawa Atoa Siku Tatu Ukarabati Reli Ya Kati Iliyosombwa na Mafuriko

$
0
0
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka watendaji wa Shirika la Reli nchini (TRL) na Kampuni Hodhi ya Mali za Reli (RAHCO) kuhakikisha sehemu ya reli iliyosombwa na mafuriko wilayani Kilosa mkoani Morogoro inaunganishwa ndani ya siku tatu na huduma za treni kurejea.    Prof. Mbarawa amesema hayo baada ya kukagua sehemu ya reli hiyo kutoka Kilosa hadi

CCM Wamvaa LOWASSA......Wamtaka Ajitokeze Hadharani Ataje Majina Ya Wafanyabiashara Waliomfadhili Ambao Wananyanyaswa

$
0
0
CCM imesema kauli ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa wafadhili wa Chadema wananyanyaswa, ina lengo la kuichonganisha Serikali na walipa kodi na kumtaka ataje waliofanyiwa vitendo hivyo. Juzi, Lowassa alikaririwa na vyombo vya habari kutoka Monduli akisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa maelekezo ya Serikali imekuwa ikiwatoza kodi kubwa wafanyabiashara kwa sababu

Ikulu Yamjibu Dk Makongoro Mahanga Aliyemtuhumu Rais Magufuli Kuunda Serikali Kubwa Tofauti Na Alivyoahidi

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema ameshangazwa na kauli ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongo  Mahanga kuwa wingi wa makatibu wakuu unakinzana na dhana ya kupunguza ukubwa wa Serikali alioahidi Rais John Magufuli. Juzi mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Segerea (CCM) alisema kuteua makatibu wakuu 27 ni sawa na kuwa na wizara 27 badala ya 15 kama

Shule sita Nchini Kufundisha Kichina

$
0
0
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imeteua shule sita za sekondari nchini kuingia katika mpango maalumu wa wanafunzi wake kufundishwa somo la lugha ya Kichina kuanzia mwaka huu.Kutokana na uamuzi huo, walimu 12 kutoka China wamekamilisha utaratibu wa mpango kazi wa namna ya ufundishaji wa somo hilo kwa shule zilizoteuliwa mara zitakapofunguliwa rasmi mwezi huu.Ofisa Elimu Mkuu wa
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images