Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Taasisi za Dini Zatajwa Kuhusika na Utoroshaji wa Makontena Bandarini

0
0
Mashirika ya dini ni miongoni mwa taasisi zilizotakiwa kuwasilisha nyaraka kwa ajili ya kuhakiki kama yalilipa ushuru wa bandari uliosababisha Serikali kupoteza Sh48 bilioni. Uwapo wa taasisi hizo za kiimani kwenye sakata hilo ulibainishwa jana katika orodha ya iliyotangazwa jana na Mamlaka ya Bandari (TPA) ambayo ina kampuni na taasisi 40 zaidi ya orodha iliyotangazwa juzi yenye kampuni

Kubenea Akana Kumtukana Dc Makonda

0
0
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (44) amekana kumtukana Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda tarehe 14 Desemba 2015 walipokutana katika Kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd. kilichopo eneo la External Mabibo kwa madhumuni ya kutatua mgogoro kati ya wafanyakazi na uongozi wa kiwanda hicho Katika kesi inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Wakili wa Serikali mwandamizi,

Lipumba Amtwika Zigo Dr Shein Mgogoro Zanzibar....Asema Mgogoro Utakwisha Iwapo Dr Shein Atakubali ZEC Iendelee Kutangaza Matokeo

0
0
Mwenyekiti wa zamani wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kumaliza mgogoro wa Zanzibar. Akizungumza Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mgogoro wa Zanzibar utamalizwa kwa Dk Shein kuiruhusu Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25. Alisema pamoja na

Kamanda Suleiman Kova Astaafu Rasmi Jeshi la Polisi Tanzania!

0
0
Leo ni siku ya mwisho kwa Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova, kulitumika jeshi la Polisi nchini kwa kuwa muda wake wa kulifanyia kazi jeshi hilo umeisha. Kamanda Kova ametoa taarifa hiyo leo asubuhi alipokuwa akizungumza katika kipindi cha kumekucha cha ITV, na kusema kuwa mkataba wake na jeshi la Polisi umeishia leo, hivyo analazimika kukaa pembeni. "Mmepata bahati

Karibu Mwaka Mpya 2016, Mwaka wa Matumaini Mapya Kwa Watanzania

0
0
Mwaka 2016 ni mwaka wa matumaini mapya kwa Watanzania wote walioanza kukata tamaa ya maisha bora. Biashara nyingi zimefilisika kutokana na vikwazo mbalimbali. Familia nyingi zimeparaganyika kutokana na kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili ya kitaifa na kunyauka kwa utu wa ubinadamu uliochochewa na hali duni ya maisha miongoni mwa jamii. Watu masikini na wenye kipato cha chini

Jeshi La Polisi Lawatahadharisha Wananchi Kuhusu Mkesha Wa Mwaka Mpya.

0
0
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TAHADHARI KATIKA MKESHA WA MWAKA MPYA    Tunapoelekea kumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha  mwaka mpya wa  2016, wananchi hutumia muda huo kwenda  katika nyumba za ibada ama kusherekea katika maeneo mbalimbali ya starehe, ambapo uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo  vinavyohatarisha

CUF Watangaza Kutoshiriki Sherehe za Mapinduzi Zanzibar....Tamko Zima Liko Hapa

0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Tokea yalipofanyika Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964, tumekuwa tukiadhimisha tukio hilo kubwa katika historia ya Zanzibar kila mwaka inapofika siku hiyo.  Tukio hilo kubwa ndilo lililopelekea kutangazwa kwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume. Chama Cha Wananchi (CUF) kimekuwa kikishiriki

Serikali Yasema Haijengi Nyumba za Kuwapa Wananchi Bure

0
0
SERIKALI imesema kuwa haina mpango wakujenga nyumba za kuwapa Wananchi bure kutokana na gharama ambazo Serikali inagharamia katika ujenzi nyumba hizo. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula (Pichani)wakati alipotembelea Shirika la Nyumba la Taifa(NHC). Angeline amesema kuwa shirika la nyumba la Taifa linajenga nyumba kwaajili ya kuuzwa

Makatibu wakuu na Manaibu Wao Walioteuliwa Jana Wataapishwa Kesho Ikulu Dar es Salaam na Kisha Kusaini Ahadi Ya Uadilifu

0
0
Kesho Tarehe 01 Januari, 2016 Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wataapishwa rasmi katika Ukumbi wa Ikulu, uliopo lango kuu litazamalo baharini kuanzia saa nne asubuhi. Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao wataapishwa na wale ambao walishaapishwa wanapaswa kuhudhuria katika tukio hili, ili

Serikali yapiga Marufuku Matumizi ya Barua pepe za Kawaida katika Mawasiliano yake.

0
0
Serikali imepiga marufuku matumizi ya Barua pepe za kawaida kwa watumishi wa umma wanaotuma au kupokea taarifa za Serikali na kuwataka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatumia mfumo rasmi wa Mawasiliano ya Barua Pepe Serikalini (GMS) ulioanzishwa na Serikali  kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kwa njia ya Mtandao. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya

Dk Harrisson Mwakyembe atembelea Tume ya Haki za Binadamu

0
0
Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dk Harrisson Mwakyembe ameitembelea  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na kusema kuwa ni  chombo muhimu ambacho uwepo wake unaipa heshima kubwa Tanzania kimataifa. Akizungumza katika ziara aliyoifanya katika Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2015, Dk Mwakyembe alisema Tume ni chombo muhimu kwa taifa kilichoanzishwa kikatiba

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa Ya Tarehe 1 Januari 2016

Taarifa Muhimu Kutoka Baraza La Mitihani Kuhusu Viwango Vya Ufaulu (Grade Ranges)

0
0
Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa limebadilisha Viwango vya Ufaulu (Grade Ranges). Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki.  Hivyo, Baraza

Profesa Ndalichako Atoa Siku 30 Kwa Katibu Mtendaji NACTE Kuvichunguza Vyuo Vyote Nchini Kujua Ubora Wake

0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ametoa siku 30 kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), Dk Primus Nkwera kufanya ukaguzi wa vyuo vyote na kumkabidhi ripoti ili kujiridhisha na ubora wa elimu inayotolewa. Pia, amewataka watendaji wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kuandaa mitalaa yenye matokeo ya kujenga wanafunzi

Sheria Ya Kuzuia Kelele Yaanza Kutumika....Kufanya Sherehe Mtaani, Kupiga Mziki, Kufanya Ibada Kwa Kelele ni Milioni 10

0
0
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeanza kung’ata kwa kutumia kanuni ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kelele na mitetemo.  Kwa sasa mtu akitaka kufanya sherehe mtaani, kupiga muziki kwa kelele, kuendesha ngoma za kukesha za nusu uchi (vigodoro) au ‘bai koko’ au kufanya ibada kwa kelele mitaani, atapaswa kulipa Sh milioni 10. Pia, baa na kumbi za

Jumba la Mchungaji Mama Rwakatare, Hoteli za Double Tree na Slip Way Kubomolewa

0
0
Wakati operesheni ya kuweka alama ya X kwenye nyumba zilizojengwa mabondeni, maeneo ya wazi na kinyume na taratibu ikiendelea, Hoteli za Double Tree na Slip Way nazo zimekumbwa na pigo hilo. Hoteli hizo pamoja na nyumba ya Maheshbhai Patel na baadhi ya wamiliki wengine wa nyumba ambao kuta zake zimejengwa karibu na barabara ya Slip Way eneo la Msasani Peninsula, wamepewa siku saba

Mkuu Wa Wilaya Akanusha Familia Kuchemsha Mawe Na Pumba Kutokana na Kukithiri Kwa Njaa

0
0
MKUU wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mohamed Utaly amekanusha taarifa za watu wa wilayani yake kuchemsha mawe kwa ajili ya kukosa chakula kutokana na kukithiri kwa njaa. Akitoa taarifa ya hali ya njaa kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa kutoka ofisi ya Waziri mkuu, Mbazi Msuya, mkuu huyo wa wilaya alisema kuna vyombo vya habari na mitandao ya kijamii imeripoti kuwa wananchi wa

Fatilia Live Hafla Ya Kuapishwa Kwa Makatibu Na Naibu Makatibu Wakuu

Huyu Ndo Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi .....Kazi Kwenu Majangili

0
0
Pichani ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye leo ameapishwa rasmi kuanza kupambana na majangili ambao wamekuwa kero kwa nchi hii. Ikumbukwe kuwa kuna wakati Tanzania ilifikia kuwa kinara cha matukio ya ujangili kiasi cha Serikali ya Awamu ya Nne kuanzisha Operesheni Tokomeza ambayo nayo haikuisha vizuri. Maliasili ya Tanzania ikitunzwa vizuri

Picha: Rais Dkt John Pombe Magufuli Awaapisha Makatibu Wakuu Na Manaibu Wake Elo Ikulu Jijini Dar.

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence S.Milanzi akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images