Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Disemba 23


Serikali Yafuta ‘Semina Elekezi’ Kwa Madiwani

$
0
0
Serikali imesema mafunzo kwa ajili ya madiwani wote hayatakuwepo na badala yake wenyeviti na makamu wa wenyeviti kote nchini ndio watapatiwa mafunzo ya namna ya kusimamia halmashauri zao. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jafo alisema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Chuo cha Serikali

Mhe. Jenista Aagiza Kamati Za Menejimenti Ya Maafa Nchini Kuwatoa Wanaoishi Kwenye Maeneo Hatarishi Mara Moja ......Vinginevyo Kamati Itawajibishwa

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UTEKELEZAJI WA AGIZO LA MENEJIMENTI YA MAAFA KWA KAMATI ZA MAAFA NGAZI ZA MIKOA, WILAYA, KATA NA VIJIJI Kufuatia taarifa ya tahadhari ya uwezekano wa kuwepo kwa mvua za El-Nino iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Mwezi Agosti 2015, Ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa agizo kwa Mikoa yote nchini kuchukua hatua za kujiandaa na kukabiliana na maafa yanayoweza kutokea

Magufuli Mgeni Rasmi Mkesha wa Kuiombea Amani Tanzania.

$
0
0
RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkesha wa kuiombea Amani Tanzania utakaofanyika Desemba 31 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Pentekoste (TFC), Godfrey Malassy alisema hayo jana jijini Dar es Salaam.   Alisema maandalizi yote yamekamilika ikiwemo kibali kutoka Polisi, pamoja na washiriki mbalimbali wa mkesha huo.

Maombi ya Kupandisha Ada Yatinga Wizarani

$
0
0
Shule nyingi za msingi na sekondari zisizo za Serikali, zimetuma maombi kwa Kamishna Mkuu wa Elimu nchini kuomba kibali cha kupandisha ada katika mwaka ujao wa masomo. Hatua hiyo ni kuitikia amri ya Serikali ya kuzipiga marufuku shule binafsi, kupandisha ada kiholela na badala yake shule zote zinatakiwa kuwasilisha maombi ya kupandisha ada hiyo mpya kwa kamishna huyo ili yajadiliwe. “

Samwel Sitta Atangaza Kustaafu Siasa .....Asema Atakuwa Mwandishi wa Vitabu na Mshauri

$
0
0
Kwa mara ya kwanza tangu Kamati Kuu ya CCM ilipomuengua kwenye kinyang’anyiro cha uspika, Samuel Sita ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, jana ameweka bayana mustakabali wake; ameamua kustaafu siasa. Sitta aliongoza kwa mafanikio Bunge la Tisa kiasi cha kumfanya apewe kirahisi uenyekiti wa Bunge la Katiba na hivyo kujijengea jina miongoni mwa wana-CCM kiasi cha kujitumbukiza kwenye mbio

Jela kwa kupongeza majambazi yaliyovamia Polisi Stakishari

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Bruno Kimaryo, kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza ujumbe katika mtandao wa kijamii wa kuyapongeza majambazi yaliyovamia Kituo cha Polisi cha Stakishari na kuua polisi.  Aidha, mshtakiwa huyo ametakiwa ama kulipa faini ya Sh. 600,000 kwa kosa hilo. Katika tukio la Stakishari lililotokea Julai 12, mwaka huu,

Serikali Yahimiza Ujenzi Wa Viwanda Vidogo Vidogo Nchini

$
0
0
Serikali imesema kuwa Tanzania haiwezi kubadirika ikiwa mawazo ya watu hayatabadirika katika ujenzi wa viwanda vidogo nchini kote na kuondoa mawazo ya kujenga viwanda vikubwa kama vya wafanyanyabiashara wakubwa, kwa kuwa vinahitaji mtaji mkubwa wakati ajira zake ni chache. Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Seleman Jaffo alitoa kauli hiyo tarehe 22

Jopo la Umoja wa Mataifa Linaloongozwa na Jakaya Mrisho Kikwete Lakamilisha kazi Yake New York, Marekani

$
0
0
Jopo la Watu Mashuhuri la Umoja wa Mataifa la Kupendekeza Namna Bora ya Dunia Kukabiliana na Majanga ya Afya limekamilisha kazi yake wiki iliyopita jijini New York.   Jopo hilo linaloongozwa na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete lilikabidhiwa jukumu hilo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon tarehe 2 Aprili, 2015 na kupewa muda wa kuanzia Mei hadi Desemba 2015 kukamilisha kazi

Dk. Magufuli Afuta Hatimiliki Shamba la Mkonge Kikwetu

$
0
0
Serikali imefuta hatimiliki ya shamba la mkonge la Kikwetu, mkoani Lindi baada ya mmiliki wake kampuni ya Amboni Estates Ltd, kushindwa kuliendeleza. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa manispaa hiyo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Ilulu mjini hapa juzi. Shamba hilo linalodaiwa kupewa hati ya umiliki wa miaka 99 na baadaye

Watu 7 Wafariki Kwa Kuungua Moto Baada ya Gari Kupinduka na Kuwaka Moto

$
0
0
WATU saba wamefariki duniani na wengine kumi wamejeruhiwa katika ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kulipuka na kuwaka moto. Akiongea na mtandao huu ofisini kwake Mganga Mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Kigoma Maweni Dkt. Leonard Subi amesema kuwa jana majira ya saa 12 jioni walipokea miili ya marehemu 6 na majeruhi 11 ilipofika saa 6 usiku majeruhi mmoja alifariki duniana na

Rais Magufuli Atoa Zawadi Za Sikukuu Ya Krismasi Kwa Watoto Wa Kijiji Cha Matumaini Mkoani Dodoma

$
0
0
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma Bi. Ziada Nkinda (Aliyebeba Mtoto) akikabidhi zawadi za siku kuu ya Noeli (Christmas) zilizotolewa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa watoto wanaoishi kwenye kituo cha kuhudumia watoto cha kijiji cha matumaini Mkoani Dodoma. Meneja wa kituo cha kuhudumia watoto cha kijiji cha matumaini kilichopo Dodoma  Padiri Vicent,

Wakuu wa Mikoa na Wilaya Dhibitini Migogoro Ya Ardhi – Waziri Mkuu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa wanaongeza udhibiti na usimamizi wa migogoro ya  ardhi kwenye maeneo yao husika.   Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatano, Desemba 23, 2015) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Lindi kwenye Ikulu ndogo mara baada ya kuwasili akitokea jimboni kwake Ruangwa

Waziri Wa Afya Amsimamisha Kazi Kaimu Mkurugenzi Wa Taasisi Ya Ocean Road Dk.diwan Msemo.

$
0
0
WAZIRI wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.Diwani Msemo ili kupisha uchunguzi pamoja na mambo mengine ili kubaini  mgongano wa kimaslahi ulioathiri utendaji wa taasisi  hiyo chini ya kaimu mkurugenzi huyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,

Madereva Watakaozidisha Abiria Kwenye Vyombo Vya Usafiri Kukiona

$
0
0
JESHI la Polisi Nchini limewatahadharisha madereva  watakaozidisha  idadi ya abiria kuliko uwezo wa chombo cha usafari kwani ni kosa kisheria na watakaozidisha abiria kwenye vyombo vyao vya usafiri watachukuliwa hatua za kisheria. Operesheni hiyo inaanza leo baada ya tamko la Jeshi la Polisi na kuanza kutekeleza kwa wale wote wataobeba abiria wengi tofauti na uwezo wa basi.

Mtendaji Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo Asimamishwa KAZI Kupisha Uchunguzi

$
0
0
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA - TAMISEMI TAARIFA KWA  VYOMBO VYA HABARI Ndugu wanahabari nimewaita hapa leo ili mnisaidie kufikisha ujumbe kwa wananchi kuhusu mradi wetu wa Mabasi yaendayo Haraka katika Jiji la Dar es Salaam (DART – BRT).    Kama mnavyofahamu Serikali ilianzisha mradi huu ili kupunguza msongamano wa magari barabarani kwa madhumuni ya kurahisisha usafiri na

Rais Magufuli Aonana Na Mjumbe Maalumu Wa Rais Paul Kagame Wa Rwanda Na Mabalozi Wa Uswisi Na Kuwait

$
0
0
Uswis iimeahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za maendeleo huku mkazo mkubwa ukiuelekeza katika kuendeleza elimu ya mafunzo ya ufundi stadi. Balozi wa Uswisi hapa Nchini Mheshimiwa Florence Tinguelly Mattli, amesema hayo leo tarehe 23 Desemba, 2015 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu

Breaking News: Rais Magufuli amemalizia kuwateua Mawaziri Wanne Waliokuwa Wamebaki

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano yautawala wake Uteuzi huo ni kama ifuatavyo; 1.Profesa Jumanne Maghembe -Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. 2.Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Disemba 24

Uamuzi wa Mwisho wa NEC kuhusu Uteuzi wa Madiwani viti Maalumu Kyerwa Baada ya Chadema Kulalamika

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images