Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kinana Ampa Makavu Lowassa

0
0
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amemjibu aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, aliyedai kuwa kazi nzuri anazofanya Rais John Magufuli, ni utekelezaji wa sera za vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea ubunge wa Arusha, Philemon Mollel (Monaban), uliofanyika katika kata ya Daraja

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi

Ajira za makatibu wakuu ziko salama- Ikulu

0
0
Uamuzi wa Rais John Magufuli kuunganisha wizara kutoka 30 hadi kuwa 18 na idadi ndogo ya mawaziri, hautasababisha kupunguzwa kwa watumishi, hasa makatibu wakuu, Ikulu imeeleza. Juzi, Rais Magufuli alitangaza kuunganisha wizara na kuunda Baraza la Mawaziri lenye wizara 18 kutoka 30 za Serikali ya Awamu ya Nne, uamuzi ambao umeibua hofu kwa baadhi ya watumishi kuwa panga hilo linaweza

Wakuu wa Mikoa na Wilaya Kupukutishwa

0
0
Baada ya kutaja Baraza la Mawaziri lenye sura mpya nyingi juzi ikiwa moja ya hatua katika ukamilishaji wa safu za uongozi wa serikali ya awamu ya tano, Rais John Magufuli anataraji kuondoa Wakuu wengi wa Mikoa na Wilaya kutokana na kukosa sifa, taarifa za uhakika zinasema. Mbali na wawakilishi wa Rais hao katika ngazi ya Mkoa na Wilaya, panga kubwa litawakumba wakurugenzi wa Taasisi na

Lowassa: Nilishinda Urais Lakini CCM Wakaupora Ushindi Wangu na Dunia Nzima Inajua

0
0
Aliyekua mgombea Urais anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, ameendelea kudai ndiye mshindi kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita na dunia inajua. Katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari kupitia msemaji wake, Aboubakary Liongo, Lowassa alisema ushindi wake uliporwa na kupewa mtu mwingine lakini amewataka Watanzania wasikate tamaa.

Rais Magufuli Awaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu Dar es Salaam

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, wazee na

Mwakyembe Aomba Apewe Muda......Azungumzia Katiba Mpya

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye ameapishwa leo na rais John Magufuli kushika wadhifa huo amewaomba wadau na wananchi kwa ujumla kumpa muda. Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa, Dkt. Mwakyembe ambaye alikuwa waziri wa wizara mbalimbali katika serikali ya awamu ya nne amesema kuwa anafahamu changamoto nyingi katika mfumo wa sheria ya nchi

CUF wapinga Uteuzi wa Prof. Muhongo

0
0
JUMUIYA ya Vijana wa Chama cha Wananchi (CUF) imesema wanasikitishwa na uteuzi wa baraza la mawaziri lililotajwa juzi na Rais John Magufuli na kudai  kuwa, katika baraza hilo wamerudishwa wale mawaziri waliokumbwa na kashfa za ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.    Pia imesema katika baraza hilo hakuna uteuzi  ambao umewiana hasa katika suala la usawa wa kijinsia na wala haukuzingataia

Waziri Wa Afya Na Naibu Wake Wafanya Ziara Za Kushtukiza Katika Hospitali Ya Mwananyamala Na Amana

0
0
Mwanasayansi wa Maabara ya Hospitali ya rufaa ya Amana, Jabir Mukhsin (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Dkt. Hamis Kigwangala kuhusu ubovu wa mashine inayotumika kufanya vipimo mbalimbali (MS4S) ikiwemo mzunguko wa damu mwilini ambayo kwa sasa imeharibika na kubakiwa na mashine moja ambayo ufanyaji wake wa kazi unachukua muda mrefu kutoa majibu sahihi. Na Rabi Hume, Modewjiblog

Profesa Muhongo Aahidi Kushusha Bei ya Umeme

0
0
WAKATI wapinzani wakipinga uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, waziri huyo amewasihi wananchi kumvumilia kidogo, ili baada ya muda mfupi atoe mpango wa maendeleo ya wizara hiyo, ambao pamoja na mambo mengine, utaelezea bei ya nishati hiyo itakavyoshuka.    Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo jana Ikulu jijini

Fredrick Sumaye Atangaza Rasmi kuwa Mwanachama wa Chadema.........Akabidhiwa Kadi na Mbowe

0
0
   Waziri  mkuu wa awamu ya tatu Mh.Fredirick Sumaye jana alitangaza  rasmi kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) na  akakabidhiwa kadi na Mwenyekiti  wa chama hicho Mh.Freeman  Mbowe.   Sumaye ambaye wakati wa uchaguzi alitangaza kujiondoa  CCM na  kudai  kuwa  anaunga mkono  mageuzi yanayofanywa na vyama  vinavyounda  katiba  ya  wananchi (UKAWA) bila  kuweka  wazi 

Je, Hawa Hawakufahamu Utoroshwaji Wa Makontena Bandarini?

0
0
Miongoni mwa mambo yanayotikisa duru za vyombo vya habari nchini Tanzania na nje ya nchi ni kuhusu ukwepaji wa kodi kupitia utoroshwaji wa makonte kutoka bandari ya Dar es Salaam.    Hadi sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya makontena 2,500 yalitolewa pasipo kulipiwa kodi stahiki kutoka bandari ya Dar es Salaam kati ya mwaka 2013 hadi 2015. Bandari ni shirika la Umma ambalo kwa muundo wa

Wafanyabiashara 15 Waliokaidi Agizo la Rais Kukiona Cha Moto

0
0
MAKAMPUNI 15 yaliyokwepa kodi baada ya kutorosha makontena yao, yamejisalimisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini yameshindwa kulipa kodi ndani ya siku saba za msamaha wa Rais John Magufuli. Kodi inayodaiwa kwa kampuni hizo ni Sh bilioni 3.75, hivyo watachukuliwa hatua za kisheria kwa kukwepa kulipa kodi, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani. Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Disemba 14

Serikali Imetoa Waraka wa ElimuBure......Shule 11 za Serikali Hazitahusika na Utoaji wa Elimu Bure

0
0
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Ufundi imetoa waraka wa elimu kuhusu elimumsingi bila malipo na kutoa orodha ya shule za msingi 11 za Serikali ambazo hazihusiki na utoaji wa elimu bure uliotangazwa na Rais John Magufuli.    Elimumsingi inajumuisha elimu ya awali, ya msingi na sekondari ambayo itaanza Januari mwakani. Katika Waraka Elimu Namba 6 wa Mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa elimu bure

Mufti Mkuu wa Tanzania 'Atumbua Majipu' Mengine.......Aivunja Mamlaka ya Usimamizi wa Msikiti Mkuu Arusha na Kuweka Mpya

0
0
Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Alhaji Abubakari Zuberi ameivunja mamlaka ya uendeshaji na usimamizi wa msikiti mkuu wa mkoa wa Arusha na kuweka mamlaka mpya ili kuimarisha utendaji.   Akitangaza maamuzi hayo kwa niaba ya mufti Sheikh mkuu wa mkoa wa Arusha Shabani Juma alisema anaamini kuwa mamlaka mpya iliyowekwa itafanya kazi kwa ufanisi na kwa kasi ya hali ya juu pamoja na kujipanua ili

Sumaye Akosoa Uamuzi Wa Rais Magufuli Kuhusu Wakwepa Kodi

0
0
Waziri Mkuu mstaafu ambaye juzi alichukua kadi ya uanachama wa Chadema, Frederick Sumaye ameukosoa uamuzi wa rais John Magufuli kuwasamehe watu waliorejesha kiasi cha fedha walichokwepa kulipa kodi. Sumaye alitoa mtazamo wake huo juzi  jijini Arusha baada ya kukabidhiwa kadi ya uachama wa Chadema ikiwa ni miezi takribani mitatu tangu alipojiunga na harakazi za Ukawa na kutangaza kuihama

Nape: Nitaanza Kushughulikia Sheria na Nidhamu Michezoni

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ameahidi kushughulikia sheria mbalimbali zinazosimamia sekta hiyo ili kuongeza nidhamu michezoni. Nape aliyeapishwa juzi kuanza kibarua hicho, ataiongoza wizara hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Dk Fenella Mukangara, huku ndoto za Watanzania zikiwa ni kuona kiwango cha michezo kilichoporomoka, kinakua. Akizungumza na mwandishi

Watumishi 15 wa Manispaa ya Bukoba Watiwa Mbaroni Kwa Ufisadi

0
0
Watumishi 15 wa Idara za Ardhi, Mipango Miji na Ujenzi katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera akiwemo Msanifu wa Majengo wa Manispaa hiyo, Abukar Issa, wanashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi dhidi ya tuhuma za kugawa hati ya ardhi kinyume cha Sheria ya Ardhi ya Mwaka 2004. Agizo la kuwakamata watumishi hao limetolewa na Mkuu wa Mkoa, John Mongella kutokana na kikao cha dharura

Tume Ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Yalaani Hatua za Wakuu wa Wilaya Kuwatupa Selo Watumishi Wa Umma

0
0
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRGG) imelaani hatua zilizoripotiwa kuchukuliwa na baadhi ya wakuu wa Mkoa na wakuu wa wilaya kuwaweka selo watumishi ambao wameshindwa kutimiza majukumu yao ya kikazi. Kwa mujibu wa tamko lililotolewa juzi na mwenyekiti wa CHRGG, Bahame Nyanduga, kamisheni hiyo ilipokea ripoti ya vitendo vya baadhi ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kutoa amri
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images