Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mgomo Dar: Kiwanda Cha Nguo Urafiki Chafungwa Kwa Muda

$
0
0
Jeshi la Polisi  Dar es Salaam  leo limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki ambao walifanya mgomo na kuufungia uongozi wa kiwanda hicho  ndani kwa madai ya kutolipwa ongezeko la mishahara yao kwa muda mrefu. Kutokana na Sekeseke hilo,Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ,Paul Makonda ameamuru kiwanda hicho kifungwe kwa muda ili kusaka suluhu

Watu Wawili Wafikishwa Mahakamani Kwa Kutaka Kumuua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva

$
0
0
WATU wawili wakiwemo Mwanasheria na Mwalimu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama za kumuua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva na familia yake. Washitakiwa hao, Mwalimu Samwel Gikaro (30) na Mwanasheria Angela Mbonde (32) walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa

Ada Elekezi kwa Shule Binafsi Kutolewa Desemba 15

$
0
0
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imewataka wazazi na walezi wenye wanafunzi wanaotegemea kuanza masomo au kuendelea na masomo katika shule binafsi mapema Januari mwezi ujao, kuvuta subira hadi Desemba 15, mwaka huu serikali itakapotoa maelekezo mbalimbali ikiwemo suala la ada elekezi. Akizungumzia hatua zinazofanywa hivi sasa na serikali kuhusu ada elekezi kwa shule binafsi, Katibu

Rais Magufuli Kukutana na Wafanyabiashara Leo

$
0
0
RAIS John Magufuli anatarajiwa kukutana na wafanyabiashara na wawekezaji jijini Dar es Salaam leo. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Rais kukutana na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji tangu aingie madarakani. Taarifa iliyotolewa jana na Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli atakutana na jumuiya hiyo Ikulu kwa nia ya kufahamiana na kuona namna ya

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Disemba 3

Mawaziri wa JK watajwa kuhusika Ufisadi wa Mabilioni

$
0
0
Watu tisa wakiwamo mawaziri wawili wa Fedha wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jakaya Kikwete wametajwa kushiriki kwenye kashfa ya rushwa ya Sh13 bilioni wakati Serikali ya Tanzania ilipokopa Dola za Kimarekani 600 milioni (Sh1.3 trilioni) kutoka benki ya Standard ya Uingereza.Ripoti ya Taasisi ya Kuchunguza Ufisadi (SFO) ya Uingereza iliyokuwa inafuatilia kashfa hiyo imewataja maofisa hao kuwa

Prof. Lipumba na wafuasi wake 30 Waachiwa Huru na Mahakama Ya Kisutu Leo

$
0
0
PROF. Ibrahim Lipumba, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ameachiwa huru na mahakama ya Hakim Mkazi, jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai nchini (DPP), imewasilisha hati maalum mahakamani hapo kueleza kutokuwa na dhamira ya kuendelea na mashitaka yanayomuhusu Prof. Lipumba na wenzake.Prof. Lipumba ameachiwa huru siku tatu baada ya kukutana na John Pombe

CHADEMA Wasema Magufuli Anatekeleza Sera za Wapinzani

$
0
0
Wakati Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli akionekana kuteka hisia za Watanzania wengi, Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  kimesema hakishtushwi kwani amekuwa akitumia  hoja, mikakati na Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho. Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu, amesema kuwa wakati wa kampeni Chadema ilieleza jinsi ya kupambana na  ufisadi, kuwa na utaratibu

Afisa Ardhi Morogoro Kapewa Siku 14 Za Kujieleza Kwa Nini Asifukuzwe Kazi

$
0
0
Katibu mkuu ofisi ya Waziri mkuu (TAMISEMI) Jumanne Sagini ametoa siku 14 kwa afisa ardhi, mhandisi wa majengo na Afisa mipango miji manispaa ya Morogoro kuandika maelezo ya kwanini wasifukuzwe kazi kutokana na kufanya kazi chini ya kiwango na kukiuka maadili ya utumishi wa umma Agizo hilo limekuja kufuatia watendaji hao wa serikali kutumia vibaya mamlaka waliyopewa na serikali ikiwemo

Taarifa Kwa Umma Toka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Rais Dkt. Magufuli atoa siku saba kwa wafanyabiashara wakwepa kodi.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.John  Pombe  Magufuli amewapa siku saba kuanzia tarehe 03/12/2015 wafanyabiashara wote ambao waliingiza mizigo yao bila kulipa kodi wakalipe kwani baada ya hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria   Hayo  yamesemwa leo Ikulu  jijini Dar es Salaam na Mheshimiwa Rais katika mkutano wake na wadau wa sekta binafsi  alipoamua kufanya

Breaking News: Waziri Mkuu Afanya Tena Ziara ya Kushtukiza Bandarini na TRL........Abaini Upotevu wa Makontena zaidi ya 2431

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo na utozaji wa malipo baada ya kupewa taarifa kwamba kuna makontena 2,431 yametolewa bila kulipiwa ushuru.   Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi wa bandari ya kuanzia Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita bila kulipiwa kodi

Mwanasheria Mkuu Awakana Wakuu Wa Mikoa Wanaositisha Likizo Za Watumishi

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amezungumzia suala la wakuu wa mikoa kutoa matamko ya kusitisha likizo za watumishi wa umma kwa kuwataka wafanye kazi tu. Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na kituo cha runinga cha Azam, Masaju amesema amekuwa akisikia kupitia vyombo vya habari kuhusu taarifa za kuwepo matamko hayo kutoka kwa baadhi ya wakuu wa mikoa.

[Audio] Kauli ya Januari Makamba kuhusu kumkejeli Rais Magufuli

$
0
0
January Makamba ameamua kutoa ufafanuzi wa picha mbalimbali zilizowekwa katika akaunti yake ya Instagram ambazo zinadaiwa kumkashfu Rais Magufuli baada ya kumnyima Uwaziri Mkuu. Hizi ndo Picha alizoweka ambazo zinadaiwa kumkejeli Rais Magufuli Picha hii inaonyesha   sokwe mtu wakiwa wamevalia suti  na  huyo mtu anayeonekana kurukia kamba huku nyuma ana mkia lakin akiwa amevalia kaptula

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Desemba 4


Magufuli: Sijachangiwa na Mfanyabiashara Yeyote Kuingia Ikulu.

$
0
0
Rais Dk. John Magufuli, amesema hakuna mfanyabiashara aliyemchangia  kumuwezesha kuingia Ikulu katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, ili aweze kusimamia ipasavyo makusanyo ya kodi kwa faida ya wananchi. Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji wa sekta binafsi, katika kikao cha pamoja

Kafulila atakiwa Kulipa Milioni 7.5 Kama Dhamana Ya Kesi Yake Ya Kupinga Matokeo Ya Ubunge

$
0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) kwa miaka mitano iliyopita, David Kafulila ameamriwa na Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora kulipa Sh7.5 milioni kama dhamana, ili ombi lake lakutaka itengue matokeo ya ubunge wa jimbo hilo yasikilizwe. Mahakama imetoa uamuzi huo kupitia kwa Jaji Leiyla Mgonya, baada ya kuzingatia maombi ya Kafulila aliyetaka apunguziwe gharama  ya fedha za

Magufuli Aitaka TRA Kutoa Mashine za EFDs Bure.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ameishangaa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kutogawa bure Mashine za EFDs, na wao kubaki na kazi ya kukusanya mapato. Akizungumza katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji jana jijini Dar es Salaam, ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), alisema muda uliopotea na kodi

Tahadhari Kuhusu Kuingilia Au Kufuatilia Mawasiliano Ya Watu

$
0
0
 MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA ISO 9001:2008 CERTIFIED TAARIFA KWA UMMA TAHADHARI KUHUSU KUINGILIA AU KUFUATILIA MAWASILIANO YA WATU *** Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa Programu (Application) ya simu ikijulikana kama SOFTBOX TANZANIA iliyosemekana iko kwenye Google PLAYSTORE. Ilidaiwa kuwa program (Application) hiyo ya SOFTBOX TANZANIA ilikuwa na

Gari la Magazeti ya Mwananchi Lapata Ajali....Wawili Wafariki Dunia Papo Hapo

$
0
0
WATU wawili wamefariki dunia Papo hapo baada ya Gari walilokuwa wakisafiria lililobeba Magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti kwenda mkoani mkoani Mbeya kupata ajali Eneo la Kitonga Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa. Ajali hiyo imetokea leo alfajiri baada ya dereva wa Gari hilo kujinusuru kugongana uso kwa uso na gari jingine, hivyo kulazimika kuingia nyuma ya lori na kupelekea kifo
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images