Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Pinda Akabidhi Rasmi Ofisi Kwa Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa

0
0
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkaribisha Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda  ambaye Novemba 30,2015 alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kukabidhi Ofisi. Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo  Pinda ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015 kukabidhi Ofisi.  Waziri

Magufuli Aitikisa Dunia Kwa Uchapakazi......Jina Lake Latawala Magazeti ya Marekani, Afrika Kusini na Australia

0
0
Kwa wiki ya pili sasa Rais Dkt Magufuli ameendelea kuwa gumzo barani Afrika na sasa hadi nchi za Ulaya zimedata naye. Gazeti kubwa la Marekani, The Guardian limeandika habari isemayo: What would Tanzania’s cost-cutting president do? Twitter responds. Pai  gazeti kubwa la  Australia,The Courier-Mail limeandika makala ndefu likimtaka Waziri mkuu wao,  Malcolm Turnbull ajifunze achapakazi

Update za Makontena 9 Yaliyokamatwa: TRA Imetoa Masaa 24 Kwa Mmiliki Wake Kujitokeza,Vinginevyo Watayataifisha

0
0
Mkurugenzi wa elimu kwa mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato nchini TRA Richard Kayombo ametolea ufafanuzi juu ya kukamatwa kwa makontena 9 katika eneo la Mbezi Tank Bovu jijini Dar es Salaam ambapo mpaka sasa hivi Makontena hayo pamoja na madereva waliokuwa wanayasafirisha yako chini ya ulinzi mpaka wahusika watakapojitokeza. Kayombo amesema kuwa makontena hayo yamenaswa usiku wa manane kwa

Sakata la Ufisadi Lililoibuliwa na Zitto Kabwe ......IKULU Yatoa Tamko,Yaitaka Stanbic Tanzania Ilipe Fidia ba Bilioni 13 Kwa Kufanya Udanganyifu

0
0
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue akiongea na Waandishi wa Habari leo 01 Disemba, 2015 katika Ofisi ya Mawasiliano Ikulu kuhusu Tanzania kurejeshewa dola za Marekani milioni 7( sawa na bilioni 13) katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Jijini Uingereza dhidi ya Benki ya Stanbink Tanzania. Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari leo 01

Baraza la Mawaziri la Magufuli ni Balaa......Yadaiwa Kila Waziri Atatia Saini Kukubali Masharti Yaliyowekwa na Magufuli

0
0
Kusuasua kwa Rais John Magufuli, kutangaza Baraza la Mawaziri kunatokana na msimamo wake wa kuwachambua watu anaotarajia kuteua katika nafasi hiyo huku akiaandaa mikataba ya makubaliano itakayokuwa mwongozo kwa mawaziri hao. Nia ya Rais, hadi kufikia hatua hiyo imetafsiriwa kwamba anataka kupata mawaziri ambao wataweza kwenda sambamba na kasi yake pamoja na wawajibikaji. Chanzo cha

CCM Yatoa Tamko Juu ya Kasi ya Rais Magufuli.....Yaahidi Kumpa Ushirikiano wa Kutosha ili Atekeleze Ilani Kikamilifu

0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitampa ushirikiano mkubwa, Rais Dk. John Magufuli, ili aweze kwa ufanisi zaidi mapambano yake dhidi ya mafisadi na mikakati mingine ya kuinua uchumi wa Watanzania. Kimesema, kitampa ushirikiano huo Rais Dk. Magufuli, kwa sababu, aliyoanza kuyafanya na atakayoyafanya baadaye katika uongozi wake wa Urais anatekeleza yale yaliyomo katika ilani ya Uchaguzi

Taarifa Rasmi ya IKULU Kuhusu Sakata la Ufisadi wa Mabilioni katika Serikali ya JK Lililoibuliwa Jana

0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI ______________________ 1.0  Utangulizi 1.1 Jana, tarehe 30 Novemba, 2015, mahakama jijini London ilitoza Standard Bank $ 32.2 milioni. Kati ya hizo $ 16.8 milioni ni faini inayolipwa kwa Serious Fraud Office (SFO), $8.4 milioni ni “disgorgement of profits”; na $ 7 milioni zinalipwa kwa Serikali ya Tanzania. Fedha hizo ni $ 6 milioni ambazo tulitozwa

Sad News: Basi la Takbir Lagongana na Lori Usiku Huu na Kuua Watu Kadhaa

0
0
Habari zilizotufikia usiku huu zinaarifu kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha katika ajali mbaya iliyotokea baada ya basi la abiria la Takbir lenye namba za usajili T 230 BRJ lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana na lori eneo la Shelui, kijiji cha Kizonzo omkoani Singida.

Mrema Asema Hajutii Kumnadi Rais Magufuli

0
0
MWENYEKITI wa Taifa wa chama cha siasa cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema amesema hakufanya makosa na wala hajutii kumnadi Rais John Magufuli kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa sababu alitambua Watanzania wamelamba dume la maendeleo. Akizungumza na mtandao huu jana mjini Moshi, Mrema alisema Watanzania wamepata mtu wa kuendeleza kazi aliyokuwa akiifanya kipindi yeye wakati

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Disemba 2

Kafulila Aanza Vizuri Kesi Yake Ya Kupinga Matokeo Ya Ubunge Baada Ya Pingamizi Kutupiliwa Mbali Na Mahakama

0
0
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na David Kafulila dhidi ya washtakiwa; Husna Mwilima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya uvinza kama msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa Serikali ilipokea pingamizi toka kwa wakili wa Husna Mwilima kutaka Mahakama Kuu isiendelee na kesi hiyo kwakuwa Mhe Kafulila

Dr. Slaa Ammwagia Sila Rais Magufuli Kwa Kasi Aliyoanza Nayo

0
0
Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini. Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli. “Nadhani sasa unaelewa niliposhikilia msimamo wangu. Katika mazingira ya sasa Magufuli ni bora zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa siku za

Wafuasi wa CCM na UKAWA Wachapana Makonde Wilayani Masasi

0
0
Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wilayani Masasi, mkoa wa Mtwara wamechapana makonde kufuatia mzozo wa kisiasa ulioibuka kati ya vyama hivyo. Kufuatia vururugu hizo, polisi waliingilia kati na kufyatua risasi hewani kuwatawanya. Wafuasi hao walichapana makonde pamoja na kurushiana mawe jana katika maeneo ya T.K, kwenye

Pinda Avutiwa Na Kasi ya Dr. Magufuli......Awataka Watanzania Wazidi Kumuonbea

0
0
Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, amesema ameridhishwa na kasi ya utendaji kazi ambayo Rais Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim, wameanza nayo na kwamba ana imani kwa uchapakazi na uadilifu wao, wataivusha Tanzania na kuifikisha kwenye uchumi wa kati ambako serikali imejielekeza kufika. Pinda amesema yeye anaona kasi hiyo ya utendaji inayochukuliwa na serikali ya awamu ya

Tajiri Anayemiliki Makontena Yaliyopotea Bandarini Ajitokeza......Amtupia Lawama Wakala Wake

0
0
Tajiri huyo anayetambulika kwa jina la Nassoro Ahmed bin Slum anayemiliki kampuni ya Bin-slum Tyres Ltd, amejitokeza na kukiri kumiliki baadhi ya makontena yaliyokumbwa na kashfa hiyo lakini  amekana kosa lenye sura ya kukwepa kodi  akidai kuwa limefanywa na wakala wake. “Wafanyabiashara hatuna mamlaka ya kulipa kodi moja kwa moja serikalini. Tunalipa kodi kupitia kwa wakala

Balozi Sefue Awaagiza Watumishi Wa Umma Kuvaa Beji Zenye Majina Yao Wawapo Katika Maeneo Yao Ya Kazi

0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa  katika maeneo  ya  kazi. Mhe. Balozi Sefue aliutoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine. Alisema mwishoni mwa

Mkuu wa Mkoa Mwanza aigomea Mwauwasa Kuongeza Bei Ya Maji

0
0
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amepinga hatua za Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa) kuongeza bei ya maji kwa madai ongezeko hilo litasababisha wananchi wengi kukosa huduma. Mulongo alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mwauwasa, namna wanavyotoa huduma kwa wananchi, changamoto zinazowakabili pamoja na mafanikio ya mamlaka hiyo. Hivi

Watuhumiwa wa Kobe Wafikishwa Mahakamani

0
0
Wakazi watano wa Zanzibar wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ya kusafirisha kobe 201 aina ya India wenye thamani ya Sh30 milioni. Wakili wa Serikali Ester Martin akishirikiana na Neema Mwanga, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni David Mungi (36), Mustafa Bakar (43), Mohammed Seleman (43), Salum Wakili (30) ambao ni wafanyabiashara na mvuvi, Shaban Haji (45).

Taarifa Kwa Wananchi Wote Kuhusu Majina Sahihi Ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa (Pichani) anatumia majina matatu kama ifuatavyo: Kassim Majaliwa Majaliwa au Kassim M. Majaliwa. Tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, kumekuwa na uchanganyaji wa majina yake na hii ni kwa sababu tangu akiwa chuoni na jeshini, alikuwa akitanguliza kutaja ubini (jina la ukoo) na ndiyo maana ikawa inasomeka Majaliwa Kassim

Habari Mpya Toka Wizara ya Afya : Milioni 500 Zaokolewa kwa Wagonjwa wa Moyo ,Mashine za CT Scan na MRI zimeanza Kufanya Kazi

0
0
Baada ya agizo la Rais John Magufuli kutembelea hospitali ya Taifa Muhimbili..aliagiza badhi ya mambo kufanyiwa utekelezaji ikiwemo mashine za CT Scan na MRI ambazo zilikuwa na matatizo kutengenezwa ili kuwasaidia wagonjwa. Leo Katibu mkuu wa Wizara ya Afya Donan Mbando ametembelea hospitali hiyo na kukagua maeneo mbalimbali na kuzindua duka la dawa la MSD pamoja na kukagua mashine za CT
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images