Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mbatia Amkaanga Dr. Slaa.......Ampa Makavu Samweli Sitta

0
0
MWENYEKITI Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, amewataka Watanzania kumpuuza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa kwa kauli zake zilizojaa uchochezi na propaganda za siasa. Pia alionya kauli za ovyo zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba wapinzani wakishinda vyombo vya ulinzi

Rostam Aziz Amrushia Makombora Dk. Slaa.

0
0
Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, amemvaa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akimuita kuwa ni mtu mwongo, mbinafsi na mpotoshaji mkubwa. Rostam alieleza hayo katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi yake jijini Dar es Salaam juzi, alipozungumza na vyombo vya habari

Magufuli: Polisi Atakaeua Jambazi Hatashtakiwa.

0
0
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema serikali yake haitamshtaki askari polisi ikiwa ataua jambazi mwenye silaha. Mgombea huyo alitoa ahadi hiyo jana katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye  uwanja wa Mashujaa, mjini Mtwara. “Katika serikali yangu askari akimpiga jambazi mwenye silaha kwa risasi hashtakiwi.

Mke wa Dr. Slaa Amwaga Mboga......Asema Slaa ni Muongo, Dhaifu na Anatumiwa na CCM

0
0
Mke wa zamani wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, Rose Kamili jana aliibuka na kumtuhumu mzazi mwenzake huyo kwamba anatumiwa kuvuruga upinzani katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu. Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamili alitamka bila kuthibitisha moja moja kwamba mumewe huyo wa

Lowassa aahidi kuchunguza upya Sakata la Operesheni Tokomeza

0
0
Mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa Awamu ya Tano, ataunda tume tatu ikiwamo ya kuchunguza upya sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili ambalo utekelezaji wake ulilalamikiwa na wananchi. Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili mjini Mpanda mkoani hapa, Lowassa alitaja

Tanesco Yamshtaki Askofu Gwajima Polisi

0
0
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeishtaki polisi Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kutokana na kuharibu miundombinu ya umeme katika maeneo ya shirika hilo Jumamosi iliyopita na kusababisha umeme kukatika kwa baadhi ya mikoa na Jiji la Dar es Salaam. Kutokana na kukatika kwa umeme kwa muda huo, shirika limepata hasara ya zaidi ya Sh milioni 30 ambayo

Vijana 100 Arusha Wanaomuunga Mkono Dr. Slaa Wahama UKAWA na Kujiunga ACT-Wazalendo

0
0
WANACHAMA zaidi ya 100 wa Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF wameandamana mjini Arusha na kuchoma moto bendera na kadi za vyama hivyo, wakimuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa. Watu hao waliandamana jana na maandamano hayo yamefanyika siku mbili baada ya Dk Slaa kutangaza hadharani, Dar es Salaam kuwa ameachana na siasa. Wakiwa katika maandamano yaliyoambatana na

Gaeti la Mwanahalisi Lafungulia Rasmi.......Kubenea Ashinda Kesi Mahakama kuu

0
0
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imesema Waziri wa Habari, Dk. Fennela Mkangara hakufuata utaratibu wa kisheria katika kulifungia gazeti la MwanaHALISI Julai 30 miaka mitatu iliyopita.    Jaji Salvatory Bongole amesema Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 aliyoitumia kufungia gazeti hilo lililokuwa linachapishwa kila Jumatano na kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), inaelekeza kuwa pamoja na

Godbless Lema Aachiwa Kwa Dhamana.

0
0
Mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema na wenzake wanne wameachiliwa kwa dhamana jana baada ya kushikiliwa na polisi  juzi. Polisi mkoani Arusha walimkamata mwanasiasa huyo pamoja na watu wengine wanne juzi jioni mara baada ya kuzindua kampeni yake ya kuwania ubunge katika jimbo hilo kwa awamu ya pili katika Shule ya

Picha 6: Lowassa Aendelea na Ziara zake za Kampeni Mkoani Kigoma

Mgombea Mwenza wa CCM Aahidi Makubwa kwa Bodaboda

0
0
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi kuanzisha madawati maalumu katika Manispaa za Dar es Salaam kwa ajili ya kusajili madereva wa bodaboda na bajaji, iwapo chama chake kitachaguliwa katika uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu. Akizungumza katika mikutano ya kampeni katika Viwanja vya Mbezi Centre, Jimbo la Kibamba, wilaya ya Kinondoni, viwanja vya

Mashehe waliotekwa DRC warejea Dar

0
0
MASHEHE sita waliokuwa wametekwa na waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC) wamerejea nchini jana, huku wakieleza kuwa kulitaja jina la Tanzania kumewaokoa na kifo kutoka kwa waasi hao. Kitendo cha mashehe hao kutaja wanatokea Tanzania kimewasaidia kwani kwa mujibu wao, waasi hao walisema hawana shida na Tanzania, lakini Wakongo waliwadanganya hivyo hawawapendi. Akizungumza

UVCCM yataka Ukawa wasitafute mchawi

0
0
Katibu Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano Umoja wa Vijana wa CCM, Egla Mamoto amesema Ukawa wasitafute mchawi kwa kuwa wanavurugana wenyewe kwa wenyewe. Akitoa tathimini ya kampeni za uchaguzi zinazoendelea za mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli alisema kuwa wao kwa sasa wamejielekeza katika kutafuta kura na kunadi sera zao. Akitoa tathmini ya kampeni katika mikoa sita aliyozunguka

Mabango ya LOWASSA Yazua Kizaazaa

0
0
Mabango yenye picha ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, yanayoendelea kubandikwa katika maeneo mbalimbali nchini yamezua kizaazaa, baada ya mengine kuondolewa na wale wanaofanya kazi ya kuyaweka kutishwa na hata kuwekwa ndani na Jeshi la Polisi. Hali hiyo imejitokeza mkoani Iringa, ambako vijana wanaofanya kazi ya kuweka mabango hayo

Magufuli awahakikishia neema wahandisi wazawa

0
0
Waziri  wa Ujenzi, Dk John Magufuli amewahakikisha wahandisi kwamba endapo atachaguliwa kuwa Rais wa serikali ya Awamu ya Tano hatawaangusha na atahakikisha anawatumia vyema kwa ajili ya kujenga uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati. Dk Magufuli ambaye pia ni mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akifunga maadhimisho ya Siku ya Wahandisi

‘Ukomedi’ Wamsaidia Kingwendu Kuomba Kura Jimbo la Kisarawe

0
0
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kisarawe kupitia Cuf, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ juzi alikuwa kivutio wakati akitambulishwa na mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri, Juma Duni Haji. Juma Duni Haji ni mgombea mwenza wa Edward Lowassa anayegombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, lakini wakiwa chini ya mwamvuli wa vyama vinavyounda Ukawa (Chadema, Nccr-Mageuzi,

Lipumba Akana Kutumiwa na CCM Kuvuruga Upinzani

0
0
Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema wanaodhani wanatumika CCM wamekosa mwelekeo kwani alikuwa kinara wa kuitaka itoke madarakani. Profesa Lipumba aliyekuwa mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alijiengua kwenye wadhifa huo kwa kile alichodai nafsi yake itamhukumu kwa kumkaribisha kundini, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

Mke Mdogo wa Dr. Slaa Naye Ajibu Mapigo......Asema Mumewe ameachana na Siasa na Anampango wa Kuwekeza Katika Shule na Hospitali

0
0
Hatimaye mke mdogo wa Dk. Willibrod Slaa, Josephine Mushumbusi, ameibuka na kujibu baadhi ya hoja ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake yeye binafsi na kwa mume wake na zaidi akisema yote yanayosemwa dhidi yao hayako katika fikra zao kwani kwa sasa baada ya kuachana na siasa wanajipanga kuelekea upande mwingine wa kuwa wawekezaji. Akizungumza na gazeti  la  mtanzania jana, Mushumbusi

Mzindakaya: Msipige Kura kwa Ushabiki

0
0
MWANASIASA mkongwe nchini na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Chrisant Mzindakaya amewataka Watanzania wasikubali kupiga kura kwa ushabiki. Ameonya kuwa upigaji kura kwa ushabiki, utaligharimu taifa hivyo Watanzania wapige kura wakijua wanachagua kiongozi ambaye atawakilisha nchi kitaifa na kimataifa. Mzindakaya alisema hayo jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wake na waandishi

Kinana Amsafishia njia Magufuli

0
0
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameongoza timu ya chama hicho kumsafishia njia Mgombea Urais wao, Dk John Magufuli mkoani Kilimanjaro, huku akiwaambia wananchi wa mkoa huo kuwa mgombea huyo ndiye kiongozi anayestahili kuongoza Tanzania. Akizindua kampeni za CCM mjini Moshi, Kinana aliongozana na mgombea ubunge wa Jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images