Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais wa Sudan Omar al- Bashir Azuiliwa Kuondoka Afrika Kusini

0
0
Hakimu wa Afrika Kusini ameamuru serikali ya nchi hiyo kumzuia Rais Omar al- Bashir wa Sudan ambaye yuko Afrika Kusini kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Afrika kuondoka nchini humo.. Jaji Hans Fabricuis amerefusha amri ya kuzuiliwa kuondoka kwa rais huyo hadi hapo itakapotowa maamuzi ya mwisho leo Jumatatu na kuitaka serikali kuchukuwa hatua zote muafaka kumzuia la Bashir al-

Ajali Mbaya ya Coaster na Lori Yaua 23 na Kujeruhi 34 Iringa.

0
0
WATU   23 wamepoteza maisha na wengine 34 wamejeruhiwa  usiku   wa  kuamkia  leo baada ya  gari aina  ya costa mali ya Another G inayofanya  safari  zake kati ya Njombe na  Iringa kugongana  na Lori mkoani Iringa.Ajali hiyo imetokea  eneo la Kinyanambo nje  kidogo na mji wa Mafinga wilaya ya  Mufindi  mkoani Iringa wakati  gari hiyo ya Another G ikitokea  Iringa   kwenda  NjombeMkuu  wa

Wanawake Washauriwa Kuepuka Rushwa ya NGONO Kwenye Uchaguzi

0
0
Wanawake nchini wametakiwa kuacha kutumia rushwa ya ngono ili waweze kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi bali watumie uwezo wao kupambana ili waweze kushika nafasi za juu kwenye ngazi za maamuzi. Hayo yalibainishwa na aliyekuwa mbuge wa Ukerewe (CCM), Balozi Getruda Mongela (pichani), wakati alipokuwa akifungua kongamano la kitaifa la wanawake mjini Dodoma. Alisema mwanamke

Shindano la Fanya Kweli Kiwanjani Lafikia Tamati......Baa ya Kinondoni M.K Pub Yaibuka Kidedea

0
0
Bi.Johari Haiman (kushoto) akipokea zawadi toka kwa wahudumu wa tusker wakati wa sherehe ya kuipongeza MK Pub ya kinondoni baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa mwisho wa shindano la Fanyakweli Kiwanjani lililokuwa likidhaminiwa na bia ya Tusker. ****** Shindano la Fanya Kweli Kiwanjani limefikia tamati kwa jiji la Dar es salaam huku wapenzi wa bia ya Tusker wakishuhudia baa ya Kinondoni

Rais Bashir wa Sudan aondoka Afrika Kusini pamoja na kuziwa na Mahakama

0
0
Omar Al Bashir, Rais wa Sudan ameripotiwa kuondoka Afrika Kusini pamoja na kuwepo kwa amri ya mahakama ya nchi hiyo kumzuia kuondoka. Awali ndege ya Al Bashir iliripotiwa kuwa ilikuwa imetoweka katika kiwanja cha ndege Johannesburg na kuhamishiwa katika kiwanja cha jeshi nchini humo. Tayari mtandao wa habari wa AFP umeripoti kuwa Rais Bashir ameshatua mjini Khartoum, Sudan.

Wema Sepetu Atoa Sababu kwanini HATOMSAMEHE Kajala Masanja

0
0
Kwa muda mrefu sasa hivi watu wanaofatilia habari za mastaa wa bongo wanafahamu kwamba Waigizaji Wema Sepetu pamoja na Kajala ambao walikua marafiki mpaka Wema akamuokoa Kajala kwenda Jela kwa kumlipia faini ya MILIONI 13, hawapatani sasa hivi hata wakikutana hawasalimiani.    Wema Sepetu alikutana na Zamaradi Mketema kwenye show ya CloudsTV (TAKE ONE) na kuongea mengi kuhusu Kajala

Waziri wa Habari Na Michezo Atuma Salamu Za Rambi Rambi Kwa Baraza Kuu La Waislamu Kufuatia Kifo Cha Sheikh Mkuu wa Tanzania

0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Mb.) ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA) na Waislamu wote nchini kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni 15,2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa. Katika salamu hizo, Mhe.

Bunge Latoa Ufafanuzi Kuhusu VICOBA

0
0
Ofisi ya Bunge imebaini uwepo wa Waraka usiokuwa na Nambari ya Kumbukumbu wala Tarehe wenye kichwa “KUIDHINISHWA KWA MFUKO WA FOCUS VICOBA” unaosambaa kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao maarufu ya Facebook na WhatsApp. Waraka huo una maneno yafuatayo:   “Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linaidhinisha na kutambua uwepo wa mfuko wa utoaji mikopo FOCUS VICOBA. Viongozi wakuu

Rais Kikwete Atuma Salamu za Rambi Rambi kwa Waislam Wote na Bakwata Kufuatia Kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania.

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Waislamu wote nchini na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA)) kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania  Mufti Sheikh  Issa Bin Shaaban Simba. Marehemu Mufti amefariki  leo 15/6/2015 asubuhi katika hospitali ya TMJ – DSM alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu (pressure). "Kifo kinaleta

Mwili wa Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba Kusafirishwa Kesho Kwenda Mkoani Shinyanga Kwa Taratibu za Mazishi

0
0
MWILI wa  Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba unataraji kusafirishwa kesho Jumanne Juni 16, kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya taratibu za mazishi. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj  Mussa Salum, amesema mwili wa marehemu utaswaliwa kesho katika Msikiti wa Msilimu, viongozi

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Tarehe 16 Juni 2015

0
0
Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Jumanne  ya  Tarehe 16 Juni 2015

Magereza yaaswa kuruhusu wafungwa kujiandikisha BVR

0
0
JESHI la Magereza nchini limeshauriwa kuhakikisha wanaruhusu wafungwa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo wa kielektroniki (BVR), unaosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Hatua hiyo ni kuwawezesha kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi katika uchaguzi ujao. Rai hiyo ilitolewa jana na Mratibu wa marafiki wa Waziri Mkuu wa zamani,

Akina Mama Waandamana Kudai miili ya Waliouawa na Askari Kwa Kupigwa Risasi Mkoani Simiyu

0
0
KINAMAMA kutoka Kata ya Bukundi Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, wameandamana hadi kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Erasto Sima, kushinikiza wapewe miili ya vijana wao wawili waliouawa na askari Mei 29, mwaka huu.   Vijana hao Gineu Gidahasi na Gitienga Gidahasi ambao ni ndugu wa familia moja wanadaiwa kupigwa risasi na askari wa Kampuni ya ulinzi ya Mwiba Holding kwa madai ya kuingiza mifugo eneo

Wema Sepetu, Jokate Waungana Kumpiga Vijembe Diamond

0
0
Mwigizaji Wema Sepetu na staa wa single ya ‘leoleo‘ Jokate ambao wamekuwa  mapenzini na Diamond Platnumz kwa nyakati  tofauti baada ya kutolewa tuzo za KILI 2015 nchini Tanzania ambako Ali Kiba alipata ushindi wa tuzo nyingi kuliko yeyote mwingine usiku huo walitumia page zao kumpongeza Kiba kwa kuandika maneno yafuatayo.    Jokate ambaye anatajwa kuwepo mapenzini na Ali Kiba sasa hivi

Wakili Akanusha Kumtesa "House Girl"

0
0
WAKILI wa kujitegemea Yasinter Rechungura (45), ametoa ushahidi Mahakamani na kudai kwamba aliyekuwa mfanyakazi wake wa ndani Merina Mathayo (16), hakuwahi kumpiga wala kumjeruhi badala yake  alijeruhiwa wakati akichota maji katika SIMTANK lililopo nyumbani kwake Boko Magengani.   Yasinter alitoa ushahidi huo jana Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam mbele ya Hakimu Amalia

Majambazi Yauawa Jijini Dar

0
0
MAJAMBAZI watatu wameuwawa katika matukio mawili tofauti Jijini Dar es Salaam, likiwamo la majambazi wawili kufariki dunia baada ya kujibizana  kwa risasi na Polisi.   Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana, Naibu Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simoni Sirro, alisema tukio hilo lilitokea juzi katika eneo la Mbagala Charambe wakiwa na silaha mbili ambazo ni Mark IV yenye

Basi la timu ya Taifa, Taifa Stars Lapigwa Mawe.

0
0
Watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe basi la timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam. Basi hilo lililokuwa limebeba baadhi ya wachezaji wa timu hiyo waliokuwa wakitoka mazoezini uwanja wa Karume, lilishambuliwa kwa mawe na watu wanaosadikiwa kuwa mashabiki wenye hasira.   Taifa Stars juzi ilifungwa mabao 3-0 na Misri katika

Rais Kikwete Aongoza Maziko ya Sheikh Mkuu wa Tanzania Muft Issa Shaaban Simba

0
0
Rais Jakaya Kikwete  jana jioni  ameongoza maziko ya sheikh mkuu wa Tanzania Muft Issa Shaaban Simba aliyefariki jana katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam. Maziko hayo yalifanyika katika makaburi ya waisilamu ya nguzo nane mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Shinyanga wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo Ally Nassoro Lufunga. Mwili wa marehemu uliwasili nyumbani

Urais 2015: Mtwara Wajitokeza Kwa Wingi Kumdhamini Magufuli

0
0
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika  mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mtwara. Mchakato wa udhamini ukiendelea kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Mtwara mjini.

Urais 2015: Pinda Aiteka Katavi.......Apata Wadhamini 9, 141

0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wanaCCM waliofika kwenye Ofisi ya CCM ya kata ya Kibaoni kumdhamini katika nia yake ya kuwania uteuzi wa CCM katika kugombea nafasi ya urais Juni 15, 2015. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimian na baadhi ya wananchi wa Mpanda waliofika kwenye ofisi ya CCM ya Wilaya ya Mpanda kushuhudia na kumdhamini ilia pate sifa za kuteuliwa kuwa
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images