Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Urais 2015: Profesa Lipumba Kuchukua Fomu ya Urais Jumapili ya Wiki hii.......Tukio hilo Litarushwa Moja Kwa Moja na Runinga Kadhaa

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa  Ibrahim Lipumba, Jumapili atachukua fomu ya kugombea urais ndani ya chama hicho na atawaeleza Watanzania sababu ya kuwania nafasi hiyo.    Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Shaweji Mketo alisema, Profesa Lipumba ndiye mgombea pekee wa urais aliyetangaza nia ya kuwania nafasi hiyo.   Alisema muda wa

Urais 2015: Benard Membe Anusurika Kufa Baada ya Ndege yake Kutaka Kugongana "Uso kwa Uso" na Ndege Nyingine

$
0
0
Mio  za kuwania kumrithi Rais Jakaya Kikwete miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimezidi kushika kasi, safari hii Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akinusurika kifo baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kuwapo katika hatari ya kugongwa na ndege nyingine angani alipokuwa akielekea Zanzibar.   Waziri Membe akiwa na ujumbe wake wa watu nane

Urais 2015: Kambi Ya Lowassa Yazidi Kutanuka........Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Atangaza Rasmi Kumuunga Mkono Edward Lowassa

$
0
0
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Steven Masele, ametangaza kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika harakati zake za kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).   Masele aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini kabla ya Baraza la Mawaziri kuvunjwa, jana aliibukia katika mkutano wa kutafuta wadhamini wa Lowassa uliofanyika mjini

Urais 2015: Pinda achukua fomu, apanga kukuza uchumi

$
0
0
Waziri Mkuu , Mizengo Pinda akiwa ameshika fomu ya kuwania uteuzi wa CCM ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma Juni 12, 2015. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitia saini kitabu baada ya kuwasili kuwasili kwenye Ofisi Kuu ya CCM mjini Dodoma kuchukuwa fomu za kuwania uteuzi wa CCM ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Lowassa Azidi Kuvunja Rekodi.......Msafara Wake Waingia Tabora Kwa Kishindo, Apata Wadhamini 9516

$
0
0
Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM waliofika kumdhani pamoja na wananchi wa Mji wa Tabora, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015. Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wana CCM waliofika kumdhamini pamoja na wananchi wengine, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora

Kortini kwa Kumpa Mwanafunzi Mimba

$
0
0
MKAZI wa Mpiji Magoe Hamis Mohameid (21), amefikishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Dar es Salaam akikabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanafunzi (14)Jina limehifadhiwa na kumpa mimba.   Akisomewa mashtaka mawili mbele ya Hakimu Flora Mtarania, Wakili wa Serikali Grace Lwila, alidai kuwa tukio hilo lilitokea  kati ya Aprili na Mei24 mwaka huu maeneo ya huko Mpiji

Sita wafa katika ajali, 45 wajeruhiwa Singida

$
0
0
WATU sita wamekufa na wengine 45 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti za barabarani zilizotokea juzi na jana mkoani Singida.   Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema mjini hapa jana kuwa ajali ya kwanza ilitokea Juni 11 mwaka huu saa 1.30 usiku eneo la Manga nje kidogo ya mji huu kwenye Barabara Kuu ya Singida – Mwanza.   Alisema ajali hiyo ililihusisha

Atuhumiwa Kuiba Mtoto.

$
0
0
MAMA wa mtoto aliyeibwa kabla hajatimiza mwezi tangu azaliwe, Fatuma Bakari ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jinsi mtoto huyo alivyoibwa na mshtakiwa Neema Patrick.   Shahidi huyo na mwingine walitoa ushahidi wao jana mbele ya Hakimu Adelf Shachore kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali, Anunciata Leopold.   Awali mashahidi hao walikuwa watano ambao walifika mahakani  kwa ajili ya

Orodha kamili ya washindi wa Kilimanjaro Music Awards 2015........Ali Kiba Kashinda Tuzo 5, Diamond 2

$
0
0
Hii ni orodha kamili ya washindi wa tuzo za muziki Tanzania Kilimanjaro Music Awards 2015 zilizofanyika 13 June 2015 Mlinani City jijini Dar es salaam. 1. KIKUNDI BORA CHA MWAKA - BONGO FLEVA - YAMOTO BAND   2. KIKUNDI BORA CHA MWAKA TAARAB - JAHAZI MODERN TAARAB   3. BENDI BORA YA MWAKA - FM ACADEMIA   4. MSANII BORA CHIPUKIZI - BARAKA DA PRINCE   5. WIMBO BORA

Mafuriko Ya Lowassa Yatua Kigoma......Azoa Wadhamini 11,250

$
0
0
Umati wa WanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Kigoma, ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma, kuja kumuona Mh. Edward Lowassa (anaeonekana kule mbele) wakati alipofika kuomba udhamini wa wanachama wa CCM, ili aweze kupata ridhaa ya Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.    Mh. Lowassa alipata udhaminiwa na

Shule yafungwa kwa hofu ya simba mla watu

$
0
0
SHULE ya Msingi Saadani Chumvi iliyopo Kata ya Mkange wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, imefungwa baada ya wazazi kuwa na hofu baada ya watu wawili na mbuzi 70 kuliwa na Simba kutoka kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani.   Shule hiyo ambayo iko jirani na hifadhi hiyo ilifungwa mwishoni mwa mwaka jana kutokana na matukio hayo hali ambayo ilisababisha wazazi kuogopa watoto wao kudhuriwa

Lowassa Kumzuia Serukamba Kugombea Ubunge

$
0
0
WAZIRI Mkuu mstaafu Edward Lowassa amesema huenda akamzuia Mbunge wa Jimbo la Kigoma, Peter Serukamba kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu ili amsaidie jukumu muhimu kwenye safari yake ya matumaini.   Akizungumza wakati wa kuomba udhamini kutoka kwa wanachama wa CCM mkoa Kigoma katika ofisi kuu ya CCM mkoa, Lowassa alisema Serukamba ni mmoja wa wanakamati katika

Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo Kujulikana Agosti 10

$
0
0
MGOMBEA wa Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu kupitia chama cha ACT-Wazalendo, anatarajia kujulikana Agosti 10 mwaka huu.   Atakayebahatika kupeperusha bendera ya ACT-Wazalendo pia atawajibika kuwa tayari kutangaza mali binafsi na vyanzo vyake kwa kutokana na utaratibu ulioainishwa katika sehemu ya sita ya nyongeza ya kwanza ya Katiba ya Chama hicho.   Hayo yalisemwa jana mjini

Yamoto Band kutimkia kwa GodFather

$
0
0
Kundi la muziki wa bongo flava nchini, Yamoto Band wanatarajia kukwea pipa kwenda Afrika Kusini kwa ajili yakufanya video ya wimbo wao ‘Cheza kwa Madoido’ na muongozaji mahili barani Afrika, Godfather.   Yamoto Band ambao usiku wa kuamkia jana walitwaa tuzo ya Kili katika kipengele cha ‘Kikundi bora cha muziki (Bongo Flava) wameamua kwenda Afrika Kusini kufanya video ikiwa ni hatua

Dk Asha-Rose Migiro Ajitosa Kuwania Urais Kupitia CCM......Samuel Sitta Kurudisha Fomu ya Urais Leo

$
0
0
WAZIRI wa Sheria na Katiba, Dk Asha-Rose Migiro leo anatarajia kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).   Aidha, taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii, kuwa Waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein kuwa atachukua fomu si za kweli kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya CCM.  

Urais 2015: Wanachama CUF waitikisa Dar, Prof. Lipumba Achukua Fomu ya Urais........Aweka Hadharani Vipaumbele Vyake

$
0
0
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba jana alianzisha mchakato wa kuwania urais kupitia muungano wa kambi ya upinzani nchini unaofahamika kama Ukawa, huku akisema yeye ndiye mtu pekee anayefaa kupeperusha bendera ya vyama vya upinzani.   Akitangaza azma yake ya kuwania urais baada ya kuchukua fomu jijini Dar es Salaam, alisema kutokana na kubobea katika

Rais Obama Kupelekewa ‘kifimbo’ cha Nyerere

$
0
0
RAIS wa Marekani, Barack Obama anatarajiwa kuwa kiongozi wa tatu duniani kuanza kubeba kifimbo kama kile cha Mwalimu Nyerere ambacho tayari kimechongwa kwa ajili yake na msanii yule yule aliyetengeneza fimbo ya Baba wa Taifa.   Kiongozi wa pili kukabidhiwa ‘kifimbo cha uongozi,’ kama kile cha Nyerere alikuwa ni Rais Jakaya Kikwete aliyepewa rasmi fimbo yake mwishoni mwa wiki mjini

Lowassa Aendelea Kupata Maelfu ya Wadhamini Mikoa ya Katavi na Rukwa.

$
0
0
Waziri mkuu wa zamani Mh. Edward Lowasa ameendelea na ziara yake ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Katavi na Rukwa na kupata   maefu ya wadhamini na amewataka waananchi waliojiandikisha kutunza vizuri shahada zao kwani ndio tiketi ya kuwawezesha kufikia ndoto zao za kuchagua kiongozi wanayemtaka.   Mh. Lowasa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda na kupata mapokezi

Faiza Ally Awaacha Watu hoi Tuzo za Kill 2015

$
0
0
Mwanadada faiza ally  amezua gumzo kwenye fainali  tuzo za Kilimanjaro music Award zilizofanyika usiku wa  kuamkia jana  katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.   Mwanadada huyo alitinga kwenye Red kapeti tuzo za kili akiwa na vazi linao onesha baadhi ya sehemu za makalio zikiwa wazi kama ambavyo anao onekana katika picha hapo chini suala lililozua minong’ono kwa baadhi

Tanzia: Mufti Issa Bin Shaaban Simba( Kiongozi Mkuu wa Waislamu nchini Tanzania) Afariki Dunia

$
0
0
Kiongozi Mkuu wa Waislamu nchini Tanzania, Mufti Issa Bin Shaaban Simba amefariki dunia leo asubuhi akiwa Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa.   Marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari pamoja na shinikizo la damu.   Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images