Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Fisi akwapua mtoto mgongoni kwa mamaye

$
0
0
Mtoto  wa miezi mitatu, Ng’wanza Samweli, amekufa baada ya kukwapuliwa na fisi kutoka mgongoni mwa mama yake wakiwa njiani kwenda nyumbani kwao katika kijiji cha Ngugunu, wilayani Meatu mkoa wa Shinyanga.   Fisi huyo aliwashambulia mama na mtoto huyo katika kijiji hicho kilichoko kata ya Kisesa mkoani Shinyanga.   Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi, Kamanda wa Polisi wa

Ajinyonga mtini kwa Shati lake.....Kabla ya Kujinyonga Aliwafuata Polisi na Kutaka Awekwe Mahabusu

$
0
0
Mkazi wa Ilembo wilayani Mpanda , Petro Magawe (40) amejinyonga kwa kujitundika mtini akitumia shati lake. Mtu huyo alijinyonga hadi kufa saa 2 asubuhi juzi karibu na Ofisi ya Misitu iliyopo Mtaa wa Majengo A mjini Mpanda.   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari alisema Mei 30 , mwaka huu, Magawe alifika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Mpanda mjini Mpanda,

Msanii Salma Jabu ‘Nisha’ Abadili Jinsia Yake........Asema Aliamka Asubuhi na kujikuta Kawa Mwanaume!

$
0
0
Staa wa kike wa bongo Movies mwenye visa na vituko, Salma Jabu ‘Nisha’ amabaye kwa sasa anatamba sokoni na MTAA kwa MTAA  amewaaacha hoi mashabiki wake baada ya  kuwaeleza  kuwa  viongo  vyake  vimebadilika  na  sasa  sio  mwanamke  tena. Nisha  aliuanika  ukweli  huo  kupitia  ukurasa  wake  wa  Instagram  ambapo  alitupia  picha  hii na  kuandika;  “Nimeamka nimejikuta nna mabadiliko

Shamsa Ford Aonyesha Jeuri kwa Mzazi Mwenzake

$
0
0
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameonesha jeuri kwa kueleza kwamba anamlea mwanaye Terry kwa mapenzi tele ili asimkumbuke baba yake, Dickson ambaye wamemwagana. Amesema tangu wamwagane na mzazi mwenzake, mtoto wake hajawahi kumuuliza baba yuko wapi kitendo kinachomfanya azidishe mapenzi kwake kwani hata yeye alilelewa na mama yake bila baba.   “Kama baba yake alikuwa

Mgombea Urais UKAWA Kujulikana Mwezi Huu

$
0
0
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amesema mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) atapatikana wakati wowote kuanzia sasa ndani ya mwezi huu. Mbatia alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam juzi wakati akihojiwa katika Kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV.   Alisema mchakato wa kumpata rais ndani ya umoja huo unakwenda

Daftari la Wapiga Kura: Wananchi kuandikishwa siku 7 kwa kila kituo kanda ya ziwa (Geita,Simiyu,Mwanza na Shinyanga)......Mwisho tarehe 4 July

$
0
0
Zoezi la Uandikishaji  daftari la kudumu la wapiga Kura linatarajia  kuanza  katika mikoa ya Geita, Simiyu, Mwanza na Shinyanga, zoezi litakaanza rasmi tarehe 2/06/2015 hadi 04/07/2015.   Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi imebainisha kuwa zoezi hilo litafanyika kwa kutumia teknolojia ya BVR (Biometric Voters Registration.Vituo vya uandikishaji vitakuwa

Nyalandu Kuchukua Fomu ya Urais Juni 8

$
0
0
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu atahutubia wananchi mkoani Singida mwishoni mwa wiki hii, ikiwa ndio mwanzo wa kwenda kuchukua fomu za kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).   Tukio hilo litaoneshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya EATV, STAR TV na ITV kuanzia saa 10 jioni kutoka kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.   Baada ya kuhutubia

Picha: Mwandosya achukua fomu ya kugombea Urais

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya akionesha fomu ya kugombea Urais.   Wajumbe wa CCM waliohudhuria mkutanoa huo.   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya akizungumza na waandishi wa habari .   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya  amechukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya

Urais 2015: Wassira atinga makao Makuu CCM kuchukua fomu ya Urais

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira akikabidhiwa fomu ya kugombea urais.   Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira akishuka kwenye Gari ili kuchukua fomu ya kugombea urais 2015 .   Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira akiwasili ukumbini katika mkutano na Waandishi wa Habari leo. Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen

Lowassa aahirisha Kuchukua fomu ya Kugombea Urais

$
0
0
Mbunge wa Monduli ambaye aliwahi kuwa Waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa amaeahirisha kuchukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi hadi siku ya kesho ambayo ni alhamisi.   Hadi sasa mwanasiasa  aliyefungua dimba la kuchukua fomu ya urais  ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Majina ya watakaochukua Fomu ya Kugombea Urais Kesho Alhamisi

$
0
0
Majina  ya  watakaochukua  Fomu  ya  Kugombea    Urais  Kesho  Alhamisi

Samweli Sitta: Nina Ari, Uwezo Na Utayari Wa Kuliongoza Taifa Hili......Nipeni Hii Miaka Mitano Nifanye Mabadiliko Makubwa

$
0
0
WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta ametangaza rasmi nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM na kusema ana ari, uwezo na utayari wa kuiimarisha nchi na kwamba kipindi kimoja tu cha miaka mitano kinamtosha.   Mbali na hilo, Sitta amesema akifanikiwa kupata nafasi ya kuongoza nchi atahakikisha anatenganisha masuala ya siasa na biashara, kwa sababu ndiyo

Dr. Bilal na John Magufuli Wajitosa Urais Kimya Kimya......Leo wataungana na Akina Lowassa Na Sumaye Kuchukua Fomu

$
0
0
WANACHAMA watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo wanatarajiwa kuchukua fomu, kuomba ridhaa ya uteuzi wa kuwania urais wa Tanzania, wakati wakiwa hawajatangaza nia kama ilivyo kwa wengi wao.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na Katibu Msaidizi wa Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi Ndogo ya CCM,

Aunt Ezekiel Alimwa Talaka

$
0
0
Kuna madai kwamba, Aunt Ezekiel alishaandikiwa talaka na ipo nyumbani kwa wazazi wa aliyekuwa mumewe, Sunday Demonte, Temeke Mwisho jijini Dar.    Kwa mujibu wa chanzo, talaka hiyo iliandikwa na mumewe huyo baada ya kupata taarifa kwamba, mkewe huyo ana ujauzito unaodaiwa kuwa ni wa Mnenguaji wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moze Iyobo.   “Hivi mnajua kwamba, Aunt

Nkurunziza aahirisha Uchaguzi wa Rais na Wabunge

$
0
0
Serikali ya Burundi imetangaza kuwa uchaguzi wa rais na wabunge uliotarajiwa kufanyika Ijumaa hii umehairishwa mpaka tarehe nyingine itakapopangwa.   Msemaji wa rais Nkurunzinza,Wily Nyamitwe amesema  kuwa tarehe itapangwa na wasimamizi wa uchaguzi wa nchi hiyo.   Mabadiliko hayo yamekuja kutokana na taifa hilo kuingia kwenye machafuko tangu Rais Piere Nkurunzinza kutangaza

Pinda aongoza wabunge kumuaga mbunge wa Ukonga Aliyefariki Dunia Juzi

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mbunge wa Ukonga Eugen Mwaiposa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 3, 2015.   Mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga ukiwasili kwenye viwanja vya bunge jana  mjini Dodoma kwa ajili ya kuagwa.   Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya

'Mimba' Ya Lulu Michael Yapotea

$
0
0
Miezi miwili iliyopita kuliibuka madai mazito kwamba staa bei mbaya wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameongezeka tumbo hivyo mashabiki wake wakapiga vigelegele kwamba huenda ana mimba lakini sasa tumbo hilo limeyeyuka. Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Lulu kwa sasa anakatiza viunga vya chuo anachosoma cha Magogoni jijini Dar akichukua masomo ya Uhusiano wa Umma,

Mpinzani wa Lipumba afukuzwa uanachama

$
0
0
BARAZA Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), limemvua uanachama mjumbe wake kutoka Mkoa wa Shinyanga, Chifu Lutayosa Yemba.   Chifu Yemba ambaye pia alikuwa ni mpinzani wa Profesa Ibrahim Lipumba katika kuwania uenyekiti wa CUF kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka jana, alivuliwa uanachama kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za chama pamoja na kutumia vibaya jina la mwenyekiti wa

Plot for sale.......Kinauzwa!!!...Kinauzwa!!!.....Kiko Bunju B. Changamkia Dili

$
0
0
Plot for sale Bunju B. Plot size Sq 2000 meter and its located in cool neighborhood just 1km from tarmac road with clean tittle deed access is good for residential house,Dawasco water and power is available!!.   It is located in a prime area.More details see the pictures and call +255784333968.

Mwakyembe Akana kutumia Richmond Kumchafua Lowassa...... Umoja wa Ulaya nao wakana kuhusika Kumchafua.

$
0
0
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, ameibuka na kusema hajawahi kumshambulia kwenye mitandao Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhusu sakata la Richmond.   Kauli hiyo ya Dk. Mwakyembe imekuja siku chache baada ya kusambazwa kwa waraka unaodaiwa kuandikwa naye, ukimuhusisha na tuhuma za kumshambulia Lowassa, jambo ambalo amelifananisha kuwa ni sawa na
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images