Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Maazimio Ya Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo Katika Vikao vyake vya Mei 23-24

$
0
0
KAMATI Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo, ilikuwa na kikao chake cha kawaida cha siku mbili kilichokaa tarehe, 23 na 24 mwezi huu na kuongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Anna Mghwira, pia kilihudhuriwa na kiongozi wa Chama Zitto Zuberi Kabwe.   Agenda za vikao hivyo vya siku mbili zilikuwa ni Uteuzi wa nafasi mbali mbali za kiutendaji ndani ya chama Operesheni majimaji Ratiba ya Uchaguzi

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Tarehe 27 May 2015

$
0
0
Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti ya  Leo  Jumatano  ya  Tarehe  27  May  2015

Rais Kikwete aagana na mabalozi wa Tanzania....Awasihi Walinde Usalama Wa Nchi

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana amewaaga rasmi mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi katika mkutano wa siku nne ulioanza  jana jijini DSM. Katika salam zake Rais Kikwete amewataka wawakilishi hao wa nchi kuhakikisha kuwa wanaendeleza diplomasia nzuri ya kimataifa iliyojijengea Tanzania ambayo mara zote imehakikisha kuwa inakuwa na maadui wachache na marafiki wengi.   Rais

Wema Sepetu msamehe Kajala-Mashabiki

$
0
0
Ni Siku  moja  tu   imepita  toka msanii wa filamu nchini Kajala Masanja kufunguka ya moyoni juu ya Wema Sepetu na Petit Man na kueleza kuwa kamwe katika maisha yake ya hapa Duniani hawezi kusahau fadhila na moyo wa upendo ambao  ulioneshwa na watu wao kipindi ambacho alikuwa na matatizo na jinsi walivyoweza kujitolea mpaka kufikia hatua ya kuweza kumsaidia katika matatizo ambayo

Madereva Bado Hakijaeleweka......Mgomo Mwingine Wanukia

$
0
0
UMOJA wa Madereva umeilalamikia Kamati ya Waziri Mkuu iliyoundwa kutatua hoja za madai yao kwa kile walichodai inajadili malalamiko ya wamiliki badala ya hoja zao kama ilivyoagizwa.    Akizungumza Katibu Mkuu wa Madereva Tanzania, Rashid Salehe, alisema kuwa tangu kuundwa kwa kamati hiyo kwa ajili ya kujadili hoja za madereva ni kikao kimoja ndicho kilichojadili hoja moja tu ya namna ya

Polisi wakamatwa kwa upotevu wa bunduki

$
0
0
JESHI la Polisi Mkoa wa Rukwa, linawashikilia askari polisi wawili kwa tuhuma za kuiba  bunduki aina ya SMG mali ya jeshi hilo. Akizungumza mjini hapa jana, Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Rukwa, Leons Rwegasira,  alisema bunduki hiyo iliibwa Mei 19 mwaka huu katika Kituo cha Polisi mjini Namanyere, Wilaya ya Nkasi. Pamoja na kuthibitisha wizi huo, Kamanda Rwegasira hakutaka kutaja

Pinda ajiandikisha Daftari la Kudumu

$
0
0
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amewataka Watanzania wajiandikishe kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Amesema kwamba, kama watafanikiwa kufanya hivyo, watakuwa na sifa za kuwachagua wagombea wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25, mwaka huu. Waziri Mkuu Pinda aliyasema hayo juzi alipokuwa akizungumza baada ya kujiandikisha kwenye ofisi ya Ofisa Mtendaji wa

Majimbo ya Mbeya kugawanywa.....Majimbo hayo ni Mbeya mjini Linaloongozwa na Joseph Mbilinyi (Chadema) na lile la Mbeya Vijijini

$
0
0
KIKAO cha Kamati ya Ushauri cha Wilaya ya Mbeya, jana kilikaa na kupitia  mapendekezo ya kuyagawa majimbo mawili ya Mbeya na kuwa majimbo manne ya uchaguzi kwa mwaka 2015. Kikao hicho kiliwahusisha madiwani, wanasiasa, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na vyombo vya habari. Katika kikao hicho, wajumbe walikubaliana kuyagawa majimbo hayo ambayo ni Jimbo la Mbeya Mjini linaloongozwa 

Mbunge wa CHADEMA Ataka Bangi Ihalalishwe Kwa Matumizi Ya Tiba Na Chakula

$
0
0
MBUNGE wa Viti Maalumu, Christowaja Mtinda (Chadema),ameitaka Serikali kuufanyia utafiti mmea wa bangi ili kubaini iwapo unaweza kutumika kama dawa ya kutibu magonjwa ya binadamu.   Akiuliza swali la nyongeza bungeni jana Mtinda alisema iko mikoa ambayo bangi huota yenyewe kama vile Njombe, Iringa na Mara na kwamba wakazi ya mikoa hiyo huitumia kama chakula.   “Sasa ni utafiti gani ambao

‘Acheni kuweka vyakula vya moto kwenye plastiki ili Msipate Magonjwa’

$
0
0
SERIKALI imewataka Watanzania kuacha kuweka vyakula vya moto katika mifuko ya plasiti kutokana na uwepo wa uwezekano wa kupata magonjwa mbalimbali.   Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Stephen Masele wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mkiwa Adam Kimwanga (CUF).   Katika swali lake Kimwanga alitaka  kauli ya Serikali

Wahamiaji haramu 250 wasambazwa magereza mbalimbali ya Tanzania

$
0
0
JUMLA ya wahamiaji haramu 250 kutoka nchini Ethiopia wapo katika magereza mbalimbali nchini.   Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima wakati akijibu swali la Mbunge wa Koani, Amina Andrew Clement. Katika swali lake Mbunge huyo alitaka kujua idadi ya wahamiaji haramu kutoka Ethiopia walioko katika magereza nchini na hatua zinazochukuliwa

Rais Kikwete ateua Makatibu Tawala Singida na Shinyanga

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua makatibu tawala wa Mikoa ya Singida na Shinyanga kuanzia Jumatatu, Mei 25, 2015. Katika uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Ndugu Festo Luganda Kang’ombe kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida na Ndugu Abdul Rashid Dachi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.   Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Kang’ombe

Wizi TTCL Unatisha......Kambi Ya Upinzani Yaibua Tuhuma Nzito, Serikali Yabanwa Itoe Majibu

$
0
0
KAMBI Rasmi ya Upinzani bungeni, jana imeibua tuhuma nzito bungeni Mjini Dodoma dhidi ya Kampuni ya Simu nchini (TTCL), ikidai aliyekuwa Meneja Biashara wa kampuni hiyo (bila kutajwa jina), amefungua akaunti nchini yenye kiasi cha sh. bilioni moja. Waziri Kivuli wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. Habib Mnyaa (CUF), aliyasema hayo wakati akisoma hotuba ya kambi ya upinzani kuhusu

ACT Wazalendo wawapiga msasa wanachama wao

$
0
0
CHAMA cha ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani kimeanza  kuwapiga msasa viongozi wake wa ngazi ya kata na vijiji kama sehemu ya kuwaandaa kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu. Mafunzo hayo yameanza kutolewa juzi katika Wilaya ya Kibaha Mjini kwa kuwahusisha wenyeviti, makatibu, watunza hazina, wajumbe wa vikao mbalimbali na wanachama wengine. Katibu wa ACT Wazalendo

UNYAMA Jijini Mwanza: Bibi Amchoma Visu Vya Moto Mjukuu Wake Akimtuhumu Kupoteza Peni Ya Sh. 200

$
0
0
Jeshi  la  Polisi  Mkoani  Mwanza  linamshikilia  bibi  mmoja  ajulikanaye   kwa  majina  ya  Laurencia  Athanas  mkazi  wa  Kiseke, Ilemela  jijini  Mwanza kwa  tuhuma  za  kumchoma  visu  vya  moto mjukuu  wake  na  kumsababishia  majereha  mbalimbali  mwilini  akimtuhumu  kupoteza  peni  ya  sh. 200. Mtoto  huyo  aitwaye  Jackson  Hosea ( 10 )  ambaye  ni  mwanafunzi  wa  darasa  la 

Mipasho Yaendelea Bungeni.....Waziri Simba Adai Wabunge Wa Upinzani "Wanawashwa"

$
0
0
Kama unadhani mipasho ipo katika nyimbo za taarabu tu, hakika utakuwa umekosea sana.   Hapa bungeni kauli zenye utata, kejeli na dhihaka ni mambo yaliyoshika hatamu tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti Mei 12. Unajua ilikuwaje? Juzi usiku wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, waziri wa wizara hiyo Sofia Simba ni kama

Nyota Ya Lowassa Bado Inang'aa: Utafiti Mpya Waonyesha Anaongoza Kwa Kupendwa na Wapiga Kura Wengi......Wafuatia Slaa, Magufuli na Membe

$
0
0
Nyota ya Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, imeendelea kung’aa baada ya Taasisi ya Samunge Social Sciences Research Center (SSSRC), kufanya utafiti na kubaini kuwa kiongozi huyo ni chaguo la kwanza kwa wananchi. Utafiti huo uliofanywa miaka miwili kuanzia 2013 hadi 2015, unaonyesha Lowassa anaongoza kwa asilimia 20.7 dhidi  ya wagombea 31. Akizungumza na

Tuhuma Za Sitti Mtemvu Kudanganya Umri, Kuitwa "Bibi Bomba" na Kutembea Na Baba Yake Zamuathiri Kisaikolojia Mdogo Wake

$
0
0
Aliyekuwa mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amekiri kuumizwa na kashfa mbalimbali zilizoandikwa kwenye vyombo vya habari ambazo zilipelekea familia yake kutawaliwa na huzuni jambo ambalo lilisababisha kuvua taji hilo.   Amesema tuhuma hizo zilimuumiza sana hasa baada ya mdogo wake wa mwisho kutaniwa na wanafunzi wenzake wakidai kuwa amekuwa akiwadanganya Sitti, ni dada

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Tarehe 27 May 2015

$
0
0
Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Alhamisi ya  Tarehe 27  May 2015

Jiji la Dar es Salaam lashika ‘nafasi ya sita’ katika Majiji bora kwa Vijana Afrika

$
0
0
- Nafasi tatu za juu zimechukuliwa na Johannesburg, Casablanca na Durban - Ripoti ya YouthfulCities imetolewa kuyahusu majiji hamsini na tano duniani baada ya utafiti uliotumia viashiria 101   London, 7 Mei 2015: ​DAR ES SALAAM leo imetajwa kuwa jiji bora la 6 kwa vijana Afrika na jiji la 53 katika majiji bora kwa vijana duniani kulingana na utafiti mkubwa na wa aina yake  uliofanyika
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images