Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Jeshi la Polisi Latangaza Kiama Kwa Wahalifu.......... Helkopta ya Jeshi Kutumika Kuwasaka, Kova Aeleza Sababu Za Wananchi Kukaguliwa Kwa Mashine Kivuko cha Kigamboni.

0
0
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewatangazia kiama wahalifu, ambapo imeamua kuwasaka kwa kutumia helkopta, baada ya kupata taarifa kwamba wamekimbilia mpakani mwa mkoa huo na wa Pwani. “Tunaendelea na operesheni kali dhidi ya wahalifu, kwani tumepata taarifa kwamba kuna wahalifu wamekimbilia mpakani mwa Mkoa wa Dar es Salaam na  Pwani,” alisema Kamishna wa Kanda hiyo, Suleiman Kova

PICHA: Dk. Shein Aongoza Kumbukumbu ya Kifo Cha Karume

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein, ameongoza mamia ya wananchi kuadhimisha Siku ya Mashujaa wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.   Maadhimisho hayo yalifanyika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar kisha Rais Shein aliwaongoza wananchi kutembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Karume.  

Rose Ndauka: Pengo la Steven Kanumba Haliwezi Kuzibika

0
0
Nyota wa kike wa filamu nchini, Rose Ndauka, amesema pengo la msanii mwenzake, marehemu Steven Kanumba, litaendelea kuwepo kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwenye tasnia hiyo.   Wakati jana ikiwa ni kumbukumbu ya miaka mitatu tangu Kanumba afariki dunia, Rose alizungumza na  DjHaazu  katika  Exclusive  Interview  na kusema kwamba msanii huyo aliikuza tasnia hiyo kwa kutumia

Waislam Watoa Tamko Zito Litakalosomwa Misikiti Yote Nchini......Wasema Wamechoka Kuonewa, Wawataka waamini wao Kufanya Maamuzi Magumu Wakati wa Uchaguzi

0
0
SIKU chache kupita baada ya Mkutano wa  19 wa Bunge kumalizika na serikali kuutupilia mbali mswaada wa sheria ambao unaruhusu kuwepo makakama ya Kadhi nchini, Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini wameibuka na kutoa tamko zito kwa kuwataka waislam wote nchini kutoshiriki kwenye kura ya maoni ya kupitisha katiba pendekezwa kwa madai kwamba serikali haina nia nzuri na waislam nchini kwa kitendo

Kakobe Amshukia Lowassa...... Awataka Watanzania Kususia Kura Ya Maoni Kwa Madai Kuwa Katiba hiyo ni ya Kishetani na Mwandishi Wake Ni "Nyoka Wa Makengeza" ( Shetani)

0
0
Akihubiri siku ya Pasaka katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lililopo Mwenge katika Jiji la Dar-Es-Salaam, Askofu Mkuu Zachary Kakobe alisema kwamba, inajulikana wazi kwamba Lowassa amekuwa anautaka Urais kwa udi na uvumba kwa miaka mingi, hata mwaka 1995 alijitosa hadharani kuuwania, sasa anapodai kwamba hivi sasa kuna makundi yanayokwenda kwake kumshawishi agombee Urais, kana

Askofu wa Kanisa Katoliki Atamani Kumchapa Makofi Waziri

0
0
Askofu wa Kanisa Katoliki Mbeya amesema kama angekuwa na Mamlaka dhidi ya Waziri angemchapa makofi Waziri aliyeshindwa kutekeleza kauli ya kuzuia malori yanayoharibu barabara.    “Yupo Waziri ambaye alisema malori makubwa yanaharibu barabara hivyo mizigo yote inatakiwa kusafirishwa kwa Reli lakini mpaka sasa hajatekeleza.. Kama ningekuwa na uwezo ningemchapa makofi” alisema Askofu

Mkazi Wa Kahama Auwa Kwa Kuchomwa Moto Katika Msiba Wa Jirani Baada Ya Kutuhumiwa Kuhusika Na Kifo Cha Marehemu

0
0
Picha  Ya  Maktaba Mkazi mmoja wa Kijiji cha Ulowa Kahama, Chausiku Hamis ameuawa kwa kuchomwa moto na watu waliokusanyika katika msiba wa mtoto wa jirani baada ya kutuhumiwa kuhusika na kifo cha mtoto huyo.   Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja alifariki usiku katika mazingira tata ambapo mwanamke huyo aliuawa baada ya mmoja wa waombolezaji kupandisha mapepo na kumtuhumu Chausiku

Mgomo Mkali Wa Madereva Nchi Nzima Wanukia

0
0
Madereva wa vyombo mbalimbali vya moto, wanakusudia kushiriki mgomo wa nchi nzima Ijumaa wiki hii, kuishinikiza serikali kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa ajira za uhakika pamoja na agizo la kutaka kwenda kusoma. Wakizungumza kupitia Katibu wa Muungano wa vyama vya madereva Bw. Rashid Saleh, Madereva hao wamesema kuwa suala la kurudia kusoma kila

Waziri Wassira Awafuta Kazi Watendaji Watatu wa Shirika la Rubada.......Watendaji Hao Wameitia Hasara Serikali Ya Bilioni 2.5

0
0
WAZIRI wa kilimo, Chakula na Ushirika Steven Wasira amewafukuza kazi wakurugenzi watendaji watatu wa Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (Yaani Rufiji River Basin Development Authority – RUBADA) kutokana na matumizi mabaya ya ofisi ya Umma ambayo yameitia  hasara ya Bilioni 2.5 Serikali . Akitoa agizo hilo leo mbele ya Waandishi wa Habari, Waziri Wasira amewataja Watendaji hao kuwa

Mzee Wa Miaka 68 Auawa Na Wananchi Kwa Kupeleka Waganga Kijijini Kilimanjaro

0
0
Mzee mwenye umri wa miaka 68, Celestine Mushi, mkazi wa kata ya Motamburu wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, ameuawa na wananchi wanaotajwa kukasirishwa na kitendo chake cha kupeleka waganga wa jadi kijijini kwa lengo la kuifanyia zindiko nyumba yake.   Mushi anadaiwa kuwatoa waganga hao wawili jijini Dar es Salaam na kuwapeleka Rombo kwa kazi hiyo maalumu.   Tukio hilo limethibitishwa

Mwanajeshi wa JWTZ Ajinyonga Jijini Mwanza

0
0
Fundi wa magari wa Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi namba 512 MTC Nyegezi, jijini Mwanza, Jacob Mponeja (55) amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya katani huku akiacha ujumbe.   Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Joseph Lusungu tukio hilo lilitokea Aprili mosi mwaka huu majira ya saa moja asubuhi.   Alisema ujumbe huo ulioandikwa kwenye

Wakili: Gwajima Yupo Tayari Kwa Mahojiano

0
0
Mahojiano baina ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na Polisi yanatarajiwa kuendelea leo katika Kituo Kikuu cha Polisi, jijini Dar es Salaam.   Mahojiano hayo yanaendelea baada ya kuahirishwa wiki iliyopita kutokana na kile kilichodaiwa kuwa afya yake ilikuwa haijaimarika vizuri na hivyo kuwalazimu polisi kuahirisha mahojiano hayo ili kumpatia muda zaidi wa kupumzika

Wanawake Pwani Wadaiwa Kuwarubuni Wavulana

0
0
Wanawake wenye umri mkubwa wametakiwa kuacha kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na vijana wenye umri mdogo, kwani jambo hilo linawapunguzia heshima katika jamii.   Ushauri huo ulitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani yaliyofanyika eneo la Kituo cha Afya Mlandizi, wilayani Kibaha mkoani Pwani.   Kihemba, ambaye kitaaluma

Kesi Ya Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Nchini, Johnson Minja Kuanza Leo Ambapo Atasomewa Maelezo Ya Awali Ya Kesi Yake

0
0
Kesi ya kushawishi wafanyabiashara wasilipe kodi kwa serikali inayomkabili Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Nchini, Johnson Minja inaanza kusikilizwa leo.   Kesi hiyo iko katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini mbele ya Hakimu Mkazi, Rebecca Mbilu ambapo leo itaanza usikilizwaji kwa mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali ya kesi yake.   Mshitakiwa huyo ambaye yuko nje kwa dhamana

Polisi Yazuia Wafuasi Wa Askofu Gwajima.....Vikosi vya Mbwa, Farasi,Magari sasa kila Kona.

0
0
Jeshi  la  polisi  kanda  maalumu  ya  Dar  es  salaam  limesema  wafuasi  wa  Askofu  mkuu  wa  kanisa  la  ufufuo  na  uzima,Josephat  Gwajima  wasithubutu  kutia  mguu  eneo  atakalohojiwa  askofu  huyo. Kauli  ya  jeshi  hilo  imekuja  siku  chache  baada  ya  Askofu  Gwajima  kuwataka  wafuasi  wake  kumsindikiza  leo  kituo  cha  polisi  kanda  maalumu  ya  Dar  es  salaam  ambako 

Zitto Kabwe Aanza Na Ngome Kuu ya CCM

0
0
Kiongozi  wa  Chama  cha  ACT-Wazalendo, Zitto  Kabwe  anaanza  ziara  yake  ya  kwanza  ya  ujenzi  wa  chama  hicho  kipya  mwishoni  mwa  wiki  hii  kwa  kutembelea  mikoa  ambayo  inachukuliwa  kama  ngome  za  Chama  Cha  Mapinduzi ( CCM ). Zitto  ambaye  aliacha  uanachama  na  ubunge  wake  wa  CHADEMA  mwishoni  mwa  mwezi  uliopita, atafanya  mkutano  wake  wa  kwanza  wa 

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Tarehe 9 April 2015

0
0
Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  Ya  Leo  Alhamisi  Ya  Tarehe  9  April  2015

Wabunge 50 Kujiunga Na Chama Kipya Cha ACT-Tanzania......Zitto Kabwe Asema Majimbo Yote 8 Ya Kigoma Lazima Yachukuliwe na Chama Chake

0
0
Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe amesema zaidi ya wabunge 50 wa vyama mbalimbali vya siasa nchini watajiunga na chama hicho kipya na kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.   Zitto ambaye alijivua ubunge wa Kigoma Kaskazini baada ya kufukuzwa uanachama wa Chadema, amebainisha kuwa wabunge hao, wakiwamo wa CCM na Chadema, ni miongoni mwa watu

Lowassa: Nafuatiliwa Kwa Ukaribu Sana na Chama Changu (CCM).....Muda Ukifika Nitatangaza Nia na Kuweka Mikakati Yangu Wazi ili Wananchi Waijue

0
0
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amesema anashindwa kujitokeza kuzungumzia au kufanya mambo yanayohusiana na urais kwa kuwa Kamati ya Maadili ya CCM inamfuatilia kwa karibu.   Alisema hayo jana alipoulizwa kuhusu kauli ya Rais Jakaya Kikwete wiki iliyopita akiwa Marekani ambako alielezea mafanikio na changamoto alizokumbana nazo wakati wa uongozi wake wa miaka 10.   Kikwete

Mtanzania Anayetuhumiwa Kwa Ugaidi Kenya Kumbe Alitoroka Shuleni Dodoma Tangu Novemba Mwaka Jana.....Mkuu Wa Shule, Wazazi Wake Wafunguka

0
0
Mtanzania aliyekamatwa Kenya akidaiwa kufanya ugaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa uliosababisha vifo vya watu 148, Rashid Charles Mberesero (20) ni mwanafunzi wa kidato cha tano, lakini uongozi wa shule anayosoma umesema alitoweka shuleni hapo Desemba Novemba 2014.   Habari zilizothibitishwa na wazazi wake ni kuwa mwanafunzi huyo anasoma katika Shule ya Sekondari ya Bihawana,
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images