Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kamanda Siro Atoa Ushahidi wake Katika Kesi ya Maandamano ya Mbunge Halima Mdee na Wenzake

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeambiwa na Naibu Kamishna wa Polisi, Kamanda Simon Siro (54), ambaye amedai mahakamani kwamba alitoa zuio la kuandamana kwenda Ikulu kwa Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha) kwa sababu maandamano hayo yangesababisha uvunjifu wa amani.   Alitoa madai hayo, wakati akitoa ushahidi dhidi ya Mbunge Halima Mdee na

Stara Thomas akana kufumaniwa na mpenzi wake

$
0
0
Aliyekuwa mwimbaji muziki wa gospel na baadaye kurudi kwenye Bongo Fleva,Stara Thomas amekana habari zilizoenea hivi karibuni kuwa amefumaniwa na mpenzi wake nyumbani kwake.     Akizungumza na Soudy Brown kupitia Uheard alisema kuwa mwanamke kama yeye hawezi kufumaniwa na kwamba mpenzi wake wa sasa kinachomsumbua ni wivu wa kimapenzi bila kumtaja jina mpenzi wake huyo wa sasa.  

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Aua Mwanafunzi Mwenzake Darasani Wakati Wakigombania Daftari la Notes

$
0
0
Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Ilola iliyopo katika wilaya ya Shinyanga vijijini aitwaye Veronica Venance mwenye umri wa miaka 12 amefariki dunia kwa kupigwa na mwanafunzi mwenzake wakati wakigombania daftari darasani kwa ajili ya kuandika notes. Walioshuhudia tukio hilo wamesema limetokea Februari 24 mwaka huu, saa 7 na nusu mchana katika darasa la tano katika

Sheria: Namna ya Kuwashitaki Askati Wanaowabambikiza Kesi Raia

$
0
0
Hapa kwetu Tanzania  habari ya kubambakiziana kesi ni kama mtindo. Mara nyingi matendo haya yamekuwa yakifanywa na watu wenye uwezo  kifedha dhidi ya wasio na fedha  pia kati ya  maofisa wa polisi na raia.    Mtu kwasababu ana pesa au cheo anaweza kuamua  kumfungulia yeyote mashtaka.  Watu wengi wako magerezani kwa kubambikizwa kesi, hili wala sio siri tena.    Sisemi walio mahabusu, hao

Andrew Chenge Agoma Kuhojiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Umma.....Adai kuna zuio la mahakama kuu, hatima yake kujulikana leo

$
0
0
MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Mtemi Andrew Chenge, jana ameonyesha utemi wake mbele ya Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma, baada ya kusema haiwezi kumjadili kwa sababu kuna kesi mahakamani.   Alisema kuna zuio la Mahakama Kuu ambalo limevitaka vyombo vyote vya Serikali kutojadili suala la miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hadi kesi ya msingi itakapoamuliwa.   Tume hiyo inamtuhumu

Waliomuiba Mtoto Albino Pendo Wakamatwa Jijini Mwanza

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amesema watu wote waliohusika ‘kuiba’ mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Pendo Emmanuel (4) katika kijiji cha Ndami wilayani Kwimba, Mwanza, wamekamatwa. Akizungumza wakati akiwaapisha wakuu wapya wa wilaya wa mkoa huo jana, Manju Msambya (Misungwi), Zainab Rajab (Sengerema) na Pili Moshi (Kwimba), Mulongo alisema watu wote waliohusika

Breaking News: Chid Benz Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Miwili Jela au Kulipa Faini ya sh. 900,000

$
0
0
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae. Chid Benz

Polisi Jijini Arusha Wadaiwa Kumvunja Mikono Raia....Ni baada ya kukodiwa na mfanyabiashara aliyekuwa anamdai mtuhumiwa sh.250,000

$
0
0
MKAZI wa Loksale wilaya ya Monduli, Samwel Petro Shani(47) amelalamikia hatua ya kuvunjwa mikono yake miwili kwa kipigo cha askari polisi katika kituo cha Leskale kwa madai ya kushindwa kulipa deni ya shilingi 250,000 alizokuwa akidaiwa ana mfanyabiashara wa eneo hilo.   Aidha anawatuhumi askari hao kukodiwa na mfanyabiashara mmoja mkazi wa eneo hilo kwa lengo la kumshikisha adabu baada ya

Wakazi wa Ilula Mkoani Iringa Wagoma Kupokea MAITI Aliyeuawa na Polisi

$
0
0
Wakazi wa Ilula Mkoani Iringa wamegoma kupokea maiti ya mama aliyeuwawa wakati wa mapambano yalioyotokea juzi mkoani Iringa kati yao na polisi kwa masharti mawili:   Mosi: Wananchi 18  Waliokamatwa  na  jeshi la polisi  baada  ya vurugu  hizo  waachiwe  mara  moja  bila  masharti  yoyote. Pili: Polisi walio sababisha mauaji hayo wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria . Katika tukio

Picha ya Mpenzi wa Diamond , Zari akioga bafuni yazua gumzo mtandaoni

$
0
0
Picha ya mpenzi wa Staa wa Bongo Fleva,Diamond Platinum,Zari aliyoipost kwenye Account yake ya Instagram akiwa kwenye bafu akioga imezua gumzo kwenye mitandao huku wengine wakisema kuwa hakupaswa kuweka picha ile na kwamba amejianika na haina maadil Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki wakizungumzia picha hiyo:    faridahfakhi :Noo kinachotia kinyaa ni kwamba haikupaswa ajianike

TRA yasisitiza usajili wa pikipiki ndani ya muda.....Usajili huo ni wa namba mpya zinazoanza na MC

$
0
0
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewakumbusha wamiliki wa pikipiki maarufu kama bodaboda kuzifanyia usajili kwani watakaoshindwa kufanya hivyo ndani ya muda uliopangwa watachukuliwa hatua za kisheria.   “Tunawaomba na kutoa mwito kwa wamiliki wa pikipiki kutii sheria na kusajili namba mpya kabla Machi 31, 2015,” alisema Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo

JWTZ wapewa mafunzo kukabili majanga ya moto

$
0
0
ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kambi ya Ihumwa mjini hapa wamepatiwa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto na uwezo wa kukabiliana na matukio ya moto.   Kutokana na mafunzo hayo sasa Jeshi hilo kupitia Kambi yake ya Ihumwa litaanza kutoa huduma za kuzima moto kutokana na kuwa na gari kwa ajili ya shughuli hiyo.   Hayo yalibainika jana wakati wa kufungwa kwa mafunzo

Baada ya CHADEMA Kuigaragaza CCM, Mbunge wa Sumbawanga Apangua Shinikizo la Kujiuzulu

$
0
0
MBUNGE wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeish Hilaly amesema hatajiuzulu ng’o nafasi yake kama Mbunge kwa sababu za CCM kushindwa vibaya katika uchaguzi wa marudio uliofanyika juzi katika kata tatu na mitaa miwili wilaya ya Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa.   Uchaguzi huo uliofanyika katika kata za Msua ,Kizwite na Chanji pamoja na mitaa miwili ya Bangwe kata ya Izia na Tambazi kata ya Sumbawanga

Watoto wa vigogo marufuku kupewa vizimba Mwanjelwa

$
0
0
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amepiga marufuku watoto wa vigogo wa serikali, mashirika binafsi, taasisi , madiwani na wanasiasa wengine kupewa vizimba vya biashara katika soko kuu la kisasa la Mwanjelwa mkoani humu, kuruhusu waliounguliwa bidhaa kwenye soko la awali wapate nafasi.   Akihutubia maelfu ya wananchi katika eneo la soko hilo kwenye halmashauri ya Mbeya Mjini, baada ya kuweka jiwe

Ukuaji wa Uchumi waporomoka kutoka 7.4% hadi 6.8%

$
0
0
Pato la Taifa kwa kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka 2014 toka Julai mpaka hadi Septemba 2014 limekuwa na kufikia Trillion 21.2 ikilinganishwa na Trillion 19.8 kipindi kama hiki mwaka 2013. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi toka Ofisi ya Taifa za Takwimu Mourice Oyuke alisema kuwa kukuwa kwa pato la taifa kumetokana na

Mwanaume wa Miaka 45 Ahukumiwa kifungo cha maisha Jela kwa kosa la Kumbaka Mtoto wa Miaka Minne

$
0
0
Mwanaume mmoja Yusufu Chatambala (45) mkazi wa Kijiji cha Makutupa Kata ya Lupeta Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukiri kosa la kumbaka mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne.   Mwendesha mashtaka wa polisi Godwill Ikema ameiambia mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Feb 20 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika

Serikali yaombwa kuongeza muda wa uandikishaji BVR

$
0
0
Wakati zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR likiingia katika siku ya Nne katika halmashauri ya Makambako mkoani Njombe baadhi ya wananchi waliofika katika vituo mbalimbali vya uandikishaji wameiomba serikali kuongeza siku za zoezi hilo kutokana na changamoto lukuki zinazokabili zoezi hilo.   Mpekuzi imetembelea baadhi ya vituo vya uandikishaji na

Watu 3 Wateketea Kwa Moto Baada ya Lori La Mafuta Kupinduka na Kuwaka Moto

$
0
0
Watu watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa akiwemo dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na kupinduka na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro Dar es Salaam. Mwandishi wetu  alishuhudia kikosi cha zimamoto ambao walichukua muda kuuzima moto huo kutokana na kusambaa ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya watu

Profesa Anna Tibaijuka Ahojiwa Na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma.....Mashitaka yanayomkabili na Utetezi wake Vyote Viko Hapa

$
0
0
BARAZA la Maadili ya Viongozi wa Umma, limemsomea rasmi mashitaka aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (pichani), na kubainisha kuwa kiongozi huyo anastahili kujibu mashitaka kwa kosa la kuomba na kujipatia fedha kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.   Hata hivyo, Profesa Tibaijuka alikana mashitaka hayo, na kusisitiza kuwa hakukiuka

Andrew Chenge AGOMA Tena Kuhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma.....Aomba Aruhusiwe kukata Rufaa Mahakama kuu

$
0
0
MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ameendelea kupambana ili Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, lisiendelee kusikiliza shauri lake, licha ya pingamizi lake kutupiliwa mbali jana.   Chenge amewasilisha ombi la kukata rufaa Mahakama Kuu dhidi ya uamuzi wa baraza hilo, uliotolewa jana na kusomwa na Jaji Hamisi Msumi, ukisema madai yaliyowasilishwa kwenye pingamizi la mbunge huyo,
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images