Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wanafunzi Waliofaulu Darasa la Saba Watakiwa Kuripoti Kabla ya March 28

$
0
0
Serikali imeagiza wakuu wote wa mikoa, kuweka mikakati ya kuhakikisha watoto wote waliofaulu mitihani ya darasa la saba, wanajiunga na shule za sekondari katika kipindi hiki kabla ya Machi 28 mwaka huu, vinginevyo watakaokwamisha watoto hao watachukuliwa hatua kali. Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri MkuuTawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia

CCM Yakana Kuandaa Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha, imesema chama hicho hakina mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, aliyeandaliwa hadi sasa. Kimesema mgombea  mwenye sifa za kulikomboa jimbo hilo, ambalo liko Chadema, hajajitokeza mpaka sasa.   Akizungumza na Mpekuzi, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Arusha ,Feruzi Banno alisema  chama kina utaratibu wake wa kampeni na chama hakina mgombea

Wahitimu wa JKT Watangaza kufanya Maandamano ya Siku tatu Mfululizo jijini Dar Jumatatu Ijayo.....Lengo ni Kushinikiza Serikali Iwape AJIRA

$
0
0
Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wanatarajia kufanya maandamano ya siku tatu mfululizo usiku na mchana jijini Dar es Salaam kuanzia Jumatatu ijayo, kushinikiza kuonana na Rais Jakaya Kikwete kumweleza matatizo ya ajira wanayokabiliana nayo. Wahitimu hao jana walifanya mkutano katika eneo la Msimbazi Centre, Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Vijana waliohitimu

Dawa Zilizopigwa MARUFUKU Zazagaa Mitaani....Wananchi Wataka TFDA Ichue hatua za Haraka kuwanusuru

$
0
0
Licha ya Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) kufuta usajili na kupiga marufuku uuzaji wa dawa duni, zenye madhara na zisizofaa kwa matumizi ya binadamu, dawa hizo zimegundulika kuuzwa holela na baadhi ya wamiliki wa maduka ya dawa  katika kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza. Hayo yameelezwa na wakazi wa Kisesa wilayani hapa, wakati wa semina ya siku moja iliyojadili

CUF Yaitikisa UKAWA......Yatangaza Profesa Lipumba Atawania Urais Mwaka huu

$
0
0
Chama cha Wananchi (CUF) kimetangaza Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, kuwa ni mmoja kati ya wanachama wa chama hicho, atakayewania nafasi ya Urais. Pia chama hicho, kimetoa rasmi ratiba ya uchukuaji fomu na utaratibu wa kura ya maoni kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uwakilishi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa udiwani, ubunge,

Shule za Vipaji Maalumu zashindwa KUFURUKUTA katika Matokeo ya Kidato cha Nne

$
0
0
Shule za sekondari za Serikali zinazochukua watoto wenye  vipaji, zimeshindwa kung'aa kwenye matokeo ya kidato cha nne 2014 huku shule ya Ilboru ya mjini Arusha ikiwa ni shule ya kwanza ya Serikali na iko nafasi ya 35 kati ya shule 2,320 zilizofanya mtihani  wa kidato cha nne 2014. Mwaka 2013, Ilboru ilishika nafasi ya 41 chini ya shule nyingine yenye vipaji ya Mzumbe ambayo katika matokeo

Mapambano Makali Bado Yanaendelea Kuwasaka MAGAIDI wa Tanga.....Hii ni Video ya Magaidi hao Wakijisifia

$
0
0
Kutokana na wahalifu wanaopambana  na polisi na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kutokamatwa, hali ya wasiwasi imeendelea miongoni mwa wakazi wa mjini hapa. Sasa wananchi hao wameiomba Polisi kutoa tamko, kuhusu kikundi kilichorushiana risasi na askari Polisi na kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja.   Aidha, wananchi  hao wameitaka Polisi kutoa ufafanuzi kuhusu mwendelezo wa matukio  mengi ya

Mungu ni Mkubwa: Mama yake Diamond Arejeshwa toka India......Afya yake kwa sasa inatia Moyo

$
0
0
Mungu ni  mkubwa :Mama mzazi wa Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’, amerejeshwa Bongo kutoka India ambapo afya yake imetengemaa. Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya familia ya jamaa huyo, kimesema kwamba tayari  Sandra amesharejea katika hali yake ya kawaida na ndiyo maana akarudi Bongo baada ya kulazwa hospitalini nchini India kwa

Mamia wamzika Baba Mzazi wa Dully Sykes, Mzee Abby Sykes Jijini Dar

$
0
0
Baba wa staa wa muziki Dully Sykes, Marehemu Abby Sykes aliyefariki dunia juzi katika hospitali ya taifa Muhimbili amezikwa jana katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam. Msiba huo mkubwa katika tasnia ya Burudani umeweza kugusa mamia ya waombolezaji wakiwepo mastaa mbalimbali na wadau wa sanaa hiyo, ambao walimfahamu marehemu kutokana na shughuli zake za muziki.   Mpekuzi

Buzwagi Kusitisha Uchimbaji wa Dhahabu

$
0
0
Kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Buzwagi mkoani Shinyanga, imesema ndani ya miaka miwili, itasitisha shughuli za uchimbaji na uzalishaji madini hayo, kutokana na soko kuzidi kushuka. Meneja Mkuu wa mgodi huo, Filbert Rweyemamu alisema hayo juzi  katika kikao cha pamoja baina ya mgodi na wajumbe wa Kamati ya Kijiji cha Mwime,  iliyoundwa na uongozi wa mtaa wa Mwime kwa

Watu 50 Waliohusika na Vurugu za Geita Wakamatwa.....Mkuu wa Wilaya Aagiza Walimu wakuu Walioruhusu Wanafunzi Kufanya Fujo Washushwe Vyeo

$
0
0
Zaidi ya watu 50 wamekamatwa na jeshi la polisi kufuatia vurugu kubwa iliyotokea katika mji wa katoro mkoani Geita. Chanzo cha vurugu hizo ni mgomo wa wanafunzi wa shule za msingi kilimani, Mkapa na Ludete ambapo walilala katikati ya barabara, kushinikiza kuwekewa matuta kutokana na matukio ya ajali ya mara kwa mara hivyo kutishia usalama wao.   Hata baada ya kuwekewa matuta kuzuia

Ajira 40,735 Zazalishwa Ndani ya Miezi Mitatu

$
0
0
Ajira 40,735 zimezalishwa ndani ya miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka jana na kufanya jumla ya ajira 173,787 kupatikana kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana. Wizara ya Kazi na Ajira imesema ongezeko hilo la ajira limejitokeza katika maeneo makuu mawili ikiwemo ajira serikalini ambazo ni 2,652 sawa na asilimia 6.5 na ajira kupitia sekta rasmi binafsi

Anaswa Akiwa na Lundo la Vyeti Feki

$
0
0
Mtu anayetuhumiwa kwa utapeli, amekamatwa wilayani Hanang’ mkoani Manyara akidaiwa kuwa na vyeti bandia vitatu vya ajira tofauti akidai ni mwalimu, ofisa mifugo na polisi. Mtuhumiwa huyo, Hamis Yusufu alikamatwa katika kata ya Gissambalang’ wilayani Hanang kwa ushirikiano wa ofisi ya diwani pamoja na polisi jamii.   Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Diwani wa kata ya Gissambalang

Kesi ya Ugaidi: Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Afikishwa Mahakamani chini ya Ulinzi Mkali

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, iliimarisha ulinzi wakati kesi ya ugaidi inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Shekhe Farid Hadi Ahmed na wenzake ilipotajwa. Askari walikuwa wengi katika eneo la Mahakama huku kila mtu aliyeingia getini akikaguliwa  kwa kifaa maalumu na kupapaswa ili kuangalia kama ana silaha.   Jana kesi

Rais Kikwete aongoza maziko ya Chifu Abdul Mkwawa ambapo Mwanafunzi wa Miaka 13 Ametawazwa kuwa Chifu Mpya wa Wahehe, akirithi nafasi ya baba yake

$
0
0
Mwanafunzi wa Darasa la Saba, Adam Abdul Sapi (13) ametawazwa kuwa Chifu mpya wa Wahehe, akirithi nafasi ya baba yake, aliyefariki na kuzikwa mkoani Iringa. Rais  Jakaya Kikwete alishiriki maziko ya Chifu huyo wa Wahehe, Abdul Sapi Mkwawa (66)  yaliyokwenda sanjari na hafla ya kumsimika mtoto huyo kushika wadhifa huo wa kimila.   Maziko ya kiongozi  huyo aliyefariki Februari 14, mwaka

Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta Amsimamisha Kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),Madeni Kipande

$
0
0
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande kutokana na kile kilichoelezwa kuwa uendeshaji mbovu wa utoaji wa zabuni. Aidha, amemteua Awadhi Massawe kushika wadhifa huo. Kabla ya uteuzi huo, Massawe alikuwa Meneja wa Bandari.   Akizungumza na waandishi wa habari, Sitta alisema uamuzi huo umetokana na kuwapo

'Magaidi wa Tanga' Watiwa Mbaroni.....Mwili wa Mwanajeshi wa JWTZ Aliyeuawa katika Mapigano hayo Waagwa

$
0
0
Serikali imetoa taarifa rasmi kuhusu uhalifu uliotikisa mkoani Tanga, ikisema hali ni shwari na umma wa Watanzania upuuze taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikitia hofu. Aidha, imesema  watu kadhaa wanashikiliwa wakihusishwa na uhalifu huo.   “Tunawashikilia ila mpaka sasa siwezi kukueleza idadi yao na kwamba ni wa kikundi cha ugaidi au la. Hao watu tunafanya nao

Mama wa mtoto albino aliyetekwa Geita azungumza alivyojeruhiwa na kuporwa mtoto wake

$
0
0
MAMA wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Yojana Bahati (1), Ester Thomas aliyelazwa katika hospitali ya Bugando akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa, ameelezea jinsi alivyovamiwa na watu wasiojulikana.   Akizungumza na mwandishi wetu, Ester (30) alisema alijeruhiwa juzi nyakati za usiku na watu wasiojulikana mkoani Geita baada ya kumvamia nyumbani kwao na kumpora mtoto wake mwenye ulemavu

Wanafunzi Wanaoshindwa Kulipa ADA Wasifukuzwe Shule

$
0
0
WAKUU wa shule za sekondari wilayani Namtumbo, wamepigwa marufuku kuwafukuza wanafunzi ambao wanashindwa kulipa ada na michango mingine kwa kuwa inawasababisha watoto kupoteza muda wao mwingi wa masomo na hatimaye kufanya vibaya katika mitihani yao.   Aidha wameshauriwa kutafutia njia mbadala na kuandaa utaratibu utakaowabana wazazi hao kulipa ada za watoto wao bila usumbufu, ikiwemo

Ashitakiwa kwa Kumtia Vidole Sehemu za Siri Mtoto wa Miaka Minne

$
0
0
MKAZI wa Bangulo Hali ya Hewa, Baraka Benson (30) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, akikabiliwa na mashitaka ya kumnajisi mtoto wa miaka minne.   Benson alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Hassan Juma.   Wakili wa Serikali, Florida Wenslaus alidai kwamba Desemba 23 mwaka jana, maeneo ya Bangulo Hali ya Hewa
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images