Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Apandishwa Kizimbani kwa Rushwa

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewapandisha mahakamani Mkuu wa  Wilaya ya Mufindi,  Evarista Kalalu na wakurugenzi wawili kwa makosa mawili yanayohusiana na rushwa kinyume na Kifungu cha 32 cha Sheria ya Takukuru Namba 11 ya mwaka 2007. Katika kesi hiyo inayowaunganisha maofisa wengine wawili wa halmashauri ya  wilaya ya Mufindi,  wanatuhumiwa kuisababishia

Uandikishaji Wapiga Kura kwa BVR Wasogezwa Mbele......Utaanza Februari 23

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema katika majaribio ya uandikishaji wananchi kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, mfumo mpya wa uandikishaji wa 'Biometric Voter Registration Kit' (BVR), umefanikiwa kwa asilimia kubwa licha ya changamoto kadhaa, na ina uhakika mfumo huo utatumika kuwaandikisha Watanzania wote katika daftari hilo bila matatizo. Aidha, Tume hiyo imebadilisha tarehe

Mshindi wa Tweet ya Reginald Mengi Atangazwa na Kukabidhiwa Milioni 10 Zake

$
0
0
Mshindi wa Sh milioni 10 katika shindano la wazo bora la biashara linaloendeshwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa twitter ametangazwa na wengine kumi wamejinyakulia kitita cha Sh milioni moja. Fredrick Shayo,  mhitimu wa chuo kikuu na mjasiriamali anayejishughulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji ndiye aliyetangazwa kuwa mshindi

Ray C Amtibua Baba Mwenye Nyumba.....Ni baada ya mkataba wake Kuisha kisha kugoma kutoa Vitu Vyake

$
0
0
Inadaiwa kuwa kimenuka kati ya msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ na baba mwenye nyumba wake, Hussein Kassim baada ya mdada huyo kudaiwa kugoma kutoa vyombo vyake kwenye mgahawa aliopangishwa na mkataba kuisha. Ray C aliyekuwa akitoa huduma ya chakula na vinywaji kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar kupitia mgahawa wake maarufu kwa jina la Ray C Restaurant, alifikia

Upelelezi Kesi ya Wafuasi wa CUF Bado kukamilika

$
0
0
Upelelezi wa kesi ya kutotii amri halali ya polisi na kufanya mkusanyiko usio halali inayowakabili wafuasi 30 wa Chama cha Wananchi (CUF) haujakamilika. Wakili wa Serikali Joseph Maugo alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Emilius Mchauru wakati kesi hiyo ilipotajwa.   Hakimu Mchauru aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 26, mwaka huu itakapotajwa kwa

Alama za Ufaulu Zatesa Wamiliki wa Shule Binafsi

$
0
0
Siku chache baada ya Serikali kusema itazifutia usajili shule zitakazokaidi agizo la kuweka viwango maalumu na tofauti vya ufaulu kutoka kidato kimoja kwenda kingine, wadau wa elimu wamezungumza na kusema agizo hilo linalenga kuua ubora wa taaluma nchini. Akizungumza na mwandishi, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Visivyo vya Serikali (TAMONGSCO), Benjamin

Askari Apigwa Chupa Usoni wakati wa VITA Kati ya Polisi na Bodaboda Dar

$
0
0
Askari wa Jeshi la Polisi amejeruhiwa na madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda katika fujo zilizoibuka juzi jioni katika eneo la Mzinga, Kongowe Mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam katika Manispaa ya Temeke. Akizungumza kwa njia ya simu kuhusiana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Kihenye Kihenya alisema askari walikuwa kwenye doria kwa kutumia pikipiki

Kesi ya Mauaji ya Daudi Mwangosi : Shahidi aeleza Walivyotekeleza Agizo la Kamanda Kamuhanda

$
0
0
Kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Chanel ten, Daudi Mwangosi inayomkabili askari polisi, Pacificus Cleophace, jana ilianza kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Iringa chini ya Jaji Paulo Kihwelo kwa shahidi wa kwanza kuelezea namna walivyotekeleza agizo la aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda.    Shahidi huyo ambaye

CCM watakiwa kuacha Siasa za VITISHO maana Hakuna Mtu Mwenye Hatimiliki ndani ya Chama hicho

$
0
0
MJUMBE wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khamis Mgeja, amewataka baadhi ya viongozi wa chama hicho kuheshimu haki za wanachama na kuacha siasa za kibabe na kibaguzi kwa kuchunga kauli zao.   Pamoja na hilo, amewataka viongozi hao kutambua hakuna mtu mwenye hatimiliki ndani ya chama hicho ila kila mwanachama ana haki sawa ya kukipigania na kukijenga wakati wote.

[VIDEO] Huyu ndo Kiongozi wa Kikundi cha Kigaidi Kinachoua Polisi na Kuiba Silaha Kwenye Vituo Nchini.....Anaitwa Kaisi Bin Abdullah

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu Hatimaye kuvamiwa kwa vituo vya polisi na kuporwa silaha huku askari wake wakiuawa kikatili kumejulikana kunafanywa na nani kufuatia gazeti la Ijumaa kunasa mkanda wa video wa mtu mmoja anayejiita Kaisi Bin Abdullah akijitapa kufanya hivyo kwa lengo la kukusanya silaha ili kulipa kisasi siku si nyingi!   Gazeti  hilo linadai  kuunasa

Je, kwa Hili JB na Kampuni Yake ya Jerusalem Wameteleza Au ndo SWAGA Zenyewe?

$
0
0
Haya ni maoni ya mwanasheria kijana, Alberto Msando kuhusu makosa ya uandishi wa lugha ya kingereza kwenye kasha la filamu ya Mzee wa Swaga, iliyotengenezwa na kampuni ya Jerusalem, inayomilikiwa na msanii nguli wa filamu, Jacob Stephen 'JB '.   Alberto aliandika haya mara baada ya kubandika picha hiyo ya kwenye kasha :   “Bado ni marafiki zangu tu. Ninachotaka ni sanaa yenu

Lipumba Asitisha Maandamano ya Vijana wa CUF

$
0
0
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF)  Profesa Ibrahim Lipumba leo amewasihi Jumuiya ya Vijana wa CUF(JUVICUF) kusitisha maandamano kama jeshi la polisi lilivyoagiza .   Akizungumza leo katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, jijini Dar e s Salaam,  amesema kuwa vijana hao waache kuandamana kwa sababu kunaweza kutokea madhara makubwa ikiwa ni pamoja na  kupigwa risasi,

Umeme Washuka Bei......Bei Mpya Kuanza kutumika Machi Mosi mwaka huu

$
0
0
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imeshusha kidogo bei ya umeme kuanzia Machi Mosi mwaka huu, huku ikisisitiza kwamba bei hiyo itaendelea kupungua zaidi mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam utakapoanza kazi.   Taarifa za hivi karibuni, zimeeleza kuwa bomba hilo limekamilika kwa asilimia 99 na kinachosubiriwa ni pamoja na majaribio ya usafirishaji

Gadner alitongoza na kuwashika makalio wanawake mbele yangu – Lady Jaydee

$
0
0
Wiki hii Lady Jaydee amewapa nafasi mashabiki wake kumuuliza maswali naye kuyajibu kupitia akaunti yake ya Instagram. Ameulizwa maswali mengi, na miongoni mwa maswali hayo ni la kuhusu ndoa yake na mtangazaji wa Radio E-FM Gadner G. Habash. Haya ni maswali na majibu kama alivyopost Instagram. Tunasikia umeachana na mume ni kweli au uzushi? JIBU : Hatuja achana niliamua kumuacha  

Rais Kikwete Afuta ADA ya shule za Sekondari Nchi Nzima

$
0
0
HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete ametimiza ahadi yake aliyoitoa Agosti mwaka jana katika Chuo Kikuu cha Mzumbe cha Morogoro, kwamba amekusudia kufuta ada ya shule za sekondari nchi nzima.   Akizindua Sera mpya ya Elimu na Mafunzo 2014 katika Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Kipawa jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alitangaza kufutwa kwa ada ya sekondari, kuanzia mwakani.   Kwa

Matokeo Form Four: Shule 10 Bora kwa Ufaulu na Shule 10 za Mwisho ziko hapa

$
0
0
Katibu Mtedaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dk Charles Msonde ametangaza matokeo ya mitihani ya Shule za Sekondari ya Kidato cha Nne ya mwaka jana na kusema, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2013. Akizitaja shule kumi bora kwa ufaulu, Dkt Msonde amesema shule hizo ni: Kaizirege mkoa wa Kagera Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza Marian

Watahiniwa 10 waliofanya vizuri Katika Matokeo ya Kidato cha nne

$
0
0
Katibu Mtedaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dk Charles Msonde ametangaza matokeo ya mitihani ya Shule za Sekondari ya Kidato cha Nne ya mwaka jana na kusema, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2013. Dkt Msonde  ametaja watahiniwa 10 waliofanya vizuri kuwa ni: Nyakaho Marungu kutoka Baobab Pwani Elton Sadock Jacob kutoka Feza Boys Dar

Kikundi cha Magaidi kilichoko Tanga Chajeruhi Polisi Wanne na Kuua Mwanajeshi mmoja wa JWTZ wakati wa Mapigano yaliyoanza Juzi Usiku

$
0
0
Askari sita wakiwemo wanne wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamejeruhiwa vibaya kwa risasi wakati wa mapigano baina yao na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wakati wa Msako Maalum wa kutafuta silaha zinazodaiwa kufichwa kwenye moja ya eneo la mapango ya Amboni. Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, amebainisha hayo alasiri ya  jana, wakati akitoa taarifa

Matokeo ya Kidato cha Nne na QT 2014

$
0
0
Ili kuona matokeo ya CSEE, bofya >  Na kwa matokeo ya QT, bofya > Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa ni ongezeko la 10.08% kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235227 sawa na 58.25 walifualu.   Akitangaza matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2014 leo jijini

Moto Wateketeza Maduka eneo la Kibangu, Ubungo jijini Dar es Salaam

$
0
0
Moto  mkubwa uliozuka eneo la Kibangu, Ubungo jijini Dar es Salaam umeteketeza viwanda vya kusaga plastiki, kuchomelea, useremala na kuunguza maduka mawili ya karibu pamoja na vibanda vingine vya biashara eneo hilo.   Watu walioshuhudia moto huo wamesema moto ulianzia katika kiwanda cha plastiki na baadaye kusambaa maeneo mengine huku wakilaumu kikosi cha zimamoto kuchelewa kufika
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images