Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Bunge Linaanza Leo.....Miswada Mitatu Itajadiliwa, Umo ule wa Kuanzisha Mahakama ya Kadhi

$
0
0
Mkutano wa 18 wa Bunge unatarajiwa kuanza leo mjini Dodoma, lakini hoja nzito ambazo zinatarajia kuibua mijadala mizito ni Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2014 na taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Jumla ya miswada mitatu itawasilishwa kwenye mkutano huo, lakini tayari kuna dalili kuwa muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali, ambao

Aunt Ezekiel: Mimba haijanibadili Tabia

$
0
0
Huku kukiwa na tabia kuwa baadhi ya wanawake wanapokuwa wajawazito wanakuwa na tabia za kusumbua na kubagua baadhi ya vitu, msanii wa filamu za Kibongo Aunty Ezekiel ‘Mama Kijacho’, amesema kwa upande wake yuko vile vile na wala hajabadilika. Akiongea  na mpekuzi, Aunty alisema kuwa haoni kama amebadilika kitabia au kuwa msumbufu bali anajiona yupo kawaida ingawa mara nyingine

Jukwaa la Wakristo lapinga Mahakama ya Kadhi kujadiliwa bungeni

$
0
0
Wakati macho na masikio ya Watanzania wengi yakielekea mjini Dodoma kesho katika vikao vya Bunge vinayotarajia kujadili Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali, Jukwaa la Wakristo nchini limeitaka Serikali isitishe kujadili marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria ya Kiislam ya mwaka 1964.    Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo jana inasema Muswada huo unaolenga kuanzishwa kwa

Huyu ndiye aliyekuwa msichana ‘special’ kwenye birthday ya Millard Ayo

$
0
0
Mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Millard Ayo, jana alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa. Kwenye party yake ndogo ambayo aliamua kuifanyia nyumba kwake, ni msichana mmoja tu special aliyepata nafasi exclusive ya kusherehekea naye – Jokate Mwegelo.   “This is what you do after you cook. You eat cake lol. Happy Birthday to the GREATEST to ever do it @millardayo,

Hakuna wa kutembelea nyota yangu -Ray C

$
0
0
Mwanamuziki Ray C ambae alitamba miaka ya nyuma na ngoma kali kibao ikiwemo Na wewe milele,Sogea sogea na nyingine nyingi amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hakuna mtu atakae weza kutembelea nyota yake katika muziki kwani sasa maisha yake ameyakabidhi kwa Mwenyezi Mungu ambaye ndiye mlinzi wake na mwongozaji wake katika maisha,Ray C amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instragram.

Demu wa Kenya Tiara Arudi Tena....Atuma Video Nyingine kwa Diamond Akiwa Anaoga na Kusema Yupo Tayari Kufanya Nae Project

$
0
0
Kuwa Staa raha sana.Baada ya Diamond kutumiwa video na mrembo wa Kenya akimtaka amchukukue yeye bila Malipo huku akijichezesha  kimahaba kwenye hiyo video, Diamond inaonekana hakupata Ujumbe wa kwanza sawa sawa....   Sasa Mrembo huyo amerudi tena na kali zaidi ya ile . Mrembo huyo ajulikanae kama Tiara ameachia  video  nyiningine  akiwa bafuni akioga huku wimbo wa Bebe Cool unaitwa i

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Amsuta Kamanda Kova kuhusu Panya Road.....Ataka Jeshi la Polisi Lijitathmini Upya na Litoe Majibu

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe amesema Watanzania wamepoteza imani na Jeshi la Polisi na ameliagiza kujitathmini na kutoa majibu kuhusu kukamatwa kwa vijana 1,200 wa kikundi cha uhalifu maarufu Panya Road.    Waziri Chikawe aliyekuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka kwa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, amelitaka jeshi hilo kujiuliza na kutoa majibu

Polisi Wavamiwa tena na Majambazi.....Wajeruhiwa na Kuporwa Bunduki Mbili

$
0
0
Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamewavamia na kuwajeruhi askari mwenye no G369 PC Mansour na Hv507 PC Mwalimu, wakiwa doria ya pikipiki ambao walinyang'anywa silaha mbili aina ya SMG no 14301230 na 14303545 na watu wasio julikana mkoani Tanga. Taarifa ya Jeshi hilo kwa vyombo vya habari imesema tukio hilo limetokea Januari 26, 2015 majira ya saa 23:30hrs eneo la barabara 04

Kutoka Bungeni: Muswada wa Takwimu wadunda tena bungeni, warudishwa

$
0
0
Muswada wa Sheria ya Takwimu uliokuwa uwasilishwe bungeni katika mkutano wa 18, hautawasilishwa tena hadi hapo taratibu za kikatiba zitakapokamilika.    Taarifa ya kutowasishwa kwa muswaada huo bila kutaja sababu zilitolewa na Spika wa Bunge, Anne Makinda, muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha leo.   “Muswada wa Takwimu unaondoka kwasababu bado serikali inataka kuufanyia kazi,”

UCHAGUZI MKUU 2015: "Watakaopitishwa kugombea Urais wote wapimwe afya zao kwanza"

$
0
0
Wagombea nafasi ya urais  kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wameshauriwa kupima afya zao kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho, ili kuepuka gharama za matibabu ya mara kwa mara za kiongozi huyo mkubwa wa nchi.  Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, ambapo pamoja na wagombea urais

AIBU: Shilole Amchapa Makofi Mpenzi wake Nuhu Mziwanda

$
0
0
Jumamosi iliyopita ndani ya Tamasha la Kiboko Yao lililofanyika Leaders Club, Gazeti la Makorokocho lilishudia live Msanii Shilole akimchezeshea kichapo mchumba wake Nuh Mziwanda kwa madai kuwa Nuh alikua hataki kuondoka nae eneo la tukio....   Mchekeshaji Steve Nyerere alijitokeza kuamulia ugomvi na kufanikiwa kumtoa Shilole eneo lile lakini baada ya muda Shilole akarudi na kumdai funguo

Mabomu Yatawala Mbagala katika Maandamano ya CUF.....Profesa Lipumba na wafuasi wake watiwa mbaroni

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata wananchama wa Chama cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti Taifa wa chama hicho,Profesa Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano ambayo si halali. Awali polisi ilizuia  maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho ya  kuadhimisha kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na mateso ya wananchi wa Zanzibar na Bara

Serikali yapiga marufuku shule binafsi nchini kuwafukuza wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani

$
0
0
Serikali imezipiga marufuku shule binafsi nchini kuwafukuza ama kuwasitishia masomo wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani na kwamba shule zote zitakazokiuka agizo hilo zitachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili. Serikali pia imesema kuwa kuanzia mwaka 2016 itaanza kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha Nne.   Onyo hilo la serikali kwa wamiliki wa

Chenge,Tibaijuka kuburuzwa baraza la Maadili

$
0
0
Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma litawaweka kiti moto watuhumiwa  9 ambao ni viongozi wanaohusishwa na kashfa ya akaunti ya uchotaji wa fedha kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow. Viongozi hao watawekwa kiti moto kwa uwazi mwanzoni mwa mwezi ujao kwenye ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam. Habari zinaeleza kuwa watakaoitwa ni wale viongozi wote ambao wanaowajibika chini ya Sheria ya

Kijana Auawa na Kutelekezwa Karibu na Kambi ya FFU

$
0
0
Kijana ambaye hakufahamika jina anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35 amekutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa katika eneo la kambi ya Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kata ya Nshambya mkoani Kagera. Mwili huo uligundulika majira ya saa sita mchana baada ya watu waliopita katika eneo hilo kuuona ukiwa umelazwa karibu na moja ya shamba lililopo mtaa wa Bunkango eneo

Wanasayansi ‘Bongo’ kusafisha maji ya kinyesi kuwa ya kunywa

$
0
0
Umeshikwa na kiu? Unaingia katika duka lililo jirani na kununua maji ya chupa kwa ajili ya kunywa. Lakini ukapatwa na udadisi kutaka kujua maji hayo yametengenezwa na nini. Unaposoma kilichotumika kutengeneza maji hayo, unagundua kuwa yametengenezwa kwa kinyesi.    Je, utakunywa au kiu yako ya maji itakatika kwa kinyaa na mshangao.   Kama ilivyowezekana Marekani katika Kampuni ya

Sakata la Lipumba kupigwa jana: Vurugu zaibuka Bungeni, Spika Makinda ahairisha Bunge hadi saa 10 jioni [Video ya tukio iko hapa]

$
0
0
Spika wa Bunge Anna Makinda leo amelazimika kuahirisha kikao cha Bunge kilichoanza jana, baada ya vurugu zilizotokea  baada ya kutolewa kwa hoja binafsi kutoka kwa Mbunge na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia kuhusu jeshi la polisi kumshambulia Profesa Ibrahimu Lipumba jana akiwa kwenye maandamano .   Akizungumza katika Bunge hilo Mbatia amesema kuwa kitendo cha polisi

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara nchini Afikishwa Mahakani chini ya Ulinzi Mkali

$
0
0
Mwenyekiti wa taifa wa jumuiya ya wafanyabishara bwana Johnson Minja aliyekamatwa na jeshi la Polisi juzi tayari leo tarehe 28 amefikishwa katika Mahakama kuu kanda ya Dodoma akikabiliwa na makosa mawili  ambayo  ni  : 1.kosa la uchochezi. 2.Kuhamasisha wafanya biashara kukataa matumizi ya mashine za kieletronic za kutolea risiti za EFDs.   Wafanyabiashara wa  soko  la  kariakoo

Lipumba kupigwa: Bunge Lahairishwa tena hadi Kesho Asubuhi

$
0
0
Spika wa Bunge Anna Makinda   jioni  hii  amelazimika kuahirisha  tena  kikao cha Bunge hadi kesho asubuhi  kwa  madai  kuwa  serikali  bado  inajipanga  kutoa  majibu  sahihi  kutokana  na  tukio  la  kupigwa  mabomu  Mwenyekiti  wa  Chama  cha  CUF, Profesa  Ibrahim  Lipumba. Kuahirishwa  kwa  bunge  kumetokana na vurugu zilizotokea    leo  asubuhi bungeni baada ya kutolewa kwa hoja

Kwa nini Leo Zitto Kabwe Alitia Mgomo wa kwenda kusoma taarifa ya PAC Bungeni?????.....Majibu yote Yako hapa.

$
0
0
Wakati  wa  Vurugu  za  Asubuhi  leo  Bungeni, Spika  wa  Bunge  alimtaka  Mwenyekiti wa  PAC, Mh Zitto  Kabwe  aende   kusoma  taarifa  ya  kamati yake.... Kilichotokea  ni  kwamba, Zitto  alitia  mgomo, nikiwa  na  maana  kwamba  alipuuza  agizo  hilo  na  hakunyanyuka  kabisa.    Unajua  ni  kwa  nini? Zitto  Kabwe  mwenyewe  amekwisha  lijibu  hilo  swali  kupitia  ukurasa  wake  wa
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images