Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ngono, bangi ‘nje nje’ mgodini Ihanzutwa

0
0
Wengi huisikia dhahabu, sifa zake na thamani yake. Wenye fedha zao hununua vidani vya madini hayo adimu ulimwenguni na kujirembesha, lakini wale maskini hujikuta wakivaa vidani yaliyotiwa tu nakshi ya madini hayo, huku asilimia kubwa vikiwa vimetengenzwa kwa bati.    Mbali ya wenye fedha kidogo, wapo baadhi ambao maisha yao yote hutegemea ‘kupiga roba’ watu waliovaa vidani hivyo ili

Chuchu Hans Afungukia madai ya kuachana na Mpenzi wake Vicent Kigosi ‘Ray’

0
0
Staa  wa Filamu Bongo, Chuchu Hans juzikati alifungukia madai ya kwamba ameachana na mchumba wake Vicent Kigosi ‘Ray’, akaeleza kuwa, hakuna ukweli wowote juu ya hilo.   Chuchu alifikia uamuzi wa kufafanua juu ya madai hayo juzi kufuatia tetesi zilizokuwa zimeenea kwamba yeye na kipenzi chake huyo wametibuana na sasa kila mtu kimpango wake. Akifungukia juu ya uvumi huo Chuchu

Jina la Kajala Kuonekana Kwenye Soda za Kopo za Coca-Cola

0
0
Mwigizaji wa filamu mwenye sura ya upole na umbo la Kiafrika, Kajala Masanja ni moja kati ya watu ambao majina yao yataonekana kwenye makopo mapya ya kinywaji cha Coca-cola.   Jana  mchana, wawakilishi wa coca-cola walimtembelea Kajala nyumbani kwake na kumpatia  zawaidi ya kinywaji hicho kikiwa kwenye chupa yenye jina lake.   Endelea kuwa nasi kujua kinanani wengine wamebahatika

Mtoto afariki kwa kunywa pombe yenye sumu Singida

0
0
Mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja amefariki dunia baada ya kunywa pombe ya kienyeji aina ya Mtukulu inayosadikiwa kuwa na sumu mkoani Singida. Kamanda wa Polisi Mkoani Singida ACP Thobias Sedoyeka amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea majira ya saa 3 asubuhi siku ya Alhamisi tarehe 08 Januari, 2015 na kusema kuwa mama wa mtoto amelazwa katika hospitali ya Makingu

Rais Kikwete Awataka Viongozi wa Dini Waendelee Kuliombea Amani Taifa

0
0
Rais Jakaya Kikwete amewaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuendelea kuliombea taifa na watanzania kwa ujumla ili waweze kukabiliana na majukumu mengi na makubwa yaliyoko mbele yao kwa amani na utulivu likiwemo la kupata katiba mpya.   Katika salam zake kwenye hafla ya kumsimika Askofu Solomon Masangwa wa Dayosisi ya Kaskazin Kati

Kafulila: watimueni kabla ya Bunge

0
0
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila amesema kuna kila sababu wahusika wote wa sakata la uchotwaji Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow, wawe wamefukuzwa kazi kabla ya kuanza kwa mkutano ujao wa 18 wa Bunge.   Pia, amesema fedha zilizochotwa zirejeshwe kama ilivyokuwa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na wafikishwe mahakamani.   Akihutubia mamia ya

Askari waliosababisha kifo Serengeti kubanwa

0
0
Polisi mkoani Mara imesema itawachukulia hatua askari watakaobainika kuhusu katika kifo cha Samson Nyakiha (70) baada ya uongozi wa jeshi hilo kukutana na ndugu wa marehemu waliotelekeza maiti katika Kituo cha Polisi cha Wilaya.   Kamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai wa mkoa, RCO Rogathe Mlasani alitoa ahadi hiyo katika kikao cha pamoja cha ndugu na uongozi wa polisi wa Wilaya ya

Lowassa asema kulinda amani ni jukumu la wote

0
0
Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa  amesema hakuna mtu yeyote mwenye hatimiliki ya  Tanzania hivyo Watanzania wote wanao wajibu wa  kuilinda na kudumisha amani na utulivu uliopo.   Akitoa salamu wakati wa ibada ya kumweka wakfu Mchungaji Solomon Massangwa kuwa Askofu wa Kanisa  la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi  ya Kaskazini Kati, Arusha jana, Lowassa alisema  amani

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' Anusurika Kufa katika Ajali ya Gari

0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) amenusurika kifo baada ya kupata ajali katika Milima ya Kitonga, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.   “Shetani amefeli, Mungu ni mwema. Tuko salama mimi na wote niliokuwa nao kwenye gari,” alisema mbunge huyo anayejulikana zaidi kwa jina la Sugu, katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa facebook.   Akizungumza kwa simu kutoka

Wafanyabiashara wa nyama Bukoba wagoma

0
0
Wafanyabiashara wa mifugoa mjini Bukoba wamegoma kuchinja mifugo yao na kutofungua mabucha wakilalamikia kuamrishwa na serikali kupunguza bei ya nyama kutoka shilingi 5,000 hadi 4,000 kwa kilo. Wakiongea katika machinjio ya Rwamishenye mjini Bukoba wafanyabiashara hao wamesema wamegoma kuchinja mifugo hiyo na kutofungua mabucha kabisa kutokana na barua waliyopewa kutoka kwa

Magari 150 Tanzania yazuiwa kuingia Kenya

0
0
MAGARI zaidi ya 150 yanayofanya safari za kupeleka wageni na watalii maarufu ‘Shuttle’ kati ya jijini Arusha na Moshi kwenda katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata nchini Kenya yamezuiliwa kuingia katika uwanja huo toka Desemba 22 mwaka jana.   Uamuzi huo wa serikali ya Kenya unataka kuishinikiza Serikali ya Tanzania kutaka lango la Bologonja lililofungwa toka enzi za utawala

Pinda asema kauli yake ya wapigeni ilimaanisha amani

0
0
Neno “piga” lina maana ya “fanya kitendo cha kukutanisha vitu kwa nguvu, fumua, ezeka, zaba, shambulia, chapa na tandika” kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Oxford, lakini kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda neno “wapigeni” lilimaanisha “kuendelea kulinda amani”.   ‘‘Baada ya kutoa kauli  hiyo  kuna watu wakaeleza kuwa sasa Waziri Mkuu analeta sera za kupiga. Hapana ilikuwa kujaribu

Wazungu Wazidi Kukaza Kamba Kashfa ya Escrow......Mabalozi wasema hawajaridhishwa na Maamuzi yaliyochukuliwa na Srikali

0
0
 Licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa ufafanuzi wa sakata la uchotaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu na kutangaza kuchukua hatua dhidi ya baadhi ya viongozi na watendaji, nchi wahisani wamesema bado suala hilo linawachanganya na wanasubiri tamko la Serikali.   Nchi hizo, ambazo zilizuia takriban Sh1 trilioni za ufadhili na kuchangia nakisi ya bajeti ya

Rais Kikwete Aongoza kikao cha kamati kuu ya CCM Mjini Unguja leo

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mjumbe wa Kamti Kuu ya CCM Taifa Dk.Mohammed Gharib Bilali wakati alipowasili Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo katika Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.

Lulu: Mapedeshee ndiyo wanawalipa wasanii wa kike siyo filamu

0
0
ELIZABERTH Michael‘ Lulu’ amefunguka kuwa wasanii wa kike wa filamu wana biashara nyingine iliyojificha ndani ya ile ya filamu ambayo inawalipa zaidi.   Lulu amepasua kuwa wasanii hao wanawategemea mapedejshee kuendesha maisha yao huku wengi wakiamini kwamba mabinti hao wa Bongo Movie wanalipwa vizuri kutokana na filamu wanazoigiza.   “Ukweli hauko hivyo, hali hii inatokana na wengi

Monalisa: Taratibu tunatoboa kimataifa

0
0
Muigizaji wa filamu hapa Bongo, Yvone Cherry maarufu kama Monalisa, amesema kuwa milango ya kufanya kazi za filamu kimataifa imeanza kufunguka, akiwa tayari na project aliyofanya na timu kutoka Marekani, Daddy's Wedding itakayotoka Februari 14.   Monalisa amesema kuwa, mbali na kazi hii, ana project nyingine na timu kutoka UK kati ya nyingine ambazo zinaonesha kuwa taratibu sanaa hii

Irene uwoya- Nataka kutambulika nje ya Nchi kuliko Tanzania

0
0
Katika kile kinachoonekana waigizaji wa kike kutaka kukuza tasnia ya uigizaji kwa kuvuka mipaka ya nchi, mwigizaji Irene Uwoya amesema kuwa anataka atambulike nje ya nchi kuliko ndani.   Akiweka hoja yake sawa, mwanadada huyo anayedaiwa kuendelea kuwa na mvuto katika tasnia ya filamu alisema anajua kuwa siyo jambo rahisi kufanya vizuri nje ya nchi, lakini huko ndiko anakotaka kufika,

Shamsa: Nalala na Mume Wangu Nikiwa Kambini

0
0
Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ambae ameolewa na ana mtoto mmoja, amesema kuwa mara kadhaa anapokuwa kambini akishuti filamu mume wake, Dickson Matoke huwa anamfuata na kulala naye hadi asubuhi huku akiamini kufanya hivyo kunachangia kutochepuka.   Akizungumza na Uwazi, Shamsa alisema kuwa kitendo cha mumewe kumfuata haina maana kwamba wanavunja sheria zao bali hilo

Utafiti: Matangazo ya barabarani yenye wasichana waliovaa kimitego huwachanganya madereva

0
0
Matangazo ya barabarani (billboards) yenye picha za wanawake waliovaa nguo za mitego huwachanganya madereva na yanaweza kusababisha ajali, utafiti umesema. Watafiti kwenye chuo kikuu cha Alberta wamebaini kuwa matangazo yenye picha za aina hizo huathiri tabia za uendeshaji.   Utafiti huo ulionesha kuwa matangazo ya aina hiyo yana madhara ikiwemo kuhatarisha usalama wa watu,

Vanessa Mdee awa msanii wa pili Tanzania kuwa na akaunti ya VEVO, baada ya Gosby

0
0
Vanessa Mdee a.k.a Vee Money amekuwa mwanamuziki wa pili Tanzania kupata akaunti ya VEVO kwaajili ya kuweka video zake. VEVO ni mtandao mkubwa namba moja duniani unaohusika kuhifadhi na kurusha kazi za wanamuziki maarufu duniani kama kina Nicki Minaj, Beyonce, Jay Z na wengine.   Gosby ndiye alikuwa msanii wa kwanza wa kizazi kipya kupata akaunti kwenye mtandao huo unaomilikiwa na
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images