Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Diamond aonjesha picha ya video mpya na model mrembo wa kizungu!

0
0
Diamond Platnumz alipata A kwenye somo la kucheza na akili ya mashabiki wake. Siku za hivi karibuni staa huyo amekuwa akitease mashairi ya kile kinachoonekana kama wimbo wake ujao. Na sasa amewapa mashabiki wake kitu kingine.. picha inayoonekana kuwa ni video yake mpya. Hicho ndicho kitu pekee ambacho staa huyo huwa hatua 100 mbele zaidi ya wasanii wengi katika kazi zake. Kupitia

Tanzania yaingia kwenye kashfa mpya, ni mpango wa kuwahamisha wamasai 40,000 ili kuwapa Waarabu eneo la kuwindia

0
0
Ikiwa bado Tanzania inakabiliwa na skendo ya pembe za ndovu zinazodaiwa kuondoka na ndege ya rais wa China alizuru nchini, kashfa nyingine kubwa imezuka! Tanzania inashutumiwa kurejesha mpango wa kuwahamisha wamasai 40,000 katika eneo waliloishi kwa miaka na miaka, ili kuipa eneo hilo familia ya kifalme ya Dubai kwaajili ya kuwinda wanyama.   Mwaka jana serikali ilidai kuahirisha

Hospitali Za Serikali Majanga Matupu.....Muhimbili Vifo Nje Nje!

0
0
Hakufai. Pengine ni neno linaloweza kuwakilisha uhalisi wa hali ilivyo katika baadhi ya hospitali kadhaa za Serikali nchini, ambako mamia ya wagonjwa wanateseka kutokana na uhaba wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba ambao umeendelea kuzikumba.   Wengi wa wagonjwa waliohojiwa wanalalamikia kushindwa kumudu gharama za dawa ambazo wanapaswa kuzinunua kwenye maduka wakisema hali hiyo

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu Aongeza Askari Kiteto Kuimarisha Ulinzi

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akimsikiliza Diwani wa Kata ya Matui Wilayani Kiteto Bw.Athuman Kidawa wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa  vifo.kushoto ni Afisa tarafa wa Matui Bw.Eliakimu Ndelekwa.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la  Polisi)

Sijatangaza Kugombea Au Kutogombea Urais- Dkt. Shein

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema hajatangaza kugombea au kutogombea Uraisi kwa Awamu nyingine visiwani humo na wanaomtangazia kuwa hagombei tena waache kudanganya.   Dkt. Shein ametoa kauli hiyo Visiwani humo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM, ikiwa ni miongoni mwa mikakakati ya kuimarisha chama ambapo amesema

Mwanamke Afanyiwa Ukatili wa Kutisha Jijini Arusha

0
0
Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Olkokola Wilayani Arumeru Mkoani Arusha amefanyiwa ukatili wa kutisha kwa kukatwakatwa na Panga kichwani na kuondolewa kiganja cha Mkono, sikio na sehemu nyingine za mwili wake    Mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Paulina Joseph amefanyiwa ukatili huo na mtu anayedaiwa kuwa ni shemeji yake kwa madai ya kuingilia ndoa yake.   Tukio hilo

Soko la Vinyago Arusha lateketea kwa moto

0
0
Soko  la  vinyago  lililoko  karibu na  ofisi ya   CCM   wilaya   ya   Arusha  limeteketea   kwa   moto  usiku  wa  kuamkia    tarehe 18 Novemba 2014  na kusababisha  hasara  ya  mabilioni  ya  fedha. Wananchi  na  wafanyabiashara  ambao  vibanda  na  mali  zao   zote zimeteketea   wamesema walianza kupata   taarifa   za  moto  huo  usiku  wa kati ya saa  tatu  na saa   Nne    na  

Tarehe ya kujiandikisha kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa

0
0
Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Bwana Kharist Michael Luanda amesema wananchi wanapaswa kujiandikisha katika daftari maalum la kupigia kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia tarehe 23/11/2014 hadi tarehe 29/11/2014. Mkurugenzi huyo alisema kuwa wananchi wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za

Wema Sepetu Aanika Kisa Cha Kuachana na Diamond

0
0
MISS Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amevunja ukimya kwa kuamua kuanika kisa cha yeye kummwaga aliyekuwa mwandani wake, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Akizungumza na Amani katika mahojiano maalum jijini Dar, juzikati, Wema alianza kwa kufunguka kwamba, kuna watu wamekuwa wakizungumzia ishu ya yeye

Miss Sinza 2001, Husna Maulid Akumbwa na Skendo ya Picha Za Utupu

0
0
Miss Sinza 2001 na aliyekuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid ameonesha kuwa ni sikio la kufa baada ya kupiga picha za utupu kwa mara nyingine. Picha hizo zilizotapakaa kwenye mitandao mbalimbali zimewashangaza watu ambapo Husna anaonekana akiwa kama alivyozaliwa huku akiwa katika mapozi tofauti hali inayoonesha kwamba alikuwa akipigwa picha hizo na mpenzi wake.  

Udini vyuo vikuu : Serikali yapiga marufuku wanafunzi kufanya mitihani siku ya Ijumaa na Jumamosi .....Wizara yatoa waraka maalumu

0
0
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imezuia uongozi wa vyuo vikuu nchini kuwalazimisha wanafunzi kuingia darasani au kufanya mitihani kwa siku zao za ibada. Ingawa hazikutajwa, siku maalum za ibada zilizozoeleka kwa madhehebu mengi ni Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Agizo la Serikali limetolewa na C.P. Mgimba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya

Polisi aliyeua mwanafunzi wa Chuo Kikuu jijini Mbeya ahukumiwa kifo

0
0
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya imemhukumu kunyongwa hadi kufa polisi wa upelelezi, Maduhu, F 5842, aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Daniel Mwakyusa. Aidha, mahakama hiyo imewaachia huru washitakiwa wengine wawili wa kesi hiyo, polisi wa upelelezi, Shaaban, F 7769, na polisi wa kike mpelelezi, Neema, F 6545, baada ya

Mfanyabiashara Afariki Dunia Akifanya Mapenzi Ndani Ya Gari Lake Huko Kagera

0
0
Polisi mkoani Kagera inachunguza kifo cha mmiliki wa ukumbi wa klabu ya usiku ya Linas Night, Leonard Mtensa (50) ambaye inadaiwa alifariki dunia wakati akifanya mapenzi kwenye gari lake. Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alisema Mtensa, ambaye alikuwa na mpenzi wake kwenye gari maeneo ya Buyekera, alifariki dunia kabla ya kufikishwa kituo cha afya cha ELCT Ndolage.

Vijana, wanawake waongoza kwa maambukizi ya UKIMWI

0
0
Tume ya kudhibiti ukimwi nchini Tanzania TACAIDS imelitaja kundi la Wanawake na Vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 25 kuwa ndio makundi makubwa yanayoongoza kwa kuwa na virusi vya ugonjwa hatari wa ukimwi hapa nchini.   Mwenyekiti wa TACAIDS Dkt. Fatma Mrisho amesema hayo jana jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani Desemba

Taarifa ya Haraka kwa Vyombo vya Habari Kuhusu Mpango wa Serikali Kuwahamisha Wamasai 40,000 kumpisha Mwarabu afanye kazi ya Uwindaji

0
0
Sisi Viongozi wa Mila, Kisiasa, Wawakilishi wa Wanawake tumesikitishwa sana na Taarifa ya uongo aliyoitoa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu juu ya ukweli wa Mgogoro wa Loliondo. Ifuatayo  ni ufafanuzi wa hali halisi kinyume na Waziri alivyodanganya Dunia kupitia BBC tarehe 19/11/2014 na Gazeti la leo la Mwananchi Kwamba eneo la Loliondo halina Wamaasai 40,000

Rais Kikwete atolewa nyuzi.....Afya yake inaimarika na Anaendelea Vizuri

0
0
Rais Jakaya M. Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri. Kulia kwake ni Daktari wa Rais, Profesa Mohamed Janabi Rais Kikwete akiwa amepumzika kwenye hoteli

Serikali kuja na adhabu mbadala kwa makosa madogo ili kupunguza msongamano Magerezani

0
0
Serikali ya Tanzania imesema ipo kwenye mchakato wa kuandaa adhabu mbadala kwa wahalifu wa makosa madogo madogo ili kupunguza msongamano magerezani ambao kwa sasa unapelekea hali mbaya katika Magereza hayo.   Akijibu swali bungeni mjini Dodoma jana kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi Bi. Celina Kombani amesema hali ya msongamano kwa

Kaimu Rais Atimuliwa Zambia

0
0
Aliyekuwa rais wa mpito nchi ya Zambia, Guys Scott.   Chama tawala nchini Zambia (PF) kimemtimua kaimu rais wa nchi hiyo Guys Scott kutoka chamani kwa kuvunja utaratibu wa katiba.   Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho. ''Amekuwa akiwaajiri na kuwafuta watu kazi ovyo na pia bila ya kushauriana na kamati kuu ya chama,'' amesema Malozo Sichone.   Bwana Scott, ambaye

Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono Alishwa SUMU

0
0
Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono amelishwa sumu wakati akiwa kwenye safari ya kikazi jijini London nchini Uingereza, imeelezwa.   Kwa mujibu wa tovuti ya The Citizen, Mkono ambaye pia ni mwanasheria maarufu, aliugua ghafla alipokuwa jijini humo.    Madaktari wake walisema kuwa alikuwa amelishwa sumu iliyokuwa imekusudiwa kuharibu figo zake ndani ya saa 72.   “Ilikuwa siku

Sita wafariki kwa kupigwa na radi Songea

0
0
Watu Sita wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa wilayani Songea mkoani Ruvuma baada ya kupigwa na radi kufuati mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo.   Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela amesema kuwa maafa hayo yalitokea majira ya saa mbili usiku wakati watu hao wakila chakula cha usiku kwenye mgahawa wa chuo cha kilimo na mifugo cha Liti Madaba
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images