Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Watu Watatu wauawa katika mapigano ya wakulima na wafugaji huko Kigoma

0
0
Watu watatu wamekufa na wengine hawajulikani walipo baada ya kuzuka mapigano ya kugombea ardhi kati ya Wafugaji na Wakulima katika kijiji cha Kinyinya kata ya Nyamtukuza wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.   Mapigano hayo yametokea siku ya Jumatatu (Oktoba 20) katika eneo la mashambani katika kijiji hicho, baada ya mfugaji mmoja kuuawa na mifugo yake kukatwakatwa Jumatano iliyopita,

Muigizaji Wa Filamu Nchini Sherry Charles Magali Afariki Dunia.

0
0
Muigizaji wa filamu hasa za vichekesho nchini Sherry Charles Magali amefariki dunia jana saa nne asubuhi  katika hospitali ya rufaa Morogoro.    Sherry ambaye amecheza filamu nyingi amefariki baada ya kuugua muda mrefu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Ufisadi wa kutisha.......CAG afichua Sh. milioni 214/- zilivyolipwa waliofeli UDOM, IFM na mabilioni yanavyoliwa Tanesco

0
0
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inayoishia Juni 30, mwaka 2013, imeanika matumizi mabaya ya fedha za umma. Ripoti hiyo imehusisha mashirika mengi ya umma yakiwamo Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), Bodi ya Korosho, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),

JWTZ na Jeshi la China Wafanya Mazoezi ya Kijeshi Pamoja......Picha zote ziko hapa

0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kamandi ya Jeshi la Wanamaji  kwa kushirikiana na Jeshi la Watu wa China wamezindua mazoezi ya siku 30 kwa kikosi maalumu cha Marine. Lengo la mazoezi hayo ni kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi kwa maafisa ikiwa ni njia mojawapo ya kukuza uhusiano uliodumu kwa miaka mingi kati ya China na Tanzania. Mkuu wa mafunzo na utendaji wa

Watu 40 wakamatwa mkoani Katavi baada ya kukutwa wakinywa pomba saa za kazi za ujenzi wa taifa.

0
0
WAKAZI 40 wa Tarafa ya Inyonga, Makao Makuu ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wamekamatwa baada ya kukutwa wakinywa pombe asubuhi vilabuni na kwenye maduka yanayouza aina mbalimbali ya vinywaji.   Wakazi hao ni pamoja na wanywaji wenyewe na wauzaji wa pombe hizo wakiwemo pia wachezaji wa mchezo wa pool ambapo walikiuka amri ya Mkuu wa Wilaya, Kanali Ngelela Lubinga ya kutocheza pool au

Kimenuka sare za jeshi ( JWTZ) .....Meneja wa Diamond akamatwa na Polisi, Nay wa Mitego naye matatani

0
0
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Diamond Platnumz, Nay wa Mitego na wasanii wengine waliovaa sare za jeshi kwenye show ya Fiesta Jumamosi iliyopita wapo matatani. Wasanii hao wamepewa amri na jeshi la polisi kuzirudisha wao wenyewe sare hizo kwenye kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kuna taarifa kuwa meneja wa Diamond, Babutale alikuwa akishikiliwa na polisi

Taarifa kuhusiana na bweni la wanafunzi wa shule ya Sekondari kuteketea kwa moto huko Tabora

0
0
Ajali kubwa ya moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika, imetokea na kuteketeza bweni la wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mtakatifu Petro iliyopo eneo la Iwanzari, Tabora pamoja na vitu vyote vilivyokuwemo ndani ya bweni hilo.    ITV wameripoti kuhusiana na tukio hilo, ambapo moto huo umezuka ghafla wakati wanafunzi wakiwa katika ibada na hata baada ya taarifa kuwafikia askari wa

Mwanajeshi wa JWTZ Aliyeua Mtu akimtuhumu kumsumbua Mkewe Afikishwa Mahakamani

0
0
Polisi wakiondoka mahakama ya wilaya Temeke leo na Mwanajeshi huyo. ****** Mwanajeshi wa JWTZ aliyeua mtu mwishoni mwa wiki iliyopita  akimtuhumu  kumsumbua  mkewe  wakati  wakiwa  baa, Octavian Maurus Gowele amefikishwa mahakama ya wilaya Temeke leo akishtakiwa kwa mauaji.    Mwanajeshi  huyo  amekana shitaka hilo na  kesi yake imeahirishwa mpaka Novemba 4, 2014.

Kauli rasmi ya Serikali kuhusu tetesi za kuwepo 'mgonjwa wa Ebola' Nchini

0
0
Utangulizi Mnamo tarehe 18 Oktoba 2014, Wizara ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ya kuwepo kwa mgonjwa aliyehisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola. Mgonjwa huyu aliyekuwa na umri wa miaka 17, jinsia ya Kike na mkazi wa kijiji cha Bupandwa Tarafa ya Kahunda Wilaya ya Sengerema, alilazwa akiwa na dalili za homa kali, manjano, kutokwa na damu sehemu mbalimbali za

Diamond Platnumz akamatwa na jeshi la Polisi.....Ahojiwa kwa masaa kadhaa na kuachiwa kwa Dhamana!

0
0
Baada ya meneja  wake  kukamatwa  jana  jioni  na wacheza shoo wake kukamatwa  leo  asubuhi, hatimaye Diamond naye amejisalimisha  Kituo cha Polisi cha Oyster Bay... Baada  ya  msanii  huyo  kujisalimisha, alihojiwa kwa masaa kadhaa kisha akaachiwa kwa dhamana baada ya kukabidhi sare za JWTZ  kituoni hapo.

Picha: Wengi wajitokeza kumzika msanii wa TMK Wanaume Family, YP

0
0
Mwili wa msanii 'YP' ambaye alifariki usiku wa kuamkia juzi katika hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam, umezikwa jana  kwenye makaburi ya Chang'ombe.   Mwili wa marehemu YP uliagwa jana mchana huko TCC Sigara Chang'ombe ambapo wasanii na wadau mbalimbali katika tasnia ya burudani walihudhuria mazishi ya msanii huyo kutoka kundi la TMK Wanaume Family.   Mungu ailaze roho ya

Vyeti vya Miss Tanzania 2014 vyaanza kuchunguzwa na RITA, ikibidi Polisi kuhusishwa

0
0
WAKALA wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), imeanza uchunguzi wa vyeti vya Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu, baada ya kuibuka utata wa taarifa za kuwapo vyeti viwili vinavyotofautiana maelezo.Uchunguzi wetu umethibitisha kuwapo upekuzi maalumu wa nyaraka alizowasilisha Sitti katika ofisi za RITA Temeke ili kubaini kwanza uhalali wa cheti, kabla ya kutafuta ukweli wa taarifa

Pinda atangaza Rasmi Kuwania Urais 2015

0
0
Siyo tetesi tena. Sasa ni rasmi kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amekuwa akitajwa kuwania urais amethibitisha wazi kuwa atagombea kiti hicho katika uchaguzi mkuu mwakani.    Alitoa uthibitisho huo juzi akiwa London, Uingereza ambako yuko katika shughuli za kikazi. Hatua hiyo inaondoa uvumi ambao umekuwapo kwa takriban miezi mitatu sasa kwamba naye tayari ameingia katika

Kiwango cha uwekezaji wa China kinavutia – Kikwete

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anafurahishwa na kiwango cha uwekezaji wa makampuni ya Jamhuri ya Watu wa China katika uchumi wa Tanzania ambao hadi mwishoni mwa mwaka jana ulikuwa umefikia miradi 522 yenye thamani ya dola za Marekani 2,490.21 milioni (dola bilioni 2.5).   Rais Kikwete amesema kuwa kiwango hicho kinaufanya

Mauaji yasababisha machimbo kufungwa Kigoma

0
0
Serikali mkoani kigoma imeyafunga machimbo madogomadogo ya dhahabu katika kata ya Nyamtukuza wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, kutokana na kudaiwa kuwa chanzo cha mauaji ya watu watatu yaliyotokea mwishoni mwa wiki kufuatia ugomvi wa kugombea ardhi katika kijiji cha Minyinya. Akihutubia wananchi katika kijiji cha Minyinya, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya amesema,

Mgombea Udiwani 2015 Anaswa na Mwanafunzi Gesti

0
0
Mwanaume mmoja anayesemekana ni mfanyabiashara ambaye pia anatajwa kugombea udiwani wa kata moja iliyopo  Kinondoni jijini Dar es Salaam, aliyetajwa kwa jina moja la  mzee Beno amenaswa akiwa chumba cha gesti na mwanafunzi wa chuo kimoja kilichopo Kibamba jijini Dar. Tukio hilo la aina yake lilijiri Oktoba 20, mwaka huu ndani ya gesti moja  iliyopo Kimara-Suka jijini Dar es Salaam

Rais Kikwete Asema Urais ni kazi ngumu sana....Aona muda wa kumaliza Ngwe yake 2015 unachelewa, Aeleza anavyotamani kuishi baada ya kutoka Ikulu

0
0
RAIS Jakaya Kikwete amesema mfumo unaotumika Tanzania ambako Rais anatumikia nafasi ya uongozi kwa muhula wa miaka mitano na si zaidi ya miaka 10 ni mzuri na unaovutia kwa sababu unaiwezesha nchi kupata fikra na mawazo mapya.   Aidha, Rais Kikwete amesema, anaamini Tanzania itapata Rais bora zaidi kuliko yeye, atayeiwezesha Tanzania kusonga mbele kwa kasi kubwa zaidi.   Rais Kikwete pia

Mume Ajinyonga kwa kamba ya katani hadi kufa baada ya KUMUUA Mkewe kwa kumchinja Shingo

0
0
MWANAMUME mwenye umri wa miaka 30 amejinyonga kwa kamba ya katani hadi kufa baada ya kumuua mkewe kwa kumchinja shingo kwa kisu kutokana na kile alichodai kuwa ni kudharauliwa na mkewe.   Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela ambaye amemtaja mwanamume huyo kuwa ni Ramadhani Abdallah, mkulima na mkazi wa kijiji cha Makale katika kata ya Mitundu,

Majambazi yapora Sh. Bilioni moja Benki ya Stanbic Dar....Wafanyakazi tisa wa Benki hiyo watiwa mbaroni

0
0
Watu 13 wakiwamo wafanyakazi tisa wa Benki ya Stanbic jijini Dar wanashikiliwa na polisi baada ya majambazi kuiba fedha zaidi ya Sh1 bilioni jana jioni.    Watu hao wanashikiliwa katika Kituo cha Oysterbay kwa uchunguzi zaidi wa uporaji huo uliofanywa na majambazi yenye silaha yaliyoingia katika Tawi la benki hiyo la Mayfair Plaza lililopo Barabara ya Mwai Kibaki na kutokomea na kitita

Je, unasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume?? Unataka kuimarisha mishipa yako ili uweze kwenda Raundi mbili na kuendelea??....Bofya hapa ukutane na JIKO

0
0
Neema  Herbalist  & Nutritional  Foods  Clinic  ni  wauzaji wa dawa  mbalimbali  za  asili. Tunapenda  kuwatangazia  wateja  wetu  kuwa  tunayo  dawa nzuri  ya  asili  inatibu na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.  Dawa  hii iitwayo  JIKO  ni  ya  asili  kabisa  (PURE HERBAL) na inaponyesha  na  kumaliza  kabisa  tatizo  la  nguvu  za kiume
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images