Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

‘Kwaheri Tanzania’ Davido atoa shukrani zake baada ya kutumbuiza kwenye Fiesta!

$
0
0
Kuanzia Ijumaa iliyopita kulikuwa na taarifa kuwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam imemzuia Davido kutumbuiza kwenye show ya Fiesta jijini Dar es Salaam kwakuwa msanii huyo alikuwa ameshaingia mkataba wa show nyingine na kituo cha redio cha Times FM kilichokuwa kimepanga kuwa na tamasha November 1. Hata hivyo huenda Clouds FM walimpa ofa kubwa zaidi msanii huyo kiasi cha

Kambi ya Diamond yazungumzia tukio la kuzomewa kwenye Fiesta

$
0
0
Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amesema haoni kama wameathirika na kundi la watu waliomzomea msanii huyo wakati akitumbuiza Jumamosi hii kwenye show ya Serengeti Fiesta, Leaders Club jijini Dar es Salaam. Tale amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa walikuwa na taarifa kuhusu mpango huo hata kabla ya show na hivyo walijiandaa. “Tulikuwa tumemjenga kisaikolojia, kwahiyo

Katiba yakoleza kasi urais CCM

$
0
0
Siku chache baada ya Bunge Maalumu kupitisha Katiba Inayopendekezwa, mchuano wa urais ndani ya CCM umeshika kasi baada ya makada wanaowania nafasi hiyo kujihakikishia uzito wa madaraka wanayoyatafuta.    Mjadala wa Katiba ulikuwa umewaweka njiapanda makada hao, baadhi wakiwa wameshajitangaza na wengine wakijipanga chinichini, huku wakijiuliza wawanie urais upi; wa Muungano, Tanganyika

Aliyedaiwa kufa kwa Ebola huko Sengerema mkoani Mwanza azikwa

$
0
0
Mwili wa Salome Richard (17) aliyefariki dunia katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza akidaiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa ebola ulizikwa juzi katika makaburi ya misheni mjini hapa chini ya uangalizi maalumu.    Mgonjwa huyo alifariki dunia Ijumaa saa 2 usiku baada ya kufika hospitalini hapo akiwa na homa kali. Vile vile madaktari waliokuwa wanatoa huduma kwa

Maaskofu Katoliki wawagomea mashoga

$
0
0
MAASKOFU wa Kanisa la Katoliki juzi waligoma kupitisha mabadiliko makubwa ya kihistoria kuhusu msimamo wao mkali dhidi ya masuala ya ushoga, utoaji mimba na wanandoa waliotalikiana.   Uamuzi huo,ulifichua uwapo wa pengo kubwa ndani ya kanisa hilo mwishoni wa mkutano huo wa wiki mbili.   Maaskofu wa kanisa hilo walikuwa wamekutana kujadili jinsi mafunzo ya kanisa hilo yanavyoweza

Mama na Watoto wake Wawili wachinjwa kinyama mkoani Tabora

$
0
0
WIMBI la mauaji ya kutisha limeendelea kutikisa nchini, baada ya watu wasiojulikana kuwaua mama na watoto wake wawili kwa kuwakatakata kwa mapanga usiku wa kuamkia juzi.   Tukio hilo la kusikitisha lilitokea katika Kijiji cha Nata wilayani Nzega mkoani Tabora.   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda, jana aliwataja waliouawa kuwa ni mama Leticia Thomas, Marietha Nicolaus

Y-P wa TMK Wanaume Family afariki dunia....kuagwa TCC Chang’ombe na kuzikwa kesho (Oct 22) katika makaburi ya Chang’ombe

$
0
0
Msanii wa kundi la Wanaume Family YP aliyefariki usiku wa kuamkia leo kwa ugonjwa wa kifua, anatarajiwa kuagwa kesho (October 22) kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe na baada ya hapo atazikwa katika makaburi ya Chang’ombe karibu na maduka mawili. Akizungumza na mtandao huu jioni hii, kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Family amesema mpaka sasa wapo kwenye maandalizi ya mazishi

Oscar Pistorius ahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela

$
0
0
Oscar Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp, baada ya timu yake ya utetezi kushindwa kumshawishi jaji Thokozile Masipa kumpa kifungo cha nje. Pia alihukumiwa miaka mitatu, iliyojumuishwa kwenye hukumu ya miaka mitano baada ya kushoot pistol kwenye mgahawa huko Johannesburg, January 2013. Hukumu hiyo inaanza mara moja.   Mwezi

Tamko la JWTZ kuhusu katazo kwa wananchi kuvaa sare la jeshi linakanganya

$
0
0
Jumatatu ya wiki hii Jeshi la Wananchi Tanzania, JWTZ, lilitoa tamko kuhusu wananchi kumiliki au kuvaa sare za jeshi hilo. Japo tamko hilo la JWTZ limetoka kwa ufupi bila kuweka wazi kwanini wameamua kulitoa tena wiki hii, ni wazi kuwa limetokana na wasanii kadhaa wakiwemo Diamond na dancers wake, Chege na Nay wa Mitego kuvaa sare hizo kwenye show ya Serengeti Fiesta iliyofanyika kwenye

Sitti Mtemvu akanusha kuwa na mtoto, asema ana miaka 23, hatovuliwa taji

$
0
0
Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amevilaumu vyombo vya habari kwa kueneza habari za uongo kuhusiana umri na maisha yake binafsi. Mtemvu amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. “Ukweli ni kwamba nina miaka 23 na cheti hicho hapo kinajielezea, mkitaka mnaweza kwenda hizo sehemu wanazotoa vyeti mkawauliza,” alisema Sitti. Mtemvu alisema cheti

Umesikia kuhusiana na chanjo ya Ebola? Habari yote iko hapa

$
0
0
Shirika la afya duniani, WHO limearifu kuwa liko mbioni kufanya majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola, ambao umeripotiwa kuua takribani watu 4,500 huku nchi za Afrika Magharibi zikiripotiwa kuathirika zaidi tangu kulipuka kwa ugonjwa huo.    Taarifa iliyoripotiwa na CNN imesema kuwa shirika hilo limepanga kuanza utekelezaji wa jaribio hilo mapema Januari mwaka 2015 katika

Baada ya T.I kupiga show ya nguvu Serengeti Fiesta na Kurudi Marekani, waandishi wa huko walimvaa na kumhoji kuhusu uwepo wa Ebola Tanzania

$
0
0
Msanii  mkubwa  wa  Marekani, T.I alikua mgeni kwenye stage ya Tamasha la Fiesta lililofanyika Leaders club October 18 2014 akiwa na timu yake ya watu wasiopungua watano na kuisimamia hiyo show kwa zaidi ya dakika 60.    Baada ya show Jumamosi, T.I aliondoka Tanzania Jumapili kurudi kwao Marekani kwa ajili ya kuhakikisha promo inakwenda vizuri sababu album yake mpya ilikua inatoka

Wanafunzi Waliwa Miguu na Mamba Wakioga Mtoni

$
0
0
Wanafunzi  wawili wa shule za msingi za Nyabisara (Murito) na Kerende Kata ya Kemambo wilayani Tarime, Mara wameumwa hadi kuondolewa nyama zao za miguu na mamba walipokwenda kuoga maji ya mto kwa nyakati tofauti. Wanafunzi hao ni Penina Joseph Mangure  (11) wa darasa la nne Shule ya Msingi Nyabisara katika Kijiji cha Murito ambaye ni mtoto wa mwenyekiti wa kijiji hicho, Joseph

Bibi Harusi Atoroshwa siku chache kabla ya Ndoa kufungwa

$
0
0
Mkazi wa Buguruni, Rukia Nassor amekimbilia Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar kutoa taarifa ya bintiye Saida Said (18) (pichani)kutoroshwa nyumbani kwake siku chache kabla ya ndoa.Alipofika kituoni hapo, mwanamke huyo alimtaja mtu mmoja kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye aliyefanya kitendo hicho.   Mmoja wa ndugu ambaye hakupenda jina lake liandikwe alisema mama huyo amekuwa

Majonzi Yatawala katika Msiba wa Mwananchi aliyeuawa na Askari wa JWTZ.....Chanzo cha kuuawa ni Marehemu kudaiwa kumsumbua mke wa mwanajeshi

$
0
0
Baadhi ya ndugu waliokuwa wakiuaga mwili wa Aron Kihundwa (28) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar walijikuta wakidondoka na kuzimia kufuatia uchungu wa kumpoteza mpendwa wao huyo aliyedaiwa kuuawa na Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Octavian Mgowele. Tukio hilo lilijiri wiki iliyopita na kumfanya Mchungaji  Elaina Msuya wa Kanisa la KKKT aliyekuwa akiongoza misa ya

LHRC inafikiria uwezekano wa kupinga kura ya maoni ya katiba mpya

$
0
0
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania – LHRC, pamoja na wadau mbalimbali wa mchakato wa katiba, wanajadili uwezekano wa kuchukua hatua za kisheria kuzuia zoezi la kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo imepangwa kufanyika mwakani. Akizungumza katika mahojiano na East Afrika Radio ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Dkt.

Nicki Minaj na boyfriend wake wamwagana? Boyfriend wake aifuta tattoo ya Nicki

$
0
0
Wanasema dalili ya mvua ni mawingu, hivi ndivyo inavyoonekana katika uhusiano wa Nicki Minaj na mpenzi wake Safaree Sam ambaye alikuwa amejichora tattoo yenye picha ya Nicki na jina lake pia.   Wiki hii, Safaree ameonekana akiwa kifua wazi huku akiwa ameifunika tattoo ya picha ya Nicki na jina lake kwa michoro mingine. Tattoo nyingine aliyokuwa ameichora mkononi mwake inaonekana pia

Video: Ampiga mawe binti yake hadi kufa kwa kosa la kufanya mapenzi kabla ya ndoa

$
0
0
Mfuasi mmoja wa kundi la ISIS la Syria ameungana na wanajeshi kadhaa wa kundi hilo kufanya mauaji ya kinyama kwa kumpiga mawe binti yake wa kumzaa hadi kufa baada ya kugundulika kuwa alizini.   Kundi la ISIS limeachia video inayoonesha tukio hilo la kusikitisha linaloelezwa kufanyika katika jiji la Hama nchini Syria.   Katika video hiyo iliyoripotiwa pia na mtandao wa Mirror wa

Walimu 422 Wafukuzwa Kazi kwa Makosa Mbalimbali

$
0
0
Jumla ya walimu 422 wamefutwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwemo kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi kwa kipindi cha mwaka 2013/2014.   Kiwango cha walimu wanaokwenda kinyume na maadili na kufutwa kazi kimeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka, ambapo katika kipindi cha mwaka 2013/2014 walimu 422 wamefutwa  katika maeneo mbalimbali nchini, wakiwemo watatu kwa kubainika

Diamond angemuoa Wema kabla ya Ramadhan, aeleza sababu ya kuahirisha.....Amsamehe baba yake kwa aliyomtendea akiwa mdogo

$
0
0
Kama mambo yangeenda yalivyokuwa yamepangwa, baada ya Ramadhan, Wema Sepetu angekuwa akiitwa Wema Naseeb! Lakini kutokana na sababu mbalimbali Diamond Platnumz alisogeza mbele mipango ya kufunga ndoa na mpenzi wake huyo. “Kabla ya Ramadhan ilikuwa tufunge ndoa kabisa, lakini mambo yakaingiliana,” Diamond alikiambia kipindi cha The Sporah Show.    “Mtoto naye ni majaliwa sio kama
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images