Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mwanaume afunga ndoa na mama yake wa kambo

0
0
Mwanamke nchini Ufaransa, juzi amefunga ndoa na mwanae wa kambo baada ya kusuguana na mamlaka za nchini humo kuhusu haki yake ya kuolewa. Elisabeth Lorentz, 48, amefunga ndoa na Eric Holder, kanisani kwenye kijiji kidogo Dabo huko Alsace-Lorraine, kaskazini mashariki mwa Ufaransa. Ms Lorentz alikutana na baba yake na Holder mwaka 1989, wakati huo akiwa na miaka 24.   Wawili hao

Jokate awaomba mashabiki wamvumilie kwa kuchelewa kutoa video yake, atoa sababu zilizoichelewesha

0
0
Jokate Mwegelo ambaye hivi karibuni alishoot video ya wimbo wake wa kwanza kama msanii wa muziki nchini, ametoa sababu za kwanini mpaka sasa video wala wimbo huo havijafanikiwa kutoka. Jokate a.k.a Kidoti amesema  kuwa video aliyoshoot Kenya imechelewa kwasababu kuna vitu ambavyo hakuvipenda katika video, hivyo vimechukua muda kurekebishwa ili kupata kitu bora zaidi.   “Kuna delay

Noorah, asimulia tatizo alilokuwa nalo ambalo madaktari walishangaa iweje awe hai!

0
0
Rapper Noorah aka Babastylez amesema kama isingekuwa neema za Mungu, leo hii asingekuwepo duniani. Akiongea kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV hivi karibuni, Noorah alidai alikuwa na tatizo la kujikunja kwa utumbo lililodumu kwa miaka 20. Amesema wakati tumbo likimuuma alikuwa akidhani ni vidonda vya tumbo.   “Doctor amekuja kunifanyia operesheni, baada ya operesheni akamuita

Polisi waeleza kwanini walimkamata Redsan kwa kumhisi ‘gaidi’

0
0
Maofisa wa polisi nchini Kenya wameeleza kwanini waliamua kumkamata muimbaji wa dancehall wa Kenya, Mohamed Swabir aka Redsan weekend iliyopita.    Polisi wamesema msanii huyo pamoja na washkaji zake akiwemo producer wake, Sappy ambaye ni Mtanzania, waliwasili kwenye viwanja vya ‘Nairobi International Trade Fair’ siku ya Ijumaa tayari kwa show lakini waligoma kukaguliwa.   Hiyo ni baada

Jokate arejea kwenye Top 10 Most ya Channel O, Ice Prince ni host mwenza

0
0
Jokate Mwegelo anarejea tena kwenye kipindi cha Top Ten Most cha Channel O. Awamu hii mtangazaji mwenza ni rapper Ice Prince Zamani wa Nigeria. Kipindi hicho kitaonekana Jumatano hii saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Kupitia website yao, Channel O wameandika: This month, rap superstar Ice Prince joins Channel O VJ Jojo as host on the brand new season of their hit show ‘Top

Diamond ambwaga Davido kwenye tuzo za IRAWMA.....Anyakua tuzo ya Best African Entertainer

0
0
Diamond Platnumz amewabwaga Davido, Awilo Longomba, Willy Paul Msafi (Kenya) na Eddy Kenzo wa Uganda na kushinda kipengele cha ‘mtumbuizaji bora wa Afrika – Best African Entertainer kwenye tuzo za IRAWMA (International Reggae and World Music Awards). “It always seems impossible until it’s Done!…ningependa kuwataarifu Wadau wangu kwamba #MdogoMdodo ndio nyimbo bora yenye Mahadhi ya

ARUSHA: Kijana Achapwa Viboko 120 na wazee wa Mila kwa kosa la kutofua Nguo zake na kuwa mchafu kupitiliza

0
0
SHERIA iliyopitishwa na wakazi wa Arumeru mkoani Arusha ya kuwachapa viboko 70 hadi 120 wasichana wanaovaa nusu uchi na wavulana wanaovaa mlegezo, kuvuta bangi, wizi, matusi na ulevi nyakati za kazi imeanza kufanya kazi baada ya kijana Zakayo Leonard (26) kuchapwa viboko 120 kwa makosa mbalimbali likiwemo uchafu wa kutofua nguo zake. Kijana huyo mkazi wa Ilboru, alihukumiwa adhabu

RUKWA: Wanawake wajiremba kwa Kutumia kondom

0
0
MATUMIZI ya kondomu za kike yamekuwa changamoto kubwa baada ya wanawake mkoani Rukwa kukataa kuzitumia, huku wengine wakibadili matumizi yake kwa kuzivaa kama urembo wa bangili.   Hayo yalibainika hivi karibuni wakati wa ziara ya siku nne ya timu za maofisa wa asasi mbili zisizo za kiserikali za Health Actions Promotion Association (HAPA ) ya Mkoa wa Singida na Resource Oriented

Serikali Yaiagiza Tanesco kuunganisha umeme siku moja kwa mteje atakayelipa Kabla ya Saa nne Asubuhi.....Meneja asiyeweza aachie ngazi

0
0
SERIKALI imelitaka Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kuunganishia wateja umeme ndani ya siku kama watalipa kabla ya saa nne asubuhi.    Agizo hilo lilitolewa jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga wakati akizungumza na menejimenti ya Tanesco mkoa wa Mwanza katika ziara yake ya kukagua miradi ya umeme.   “Baada ya Februari mwakani, mtu akija akalipia huduma ya

KISUTU: Lundenga apinga kuzuiwa kuandaa mashindano ya Miss Tanzania

0
0
MWANDAAJI wa mashindano ya urembo Tanzania, Miss Tanzania, Hashim Ludenga amewasilisha pingamizi la awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akipinga kuzuiwa kuendelea kuendesha mashindano hayo yanayotarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 11, mwaka huu.    Lundenga kupitia kwa Wakili Audax Kahendaguza, aliwasilisha pingamizi hilo dhidi ya ombi la kuzuiwa kuendelea

MOSHI: Mwalimu afumwa gesti na mwanafunzi wake wa Kike Wakifanya Mapenzi

0
0
MWALIMU wa Shule ya Sekondari ya Muungano iliyopo mji mdogo wa Himo wilayani Moshi, Richard Ndoile (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, kwa tuhuma za kukutwa gesti na mwanafunzi wake wakifanya mapenzi.   Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita alisema jana ofisini kwake, kuwa tukio la kukamatwa kwa mwalimu huyo lilitokea Oktoba 4, saa 5.00 asubuhi,

Rais Kikwete amteua Biswalo mganga kuwa Mkurugenzi mpya wa mashtaka (DPP)

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.   Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, jana, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter Ilomo inasema kuwa uteuzi huo umeanza Ijumaa iliyopita, Oktoba 3, mwaka huu, 2014.   Kabla ya uteuzi wake,

Waliomlawiti Mwanaume mwenzao na kisha kumfotoa picha za Uchi baada ya kumfumania na mke wa mtu Wapandishwa Kizimbani

0
0
WASHITAKIWA wanaokabiliwa na mashitaka ya kulawiti na kutuma picha katika mitandao ya kijamii, wamepandishwa kizimbani kusomewa maelezo ya awali ambapo walidaiwa kumlawiti mwanaume mwenzao na kumpiga picha kwa madai ya kutaka kulipwa Sh milioni moja.   Washitakiwa hao ni Erick Kasira (39) na Juma Richard (31) ambao wanadaiwa kulawiti sanjari na kupiga picha za tukio hilo.   Wakili wa

Vituko Vya Big Brother Vimeanza: Video ya Mshiriki wa Nigeria na Namibia "Wakichezeana Makalio" Yavuja

0
0
Ikiwa  ni  siku  moja  tu  Imepita  tangu  shindano  la  Big Brother Africa  lianze, tayari  Video   za  washiriki  wakifanya  mambo  ya  kikubwa  na  vituko  vingine  zimeanza  kuvuja.   Lilian  ambaye  ni  mshiriki toka  Nigeria  na  Luis  ambaye  anaiwakilisha  Namibia  wamenaswa  Live  na  kamera  za  jumba  hilo  wakichezeana  Makalio.....   Unataka  kuiona  Video?  Ingia  >

Heri ya Kuzaliwa Rais Wetu Jakaya Mrisho Kikwete

0
0
Leo ni siku ya kuzaliwa kwa Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alizaliwa tarehe 7 Oktoba, 1950 kijiji cha Msoga kilichopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani . Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Msoga kati ya mwaka 1958 na 1961.   Baada ya hapo alihamia shule ya kati(middle school) Lugoba kati ya mwaka 1962 mpaka

Serikali Yaondoa Zuio la Mikutano ya Vyama vya Siasa Lindi na Mtwara

0
0
Serikali imeondoa zuio la mikutano ya Vyama vya Siasa lililokuwa limetangazwa mwezi Mei mwaka juzi kuzuia mikutano hiyo kufanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Zuio hilo limeondolewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe.   Mikutano hiyo ilizuiliwa kutokana na vurugu za wananchi waliokuwa wakipinga ujenzi wa mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara

Maandalizi ya kukabidhi Katiba Mjini Dodoma yakamilika

0
0
Mkoa wa Dodoma umeendelea kufanya maandalizi makubwa kwa ajili ya hafla ya kukabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete Wakati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akitarajiwa kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalum kesho mjini Dodoma, maandalizi kabambe kwa ajili ya hafla hiyo yamefanyika mjini humo huku idadi kubwa ya

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman AFUTWA Kazi

0
0
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, leo amemfuta kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman na nafasi yake kuchukuliwa na Said Hassan Said.   Rais Shein amefanya uteuzi huo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar

Mbunge wa Kawe Halima Mdee Apelekwa Segerea baada ya Kushindwa Kutimiza Masharti ya Dhamana Mahakamani

0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama cha Demokrasia na Maendeleo BAWACHA ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar es salaam Mhe. Halima Mdee leo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu. Mdee amefikishwa katika mahakama hiyo pamoja na wanachama wengine wanane wa chama hicho na kusomewa mashtaka mawili ya kukusanyika kinyume cha sheria pamoja na

Matusi ya Mama Wema: Kajala na Wema Sepetu Watoana Jasho Polisi

0
0
Kufuatia matusi ya mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu kwenda kwa mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, mastaa hao wamejikuta wakitoana jasho kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama almaarufu Mabatini jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita. Duru za ‘kiubuyu’ zilidai kwamba Kajala, baada ya kuchoshwa na matusi hayo ambayo yalianzia kwenye sherehe ya kuzaliwa
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images