Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kwenye rekodi za Mwaka huu na hii ya huyu Mungu anaeonekana Kenya imo.

0
0
Kituo cha TV cha K24 kiliripoti juu ya uwepo wa Mungu nchini Kenya ambae ibada zinafanyika nyumbani huku yeye mwenyewe akisema "Mimi ni Mungu, nimekuja kuvunja mambo yote yaliyoandikwa" Zaidi mtazame hapa chini…

Sababu za kufukuzwa kazi Rais wa shirikisho la muziki Tanzania.

0
0
Hii ni moja ya habari kubwa za Magazeti ya leo Tanzania ambapo gazeti la Uhuru limeandika kwamba Rais wa shirikisho la muziki Tanzania Addo Novemba amefutwa kazi baada ya kuhusika na upotevu wa pesa za rambirambi ya Mwanamuziki.    Zilikua ni pesa zilizotolewa kama rambirambi kwenye msiba wa Mwanamuziki wa siku nyingi Tanzania mzee Gurumo ambazo zilikua ni milioni 1.1. Fedha hizo zilikua

Hii ni kwa wale Wanafunzi waliotaka kujiunga na Vyuo Vikuu Tanzania.... Wanafunzi Elfu 12 wamekosa nafasi, Wafanye nini sasa??...BOFYA HAPA

0
0
Kwa ufupi  tu  ni kwamba Tume ya vyuo vikuu TCU  imetangaza kwamba Wanafunzi wapatao elfu 12 wanaotaka kujiunga na elimu ya vyuo vikuu Tanzania wamekosa nafasi za kujiunga na vyuo hivyo kwa sababu ya walichagua sehemu zenye ushindani mkubwa na wamekosa nafasi sababu alama zao zilikua ndogo.  TCU  wametoa  maelekezo  mengi  na  wanasema  nafasi  bado  zipo  tena  ni  nyingi  tu  kuliko

Kesi ya Trafiki FEKI Yaendelea kupigwa kalenda

0
0
Kesi ya aliyejifanya askari polisi wa usalama barabarani, James Hassan (45) imeendelea kupigwa kalenda kutokana na mshitakiwa kutofika mahakamani hapo licha ya kuwepo kwa mashahidi wawili.   Kesi hiyo iliyofikia hatua ya kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imekuwa ikipigwa kalenda mara kwa mara kutokana na mshitakiwa huyo kudai kwamba anaumwa hivyo kukwamisha kesi hiyo

Habari Njema: Mtanzania (Kay Madati) ateuliwa kuwa makamu mkuu wa rais na pia kama Chief Digital Officer wa BET Networks huko Marekani

0
0
Mtanzania Kay Madati amechaguliwa kuwa makamu wa Rais na pia kama Chief Digital Officer katika kituo kikubwa cha Television nchini Marekani BET. Taarifa iliyoandikwa na Mtandao maarufu wa Forbes imesema amechaguliwa ‘.....Kay Madati as Executive Vice President and Chief Digital Officer. Madati, a Tanzanian citizen who has lived in Africa, the United Kingdom, and the United States’ CV

Wabunge Wapendekeza Wala Rushwa Wanyongwe

0
0
 Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wamesema wala rushwa pamoja na wahujumu uchumi adhabu yao iwe ni kunyongwa.   Wametaka  Katiba mpya inayoenda kuandikwa itamke hivyo ili kufanya viongozi wa kisiasa kuogopa kama ilivyo kwenye nchi nyingine.   Sababu ya wajumbe hao kupendekeza jambo hilo ni kwamba uhujumu uchumi na rushwa nchini limekuwa tatizo kubwa  kwa viongozi.  

Oscar Pistorius apona , jaji asema hana hatia katika kesi ya kuua kwa kukusudia

0
0
Hatimaye Jaji Thokozile Masipa ametoa maamuzi juu ya kesi iliyokuwa inamkabili mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius na kutupilia mbali madai kuwa aliua kwa kukusudia. Baada ya muda mrefu na mgumu wa muenendo wa kesi hiyo, jaji huyo ameamuru kuwa Pistorious hana hatia katika mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabili.   Jaji Masipa ameeleza kuwa upande wa mashitaka umeshindwa

Cheyo Awazima UKAWA Bungeni.....Asema Rais Kikwete hawezi kuahirisha bunge la katiba, Adai si makabaliano waliyofikia katika kikao

0
0
MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), Bw. John Cheyo, amesema mchakato wa kupata Katiba Mpya, utamalizwa kwa kura za maoni ya wananchi hivyo Rais Jakaya Kikwete, hawezi kutoa tamko la kuahirisha Bunge hilo kwa kuwa vikao hivyo vinafanyika kisheria.   Alisema kitakachoahirishwa ni mchakato wa kura za maoni ya wananchi si Bunge hilo

Ukaguzi leseni na vyeti vya madereva waanza

0
0
JESHI la Polisi jana limeanza kufanya ukaguzi wa leseni na vyeti vya madereva kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani na nchi jirani Ubungo (UBT), jijini Dar es Salaam kufuatia ajali za barabarani nchini kuongezeka.   Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, alisema kuwa ukaguzi huo una lengo la kuchunguza madereva ambao wanafanya

Serengeti Fiesta kufanyika leo Shinyanga

0
0
Baada ya kufanya maonyesho ya kuvutia katika zaidi ya mikoa sita nchini, Serengeti Fiesta inaendelea Ijumaa hii mjini Shinyanga. Onyesho la Serengeti Fiesta mjini humo lilipaswa kufanyika Septemba 6 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kambarage, lakini likaahirishwa kutokana na ajali mbaya iliyotokea mkoani Mara ikihusisha magari matatu.   Wakazi wengi wa Shinyanga wamefurahia na kuipongeza

Mkanda wa ngono wa Iggy Azalea kuuzwa kwa kampuni ya Vivid Entertainment

0
0
Kuna mkanda wa ngono wa rapper Iggy Azalea na mpenzi wake wa zamani unauzwa kwa kampuni maarufu ya video za mambo hayo. Wanasheria wa Iggy Azalea wamedai kuwa ni kweli msichana anayeonekana kwenye video hiyo ni Iggy lakini huenda alikuwa na miaka chini ya 18 wakati akishoot tape hiyo. Mkanda huo unauzwa kwa kampuni ya video za ngono, Vivd Entertainment.    Wanasheria wa rapper huyo

Oscar Pistorius apatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake bila kukusudia

0
0
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp bila kukusudia. Akitoa uamuzi wake jaji Thokozile Masipaal alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango wake wa choo akiwa katika hali ya mshtuko akidhani kuwa jambazi aliyekuwa amevamia nyumba yake.   Alisema kuwa upande

Queen Darleen akanusha kumtafutia mademu Diamond

0
0
Queen Darleen amekanusha tuhuma kuwa ana mtindo wa kumtafutia mademu kaka yake Diamond Platnumz. Queen amesema kwa heshima aliyonayo kwake, sio rahisi kumpa kazi hiyo.   “Unajua Naseeb miye ananiheshimu sana hata akiwa na wenzake kama alikuwa anaongea ujinga nikiwepo haongei kwakuwa anajua miye ni mkubwa wake,” Amesema Queen   “Na pia naweza kukaa hata miezi mitatu hatujaonana

Tatizo ni Anaconda? Mkuu wa shule aliyosoma Nicki Minaj amkatalia kuongea na wanafunzi wake

0
0
Nicki Minaj amekutana na kikwazo kikubwa katika mpango wake wa kuzungumza na wanafunzi wa shule aliyosoma.   Mwimbaji huyo ameeleza jinsi alivyoumia baada ya mkuu wa shule hiyo kulikataa ombi lake la kuongea na wanafunzi hao kwa nia ya kuwa-inspire wafanikiwe kama yeye.   Huenda mkuu huyo wa chuo ameona Nicki Minaj sio mtu sahihi wa kuwa-inspire wanafunzi wake kwa kuzingatia video

Msikiti mkubwa wa Mtambani Kinondoni Waungua Tena

0
0
Msikiti  wa  Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es Saam uliungua kwa mara ya pili leo.  Msikiti huo  uliungua  kwa  mara  ya  kwanza  mnamo Agosti 13, 2014 katika ghorofa yake ya juu na kuteketeza  eneo kubwa ambalo hadi sasa bado halijanza kufanyiwa  ukarabati. Leo hii moto  huo inasemekana ulianza majira ya saa sita na nusu mchana   katika moja ya chumba ambacho wanafunzi wa kidato cha

Dereva atakaye kamatwa akiendesha gari huku akiongea na simu Atafutiwa Leseni yake

0
0
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri wa Nchi kavu na Majini SUMATRA limeanzisha mkakati wa kuwafungia leseni madereva watakaobanika kuendesha magari huku wakiwa manazungumza na simu za mkononi.   zoezi hilo limekuja kufuatia kile kinachodaiwa kuwepo kwa ongezeko la ajali za barabarani ambazo zinasababishwa na uzembe ambao unasababishwa na

Steve Nyerere ajiuzulu Urais Bongo Movies

0
0
Muigizaji wa filamu za Kiswahili, Steve Nyerere aliyekuwa Rais wa Klabu ya Bongo Movie Unity ameamua kujiuzulu nafasi hiyo.   Steve ameeleza uamuzi wake kupitia Instagram bila kutoa sababu zilizopelekea kujiuzulu kwake. “Napenda kuwashkulu ndugu zangu wote wasaniii wenzangu kaka zangu mama zangu rafiki zangu mimi pamoja na family yangu nimeamua kujiuzuru uongozi wa bongo move nabaki kuwa

Wolper Atumika kwenye Utapeli wa Mamilioni

0
0
Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Jack Wolper’ amejikuta akitumika kwenye utapeli wa mamilioni ya shilingi kupitia mitandao ya kijamii bila yeye kujua.   Akizungumzia sakata zima huku alibubujikwa na machozi, Wolper alisema:    “Siku moja nilikutana na dereva teksi mmoja aitwaye Ismail, baada ya kupiga stori nilimpa namba yangu ya simu na yeye akanipa yake, tukaagana.

Familia ya Reeva imesemaje baada ya maamuzi ya Jaji kwenye kesi ya mauaji ya Oscar Pistorius ?

0
0
September 12 2014 Mahakama ya Pretoria nchini Afrika Kusini ilimpata Oscar Pistorius na hatia ya kumuua mpenzi wake bila kukusudia kwenye siku ya Wapendanao February 14 2013.    Baada ya maamuzi hayo kutangazwa, familia ya binti aliyeuwawa Reeva Steenkamp imekasirishwa na uamuzi wa jaji wa kesi hiyo kwani mtoto wao alikufa kifo kibaya na ndio maana hawajaamini kilichotokea kwamba Jaji

Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 Lafunika Shinyanga.....Leo kusambaza upendo kwa wakazi wa Geita

0
0
  Pichani kati ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Rachael akiwa na madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa namna ya kipekee  kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga. Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akiwaimbisha mashabiki huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na wakazi wa
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images