Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,pichani wa tatu shoto Ruge
Mutahaba akiwa sambamba na baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajiwa
kutumbuiza leo usiku mjini Musoma kwenye tamasha la Fiesta,lakini hata
hivyo Uongozi wa Clouds Media Group,Prime Time Promotions ambao ndio
waandaaji pamoja na Wadhamini wa tamasha hilo kwa pamoja wamekubaliana
kuaihirisha onyesho hilo
Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 Musoma Lasitishwa kufuatia Ajali Mbaya Iliyotokea Leo
↧
↧
Dr. Mwakyembe Aamuru kufungiwa kwa Mabasi Yaliyosababisha Ajali Musoma
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe ameagiza makampuni ya Mabasi ya J4 Express na Mwanza Coach yafungiwe mara moja.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao Dk
Mwakayembe amesema sehemu iliyotokea ajali na kusababisha vifo vya watu
39 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ni sehemu ambayo kila dereva
alikuwa akimuona mwenzake, hivyo ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu.
“Ile sehemu
↧
Majambazi Yavamia Kituo cha Polisi na Kuua Askari Wawili.....SMG 10, risasi na mabomu vyaporwa
Watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamevamia Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Bukombe kilichopo Ushirombo, mkoani Geita na kuua askari wawili na kuiba silaha za moto.
Taarifa za awali za tukio hilo zimethibitishwa na Kamishna wa Polisi, Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema uvamizi huo unatajwa kufanywa majira ya saa 9 usiku
↧
Ajali ya Mabasi Musoma Yamsikitisha Rais Kikwete
Rais Jakaya Kikwete ameelezea huzuni na masikitiko yake makubwa kufuatia vifo vya watu 39 vilivyotokea katika ajali ya barabarani wilayani Butiama, Mkoa wa Mara, ambako pia watu 79 wameumia, baadhi yao vibaya.
Mara baada ya kupata taarifa hiyo iliyotokea juzi asubuhi, Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Arusha, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa
↧
Tume ya Oparesheni Tokomeza Ujangili Yaanza Kazi kubaini Mateso waliyotendewa Wananchi Wakati wa oparesheni hiyo
Tume iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza vitendo vilivyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili nchini, imeanza rasmi kazi kwa kupokea taarifa na malalamiko mbalimbali kuhusu operesheni hiyo.
Aidha, katika kufanikisha majukumu yake, Tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji na Balozi mstaafu Hamisi Msumi, itatembelea maeneo mbalimbali nchini ili kukutana na
↧
↧
CHADEMA Waanza Mkutano mkuu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana kilianza mkutano mkuu wa chama hicho ambapo Baraza la Wazee wa chama hicho lilichagua viongozi wake.
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza hilo anayemaliza muda wake, Nyangaki Shilungushela aliwataka wazee kushikamana na kusaidia ujenzi wa taifa kwani wazee ni hazina ya busara.
Alisema kupitia mkutano huo ambao pia
↧
Bosi Aliyembaka Mfanyakazi wa Ndani ( Hausigeli) Afungwa Jela Miaka 30
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imemhukumu kwenda jela miaka 30 mlinzi wa Shule ya Sekondari ya Mbwawa Steven Solomon (29) kwa kosa la kumbaka mfanyakazi wake wa nyumbani mwenye umri wa miaka 16.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu wa mahakama hiyo, Harieth Mwailolo alisema iliridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa chini ya mwendesha mashitaka Salim Msemo
↧
Tamasha la Serengeti Fiesta kufanyika Leo Musoma
TAMASHA
la Serengeti fiesta lililokuwa lifanyike Ijumaa katika Uwanja wa
Karume mjini Musoma na kuahirishwa kutokana na ajali mbaya ya gari
iliyotokea mjini humo sasa linatarajiwa kufanyika Jumapili ya
leo jioni katika uwanja huo huo imeelezwa.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengetj ambao ndio wadhamini wakuu wa
tamasha hilo, Ephraim Mafuru alisema kampuni yao pamoja
↧
Msichana Anayedai Kubakwa na Emmanuel Mbasha Atoa Ushuhuda Mahakamani
Shahidi wa kwanza katika kesi ya ubakaji inayomkabili mume wa mwimbaji wa muziki wa injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32) ameieleza mahakama jinsi alivyobakwa akiwa kwenye gari na nyumbani kwao.
Shahidi huyo mwenye umri wa miaka 17 (jina limehifadhiwa) ambaye pia ni shemeji wa Mbasha, alidai mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago kuwa Mei 23 mwaka huu, Mbasha alimbaka kwa mara ya
↧
↧
Benki Kuu ya Tanzania Imetoa Toleo Jipya la Sarafu ya Sh. 500
BENKI Kuu ya Tanzania imetoa toleo jipya la sarafu ya shilingi 500
itakayoanza kutumika Oktoba 2014 itakayokuwa mbadala wa Noti ya shilingi
500 inayoonekana kuchakaa haraka.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za
kibenki wa benki hiyo Bw. Emmanuel Boaz wakati wa mkutano na waandishi
wa habari.
“Noti ya shilingi 500 hupita kwenye mikono ya watu wengi
↧
Mke Wa Mtu Atia AIBU baada ya kusaula nguo zote mbele ya Watoto wakati akicheza ngoma za Vigodoro
Wakati serikali ikipiga marufuku disko la mitaani maarufu kwa jina la
‘Vigodoro’ bado kuna baadhi ya mikoa inapuuza agizo hilo ambapo
mwanamke mmoja ambaye mumewe anafanya kazi kwenye mgahawa uliopo ofisi
za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Morogoro, aliyetajwa kwa jina la
Mama Abdul (pichani), amejitoa fahamu kupitia Kigodoro na kujikuta
akisaula nguo hadharani.
Tukio
hilo
↧
Mbowe awekewa pingamizi CHADEMA
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe, amewekewa pingamizi la kutogombea nafasi hiyo kwa awamu ya tatu
kwa madai ya kukiuka katiba ya chama hicho na maagizo ya Msajili wa
Vyama vya Siasa nchini.
Pingamizi hilo limewekwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tabora, Kansa Mbarouk, ambaye pia ni mgombea wa nafasi hiyo.
Barua ya Mbarouk yenye
↧
Urais CCM Wazidi Kupamba moto....Dkt. Kigwangalla naye Atangaza Nia 2015, Asema anauwezo mkubwa na amekulia familia Masikini
WIMBI la wanachama wa CCM kutangaza nia ya kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu 2015 baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake wa miaka 10 kikatiba, limezidi kushika kasi ambapo Mbunge wa Nzega, mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla, naye ametangaza dhamira hiyo.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Dkt. Kigwangalla aliambatana na wazazi wake, mkewe
↧
↧
Picha: Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 Lasambaza Upendo wa Kutosha kwa Wakazi wa Musoma
Wasaniii
walioshiriki tamasha la Fiesta 2014 wakiwa na mishumaa jukwaani
wakisambaza upendo na kuwafariji wale wote waliopotelewa na ndugu
zao,waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea hivi karibuni wilayani
Butiama mkoani Mara,ambapo watu zaidi ya 40 walipoteza maisha na wengine
kujeruhiwa vibaya.
Sehemu
ya umati wa wakazi wa mji wa musoma wakiwa ndani ya uwanja wa
Karume,wakati
↧
Pinda Afunguka Rasmi Urais 2015.....Ahofu WAPAMBE Wanaotegemea Fdhila
BAADA ya jina lake kutajwa kuwa miongoni mwa watu watakaowania urais,
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amesema zipo taratibu ndani ya chama chake
za kutangaza kuwania nafasi hiyo na kusema kinachoendelea hivi sasa ni
juhudi binafsi za watu.
Pinda alisema hayo jana nyumbani kwake jijini Dar es Salaam
alipokutana na wahariri wa Mtanzania, kuzungumzia masuala mbalimbali
yanayolikabili taifa.
↧
Msanii Wa Bongo Movie Aumbuka baada ya picha zake za Utupu kuvuja mitandaoni.....Amtupia Lawama Nay wa Mitego
Msanii wa Bongo Movies, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ aliyewahi kuripotiwa
kujiachia kimahaba na mwanamuziki Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’
ametia aibu kubwa baada ya picha zake za utupu kuzagaa mitandaoni.
Kutokana na picha hizo ambazo zimeonekana kuzagaa katika mitandao
mbalimbali na kuacha viulizo kwa wasanii wengi wanaomfahamu, mwandishi
wetu alimtafuta Bozi ambaye alionekana
↧
Jeshi la polisi mkoani Geita Lakamata Bunduki 7 Zilizoporwa kituo cha polisi Bukombe.....Jambazi mmoja akamatwa, msako mkali bado unaendelea
Jeshi la polisi mkoani Geita, limefanikiwa kulitia mbaroni jambazi moja
na kufanikisha kuzinasa bunduki sita ambazo ziliporwa na kundi la
majambazi usiku wa kumkia juzi katika kituo cha polisi wilayani Bukombe.
Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu, alisema
jambazi hilo lilinaswa porini likiwa na silaha hizo ambazo ziliporwa
baada ya kuvamia kituo hicho na kuua
↧
↧
Ukatili wa Kutisha: Familia Yateketezwa kwa Moto.....Watoto watatu wafa, mmoja hoi hospitali.... Baba na mama nao walazwa
WATOTO watatu wa familia moja, wakazi wa Nyankumbu, Wilaya ya Geita, mkoani Geita, wamefariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya nyumba yao kuteketezwa kwa moto uliowashwa kwa mafuta ya petroli na mtu asiyefahamika.
Dada mkubwa wa marehemu hao ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Sekondari Mwatulole na wazazi wao, walijeruhiwa vibaya katika tukio hilo ambalo chanzo chake ni ugomvi
↧
Breaking News: Ajali nyingine mbaya ya basi yaua watu zaidi ya 10 maeneo ya Gairo
Basi la kampuni ya Airbus lililokuwa likitoka Dar es Salaam leo
kuelekea Tabora limepinduka katika maeneo ya Kiegeya Gairo.
Haijulikani idadi kamili ya watu waliopoteza maisha lakini ni wengi na wengine wamejeruhiwa vibaya sana.
“Picha hazifai kuonwa na mimi niko eneo la tukio kwa ajili ya
uokozi..viongozi mbali mbali wa serikali tunao hapa..kwakweli ni majonzi
vilio nk,” amesema
↧
Rais Kikwete Akutana na Wajumbe wa kituo cha Demokrasi Tanzania ( TCD ) mjini Dodoma leo
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wajumbe wa Kituo cha Demokrasia
Tanzania (TCD) wakati alipokutana nao kwenye Ikulu ndogo mjini Dodoma
leo Septemba 08,2014.
↧