Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mgomo wa wafanyabiashara watikisa Kariakoo

$
0
0
WAFANYABIASHARA wa maduka ya soko la Kariakoo wameanza mgomo kwa muda usiojulikana kuanzia jana, sambamba na kuishinikiza Serikali kupunguza kodi ya asilimia 18 wanayotozwa kupitia mashine za kielektroniki (EFDs).   Wamefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja baada ya TRA kutangaza kufanya ukaguzi endelevu na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wale watakaokaidi kutumia mashine hizo.  

Ndege Yaanguka Serengeti...Watatu wahofiwa kupoteza maisha

$
0
0
UCHUNGUZI wa awali kuhusu kupotea kwa ndege ya mizigo ya Shirika la Safari Express ya nchini Kenya, umeonesha kuwa ndege hiyo yenye usajili namba 5Y SXP, aina ya Fokker 27, imepata ajali.   Taarifa ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), iliyotumwa jana jioni katika vyombo vya habari, imeonesha kuwa ndege hiyo iliyopoteza mawasiliano juzi usiku, imeonekana ikiwa imeanguka katika

Baba AMNYONGA Mtoto wake na kumzika mwenyewe kwenye kibanda chake.....Kisa cha kumnyonga eti ni kwa sababu Mtoto alitanguliza MAKALIO wakati wa kuzaliwa

$
0
0
Mtoto  mwenye umri  wa mwaka mmoja na miezi miwili , Regina Geofrey ameuawa kikatili kwa kunyongwa  na baba yake mzazi Geofrey Kilngwa ‘Simbaiwe” (27) kwa kuwa alizaliwa  akiwa ameatanguliza makalio yake . Baba wa  binti  huyo  ambaye pia  ni  mganga wa kienyeji  anayeishi kitongoji cha Mwikang’ombe, kijijicha cha Katuma  ,wilayani Mpanda alitenda unyama huo  kwa madai kuwa mtoto 

Tamko Zito la Jukwaaa la Wakristo Tanzania juu ya Mchakato wa Katiba

$
0
0
Sisi, wajumbe wa Jukwaa la Wakristo Tanzania, tuliokutana tarehe 27 hadi 28 Agosti, 2014, Dar es Salaam , tumepata fursa ya kutafakari, kujadili na kujielimisha kwa kina yaliyomo katika Rasimu ya pili ya Katiba na mjadala unaoendelea katika Bunge Maalumu la Katiba. Baada ya mjadala wa kina, tunatoa tamko letu kama ifuatavyo:   Tunaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilikusanya

Kibaka Achomwa Moto Mjini Kahama na Wananchi Wenye hasira kali.....Polisi Watumia Risasi za Moto kumnusuru kibaka mwingine

$
0
0
Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga Jana lililazimika kutumia risasi za moto baada ya wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuua watuhumiwa kisha kuwachoma moto.   Inasemekana watuhumiwa hao walivamia chumba ya mkazi mmoja wa mtaa wa Muhungula Kahama na kujeruhi kwa mapanga watoto wawili usiku wa kuamkia  jana.   Kwa mujibu wa  habari kutoka wilayani Kahama, juzi usiku

Picha za Uchi za Watu maarufu Zaanikwa mitandaoni .....FBI Waingia Mzigoni kunusuru jahazi

$
0
0
Idara ya upelelezi ya nchini marekani FBI imetoa tamko kuwa  inachunguza kwa ukaribu madai ya maelfu ya accounts za watu maarufu kutekwa,na kinachotafutwa hasa ni picha za utupu za watu hao maarufu ambazo zimekua zikianikwa mitandaoni bila ya muwekaji kujulikana. Katika tamko la FBI liliripotiwa na NBC News, wameeleza kuwa walikuwa wanafahamu kuhusu vitendo vya wezi wa njia za mtandao

Kampuni ya Ujerumani yaelezea kiini cha Vurugu kwenye show ya Diamond, yaahidi show ya bure kuwapoza mashabiki

$
0
0
Kampuni ya Britts Event iliyohusika kuandaa show ya Diamond Stuttgart, Ujerumani imeeleza kwa kina kiini cha vurugu kubwa zilizotokea kwenye show hiyo na kusababisha uharibifu mkubwa huku baadhi ya watu wakijeruhiwa vibaya.   Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Awin Williams Akpomiemie ameeleza kwa kina kuhusu mzozo uliokuwepo ndani ya kampuni hiyo ulioathiri show hiyo kwa ujumla.

Lady Jay Dee ateuliwa kuwa balozi wa kampeni ya uzazi wa Mpango

$
0
0
Hospitali ya Marie Stopes imemchagua Lady Jay Dee kuwa balozi wa kampeni ya kuhamasisha uzazi wa mpango na kupinga mimba za utotoni inayoitwa ‘Chagua Maisha’.   Akiongea na TBC, Lady Jay Dee amesema kuwa anaweza kufikisha ujumbe kwa jamii kwa kuimba nyimbo ambazo zitasaidia kuwahamasisha wananchi kuchagua jinsi ya kuishi kwa kutumia uzazi wa mpango.

Ofisa Usalama wa Taifa feki Atiwa Mbaroni

$
0
0
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata Ofisa Usalama wa Taifa feki ambaye amekuwa akijipatia fedha kutoka kwa wafanyabiashara kwa kuwahusisha na makosa yanayohatarisha usalama wa nchi.   Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam; Kamishna Suleiman Kova, alimtaja ofisa huyo feki kuwa ni Saimoni Meena

Ufisadi Nusura Umtoe CHOZI Waziri Chiza

$
0
0
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, nusura atokwe na machozi baada ya kukuta bwawa la umwagiliaji lililojengwa kwa zaidi ya sh. bilioni 3 limebomoka.   Hali hiyo ilimfanya awaweke kitimoto wahandisi wa Ofisi ya Umwagiliaji Kanda ya Mbeya.   Alisema ujenzi wa bwawa hilo ambalo lilikuwa linatarajiwa kutumiwa na wananchi zaidi 6,000 umejaa harufu ya ufisadi, hivyo

Samuel Sitta Ageuka Mbogo kwa Wanaombeza kwamba Hafai kuwa Rais wa Tz kwa kuwa Bunge la katiba Limemshinda....Ahamishia hasira kwa Kubenea

$
0
0
MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, amewashukia wanasiasa wanaomkejeli kwa kudai kuwa hafai kuwa rais na amesisitiza kwamba wenye maamuzi juu ya suala hilo ni wananchi na si vinginevyo.   Sitta alitoa kauli hiyo jana bungeni mjini Dodoma wakati akitoa taarifa juu ya utaratibu wa kupokea mawasilisho ya kazi zilizofanywa na Kamati za Bunge Maalum la Katiba.   Alisema wapo

Jumba la Big Brother Africa lateketea kwa moto, uzinduzi wa msimu mpya uliotarajiwa kufanyika Tarehe 7 Umeahirishwa

$
0
0
Moto mkubwa umezuka kwenye jumba la Big Brother Africa Hotshots katika studio za Sasani jijini Johannesburg, Afrika Kusini na hivyo kuahirishwa kwa kuanza msimu mpya uliokuwa uzinduliwe Jumapili hii, September 7. Hakuna aliyeumia kutokana na moto huo uliotokea kwenye studio hizo zilizopo Highlands North jijini Johannesburg jana Jumannne . Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. 

UTAFITI: Wanafunzi shule za msingi wakithiri kwa ngono

$
0
0
UTAFITI uliofanywa na mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia uwezekano wa vijana kupunguza ngono, umebainisha elimu ya afya ya uzazi bado inahitajika ili kuwakinga na tabia hatarishi.   Akitoa matokeo ya awali ya utafiti huo, mmoja wa watafiti wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili, kitengo cha magonjwa na afya ya akili, Lusajo Kajula, alisema kuwa asilimia

Rais Kikwete Ajadili Ugaidi Kenya

$
0
0
RAIS Jakaya Kikwete amewasili jijini Nairobi, nchini Kenya, juzi usiku kuhudhuria mkutano maalumu wa wakuu wa nchi zinazounda Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU), ambalo Tanzania ni mwanachama. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, mkutano huo wa siku moja uliofanyika jana, umejadili ugaidi na athari zake kwa nchi za Afrika. Mkutano

Babu Tale aeleza ujumbe waliotumiwa na Promota wa Ujerumani kuhusu Diamond na walichoamua baada ya Vurugu

$
0
0
Kufuatia tukio la vurugu kubwa zilizotokea wakati wa show ya Diamond Platinum huko Stuttgart, Ujerumani, promota wa kampuni ya Britts event ameutumia ujumbe uongozi wa Diamond. Akiongea na The Jump Off ya 100.5 Times Fm, Babu Tale ameeleza kuwa promota huyo amewatumia barua pepe kuwaomba radhi na wao wamemuelewa na kumsamehe.   “Promota ametupigia simu kuapologize ametuma na email,

Lukuvi azomewa mbele ya Rais Kikwete

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi amejikuta katika wakati mgumu mbele ya Rais Jakaya Kikwete baada ya kuzomewa hadi kukatisha hotuba yake akipingwa na wananchi pamoja na madiwani wa CCM wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma alipokuwa akitetea kuwapo kwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA).    Lukuvi alikumbana na mkasa huo wakati akijibu

Lady Jaydee Adai Maadu zake Wamebadilisha Wimbo.....Walianza kusema Jay Dee ni Mgumba, Wakasema Jide ni Tasa.....Sasa Wamekuja na jipya tena

$
0
0
Malkia wa muziki wa R&B, Lady Jay Dee amedai kuwa maadui zake wamebuni njia mpya ya kumwangusha, baada ya zile za awali kutofanikiwa.    Katika waraka mrefu aliouandika katika mtandao wa facebook, Lady Jay Dee alisema watu wasiopenda mafanikio yake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kumwangusha, lakini hata hivyo wameshindwa.   Jay Dee analalamikia habari iliyoandikwa juu yake kuwa

VIDEO Inatisha: Kundi la ISIS lamkata kichwa Mwandishi Mwingine wa Marekani, latishia kumkata mwingine raia wa Uingereza kulipa kisasi ( Video Inatisha)

$
0
0
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Iraq na Syria (ISIS) limetekeleza mauji mengine ya kutisha kwa kumkata kichwa mwandishi  mwingine wa habari wa Marekani.     Mwandishi huyo aliyetajwa kwa jina la Steven Sotloff mwenye  umri  wa  miaka 31 alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwaka jana.Mwezi uliopita Sotloff alionekana mwishoni katika picha za video zilizoonyeshwa kuhusiana na

Nyani awagawia watu pesa India...Kazitoa Wapi??

$
0
0
Nyani mmoja katika jimbo la Himachal Pradesh Kaskazini ya India, amewagawia watu pesa taslimu kutoka mtini.   Taarifa zinasema kuwa watu waliokuwa wanajivinjari katika mji wa Shimla jimboni humo, walianza kukimbia huku na kule wakiokota pesa zilizokuwa zinarushwa na Nyani huyo kutoka juu ya mti kwa karibu saa moja. Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa Nyani huyo kwa jina Simian

Gari la Rais lililoibwa Kenya lapatikana Uganda

$
0
0
Jumatano ya wiki iliyopita ndio liliibwa hili gari aina ya BMW lisilopenya risasi ambalo huwa linakuwepo kwenye msafara wa Rais Kenyatta, na taarifa ya Ikulu ilisema liliibwa wakati dereva wake ambae ni askari alikua akielekea kwenye makazi ya Polisi Nairobi, njiani akasimamishwa na watu waliokuwa na AK 47 wakamtupa mtaroni baada ya kumvua nguo na kukimbia nalo. Taarifa mpya ambayo
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images