Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Freeman Mbowe apata ‘mbabe’ mwenzake nafasi ya uenyekiti CHADEMA Taifa......Chadema Wadai ni Msaliti

$
0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tabora, Kansa Mbarouk amejitokeza ‘kupimana kifua’ na Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe katika uchaguzi wa ndani unaotarajiwa kufanyika Septemba 14.    Mbarouk alirejesha fomu hizo makao makuu ya Chadema jana mchana huku akikumbana na kizingiti cha kuzuiwa na walinzi kuingia ndani kurejesha fomu akiwa pamoja na waandishi wa habari na

Mfanyabiashara afia GESTI Jijini Arusha

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Olais Metili mkazi wa Uzunguni jijini Arusha, amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni ya Hoteli Diamond Motel iliyopo eneo la Sakina jijini hapa.    Mwili wa mfanyabishara huyo anayemiliki mali mbalimbali ikiwamo mgahawa wa Bite Bite na duka maarufu la vinyago eneo la Kisongo uligundulika jana saa 7:00 mchana, wakati wahudumu wa hoteli hiyo

Tatizo la mwanaume kupoteza au kukosa korodani

$
0
0
Ni tatizo au ugonjwa unaoweza kumpata mwanaume yeyote lakini zaidi kwa watoto wa kiume, hali hii inatokana na mtoto wa kiume kuzaliwa bila kuwa na korodani na hivyo mifuko ya korodani japo ipo lakini mitupu, au kuzaliwa na korodani lakini baadae zikapotea ghafla ukubwani.   Kupotea au kutokuwepo kwa korodani kunaweza kuhusisha korodani zotembili au moja, ni tatizo linalotokea kwa mtoto

Rais Kikwete akataa wanafunzi kugeuzwa ‘matrekta’

$
0
0
RAIS Jakaya Kikwete ametaka kuondolewa kwa mpango wa kuwalimisha wanafunzi ili waweze kupata chakula wakiwa shuleni kwani dhamana ya kumlisha mtoto ni ya mzazi na mtoto hatakiwi kujilisha mwenyewe.   “Dhamana hii lazima wazazi wabebe ili mtoto asilimie uji wake,” alisema Rais Kikwete. Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Serengeti Fiesta Moshi ilikuwa ni Balaaaaaa......Bofya hapa ujionee

$
0
0
MAPEMA saa za jioni, makundi ya wakazi wa Moshi yalimiminika kwenye Uwanja wa Majengo kwenda kushuhudia tukio lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa, onyesho la Serengeti Fiesta. Kwa kuwa hata mwaka jana lilifanyika hapa, mashabiki walifahamu fika ni nini cha kutarajiwa haswa katika ubora, lakini safari hii kukiwa na kitu kingine tofauti. Kampuni ya Bia ya Serengeti, kupitia kinywaji chake

Gari lateketea kwa moto mkoani Morogoro

$
0
0
GARI dogo ambalo halikupatikana namba zake limeteketea kwa moto leo maeneo ya Msamvu mkoani Morogoro. Mpaka mpigapicha hizi akiondoka eneo la tukio, chanzo cha moto huo kilikuwa bado hakijafahamika.  

Lady Jaydee ajibu habari ya gazeti la udaku kuwa na uhusiano na ‘Dogo Dogo’

$
0
0
Lady Jaydee ameamua kujibu habari iliyoandikwa kwenye gazeti la udaku la Risasi kuhusu kuwa na uhusiano na aliyewahi kuwa mtuma salamu maarufu kwenye redio, Meddy Ahmed aka ‘Mtoto wa Vitoto’. Kwenye habari hiyo, Risasi wanadai kuwa Jaydee ambaye anadaiwa kuachana na mume wake Gadner G Habash ameonekana mara kadhaa na Mtoto wa Vitoto na kwamba amewahi kuonekana akiwa na gari lake.  

Rais Kikwete Akutana na Wajumbe wa kituo cha Demokrasia Tanzania ( TCD)

$
0
0
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo akiongea na Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. ABdulrahman Kinana na Mhe Isack Cheyo walipowasili Ikulu ndogo mjini Dodoma kukutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo. Nyuma yao ni Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mwenyekiti wa UPDP Mhe Fahmi Dovutwa leo.TCD inaundwa na

Je, unasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume?? Unataka kuimarisha mishipa yako ili uweze kwenda Raundi mbili na kuendelea??....Bofya hapa ukutane na JIKO

$
0
0
Neema  Herbalist  & Nutritional  Foods  Clinic  ni  wauzaji wa dawa  mbalimbali  za  asili. Tunapenda  kuwatangazia  wateja  wetu  kuwa  tunayo  dawa nzuri  ya  asili  inatibu na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.  Dawa  hii iitwayo  JIKO  ni  ya  asili  kabisa  (PURE HERBAL) na inaponyesha  na  kumaliza  kabisa  tatizo  la  nguvu  za kiume

Upepo umegeuka: Kajala kumwajiri Wema Sepetu

$
0
0
AMA kweli fedha mwanaharamu! Kama bado ulikuwa ukiamini kwamba Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu anayependelea kuitwa Madam ana mtonyo (fedha) kumzidi aliyekuwa shosti wake, mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, umekosea sana kwani upepo umegeuka.   Habari za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa utajiri alionao kwa sasa, Kajala anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo chanzo.

Mwafaka wa Katiba Waja.....Mkutano wa Rais Kikwete na Vyama vya Siasa Wazaa Matunda.....Maridhiano kamili kupatikana kwenye mkutano wa TCD Wiki ijayo

$
0
0
MKUTANO wa Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa juu wa vyama vya siasa uliofanyika jana mjini Dodoma umetajwa kuwa na dalili nzuri zinazoashiria mwafaka utapatikana juu ya mchakato wa utengenezaji Katiba mpya.  Kikwete alikutana jana na vyama hivyo kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kinachoongozwa na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo kukiwa na ajenda mbili mojawapo ikihusu mchakato

Waraka wa makanisa kusambazwa hadi jumuiya

$
0
0
Waraka uliotolewa juzi na Jukwaa la Wakristo Tanzania wakitaka mchakato wa Katiba Mpya usitishwe, jana ulisomwa katika baadhi ya makanisa na sasa utasambazwa katika jumuiya ndogo za Kanisa Katoliki.    Akizungumzia waraka huo katika Ibada ya Jumapili, Paroko wa Parokia ya Mkwawa ya Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa, Padri Oscar Rutechura alisema amechukua uamuzi huo ili kuwawezesha

Polisi Ujerumani Wamuokoa Diamond kutoka kwa Mashabiki wenye hasira kali

$
0
0
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri, Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava Nasib Abdul 'Diamond Platnumz' alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show. Washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00

Shilole akiri kutotumia Condom kwenye mapenzi

$
0
0
Mwigizaji  wa  filamu  na  mwanamuziki  wa  miondoko    ya  kizazi  kipya, Zuwena  Mohammed  'Sholole'  amesema  kuwa  matumizi  ya  kondom  wakati  wa  mahaba  hayaleti  ladha  ndio  maana   alilazimika  kwenda  kupima  ngoma  na  mpenzi  wake  Nuh  Mziwanda  ili  wasiwe  wanatumia  kondom. Akizungumza  na  Mpekuzi  wetu, Shilole  alisema  kuwa  raha  ya  mapenzi  ni  kila  mmoja  kuwa 

Martin Kadinda: Wema Sepetu Hana Pesa Ya Kunilipa, Nahangaika Ili Tusilale Njaa

$
0
0
Martin Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa Wema Sepetu aliyekuwa akimwaga pesa vilivyo kwasasa hana pesa ya kumlipa bali yeye Martin anahangaika kwa issue zake binafsi ili wasilale njaa... Kadina amesema kuwa yeye na Wema hawana mkataba wa kulipana bali wapo kishkaji zaidi. "Wema hana pesa ya kunilipa mimi, ninachokifanya ni  kuhangaika kutafuta deals

Ujerumani yajitosa Katiba mpya

$
0
0
UBALOZI wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani nchini umejitosa katika mjadala wa Bunge la Katiba mpya linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma.   Pamoja na hali hiyo, Ujerumani imekanusha kuhusika kusaidia kikundi chochote nchini kinachojihusisha na masuala ya siasa, ikiwamo suala la Katiba.   Tamko kwa vyombo vya habari lililotolewa jana na Ofisa Mawasiliano wa Ubalozi wa Ujerumani

Mrema amwomba Rais Kikwete amfukuze Mbatia ubunge

$
0
0
MBUNGE wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP), amemwomba Rais Jakaya Kikwete amnyang’anye ubunge Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia.   Mrema alitoa ombi hilo juzi mjini Dodoma, alipokuwa akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Rais Kikwete kwa ajili ya kutafuta mwafaka wa Bunge Maalumu la Katiba.   Chanzo chetu cha habari kilichokuwa

Mawakala wa makomandoo wa Nepal waliotua nchini kinyemela na kujifanya 'Walinzi' wapandishwa kortini

$
0
0
MKURUGENZI wa Kampuni ya Ulinzi ya Advanced Limited, Juma Ntinginya (47) na wenzake wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuwahifadhi raia wa Nepal.   Washtakiwa hao walipanda kizimbani jana mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji, Patrick Ngayomela.   Ngayomela alidai washtakiwa

Mjane Alipuliwa kwa Petrol usiku akiwa amelala....Kitendo cha mama huyo kuhama Ulokole na kujiunga na Uislam chadaiwa kuwa chanzo

$
0
0
MAMA mmoja mjane, Mwajuma Hamisi Lissu (42) ameteketea kwa moto baada ya nyumba aliyokuwa amelala eneo la Kibamba Hondogo A maarufu Miti Mirefu jijini Dar es Salaam, kulipuliwa kwa petroli usiku wa  Agosti 24, mwaka  huu. Tukio hilo la kusikitisha inadaiwa linahusishwa  na ugomvi baada ya mama  huyo kuachana na ulokole na  kujiunga tena katika dini yake ya zamani ya

Sheikh Ponda aiangukia mahakama....Aiomba itumie busara kusimamisha kesi ya uchochezi inayomkabili

$
0
0
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameiangukia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa kuiomba itumie busara kusimamisha kesi ya uchochezi inayomkabili mkoani Morogoro.   Maombi hayo yaliyokwama mara kadhaa kutokana na sababu za kisheria, yaliwasilishwa jana kupitia wakili wake, Juma Nassoro, wakati rufaa yake ya kupinga hukumu ya Mahakama ya
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images