Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Walichokizungumza Chama cha ADC kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa

$
0
0
Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimesema licha ya baadhi ya wagombea wake kuenguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, kitashiriki uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 24, 2019.

Katibu mkuu wa chama cha ADC, Hassan Doyo amezungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya chama hicho na kuweka wazi kuwa hawatajitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019.

Wakati ADC wakieleza hayo vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, UPDP, NLD, Chauma, ACT-Wazalendo na CUF vimeshatangaza kutoshiriki uchaguzi huo kwa madai ya kutotendewa haki ikiwa ni pamoja na wagombea wake wengi kuenguliwa.

“Sisi ni mabingwa wa changamoto hatupelekwi na mihemko ya watu, tunapelekwa na misingi ya chama cha siasa kwa sababu hata walipofuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar wengine walisusa lakini sisi hatukufanya hivyo,” amesema Doyo

Wanafunzi Wachomana Visu Kisa Kumwagiana Maji Machafu Siku Ya Birthday

$
0
0
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Ufundi Trade Peramiho wilayani Songea, Grayson Maselin (23), amejeruhiwa na mwanafunzi mwenzake Mosses Ngole (23), kwa kuchomwa kisu shingoni baada ya kummwagia maji machafu siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake (birthday).

Ngole, mwanafunzi wa mwaka wa nne katika chuo hicho, anadaiwa kumchoma kisu shingoni mwanafunzi mwenzake huyo na kumsababishia jeraha na kuvuja damu nyingi kwenye sherehe hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, alidai tukio hilo lilitokea Jumatano majira ya saa saba mchana katika chuo hicho.

Alidai kuwa, siku ya tukio, Ngole alikuwa analazimishwa kumwagiwa maji na kupakwa matope na wanafunzi wenzake ndipo alipopandisha hasira na kufikia uamuzi wa kumchoma kisu mwanafunzi mwenzake huyo.

Kamanda Maigwa alidai mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi mwenzake, ambaye kwa sasa amelazwa Hospitali ya Kanisa Peramiho.

NIDA Yasema Apps Za Kitambulisho Cha Taifa Zinazosambaa Mitandaoni Ni Batili

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili November 17

Biteko Ang’aka Kuhusu Mishahara ya Watanzania Migodini Na Issa Mtuwa – Geita

$
0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko pamoja na kuupongeza uongozi wa mgodi wa dhahabu wa Geita “GGM” katika  mambo mengi leo tarehe 16/11/2019 alikuwa “mbogo” kwa uongozi huo kuhusu suala la mishahara wanayolipwa Watanzania ambapo amebaini kutokuwepo kwa usawa. 
 
Biteko amesema anaumizwa sana na jambo la malipo ya mishahara kati ya Watanzania na wageni licha ya kulingana kwa sifa, ujuzi na elimu na wakati mwingine mtazania anasifa zaidi kuliko mgeni lakini bado mtanzania analipwa chini kuliko yule mgeni.  

Kutokana na hali hiyo, Biteko ameuagiza uongozi wa GGM kuwasilisha orodha ya malipo ya mishahara ya wafanyakazi wote (Payroll) kwa Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa wiki ijayo. Biteko alianza kuhoji idadi ya idara zilizopo na zinaongozwa na akina nani huku akiuliza kuna watu wangapi wa kigeni katika idara hizo na majukumu yako.  

“Sheria ya madini hasa sheria ya Local content inatoa muongozo ni namna gani na wakati gani mgodi unaweza kumuajiri mtaalamu wa fani fulani kutoka nje endapo hakuna mtanzania wa kuweza kushika wadhifa huo” amesema Biteko.  

Ameongea hayo wakati akiongea na uongozi wa mgodi wa GGM mkoani geita alipotembelea mgodini hapo kwa ziara maalum ya kikazi kwa lengo la kufuatilia na kukagua uendeshaji wa shughuli za mgodi huo, ufuatilia na kuangalia utekelezaji wa malalamiko ya wananchi na malipo ya ushuru wa Halmashauri (Service Levy) ambapo mgodi huo unawajibika katika malipo hayo. 

Aidha, Biteko amekwenda kujiridhishi katika masuala mbalimbali ambayo kamati maalumu aliyoiunda kwenda mgodini hapo kwa ajili ya kuangalia na kukagua ili ajiridhishe kabla ya kutoa idhini ya kuruhusu mgodi huo kuanza uchimbaji wa chini kwa chini (Underground) kufuatia maombi ya mgodi huo kwa waziri. 

Kwa mujibu wa kifungu cha 40 cha marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2017  hairuhusu uchimbaji wa chini kwa chini kwa mwekezaji au mgodi mpaka apate idhini (Kibali) ya waziri mwenye dhamana ya Madini ambapo Waziri alianisha mambo mengi ya kuzingatiwa na mgodi kabla hawajaruhusiwa. 

Biteko ameendelea kusisitiza kauli yake ya mara kwa mara kuwa raslimali hizi ziwe neema kwa wananchi na sio mateso. Kauli hiyo ameitoa kufuatia malalamiko ya wananchi wapatao 350 ambao makazi yao yalipitiwa na tetemeko wakati wa milipuko mbalimbali mgodini hapo wakati wa ulipuaji wa miamba. 

Ameongeza kuwa hadi kufikia mwisho mwaka huu ukurasa wa suala la malipo ya fidia ya suala hili liwe limefungwa na kwamba wenye malalamiko wote wapeleke kwa Mkuu wa Wilaya Geita kuanzia tarehe 18-23/11/2019. 

Kwa upande wa uongozi wa mgodi ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi Richard  Jordanson na Makamu Mkurugenzi Mtendaji Simon Shayo kwa nyakati tofauti wametoa shukrani kwa ujio wa Waziri kwenye mgodi wao ikiwa ni mara yake ya kwanza kutembelea tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Madini.  

Wameongeza kuwa mgodi wao upo mstari wa mbele kutekeleza maagizo ya serikali na kwamba wanapenda kuwa msistari mbele na wawe wa kwanza katika kuchangia sehemu kubwa itakayo changia pato (GDP) la taifa kwa upande wa madini. 

Shayo amemwambia waziri kuwa mambo mengi aliyoyasema Waziri kama vile; mpango wa ufukiaji mashimo baada ya mgodi kufungwa, ulipaji wa ushuru wa Halmashauri za wilaya (Service levy), mchakato wa ulipaji wa fidia ya wananchi na utekelezaji wa sheria ya local content vinatekelezwa baadhi vimeshakamilishwa na baadhi vipo kwenye taratibu za kukamishwa.  

Akiwa kwenye mgodi wa RZ unaomilikiwa na mwekezaji kutoka china anae fahamika kwa jina la “Lyuu” amemtaka mwekezaji huyo kwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia sheria zote zikiwemo za madini, kazi na utoaji wa mikataba ya ajira na makato ya NSSF kwa wafanyakazi wake na kuiwasilisha kwa mamlaka husika.  

“Lyuu” amesema ameshukuru waziri kutembelea mgodi kwake na amepokea maelekezo ambayo ameyakubali na kuahidi kuyatekeleza. Wakati wakati huo huo wafanayakazi walipo mgodini hapo amewataka kuwa waaminifu na kuepuka vitendo vihovu kwa mwekezaji. 

Rais Magufuli Na Mkewe Janeth Magufuli Wameshiriki Misa Takatifu Dominika Ya 33 Mwaka “C” Katika Kanisa Katoliki La Mtakatifu Petro

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtoto Cephas Kinunda mara baada ya ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko wa parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi, Novemba 17, 2019.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Paroko wa parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi na Mzee wa Kanisa Dkt. Adelhelm Meru mara baada ya ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Novemba 17, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko wa parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi, Novemba 17, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) wakipeana mikono ya Amani na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakati wa ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko wa parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi, Novemba 17, 2019.

Bodi Ya Rea Yampa Siku 14 Mkandarasi Wa Umeme Mkoani Simiyu Kujirekebisha

$
0
0
Na Teresia Mhagama, Simiyu
Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imempa siku 14 mkandarasi wa umeme vijijini mkoani Simiyu kuongeza kasi ya usambazaji umeme katika vijiji alivyopangiwa la sivyo Bodi hiyo haitasita kuchukua hatua mbalimbali za kimkataba ikiwemo ya kusitisha mkataba.

Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Wakili Julius Kalolo  alisema hayo tarehe 16 Novemba, 2019 wilayani Busega mkoani Simiyu mara baada ya kukagua kazi ya usambazaji umeme katika Vijiji mbalimbali vya wilaya ya Bariadi na Busega akiwa amembatana na Mjumbe wa Bodi hiyo, Dkt Andrew Komba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga.

” Bodi haijaridhishwa na kasi ya mkandarasi huyu kwani amepewa kazi ya kupeleka umeme katika vijiji 152 vya Mkoa wa Simiyu lakini mpaka sasa amesambaza katika vijiji 54 ambayo ni takribani asilimia 30 tu ya kazi anayopaswa kufanya hivyo tumempa siku 14 aonyeshe mabadiliko la sivyo tutachukua hatua.” Alisema

Wakili Kalolo alieleza kuwa, Serikali imetimiza jukumu la kutoa malipo kwa mkandarasi huyo ili kazi ya usambazaji umeme ifanyike kwa kasi hivyo visingizio vya ucheleweshaji wa kazi havikubaliki kwani kwa mujibu wa mkataba wa mkandarasi huyo anapaswa kumaliza kazi mwezi Aprili mwaka 2020.

Aidha, alimwagiza mkandarasi huyo kampuni ya Whitecity Guangdong JV, kuwasilisha mpango kazi wake kwa Bodi hiyo, Mameneja wa TANESCO mkoani Simiyu pamoja Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu ili kuweza kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa kazi anazofanya.

Awali Bodi hiyo ilikutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini ambapo, Mjumbe wa Bodi ya REA, Dkt. Andrew Komba alitoa shukrani kwa viongozi wa mkoa wa Simiyu kwa kufuatilia utekelezaji wa kazi ya usambazaji umeme vijijini.

Aidha, aliomba kasi hiyo iongezeke ili Mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA III) ukamilike kwa wakati.

Alisema kuwa, msukumo wa kuwafuatilia wakandarasi unahitajika ili kutimiza lengo la Serikali  la kupeleka umeme katika vijiji vyote vilivyopo katika mpango  wa REA III mzunguko wa kwanza ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

Aidha alitoa wito kwa viongozi wa Serikali katika  ngazi mbalimbali za mkoa, kuhamasisha wananchi kujiunga na huduma ya umeme kwani Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika kuwasambazia umeme wananchi hivyo wanapaswa kuunganisha umeme kwa wingi na kuutumia katika shughuli za kiuchumi na kijamii

Wanajeshi wa China wasafisha mitaa ya Hong Kong Iliyokuwa Imefungwa na Waandamanaji

$
0
0
Wanajeshi wa China wametoka jana katika kambi zao mjini Hong Kong na kwenda mitaani kusaidia kuisafisha na kuondoa vifusi na vizuizi vilivyowachwa na waandamanaji.

Lilikuwa tukio lisilo la kawaida kwa Jeshi la China kuingia katika mitaa ya jimbo hilo lenye mamlaka ya ndani, ambalo kushindwa kwa serikali yake kumaliza maandamano yaliyodumu kwa zaidi ya miezi mitano kumezusha uvumi kuwa China huenda ikawatumia wanajeshi wake kisiwani humo.

Serikali ya Hong Kong imesema haikuomba msaada wa jeshi katika shughuli ya usafishaji, ikiielezea kuwa shughuli ya kujitolea ya kijamii. Wengi wa waandamanaji wanaoipinga serikali waliondoka kwenye vyuo vikuu vya Hong Kong baada ya kuvidhibiti kwa karibu wiki moja.

Serikali yaamua kumfariji Binti ambae alifichwa kufariki kwa Wazazi Wake Wote na Ndugu Zake Watatu

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ameeleza kuguswa na tukio la kupoteza wazazi wawili, na ndugu zake watatu lililomkuta mwanafunzi Anna Zambi ambaye amemaliza kidato cha 4 hivi karibuni ambapo Waziri Ummy ameahidi ataenda kumjulia hali mtoto huyo na kumpa salam za pole.

Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake Twitter kufuatia jana mtoto huyo kupelekwa mahali ambapo wazazi wake na ndugu zake wamezikwa baada ya kufariki Dunia walipokuwa wakielekea kwenye Mahafali yake ambapo walifariki Dunia wakiwa mkoani Tanga kutokana na mafuriko ya maji.

Waziri Ummy ameandika kuwa; "Suala la mtoto Anna Zambi, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii tunachukua jukumu la kuratibu na kusimamia psychosocial support ya mtoto huyu pamoja na ustawi wake kwa ujumla, Katibu Mkuu Dkt. John Jingu leo ataitembelea familia yake iliyopo Goba” – Waziri Ummy

Wazazi walikuwa wakifahamika kwa majina ya Lingston Zambi na Winifrida Lyimo na wadogo zake watatu, Lulu, Andrew na Grace walikufa katika ajali hiyo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Handeni mkoani Tanga.

Kampeni Ya Elimu Kwa Mlipakodi Yawafikia Wafanyabiashara Zaidi Ya 700 Morogoro

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewafikia na kuwaelimisha wafanyabiashara zaidi ya 700 kupitia kampeni ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi iliyofanyika mkoani Morogoro.

Lengo la kampeni hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki, Afisa Msimamizi wa Kodi Mkuu wa TRA, Julius Mjenga amesema kuwa, mamlaka hiyo ililenga kuwafikia wafanyabiasha 500 lakini kutokana na mwitikio mkubwa, TRA imefanikiwa kuvuka lengo hilo na kuwafikia zaidi ya 700.

“Wiki hii moja ya elimu kwa mlipakodi, tuliwalenga wafanyabiashara wa wilayani ambapo kumekuwa na changamoto ya kutokupata elimu ya kodi kwa wakati. Nashukuru tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu tumeweza kuwaelimisha wafanyabiashara 774 katika kampeni hii”, alisema Mjenga.

Mjenga ameongeza kuwa “Tumefika karibu wilaya zote za mkoa huu wa Morogoro ambazo ni Malinyi, Ulanga, Kilosa, Mvomero, Kilombero na Gairo na kila mahali tulipopita tumepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi mbalimbali.”

Kwa upande wa wafanyabiashara waliotembelewa na TRA, wameishukuru mamlaka hiyo kwa kuwaelimisha masuala mbalimbali yanayohusu kodi na kuomba elimu hiyo iwe endelevu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema kuwa, TRA ya sasa sio ile ya zamani kwa sababu sasa hivi maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wamekuwa karibu na walipakodi na siku hizi hawana tabia ya kufunga biashara zao.

“Zamani mtu alikuwa akisikia watu wa TRA wanakuja, anafunga duka anaondoka lakini siku hizi, TRA wamekuwa marafiki, wanatuelimisha na wala hawafungi biashara zetu, kwakweli tunashukuru sana,” alisema Eleonora Kisimba, mfanyabiashara wa duka la nguo wa wilayani Mvomero.

Naye Stanphord Mjumbe ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi wilayani Gairo mkoani hapa alisema kuwa, kampeni ya elimu kwa mlipakodi ifanyike mara kwa mara kwa sababu wafanyabiashara walio wengi hususani wadogo hawajasoma hivyo wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya haki na wajibu wao katika ulipaji kodi.

“Sisi wafanyabiashara wadogo, tulio wengi hatujasoma hivyo tunahitaji elimu hii angalau kwa mwaka mara tatu ili tuweze kuelewa kwa kina haya mambo ya ulipaji kodi maana wakati mwingine tunakuwa hatujui haki zetu,” alisisitiza Mjumbe.

Aidha, wafanyabiashara hao wameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania kurejesha Kodi ya Zuio kwa wamiliki wa majengo kwa kuwa baadhi yao hawataki wapangaji kuzuia asimilia kumi na kuiwasilisha TRA.

Vilevile, wameomba kuelimishwa jinsi ya kulipa kodi ya mapato kwa awamu mara tu wanapokadiriwa kodi hususani kwa wafanyabiashara wapya kwani wengi wao wanapitiliza tarehe za kulipa kodi hiyo kwa kukosa uelewa.

Kampeni ya huduma na elimu kwa mlipakodi imemalizika tarehe 17 Novemba, 2019 na ilifanyika katika Mikoa ya Morogoro na Pwani ambapo wafanyabiashara wamepata fursa ya kutembelewa katika maduka yao na wengine walihudhuria semina kwa ajili ya kuelimishwa masuala mbalimbali yanayohusu kodi.

Mwisho.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu November 18

PolePole: CCM Imejipanga Vizuri Uchaguzi Serikali Za Mitaa

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud,Arusha
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM),kimesema kuwa kimejipanga kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika novemba 24 mwaka huu na kimewaonya wale wote ambao wamepanga kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kuacha mara moja kuchochea wananchi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa,Humphrey Polepole alitoa kauli hiyo Novemba 17 jijini Arusha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha na kueleza kuwa ushindi wa kishindo wanaotarajia kuupata ni kutokana na wananchi kuridhishwa na utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

Amevitaka vyama vyama vya upinzani kuheshimu kanuni,sheria na taratibu za uchaguzi na kwamba wasipange au wasiwashawishi wafuasi wao kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani wakati wote kuanzia kipindi cha kampeni,upigaji kura,kuhesabu matokeo pamoja na kutangazwa kwa mshindi kwa kuwa chama hicho kimejipanga kikamilifu.

“Wananchi wameridhishwa na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwani katika kipindi cha miaka mine ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano miradi mingi ya maendeleo inayogusa moja kwa moja maisha ya mwananchi wa kawaida imetekelezwa kwa kiwango kikubwa sana”alisema.

Polepole aliitaja baadhi ya miradi ambayo imetekelezwa kwa kiwango kikubwa katika kipindi kifupi cha miaka mine kuwa ni ujenzi wa vituo vya afya na hosipitali za Wilaya,upatikanaji wa maji safi na salama,ujenzi wa barabara na madaraja,usambazaji wa umeme katika maeneo mengi ya mijini na vijijini,ujenzi wa vyumba wa madarasa,nyumba za walimu pamoja na maabara.

Alisema kuwa mkutano huo na wanahabari ni matokeo ya kikao kazi cha kufanya tathmini ya kimaendeleo ya miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli na kueleza kuwa Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa hapa nchini ambayo miradi mingi ya kimaendeleo imetekelezwa.

Alisema kuwa wimbi la wananchama waliotoka kwenda vyama vya upinzani mara baada ya mzee na Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kuhamia huko ndio lililopelekea chama hicho kuanza kujitathmini na kuandaa mikakati ya ushindi ikiwemo kurudi nyumbani kwa kiongozi huyo kumekisaidia chama hicho kuvuna wanachama wengi zaidi kwa kipindi kifupi.

Alisema kuwa mkutano huo na wanahabari ni matokeo ya kikao kazi cha kufanya tathmini ya kimaendeleo ya miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli na kueleza kuwa Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa hapa nchini ambayo miradi mingi ya kimaendeleo imetekelezwa.

Kadhalika katibu huyo wa Itikadi na uenezi alieleza kushangazwa kwake na baadhi ya vyama vya upinzani ambavyo vimetangaza kujitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kueleza kuwa baadhi ya vyama vilivyotangaza kujitoa havikuwahi kusimamisha mgombea hata mmoja na kuhoji wanajitoa wapi.

Awali akimkaribisha Katibu huyo wa Itikadi na uenezi Taifa,Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha,Mussa Matoroka alisema kuwa kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa CCM Mkoa wa Arusha imejipanga kikamilifu, kimkakati na kisayansi  kwa kuhakikisha kuwa wanashinda kwa kishido katika uchaguzi huo.

Aliwataka wananchi wa mkoani hapa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kutimiza haki yao ya msingi kikatiba ya kuchagua katika maeneo mbalimbali yaliyotengwa kwa ajili ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambapo pia amewasishi kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani kabla na baada ya uchaguzi.

Katika mkutano huo katibu huo wa Itikadi na uenezi taifa aliambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya Mkoa na Wilaya ambapo kila mmoja alipata fursa ya kuzunguza juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika eneo lake.

Waziri Jafo Ameagiza Kufukuzwa Shule Kwa Mwanafunzi Ambaye Ataharibu Miundombinu Shuleni Kwa Makusudi

$
0
0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo ameagiza kufukuzwa shule kwa mwanafunzi yeyote atakayebainika   kuharibu kwa makusudi miundombinu au samani  katika shule za umma  kwa lengo la kuhakikisha usalama wa muda wote wa miundombinu hiyo.

Jafo ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akiwataka wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za mitaa kuhakikisha shule zote katika maeneo yao zimeboresha fomu ya maelezo ya kujiunga na shule (Joining Instructions)

Alisema sababu ya kuboresha fomu hizo ni hatua inayolenga kuweka adhabu za kuchukuliwa dhidi ya mwanafunzi au kikundi cha wanafunzi kitakachobainika kufanya uharibifu huo.

Alisema hatua hiyo imetokana  na tabia iliyoanza kujitokeza siku za hivi karibuni  ikiwemo mkoani Mbeya na Morogoro kwa baadhi ya wanafunzi hao kufanya uharibu wa miundombinu na samani za shule, jambo alisisitiza kuwa ni kinyume na utaratibu lakini pia zikirudisha nyuma juhudi za Serikali na wadau wengine wa maendele katika suala la ujenzi wa shule hizo.

Alisema Serikali isingependa kuona uharibifu wa miundombinu hiyo ikitokea kama walivyofanya wanafunzi wa Shule  ya Sekondari ya Mji Mpya ya Manispaa ya Morogoro na Shule ya Sekondari ya  Kiwanja  ya Halmashauri ya Chunya ambao wameonyesha nidhamu mbovu ya kuanza kuharibu miundombinu ya shule huku akiwapongeza viongozi katika mikoa hiyo kwa kuchukua hatua stahiki.

“Wazazi na walezi watawajibika kutengeneza kifaa au mali hiyo na kuirejesha katika hali yake ya awali, aidha mzazi au mlezi wa mwanafunzi atakayekiuka masharti hayo ya shule, mwanaye asimamishwe masomo au afukuzwe shule kwa maana hatuwezi kuvumilia kuendelea kuwa na wanafunzi waharibifu na wasio na maadili mema katika shule zetu” aliongeza Jafo.

Aidha alizitaka bodi za shule zifanye kazi yao ipasavyo ili kuilinda miundombinu hiyo na samani za shule na kuwaomba wadau mbalimbali wa maendeleo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha maendekeo ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na kusimamia nidhamu ya wanafunzi na watoto ambao ndiyo nguzo na viongozi wa baadae wa Taifa hili.

Waziri wa Kilimo Abaini Ubadhilifu Bodi Ya Korosho, Aunda Tume Kuchunguza

$
0
0
WAZIRI wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya uchunguzi kwenye mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao la Korosho baada ya kubaini kuwepo na udanganyifu.

Mhe Hasunga amemuagiza CAG kuchunguza kiasi cha Shilingi Bilioni 53.2 kilichobaki kwenye akaunti ya Mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao la Korosho ambazo zilikuwa kwa ajili ya kujenga viwanda vitatu vya kubangua korosho na maghala.

Aidha Mhe Waziri ameunda timu ya watu wasiozidi watano kwa ajili ya kuhakiki kiasi cha korosho kilichopokelewa na kilichouzwa katika msimu wa Korosho wa mwaka 2018/2019 baada ya kubaini uwepo wa udanganyifu.

Hayo ameyasema jana tarehe 17 Novemba 2019 jijini Dodoma mbele ya wandishi wa habari ambapo amezitaka pia kamati za ulinzi na usalama kusimamia zoezi la uhakiki ambalo linaonekana kutawaliwa na udanganyifu ambapo timu iliyoundwa itashirikiana na timu iliyokuwepo chini ya wizara hiyo kuhakiki pia fedha zilizopatikana ili wahakikishe wanaolipwa ni wale wanaostahili.

Aidha amesema timu hiyo ihakikishe kuwa majina yaliyotoka kwenye vyama vya msingi kwenda kwenye vyama vikuu hadi fedha zilizoingia benki  kama kweli ziliingia kwenye akaunti za wakulima na kama kuna unyaufu uliojitokeza wabainishe ni kwa kiwango gani ili kusaidia serikali kutoa taarifa yenye uhalisia.

Waziri Hasunga amesema mwaka 2016 serikali iliamua kufuta mfuko wa Wakfu na kwenye akaunti kulikuwa na kiasi cha shilingi bilioni 53.2 lakini bodi ya Korosho iliamua kubadili matumizi na kutumia fedha hizo tofauti na maagizo yaliyotolewa na serikali.

"Kama Wizara hatupo tayari kuona ubadhilifu wowote wa fedha za umma unafanyika, Serikali ya awamu ya tano haiwezi kukubali kuona watu wachache wanafaidika na fedha za walipa kodi wa Tanzania.

Timu zote mbili naziagiza hadi kufikia Januari 15 mwaka 2020 wawe wameshatuletea ripoti wizarani. Niwahakikishie hatutomvumilie yeyote ambaye atajaribu kugusa fedha za wananchi, " Amesema Waziri Hasunga.

Amesema bodi hiyo ilitumia kiasi cha shilingi bilioni 28.1 kununua viuatilifu,walitumia kiasi cha shilingi bilioni 12.2 kulipia magunia ilhali katika msimu huo wanunuzi walikuwa wananunua magunia wao wenyewe.

Ametoa wito kwa wakulima kuwa kama kuna anayedai ushirika apelike madai yao kwenye kamati ya ulinzi na usalama na timu iliyoundwa ili waseme kama hawajalipwa.

MWISHO

Marekani, Korea Kusini kusitisha Mazoezi Ya Kijeshi

$
0
0
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper amesema kwamba wamesitisha kwa muda usiojulikana mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Korea Kusini katika kile alichokitaja nia njema kuelekea Korea Kaskazini. 

Hatua hiyo inakuja hata baada ya Waziri wa Ulinzi wa Japan Taro Kono ambaye nchi yake imekuwa ikitishwa na majaribio ya mara kwa mara ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini kumuelezea Esper kwamba hakuna ambaye ana matumaini kuhusu kubadilisha hatua za Korea Kaskazini.

Matamshi hayo ya Kono yanaashiria kuzorota kwa mahusiano kati ya Marekani na washirika wake wa kimataifa, katika wakati wanapojaribu kuirejesha Korea Kaskazini kwenye mazungumzo ya kuachana na mipango yake nyuklia na makombora.

Ingawa katika tawala zilizopita Marekani iliyaita mazoezi  hayo kuwa ni muhimu lakini Rais Donald Trump ameyaita kuwa ni upotevu wa fedha na uchokozi dhidi ya Korea Kaskazini.

Waziri Mpina Azindua Agenda Za Utafiti Na Kuibua Tafiti Zilizofichwa Makabatini

$
0
0
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua Agenda ya Kitaifa ya Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 na kutangaza kuzifumua na kuziibua tafiti zote  zilizofanywa na wasomi na kutelekezwa kwenye makabati miaka ya nyuma na kuziingiza kwenye mfumo rasmi wa matumizi ili kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na maendeleo.

Pia agenda hizo zitaleta msisimko mpya wa kufanya utafiti nchini na kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na maendeleo tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo tafiti nyingi zilifanywa na kutelekezwa kwenye makabati na watafiti mbalimbali wakiwemo Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili (Masters Degree)  na Shahada ya Uzamivu (PHD) katika vyuo vikuu mbalimbali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa agenda hizo kitaifa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),  Kampasi ya Mazimbu mjini Morogoro, Waziri Mpina aliziagiza Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TALIRI) na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi(TAFIRI) kubadilika ili kufanya tafiti kwa vigezo vilivyowekwa na kuleta mabadiliko chanya katika sekta za mifugo na uvuvi nchini.

Waziri Mpina alisema chimbuko la kuandaliwa kwa ajenda hizo za utafiti ni baada ya kubaini kuwa ajenda zilizokuwepo awali za Mifugo na Uvuvi zilishindwa kuibua na kuzitumia tafiti zilizofanywa kuchochea mabadiliko kwenye sekta hiyo muhimu ya uzalishaji.

Pia ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi hazikuwa na utaratibu wa kuzitambua, kuziorodhesha na kuzitumia tafiti zinazofanywa na Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili (Masters Degree) na Uzamivu (PHD) lakini sasa ajenda za utafiti zilizozinduliwa zimeweka utaratibu wa namna ya kuzitambua, kuziorodhesha na kuzitumia tafiti za wasomi hao.

“Haiwezekani tafiti za wasomi wa kiwango cha juu kiasi hicho wanazozifanya wakati wa kukamilisha masomo yao ziishie kupata alama za ufaulu na kutupwa kwenye makabati, Leo kila mhitimu atalazimika kuandaa policy brief ambayo itawezesha watumiaji na Serikali kurekebisha au kuandaa Sera na Sheria” alisema Waziri Mpina.

Aliongeza kuwa Ajenda za Utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi hazikuwa na utaratibu wa kuweka Kanuni ambazo zitahakikisha kuwa utekelezaji  wa ajenda za utafiti unafanyika, lakini ajenda za utafiti iliyotangazwa inaweka Kanuni zitakazotoa mwongozo na usimamizi wa utekelezaji na wajibu wa kila mhusika.

Aidha Waziri Mpina alibainisha kuwa ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi hazikuwa na utaratibu wa kuwaunganisha Watafiti wa Mifugo na Uvuvi nchini, na hivyo kupelekea kila mmoja kufanya utafiti kivyake hali iliyosababisha jambo moja kufanyiwa utafiti na mtafiti zaidi ya mmoja na kukosa jukwaa la kuratibu na kuchambua tafiti zinazofanywa nchini.

“Agenda ninayoizindua leo inakwenda kujumuisha watafiti na wataalam mbalimbali waliobobea katika fani za mifugo, uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji ili kuyapitia matokeo ya utafiti, teknolojia zilizoibuliwa na utafiti na kuzisambaza kwa watumiaji kwa manufaa ya Taifa” alisema Waziri Mpina

Pia Waziri Mpina alibainisha mapungufu mengine yaliyomo kwenye ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi ni pamoja na kutoweka msingi mzuri wa kusimamia Watafiti na kufanya tafiti kulingana na mahitaji ya soko badala yake  Taasisi za Utafiti na Watafiti kufanya tafiti nyingi za nje na mambo muhimu ya wananchi yanayohitaji kufanyiwa utafiti kutelekezwa.

“Leo hii agenda ninazozizindua zimeweka utaratibu wa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa, kupanua mtandao wa utafiti  na kufanya tafiti zote kulingana na mahitaji ya wananchi.  Mfano katika maeneo ya nyama, maziwa, samaki, ngozi, chakula cha samaki na mifugo, magonjwa, malisho na migogoro” alisema Mpina.

Aidha dosari nyingine zilizokuwepo kwenye ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi ni kutojumuisha katika vipaumbele masuala mengi muhimu yenye changamoto nyingi ikiwemo  Mitaala na hali ya ajira.

Mpina alisema mitaala inapoanzishwa haifanyiwi utafiti wa mara kwa mara matokeo yake mafunzo yanayotolewa sio yale yanayohitajika katika soko la ajira huku Wanafunzi wanaohitimu mafunzo hawajulikani wanakwenda wapi baada ya kuhitimu na hakuna mfumo wowote wa uratibu.

“Ukienda kwa wafugaji wanaofuga na kuchunga sio hao waliosomea mifugo, ukienda kwa Wavuvi na Ukuzaji viumbe maji wanaovua na kufuga si hao waliosomea taaluma hizo, ukienda viwandani vilevile”alisema Mpina.

Pia Masoko na Biashara, Uongezaji wa mnyororo wa thamani wa mazao ya mifugo na uvuvi (Livestock & Fisheries value chain & value addition), agenda iliyopita ilizingatia uzalishaji pekee bila kuangalia upande wa soko wakati vitu hivi vinakwenda kwa pamoja kwani hakuna uzalishaji bila soko.

Waziri Mpina pia alisema licha ya kushamiri kwa migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi na eneo hilo kugubikwa na changamoto nyingi  ikiwemo  mifugo kutaifishwa, kupigwa risasi, kufilisiwa, kuuwawa kwa watu na mifugo  na kupigwa faini kubwa kiasi cha kutishia uendelevu wa sekta lakini eneo hili halikujumuishwa katika Agenda ya utafiti iliyopita.

Pia masuala mtambuka, afya ya wanyama na magonjwa ya afya ya jamii (Zoonotic Diseases) ambapo hivi sasa asilimia 60 ya magonjwa yasiyoambukiza yanatokana na mazao ya mifugo, malisho, nyanda za malisho na vyakula vya mifugo na samaki, uvuvi endelevu katika maji ya asili (Uvuvi Haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi)  ambayo nayo hayakuzingatiwa katika agenda za utafiti zilizopita .

Hivyo Waziri Mpina aliwahakikishia watanzania kuwa Wizara yake itaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha kuwa matokeo ya tafiti zinazofanywa zinawafikia walengwa kwa wakati ili tafiti hizo ziongeze tija na kipato kwa watuamiaji na Taifa kwa ujumla. 
 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Raphael Chibunda alimhakikishia Waziri Mpina kuwa kwa niaba ya watafiti wa Chuo kikuu hicho watatakwenda kuwa sehemu ya utekelezaji wa agenda hizo.

Nafasi 150 za Kazi Zilizotangazwa Wiki Hii....Zipo za Umoja wa Mataifa, WHO, Benki Mbalimbali za Tanzania Na Zingine

$
0
0


1. Associate Criminal Analyst At United Nations | Tanzania Jobs 

2. Finance and Administrative Assistant at Heifer International 

3. Finance Assistant at Heifer International | Tanzania Jobs 

4. Job Opportunity at WHO | Finance Assistant 

5. Associate Legal Officer at United Nations | Job Opportunities

6. Job Opportunity at Oxfam Tanzania | Country Funding & Partnerships Lead 

7. Job Opportunity at Standard Chartered | Head, Safety and Security 

8. Job Opportunity at THPS | LIS Global Super User and Networking Assistant 

9. Job Opportunity at Yara International | Customer Service Manager 

10. Job Opportunity at THPS | LIS Database Administrator and Networking Program Officer 

11. Job Opportunity at ActionAid Tanzania | Information Technology Coordinator 

12. Job Opportunity At Aga Khan | Clinical Epidemiologist, Medical College 

13. Job Opportunities at Tanga UWASA | Drivers II 

14.Job Opportunity at Tanga UWASA | Customer Service Manager 

15.Job Vacancy at Geita Gold Mining (GGML) | Superintendent UG Planning 

16.Job Opportunity at Tanzania Revenue Authority (TRA) | Assistant Lecturer 

17.Job Opportunity | Estate Officer At Mbeya University November 

18.Artisan II Jobs (Masonry-2 And Plumber-1) At Mbeya University 

19.Technician II Jobs (Civil) At Mbeya University

20
.New Job Opportunity at Institute of Adult Education (IAE) | Deputy Director (Academic, Research And Consultancy) 

21.Airport Services Duty Officer at Qatar Airways  

22.Job Opportunity at ICAP | Strategic Information (SI) Specialist, Tanzania 

23.Job Opportunity at ICAP | Project Director for Health Information Systems (HIS), Tanzania 

24.Job Opportunity at ICAP | Zonal Project Manager 

25..Job Vacancy at Kazini Kwetu Limited | Depot Accountants 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   

==>>Nafasi za Kazi Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania

👉Deadline; November 19,2019

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  

==>>Nafasi Mpya za kazi  Iringa katika shirika la Kimataifa FHI 360 Tanzania
👉Wanataka watu wa fani Mbalimbali
👉Deadline ni; November 23, 2019 

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

Kuangalia Nafasi Zingine Mpya Zilizotangazwa wiki hii <<INGIA HAPA>> 

Lugola Atoa Onyo Kwa Watakaofanya Vurugu Uchaguzi Serikali Za Mitaa

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka Makamanda wa Polisi nchini kusimamia kampeni zilizoanza za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwalinda wagombea wa vyama vya siasa ambavyo vilitangaza kujitoa, pamoja na kuwashughulikiwa bila huruma watu waliopanga kufanya vurugu. 

Waziri Lugola amesema ana taarifa za kutosha kuhusu baadhi ya watu waliopanga kufanya vurugu wakati wa kampeni kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo, aliwataka Makamanda hao kuwasaka kila kona, kuwakamata watu hao ambao wana nia mbaya ya kuvuruga uchaguzi huo.

“Nawataka mtende haki katika usimamizi wa uchaguzi huu, lakini wapo baadhi ya watu ambao wamepanga kufanya vurugu, watu hao msicheke nao, watu hao washughulikieni bila huruma, na badala ya kuwamwagia maji ya kuwasha, sasa watumbukizeni ndani ya tenki la maji hayo ili waweze kuwashwa zaidi, hatutaki vurugu, tunataka amani na utulivu ndani ya nchi yetu,” Lugola.

Kwa upande wa Vyama vya Siasa vilivyojitoa kushiriki uchaguzi huo, Lugola alisema wagombea wapo ambao wamekataa agizo hilo la vyama vyao, hivyo wameamua kushiriki uchaguzi huo wakigombea nafasi walizoziomba, hivyo wanapaswa kulindwa kwa nguvu zote kwani ni haki yao kugombea.

“Wameweka mpira kwapuni, lakini wachezaji wapo uwanjani bado wanataka kucheza,bado wanaenda uwanjani kuwapiga wachezaji hao wasiweze kucheza, bado wanataka kuwapiga waamuzi wasiweze kutoa pointi tatu muhimu kwa timu ambayo imeendelea kucheza,  hao muwashughulikie kiisawasawa,” Lugola.

PICHA: Muonekano wa Jengo la kisasa la abiria katika Uwanja wa Ndege jijini Mwanza mara tu ujenzi wake utakapokamilika.

$
0
0
Ujenzi wa jengo hilo la kisasa umeanza Septemba mwaka huu na litagharimu takribani shilingi bilioni 12.

Gharama za ujenzi ni kodi za wananchi kupitia mapato ya Jiji la Mwanza, Manispaa ya Ilemelea na Serikali Kuu.

Acacia Kuondolewa Soko la Hisa Dar es Salaam

$
0
0
Kampuni ya Acacia inaondolewa katika orodha ya kampuni zilizopo kwenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kuanzia leo, Novemba 18, 2019.
 

Meneja Miradi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Emmanuel Nyalali, amesema kampuni hiyo ambayo imedumu katika soko hilo kwa miaka 8 ikiorodheshwa tangu Desemba 2011, ilifutwa katika Soko la Hisa la London Uingereza (LSEG) tangu Septemba mwaka huu, hivyo utaratibu wote umefuatwa.

“Tangu Septemba 2019 Acasia ilikuwa imeshafutwa kwenye soko la Hisa la London (LSEG), ambalo ndio soko lake mama, hivyo taratibu zilikuwa zinamaliziwa tu na Ijumaa iliyopita Bodi ya DSE ilitoa maamuzi hivyo kuanzia leo kampuni hiyo inafutwa kwenye orodha ya makampuni kwenye DSE'', amesema Nyalali.

Awali kampuni hiyo ilikuwa inajulikana kama African Barrick Gold (ABG) kabla ya kubadili jina na kuitwa Acacia Novemba 2014.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images