Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa November 15


Waziri Hasunga Akitaka Chuo Cha Ifm Kuishauri Serikali Katika Kuimarisha Uchumi Wa Nchi Kupitia Sekta Ya Kilimo

0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa Taasisi za elimu ya juu zina jukumu kubwa la kusaidia juhudi mbalimbali za serikali kupitia kutoa wahitimu wenye uwezo ambao hawawezi tu kuajiriwa katika sekta tofauti za uchumi lakini pia wanaweza kujiajiri.

Mhe Hasunga ametoa rai hiyo tarehe 14 Novemba 2019 wakati wa hotuba yake aliyoitoa wakati wa sherehe za utangulizi wa mahafali ya 45 katika Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM) Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa kutoa elimu bora kwa wanafunzi nchini kutakuza mahitaji ya soko kupitia mitaala inayoendeshwa ambayo haitaweka pengo kati ya nadharia/taaluma na mazoezi.

Amesema kuwa chuo hicho kinapaswa kuendeleza juhudi za kufanya kazi kwa karibu na serikali kupitia wataalamu wake kuishauri serikali ili iweze kuwa na uwezekano katika uimarishaji wa sekta ya uchumi kupitia kilimo kadhalika viwanda.

Waziri Hasunga amesema kuwa Taasisi ya Usimamizi wa Fedha ina maeneo ya kipekee ya utaalam ambayo ni muhimu kwa ajenda ya serikali ya ukuaji wa uchumi. Taasisi hiyo inazalisha wahitimu katika eneo la benki, uhasibu, bima, kinga ya kijamii, uchumi, ushuru, tehama, sayansi ya msingi na Sayansi ya Kompyuta.

“Kwa mfano; IFM inaweza kuunga mkono serikali kupitia kuendeleza benki na bidhaa za bima na huduma, utafiti na kushauri juu ya ujumuishaji wa kifedha (benki isiyokaliwa), kuchanganya udanganyifu wa kidigitali, pensheni, mipango ya usalama wa kijamii ya gharama nafuu, suluhisho la Tehama na uvumbuzi mwingine wa kutatua shida zilizopo katika jamii na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa umma” Alisema Mhe Hasunga

Waziri Hasunga amehimiza kuwa, chuo cha IFM kinapaswa kukuza mipango ya mseto au nidhamu nyingi ambazo zinaweza kutoa wahitimu wenye ujuzi ambao wanaweza kujiajiri katika kilimo na viwanda vya kusindika chakula na hivyo kuongeza michakato ya mnyororo wa thamani ya kilimo.

Katika hatua nyingine amewataka walimu wa chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM) kuhakikisha kuwa wanafanya utafiti wa kuishauri serikali katika maeneo ambayo imeweka msisitizo ili kufanikisha miradi mbalimbali mikubwa ya kimkakati.

Alisema kufanya hivyo kutaongeza uwezekano wa mafanikio ya haraka kwa mwananchi mmoja mmoja na serikali kwa ujumla wake.

MWISHO

Serikali Kuajiri Walimu Wapya 16,000

0
0
Serikali imesema inatarajia kuajiri walimu 16,000 wa shule za msingi na sekondari muda wowote kuanzia sasa.

Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, alitangaza neema hiyo bungeni jana alipojibu swali la Mbunge wa Mlalo, Abdallah Shangazi (CCM), aliyetaka kufahamu mkakati wa serikali kuhakikisha sekta za elimu na afya zinakuwa na watumishi wengi.

"Sekta za elimu na afya zina upungufu mkubwa sana wa watumishi. Sasa, ni upi mkakati wa serikali kuhakikisha tunapata watumishi wa kutosha kwenda kuwahudumia Watanzania?" mbunge huyo alihoji.

Katika majibu yake, Waziri Mkuu alikiri sekta hizo mbili zina uhitaji wa watumishi kutokana na serikali kutanua huduma zake hadi ngazi ya vitongoji.

“Serikali imeanza kutoa vibali vya ajira katika sekta hizi mbili za afya na elimu, hata kwenye kilimo. Mwaka jana, tuliajiri watumishi 6,000 na sasa tuna kibali ambacho kitatoka hivi karibuni cha watumishi 16,000 kwa upande wa sekondari na msingi.

“Tunaamini baada ya ajira hizi kwenye sekondari na elimu msingi, tutakuwa tumepunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa walimu, hivyo hivyo kwenye sekta ya afya, tunataka kuhakikisha tunapeleka wataalamu. Mkakati wa kujenga miundombinu utakwenda sambamba na kuajiri wataalamu," alisema.

Aliongeza kuwa serikali imefanya maboresho makubwa na sera inaeleza kuwa kila kata kuwe na kituo cha afya na kila wilaya iwe na hospitali. Alisema kinachoendelea kwa sasa ni ujenzi wa zahanati na vituo vya afya vyenye uhitaji wa madaktari.

Waziri Mkuu Atoa Maelekezo Kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao Maeneo yao yana upungufu wa chakula

0
0
Serikali imewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya watoe taarifa kama maeneo yao yana upungufu wa chakula na ni kiasi gani kinahitajika.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema jana bungeni mjini Dodoma kuwa, wizara ya Kilimo ikipata taarifa hizo itaratibu vizuri na kuona namna ya kufikisha chakula kwa wananchi kwa kuwauzia ili zipatikane fedha za kununua chakula kingine kiwekwe kwenye Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA).

Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Chemba (CCM) Juma Nkamia aliyetaka kauli ya Serikali kwa kuwa baadhi ya mikoa ukiwemo wa Dodoma, Manyara na Singida ina tatizo kubwa la chakula na huenda baadhi ya wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama hawatoi taarifa sahihi kwa sababu ya woga.

“Upungufu wa chakula upo kwa baadhi ya wilaya na maeneo mengine na huu ulitokana na tatizo la hali ya hewa kwamba yapo maeneo msimu uliopita hayakupata mvua ya kutosha. Jambo hili linapotokea kule kwenye ngazi hiyo tunao viongozi…”alisema Waziri Mkuu wakati akijibu maswali ya papo hapo kutoka kwa wabunge wa Bunge la Tanzania.

“Inapotokea kama hali ya hewa imekuwa mbaya Mkuu wa Wilaya akieleza atakuwa anaeleweka kwa sababu pia baada ya kutoa taarifa hiyo timu ya Wizara ya Kilimo itakwenda kuona hali halisi na kuweza kuzungumza na ile mamlaka kuweza kupelekewa chakula kwa bei nafuu” alisema.

Alisema jambo hilo limetolewa ufafanuzi mara nyingi na kwamba, Rais John Magufuli hajazuia kutolewa kwa taarifa za upungufu wa chakula isipokuwa kwenye maeneo yenye hali nzuri ya hewa na kila mmoja ana nafasi ya kulima au kufanya kazi lakini yana upungufu wa chakula.

“Viongozi waliopo kwenye maeneoi hayo wanao wajibu wa kusimamia kila mmoja anafanya kazi pamoja na kulima mazao ya chakula na biashara ili waweze kujipatia tija inapofikia kipindi kama hiki kila mmoja anakuwa na akiba yake” alisema.

Alitoa mwito kwa wafanyabiashara watumie fursa ya tofauti za hali ya hewa kwenye maeneo kuuza chakula sehemu zenye upungufu.

Aliwataka wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wakutane na wafanyabiashara wawashawishi wapeleke chakula kwenye maeneo yenye upungufu ili kuongeza vipato vyao.

Spika Ndugai Asema Mbowe ni Mtoro Bungeni

0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema utoro wa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe umekuwa ukisababisha nafasi ya maswali ya moja kwa moja kutoka upinzani kwenda kwa Waziri Mkuu kupotea kila mara.

Ameyasema hayo jana Novemba14,2019  bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu kutoka kwa Wabunge.

Ndugai alisema kwa mujibu wa utaratibu wa mabunge ya Jumuiya ya Madola Upinzani hupewa nafasi ya kwanza kuiuliza swali Serikali, lakini kwaa hapa nchini nafasi hiyo hupotea kila wakati kutokana na utoro wa kiongozi huyo.

“Waheshimiwa Wabunge niwataarifu tu kwamba utaratibu wetu wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu swali la kwanza kabisa huwa linakuwa hakiba kwa kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni, lakini kwa leo kama mnavyoona kiongozi huyo hayupo,” alisema Spika Ndugai.

Alisema Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani anaweza siku zote asiwepo bungeni lakini siku ya Alhamisi ni muhimu awepo kutokana Waziri Mkuu kuwapo na anatakiwa awe wa kwanza kuuliza swali.

“Huwa ni fursa pekee ambayo upinzani wanapata nafasi kwa hiyo kiongozi wa upinzani anaweza asiwepo bungeni siku yoyote lakini siku ya alhamisi ambayo ni ya maswali kwa Waziri Mkuu ni lazima awepo,” alisema Spika Ndugai

Alisema hata hivyo hana taarifa zozote za udhuru kutoka kwa kiongozi huyo (Mbowe) na wala hajui yuko wapi.

“Kwa hiyo hatujapata swali lile kwa kuwa kiongozi wa upinzani bungeni hayupo, uwe wapi, uwe wapi kama Spika hana taarifa zako ni mtoro tu kwa hiyo, ni mtoro na ndiyo maana leo unaona kwamba hiyo fursa ambayo imewekwa kwenye kanuni haijaweza kutekelezwa.

“Na ndio maana mnaona kwamba nafasi inapotea potea sababu ya utoro,”alisema Spika Ndugai.

Nafasi Mpya 16 za Kazi Benki ya CRDB | Deadline ni November 21, 2019

0
0
Background
CRDB Bank Plc is an African bank and a leading Financial Services Provider in Tanzania with current presence in Tanzania and Burundi, East Africa. The Bank was established in 1996 and was listed on The Dar Es Salaam Stock exchange (DSE) in June 2009.
 
Over the years, CRDB Bank has grown to become the most innovative and preferred financial services partner in the region. Supported by a robust portfolio and uniquely tailored products, CRDB Bank remains the most responsive bank in the region.

CAREER OPPORTUNITIES
We are a collection of individuals who believe in excellence. We are always on the look out for fresh talent and we hiring people who have the drive to succeed and the will to implement the discipline required to succeed. We focus on nurturing our team and providing our team with an environment that is conductive to creative thought.

==>>Bonyeza Tangazo husika la Kazi hapo chini kupata maelekezo zaidi na namna ya kutuma Maombi
 
TITLE                                                           |  Deadline
 ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   

1. Contact Center Agent (5 Positions)    | 19th, November 2019


3. Internal Audit (5 Posts) |  20th, November 2019 
4. Department of Human Resources (5 Posts) | 21st , November 2019 
  1.   Manager; Wellness, Diversity Inclusion & Empowerment
  2.     Senior Specialist; Labour & Trade Union Relations
  3.     Manager; Learning & Development
  4.  Learning & Development Partner- Quality Assurance
  5.     Learning & Development Specialist
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   
 
Kwa Nafasi Zingine Kama Hizi <<INGIA HAPA>>

    Mahakama Yaamuru Wabunge wanne wa CHADEMA (Ester Bulaya, Halima Mdee, Peter Msigwa, na John Heche) wakamatwe

    0
    0
    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru wabunge wanne wa CHADEMA, Ester Bulaya, Halima Mdee, Peter Msigwa, na John Heche wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo kwa kukiuka masharti ya dhamana. 

    Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya wabunge hao kutokuwepo mahakamani bila taarifa yoyote. Hata wadhamini wao pia hawakuwepo.

    Pia, Hakimu Simba ametoa hati ya wito wa wadhamini wa wabunge hao kujua sababu za kutowapeleka washtakiwa mahakamani.

    Kabla ya kutoa amri hizo, Hakimu Simba amesema leo kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa, washtakiwa wengine waliwahi lakini wabunge hao wanne hadi saa 4:05 asubuhi walikuwa hawajafika mahakamani bila sababu za msingi.

    Baada ya Hakimu Simba kueleza hayo wakili wa upande wa utetezi, Faraji Mangula aliyewawakilisha mawakili Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya ameieleza mahakama hiyo kuwa ana taarifa za Bulaya.

    Kauli ya Mangula ilipingwa na Hakimu Simba aliyebainisha kuwa anayepaswa kuzungumza kuhusu washtakiwa kutofika mahakamani ni wadhamini si wakili.

    Kwa pamoja wanakabiliwa na  mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kuhamasisha hisia za chuki.

    Msanii Beka Flavour amtungia wimbo Rais Magufuli | Hapa Kazi Tu

    0
    0
    Msanii wa Bongo Fleva, Beka Flavour ametunga wimbo maalum kwa ajili ya Rais John Magufuli na Chama chake cha CCM kwa ajili ya mambo mazuri aliyoyafanya tangu alipoingia Madarakani.

    LIVE: Kongamano La Sanaa La Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Arts Festival)

    0
    0
    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere linalofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaaam.

    Rais Magufuli apiga simu LIVE kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere likiendelea

    0
    0
    Rais Magufuli amempigia simu rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Ado Novemba na kumwambia anafuatilia shughuli hiyo ya kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere.

    Kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere linafanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaaam.

    "Nakusikiliza usiwe na wasiwasi na maagizo yangu niliyoyatoa Waziri Mkuu atayawasilisha hapo kwenu, ninawapenda sana, wasanii oyeeee," alisema Rais Magufuli.

    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika Kongamano hilo.

    Watumishi 44,800 Wa Kada Ya Afya Kuajiriwa Nchini Kwa Mwaka Wa Fedha 2019/20 Ili Kuboresha Huduma Za Afya

    0
    0
    Happiness Shayo-Dodoma
    Serikali imepanga kuajiri Watumishi 44,800 wa Kada ya Afya kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa watumishi wa kada hiyo na kuboresha huduma za afya nchini.

    Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika wakati akijibu swali la Mhe. Silafu Jumbe Maufi (Viti Maalum) aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuajiri watumishi wa kada ya afya ili kuboresha huduma za afya nchini.

    Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele cha ajira kwa kada ya afya na imekuwa ikitoa vibali vya ajira kwa kuzingatia ukomo wa bajeti kuu ya mshahara na vipaumbele vya mwajiri husika.

    Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameweka bayana kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali ilitoa vibali vya ajira 8,000/= kwa kada ya afya, lakini lengo halikufikiwa kwa sababu ya kuwepo kwa wataalamu wachache wa kada hiyo waliojitokeza kuajiriwa Serikalini.

    Ili kukabiliana na upungufu wa Watumishi wa kada ya afya, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwahamasisha wananchi katika majimbo yao kusoma masomo yatakayowawezesha kuajiriwa katika kada ya afya kwa lengo la kuwahudumia Watanzania.

    Jeshi la Polisi Latoa Angalizo Uchaguzi Serikali za Mitaa

    Nafasi Za Kazi Wakala Wa Usambazaji Maji Na Usafi Wa Mazingira Ruwasa | Fundi Bomba, Muhasibu Msaidizi

    TAKUKURU yakabidhiwa jalada la kufanyia uchunguzi upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia

    0
    0
    Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeikabidhi TAKUKURU  jalada la kulifanyia uchunguzi upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe amekabidhi jalada hilo kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo katika ofisi ndogo za Wizara jijiji Dar es Salaam.

    Hatua hiyo imekuja kutokana na jitihada za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kupambana na kuzuia rushwa pamoja na matumizi mabaya ya fedha za uma.

    Uchunguzi huo unafanyika baada ya kubainika upotevu/matumizi mabaya ya fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

    Kuhusu kiwango cha fedha kilichopotea Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe, amesema kitajulikana mara baada ya Takukuru kukamilisha uchunguzi huo wa jalada walililokabidhiwa.


    Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi November 16


    Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania

    0
    0
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Daniel Budeba kuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania – GST).

    Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Budeba umeanza tarehe 15 Novemba, 2019.

    Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Budeba alikuwa Mhadhiri wa Idara ya Uhandisi wa Kemikali na Madini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

    Taifa Stars Yaichapa 2-1 Equatorial Guinea michuano ya Kufuzu Afcon 2021.

    0
    0
    Taifa stars jana imeanza vema michuano ya Afcon kwa kuibuka kidedea mbele ya timu ya Equatorial Guinea kwa kupata ushindi wa mabao 2-1 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.

    Stars iliyo chini ya Etienne Ndayiragije iliyoanza kwa kasi kipindi cha kwanza haikuweza kutumia vema nafasi saba za kipindi cha kwanza na kuruhusu wapinzani wao Equatorial Guinea kuandika bao la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa Pedro Obiang akimtungua kipa mkongwe wa Tanzania, Juma Kaseja kwa shuti la mbali.

    Dakika tano baada ya kuanza kipindi cha pili, kocha Mrundi wa Tanzania, Etienne Ndayiragijje alianza na mabadiliko ya kuongeza nguvu katika safu ys ushambuliaji, akimtoa beki wa kulia Hassan Ramadhani Kessy na kumuingiza mshambuliaji, Ditram Nchimbi.
     
    Ni mabadiliko hayo yaliyoisaidia Taifa Stars kupata bao la kusawazisha likifungwa na kiungo mshambuliaji wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco, Simon Happygod Msuva dakika ya 68 akimalizia mpira uliookolewa na kipa baaada ya yeye mwenyewe kuunganisha kwa kichwa kona ya beki wa kushoto, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
     
    Taifa Stars iliongeza kasi ya mashambulizi baada ya bao hilo na juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 90  baada ya kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar Junior ‘Sure Boy’ kufunga bao la ushindi kwa shuti la mbali.
     
    Baada ya ushindi huo, Taifa Stars itasafiri kuwafuata Libya Uwanja wa Mustapha Ben Jannet mjini Monastir Jumanne ya Novemba 19 kwa mchezo wa pili wa kundi hilo.

    Waziri Mkuu: Ukuaji Wa Uchumi Kuendana Na Maendeleo Ya Watu

    0
    0
    WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2020/2021 umelenga kutekeleza maeneo ya kipaumbele ikiwa ni pamoja na kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu kwa kuweka mkazo katika upatikanaji wa huduma bora za jamii ikiwemo elimu, maji, afya, umeme na barabara.

    Ametaja maeneo mengine ni ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda kwa kuimarisha sekta ya kilimo kwa kujenga viwanda vitakavyotumia malighafi inayopatikana nchini, kuimarisha mashirika ya viwanda na kuanzisha na kuendeleza maeneo ya viwanda.

    Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Ijumaa, Novemba 15, 2019) wakati akiahirisha mkutano wa 17 wa Bunge la 11 jijini Dodoma. Amewasisitiza wananchi kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uzalendo ili kuiwezesha nchi kufikia malengo ya kujenga uchumi imara, unaojitegemea na wenye kuweza kuhimili ushindani.

    “Ujenzi wa mazingira wezeshi katika kuendeleza miundombinu itakayosaidia maendeleo ya biashara na uwekezaji nchini; kuhakikisha Watanzania wenye sifa stahiki wanapewa kipaumbele katika kandarasi au ajira zinazotokana na utekelezaji wa miradi ya kimkakati.”

    Amesema eneo lingine ni kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa Mpango. Baada ya tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/2017–2020/2021 kwa lengo la kuimarisha usimamizi na kuanza maandalizi ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/2022–2025/2026).

    Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kusisitiza Maafisa Masuuli wazingatie maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo na wahakikishe kamati za mipango na bajeti katika mafungu yao zinatekeleza majukumu yake ipasavyo. “Serikali kwa upande wake itaandaa mipango ya kisekta, kitaasisi na kimaeneo ambayo utekelezaji wake utachochea ujenzi wa uchumi wa viwanda, mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu.”

    “Katika udhibiti wa matumizi, naendelea kuwasisitiza Maafisa Masuuli wahakikishe wanatumia mfumo wa kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (Tanzania National Electronic Procurement System – TANePS). Hivyo, kila taasisi ya nunuzi ihakikishe inatumia mfumo huo kabla ya tarehe 31 Desemba 2019.

    Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa upande wake itaendelea kufanya maboresho makubwa katika sekta zinazogusa wananchi moja kwa moja na kuhakikisha kuwa matunda ya kukua kwa uchumi yanawafikia wananchi.

    “Watanzania wanatakiwa kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, katika kipindi hiki ambacho amekuwa akichukua hatua za makusudi kuhakikisha anajenga uchumi imara, kuboresha kipato na hali ya maisha ya wananchi.”

    Amesema matunda ya maboresho hayo yanayoendelea yanaonekana katika maeneo mengi. “Ndani ya miaka 26 kuanzia 1991/1992 hadi 2017/2018 kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi kimeweza kupungua kwa asilimia 13. Kadhalika, umaskini wa chakula nao umepungua kutoka asilimia 10 mwaka 2011/12 hadi asilimia 8.0 mwaka 2017/18.”  

    Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema katika kuelekea msimu wa kilimo wa 2019/2020 hali ya upatikanaji wa chakula nchini imeendelea kuimarika kutokana na uzalishaji mzuri wa mazao ya chakula kwa msimu 2018/2019, ambao ulifikia tani milioni 16.41 ikilinganishwa na mahitaji ya tani milioni 13.84 na kuiwezesha nchi kujitosheleza kwa mahitaji ya chakula kwa asilimia 119.

    Amesema pamoja na uzalishaji huo mzuri, kumekuwepo na mahitaji makubwa ya nafaka katika baadhi ya maeneo kutokana na hali ya mvua kutokuwa nzuri na kuwepo kwa dalili za kupanda bei za nafaka, Serikali imetoa maelekezo kwa Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa kuhakikisha inasambaza nafaka kwenye maeneo yenye upungufu ili kukabiliana na changamoto ya kupanda kwa bei.

    “Nitumie fursa hii kuwahimiza wakulima kutumia vizuri mvua za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mengi ya nchi yetu kwa kupanda mazao yanayostahimili ukame na ekolojia ya maeneo husika. Aidha, tukumbuke pia kujiwekea akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya matumizi ya kaya baada ya mavuno badala ya kuuza chakula chote.”

    Kuhusu upatikanaji wa pembejeo, Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha wakulima wanapata mbolea kwa wakati na bei nafuu, Serikali imetoa bei elekezi kwa mbolea aina ya DAP na UREA ambazo zipo katika Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja. “Hivyo, nitumie fursa hii kuzikumbusha mamlaka husika kuhakikisha kwamba bei elekezi zinafahamika kwa wakulima katika maeneo yote na wauzaji wanauza kwa kuzingatia bei hizo.”

    Pia, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu masoko ya mazao ya kilimo ambapo amesema licha ya kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini, kumekuwepo na changamoto kadhaa za upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa baadhi ya mazao ikiwemo la pamba, korosho na tumbaku.

    Amesema changamoto hizo zinachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko na mwenendo wa bei katika soko la dunia pamoja na uwezo mdogo wa kuchakata mazao hayo nchini, hivyo Serikali inaimarisha mifumo ya masoko ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, kuongeza tija na kupunguza gharama za uzalishaji kwa kuimarisha viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. 

    “Hatua hizi zitasaidia kuongeza thamani ya mazao na hivyo, kuimarisha bei. Kwa sasa tunaendelea na msimu wa mauzo wa zao la korosho baada ya mazao ya pamba na kahawa kumaliza. Minada ya korosho inaendelea vizuri. Viongozi wa Mikoa na Wilaya wasimamie malipo kwa wakulima na kuhakikisha wanalipwa kwa wakati.”

    Mtoto wa miezi mitano atelekezwa nyumba ya kulala wageni Njombe

    0
    0
    Na Amiri kilagalila-Njombe
    Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limefanikiwa kumpata mtoto wa miezi mitano aliyetelekezwa nyumba ya kulala wageni na kumuhifadhi chini ya uangalizi wa idara ya ustawi wa jamii.

    Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa ametoa taarifa hiyo kwa wanahabari mkoani humo akibainisha kuwa mtoto huyo amekutwa kwenye nyumba ya kulala wageni inayofahamika kama Shamba Guest House iliyopo mjini Njombe huku akiacha ujumbe wa kuelekea mwanza .

    “Shamba Guest amekutwa mtoto ambaye ana umri mdogo zaidi na ametelekezwa na mwanamke ambaye ni mama yake na ameacha ujumbe amesema anaenda eneo la Mwanza na huyu msaidizi amemuachia huyo mtoto,na pindi mambo yatakapo kuwa mazuru atamtumia hela”anasema Hamis Issa

    Kwa mujibu wa kamanda mwanamke huyo anafahamika kwa jina la Stella Mtweve na mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miezi mitano na nusu  ametambuliwa kwa jina la Kelvin Mmagoma .

    Jeshi la Polisi Lamshikilia Halima Mdee....Kufikishwa Mahakamani Jumatatu

    0
    0
    Mbunge wa Kawe Halima Mdee anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay, kufuatia agizo la Mahakama ya Kisutu la kukamatwa kwa wabunge wanne wa CHADEMA.

    Jeshi la Polisi Kinondoni limesema Mdee ameripoti mwenyewe kituoni hapo leo Novemba 16, 2019 na atafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.

    'Ni kweli yupo hapa kituoni tunamshikilia kama ambavyo Mahakama iliagiza na yeye amekuja mwenyewe kuripoti hapa, hivyo taratibu zote za kipolisi zinafanyika na Jumatatu atafikishwa mahakami', amesema Msaidizi wa RPC Kinondoni.

    Amri hiyo ya kukamatwa kwa wabunge hao Halima Mdee, Peter Msigwa, John Heche na Ester Bulaya, ilitolewa jana, Novemba 15, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Thomas Simba, ambapo alisema kuwa kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya upande wa mashtaka kumhoji Mbowe na baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake kutoka upande wa utetezi na ndipo ilipobainika washtakiwa hao wanne kutokuwepo mahakamani.
     
    Viewing all 45270 articles
    Browse latest View live




    Latest Images