Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi November 14


Waziri Kalemani Ateua Wajumbe wa Bodi TANESCO

$
0
0
WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameteua Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) yenye wajumbe wanane.

Dkt. Kalemani amefanya uteuzi Novemba 13, 2019, unatokana na Rais John Magufuli kumteua Dkt. Alexander Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa kipindi kingine cha pili.

Rais Magufuli alimteua Dkt. Kyaruzi Novemba 9, mwaka huu baada ya kuwa ameshika wadhifa huo kuanzia Mei 2016 hadi Mei 2019.

Dkt. Kalemani alisema wajumbe hao wapya watakaa madarakani kuanzia Novemba 13, 2019 hadi Novemba 12, 2022.

Aliwataja wajumbe hao kuwa ni Balozi Dk James Nzagi (alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO iliyomaliza muda wake) na Dkt. John Kihamba (Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Saam - DUCE).

Wengine ni Dk Lugano Wilson (Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uhandisi na Mkuu wa Teknolojia za Nishati - TIRDO), John Kulwa (Mkuu wa Idara ya Ukaguzi Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi Shirikishi - MUHAS) na Denis Munumbu (Mchunguzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - TAKUKURU).

Wengine ni Dk Gemma Modu (Mkurugenzi NACTE), Mathew Kirama (Mkurugenzi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma) na Gilay Shamika (Mjumbe katika bodi iliyopita).

Dkt. Kalemani alimpongeza Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua tena Dkt. Alexander Kyaruzi kuisimamia Bodi hiyo.

Alimtaka Mwenyekiti huyo kulitumikia Shirika kwa Kasi, weledi na nidhamu ili kuwahudumia watanzania kwa kuondoa kero ndogo na kuifanya heshima ya Watanzania kwa TANESCO iendelee.

"Ni matumaini yetu mtakuja na ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya katika kutekeleza azma ya Hapa Kazi Tu ili kulipa nguvu Shirika letu," alisema Dkt. Kalemani.

Kwa wajumbe wote, aliwataka wachape kazi ili kuhakikisha wadau wa Tanesco wanafaidi huduma nzuri na kuhakikisha Umeme unawafikia watanzania wote.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Dk Kyaruzi alimshukuru Rais Magufuli kwa heshima kubwa kwake kwa kumteua tena kulisimamia shirika hilo.

Alisema TANESCO miradi mingi ya kimkakati ukiwamo Mradi wa Kufua Umeme wa Maporomoko ya Maji wa Julius Nyerere wa megawati 2,115 na wa Rusumo mkoani Kagera.

Alisema miradi hiyo na mingine wataisimamia kikamilifu kwa kuweka mikono yao humo kwa kufuata miongozo mbalimbali wanayopewa na viongozi wao.

Miongoni mwa waliohudhuria ni kikao hicho ni, Naibu Waziri Nishati Mhe. Subira Mgalu, Katibu Mkuu Nishati Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Mhandisi Leonard Masanja Kamishina wa Umeme na Nishati Jadilifu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) Dkt. Alexander Kyaruzi, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt.Tito Mwinuka na Viongozi Wandamizi wa Wizara ya Nishati.

Lugola: Laini za Simu Ambazo Hazijasajiliwa Hazitazimwa

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema hakuna Mtanzania yeyote ambaye simu yake itazuiwa kutumika, kwa sababu hajasajili, kwa kigezo cha kutokuwa na Kitambulisho cha Taifa.

Kwa maana hiyo, ikifika Desemba 31 mwaka huu, ambayo ni mwisho wa kusajili laini za simu kama mtu hajapata kitambulisho cha taifa, laini yake ya simu haitazimwa na ataendelea kuitumia.

Aidha, Lugola amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA), kuhakikisha kwamba maofisa wa NIDA wilaya zote, wanapeleka namba za vitambulisho vijijini ; na si kutegemea kuzipata katika simu.

Lugola ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana Jumatano  Novemba 13, 2019 wakati akijibu mwongozo wa  mbunge wa Kavuu (CCM) Dk Pudensiana Kikwembe.
 
Katika mwongozo wake alisema uandikishaji wa vitambulisho vya taifa, umekuwa na changamoto maeneo ya vijijini. 

Alisema kuwa tatizo hilo limekuwa kubwa hasa vijijini hususani majimbo ya Kavuu na Mlele, ambako uandikishaji umekuwa ni shida.

“Kama inavyojulikana mwisho ni Desemba mwaka huu, naomba kujua kauli ya serikali nini kinafanyika ili waweze kupata vitambulisho,”alisema Pudenciana.

Akijibu mwongozo huo, Lugola aliwatoa hofu wasiwasi Watanzania kuwa utaratibu wa utambuzi, usajili na utoaji wa vitambulisho kwa wananchi, ambao wana sifa za kupata vitambulisho ni endelevu.

“Zoezi hili halina mwisho wala halina tarehe kwamba ikifika tarehe fulani kuna Mtanzania hajapata kitambulisho, basi huyo Mtanzania hatapata kitambulisho tena, Watanzania wasiwe na wasiwasi, hili ni zoezi endelevu na ndio maana kila mwaka kuna Watanzania ambao wanafikisha miaka 18.” alisema.

Akizungumzia suala la usajili wa laini kwa vidole, Lugola alisema: “Naomba niwatoe wasiwasi Watanzania wote kwamba maelekezo Rais John Magufuli hakuna Mtanzania ambaye simu yake itazuiwa kutumika eti kwa sababu hana kitambulisho cha taifa na hivyo hajasajili laini yake.”

Viwanda Vya Nguo, Glasi Kujengwa Simiyu, Watu 2000 Kupata Ajira

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mwekezaji kutoka  nchini Uturuki, Bw. Mustafa Albayram ameahidi kujenga viwanda viwili; kiwanda cha nguo na kiwanda cha kutengeneza glasi katika eneo la Isanga Mjini Bariadi Mkoani Simiyu mwaka 2020, mara baada ya kuridhishwa na mazingira ya uwekezaji  ambapo viwanda hivyo vinatarajia kuajiri wananchi  takribani 2000.

Albayram ameyasema hayo Novemba 13, 2019 mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali kwa lengo la kuangalia mazingira wezeshi  kwa  uwekezaji wa viwanda, ambaye alifuatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo kwa ziara ya siku mbili mkoani Simiyu.

Amesema endapo miundombinu yote muhimu hususani umeme itawekwa kwa wakati katika eneo hilo uwekezaji huo utaanza mara tu baada ya kukamilisha taratibu zote muhimu zinazohitajika ikiwa ni pamoja na usajili wa kampuni na kutafuta hati miliki ya ardhi.

“Tumeamua kuwekeza Simiyu, kila kitu kikienda sawa kiwanda cha nguo kinaweza kujengwa na kufanya kazi ndani ya miezi tisa mpaka mwaka mmoja, kiwanda cha glasi ni mwaka mmoja; baada ya usajili wa kampuni nitarudi tena Simiyu kukamilisha masuala ya hati miliki ya ardhi, sitaki kumuangusha Mhe. Balozi maana amefanya mengi kwa ajili yetu,” alisema Albayram.

Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo amesema mwekezaji ameridhishwa na eneo hilo na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa kutoa ardhi bure huku akibainisha kuwa ombi kubwa la mwekezaji ni kuwa na nishati ya kutosha kwa kuwa viwanda hivyo hususani kiwanda cha nguo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemhakikishia mwekezaji huyo upatikanaji wa mahitaji yote muhimu na kuahidi kushirikiana na taasisi zote za Serikali zinazohusika kuhakikisha anapata huduma zote kwa wakati na bila urasimu wowote.

Kuhusu suala la Umeme Mtaka amesema katika Bajeti ya mwaka 2019/2020 Wizara ya Nishati kupitia Shirika la umeme TANESCO imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupozea umeme(substation) ambacho kitajengwa karibu na eneo la uwekezaji huo

Mtaka ameongeza kuwa mtazamo wa mkoa wa Simiyu ni kuwa na viwanda vichache vinavyoajiri watu wengi badala ya kuwa na viwanda vingi vinavyoajiri watu wachache, huku akitoa wito kwa wakulima wa pamba kulima pamba kwa wingi kwa kuwa kiwanda cha nguo kitakuwa mkombozi wa kuongeza thamani ya zao la pamba na itauzwa kwa bei ya uhakika.

Naye Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa pamba nchini, Bw. Boaz Ogola amesema kujengwa kwa kiwanda cha nguo mkoani Simiyu kutasaidia wakulima wa pamba kupata soko la uhakika kuondoa changamoto ya bei ya pamba kwa kuwa kitapanua wigo wa soko la pamba, ambapo pamba inayotumika hapa ni nchini ni asilimia 20-25 ya pamba yote inayozalishwa.

MWISHO

Taarifa Kwa Umma: Mkutano Wa Taasisi Za Fedha Nchini Kufanyika Arusha Novemba 21 & 22, 2019

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kushirikiana na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) imeandaa mkutano wa taasisi za fedha nchini utakaofanyika jijini Arusha kujadili namna ya kuchochea maendeleo ya sekta ya fedha nchini.

Mkutano huo wa 19 wa taasisi za fedha unatarajiwa kufunguliwa na kiongozi wa ngazi ya kitaifa. Utahudhuriwa na washiriki wapatao 300 wakiwemo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, mawaziri, wakuu wa taasisi za fedha, wachumi wabobezi, wanataaluma na washirika mbalimbali wa maendeleo.

Mada zingine zitakazotolewa na kujadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na, ‘Matumizi ya teknolojia katika kukuza sekta ya fedha ili kuleta mapinduzi ya viwanda’; ‘Maeneo yenye fursa za uwekezaji katika sekta ya fedha’ na ‘Vigezo vinavyochangia kujenga tabia za ukopaji’.

Pia, washiriki wa mkutano huo watajadili kuhusu ‘Jinsi ya kukinga vihatarishi katika sekta ya fedha’; ‘Namna ya kuoanisha sekta ya fedha na maendeleo ya viwanda’; na ‘Tathmini ya mchango wa sekta ya benki katika huduma jumuishi za kifedha nchini’.

Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikiandaa mikutano ya taasisi za fedha kila baada ya miaka miwili tangu miaka ya 1980. 

Katika mikutano hii, viongozi wakuu wa taasisi za fedha, yakiwemo mabenki, mashirika ya bima, mifuko ya hifadhi za jamii na taasisi zingine za fedha wamekuwa wakikutana na kujadili masuala mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya fedha na uchumi wa nchi kwa ujumla. Mkutano wa 18 wa taasisi za fedha ulifanyika mwaka 2016 jijini Arusha na mada kuu katika mkutano huo ilikuwa ni ‘Jinsi sekta ya fedha inavyoweza kuifanya Tanzania inufaike kiuchumi kutokana na uwepo wake kijiografia’ (Harnessing Tanzania’s Geographical Advantage: The role of financial sector).

Chama cha National League for Democracy (NLD) Chajitoa Uchaguzi Serikali za Mitaa

$
0
0
Chama cha National League for Democracy (NLD) kimetangaza rasmi kujitoa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, huku kikimtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, ajiuzulu
 
Uamuzi wa chama hicho umeongeza idadi ya vyama vya siasa vya upinzani vilivyofikia uamuzi wa kujitoa kushiriki uchaguzi huo kufikia vinane. Vingine ni ACT-Wazalendo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chauma, NCCR-Mageuzi, UPDP, Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha Kijamii (CCK).

Kwa mujibu wa taarifa ya NLD iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Oscar Makaidi, kinamtaka Jafo kujiuzulu mara moja kwa madai kuwa ameshindwa kusimamia uchaguzi huo na kulitia taifa hasara.

“NLD hatuna imani naye licha ya kuagiza kuwa wagombea wote walioenguliwa, warudishwe, agizo ambalo hana mamlaka nalo kikanuni wala kisheria," Makaidi alisema.

Katika taarifa yake hiyo, NLD kimeamua kujitoa katika uchaguzi huo kwa kuwa una kasoro kubwa na haziwezi kurekebishika katika muda uliobaki.

Chama hicho kimemwomba Rais John Magufuli kusitisha uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 na mchakato wake wote uanze upya.

“Kwa kuwa Tamisemi imeshindwa kusimamia uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, tunataka usimamiwe na tume huru ya taifa ya uchaguzi,” alisema.

Makaidi pia alisema NLD haikubaliani na uamuzi wa Jafo kuwa amefuta uamuzi wote uliofanywa na wasimamizi wasaidizi kwa kuwa hana mamlaka hayo kikanuni na kisheria.

“Tunaamini kwamba kuendelea na uchaguzi chini ya usimamizi ule ule ni kuhalalisha upungufu wote uliojitokeza, mwingi ukiwa ni wa makusudi.

"Kuendelea na uchaguzi huu ni kuendelea kutegemea makosa mengine huko mbeleni hasa wakati wa upigaji kura na utangazwaji wa matokeo yake.

“Tumepokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wagombea wetu yanazothibitisha ukiukwaji na ubakwaji wa demokrasia kwa kiwango cha kutisha kiasi cha kuufanya uchaguzi huu kuwa kituko.

“Kwa ujumla, uchaguzi umepoteza sifa ya kuitwa uchaguzi, hivyo tumeazimia kujitoa," Makaidi alieleza zaidi katika taarifa yake hiyo.

Kiongozi huyo wa NLD aliwataka wanachama na wagombea wao wote nchi nzima kuwa watulivu na kutojihusisha kwa lolote kuhusiana na uchaguzi huo mpaka hapo watakapotaarifiwa vinginevyo.

Mbunge aliedai Wahudumu wa ATCL hawana mvuto aomba Radhi Bungeni

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Mhe. Husna Mwilima leo Bungeni ameomba radhi shirika la Ndege ATCL  na Watanzania waliokwazika na kauli yake aliyosema Bungeni tarehe 7/11/2019 kwa kusema Wahudumu wa Ndege ya ATCL (Air hostess) hawana mvuto.

“Nataka nitanie kidogo, hizi ndege zetu zinafanya kazi nzuri lakini mle ndani hebu tuangalie wahudumu tunaowaajiri, tuangalie wahudumu ambao hata akigeuka abiria wanasema kweli tuna Air Hostess, sijui mnatumia vigezo gani? Unakuta Air Hostess mfupi, hana mvuto,” Alitoa Kauli hiyo  Alhamisi Novemba 7, 2019 wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo bungeni jijini Dodoma.

Leo November 14, 2019 ameomba radhi bungeni na kusema;  “Nilitoa ile kauli lengo lilikuwa ni kuboresha shirika letu la Ndege la ATCL, kwa kuwa ile kauli yangu iliwaboa sana Watanzania hasa wanawake nitumie nafasi hii kuomba radhi Watanzania hasa wanawake wenzangu"

Scholarships for Tanzanian Students| Ufadhili wa Kusoma Nje ya Nchi (Unalipiwa Kila Kitu) | Deadline ni Mwakani 2020

$
0
0
📚 FURSA ZA UFADHILI  WA KUSOMA NJE YA NCHI

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

    🎓Tanzanian Scholarships


Kama wewe ni Mtanzania mwenye Ndoto ya Kusoma nje ya Nchi lakini hukuwa na uwezo, basi hii ni Nafasi yako. Kuna Nafasi Nyingi sana za Ufadhili zimetangazwa (Scholarships)


 Zote Hizo ni Full Funded( Unalipiwa kila Kitu) Japo kuna zingine utachangia kidogo 

_______________________ 

Bado hujachelewa, Deadline ni kuanzia Mwezi huu wa  kumi na moja  hadi Mwakani-2020
._______________________ 


1.Global Scholars Program- Clark University USA 

2.Hong Kong PhD Fellowship Scheme for International Students

3.Clarendon Fund Scholarships, University of Oxford, UK

4.Holland Scholarship for Non EEA International Students

5.Justus & Louise van Effen Excellence Scholarships in Netherlands

6.Oxford Pershing Square Graduate Scholarships in UK

7.Emile-Boutmy Scholarship in France for Non EU Students

8.Karen McKellin International Leader of Tomorrow Award, University of British Columbia

9.Weidenfeld-Hoffman Scholarships and Leadership Program

10.Radboud Scholarship Programme | Netherlands

11.Global Minds Doctoral Scholarships Programme at KU Leuven

12.Chalmers IPOET Scholarships for International Students

13.ETH Zurich Excellence Masters Scholarships

14.Maastricht University Holland High Potential Scholarships for International Students

15.Uppsala University Global Scholarships

16.University of Twente Scholarships (UTS)

Bofya hapo chini kujua zaidi
👇👇👇👇👇👇👇👇


http://ajirazote.com/scholarship/

Msanii Rosa Ree afungiwa na BASATA kwa miezi 6

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limemfungia msanii wa Bongofleva nchini Tanzania, Rozaree kutojihusisha na muziki kwa miezi 6.

Hii ni kutokana na video ya wimbo wa Vitamin U aliyoshirikishwa na msanii Timmy Tdat wa Kenya kutokuwa na maadili na tayari video hiyo imeondolewa kwenye mtandao wa YouTube.

Jinsi ya Kukata Rufaa Kama Hujapata Mkopo wa Bodi Ya Mikopo Ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu au Umepewa Kiasi Ambacho Hujaridhika Nacho

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefungua dirisha la kukata rufaa kwa wanafunzi ambao hadi sasa hawajapata mkopo au hawajaridhika na kiwango cha mkopo walichopangiwa katika mwaka wa masomo wa 2019/2020.
 
Dirisha liko wazi kuanzia Novemba 13 had 23, 2019.

Benki Ya Maendeleo Ya Afrika Kusaidia Ujenzi Wa Miradi Ya Nishati Tanzania

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Johannesburg
BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kuendelea kuisadia Tanzania kutekeleza miradi yake mikubwa ya kimkakati hususan miundombinu ya Nishati na Barabara kwa kuendelea kuipatia mikopo yenye masharti nafuu ili kuharakisha maendeleo ya nchi.

Ahadi hiyo imetolewa Mjini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini na Kaimu Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayesimamia Miundombinu ya nishati, Bw. Wale Shonibare alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, kando ya Kongamano la Pili la Jukwaa la Uwekezaji Afrika lililoandaliwa na Benki hiyo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao, Dkt. Mpango amesema kuwa ameiomba Benki hiyo kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kipaumbele inayojengwa na Serikali hususan katika Sekta za nishati, barabara, uongezaji thamani wa mazao ya kilimo, elimu na maji.

Dkt. Mpango ameitaja miradi iliyowasilishwa kwa kiongozi huyo kuwa ni mradi wa kuzalisha umeme wa Ruhudji (MW 358), mradi wa umeme wa Rumakali (MW 222) mradi wa umeme wa mto Malagarasi (MW 44.5), Mradi wa kuzalisha umeme wa Kakono (MW 87) na miradi mingine ambayo itajadiliwa na Bodi ya Benki hiyo itakayokutana mwishoni mwaka huu.

Amesema kuwa miradi hiyo mikubwa itakayoiwezesha nchi kuwa na umeme wa kutosha ni muhimu kwani itasaidia kufanikisha agenda ya Seikali ya kuwa na uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

“Tumewakaribisha waje Tanzania kwa ajili ya mazungumzo na kujionea namna miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vingine kama umeme jua na ule unaozalishwa kwa njia ya upepo kama ilivyo katika maeneo mengine ya Afrika hususan Kusini mwa Jangwa la Sahara” alisisitiza Dkt. Mpango

Amesema kuimarika kwa Sekta ya nishati nchini kutaleta manufaa makubwa ikiwemo kuziwezesha biadhaa za kilimo kama vile pamba kuongezewa thamani kutokana na kuwepo kwa umeme wa uhakika wa kuendesha viwanda.

Kwa upande wake Kaimu Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw. Wale Shonibare, amesema kuwa Benki yake iko tayari kuisaidia Tanzania ili ifikie mapinduzi makubwa ya miundombinu ya nishati kutokana na umuhimu wake katika kuendesha uchumi.

Alisema nishati ni jambo muhimu ili nchi iweze kufikia mapinduzi ya viwanda na aliahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha Benki yake inachangia juhudi za serikali za kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme, kujenga njia za kusafirishia umeme na usambazaji wake kwa kulijengea uwezo Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO)

Mwisho

TRA Yafafanua Mabadiliko Ya Sheria Kwenye Viwango Vya Kodi

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi wa mabadiliko ya viwango vya kodi kama vilivyoainishwa na Sheria ya Fedha ya mwaka 2019 ambapo mabadiliko hayo yamegusa Sheria za Kodi ya Mapato, Ongezeko la Thamani (VAT), Usajili wa Vyombo vya Moto pamoja na Usalama Barabarani. 

Akizungumza wakati wa Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani Morogoro katika Wilaya ya Mvomero, Afisa Msimamizi wa Kodi Mkuu wa TRA, Julius Mjenga amesema kuwa, mabadiliko katika sheria ya kodi ya mapato, jedwali la viwango vya kodi kwa wafanyabiashara wadogo wakazi, vimepunguzwa kutoka sh. 150,000 hadi kufikia sh. 100,000, kwa wale wenye mzunguko wa mauzo yanayozidi sh. milioni nne hadi milioni 7 kwa mwaka.

“Kwa wafanyabiashara wenye mauzo kati ya sh. milioni saba hadi sh. milioni 11, viwango vya kodi vimepunguzwa hadi kufikia sh. 250,000 kutoka sh. 318,000 iliyokuwepo hapo awali,” alisema Mjenga.

Pia, kwa wafanyabiashara wenye mauzo kati ya sh. milioni 11 hadi sh. milioni 14, viwango vya kodi vimepunguzwa hadi kufikia sh. 450,000 kutoka sh. 546,000.

“Lengo la kupunguza viwango hivi ni kukuza ridhaa ya kulipa kodi kwa hiari na kuongeza Mapato ya Serikali,” alifafanua Mjenga.

Kwa upande wa sheria ya usajili na uhamishaji wa umiliki wa vyombo ya moto, Mjenga ameeleza kuwa, ada ya kupata nakala ya kadi ya gari ni sh. 50,000, pikipiki ya magurudumu matatu (bajaji) sh.30,000 na pikipiki ni sh. 20,000 badala ya sh. 10,000 iliyokuwa ikitozwa kwa vyombo vya aina hiyo kabla ya tarehe 1 Julai, 2019.

Aidha, akizungumzia juu ya mabadiliko ya viwango vya leseni za udereva chini ya sheria ya usalama barabarani, Mjenga amesema kuwa, leseni ya udereva inalipiwa sh. 70,000 kila baada ya miaka mitano ambapo kabla ya mabadiliko ilikuwa inalipiwa sh. 40,000 kila baada ya miaka mitatu.

“Mabadiliko haya kwa ujumla wake yamelenga kuongeza fursa kwa walipakodi na wananchi kwa ujumla kuongeza ufanisi katika biashara zao na hatimaye kuongeza mapato ya Serikali. Hivyo, natoa rai kwa walipakodi wote kutumia fursa hii adhimu kwa maendeleo ya taifa letu,” alieleza Mjenga.

Wiki ya elimu kwa mlipakodi katika Mikoa ya Morogoro na Pwani itamalizika tarehe 17 Novemba, 2019 ambapo shughuli zinazofanyika ni pamoja na usajili wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), kupokea mrejesho, kusikiliza kero na kujibu maswali yanayoulizwa na wafanyabiashara pamoja na wananchi kwa ujumla.

Simbachawene Afuta Leseni Za Kampuni Zilizofanya Udanganyifu

$
0
0
Na Lulu Mussa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene ameagiza waliobainika kusafirisha vyuma chakavu ambavyo ni miundombinu ya majitaka na maji safi wachunguzwe kujua walikovitoa ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Pia ametahadharisha kuwa yeyote atakayekutwa amebeba, kuhifadhi, kuuza au kusafirisha vyuma chakavu bila kibali, atakuwa ametenda kosa la kisheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Simbachawene ametoa agizo hilo jana ofisini kwake jijini Dodoma ambapo ameagiza Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuichukulia hatua Kampuni ya Press Freight Tanzania Ltd (Wakala wa usafirishaji) kwa kusafirisha makontena ya chuma chakavu mali ya kampuni ya Eco Steel ambayo hayakuwa na kibali na ilisafirisha makontena hayo baada ya katazo alilotoa na kusisitiza hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Alisema kuwa katika makampuni nane yaliyokuwa yanamiliki makontena 147 yaliyokuwa Dar es Salaam yalipokaguliwa, makampuni manne 177 yalisema uongo kwani yaliweka vitu visivyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya kusafirishwa nje na havijulikani wamevitoa wapi.

“Kwa kampuni ya Eco steel Limited na Mahavir Implex Tanzania Limited ambazo zilikiuka agizo langu la kusafirisha taka hatarishi nje ya nchi,  naagiza taasisi zilizowapa leseni yaani Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira wazifutie leseni kwani wamekiuka sheria ya mazingira ya vibali vya kukusanya na kusafirisha taka hatarishi ndani ya nchi, vile vile kwa mamlaka niliyonayo sitatoa leseni kwa kampuni hizo kwa ajili ya kufanya biashara hiyo hata kile kinachoruhusiwa,” alisisitiza.

Hata hivyo alizitaka kampuni nne zilizodanganya ambazo zilikuwa na mapungufu madogo kwenda NEMC kwa ajili ya kufuata utaratibu kwa kulipa faini na kuanza upya mchakato wa kupata kibali cha Waziri cha kusafirisha nje ya nchi taka hatarishi.

Pia ameagiza kampuni manne yaliyokutwa na makosa kulipa faini ya sh. 460,000 kwa kila kontena lililokaguliwa na wataalamu pia mengine yenye makossa kulipa faini iliyopangwa kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004.

Aidha Waziri huyo alisisitiza kuwa biashara zote za ukusanyaji wa vyuma chakavu kwa mtu mmoja mmoja kwa ngazi za chini zitasimamiwa na Serikali za Mitaa huku akiagiza utekelezaji huo kuanza mara moja.

Itakumbukwa jumla ya makontena 142 yanayomilikiwa na makampuni tofauti yalifanyiwa ukaguzi na taarifa kuwasilishwa na Timu ya kitaifa ya ukaguzi Oktoba 16, 2019 na kuwa taarifa ilionesha uwepo wa ukiukwaji wa sheria na kanuni zinazosimamia na kudhibiti taka zenye madhara nchini na mkataba wa kimataifa wa Basel unaoruhusu udhibiti wa usafirishaji wa taka zenye madhara na taka nyingine baina ya nchi na nchi ambazo Tanzania ni mwanachama.

Wafanyabiashara Arusha Wapewa Siku Moja Kuhamishia Shughuli Zao Ndani Ya Soko

$
0
0
Na Tito Mselem Arusha,
Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa siku moja kwa Wafanyabiashara wote wa Madini Mkoani Arusha kuhamishia shughuli zao ndani ya Soko na watakao bainika kununua madini nje ya Soko watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni zao na kufikishwa Mahakamani. 

Hatua hiyo inafuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Biteko aliyoifanya Sokoni hapo Novemba 13, 2019 na kubaini changamoto za wanunuzi Wakubwa wa Madini kutolitumia Soko hilo na badala yake wameendelea kununua Madini nje ya Soko.

Katika zira yake hiyo, Waziri Biteko ameambatana na viongozi mbalimbaliwa Serikali pamoja na Wizara ya Madini akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula, Mkuu wa Jeshi la Polisi la Mkoa wa Arusha Jonathan Shanna na wengine.

Pia, Waziri Biteko amemtaka Mkandarasi anayeendelea na ujenzi katika Soko hilo ahakikishe anamalizia haraka ujenzi huo huku wafanyabiashara wakiwa wanaendelea na shughuli zao katika Soko hilo.   
 
Aidha, Waziri Biteko amemuagiza Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula kumuondoa Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Robert Erick kwa kushindwa kusimamia ipasavyo shughuli za Madini Mkoani humo.
 
Afisa Madini huyo anadaiwa kuwaachia wafanyabiashara wakubwa wa Madini Mkoani Arusha kufanya biashara ya Madini maofisini mwao tofauti na maelekezo ya Serikali iliyowataka wafanye biashara hiyo kwenye Masoko ya Madini ambapo ofisi nne tu ndizo zilikuwa wazi wakati Soko hilo lina ofisi za wafanyabiashara wakubwa 40 lakini kwa zaidi ya miezi minne hawajahamia katika ofisi hizo.
 
Alisema jukumu hilo la kusimamia kufanya biashara ndani ya Soko hilo na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wenye madini majumbani mwao ni jukumu la Afisa Madini, lakini kazi hiyo kwa sasa inafanywa na Waziri hatua ambayo haikubaliki kabisa, wakati wa kulindana umepitwa na wakati sio kwa Serikali hii iliyopo madarakani.
 
Waziri Biteko alisema kuwa, biashara ya Madini ya Tanzanite Mkoani Arusha imeshuka kwa asilimia kubwa na wanaofanya biashara hiyo wanajulikana  lakini hawachukuliwi hatua  na kwamba ofisi yake haiko tayari kuona ubadhilifu wa aina hiyo.
 
Pamoja na mambo mengine, Waziri Biteko amesema kuwa haoni sababu za msingi za wafanyabiashara wakubwa wa Madini Mkoani Arusha kushindwa kufanya biashara katika Soko la Madini lililoandaliwa na Serikali na badala yake wafanyabiashara hao wanafanya biashara katika ofisi zao.
 
Amewaeleza wafanyabiashara Wakubwa na Wadogo wa Madini Mkoani Arusha kuwa haitaji kupigiwa makofi kwani yeye anasimamia kanuni na sheria namba 20 ya Madini inayosema kuwa kila mfanyabiashara wa Madini awe Mdogo ama Mkubwa anapaswa kufanya biashara ndani ya Soko la Madini na sio vinginevyo.
 
Ameongeza kuwa, Wafanyabiashara wakubwa waliomba muda wa mwezi mmoja katika kufanya biashara ndani ya Soko hilo na Wizara iliongeza muda huo waliohitaji lakini hadi sasa ni zaidi ya miezi minne hakuna mfanyabiashara mkubwa aliyekuwa akifanya bishara katika Soko hilo na badala yake wanafanya biashara katika ofisi zao na wanamiliki kilo nyingi za madini kinyume cha utaratibu.
 
Waziri amesema anazo taarifa za uhakika baadhi ya wafanyabiashara wakubwa 97 wana ofisi za madini Arusha na Nairobi na wanafanya ujanja ujanja ili wafanye biashara hiyo kwa njia haramu na kuikosesha Serikali mapato hilo halikubaliki watachukuliwa hatua kali ikiwemo kufilisiwa mali zao na kufikishwa Mahakamani.
 
Akizungumzia suala la wafanyabishara Wadogo wa Madini amesema ofisi yake ina idadi ya wafanyabishara wenye leseni  263 lakini wanaofanya biashara hiyo mtaani ni zaidi ya watu 1,300 hali inaonesha wazi kuwa  zaidi ya wafanyabiashara 1037 wanafanya biashara bila ya kuwa na leseni na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Arusha analijuwa hilo lakini ameshindwa kusimamia majukumu yake ya kazi.
 
Pamoja na mambo mengine Waziri Biteko amesisitiza uaminifu katika sekta ya madini.

Idriss amuomba msamaha Rais Magufuli

$
0
0
Msanii wa vichekesho, Idris Sultan amemuomba radhi Rais Dk. John Magufuli kwa kitendo cha kufanyia ‘photoshop’picha yake akidai alifanya vile kwa dhumuni la kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa kwa kutumia sanaa ya uchekeshaji ambayo ndiyo anayoitumia kufanya kazi zake.

Idris ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Novemba 14, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa amepitia mafunzo ya jeshi na kwamba anauelewa uongozi mzima hivyo hawezi akawa mmoja kati ya watu wanaotaka kumkebehi rais.

“Katika hali ya ubinadamu tukiachana na sheria kama picha ile ilimkera na hajapenda kwa namna nilivyomtakia kheri katika hali ile sina budi kumuomba radhi kama babaangu na kiongozi wangu kwani sikuwa na nia mbaya bali ilikuwa kufurahisha watu lakini bahati mbaya safari hii imechukuliwa katika hali ya tofauti na watu wengi sana tumeshtushwa na tunaiacha sheria ichukue mkondo wake.

“Hiki kitu kimeathiri sana kazi yangu kwasababu sina simu yangu wala kompyuta yangu na hivyo ndio vitendea kazi vyangu vikubwa, watu wengi waliokuwa wakinitafuta kwaajili ya kufaya kazi imebidi zipelekwe mbele na hii imetokana na kutoeleweka nia yangu ni nini,” amesema Idris.

Ameongeza kuwa askari wamemuonesha ushirikiano wa kutosha kwenye jambo hilo ikilinganishwa na namna alivyotarajia akitolea mfano mitazamo tofauti ya watu wanaosema kuwa unapoenda kituo cha polisi kabla haujaanza kuzungumza ni lazima upigwe vibao kwanza lakini kwa upande wake haikuwa hivyo.

DC Sabaya Amtaka Godbless Lema Ajisalimishe Polisi

$
0
0
Polisi wilayani Hai  wamemkamata mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai (Chadema),   Helga Mchomvu kwa amri ya mkuu wa Wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya.

Sabaya amethibitisha kukamatwa kwa Mchomvu leo Alhamisi Novemba 14,2019 na kumtaka mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kujisalimisha akidai alifanikiwa kutoroka.

"Ndio tumemkamata mwenyekiti na watu wengine wawili lakini Lema nimeambiwa alifanikiwa kutoroka kupitia mlango wa nyuma na kutelekeza gari lake aina ya Toyota Landcruicer," alisema Sabaya.

Sabaya amedai kiini cha kuagiza viongozi hao wakamatwe ni kutokana na kile alichokiita kuendeleza njama zao za kuvuruga amani katika wilaya hiyo na kusababisha taharuki kwa wananchi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

"Kitendo cha mbunge Lema kutoka Arusha na kuja hapa Hai na kufanya vikao vya siri ni sawa na kuvuka mstari mwekundu na hili sisi kama Serikali hatuwezi kulivumilia. Namtaka Lema ajisalimishe mwenyewe polisi," amesisitiza Sabaya.

Waziri Mkuu: Vijiji Vyote Vitapelekewa Umeme

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema zoezi la usambazaji wa huduma ya nishati ya umeme linaloendelea kufanyika nchini hususan kwenye maeneo ya vijiji kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ni endelevu.

”Mheshimiwa Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inawaka umeme ifikapo 2021. Kazi hiyo inaendelea vizuri kwa usimamizi wa Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 14, 2019) katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza.

Mbunge huyo alitaka kupata kauli ya Serikali kuhusu vijiji ambavyo bado vitakuwa havijaunganishiwa umeme hadi 2021 ambao ni muda wa ukomo wa miradi ya REA.

Waziri Mkuu amesema hakuna kijiji kitakachokosa kuunganishiwa huduma hiyo na ili kuhakikisha inawafikia wananchi wote gharama za kuunganisha umeme vijijini zimepunguzwa na sasa ni sh 27,000 tu.

Amesema mbali na kupunguzwa kwa gharama za kuunganishiwa umeme, pia Serikali imefuta gharama za bidhaa nyingine za kupeleka umeme kwenye maeneo yao ikiwemo nguzo na nyaya.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutoa vibali vya ajira kwenye sekta za afya, elimu na kilimo na hivi sasa inatarajia kutoa vibali 16, 000 vya ajira za walimu na kisha itatoa vya watumishi wa afya.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo, Rashid  Shangazi, ambaye alihoji, nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wanapatikana watumishi wa kutosha kuwahudumia Watanzania.

Amesema mkakati wa kujenga miundombinu ya kutolea huduma mbalimbali nchini unakwenda sambamba na kuajiri wataalamu watakao wahudumia wananchi katika maeneo husika.

”Serikali imeanza kutoa vibali vya ajira katika sekta hizi mbili za afya na elimu, hata kwenye kilimo. Mwaka jana tuliajiri watumishi 6,000 na sasa tuna kibari ambacho kitatoka hivi karibuni cha watumishi 16,000 kwa upande wa sekondari na msingi.”

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,Kusafisha nyota, Mvuto wa Mwili na Biashara, ...Miguu kufa ganzi na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Waziri Mkuu Aonya Watakaovuruga Uchaguzi Serikali Za Mitaa

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa  amesema kuanzia tarehe 17 - 23 Novemba, 2019 litaanza zoezi la kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hivyo ametoa onyo kwa yeyote atakayevuruga zoezi hilo kuwa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Vikundi vya ulinzi wa jadi au vya ulinzi binafsi au vya mashabiki wa vyama vya siasa havitaruhusiwa kutumika kwenye maeneo ya mikutano ya kampeni au maeneo ya uchaguzi.”

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Alhamisi, Novemba 14, 2019)alipozindua Wiki ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasioambukiza sambamba na Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza

Waziri Mkuu amesema kuwa vyombo vya Ulinzi na Usalama hususan Jeshi la Polisi, Mgambo wenye sare na Maafisa wanaosimamia ulinzi vitatumika kuhakikisha kunakuwepo na utulivu wakati wa kampeni na uchaguzi.

Kadhalika,Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuendelea kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na Serikali imejipanga vya kutosha kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewataka wananchi kuchukua hatua stahiki za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ikiwa ni pamoja na kubadili tabia na mwenendo wao wa ulaji wa vyakula kwa kuongeza ulaji wa mbogamboga, matunda.

Waziri Mkuu amesema kila mtu ana wajibu wa kudhibiti matumizi ya vilevi kama sigara na pombe; kuhamasisha jamii kushiriki mazoezi au shughuli za nguvu; kuzingatia mlo unaofaa hasa kwa kuondoa au kupunguza chumvi, sukari na mafuta. “Tujipange kukabiliana na madhara mengine yatokanayo na uharibifu wa mazingira na tabianchi.”

Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa wajenge utamaduni wa kufanya mazoezi angalau dakika 30 mara tatu kwa wiki. “Katika eneo hili, niweke msisitizo kwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendeleza utaratibu wa mazoezi uliozinduliwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan.

“Tuendelee kuhamasisha kuanzisha na kujiunga kwenye vikundi vya mazoezi ya pamoja ambavyo husaidia sana kuleta hamasa ya kufanya mazoezi. Tutumie vikundi vya joggingvilivyopo kwenye kata na mitaa au vijiji vyetu ili kupata mwendelezo wa jitihada zao.

Amesema Halmashauri zote zihakikishe zinatenga na kuyaendeleza maeneo ya wazi katika kila kata au mitaa ili pamoja na shughuli nyingine wananchi pia watumie maeneo hayo kwa ajili ya kufanya mazoezi.

“Kwa upande wa wanafunzi kuanzia sasa kabla ya kuingia darasani wawe wanakimbia mchaka mchaka ili waweze kujiimarisha kiafya jambo ambalo litawaepusha na magonjwa yasiyoambukiza.”

Amesema magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa tishio kwenye jamii na ulimwenguni kote, takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka 2016 zinaonesha kuwa magonjwa hayo yanachangia zaidi ya vifo milioni 41, sawa na asilimia 71 ya vifo vyote milioni 57 vilivyotokea mwaka 2016.

“Taarifa za mwaka 2013 za Shirika la Maendeleo Duniani (UNDP) zinaonesha kuwa, pamoja na changamoto hizo za kiafya, magonjwa yasiyoambukiza yanaathiri sana nyanja nyingine za maisha. Inakadiriwa kuwa katika kipindi cha miaka 20, kuanzia mwaka 2013 gharama zitokanazo na magonjwa haya zitafikia Dola za Marekani trilioni 47.”

Waziri Mkuu amesema fedha hizo zingeweza kutumika kupunguza umaskini kwa watu bilioni 2.5 kwa kipindi cha miaka 50. Kwa nchi za uchumi wa kati na chini, magonjwa hayo yatagharimu mataifa hayo Dola za Marekani, trilioni saba katika kipindi cha 2011 hadi 2025.

Amesema gharama hizo zinatokana na kuongezeka kwa gharama za huduma za matibabu na upotevu wa nguvukazi unaosababishwa na maradhi hayo, mfano, makadirio yanaonesha kuwa gharama za huduma kwa magonjwa yasiyoambukiza itafikia asilimia 75 ya mzigo wote wa bajeti ya afya. Ugonjwa wa kisukari pekee utagharimu zaidi ya Dola za Marekani bilioni 465 sawa na asilimia 11 ya bajeti yote ya afya duniani.

Awali,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema magonjwa yasiyoambukiza yanajumuisha magonjwa ambayo hayawezi kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Aliyataja magonjwa hayo kuwa ni pumu, shinikizo la juu la damu, kisukari, saratani, siko seli, magonjwa ya akili, ajali, magonjwa mengi ya macho, kinywa, masikio, pua na koo. “Magonjwa haya yamekuwa yakiongezeka duniani kote na kuathiri nyanja zote za kimaisha.”

Waziri Ummy alisema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita Tanzania ilishuhudia ongezeko la idadi ya watu waliopatiwa huduma za magonjwa yasiyoambukiza kutoka wagonjwa milioni 3.4 kwaka 2016 hadi wagonjwa milioni 4.2 mwaka 2018, ilkiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 24.

Kwa upande wao, wadau wa masuala ya afya wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuongeza kiwango cha bajeti ya dawa kutoka sh. bilioni 31 hadi sh. bilioni 270.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

New Job Vacancies at MBULU District Council | Nafasi za kazi Watendaji wa Vijiji

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images