Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Jaji Mkuu wa Tanzania Atoa Neno Mimba Za Utotoni Rukwa......Aishauri Serikali Kuwatathmini Wapelelezi Na Waendesha Mashitaka

$
0
0
Na Lydia Churi-Mahakama Sumbawanga
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameishauri Serikali kufanya tathmini ya kazi inayofanywa na wapelelezi pamoja na waendesha mashitaka katika kesi iwapo wanatekeleza wajibu wao ipasavyo. 

Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joachim Wangabo alipomtembelea ofisini kwake akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo, Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Tanzania inakabiliwa na changamoto ya kesi kutomalizika kwa wakati na wakati mwingine haki kutotendeka kutokana na wapelelezi pamoja na waendesha mashitaka kutotekeleza wajibu wao ipasavyo.

Aidha Jaji Mkuu ameishauri Serikali kuwabana wapelelezi na waendesha mashitaka ili wawe wanajiandaa vizuri katika kesi mbalimbali.

Alisema endapo kutakuwa na maandalizi hafifu ya hati ya mashitaka katika kesi huweza kusababisha upelelezi wa kesi hiyo kutofanyika inavyotakiwa na hivyo kupelekea wakati mwingine haki kutotendeka na kusababisha mfumo wa sheria kutoaminiwa na wananchi.

Alisema matumizi ya Tehama katika kesi yatarahisha na kusaidia haki kutendeka na kesi kumalizika kwa wakati huku akitolea mfano wa matumizi ya kipimo cha DNA kwenye kesi kubwa kama vile za mauaji na ubakaji. Alisisitiza umuhimu wa hivyo kuchukuliwa mapema kabla ya ushahidi haujapoa.

Akitolea mfano wa kesi kwenye Mahakama ya Rufani, Jaji Mkuu alisema wakati mwingine Majaji hukutana na changamoto ya maandalizi hafifu ya hati ya mashitaka kwa kuwa inakuwa haiendani na tukio lenyewe.

Alisema kutokana na kukua kwa sayansi na Teknolojia, hivi sasa wapelelezi hawana budi kuchukua maungamo ya kesi kwa njia ya picha video. “Upelelezi bado uko karne ya 16 wakati wahalifu wako karne ya 21”, alisema Jaji Mkuu. 

Kuhusu Mahakama kuanza kutoa hukumu kwa lugha ya Kiswahili, Jaji Mkuu amesema suala hilo ni muhimu na Mahakama italifanyia kazi. Aliongeza kuwa hivi sasa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kinatoa mafunzo kwa Mahakimu ya uandishi wa hukumu kwa lugha nyepesi na inayoeleweka zaidi.  

Awali akizungumza, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliiomba Mahakama kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha kesi  zinamalizika kwa wakati hususani zile zinazohusiana na mimba za utotoni kwa wananfunzi wa shule za msingi pamoja na Sekondari zilizopo kwenye mkoa wake.

Alisema tayari kesi 40 za makossa hayo zimefikishwa mahakamani lakini kati ya hizo ni kesi tatu tu ambazo zimesikilizwa na kutolewa maamuzi. Alisema katika kipindi cha mwaka moja kanzia Julai 2018 mpaka Oktoba 2019 katika mkoa wake kuna jumla ya wanafunzi 294 waliopata mimba wakiwemo 209 wa shule za sekondari na 85 wa shule za msingi.  

Naye Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Mhe. Halfan Haule aliiomba Mahakama kuangalia uwezekano wa kuanza kutoa hukumu kwa lugha ya kishwahili hasa kwenye ngazi ya Mahakama za wilaya ili kuwawezesha wananchi kuzielewa kwa urahisi.

Alisema hivi sasa wananchi walio wengi hutumia muda mwingi kuzunguka kwenye ofisi mbalimbali za wanansheria ili kupewa tafsiri za hukumu zao hatua inayowafanya kuchelewa kupata haki ikiwemo kuchelewa muda wa kukata rufaa endapo wanakuwa hawajaridhishwa na hukumu zilizotolewa.   

Jaji Mkuu ameanza ziara ya kikazi Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga ambapo awali alikagua miradi ya ujenzi katika mkoa wa Songwe pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji ya Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga. Jaji Mkuu anaendelea na ziara kukagua shughuli za Mahakama katika wilaya za Nkasi na Kalambo.

Serikali Yapiga Hatua Kubwa Urejeshwaji Wa Kodi Ya Ongezekola Thamani

$
0
0
Na. Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imefanikiwa kuwarejeshea wafanyabiashara na wawekezaji Kodi ya Ongezeko la Thamani-VAT baada ya uhakiki wa madai yao kwa lengo la kuimarisha kipato cha mtu mmoja mmoja na uwekezaji nchini.

Hayo yamesemwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Khadija Nassir Ali, aliyetaka kujua namna Serikali ilivyojipanga kurejesha Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa wawekezaji ili kuimarisha uwekezaji.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, Serikali imelipa zaidi ya asilimia 90 ya VAT kwa watu waliokuwa wakidai Serikali baada ya kufanyika kwa uhakiki wa madai hayo, uhakiki unaendelea kwa asilimia kumi iliyobaki ili kujiridhisha kabla ya kufanya malipo.

“Tulikua na changamoto kubwa ya udanganyifu kwenye eneo la urejeshwaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani, hivyo Serikali ilianza mkakati wa kujiridhisha na kila muamala unaoletwa ili kuweza kuirejesha kwa wazalishaji, wanunuzi pamoja na viwanda vilivyopo nchini”, alieleza Dkt. Kijaji.

Aidha, akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni, aliyetaka kujua maana ya dhana ya ukuaji wa uchumi kwa kuoanisha na Maisha ya wananchi, Dkt. Kijaji alisema kuwa dhana hiyo inatafsiriwa kwa kuangalia upatikanaji, ubora na gharama ya huduma za jamii zinazotolewa na Serikali.

Alisema baadhi ya huduma hizo ni pamoja na elimu, afya, maji, umeme na miundombinu ya usafiri na usafirishaji inayosaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa na na matengenezo ya vyombo vya usafiri.

Dhana nyingine ya kutafsiri ukuaji wa uchumi na maisha ya wananchi ni ushiriki wa wananchi wenyewe katika shughuli za kiuchumi hivyo ukuaji wa uchumi ni matokeo ya ushiriki wa wananchi katika uzalishaji mali na huduma.

Alisema kuwa wananchi wanaoshiriki katika shughuli za uchumi wananufaika kwa tafsiri ya dhana ya ukuaji wa uchumi kupitia huduma za kijamii zinazotolewa na Serikali pamoja na matokeo ya shughuli zinazofanywa na mwananchi.

Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kufanya jitihada za kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara ili kila mtanzania aweze kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika uzalishaji na huduma.

Naibu Waziri Dkt. Kijaji alisema kuwa uwekezaji katika viwanda utaongeza ajira na uzalishaji katika Sekta ya kilimo kwa kuwa Sekta hiyo inaajiri idadi kubwa ya watu nchini.

Mwisho

Nafasi Mpya Za Kazi 271 The Karanga Leather Industries Company, Moshi | Deadline: 25th November, 2019

$
0
0
POSITION: Machine Operator (250 Positions)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Form Four certificate at least with three D pass with a Diploma or certificate in shoes or leather articles making, VETA certificate or other related certificate, Diploma in Mechanical/electrical engineering or any other related education with working experience in shoes, textile or other leather articles making industry is added advantage.


POSITION: Cost Accountant (1 Position)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Bachelor Degree in Accounting, Finance or related field from a recognized Higher Learning Institutions plus CPA (T) certificate with at least 5 years’ experience in Cost Accounting in manufacturing industries; Knowledge of IFRS and IPSAS will be an added advantage

POSITION: Assistant Procurement and Logistics Officer (1 Position)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Bachelor Degree or NTA level 8 in Materials Management or Procurement, Supplies Management or Procurement and Logistics Management or Supply Chain Management from a recognized Higher Learning Institutions. The candidate must be registered by the Procurement and Supplies Professional and Technician Board (PSPTB) as a graduate professional (GP) or a holder of CPSP with not less than two (2) years’ work experience in a relevant field.

POSITION: Quality Supervisor (3 Positions)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Bachelor Degree in science, Production and Operations Management with at least 3 years working experience as a Quality supervisor/manager in a manufacturing industry especially in tannery, sole, shoes and leather articles.

POSITION: Machine Technician – Electrical (2 Positions)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Diploma/advance Diploma in electrical Engineering with at least two years’ experience in the field of maintenance, troubleshooting/fault finding in a wide variety of electrical equipment.

POSITION: System Administrator (1 Position)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Bachelor Degree in Computer Science/Software Engineering or related IT discipline, with at least 3 years of working experience in complex system design, programming and systems software and support; excellent oral/written communication and documentation skills; able to work under pressure and tight deadlines.

POSITION: Financial Planning and Analyst (1 Position)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Bachelor Degree in Accounting, Finance, Economics or related field plus CPA (T) certificate with at least 5 years of working experience in Manufacturing Industries MBA degree will be added advantage.

POSITION: Quality Improvement and Assurance Supervisor (1 Position)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Bachelor Degree preferably in BSc Engineering, Physics, Chemistry, Biology, or Food Science with at least 3 years working experience as a Quality Improvement and Assurance Supervisor in a manufacturing industry

POSITION: Quality Control Operator (5 Positions)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Diploma Laboratory in Science or the equivalent with at least Oneyear experience in a similar job is recommended.
 

POSITION: Quality Manager (1 Position)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Bachelor Degree in Science with at least 5 years working experience as a Quality supervisor/manager in a reputable manufacturing firm.


POSITION: Factory Managers –Sole and Leather articles (1), Footwear (1)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Bachelor Degree or Advanced Diploma/Diploma in Engineering fields e.g. Leather, Textiles, Mechanical, Electrical, Chemical, Industrial, etc. or Equivalent Qualifications from a recognized institution with at least five years working experience in a Manufacturing environment with supervisory experience. Degree in Business administration or MBA will be added advantage.

POSITION: Machine Technician – Mechanics (2 Positions)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of FTC/Diploma/advance Diploma in Mechanical Engineering with at least two years working experience in manufacturing industries especially in textiles, shoes or other leather products industry

POSITION: Factory Supervisor (1 Position)
a) QUALIFICATION AND WORK EXPERIENCE
Holder of Bachelor Degree or Advanced Diploma, Diploma in Engineering fields e.g. Textile, Leather, Mechanical, Electrical, Chemical, Industrial, etc., or Equivalent Qualifications with at least two years working experience in shoes/leather articles making with some supervisory experience. Degree in Business administration or MBA will be added advantage


==>>Kwa Taarifa Zaidi na Namna ya Kutuma Maombi Ya Kazi <<INGIA HAPA>>

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano November 13

TRA Yakabidhi Vyeti Vya Utambulisho Wa Mlipa Kodi Wilayani Kibiti Mkoa Wa Pwani

$
0
0
NA RACHEL MKUNDAI, KIBITI
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka  wafanyabiashara kujisajili na kupata namba ya utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa kuwa inatolewa bure bila malipo yoyote.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu kwa Mlipakodi inayoendelea wilayani Kibiti katika mkoa wa Pwani, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi  Richard Kayombo amesema TRA inawakaribisha wafanyabiashara wote ambao hawajajisajili kufika maeneo maalumu yanayotoa huduma na elimu kwa mlipakodi katika wiki hii ili wasajiliwe na kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi waweze  kufanya biashara zao kwa Uhuru na kulipakodi stahiki bila usumbufu.

"Tunafanya wiki ya huduma na elimu kwa lengo la kusogeza huduma karibu na walipakodi na kuwatatulia changamoto zao zinazohusu ulipaji Kodi" amesema Kayombo.

Aidha, Kayombo ameongeza kuwa mbali na kutoa elimu kwa njia ya semina na matamasha maofisa wa TRA wanapita madukani kutoa elimu kwa wafanyabiasha na kuwasajili kupata namba ya utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ili kuongeza idadi ya walipakodi na kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari miongoni mwa watanzania.

Amesisitiza kwamba, TRA imejipanga kufanya wiki ya elimu kwa mikoa miwili miwili kwa mwezi na hivyo amewataka wafanyabiashara wa kutumia fursa hii kujisajili na kupata namba ya utambulisho wa mlipakodi na kuhakikisha cheti wanatundika katika maduka yao katika sehemu inayoonekana.

Hata hivyo, ameongeza kuwa pamoja na kuwa na wiki ya elimu lakini pia TRA imetenga siku ya Alhamis kila wiki kwa mameneja wa wilaya na mikoa nchini kote kuwasikiliza wafanyabiashara na kutatua changamoto zao ili kuchochea ari ya ulipaji kodi kwa hiari.

Wiki ya elimu kwa mlipakodi inafanyika katika mikoa ya Morogoro na Pwani kuanzia tarehe 11 hadi 17 Novemba, 2019 ambapo wananchi na wafanyabiashara watapata fursa ya kuelimishwa masuala ya ulipaji kodi

Huduma zinazotolewa katika wiki hii ni usajili wa wafanyabiashara na utoaji wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi, Ulipiaji wa kodi ya majengo, elimu ya kodi na kutatua changamoto mbalimbali za walipakodi ili kuongeza ulipaji kodi kwa hiari.

Evans Aveva, Kaburu, Hans Pope Kuanza Kujitetea Novemba 20

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imesema vigogo wa Klabu ya Simba akiwamo Rais wa zamani, Evans Aveva na wenzake wawili wanaokabiliwa na tuhuma za kughushi na matumizi mabaya ya madaraka, wataanza kujitetea Novemba 20, mwaka huu.

Kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, ambapo Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto, aliomba tarehe nyingine ya kusikilizwa.

Hata hivyo, Hakimu Simba alihoji kwanini kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa wakati ilipangwa kwa kusikilizwa?

Wakili Mitanto alidai tarehe iliyopita waliitaarifu mahakama kuwa wamekata rufani kupinga uamuzi wa mahakama hiyo kuwaona washtakiwa hawana kesi ya kujibu katika Mashtaka ya kutakatisha fedha, na kwamba wanaomba tarehe nyingine kusubiri uamuzi wa rufani.

Hakimu Simba alisema mahakama hiyo itapanga tarehe ya kusikilizwa kwa utetezi na kama kutakuwa na masuala ya rufani waijulishe mahakama.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba alisema itaanza kusikilizwa utetezi wa washtakiwa Novemba 20, mwaka huu.

Mbali na Aveva, washitakiwa wengine ni aliyekuwa makamu wa rais, Geofrey Nyange maarufu Kaburu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hansppope wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashtaka saba na kuondolewa mashtaka mawili ya utakatishaji fedha.

Upande wa utetezi Walalamika Kesi Ya Kutekwa Mo Dewji

$
0
0
Upande wa utetezi katika kesi ya kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu Mo, umeulalamikia upande wa Jamhuri kuchelewesha upelelezi na kwamba mshtakiwa anateseka mahabusu.

Mshtakiwa, dereva wa teksi Mousa Twaleb, anakabiliwa na kesi ya kumteka mfanyabiashara huyo pamoja na wenzake wanne ambao bado hawajakamatwa na kufikishwa mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi.

Wakili wa utetezi, Maufudhu Mbagwa, alidai kuwa Septemba 16, mwaka huu, upande wa Jamhuri uliomba hati za kukamatwa kwa watuhumiwa wengine ambao hawajakamatwa.

Alidai kuwa mwaka mmoja sasa umeshapita tangu mteja wake awe mahabusu na hawajaambiwa hatua ya upelelezi waliyofikia.

Hakimu alihoji sababu ya upande wa Jamhuri kuharakisha kumfikisha mahakamani mshtakiwa wakati washtakiwa wengine bado hawajakamatwa.

Alisema kama inawezekana upande wa Jamhuri unaweza kuendelea na mashtaka dhidi ya mshtakiwa huyo kwa upande wake, ufanye hivyo kuliko kuleta hati ya mashtaka ya watu wengi ambao hawajulikani watakamatwa lini.

Wakili wa Serikali, Glory Mwenda, alidai kuwa anaomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itatajwa Novemba 25, mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu.

Watuhumiwa wengine ambao upande wa mashtaka inawatafuta ni raia wanne wa Msumbiji na mmoja wa Afrika Kusini wanaodaiwa kumteka mfanyabiashara huyo.

Washtakiwa hao ambao hawajakamatwa ni Phila Tshabalala raia wa Afrika Kusini, Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issac Tomo na Zacarious Junior wote raia wa Msumbiji.

Serikali Yaanza Mchakato Wa Kununua Ndege Ya Mizigo

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema serikali imeshaanza mazungumzo ya namna ya kupata ndege ya mizigo kwaajili ya kubeba mazao ya mbogamboja kuyepaleka nje ili kuwasaidia wakula.

Ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Novemba 13, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini aliyetaka kujua mkakati wa serikali katika kutafuta ufumbuzi wa masoko ya mazao ya mbogamboga.

“Jimboni Rombo tunalima sana maparachchi na yananunuliwa na wafanyabiashara walanguzi kutoka Kenya, kilimo hiki cha hot culture Kaskazini huko wakulima wanapata hasara kubwa, sasa katika mkakati wa kutafuta masoko ni kwanini tusiangalie uwezekano kama nchi kununua ndege ya mizigo itakayosaidia wakulima wetu nje ya nchi kwasababu mazao haya ya mbogamboga yanakwenda Nairobi na kusafirishwa na ndege za Kenya,” amehoji.

Akijibu hoja hiyo Waziri Kamwelwe amesema serikali imeshafanya mazungumzo juu ya suala hilo na kwamba wana mpango wa kuanza kukodisha ndege kwaajili ya kusafirisha mazao hayo na minofu ya samaki kutoka Mwanza.

“Tayari tuna miezi mitatu tulishaanza kujadiliana kuhusiana na jinsi ya kupata ndege ya mizigo kwaajili ya kubeba mazao ya hot culture Uwanja wa Ndege wa Songwe pamoja na minofu ya samaki kutoka Mwanza kwahiyo tutaanza na kukodi ndege kwasababu tuna changamoto ya mzigo wa kutoka Europe kuja huku lakini kutoka hapa kwenda kule mzigo upo,” amesema Kamwelwe.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema serikali imekuwa ikihamasisha wakulima na wadau wengine kuongeza uzalishaji wa zao la parachichi hususan aina ya hass, kutekeleza mkakati wa kuainisha maeneo yote yanayofaa kwa kilimo hicho nchini pamoja na kuongeza uzalishaji wa miche ya maparachichi aina ya hass na kuilinda ili isiharibiwe na aina nyingine za mapachichi.

Wanne Waliomuua RPC wa Mwanza Wahukumiwa Kunyongwa

$
0
0
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza imewahukumu kunyongwa hadi kufa washtakiwa wanne kati ya saba waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza (RPC), Liberatus Barlow.

Hukumu hiyo imetolewa jijini Mwanza jana  Jumanne Novemba 12, 2019 na Jaji Sirialus Matupa baada ya Mahakama kuridhika bila shaka yoyote na ushahidi uliowasilishwa na washtakiwa walitenda kosa hilo.

Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Muganyizi Michael, Magige Mwita, Abdallah Petro na Abdulrahaman Ismail.

Walioachiwa huru na Mahakama baada ya ushahidi kutowatia hatiani katika kesi hiyo ya mauaji namba 192/2014 ni Chacha Mwita, Buganizi Edward na Bhoke Marwa.

Kamanda Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi katika tukio lililotokea eneo la Kitangiri Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza saa 8:00 usiku wa kuamkia Oktoba 13, 2012.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mbolea nchini (TFC) Asimamishwa Kazi

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema Serikali imemsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mbolea nchini (TFC), pamoja na kumuagiza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya BAJUTA kuzirudisha haraka iwezekanavyo, fedha za umma kiasi cha Shilingi Bilioni 4.5 

Naibu Waziri Bashe ametoa kauli hiyo leo Bungeni Dodoma, wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Chunya, Victor Mwambalaswa, lililokuwa likihoji nini hatma ya mbolea na viuatilifu vya zao la korosho, ambavyo licha ya Serikali kutoa pesa ni mwaka sasa umepita mbolea na viuatilifu hivyo bado viko bandarini. 

Akijibu swali hilo Bashe amesema; “Ni kweli Serikali ilitoa pesa Bilioni 10 kwa ajili ya kuagiza viuatilifu hivyo na Serikali imemsimamisha Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TFC kama hatua ya awali kwa uzembe huu”.

 “Nitumie nafasi hii ndani ya Bunge hili kuagiza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bajuta kurudisha Bilioni 4.5 alizopewa na tumeongea na TPA wamekubali kutuondolea gharama zote na sasa tuko katika hatua za mwisho kuvitoa viuatilifu hivyo kabla havijaharibika ili tuweze kuwagawia wakulima” Bashe.

TRA: Wananchi Lipeni Kodi Ya Majengo, Viwango Vimepunguzwa

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Wito umetolewa kwa wananchi kulipa kodi ya majengo kwa kuwa viwango vilivyopangwa katika kodi hiyo ni rafiki na vinalipika kwa urahisi ukilinganisha na hapo awali.

Wito huo umetolewa na Afisa Kodi Mkuu, Julius Mjenga kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa Kampeni ya Usajili, Huduma na Elimu kwa Mlipakodi katika Kata ya Mlimba Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.

Mjenga amesema kuwa, sasa hivi viwango vya kulipia kodi ya majengo ni shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida, shilingi 50,000 kwa kila sakafu ya ghorofa katika Majiji, Miji na Manispaa na shilingi 20,000 kwa ghorofa zima katika Halmashauri za Wilaya.

“Sasa hivi viwango vimepunguzwa wale wenye nyumba za kawaida wanalipia shilingi 10,000 tu na wale wenye nyumba za ghorofa zilizopo kwenye manispaa, miji na majiji wanalipia shilingi 50,000 kwa kila sakafu wakati wale wenye nyumba za ghorofa zilizopo halmashauri ya wilaya wanalipia shilingi 20,000 kwa ghorofa zima,” alisema Mjenga.

Mjenga amefafanua kuwa katika majiji, manispaa na halmashauri za miji, iwapo kuna nyumba zaidi ya moja kwenye kiwanja kimoja, kila nyumba itatozwa shilingi 10,000 wakati katika halmashauri za wilaya, endapo kiwanja kimoja kina nyumba zaidi ya moja, nyumba yenye thamani ya juu ndio itakayohesabika na kutozwa shilingi 10,000.

Aidha, majengo yasiyotozwa kodi ya majengo ni pamoja na nyumba zilizoezekwa kwa nyasi na makuti, nyumba zilizojengwa kwa udongo (nyumba za tope) na majengo ya ibada kama vile misikiti na makanisa.

Julius Mjenga amewataja wazee wenye miaka 60 na kuendelea kuwa wamesamehewa kulipa kodi ya majengo kwa nyumba moja ambayo wanaishi na si vinginevyo na wazee hao wanapaswa kufika Ofisi za TRA kuomba kusamehewa kodi hiyo.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea na kampeni ya usajili, huduma na elimu kwa mlipakodi katika Mikoa ya Morogoro na Pwani na itamalizika tarehe 17 Novemba, 2019.

MWISHO

Benki Ya Biashara Na Maendeleo Mashariki Na Kusini Mwa Afrika Kusaidia Utekelezaji Miradi Ya Kimkakati Ya Tanzania

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Johannesburg
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini wa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 200 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mazungumzo ya viongozi hao yamefanyika katika Mji wa Sandton, Johannesburg nchini Afrika Kusini, kando ya Kongamano la Pili la Jukwaa la Uwekezaji Afrika lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB.

Dkt Mpango amesema kuwa Benki hiyo imekuwa mbia mzuri wa Tanzania ambapo mwaka huu pekee imetoa mkopo wa dola bilioni 1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na imeahidi kutoa kiasi kingine cha dola milioni 200 baada ya Bodi ya Benki hiyo kukutana mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu kwa ajili kuidhinisha mkopo huo

Alisema kuwa amemwalika Rais huyo wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Bw. Tadesse, kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania hivi karibuni ili kujionea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme wa Kilwa pamoja na miradi mingine ambayo Benki hiyo inaweza kutoa mkopo

Kwa upande wake, Rais wa TDB Bw. Admassu Tadesse amesifu uhusiano imara uliopo kati ya Benki yake na Serikali ya Tanzania na kuahidi kuwa Benki hiyo itahakikisha inashirikiana nayo kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya wananchi wake.

“Tumekuwa na mjadala mzuri na Mhesimiwa Dkt. Mpango na Benki yetu imekuwa mshirika mzuri wa maendeleo ya Tanzania katika kipindi cha miaka michache iliyopita kwenye yyanja za nishati ya umeme na miundombinu ya usafirishaji” alisema Bw. Tadesse

Alisema kuwa mwaka huu Benki yake kwa kushirikiana na washirika wake wengine ambao ni taasisi za kibenki imeongeza mtaji wa dola milioni 500 hatua iliyoijengea Benki yake uwezo wa kutoa mikopo zaidi ambapo mwakani itaipatia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati ya miundombinu itakayokuwa na umuhimu mkubwa si tu kwa Tanzania, bali pia kikanda.

Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) ilianzishwa mwaka 1985 ikiwa na mali zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.6 ambapo lengo lake kubwa ni kutoa mikopo inayochochea miradi inayochochea ukuaji wa biashara, ikiwemo miundombinu, utangamano wa kiuchumi na ushauri wa kibiashara kwa nchi wanachama.

Mwisho

Watu Sita wauawa kwa risasi Mtwara

$
0
0
Watu sita wameuawa katika kijiji cha Ngongo Wilaya ya Tandahimba mkoani  Mtwara na wengine saba kujeruhiwa katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana Jumanne Novemba 12, 2019.

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz amesema Watanzania sita walipigwa risasi na watu wanaodhaniwa kutoka nchi jirani ya Msumbiji wakati wakiwa visiwa vya mto Ruvuma wanakofanya shughuli za kilimo.
 
“Vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha wahalifu hao wanapatikana na sheria kali zitachukuliwa juu yao, niwasihi tu wananchi kuepuka kwenda nchi za watu bila kuwa na vibali,” amesema.

Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Leberatus Sabas, amesema kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ndio maana wahalifu wanafanya matukio hayo mipakani.

“Tusikubali hata siku moja wavuke mpaka waje huku ndani tupo bega kwa mbega na wananchi. Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vipo pamoja tutawasaka, tutawatia mbaroni na hatua kali zitachukuliwa.”

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) yabaini dawa bandia

$
0
0
NA EMMANUEL MBATILO
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) limefanya ukaguzi katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za Afya zikiwemo dawa na kugundua kuwepo kwa dawa bandia na kuzishikilia.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw.Akida Khea amesema kuwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019, baadhi ya dawa bandia zilizobainika na kutolewa taarifa ya kuwepo katika nchi za wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na dawa aina ya Gentrisone Cream 10gm toleo namba GNTRO X030,Augmentin 625mg tables toleo namba 786627 na kapsuli za Cold caps.

“Viwanda halisi vinavyotengeneza dawa hizi vilithibitisha kuwa dawa hizo hazikutengenezwa na viwanda huzika. Amesema Bw.Khea.

Aidha, Bw.Khea amesema kuwa kwa mujibu wa uchambuzi na uchunguzi uliofanywa na TMDA, matoleo ya dawa hizo husika yalithibitishwa kuwa ni bandia.

“Uchunguzi kupitia maabara ya TMDA kwa dawa ya Gentrisone cream 10gm toleo namba GNTRO XO30 ulionesha kuwa dawa hiyo haikuwa na viambato hai (active pharmaceutical ingrediets) vya dawa hiyo ambavyo ni Betamethasone Proprionate, Clotrimazole na Gentamycin sulfate”. Ameongeza Bw.Khea.

Hata hivyo Bw.Khea amesema kuwa katika operesheni ya ukaguzi katika Mikoa inayopakana na nchi za jirani ikiwemo mikoa ya Kigoma,Songwe,Kagera,Rukwa, Mbeya,Mara,Kilimanjaro, Arusha,Mwanza, Ruvuma,Mtwara na Tanga. Wakati mikoa mengine ni Dar es Salaam,Dodoma,Shinyanga,Geita,Singida ,Morogoro,Iringa, na Tabora

“Katika operesheni hii jumla ya maeneo 558 ikiwa ni famasi 209,maduka ya Dawa Muhimu 263, Vituo vya kutolea huduma za afya 27,Maduka ya Vifaa Tiba 21 na Vituo vya dawa asili na tiba mbadala 38 katika”. Ameongeza Bw.Khea.

Kwa upande wake Mratibu wa Polisi toka CID HQ, Bi. Alekunda Urio amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga kuzifuatilia kesi hizo kwa  karbu kesi zilizofungunguliwa na TMDA na kuhakikisha watuhumiwa wanachukuliwa hatua za kisheria na TMDA kwa wale wote ambao wamekutwa wakimiliki dawa bandia.

Wizara Ya Kilimo Yaahidi Kushirikiana Na Wanajeshi Wastaafu Kuimarisha Sekta Ya Kilimo

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo_Dodoma
Serikali imewahakikishia Wanajeshi wastaafu kupitia muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania (MUWAWATA) kuwa imekusudia kuwashirikisha kwa karibu katika sekta ya kilimo kwani shughuli za kilimo zitaimarisha usalama wa chakula kwa kaya zao na Taifa kwa ujumla.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 13 Novemba 2019 wakati wa ufunguzi ya mkutano wa semina ya mafunzo kwa muungano wa wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA) uliofanyika tarehe 13 na 14 Novemba 2019 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma (Dodoma Convention Center).

Aliongeza kuwa shughuli hizo zitaongeza kipato na kuboresha maisha ya wanajeshi hao kwa ujumla; Kuimarisha afya zao kwa kupunguza utegemezi wa ndugu, jamaa na marafiki kwa ajili ya kujikimu na maisha baada ya kustaafu.

Alisema kuwa Wizara ya Kilimo ipo tayari katika lengo la kufanya shughuli za kilimo kwa kutoa ushauri wa kitaalamu ikiwa ni pamoja na; kuwahakikishia upatikanaji wa mbegu bora, mbolea, zana za kisasa za kilimo na viuatilifu.

Mhe Hasunga amesema kwa kupitia Taasisi za Serikali na Mamlaka zilizopo, Wizara imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa pembejeo kwa ujumla kwani ndio muhimili mkubwa katika sekta ya kilimo.

Kadhalika, amewahimiza wanajeshi hao na wakulima wote nchini kuzingatia matumizi bora ya pembejeo na kufuata ushauri wa kitaalamu; kwa kufanya hivyo ni Dhahiri kuwawataongeza tija na faida katika uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Mhe Hasunga amesema kuwa sekta ya kilimo inachangia takribani asilimia 28.7 ya Pato la Taifa, asilimia 65.5 ya ajira, asilimia 65 ya malighafi ya viwanda na asilimia 30 ya mapato ya nje. Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau mbalimbali ili kuwezesha sekta na kilimo kuchangia kwa ufanisi katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwezesha utekelezaji wa vipaumbele vya Taifa kwa ujumla.

Jitihada za Serikali zinalenga kuondoa vikwazo na changamoto za ukuaji wa sekta na kuimarisha Mapato ya Kilimo, kuboresha ukuaji wa mapato ya wakulima wadogo, kujitosheleza kwa chakula, uongezaji thamani ya mazao, ajira na hatimaye kufikia Nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Waziri Hasunga amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni;  Kuwashirikisha wadau fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo ili kuongeza mchango wa sekta ya kilimo katika Pato la Taifa ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha ya wakulima wadogo.

Amesema kuwa katika mkutano huo MUWAWATA wanapaswa kufanya wasilisho la shughuli za kilimo wanazozifanya na zile wanazotarajia kufanya kubainisha changamoto walizonazo na mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto hizo.

Alisema kuwa matarajio ya mkutano huo ni pamoja na Kuongeza ufahamu (awareness creation) wa fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo, kupata fursa ya kuunganishwa na Wadau mbalimbali yakiwemo mabenki n.k.

Matarajio mengine ni Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini na sekta binafsi kupata fursa ya kutoa maoni, ufafanuzi na kuwashauri MUWAWATA namna ya kushiriki katika kilimo; Kusikiliza changamoto zinazowakabili MUWAWATA na kuwashauri namna ya kuzitatua; na Kujenga uelewa kwa washiriki wa mkutano kuhusu Mikakati na Mipango ya Serikali katika kuiendeleza Sekta ya Kilimo;
 
Vilevile Waziri Hasunga ameitaja Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) kuwa ni muhimu kwa wakulima nchini kwani inahimiza uongezaji thamani mazao ya kilimo kabla ya kuyauza ambapo pia itakuwa imeongeza nafasi za ajira kwa Watanzania.
 
Alisema hatua hiyo itaongeza ushindani wa bidhaa za ndani na nje ya nchi na itaiwezesha nchi kufikia malengo ya kuwa kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025. “Ninawasihi MUWAWATA kujihusisha na kilimo kwa kuzingatia mnyororo wa thamani hasa kwa mazao ya vipaumbele ambayo yamebainishwa kwa kila eneo la kiikolojia” Alikaririwa Mhe Hasunga
MWISHO

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,Kusafisha nyota, Mvuto wa Mwili na Biashara, ...Miguu kufa ganzi na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

LIVE: Uzinduzi Wa Kitabu Cha "My Life My Purpose" Cha Rais Mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anashiriki hafla ya uzinduzi rasmi wa kitabu cha Historia ya maisha ya Mhe. Benjamin William Mkapa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.Kitabu kianitwa "MY LIFE MY PURPOSE"

Mawaziri wa Mambo ya Nje, Mawaziri wa Ulinzi wa SADC Wakutana Kujadili Hali ya Amani DRC

$
0
0
Mawaziri wa Mambo ya nchi za Nje pamoja na Mawaziri wa Ulinzi na vyombo vya ulinzi  vya Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC) ijulikanao kama DOUBLE TROIKA wamekutana kwa dharura kujadili hali ya kisasa na amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha amani katika nchi hiyo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa dharura wa DOUBLE TROIKA inayojumuisha Troika ya siasa na Troika ya Ulinzi na Usalama, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amesema kuwa lengo la mkutano huo wa dharura ni kuweka mikakati itakayosaidia kuimarisha amani nchini Congo DRC na kumaliza migogoro inayotishia ustawi wa nchi hiyo iliyodumu kwa miongo mingi.

Aidha, Waziri Kabudi amebainisha kuwa mkutano huo utasaidia nchi za SADC zenye vikosi vya ulinzi na usalama nchini DRC yaani Tanzania, malawai na Afrika Kusini kuimarisha amani na DRC kwa kufanya tathmini na kukubaliana hatua za kuchukua ili vita na migogoro ya mara kwa mara inayoibuka Nchini Congo DRC ifikie tamati na amani ya kudumu ipatikane.

“Mkutano huu wa leo ni wa Troika ya Siasa na Troika ya ulinzi na usalama ambapo kupitia mkutano huu tunaamini kuwa tutafanya tathimini ya hali ya amani DRC na kukubaliana ni hatua gani za kuchukua,” amesema Prof. Kabudi

Katika hatua nyingine Prof. kabudi ameongeza kuwa ndani ya mwaka huu amani na demokrasia vimezidi kuimarika katika nchi wanachama wa SADC, kutokana na baadhi ya nchi wanachama kuendesha chaguzi za kidemokrasia zilizomalizika kwa amani katika nchi za Msumbiji na Botswana.

Aidha Prof. Kabudi amesema Tanzania na Nchi 16 wanachama wa SADC bado zinaendelea kupaza sauti kwa jumuiya za kimataifa na nchi ambazo zimeiwekea vikwazo Zimbabwe kuviondoa mara moja kutokana na vikwazo hivyo kutokuwa na uhalali jambo linalosababisha mateso kwa raia wan chi hiyo hususani akina mama na watoto .

“Katika hili la Zimbabwe lazima sisi kama SADC tushikamane na kusafiri pamoja ili tufike kwa umoja wetu” Amesema Prof. kabudi.

Awali akitoa hutuba katika mkutano huo, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC), Stegomena Taxi amesema kuwa ana matumaini makubwa na mkutano huo unaofanyika jijini Dar es salaam utatathimini na kutoa mapendekezo ya muda mfupi na mrefu kuhusu hali ya usalama, amani na siasa katika nchi ya Congo DRC  na ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ili kuhakikisha ukanda huo unakuwa salama na amani

Ameongeza kuwa amani na usalama ni nyenzo mojawapo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na hivyo kupata maendeleo yanayohitajika kwa ajili ya mataifa ya Afrika.

Atakayepokea Muhamiaji Haramu Bila Kufuata Sheria Za Nchi Faini Milioni 20 au Kutupwa Jela

$
0
0
Na  Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera 
Wananchi  mkoani Kagera wametakiwa kufuata taratibu za kuwapokea wageni kutoka nchi jirani za Uganda Rwanda Burundi na Kenya na sio kuwa pokea nakuwatunza kinyemera katika maeneo yao na kuwapa makazi bila kufuata sheria za nchi. 

Hayo yamebainishwa na mkuu wa idara ya uhamiaji nchini Tanzaia  Anna Makakala wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za mkuu wa mkoa huo akiwa katika ziara ya kikazi itakayodu kwa siku tatu hapa mkoani kagera  ambapo kwasiku hizo tatu atazungukia wilaya zote za mkoa wa kagera pamoja na kuzungukia mipaka ya mkoa wa kagera  kwa upande wa nchi jirani. 

Makakala ameongeza kuwa Wageni kutoka nchi mbalimbali jirani waingie nchini kwa kufuata taratibu maalumu na kuwa tahadharisha wananchi mkoani hapa kuwa hatakaye bainika akimkaribisha mgeni pasipo kufuata sheria na kanuni  za nchi hatua kali za kisheria na hadhabu kali ya kifungo cha miaka 20 au kutozwa faini ya milioni 20 zita chukuliwa dhidi yake. 

Naye mkuu wa mkoa Kagera brigedia Generali  Marco Gaguti  amesema kuwa mkoa wa Kagera hupo salama na hakuna wa amihaji haramu katika mkoa huu ni kutokana na kazi  nzuri zinazofanywa na idara ya uhamiaji , na kamati ya ulinzi na usalama  ya mkoa kwa kushirikiana na wananchi.

Polepole Awavaa Wapinzani..."Wameogopa Upepo wa Kisulisuli"

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa watu wa vyama vya upinzani ni waungwana sana kwakuwa wameamua kujitoa wenyewe kwenye mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, baada ya kukiona chama hicho kilivyo imara na hawawezi kushindana nacho.

 Polepole amesema hayo leo Novemba 13, 2019, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

"Watu wa vyama vya upinzani ni waungwana, wametazama wakasema mambo yatakayotokea kwenye uchaguzi huu si ya mchezo, kwetu sisi ile 2014 inawezekana ulikuwa ushindi wa Tsunami ila wa mwaka huu utakuwa ni ushindi wa kisulisuli na ndiyo maana wakaamua kabla hatujafika pabaya wakaweka mpira kwapani.


“Sisi ndiyo chama pekee wenye ilani ya chama inayotekelezwa, hata katika uchaguzi wa serikali za mitaa tumeandaa ilani ndogo ambayo itakuwa na mambo ambayo tutawaahidi Watanzania na tutayatekeleza,” alisema na kuongeza kwamba  CCM kimeweka  uzito mkubwa katika uchaguzi huu kwa sababu mambo ya maendeleo ya wananchi yanaanzia ngazi ya serikali za mitaa, na ili safu ya uongozi wa juu ikamilike inaanzia chini na safu isipokamilika kunakuwepo na wizi na ubadhirifu katika fedha za umma.
 

“Chama Cha Mapinduzi tunaingia katika uchaguzi huu tukiwa timamu  ili kupata watu sahihi watakaoweza kumsaidia Mheshimiwa Rais Magufuli kusimamia miradi yetu ya maendeleo na kuijenga nchi yetu.

“Hoja moja ambayo wapinzani wameitoa ni kuwa itungwe kanuni mpya ya uchaguzi.  Sasa tunawauliza wakati tunatunga kanuni hizi pamoja na wao,  walikuwa wamelala?” aliuliza na kuongeza:

“Kitendo cha mtu mzima kama Prof. Lipumba kunitusi na kunibeza kwamba ninaongozwa na njaa ambayo imenipanda kichwani si kitendo cha uungwana hata kidogo, anayejua nina njaa ni mke wangu peke yake na si mtu mwingine.

“Wale wote wanaonituhumu kuwa nimebadili msimamo wa kutetea mambo mbalimbali ikiwemo katiba (ya Warioba) huku wakidai njaa ndiyo imenibadilisha,  nataka niwaambie kuwa sijawahi kukana kauli yoyote niliyowahi kuisema na anayejua kuwa mimi nina njaa ni mke wangu pekee.”

Aidha Polepole amevitaka vyama vya upinzani kujifunza kulingana na historia iliyopita kwakuwa kuna baadhi ya maeneo hawana wafuasi kabisa kama ilivyo CCM.

Hadi kufikia leo Novemba 13, 2019, jumla ya vyama 7 vya upinzani, vimekwishajitoa katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kile walichokieleza kuwa hawajatendewa haki baada ya majina ya wagombea wao kuenguliwa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images