Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

CAG Kichere: Nitafanya Kazi Kulinda Matumizi Ya Kodi Za Watanzania Maana Naujua Ugumu wa Kukusanya Kodi

$
0
0
Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Bw. Charles Kichere amesema kuwa ataendelea kutekeleza majukumu ambayo yameachwa na CAG aliyemaliza muda wake Prof.Mussa Assad kwani Ofisi hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya watanzania.

Akizungumza katika makabidhiano Kichere alisema kuwa Ofisi ya CAG ni nguzo muhimu kwa watanzani kwani ndiyo ofisi inayolinda na kuangalia matumizi sahihi ya kodi yao wanayolipa kila siku.

“Tutaendelea kuifanyakazi ambayo imefanywa na Prof.Assad na timu yake, nitahakikisha kushirikiana na wafanyakazi wa Ofisi hii kuifanya kazi hii ya kulinda mapato ya kodi ya watanzania”, Alisema Kichere.

Kichere alisema kuwa katika kutekeleza majukumu hayo mapya atahakikisha kuwa atalinda Kodi ya watanzania wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wafanyakazi ili fedha inayopataikana kwenye kodi iweze kuwanufaisha wote.

Aliwahakikishia watanzania kuwa hakuna kodi inayotolewa na watanzania ambayo itapotea kwa hiyo ataangalia na kuilinda  kwaajili ya kuwaletea maendeleo.

“Nataka kufanya kazi kulinda maslahi ya watanzania nimefanyakazi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA najua ugumu wa kukusanya kodi na kupata mapato, kwa hiyo nitahakikisha kuwa nailinda kodi ya wananchi kwa wivu mkubwa sana”, Alisisitiza Kichere.


Mapendekezo Ya Mpango Wa Maendeleo Na Bajeti Ya Serikali 2020/21 Wawasilishwa Bungeni

$
0
0

UTANGULIZI
1.            Mheshimiwa Spika,naomba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kutoa ushauri kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa  na Serikali katika mwaka wa fedha 2020/21 na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2020/21.

2.            Mheshimiwa Spika,awali ya yote napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutujalia uhai na afya njema ambayo imetuwezesha kukutana tena hapa Jijini Dodoma kwa ajili ya kutekeleza majukumu muhimu ya kikatiba ya Muhimili huu wa Bunge kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa. Vile vile, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuijalia nchi yetu umoja, na amani ambavyo vimekuwa nguzo muhimu ya kutuwezesha sisi watanzania kuendelea kutekeleza majukumu yetu, kila mmoja kwa nafasi yake, na kuchangia katika ujenzi wa Taifa.

3.            Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee napenda kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufikisha umri wa miaka 60 tangu kuzaliwa kwake. Tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kumjalia afya njema na maisha marefu zaidi ili kutuwezesha watanzania wote kufurahia mafanikio makubwa ambayo yanaendelea kupatikana chini ya uongozi wake mahiri. Hakika tunajivunia kumpata kiongozi mchapakazi, mzalendo, anayechukia rushwa, mtetezi wa wanyonge na mfano wa kuigwa barani Afrika.

4.            Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru wewe binafsi kwa kuendelea kuliongoza Bunge hili Tukufu kwa weledi mkubwa katika kuishauri na kuisimamia Serikali. Aidha, napenda kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti inayoongozwa na Mheshimiwa Mashimba Mashauri Ndaki, Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi, kwa ushauri mzuri waliotupatia wakati wa kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa kuanda Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha unaofuata (2020/21).

5.            Mheshimiwa Spika,Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa fedha 2020/21 na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali yanawasilishwa katika Bunge lako Tukufu kwa mujibu wa Kanuni ya 94 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari 2016. Mapendekezo haya ya Mpango na Mwongozo yameainisha vipaumbele na masuala muhimu ya kuzingatiwa na Maafisa Masuuli wa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma wakati wa kuandaa, kutekeleza, kufuatilia, kutathmini na kutoa taarifa za utekelezaji  wa Mipango na Bajeti za Mafungu yao.

6.            Mheshimiwa Spika,Mapendekezo ya Mpango na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2020/21 yamezingatia: Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17 - 2020/21); Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015; Sheria ya Bajeti, Sura 439; Sera na mikakati mbalimbali ya maendeleo ya kisekta na kikanda (EAC, SADC na AU); na Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030.

7.            Mheshimiwa Spika,masuala yaliyoainishwa katikaMapendekezo ya Mpango Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2020/21 ni pamoja na:

A.           MWENENDO WA VIASHIRIA VYA UCHUMI

8.            Mheshimiwa Spika,uchumi wa Taifa umeendelea kuwa imara ambapo katika kipindi cha muongo mmoja uliopita (2009 – 2018), Pato halisi la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 6.4 kwa mwaka. Katika mwaka 2018, Pato la Taifa lilikua kwa asilimia 7.0 ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka 2017 kwa mwaka wa kizio wa 2015. Aidha, katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2019 (Januari – Juni), Pato la Taifa kwa mwaka wa kizio wa 2015 lilikua kwa asilimia 6.9 ikilinganishwa na asilimia 6.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2018. Ukuaji huu ulichochewa zaidi na kuongezeka kwa uwekezaji hususan katika ujenzi wa barabara, reli na viwanja vya ndege; kutengamaa kwa upatikanaji wa nishati ya umeme; kuimarika kwa huduma za usafirishaji; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini hususan dhahabu na makaa ya mawe; na kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo. Sekta zilizokua kwa kasi zaidi katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2019 ni pamoja na ujenzi (asilimia 16.5), uchimbaji madini na mawe (asilimia 13.7), habari na mawasiliano (asilimia 10.7), maji (asilimia 9.1) na usafirishaji na uhifadhi wa mizigo (asilimia 9.0). Aidha, mfumuko wa bei ulifikia asilimia 3.6 mwezi Agosti 2019 na kuendelea kupungua hadi asilimia 3.4 mwezi Septemba 2019.

9.            Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Januari hadi Juni 2019, urari wa malipo ya kawaida ulikuwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 2,257.3 ikilinganishwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 1,771.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2018, sawa na ongezeko la nakisi kwa asilimia 27.4. Hii ilitokana na kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi, hususan, bidhaa za kukuza mitaji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa hapa nchini. Akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kutosha na kukidhi mahitaji ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza bidhaa na huduma nje ambapo hadi Agosti 2019, akiba ya fedha za kigeni (bila kujumuisha bidhaa na huduma ambazo zinalipiwa na fedha za uwekezaji wa moja kwa moja) ilifikia dola za Marekani milioni 5,200.1, ikiwa ni sawa na uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje kwa miezi 6.0. Ujazi  wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) uliongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 27,163.2 Agosti 2019, sawa na ongezeko la asilimia 8.3 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2018. Mwenendo wa viashiria vya sekta ya kibenki ulikuwa wa kuridhisha ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa faida kutokana na uwekezaji wa rasilimali kutoka asilimia 6.88 Agosti 2018 hadi asilimia 8.16 Agosti 2019 na kuongezeka kwa faida kutokana na uwekezaji wa mtaji kutoka asilimia 1.68 Agosti 2018 hadi asilimia 1.89 Agosti 2019. Kwa ujumla gharama za mikopo zilipungua ambapo riba za mikopo zilifikia wastani wa asilimia 16.77 Agosti 2019 kutoka asilimia 17.09 Agosti 2018. Aidha, mikopo kwa sekta binafsi iliendelea kukua na kuchochea shughuli za kiuchumi ambapo hadi Agosti 2019 ukuaji ulifikia asilimia 8.2 ikilinganishwa na asilimia 5.2 Agosti 2018.

10.         Mheshimiwa Spika,mwenendo wa thamani ya Shilingi uliendelea kuwa tulivu katika kipindi cha mwaka unaoishia Agosti 2019, ambapo Dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa shilingi 2,289.1 ikilinganishwa na wastani wa shilingi 2,273.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2018. Deni la Serikali lilifikia shilingi bilioni 52,303.04 Agosti 2019 ikilinganishwa na shilingi bilioni 49,283.44 Agosti 2018. Tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Desemba 2018, inaonesha kuwa Deni la Serikali bado ni himilivu katika muda mfupi, wa kati na mrefu kwa vigezo vya kimataifa.

11.         Mheshimiwa Spika,maelezo ya kina kuhusu mwenendo wa viashiria vya uchumi yanapatikana katika Sura ya Pili ya Kitabu cha Mapendekezo ya Mpango na Sura ya Pili katika Sehemu ya Kwanza ya kitabu cha Mwongozo.

B.           UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2018/19

12.         Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 mapato ya ndani yalifikia shilingi bilioni 18,529.6 sawa na asilimia 88.7 ya lengo la shilingi bilioni 20,894.6. Kati ya kiasi hicho, mapato yaliyokusanywa na TRA yalikuwa shilingi bilioni 15,511.3, mapato yasiyo ya kodi yalikuwa shilingi bilioni 2,356.9 na mapato ya Halmashauri yalikuwa shilingi bilioni 661.4. Kutofikiwa kwa malengo ya makusanyo ya mapato kulichangiwa na upotevu wa mapato kutokana na shughuli za magendo, hususan kupitia bandari bubu katika ukanda wa bahari ya Hindi na njia zisizo rasmi mipakani, pamoja na ukwepaji kodi. Aidha, mapato yasiyo ya kodi yalivuka lengo kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya mifumo ya kielektroniki na kuimarika kwa usimamizi na ufuatiliaji wa vyanzo vya mapato husika.

13.         Mheshimiwa Spika,katika kipindi hicho, fedha za misaada na mikopo nafuu zilizopokelewa zilikuwa shilingi bilioni 2,083.4. Mikopo ya nje yenye masharti ya kibiashara iliyopatikana ni shilingi bilioni 1,144.8 na mikopo kutoka katika soko la ndani ni shilingi bilioni 3,950.7.

14.         Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi, Serikali ilitoa ridhaa ya matumizi ya shilingi bilioni 27,049.2, ambapo matumizi ya kawaida yalikuwa shilingi bilioni 19,099.9 na matumizi ya maendeleo yalikuwa shilingi bilioni 7,949.3. Vile vile, Serikali ililipa shilingi bilioni 6,659.6 kwa ajili ya mishahara ya watumishi na shilingi bilioni 599.94 kwa ajili ya madeni ya wakandarasi, wazabuni na watumishi wa Serikali.   Kadhalika, katika kipindi hicho, Serikali ilitoa jumla ya shilingi bilioni 7,701.7 kwa ajili ya kulipia kwa wakati mitaji (principal) na riba kwa mikopo ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

15.         Mheshimiwa Spika, Maelezo ya kina kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2018/19 yanapatikana katika Sehemu ya Kwanza ya kitabu cha Mwongozo (Sura ya Pili).

Utekelezaji wa Baadhi ya Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka 2018/19 na Robo ya Kwanza ya Mwaka 2019/20

16.         Mheshimiwa Spika,hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2018/19 na robo ya kwanza ya mwaka 2019/20 ni pamoja na:
(i)           Mradi wa kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere: Serikali iliendelea na utekelezaji wa mradi huu ambapo kazi zilizokamilika ni pamoja na: ujenzi wa daraja la muda namba 2; utafiti wa miamba na udongo; uchimbaji wa mtaro wa chini kwa chini (adit tunnel)wenye urefu wa mita 147.6 kuelekea kwenye mtaro wa chini kwa chini wa kuchepua maji ya mto Rufiji (diversion tunnel); na mtambo wa kuchakata kokoto (Batching Plant and Crusher) namba moja.
(ii)          Mradi wa Reli ya Kati ya Standard Gauge: Ujenzi wa reli ya kati ya Standard Gauge kwa sehemu Dar es Salaam – Morogoro (km 300) umefikia asilimia 63 na sehemu ya Morogoro – Makutupora (km 422) asilimia 16.

(iii)        Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania: ndege nne zimepokelewa ambapo mbili ni aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na mbili ni aina ya Airbus A220-300; kulipa sehemu ya gharama za ununuzi wa ndege moja aina ya Bombadier Dash 8 Q400 inayotarajiwa kuwasili Desemba 2019; kusainiwa kwa mikataba na kulipa malipo ya awali ya ununuzi wa ndege nyingine mpya tatu ambapo mbili (2) ni aina ya Airbus A220-300 na moja (1) ni aina ya Bombardier Q400. Aidha, Shirika limeongeza idadi ya vituo vya safari za ndani kufikia 11 na nje ya nchi kufikia vituo sita.

(iv)        Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleani (Tanga): Tanzania iliendelea na majadiliano ili kufikia makubaliano na Serikali ya Uganda na Mwekezaji (Host Government Agreement - HGA); tafiti za Mateocean, kijiolojia na kijiofizikia katika eneo la Chongoleani-Tanga zilikamilishwa; na kazi ya usanifu wa kina wa kihandisi (Detailed Engineering Design) wa eneo la ujenzi wa mradi inaendelea.
(v)          Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia – Lindi: Serikali inaendelea na majadiliano na kampuni za mafuta (Equinor na Shell) katika kitalu namba 1, 2, na 4 katika bahari kuu. Aidha,  tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii  pamoja na Mpango wa Uhamishaji wa Wananchi watakaopisha eneo la mradi vimekamilika.
(vi)        Makaa ya Mawe Mchuchuma na Vanadium, Titaniumna Chuma Liganga: Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilika kwa utafiti wa kina kuhusu wingi, aina na thamani za madini katika miamba ya Liganga na uhakiki wa mali za wananchi watakaopisha eneo la miradi.
(vii)       Shamba la Miwa na Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi: Hatua iliyofikiwa kwa upande wa Shamba la Mkulazi I, ni kukamilika kwa michoro ya ujenzi wa bwawa la maji lenye ukubwa wa mita za ujazo milioni 15 na maandalizi ya eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha sukari. Kwa upande wa Shamba la Mbigiri – Mkulazi II, hatua iliyofikiwa ni: kuendelea kwa ujenzi wa majengo ya kiwanda cha sukari; kuboresha miundombinu ya barabara na majengo; na kupatikana kwa mzabuni wa kutengeneza na kufunga mitambo ya kiwanda ambapo mkataba umesainiwa.
(viii)      Miradi ya Umeme: Mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa Msongo wa kV 220 Makambako – Songea umekamilika; na utekelezaji wa miradi ya kufua umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya nishati vikiwemo maji na gesi unaendelea. Aidha, Serikali imeendelea na juhudi za kupeleka umeme vijijini hususan kupitia awamu ya tatu ya miradi ya nishati vijijini (REA) ambapo hadi Septemba 2019, jumla ya vijiji 8,102 vilikuwa vimefikishiwa umeme kati ya vijiji 12,268 vya Tanzania Bara, sawa na asilimia 66.04.
(ix)        Miradi ya maji mijini na vijijini: Serikali iliendelea na utekelezaji wa miradi ya Maji ya Kitaifa kwa kukamilisha ulazaji wa mabomba, upanuzi na ukarabati katika maeneo yanayohudumiwa na miradi; na kuboresha huduma za maji vijijini ambapo miradi 1,659 ya maji vijijini imekamilika. Aidha,  miradi 653 ya maji vijijini ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
(x)          Miradi ya Viwanda: Serikali inaendelea kuimarisha Shirika la Viwanda Vidogo - SIDO; ukarabati na upanuzi wa kiwanda cha ngozi na bidhaa za ngozi cha Karanga - Moshi; na kuimarisha Shirika la Nyumbu ili kuongeza uzalishaji ikiwemo kuzalisha magari ya zimamoto.
(xi)        Barabara na Madaraja: Serikali imeendelea kugharamia ujenzi wa barabara za lami nchini ambapo mtandao wa barabara kuu umefikia kilomita 8,306 na mtandao wa barabara za mikoa umefikia kilomita 1,756; ujenzi wa madaraja yafuatayo umekamilika: Sibiti (Singida), Momba (mpakani mwa Songwe na Rukwa), Mlalakuwa (Dar es Salaam), na Lukuledi (Lindi). Aidha, ujenzi wa barabara na madaraja mengine upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
(xii)       Meli katika Maziwa Makuu: ujenzi wa meli ya MV Mbeya katika Ziwa Nyasa umekamilika. Vilevile, mikataba ya ujenzi wa meli mpya na ukarabati wa meli katika Ziwa Victoria na Tanganyika imeandaliwa.

(xiii)      Viwanja vya Ndege: Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III) la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere umekamilika na jengo hilo kuanza kutumika. Ujenzi na ukarabati wa Kiwanja cha Mwanza umefikia asilimia 95. Aidha, ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika baadhi ya mikoa upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
(xiv)      Bandari: uboreshaji wa gati Na.1 na Na. 2 katika bandari ya Dar es Salaam na ujenzi wa gati la RoRo vimekamilika. Aidha, uboreshaji wa gati Na. 3 umefikia asilimia 60 na uboreshaji wa bandari za Tanga na Mtwara unaendelea.
(xv)       Uwekezaji wa Sekta Binafsi: Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na: kufutwa na kupunguzwa kwa ada na tozo 54 ili kuondoa kero na urasimu kwa wafanya biashara na wawekezaji na kuzinduliwa na kuanza uzalishaji katika viwanda saba (7) ambavyo ni kiwanda cha Pipe Industries Co. Limited,kiwanda cha Chai cha Kabambe (Njombe), kiwanda cha Yalin Cashewnut Company Ltd (Mikindani – Mtwara), kiwanda cha 21st Century Food and Packaging,kiwanda cha kusaga mahindi cha Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited(MeTL), kiwanda cha bidhaa za plastiki cha Plasco Pipelines Co Ltd,  kiwanda cha kufungasha na kuhifadhi parachichi (Rungwe Avocado) na kiwanda cha kuchakata parachichi kwa ajili ya kutengeneza mafuta (KUZA Afrika).

17.         Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2018/19 na robo ya kwanza ya mwaka 2019/20 yameelezwa kwa kina katika kitabu cha Mapendekezo ya Mpango (Sura ya Tatu).

C.           MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MIAKA MITANO KWA KIPINDI CHA 2016/17 HADI ROBO YA KWANZA YA  2019/20

18.         Mheshimiwa Spika, yapo mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/17 hadi Septemba 2019. Mafanikio hayo ni pamoja na:

   (i)        Ukuaji wa Uchumi: Kuendelea kuimarika kwa uchumi wa Taifa, ambapo uchumi ulikua kwa wastani wa asilimia 7.0 mwaka 2018 kutoka ukuaji wa asilimia 6.8 mwaka 2017 na mfumuko wa bei kuendelea kupungua na kufikia asilimia 3.4 Septemba 2019.
  (ii)        Ukusanyaji wa Mapato: Kuongezeka kwa mapato ya ndani kutoka wastani wa shilingi bilioni 800 kwa mwezi katika mwaka 2016/17 hadi kufikia wastani wa shilingi bilioni 1,292.6 kwa mwezi katika mwaka 2018/19 kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika ukusanyaji wa mapato. Aidha, juhudi hizo zimeendelea kuleta mafanikio ambapo mapato ya ndani kwa mwezi Septemba 2019 yamefikia shilingi bilioni 1,740.2.

(iii)        Ulipaji wa Deni la Serikali: Tangu mwaka 2016/17 hadi Septemba 2019 Serikali imelipa jumla ya shilingi bilioni 24,499.2 kwa ajili ya deni lililoiva la fedha zilizokopwa kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
(iv)        Ulipaji wa Mishahara: Mishahara ya watumishi wa Serikali yenye jumla ya shilingi bilioni 22,169.9 ililipwa kwa wakati katika kipindi chote cha 2016/17 hadi Septemba 2019.
  (v)        Barabara na Madaraja: Ujenzi wa barabara 23 za lami umekamilika na hivyo kuongeza mtandao wa barabara kuu za lami kutoka kilomita 7,646 Juni 2016 hadi kilomita 8,306 Juni 2018 na mtandao wa barabara za mikoa umeongezeka kutoka kilomita 1,398 hadi kilomita 1,756; Barabara ya juu ya Mfugale (TAZARA – Dar es Salaam), ilikamilika na kuanza kutumika; ujenzi wa barabara unganishi ya juu ya Ubungo Interchange (Dar es Salaam), unaendelea ambapo utekelezaji umefikia asilimia 55; Madaraja yaliyokamilika ni pamoja na daraja la Magufuli katika Mto Kilombero (Morogoro), Kavuu (Katavi), Sibiti (Singida), Momba (mpakani mwa Songwe na Rukwa), Mlalakuwa (Dar es Salaam), Lukuledi (Lindi) na daraja la Waenda kwa Miguu la Furahisha (Mwanza) na kuanza kwa ujenzi wa daraja la Kigongo - Busisi (Mwanza). Aidha, ujenzi wa barabara na madaraja mengine upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
(vi)        Reli:Ujenzi wa reli ya kati ya Standard Gauge unaendelea ambapo sehemu ya Dar es Salaam – Morogoro (km 300) ujenzi umefikia asilimia 63 na Morogoro – Makutupora (km 422) asilimia 16. Aidha, ukarabati wa reli ya kati ya zamani, madaraja, na ujenzi wa makalavati upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Pia, ukarabati wa kipande cha reli ya Tanga – Moshi (km 353) umekamilika na kuanza kufanya kazi.
(vii)        Nishati: Uwezo wa kuzalisha umeme katika Gridi ya Taifa umeongezeka kufikia megawati 1,613.52; Idadi ya vijiji vilivyounganishiwa umeme imefikia 8,102 kati ya Vijiji 12,268 vya Tanzania Bara sawa na asilimia 66.04; na utekelezaji wa mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere utakaozalisha MW 2,115 unaendelea.
(viii)        Shirika la Ndege Tanzania: Jumla ya ndege mpya 11 zimenunuliwa ambapo ndege saba zimepokelewa. Utengenezaji wa ndege moja upo katika hatua za mwisho na inatarajiwa kuwasili nchini kabla ya mwisho wa mwaka 2019. Vilevile, ndege 3 zimeanza kutengenezwa baada ya malipo ya awali kulipwa. Aidha, uboreshaji wa Shirika la Ndege la Tanzania umeongeza huduma za usafiri wa anga kufikia vituo 11 nchini na vituo 6 nje ya nchi.
(ix)        Viwanja vya Ndege: Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere limekamilika na kuanza kutumika; awamu ya kwanza ya ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro umekamilika; ujenzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza umekamilika kwa asilimia 95; na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege vya mikoa unaendelea na umefikia hatua mbalimbali za utekelezaji.
  (x)        Bandari: Upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam unaendelea ambapo gati Na.1 na Na. 2 na ujenzi wa gati la Ro-Ro umekamilika na kuwezesha meli ya kwanza yenye uwezo wa kubeba magari 6,000 kuhudumiwa katika gati hilo tarehe 15 Septemba, 2019. Uboreshaji wa gati Na. 3 umefikia asilimia 60. Aidha, uboreshaji wa bandari za Tanga, Mtwara na bandari za maziwa makuu unaendelea.
(xi)        Usafiri katika Maziwa Makuu: Ujenzi wa matishari mawili (2) na meli ya MV Mbeya katika Ziwa Nyasa umekamilika; ujenzi na ukarabati wa meli tano (5) katika Ziwa Victoria (ikiwemo MV Victoria, MV  Butiama, MV Umoja na MV Serengeti) unaendelea; na mikataba ya ujenzi wa meli moja (1) mpya na ukarabati wa MV Liemba katika Ziwa Tanganyika imeandaliwa.
(xii)        Kilimo: uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa 2018/19 ulifikia tani 16,408,309 na hivyo kuwa na ziada ya tani 2,565,774 za mazao ya chakula. Hivyo, kiwango cha Utoshelevu wa Chakula kilikuwa asilimia 119.
(xiii)        Madini: Serikali imeendelea na ujenzi wa miundombinu ya kuboresha mazingira ya biashara kwenye sekta ya madini ikihusisha vituo vya umahiri (centres of excellence) katika mikoa saba, vituo vitatu vya mfano, Jengo la Taaluma ya Madini katika Chuo cha Madini, Kituo cha Pamoja cha Biashara ya Madini (One Stop Centre) Mirerani, Jengo la Wafanyabiashara (Brokers House) Mirerani, uanzishwaji wa masoko 28 ya madini na vituo vidogo 11 vya ununuzi wa madini katika mikoa 24 nchini, uwekaji wa mfumo wa ulinzi wa kidigitali Mirerani, ununuzi wa mtambo wa uchorongaji miamba kwa ajili ya kusaidia wachimbaji wadogo na kufutwa kwa kampuni ya Madini ya ACACIA na kuundwa kampuni mpya ya Twiga Mineral Corporation inayomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania (hisa asimilia 16) na Kampuni ya Barrick (hisa asilimia 84).
(xiv)        Viwanda: Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ujenzi wa uchumi wa viwanda ambapo jumla ya viwanda 3,530 vimejengwa katika mikoa mbalimbali.
(xv)        Huduma za Afya: Mafanikio yaliyopatikana yanajumuishakuendelea na ujenzi na ukarabati wa hospitali za rufaa za mikoa, kanda na kitaifa; ujenzi wa Hospitali mpya za Wilaya 67 na pia kuanza maandalizi ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru (Dodoma), Hospitali ya Wilaya ya Tunduma (Songwe) na Hospitali ya Manispaa ya Ubungo (Dar es Salaam); ujenzi na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za Afya (470) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 98; kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa nyumba 301 za watumishi wa afya; na kuendelea na ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi.
(xvi)        Huduma za Maji:Mradi wa kuboresha huduma za maji Dar es Salaam (utekelezaji umefikia wastani wa asilimia 74); Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria: ulazaji wa bomba la kusambazia maji katika miji ya Isaka, Tinde na Kagongwa imekamilika kwa asilimia 99; na ujenzi wa miundombinu ya maji katika miji ya Tabora, Igunga, Uyui na Nzega pamoja na vijiji 89 vilivyo pembezoni mwa bomba kuu umefikia asilimia 78; Miradi 1,659 ya maji vijijini imekamilika na ujenzi na ukarabati wa miradi 653 ya maji vijijini ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

(xvii)        Elimu: Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kugharamia elimumsingi bila ada; ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote; Maktaba ya Kimataifa yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 2,600 kwa wakati mmoja katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilikamilika na kuzinduliwa; utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu umeendelea pamoja na uimarishaji wa vyuo vya ufundi stadi (VETA).
(xviii)        Kuhamishia Shughuli za Serikali Makao Makuu Dodoma: Serikali ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imefanikisha ndoto ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuhamishia Makao Makuu ya Serikali jijini Dodoma kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi ambapo jumla ya watumishi 8,883 wa Wizara na Taasisi za Serikali  wamehamishiwa Makao Makuu ya Serikali, Dodoma na ujenzi wa ofisi 23 za Wizara katika mji wa Serikali, Mtumba umekamilika, ikijumuisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

19.         Mheshimiwa Spika, Maelezo ya kina kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti yanapatikana katika  Sehemu ya Kwanza -  Sura ya Pili ya Kitabu cha Mwongozo na Kitabu cha Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka 2016/17 hadi robo ya kwanza ya Mwaka 2019/20.

D.           CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI NA HATUA ZA KUKABILIANA NAZO

20.         Mheshimiwa Spika,Bajeti ya mwaka 2018/19 ilikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na: kuwepo kwa mahitaji makubwa yasiyowiana na uwezo wa mapato; ukwepaji kodi kwa njia mbalimbali ikiwemo kutokutoa stakabadhi za kielektroniki na kuendesha biashara za magendo hususan kupitia bandari bubu na  katika maeneo ya mipakani; mabadiliko ya viwango vya riba katika masoko ya fedha ya nje; kutopatikana kwa misaada na mikopo kutokana na baadhi ya Washirika wa Maendeleo kutotimiza ahadi zao kwa wakati; na ukosefu wa takwimu za uwekezaji wa sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

21.         Mheshimiwa Spika,katika kukabiliana na changamoto za utekelezaji wa bajeti, Serikali itaendelea kuchukua hatua zifuatazo: kuendelea kuwianisha mapato na matumizi; kuimarisha ulipaji wa kodi wa hiari kwa kutekeleza Mpango wa Kusimamia Vihatarishi vya Mwitikio wa Ulipaji Kodi; kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi ya mashine za stakabadhi za kielektroniki kupitia matumizi ya Mfumo ulioboreshwa; kuongeza doria na ukaguzi unaolenga kudhibiti biashara za magendo; kuendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji; kukuza soko la fedha la ndani; kuendeleza majadiliano na Washirika wa Maendeleo na taasisi za fedha za nje; kutekeleza mwongozo wa ushirikiano baina ya Serikali na Washirika wa Maendeleo; na kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ili kupata taarifa za uwekezaji wa sekta hiyo katika uchumi.


E.           MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2020/21

22.         Mheshimiwa Spika,misingi iliyozingatiwa katika kuweka malengo ya uchumi jumla ni pamoja na: Kuendelea kuwepo kwa amani, usalama, utulivu na umoja hapa nchini na katika nchi jirani; kuimarika kwa uchumi wa dunia na utulivu wa bei katika masoko ya fedha ya ndani na ya kimataifa; na kuwepo kwa hali nzuri ya hewa itakayowezesha uzalishaji wa chakula cha kutosha.

23.         Mheshimiwa Spika,shabaha na malengo ya uchumi jumla yatakayozingatiwa katika muda wa kati ni pamoja na:-
(ii)          Kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja ya wastani wa asilimia kati ya 3.0 - 5.0;
(iii)         Mapato ya ndani kufikia asilimia 14.8 ya Pato la Taifa mwaka 2020/21 na kufikia wastani wa asilimia 14.9 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2022/23;
(iv)         Matumizi ya Serikali kuwa asilimia 21.7 ya Pato la Taifa mwaka 2020/21 na asilimia 20.9 ya Pato la Taifa mwaka 2022/23;
(v)          Kuhakikisha kuwa nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada) inakuwa chini ya asilimia 3.0 kuendana na makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki; na
(vi)         Kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne (4.0).


Mfumo wa Awali wa Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2020/21

24.         Mheshimiwa Spika,katika mwaka 2020/21, Mapato ya ndani (yakijumuisha mapato ya Halmashauri) yanakadiriwa kuongezeka hadi shilingi bilioni 23,456.3 mwaka 2020/21 kutoka makadirio ya shilingi bilioni 23,045.3 mwaka 2019/20 na kukadiriwa kuongezeka kwa wastani wa asilimia 8.8 katika muda wa kati. Uwiano wa mapato ya ndani kwa mapato yote unatarajiwa kuongezeka kutoka asilimia 68.3 ya bajeti ya mwaka 2020/21 hadi asilimia 73.7 mwaka 2022/23. Mapato ya kodi yanakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 4.3 hadi shilingi bilioni 19,761.2 mwaka 2020/21 kutoka shilingi bilioni 18,955.2 mwaka 2019/20 na kukua kwa wastani wa asilimia 8.9 katika muda wa kati. Mapato yasiyo ya kodi (yakijumuisha mapato ya Halmashauri) yanakadariwa kuwa shilingi bilioni 3,601.3 mwaka 2020/21 na kuongezeka kufikia shilingi bilioni 4,340.0 mwaka 2022/23.

25.         Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21 jumla ya misaada kutoka kwa Washirika wa Maendeleo inatarajiwa kufikia shilingi bilioni 1,268.6 ambapo Misaada ya Kibajeti (General Budget Support- GBS) inatarajiwa kuwa shilingi bilioni 154.2, Misaada ya Mifuko ya Pamoja ya Kisekta (Basket Funds)shilingi bilioni 172.9 na Misaada ya Miradi (Project Funds) shilingi bilioni 941.5. Aidha, nakisi ya bajeti inayojumuisha misaada inakadiriwa kuwa shilingi bilioni 3,943.4 sawa na asilimia 2.5 ya Pato la Taifa kwa mwaka 2020/21 ambapo jumla ya shilingi bilioni 2,355.3 zitagharamiwa na mikopo ya nje na shilingi bilioni 1,588.2 zitagharamiwa na mikopo ya ndani sawa na asilimia 1 ya Pato la Taifa.

26.         Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21 matumizi ya Serikali yanakadiriwa kuongezeka hadi shilingi bilioni  34,360.2 sawa na asilimia 21.7 ya Pato la Taifa kutoka shilingi bilioni 33,105.4 mwaka 2019/20. Matumizi ya kawaida yanakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 4.7 hadi shilingi bilioni 21,660.7 sawa na asilimia 13.7 ya Pato la Taifa na matumizi ya maendeleo yanakadiriwa kuwa shilingi bilioni  12,699.4 sawa na asilimia 8.0 ya Pato la Taifa.

27.         Mheshimiwa Spika,maelezo ya kina kuhusu sera za mapato na matumizi katika muda wa kati yapo katika Sehemu ya Kwanza – Sura ya Tatu ya Kitabu cha Mwongozo.

F.            MAELEKEZO MAHSUSI YA MWONGOZO

28.         Mheshimiwa Spika,Mwongozo wa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2020/21 umeainisha maelekezo mbalimbali ambayoMaafisa Masuuli watatakiwa kuyazingatia wakati wa uandaaji, utekelezaji, ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa. Hivyo, Maafisa Masuuli watatakiwa kutekeleza kikamilifu maelekezo yote yaliyopo kwenye Mwongozo na kusimamia Sheria ya Bajeti, SURA 439 na Kanuni zake. Aidha, Kamati za Mipango na Bajeti za kila Fungu zitatakiwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Kanuni ya 17(3) ya Kanuni za Sheria ya Bajeti za mwaka 2015. Baadhi ya maelekezo yanayotakiwa kuzingatiwa na Maafisa Masuuli ni:
(i)           Kufanya mapitio ya utekelezaji wa bajeti na kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye Mafungu;
(ii)          Kubuni na kuboresha mifumo ya usimamizi wa mapato ikiwemo kuziba mianya ya ukwepaji kodi na kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari;
(iii)        Kupitia, kurekebisha na kuandaa sheria ndogo ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato na utawala bora katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
(iv)        Kuhakikisha gharama za miradi inayoendelea zinajumuishwa kwenye mpango wa muda wa kati na bajeti kabla ya kuanzisha miradi mipya;
(v)          Kufanya ukadiriaji sahihi wa stahili za kisheria kama vile posho, pango, umeme, simu na maji kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mlipaji Mkuu wa Serikali kwa kuzingatia mabadiliko baada ya shughuli za Serikali kuhamishiwa Dodoma;
(vi)        Kuweka kipaumbele katika utengaji wa fedha za kulipia madeni yaliyohakikiwa kwa kutumia ukomo wa bajeti uliotolewa;
(vii)       Kuhakikisha Kamati za Bajeti za Mafungu zinafanya kazi kwa kuzingatia Kifungu cha 18(2) cha Sheria ya Bajeti, Sura 439 na Kanuni zake;

(viii)      Kuandaa ikama na makadirio ya bajeti ya mishahara kwa mwaka 2020/21 kwa kuzingatia Waraka wa Katibu Mkuu UTUMISHI;
(ix)        Kuandaa na kuwasilisha mikakati ya uwekezaji, mwongozo wa gawio na mipango ya biashara kwa Msajili wa Hazina kwa ajili ya kuidhinishwa;
(x)          Kuandaa na kuwasilisha kwa Msajili wa Hazina mpango mkakati wa kuboresha utendaji wa mashirika ili kuepuka kujiendesha kwa hasara;
(xi)        Kubuni mikakati ya kuongeza vyanzo vya mapato ya ndani;
(xii)       Kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 10(A) cha Sheria ya Fedha ya mwaka 2015 kwa kutenga na kuwasilisha kwa wakati katika Mfuko Mkuu wa Hazina michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi;
(xiii)      Kuzingatia viwango vya ukomo wa bajeti vilivyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango; na
(xiv)      Kuandaa mpango na bajeti kwa kuzingatia muundo wa Matumizi wa Muda wa Kati (MTEF) na kuwasilisha Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya uchambuzi. Mawasilisho hayo yanatakiwa kufanyika wiki ya tatu ya Januari, 2020 baada ya kuidhinishwa katika ngazi za maamuzi husika ikijumuisha Mabaraza ya Wafanyakazi kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Majadiliano ya Pamoja katika Utumishi wa Umma, Sura 105.

29.         Mheshimiwa Spika,maelezo ya kina kuhusu maelekezo mahsusi ya Mwongozo yanayotakiwa kuzingatiwa na Maafisa Masuuli yanapatikana katika Sehemu ya Pili ya Kitabu cha Mwongozo (Sura ya Kwanza na Sura ya Pili).

G.           MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2020/21

30.         Mheshimiwa Spika,Mapendekezo yaMpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2020/21 yameandaliwa kwa kuzingatia maeneo manne ya kipaumbele yanayojumuisha miradi ya kielelezo iliyobainishwa katika Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Maeneo ya kipaumbele pamoja na baadhi ya miradi itakayopewa kipaumbele kwa mwaka 2020/21 ni kama ifuatavyo:

(i)           Ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda
Kuendelea kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuboresha upatikanaji wa mbegu na pembejeo za kilimo pamoja na kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji, maghala na masoko; kujenga viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini, hususan za kilimo; kuimarisha Shirika la Viwanda Vidogo – SIDO kuweza kuhudumia wananchi wengi zaidi ili kuchochea mageuzi ya viwanda nchini; kuanzisha na kuendeleza maeneo ya viwanda (Industrial parks) na Kanda Maalum za Kiuchumi; kuboresha utendaji kazi na kutumia taasisi za umma za utafiti na huduma za viwanda; kuanza shughuli za ujenzi katika mradi wa Umeme wa Makaa ya Mawe Mchuchuma na Kiwanda cha Kufua Chuma cha Liganga; na kuendeleza Shamba la Miwa na kuendelea na ujenzi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi.
(ii)          Kufungamanisha Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Watu
Serikali itaendelea: kuimarisha upatikanaji wa elimu na huduma za ustawi wa jamii; kuboresha huduma za afya ikiwemo kuongeza upatikanaji  wa dawa muhimu na vifaa tiba kwa ajili ya kutoa huduma za tiba kwa wananchi; kuboresha upatikanaji wa huduma za maji safi na salama vijijini na mijini; kuimarisha usimamizi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi; kuimarisha shughuli za utawala bora ikiwemo Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020; kuendelea kutekeleza sera ya elimumsingi bila ada, kusomesha wataalam na mafundi wengi wenye fani na ujuzi maalum; nakuongeza upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

(iii)        Ujenzi wa Mazingira Wezeshi kwa Uendeshaji wa Biashara na Uwekezaji:
Kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu, ikijumuisha miundombinu ya nishati, usafirishaji (reli, madaraja, barabara na bandari), usafiri wa anga na usafiri wa majini (magati, meli na vivuko); kuendelea kuboresha mazingira ya biashara ili kuvutia uwekezaji ikiwemo kutekeleza Blue Print; na kuimarisha mfumo wa ugawaji na usimamizi wa ardhi. Miradi itakayopewa msukumo ni: Mradi wa kufua umeme wa Maji wa Julius Nyerere - MW 2,115; ujenzi wa reli ya kati ya Standard Gauge; kuboresha Shirika la Ndege Tanzania; na ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania).

(iv)        Kuimarisha Usimamizi na Utekelezaji wa Mpango
Katika mwaka 2020/21, utekelezaji  Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21) unatarajiwa kukamilika ambapo Serikali itaandaa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26) kwa kuzingatia matokeo ya tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Miaka Mitano.

Miradi ya Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

31.         Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21, Serikali itaendelea kuimarisha mazingira wezeshi ili kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja wa sekta binafsi au kwa utaratibu wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika maeneo ya kipaumbele. Baadhi ya miradi itakayotekelezwa kwa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ni pamoja na: Mradi wa uzalishaji wa Dawa Muhimu na Vifaa Tiba; Kusambaza Gesi Asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara; ujenzi wa Hoteli ya Nyota Nne na Kituo cha Kibiashara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere; Ujenzi wa Reli ya standard gauge ya Mtwara – Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na Liganga; Ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika Chuo cha Elimu ya Biashara (kampasi ya Dar es Salaam na Kampasi ya Dodoma) na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP - Dodoma); Uendeshaji wa Huduma ya Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka Jijini Dar es Salaam Awamu ya Kwanza; na Ujenzi wa Reli ya standard gauge ya Tanga - Arusha – Musoma pamoja na matawi ya Engaruka na Minjingu.
32.         Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu Maeneo ya Kipaumbele kwa mwaka 2020/21 yapo katika Kitabu cha Mapendekezo ya Mpango (Sura ya Nne).


H.           HITIMISHO

33.         Mheshimiwa Spika,kwa niaba ya Serikali, napenda kuahidi kuwa maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango yatazingatiwa kikamilifu katika uandaaji wa  Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2020/21. Aidha, Mapendekezo haya yatazingatiwa na Maafisa Masuuli wote wakati wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mafungu yao. Kutokana na Mapendekezo ya Mpango huu, Serikali itaainisha na kuandaa mipango ya kisekta, kitaasisi na kimaeneo ambayo tunaamini kuwa utekelezaji wake utachochea ujenzi wa uchumi wa viwanda, mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu. Hivyo, Maafisa Masuuli wa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi na Mashirika ya Umma wanaelekezwa kuzingatia maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mapendekezo ya Mpango na ushauri makini wa Bunge wakati wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mafungu yao kwa Mwaka 2020/21. Vile vile, Maafisa Masuuli wanaelekezwa kuzingatia kikamilifu maelekezo yote yaliyopo kwenye Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2020/21 na kusimamia Sheria ya Bajeti, SURA 439 na Kanuni zake.

34.         Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia napenda kupongeza kwa dhati hatua zilizochukuliwa na Ofisi ya Bunge chini ya uongozi wako kupunguza matumizi kwa kuanza kutekeleza mfumo wa Bunge Mtandao (e-parliament) na kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zinatumika kuchapisha nyaraka mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya Waheshimiwa Wabunge.  Natoa rai kwa Wizara na Taasisi zote za Umma kufuata mfano huu mzuri.

35.         Mheshimiwa Spika,baada ya maelezo hayo naomba sasa Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kuishauri Serikali kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2020/21.

36.         Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

Miaka Minne Ya Rais Magufuli Madarakani | Tunaendelea Kujimwambafai Na Mafanikio Makubwa Ya Serikali Yake

$
0
0
Makala Imeandaliwa na; Robert PJN Kaseko
Leo ni Kumbukumbu Muhimu sana  Kwetu Watanzania tokea Kipenzi Chetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt J.P. Magufuli na Makamu wake Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan waingie Madarakani Mnamo tarehe 05 Novemba, 2019. Na leo Wametimiza Miaka Minne (4) ya Utumishi wao.

Kama Taifa, tunajivunia Utumishi wao Uliotukuka na Kwa Muda Mchache Tumepata Mafanikio Makubwa sana Katika Kuitekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Rais Magufuli na Serikali yake wamefanya Kazi Kubwa sana ya Kufanya Mapinduzi Makubwa Katika Sekta zote na Kuleta Maendeleo zaidi ya Matarajio ya wengi ( Beyond Expectations ). 

Baada ya Rais Magufuli Kuingia Madarakani pamoja na Serikali yake wengi walibeza na kusema tulishazoea na  hawana jipya, wapiga madili, Mfumo wa CCM na Serikali utambana hata kama alikuwa Mtendaji Mzuri Katika Nafasi ya Uwaziri, akiwa Rais hawezi kufanya lolote eti ni sawa na Mtu yuleyule
 
Mzee Mwenye slogan yake ya Hapa Kazi alipoanza Kupindua Meza na Kuchomoa betri ameushangaza Ulimwengu. Walisema nguvu ya soda lakini mpaka leo anatembea Katika Kasi ileile, Hadi leo Kazi Kubwa imefanyika Katika Taifa letu, Miradi Mikubwa imeendelea Kutekelezwa Nchini.

Naomba nikutajie sehemu ya Utekelezaji huo;
Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere ( Megawati 2115 ) Stiggler's Gorge -  Mto Rufiji ( Utagharimu zaidi ya Trilioni 6.5 hadi kukamilika kwake Ikiwa ni Kodi za Watanzania ),  Serikali imefanya kazi kubwa ya Kulihuisha na Kuliimarisha Shirika la Usafiri wa Anga ( ATCL ) Ikiwa ni Moja ya  Mikakati Muhimu wa Kuimarisha Uchumi Kupitia Sekta za Usafiri wa Anga na Utalii. 

Jumla ya Ndege Saba Mpya zimenunuliwa Kwa Mabilioni ya Pesa yatokanayo na Kodi za Watanzania; Bombardier 3, Airbus 2 na Dreamliners 2 ) 💪🏼 Ndege zote zimekodishwa Kwa Shirika letu la ATCL na Biashara inaendelea vizuri sana.

Tunajivunia Mapinduzi Makubwa yaliyofanywa na Rais Magufuli na Serikali yake Katika Sekta ya Afya ambapo Ule Mpango wa Kujenga Vituo Vya Afya Kila Kata Nchini, Hospitali za Wilaya/Halmashauri  na Rufaa Kwa maeneo yasiyo na Huduma hizo unaendelea Kutekelezwa kisawasawa. Zaidi ya Vituo Vya Afya  300  Vimejengwa na Baadhi kukarabatiwa/ Kuboreshwa. 

Hospitali za Halmashauri/ Wilaya 67 Zimejengwa nk. Mradi wa Ujenzi wa Mradi wa Barabara za Juu/ Daraja la Juu Ubungo ( Ubungo Interchange ) Mradi utakao gharimu zaidi ya Bilioni 200 Pesa za Kitanzania na Maendeleo ya Mradi ni zaidi ya 50% - Mbioni Kukamilika, Mradi wa Ujenzi wa Daraja Ziwa Afrika Mashariki ( Ziwa Victoria ) litakalo unganisha Mikoa ya Geita na Mwanza ( Busisi - Busisi ) Kilomita 3.2, Mradi huu umepangwa kugharimu Bilioni 699.9 Pesa za Kitanzania hadi Kukamilika kwake, Juzi nimepita Pale Mto wami Kazi ya Ujenzi wa Mradi wa Daraja la Mto Wami Inaendelea. 

Jumla ya Bilioni 71.4 Pesa za Kitanzania zitatumika Kukamilisha Mradi huu ambapo pia Barabara yenye urefu wa Kilomita 4.3 ya Lami itajengwa kila upande wa Daraja hili la Mto Wami kutokea hapo.( Ni kazi tuu hakuna kulemba 💪🏼).

 Tusisahau Miradi Mikubwa ya Kuimarisha Miundo mbinu wezeshi  ya Uchumi inayoendelea kutekelezwa na Serikali hii ya Awamu ya Tanu Chini ya Dkt. John Magufuli. 

Mfano Serikali kupitia TARURA na TANROADS imeendelea Kujenga Barabara za Lami zenye Ubora wa Hali ya Juu Kama ule Mradi wa Upanuzi Barabara ya Kumara - Kibaha kwa Njia Sita  ( 19.2 Kilomita ) Mradi utakaogharimu zaidi ya   Bilioni 140.44 Pesa za Kitanzania, Zile Barabara za Arusha za Mchepuo ( Arusha By-Pass 42.2 Kilomita ) na Ujenzi wa Barabara za Njia Nne Kutokea Pale Ngaramtoni hadi USA River 14.1 Kilomita na   ambazo zimekamilika na zinatoa Huduma bora kabisa haja Jijini Kwetu Arusha. Zaidi ya Bilioni 85 zimetumika Kuboresha Maisha ya Wananchi wa Arusha.

 Ebwana Tusisahau Miradi Mikubwa ya Maji inayotekelezwa na Serikali yetu tukufu Nchini Kote, Mfano mmoja miongoni mwa mingi ni huu Mradi wetu Mkubwa wa Maji  Unaotekelezwa hapa Arusha utakaogharimu Bilioni 520 Pesa za Kitanzania. 

Nimalizie kwa kutaja iliyofanyika Katika Kufanya Mapinduzi Makubwa Katika Sekta ya Nishati na Madini. Mabadiriko Makubwa ya Sharia ya Madini yamefanywa na Bunge letu Tukufu ili kuhakikisha Madini yetu yanatunufaisha Watanzania na niseme tu site tulishuhudia Sakata la Makinikia ambapo hadi mwisho Wahusika tamka Kuilipa Serikali yetu Mabilioni ya Pesa kama fidia dhidi ya Unyonyaji Mkubwa uliofanywa na Mabeberu.

Yapo mengi yaliyotekelezwa na Serikali ya Rais Magufuli toka Rais wetu ameingia Madarakani  Novemba 05, 2015. 

Kama Taifa Tumepiga hatua kubwa sana Kimaendeleo. Uchumi wetu umeendelea Kukua Kwa Kasi sana na Mambo yanaonekana Kwa Macho.

Watanzania tusidanganywe na Upotoshaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya watu. Hawana lolote zaidi ya Kutuvuruga na Ukweli ni Kwamba Watanzania tulikuwa na Kiu kubwa ya Kuona siasa zetu zinabadirika na Kuwa siasa zinazojikita katika Kuleta Maendeleo kwa Watanzania na Kutatua Changamoto na Kero mbali mbali zinazo wakabili Watanzania, na Mungu ametujalia Kumpata Rais ambaye akiahidi anatekeleza Kwa Vitendo, anachapa Kazi tu. 

Anasimamia Vizuri sana Ukusanyaji wa Mapato na Matumizi ya Serikali. Anasimamia VIZURI sana na kwa Uaminifu Mkubwa Raslimali za Taifa letu na Kuhakikisha Zinawanufaisha Watanzania wa Sasa na Vizazi Vijavyo.

Rai yangu kwa Watanzania wenzangu; Tumshukuru Mungu kwa Kutupatia Kiongozi Mzalendo, Mchapa Kazi, Msikivu katika Kusikiliza na Kutatua Kero na Changamoto za Wananchi wake, asiyetishika wala Kuyumbishwa, Jasiri na Mwenye hofu ya Mungu. Tuendelee Kumuombea Rais wetu Afya njema, Maisha Marefu na nguvu kubwa zaidi ya Kufanya Makubwa zaidi ya Haya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MMBARIKI RAIS MAGUFULI NA WASAIDI WAKE WOTE, AMEN.

Robert PJN Kaseko
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha.
Novemba 05, 2019.

Basi la kampuni ya Majinjah Lapata Ajali

$
0
0
Basi la kampuni ya Majinjah ambalo lilikuwa safarini kutoka Kyela kuelekea Dar, limepata ajali maeneo ya Kitonga leo.
Mashuhuda wanadai chanzo cha ajali ni kufeli kwa breki za basi hilo.
RPC Iringa amesema tayari RTO ameelekea eneo la tukio na baadae watatoa taarifa kwa undani.

Nafasi 200 za Kazi Zilizotangazwa , Tazama Hapa

$
0
0
Hapa nimekuwekea mkusanyiko wa Nafasi mbalimbali za Kazi Zilizotangazwa Wiki Iliyopita na Wiki Hii. Usisahau kushare na rafiki yako anayetafuta kazi
  1. Junior Branch Administrator and IT Support at AccessBank Tanzania (ABT)
  2. Customer Service Manager Job Opportunity at Yara
  3.  Sales Agents Job at Jubilee Insurance
  4. Grant Coordinator Job at Norwegian Refugee Council (NRC)
  5. Global Procurement Associate Job at One Acre Fund
  6. Procurement Officer Job at HelpAge International
  7. Programme Partnership Officer Job Opportunity at Oxfam Tanzania
  8.  Job Opportunity​ at CRDB Bank | Senior Specialist; Financial Literacy
  9. Job Vacancy at CRDB Bank | Manager; Strategic Partnership
  10. New Government Job | Senior Corporate Communications Officer II at UCSAF
  11. Job Vacancy at Precision Air | Reservation & Ticketing Sales Agent
  12. Job Vacancy at Precision Air | Sales Manager Northern & Lake Zone
  13.  Job Vacancy at Standard Chartered Bank | Credit Analyst, Global Subsidiaries
  14. New Job Opportunity | Sales Capability Manager – Serengeti Breweries Limited
  15. New Job Opportunity | Marketing Manager, Spirits – Serengeti Breweries Limited 
  16. Nafasi 61 za Kazi Shirika la Hifadhi ya Taifa TANAPA | Elimu ni Kuanzia Cheti/Diploma/Degree | Mwisho Tarehe 30 Mwezi Huu 
  17. Jobs at UNICEF | Individual Consultant -Evaluation of the Zanzibar Social Protection Policy  
  18. Project Finance Assistant Job at Sightsavers Singida, Tanzania
  19. Project Assistant Job at Sightsavers Singida, Tanzania 
  20. Compliance Manager at IntraHealth International Mwanza, TZ 
  21. Research and Innovation Hub Coordinator Job at International Rescue CommitteeDar es Salaam, TZ 
  22. Electrical Manager Job at Radar Recruitment Tanzania 
  23. Job Opportunity at VodacomTanzania, Network Director 
  24. Monitoring, Evaluation, and Learning (MEL) Team Lead – Tanzania PS3+ 
  25. Job Opportunity at Abt Associates, Communications Team Lead 
  26. Jobs in Tanzania 2019 : New Job Opportunities at Mom Easy Company Limited | Sales Officers (15 Post) 
  27. Job Opportunity at Bariadi District Council | Mtendaji wa Kijiji Daraja la III 
  28. Jobs in Tanzania 2019: New Job Vacancies at Oxfam Tanzania| Donor Contracts Coordinator (INT5881) 
  29. Jobs in Tanzania 2019: New Job Vacancies at Oxfam Tanzania| Warehouse Officer (INT5995) 
  30. Technical Manager Job at Mbeya Water Supply and sanitation Authority 
  31. Job Opportunity at PCI Tanzania ,Documentation Specialist 
  32. Job Opportunity at Pact Tanzania,Gender and Youth Officer 
  33. Job Opportunity at Pact Tanzania, Technical Services Coordinator-Case Management 
  34. Job Opportunity at Pact Tanzania, Technical Services Coordinator-Bi-Directional Referrals and Linkages 
  35. Job Opportunity at Pact Tanzania, Logistic Assistant/Driver 
  36. Field Assistant Grade Ii Job at Tropical Pesticides Research Institute TPRI 
  37. Job Opportunity at UONGOZI Institute, Research And Policy Department (Intern) 
  38. Job Opportunity at UONGOZI Institute, Finance And Administration Department (Intern)

==Kwa nafasi zingine za Kazi zaidi ya 5000, <<INGIA HAPA>.

Freeman Mbowe Aanza Kujitetea Mahakamani........"Sikuwepo Kwenye Maandamano. ni Hisia tu"

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hakuwepo kwenye maandamano ya wafuasi wa chama hicho yanayodaiwa kusababisha kifo cha Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (N.I.T) Akwilina Akwelini.

Mbowe ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akitoa utetezi wake katika kesi inayomkabili na viongozi wenzie 8 wa CHADEMA.

Mbowe alitoa ushahidi wake akingozwa na wakili wa utetezi, Peter Kibatala ambapo  amedai hakuwepo eneo la maandamano na kama ilitolewa amri ya Polisi yeye hawezi kukataa kutawanyika kwa sababu hakuwepo, hivyo ni hisia za Polisi tu zimeeleza kwamba alikuwepo.

Amedai kuwa baada ya kumaliza mkutano wa kufunga kampeni katika Uwanja wa Buibui Mwanyamala aliondoka uwanjani hapo akiongozwa na Askari Polisi kuelekea Makao Makuu ya CHADEMA Kinondoni.

Amedai siku hiyo wahudhuriaji wa CHADEMA wakiwa njiani walikutana na wahudhuriaji wa CCM katika makutano ya barabara ya Morocco na Mwananyamala wakiwa na mgombea wao wakisindikizwa na ngoma aina ya Mdundiko.

Mbowe amedai kuwa wanachama hao wa CHADEMA walikuwa wakiongozwa na Polisi kuelekea barabara ya Morocco ambapo yeye hakujua kilichoendelea nyuma kwani aliendelea na safari yake ya kuelekea Makao Makuu ya CHADEMA.

Akizungumzia kufikishwa kwake Mahakamani Mbowe amedai kuwa kwa mara ya kwanza alipokea wito wa kuitwa Polisi kupitia mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Amedai kuwa Kamanda huyo wa Polisi alitoa wito kwa viongozi wa CHADEMA kuripoti polisi kuhusiana tukio hilo la maandamano.

Pia amedai kuwa alipata taarifa kuhusu kifo cha Akwilina Akwiline aliyepigwa risasi katika maandamano hayo kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari na kwamba Polisi inawashilikia askari kuhusu tukio hilo.

Mbowe amedai kuwa hajawahi kula njama na washtakiwa wenzake bali waliitwa kwa nyakati tofauti kwenda Polisi.

Mbali na Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.

Baada ya kutoa ushahidi huo, upande wa utetezi ukaomba shauri hilo liahirishwe hadi siku nyingine kwa sababu mshitakiwa wa Tisa, Ester Bulaya anaumwa.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 8, 2019.

Wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

CHADEMA Kukutana Kwa Dharura Baada ya Baadhi ya Wagombea Wao Kuenguliwa Uchaguzi Serikali za Mitaa

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA , kimewataka Wagombea wa chama hicho ambao wameenguliwa  kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa madai kuwa wamekosea kujaza fomu zao kukata rufaa.

Akiongea na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema mbali na hilo ameeleza kuwa wataitisha vikao vya dharura kujadili hali hiyo ambayo wamedai kuwa imejitokeza katika maeneo mengi nchini.

“Hadi sasa tunazungumza hapa, wagombea wote wa Chadema Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Ngala (Kagera), Jimbo la Ubungo (Dar es Salaam), Jimbo la Mbeya Mjini na Busokelo wote  na maeneo mengine wameondolewa. Wanaenguliwa na wasimamizi hawatoi sababu licha ya kanuni kuwataka kufanya hivyo.

“Tunajiuliza hivi  mitaa 192 yote yaani hajakosekana hata mgombea  mmoja hata wale waliokuwa wenyeviti wakaamua kugombea tena, wameshindwa kujaza fomu?,” amedai Mrema.


Amesema kutokana na hali hiyo, Chadema kimeitisha vikao hivyo vitakavyoanza kesho kujadili mwenendo huo na kutoa msimamo wa chama na hatua watakazozichukua kutokana na sintofahamu hiyo.

Aliyekuwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange waachiwa kwa dhamana

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana aliyekuwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange maarufu ‘Kaburu’.

Septemba mwaka huu, mahakama hiyo ilitoa uamuzi wa kuwafutia mashtaka mawili ya utakatishaji wa fedha Aveva aliyekuwa rais wa simba na makamu wake Nyange, ambapo washtakiwa hao walitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh30 milioni kila mmoja, lakini upande wa Serikali ulikata rufaa kupinga dhamana hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba ameyatupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Serikali ya kupinga uamuzi huo.

Baada ya Hakimu Simba kutoa uamuzi huyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Shadrack Kimaro alidai kuwa hawajaridhika na uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo, hivyo wanakwenda kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

“Uamuzi uliotolewa sijaridhika nayo, hivyo naenda leo hii kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania,” alidai Kimaro.

Baada ya Kimaro kueleza hayo Hakimu Simba alisema hata kama wanakata rufaa haitengui uamuzi wa mahakama hiyo na ndipo wakili huyo alipoieleza mahakama kuwa anajiondoa katika kesi hiyo, kisha Wakili Kimaro alinyanyuka na kutoka nje huku mahakama ikiwa inaendelea.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 12, 2019 itakapofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

VIDEO: Maagizo ya Waziri Jafo kwa Wagombea Walioenguliwa Uchaguzi Serikali za Mitaa

$
0
0
Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo ameagiza wagombea wa uchaguzi wa Serikali za mitaa walioenguliwa kinyume na utaratibu warejeshwe kwa haki ili kujenga Demokrasia. Msikilize hapo chini.

Nafasi 18 za Kazi Chuo cha Saint John, Nafasi za Kazi Ubalozi wa Marekani Tanzania, Oxfam Tanzania, HelpAge, Shirika la Wakimbizi Duniani Na Zingine

$
0
0
==>>World Wide Fund for Nature

👉Deadline; November 15, 2019 

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   

==>>Nafasi za Kazi International Rescue Committee (IRC) Tanzania

👉Wanataka Procurement Officer – Goods & Services


Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   

==>>Nafasi za Kazi Kazini Kwetu


👉Wanataka Commercial Officer
👉Deadline; November 10, 2019

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  

==>>Nafasi 18 za Kazi St John’s University of Tanzania (SJUT)
👉Deadline; November 11, 2019 

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  
 
==>>Nafasi za Kazi Railway Children Africa (RCA)

👉Deadline; 14 November 2019

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  
 
==>>Nafasi za Kazi Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania

👉Deadline; November 19,2019

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   

==>>Nafasi za Kazi Oxfam Tanzania

👉Deadline; November 15,2019

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   

==>>Nafasi za Kazi HelpAge International

👉Deadline; November 11,2019

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  

==>>Tangazo la Nafasi za Kazi Umoja wa Mataifa Katika Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)

👉Deadline ni; November 11, 2019
👉Kituo cha Kazi ni Kigoma,Tanzania

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  

 ==>>Shirika la REPOA Limetangaza Nafasi Mpya za Kazi

👉Deadline ni; November 11, 2019
👉Wanawake Watapewa Kipaumbele zaidi

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  

==>>Nafasi Mpya za kazi  Iringa katika shirika la Kimataifa FHI 360 Tanzania
👉Wanataka watu wa fani Mbalimbali
👉Deadline ni; November 23, 2019 

Kujua jinsi ya kutuma maombi, <<Bofya Hapa>> 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

Kuangalia Nafasi Zingine Mpya Zilizotangazwa wiki hii <<INGIA HAPA>> 

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano November 6

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo Yabainisha Mkakati Wa Kudhibiti Maradhi Yanayoikumba Mimea Ya Mipapai Nchini

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imefanya utafiti na kugundua kuwa ugonjwa wa Ubwili unga ndio unaoathiri mipapai kwa kiwango kikubwa.

Baada ya kugundulika ugonjwa huo, Wizara ya kilimo imechukua hatua za kuudhibiti kwa kutumia viuatilifu vyenye viambata vya croripynfos (udhibiti wa kwenye udongo), Profenophos na Dichlorovosch (udhibiti kwenye majani).

Aidha, njia nyingine ya uthibiti ni kwa kutumia mbinu bora za kilimo (Cultural Control) kwa kupanda miche wakati wa kiangazi ili mimea isishambuliwe ikiwa michanga, kupalilia shamba kwa wakati na kug’olea miche iliyoathirika na utumiaji wa wadudu marafiki (Biological Control).

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba ameyasema hayo jana tarehe 5 Novemba 2019  bungeni Jijini Dodoma Wakati akijibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum Zainabu Mussa Bakari aliyetaka kufahamu serikali imechukua hatua gani kudhibiti maradhi katika mimea ya mipapai nchini ambayo yanahatarisha kupotea kwa mimea hiyo.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kufuata kanuni bora za kilimo ili kuepuka magonjwa mbalimbali yanayoweza kuathiri mimea ukiwemo mpapai.

Serikali kupitia Kituo cha Utafiti cha TARI-Horti TENGERU imeendelea kufanya utafiti magonjwa na wadudu wanaoathiri mazao ya bustani ikiwemo mipapai. Utafiti huo umegundua kuwa ugonjwa wa Ubwili unga unaoathiri mipapai unaosababishwa na vimelea vya kuvu (fungus) vijulikanavyo kitaalam kama Oidium caricae papaya.

Ameongeza kuwa Mipapai haiwezi kupotea nchini kwa kuwa tayari njia za kudhibiti      magonjwa na wadudu wanaoshambulia mimea hiyo zipo.

kadhalika, Wizara itaendelea kuwaelimisha wakulima na wadau mbalimbali juu ya udhibiti wa ugonjwa na wadudu wanashambulia mimea na mazao ikiwemo mipapai ili kuongeza uzaliahaji na tija.

 MWISHO

TAKUKURU Mkoa Wa Dodoma Yamnasa Afisa Mtendaji Kwa Kosa La Kushawishi Kupokea Rushwa Kutoka Kwa Mfugaji

$
0
0
Na.Faustine  Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini [TAKUKURU]  mkoa wa Dodoma inamshikilia  Bw.David Daud Tengeneza mwenye umri wa  miaka 50 ambaye ni afisa mtendaji katika kijiji cha Mapanga kata ya Itiso wilaya ya Chamwino  kwa kosa la kushawishi na kujaribu kupokea rushwa   kinyume na kifungu cha sheria Na.15[1]a cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa  Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2018.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake jijini Dodoma  Nov.5,2019,Mkuu wa TAKUKURU mkoani hapa Bw.Sosthenes Kibwengo amesemaTAKUKURU imekuwa ikipokea tuhuma kadhaa juu ya afisa mtendaji huyo kujihusisha na vitendo vya rushwa .
 
“Mtendaji huyu amekuwa na tuhuma mbalimbali za rushwa ambapo TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imekuwa ikifuatilia kwa kina na safari hii arobaini yake imewadia”amesema.
 
Bw.Kibwengo amefafanua kuwa “,baada ya kupokea taarifa mbili tofauti dhidi ya mtuhumiwa  wiki iliyopita tuliamua kufuatilia  mojawapo ambapo uchunguzi ulithibitisha kwamba ameomba rushwa ya shilingi laki tatu[300,000/=]kutoka kwa mtoa taarifa wetu ambaye ni mfugaji.
 
Tarehe 30 Oktoba ,2019 afisa wetu aliambatana na mtoa taarifa  hadi ofisini kwamtuhumiwa ambapo alielekeza apelekewe fedha hizo ndipo ampatie barua  ya kumruhusu  kuingiza kijijini Mapanga  ng’ombe arobaini na nane[48] aliowatoa kijiji jirani cha Segala  la sivyo angemchukulia hatua za kisheria  kwa kutokuwa na kibali.”
 
Mkuu huyo wa TAKUKURU ameendelea kusema kuwa,kutokana na uzoefu wa Mtuhumiwa katika vitendo vya rushwa ,mtuhumiwa alipomwona mtoa taarifa akiwa na mtu mwingine alianza kumhoji huku akisisitiza kuwa yeye ni mzoefu  na mara kadhaa amekoswa na TAKUKURU,hivyo kumtaka akaweke fedha hizo nje ya chooni lakini hakuacha fedha hiyo ya Rushwa na walipoondoka ,mtuhumiwa akaenda chooni kuangalia  na akagundua kuwa hongo yake haipo.
 
Mtuhumiwa aliamua kumfuata mtoa taarifa na kumtaka arudi na akahojiiweje hongo haipo  naye akamweleza hawezi kuacha fedha  bila kupewa barua,ndipo akaelekezwa aiweke chini ya jiwe  lililo chini ya mti  nje ya Ofisi ya mtuhumiwa na aingie ndani kuandikiwa barua.
 
Bw.Kibwengo ameendelea kusema,baada ya kuweka fedha hiyo chini ya jiwe,mtoa taarifa  aliingia ndani ya ofisi lakini mtuhumiwa hakumwandikia barua kwa kisingizio  cha kuisahau mihuri nyumbani na TAKUKURU imemkamata na atafikishwa mahakamani.
 
Hivyo ,Bw.Kibwengo amewakumbusha wananchi wote kuwa ni kosa la jinai kushawishi  na kujaribu kuchukua rushwa  na wananchi wanapokutana na hali hizo watoe taarifa mapema kwa TAKUKURU.
 
Pia,Bw.Kibwengo amewakumbusha watumishi wa Umma kwamba mkono wa sheria ni Mrefu  hivyo ukijihusisha na uhalifu ipo siku ya arobaini itafika na fedheha itakuja ni vyema kuzingatia Maadili ya kazi kwani Rushwa hailipi.

Makubaliano yafikiwa kati ya serikali na waasi wa Yemen

$
0
0
Serikali ya Yemen inayotambulika kimataifa na wapiganaji wanaotaka kujitenga upande wa kusini wametia saini makubaliano ya kugawana madaraka na kumaliza mapigano baina ya makundi hayo. 

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman alitangaza kufikiwa makubaliano hayo katika televisheni ya taifa jana, akisema ilikuwa hatua muhimu kufikisha mwisho vita vya miaka minne nchini Yemen. 

Makubaliano yanayoitwa ya Riyadh , yanakamilisha mwezi mmoja wa mazungumzo ya moja kwa moja ya amani kati ya serikali hiyo inayotambuliwa kimataifa, ikiongozwa na rais Abed Rabbo Mansour Hadi na wapiganaji wanaotaka kujitenga wakiungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu wanofahamika kama baraza la mpito la kusini mwa Yemen STC. 

Pande hizo mbili zimekuwa zikipigana licha ya kuungana dhidi ya majeshi ya wahouthi yanayoungwa mkono na Iran, ambayo yanashikilia mji mkuu Sanaa, pamoja na miji mingine mingi nchini Yemen.

-DW

Mbwana Samatta Avunja Rekodi....Ni Baada ya kuifunga timu kubwa duniani ambao ni mabingwa wa Ulaya, Liverpool.

$
0
0
Mshambuliaji kinara wa klabu bingwa ya Ubelgiji KRC Genk na nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta jana usiku ametimiza ndoto yake ya kuifunga timu kubwa duniani ambao ni mabingwa wa Ulaya, Liverpool.

Goli hilo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mpira wa miguu nchini Tanzania.

Hata hivyo, matokeo ya mwisho ya mchezo huo wa Klabu Bingwa Ulaya yalikuwa mabaya kwa Genk kwa kulazwa kwa goli 2-1.

Samatta, aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona mpaka wavuni katika dakika ya 40 ya mchezo.

Mshambuliaji huyo ambaye ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano hiyo mikubwa zaidi ya vilabu barani Ulaya tayari ameshapachika magoli mawili katika mechi nne. 

Katibu Mkuu TAMISEMI Ataka Sheria, Kanuni na Miongozo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019 Zifuatwe

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandisi Joseph Nyamhanga amewataka viongozi na wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ngazi za Mikoa, Wilaya na Halmashauri kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa karibu Kanuni, Sheria, na Miongozo mbalimbali iliyowekwa ili uchaguzi huo ufanyike katika mazingira ya amani na uwe huru na haki.

Katibu Mkuu ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akielezea hatua inayofuata baada ya zoezi la uchukuaji na urejeshwaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kukamilika hapo jana ambapo amesema zoezi linaloendelea kwa tarehe 5 Novemba, 2019 ni Uteuzi wa Wagombea katika nafasi za Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa na nafasi ya Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji na Wajumbe wa Kamati za Mitaa.

Amesema kuwa kuanzia tarehe 5 hadi 6 Novemba, 2019 ni kipindi cha watu walioomba kuteuliwa kuwa wagombea au wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ambao hawajaridhika na uteuzi uliofanywa na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuwasilisha pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea.

 “Nitoe maelekezo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kusimamia kwa weledi zoezi la uwasilishaji wa pingamizi na kutoa uamuzi wa haki kuhusu pingamizi hizo za uteuzi wa wagombea” amesisitiza Katibu mkuu.

Mhandisi Nyamhanga ameseama kwamba baada ya Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kupokea pingamizi na kutoa uamuzi, waombaji au wagombea ambao hawataridhika na uamuzi wa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi watakuwa na haki ya kukata rufaa kati ya tarehe 5 hadi 8 Novemba,  2019 kwenye Kamati za Rufani zilizoanzishwa katika kila Wilaya nchini.

Aidha, Kamati za Rufani zitatoa uamuzi kuhusu rufaa mbalimbali zilizowasilishwa kwake kati ya tarehe 5 na 9 Novemba, 2019.  Vilevile, mtu yeyote ambaye ameomba kuteuliwa kuwa mgombea au mgombea ambaye hajaridhika na uamuzi wa Kamati ya Rufani atakuwa na haki ya kufungua kesi katika Mahakama ya Wilaya ndani ya muda wa siku 30 baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.

Mhandisi Nyamhanga amevikumbusha Vyama vya Siasa ambavyo vitashiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019 kuhakikisha vinawasilisha ratiba za mikutano ya kampeni kwa Wasimamizi wa Uchaguzi tarehe 10 Novemba, 2019 kama ilivyooneshwa kwenye ratiba ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Je, Una Hofu na Usalama wa Namba Yako ya Simu?? | Tazama Hapa Jinsi ya Kujitoa au Kufuta namba yako Kwenye App ya TrueCaller

$
0
0
Kabla ya kuangalia namna ya kujitoa kwenye huduma hii, kwanza ningependa tuanze kwa kutoa ufafanuzi Truecaller ni nini?

TrueCaller ni app maarufu duniani inayowawezesha watumiaji wake kutambua majina ya watu au makampuni wanayotaka kuwasiliana nayo au yanayowapigia simu wao.

Kwa kifupi, mtumiaji wa TrueCaller anaweza kufahamu jina la mtu au kampuni  hata kama hajam save kwenye simu yake kabla ya kupiga au kupokea simu.

Mfumo wa data wa TrueCaller ni mfumo ambao  watumiaji wake wanasaidiana kupeana taarifa za data za watu walio kwenye simu zao.

Unapopakua programu hiyo kutoka kwenye Playstore/App Store kisha ukaingia ndani kwa kuweka email na password yako, basi utakuwa umeruhusu wahusika kuona namba za watu ulionao kwenye kifaa husika na kuhifadhi taarifa hizo  kwenye kompyuta zao za kutunza kumbukumbu (servers).

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   

Pamoja na uzuri wa TrueCaller, yaweza kuwa imefika mahali sasa unawaza usalama wa namba yako ya simu au data zako na taarifa zako binafsi  na hivyo unatamani kujitoa au kufuta kabisa namba yako kwenye Mfumo wa TrueCaller

Leo tutakuelekeza namna ya kujitoa maana yawezekana hata kama   bado haujajiunga na app hiyo ila namba yako tayari imeunganishwa kwenye mfumo wa TrueCaller kupitia mtu mwingine mwenye number yako ya simu.

Kuna njia mbili za  kuiondoa namba yako kwenye mfumo wa TrueCaller, hii inategemea kama tayari ulijiandikisha kwenye huduma hii au haujajiandikisha lakini kumbuka kama kuna  mtu anayetumia app hii ya TrueCaller  na  ana namba yako basi  taarifa zako zimeingizwa pia kama alitoa 'access/Kibali' ya contacts list

Jinsi ya kujitoa au kutoa namba yako kutoka kwenye app ya TrueCaller

Kwa wale wenye akaunti za TrueCaller
1.Fungua app ya TrueCaller, nenda kwenye alama ya nukta tatu upande wa kushoto juu.
2.Kisha nenda Settings, kisha About, na hapo utaona chaguo la ‘Deactivate Account’ yaani futa akaunti…
3.Ata ukishafuta akaunti yako, yaani ‘deactivate account’ bado namba yako inaweza kuwa kwenye data za TrueCaller. Na hapa ndio inabidi uchukue hatua inayofanana na wale ambao hawana akaunti ya TrueCaller.
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬   

Kwa wale wasio na akaunti ya TrueCaller au wamefuta/deactivate akaunti zao

1.Hatua inayofuata ni kuondoa namba kwenye mfumo wa kompyuta (servers) za huduma ya TrueCaller.
2.Nenda kwenye tovuti ya TrueCaller huduma ya kuondoa namba (Unlist)
3,Ukifika hapa andika namba yako ya simu, chukua hatua za kuonesha ya kwamba wewe ni binadamu (captcha) na kisha bofya ‘Unlist’

==>>Kama Bado Hujaelewa <<BOFYA HAPA>> Kusoma maelezo Kwa Kina Zaidi

Waziri wa Nishati, Medard Kalemani Atoa ONYO Kwa mameneja na wakandarasi wanaotoza Wananchi Gharama ya nguzo za umeme

$
0
0
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani ametoa onyo kwa mameneja na wakandarasi wanaotoza nguzo za umeme wananchi na kuwataka waachane na tabia hiyo mara moja kwakua serikali imegharimia nguzo hizo kwa asilimia 100.

Waziri Kalemani ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Novemba 6, katika kipindi cha maswali na majibu alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Halima Bulembo aliyetaka kujua serikali inazungumzia vipi kadhia ya kulipishwa nguzo za umeme ambayo wananchi wa Mkoa wa Kagera wamekuwa wakikumbana nayo

Akijibu hoja hiyo Waziri Kalemani amesema serikali haitaendeleakufumbia macho suala hilo na kwamba yeyote atakaekamatwa atachukuliwa hatua za kisheria bila kujali cheo chake.

“Yapo maeneo bado wakandarasi na mameneja wa Tanesco wanaendelea kutoza nguzo wateja, ninaomba nitoe tamko kali sana kwamba ni marufuku kutoza nguzo kwa wateja wote, awe mkandarasi, Meneja wa Tanesco au kibarua na hii ni kwasababu serikali imegharamia kwa asilimia 100,” amesema Dk. Kalemani.

Aidha amesema serikali imekuwa ikipeleka umeme katika maeneo yote hasa vijijini lakini baadhi ya taasisi zimekuwa hazilipiwi na hivyo amewataka wamiliki wa taasisi hizo kuhakikisha wanalipa kiasi cha Sh 27,000 ili taasisi zote zipelekewe umeme.

Serikali Yasema Haitaingilia Kupanga Bei Msimu Ujao Wa Pamba

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuelekea msimu ujao wa pamba serikali itajitahidi kupunguza gharama na kwamba haitaingilia kupanga bei bali watatafuta njia nyingine za kumlinda mkulima na kuhakikisha hapati hasara.

Ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Novemba 6, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Busega (CCM), Dk. Raphael Chegeni aliyetaka kupata tamko la serikali kuhusu wakulima wa pamba ambao waliuza pamba tangu Mei mwaka huu lakini hawajalipwa fedha zao.

“Wakulima wa pamba ambao mwaka hadi mwaka wamekuwa wakifanya kazi ya kulima wamekuwa wakipata hasara kwa mfano leo hii wakulima wa Mkoa wa Simiyu hasa wa Wilaya ya Busega wameuza pamba tangu mwezi Mei mpaka leo hawajaliwa fedha zao sasa hauoni kwamba hii ni kuwakatisha tamaa wakulima wasiweze kufanya kilimo kizuri zaidi na nini tamkola serikali juu ya hili,” amehoji.

“Ninakiri kuwa baadhi ya wakulima wa pamba hawajalipwa fedha zao, kwa mwaka huu mpaka sasa hivi jumla ya bilioni 417 zimeshalipwa kwa wakulima wa nchi nzima, ambao hawajalipwa wanadai bilioni 50 kufikia sasa hivi na sababu ya msingi ni lazima tufahamu kwamba asilimia zaidi ya 80 ya pamba inakwenda nje ya nchi, wanunuzi wetu wanakabiliwa na mtikisiko wa bei ambao umewakabili katika soko la dunia na sisi kama nchi tulitoa maelekezo ya bei ya kununulia na haya yalikuwa maamuzi ya serikali kwaajili ya kumlinda mkulima asipate hasara.

“Pamba yote iliyokuwa kwa wakulima imeshakusanywa sasa hivi kilichobaki mikononi mwa wakulima ni tani 5,000 tu ambayo tunaamini msimu unapoanza pamba yote ya wakulima itakuwa imeondoka, tunajitahidi kupunguza gharama msimu huu unaokuja na hatutaingilia kupanga bei, jukumu letu litakuwa ni kuhakikisha mkulima hapati hasara kwa kutafuta njia nyingine za kumlinda kuliko kumuathiri mnunuzi,” amesema Bashe.

Serikali Yapiga Marufuku Walengwa Wa Tasaf Kulazimishwa Kuchangia Bima Za Afya Na Michango Ya Kijamii

$
0
0
Na. Aaron Mrikaria-Dodoma
Serikali imewaagiza Viongozi wa Vijiji kutowalazimisha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kukatwa ruzuku kwa ajili ya kuchangia bima za afya na michango mbalimbali ya kijamii kwani ruzuku hiyo hutolewa na Serikali kwa ajili ya kuziwezesha kaya maskini kujikwamua kiuchumi.

Agizo hilo limetolewa Bungeni leo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kapt.

(Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Bahi, Mhe. Omary Ahmed Badwel aliyetaka kujua Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika vijiji vyote nchini.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, ruzuku inayotolewa na Serikali kwa walengwa ni kwa ajili ya kuwawezesha kupata mahitaji ya msingi kama vile chakula, gharama za elimu na Afya na kuwekeza katika kuanzisha miradi itakayowaongezea kipato na hatimaye kujikwamua na umaskini, hivyo ni maamuzi ya kaya husika kupanga matumizi ya ruzuku wanayoipata.

“Katika baadhi ya maeneo, Viongozi wa Vijiji wamekuwa wakiwalazimisha walengwa kukatwa ruzuku ili kulipia bima za afya na michango mbalimbali jambo ambalo si sahihi na halikubaliki”, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa ameelekeza walengwa kutokatwa ruzuku moja kwa moja bila ridhaa yao bali wapewe stahiki zao na kama kuna michango ya shughuli za maendeleo ya kijiji inapaswa kutozwa kwa wananchi wote wa kijiji husika.

Dkt. Mwanjelwa amewataka viongozi wote waliokuwa wanatoa amri ya kukatwa kwa ruzuku za walengwa wa TASAF moja kwa moja bila ridhaa yao, waache mara moja kwani ni kinyume cha utaratibu na iwapo wataendelea, Serikali itawachukulia hatua za kali za kinidhamu na kisheria.

Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini tangu uanze kutekelezwa na Serikali mwaka 2013 umezinufaisha kaya maskini kwa asilimia 70, na hivi sasa Serikali inajiandaa kuanza utekelezaji wa Awamu ya Tatu sehemu ya pili mwishoni mwa mwaka huu baada ya Serikali kupata fedha lengo likiwa ni kuzifikia kaya zote maskini nchini
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images