Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) Vyapewa ONYO

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Mihambwe
Vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) vimepewa onyo viwe makini zaidi kiutendaji kazi msimu huu  wa Korosho wa mwaka 2019/2020 ili kutokurudia makosa yaliyojitokeza msimu uliopita.

Hayo yamebainishwa na Afisa Tarafa Mihambwe Ndugu Emmanuel Shilatu wakati alipotembelea maghala ya AMCOS yaliyopo Tarafa ya Mihambwe ambapo amesisitiza Serikali kuwa bega kwa bega nao ili tija ionekane pande zote.

"Nimepita kote kuwapongeza kwa kazi nzuri wanazofanya lakini pia nimepita ili kujiridhisha na utaratibu unaotumika wa uuzaji wa Korosho kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani. Serikali inawasisitiza wafanye kazi kiuweledi, kusimamia haki ya Mkulima na kuhakikisha wanakusanya Korosho safi na zilizo na viwango zitakazovutia Wafanyabiashara sokoni. Lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha iwe Mkulima ama Amcos wananufaika na jasho lao." Alisisitiza Gavana Shilatu.

Maghala mbalimbali ya Amcos yamefunguliwa tayari kwa msimu 2019/2020 ambapo Wakulima wanapeleka Korosho zao ziuzwe kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.

PICHANI: Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu akipata maelezo na kujiridhisha juu ya utaratibu unaotumika kwenye ukusanyaji wa Korosho kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye msimu wa mwaka 2019/2020 alipotembelea maghala mbalimbali ya vyama vya msingi vilivyopo ndani ya Tarafa ya Mihambwe.

Rais Mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi Alazwa Tena Hospitali Wiki Mbili Baada Ya Kutoka

$
0
0
Rais  wa Zamani wa Kenya, Arap Moi  amelazwa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) katika Hospitali ya Nairobi na madaktari wanasema ni kutokana na maumivu ya kifua na shida katika kupumua

Wiki mbili zilizopita, aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo alipokuwa amelazwa huku Katibu wa Chama cha KANU, Nick Salat akisema Moi alienda kwa uchunguzi wa kawaida wa kiafya

Nick Salat amesema, "Alikuwa hospitalini hapo siku kadhaa nyuma na amerudi tu kwa ombi la madaktari wake. Yeye ni mzee na uchunguzi wa mara kwa mara kwa watu wa rika lake ni kawaida tu."

Mwaka jana, Moi aliondoka kwenda Tel Aviv, Israeli kwa uchunguzi wa matibabu akisindikizwa na mwanawe Gideon na Daktari wake, Dkt. David Silverstein

Wanaume Wanaonyonya Maziwa Ya Wake Zao Wapewa Onyo

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Lishe katika Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Moshi ametoa onyo kali kwa Wanaume wanaoendeleza tabia ya kupenda kunyonya maziwa ya Wake zao wanaonyonyesha na kuwataka kuacha mara moja kwani kufanya hivyo wanawapunja watoto.

Moshi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ikiwa  ni maandalizi ya mkutano wa mawaziri wa afya wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) ambapo amesema  mtoto ili awe na afya njema anahitajika kunyonya maziwa ya mama kwa miezi sita bila kitu chochote.

Amesema kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya wanaume kupendelea kunyonya maziwa ya Mama huku wengine wakiwapa masharti kwamba wanyonyeshe Mtoto ziwa moja na lingine wabakishiwe wao.

Amesema Wanaume lazima watambue kuwa maziwa ya Mama ni tiba na kinga kwa Mtoto huku akishangazwa na tabia ya Wanaume wanaopenda kuyanyonya akihoji maana yao hasa ni nini.

Kuhusu lishe nchini ,Moshi amesema kama nchini imepiga hatua kubwa katika eneo la lishe ukilinganisha na huko nyuma.

Ameongeza malengo yaliyowekwa duniani ni kwamba suala la lishe lisiwe zaidi ya asilimia 30 ambapo kwa Tanzania iko katika asilimia 32 ambayo ni juu ya lengo ambalo limewekwa katika eneo hilo la lishe.


Hata hivyo amesema kwa Tanzania katika eneo la lishe ilikuwa na changamoto lakini kupitia mikakati ya Wizara imefanikiwa kupunguza ukubwa wa tatizo la lishe nchini.

Hata hivyo amesema kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha ukosefu wa lishe ambao unafanya kuwepo na udumavu na kwamba  kuna mikakati mbalimbali ya kutoa elimu ya kuhamasisha jamii kuzingatia suala la lishe.

Makonda awakabidhi Suma JKT ujenzi hospitali Ubungo

$
0
0
Kitengo cha uzalishaji mali cha Jeshi la kujenga Taifa (suma JKT), kimepewa kazi ya kujenga hospitali ya wilaya ya Ubungo.

Kazi hiyo wamepewa na jana Oktoba 29, 2019 na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ambaye amesema kuwa ujenzi huo unatakiwa kamilika kwa miezi mitatu.

Amebainisha hayo jana alipotembelea eneo itakapojengwa hospitali hiyo Kimara Baruti, ambapo aliambatana na viongozi wengine na kuangalia jinsi maandalizi mbalimbali yalivyoanza kufanyika.

Makonda ametoa shukurani zake kwa mara nyingine tena kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kukubali ombi lake la sh 1.5 bilioni za ujenzi wa hospitali hiyo.

” Wilaya hii ni mpya inahitaji viongozi shupavu wa kuwaletea maendeleo, ni kazi ya viongozi wanaochaguliwa na wananchi.

“Kwa bahati mbaya Ubungo ilipata viongozi wanaojali matumbo yao tu. Hata leo hapa hawapo ila kesho watakuja na maneno matamu ili muwape kura” Alisema Mkuu huyo wa mkoa.

Mkurugenzi mtendaji wa Suma JKT, Kanali Rajabu Mabele amesema kuwa watahakikisha ujenzi huo unakamilika kwa muda uliopangwa.

Tahadhari Ya Mvua Kubwa Kanda Ya Ziwa

$
0
0
Mamlaka  ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema mikoa ya Kanda ya Ziwa itakuwa na mvua nyingi na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA, mikoa itakayokumbwa na mvua hizo ni Geita, Kagera, Mara na Magharibi mwa Simiyu.

Aidha, kiwango cha athari kinachoweza kutokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Wiki kadhaa zilizopita TMA ilitoa tahadhari ya uwapo wa mvua kwenye mikoa mbalimbali nchini ambayo itaanza Novemba hadi Aprili mwakani.

Aidha, siku chache baadaye Mamlaka hiyo ilitoa utabiri wa mvua kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga.

Tangu kuanza kwa mvua hizo, watu 25 wamepoteza maisha katika mikoa ya Morogoro na Tanga, huku madaraja manne yakisombwa na maji na kukatika kwa mawasiliano kwa mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Picha ya Rais Magufuli yamponza Idris Sultan ....Makonda Amtaka Ajisalimishe Polisi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amemtaka mchekeshaji na muigizaji hapa nchini, Idris Sultan, kuripoti katika kituo chochote cha polisi, hii ni baada ya msanii huyo ku 'post' picha katika ukurasa wake wa Instagram, akiwa amehariri picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kuweka sura yake.

Makonda ametoa agizo hilo leo Oktoba 30, 2019, kupitia ukurasa wake wa Instagramu.

"Naona mipaka ya kazi yako huijui, nenda sasa hivi kituo chochote cha Polisi, uwaambie Makonda kaniambie nije utakuta ujumbe wako" ameandika Makonda.

Idris aliweka picha hizo ikiwa ni siku moja tu imepita tangu Rais Magufuli, atimize umri wa miaka 60, ambapo msanii huyo aliandika kuwa.

 "Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani".

Mwenyekiti Wa CCM Rais Magufuli Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Ya Halmashauri Kuu Ya CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ndogo za Chama hicho mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo Oktoba 30, 2019

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM baada ya kikao kilichofanyika Ofisi ndogo za Chama hicho mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo Oktoba 30, 2019. PICHA NA IKULU

Fahamu Zaidi Kuhusu Ugonjwa Wa Mshipa Wa Ngiri (Hernia/Hydrocele)

$
0
0
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;
Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.


Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.


Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.


Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.


Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Kwa Ushauri na Msaada  Wasaliana na 
0713785111

Wanawake Washauriwa Kujitokeza Na Kuogombea Nafasi Mbalimbali Za Uongozi

$
0
0
Wanawake Mkoani Kagera wametakiwa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mnamo septemba 24 mwaka huu.
 
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa viti maalumu kutoka Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mh Conchester Rwamulaza wakati akiongea na mpekuzi blog kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mapema mwaka huu.
 
Mh Conchester amesema kuwa wanawake wengi wamekuwa na hofu ya kutotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuongeza kuwa wanayo nafasi kubwa yakuweza kugombea nafasi za uongozi kwa mwaka huu  kwa ajili ya maedeleo ya nchi kwa kuwa wana kauli mbiu ya wanawake wanaweza na kusema kuwa isiwe kauli ya maneno bali ata kwa vitendo.
 
Amesema kuwa ushindani wa mwaka huu ni mkubwa na watu wengi wana mwamuko wa kugombea kwa ajili ya maendeleo ya nchi na kuongeza kuwa uongozi unaanzia chini katika ngazi ya vitongoji na vijiji kwa kuwa viongozi hao wanakuwa karibu na wananchi.
 
Aidha Mh Conchester ameongeza kuwa wananchi wajitokeze  kwa wingi mnamo septemba 24 mwaka huu kuweza kupiga kura huku wakitambua umuhimu wa uchaguzi huo na akiwataka wananchi kutobeza uchaguzi huo kwa kuwa ni muhimu sana.
 
Pia mh Conshester amesema kuwa  ili jambo la wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali lifanikiwe inabidi akina baba kutowakataza wanawake  kugombea katika uchaguzi huo ili waweze kutimiza malengo yao.


Fahamu Zaidi Kuhusu Ugonjwa Wa Mshipa Wa Ngiri (Hernia/Hydrocele)

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa, Dalili zake Hizi Hapa..

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya maumble ya kiume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.


Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.


Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.


Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.


Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Kwa Ushauri na Msaada wa Wasaliana na  0713785111

Milioni 12 Zamsweka Ndani Kaimu meneja Mkuu Wa Kampuni Ya Ranchi Za Taifa NARCO Kagera.

$
0
0
Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera
Kaimu meneja mkuu wa kampuni ya ranchi za taifa NARCO profesa Philemoni Nyangi Wambura atafikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Bukoba leo tarehe 30 okitoba mwaka huu  kwa tuhuma za rushwa matumizi mabaya ya ofisi ubadhilifu na uhujumu uchum kinyume na sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kuzuia na kupambana na Rushwa 
 
Hayo yamebainishwa na mkuu wa takukuru mkoa wa kagera JOHN JOSEPH wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari  ofisini kwake 
 
Bw.joseph  amesema kuwa Takukuru mkoa wa Kagera ikiwa katika utekelezaji wa majukumu yake mnamo Septemba 23 mwaka huu walipata taarifa kutoka katika vyanzo vyake kuwa kaimu meneja wa NARCO profesa wambura  amekuwa akijihusisha na na vitendo vya rushwa ikiwa nikuomba na kupokea rushwa kutoka kwa baadhi ya wafugaji wenye uhitaji wa vitalu vya kufugia ng”ombe pamoja nawafugaji wanaotaka kuhuisha mikataba ya yao ya awali.
 
Akizungumza bw.Joseph amesema kuwa taarifa zinasema kuwa tarehe 3/1/2018 profesa Wambura kaimu meneja mkuu wa NARCO mkoa wa kagera alipokea jumla ya milioni 12 kutoka kwa mtu jina limeifadhiwa aliyeitaji kupewa kitalu kwa ajili yakufanya shughuli zake za ufugaji.
 
Pamoja na tukio hilo taasisi ya kuzuia na kupambana narushwa TAKUKURU mkoa wa Kagera mnamo tarehe 25/10/2019  iliwafikisha mahakamani watu wengine wanne ambao ni bw.Stansilaus Kato mwenyekiti wakamati ya ujenzi wa shule ya sekondari kashenye aliye funguliwa shauri jinai namba 226 la mwaka 2019 kwa makosa ya kughushi nyaraka nakujipatia madaraka asiyokuwanayo nakuwasilisha nyaraka za uongo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya misenyi  kwa lengo la kujipatia  shilingi milioni  tano laki saba elfu themanini na nne mia saba na arobaini.
 
Nawatu wengine waliofikishwa mahakamani na bw.Richard Machumi Kavorogo mwenyekiti wa kijiji cha omkalinzi ,bw.Joseph Desekahino Nzeye ofisa mtendaji wa kijiji omkalinzi na bw.Onesmo Mabadiliko Tiara aliyekuwa mwenyekiti wa kamati za vocher za pembejeo wa kata ya muganza halmashauri ya wilaya Ngara watatu hao wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ngara kujibu mashitaka yanayo wakabiri.
 
Vilevile bw.JOSEPH amesema nivyema wananchi waishio mkoa wa kagera waendelee kushirikiana na TAKUKURU pamoja na kutoa taarifa ili kuwabaini wala rushwa na mafisadi wanaotumia vibaya madaraka na maliza umma,kadhalika bw Joseph amesema kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi watakao shuhudia vitendo vya rushwa wasisite kutoa taarifa TAKUKURU kwa kupiga simu namba 113 bure

Nyavu Haramu Zenye Thamani ya Shilingi Bilioni 8 Zatekeketezwa Kwa Moto Kagera

$
0
0
Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera
Zana haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 zilizokamatwa kwenye doria mbalimbali za kukabiliana na uvuvi haramu ziwa Vitoria zimeteketezwa moto mkoani Kagera.
 
Hayo yamebainishwa wakati wa uteketezaji wa nyavu hizo na Kaimu Afsa Mfawidhi Wa Kitengo Cha Udhibiti Wa Rasilimali Za uvuvi Bw Gabriel Magene na kuongeza kwamba zimekamatwa  kutokana na matokeo ya kazi ambayo zimefanyika kuanzia mwaka huu wa 2019 kuanzia mwezi January. 
 
Bwana Magene amesema kwamba nyavu hizo zina thamani ya shilingi bilioni 8.7 na kuongeza kuwa zimeteketezwa kutokana na mahakama kudhibithisha kuwa ni nyavu haramu na imetoa kibali ziweze kuteketezwa kwa mujibu wa sheria.
 
Amesema kuwa nyavu ambazo zimeteketezwa ni pamoja na nyavu 196 za kokoro za kuvua sangara,nyavu zenye macho madogo chini ya inchi sita 19,620, nyavu 40 za dagaa zenye macho madogo, nyavu za double zenye macho 26 ni 12,000 pamoja na nyavu za monofilament 1,880.
 
Akizungumza wakati wa uteketezaji wa nyavu hizo mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Marco Elisha Gaguty amewataka wavuvi kuacha kutumia nyavu hizo ambazo aziruhusiwi kisheria na ikibainika wanafanya hivyo sheria itachukua mkondo wake.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Akanusha Taarifa ya Wanafunzi 350 Kuacha Shule Kwa Kupewa Mimba na Utoro

$
0
0
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma inapenda kukanusha habari ya upotoshaji  iliyotolewa na Gazeti la Habari Leo la tarehe 28 Oktoba 2019 na Kituo cha Televisheni cha ITV ikisomeka kuwa “Wanafunzi 350 waacha shule kwa utoro, mimba,”  habari hii haina ukweli wowote kama ilivyoripotiwa. 
 
Tunapenda kuuarifu umma kuwa baada ya kuwepo kwa taarifa hiyo Ofisi ya Mkurugenzi imefanya ufuatiliaji wa kina katika Shule ya Sekondari Marumba ambayo imetajwa katika habari hiyo iliyosema kuwa wanafunzi 350 wa shule hiyo wameshindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya utoro na mimba kwa kipindi cha miaka minne mfululizo  kuanzia mwaka 2016 hadi 2019. 
 
Ni vyema umma ukafahamu kuwa katika kipindi cha miaka minne yaani 2016 hadi 2019, shule hii ilipangiwa idadi ya wanafunzi 603 ikiwa wavulana 320 na wasichana 283, waliosajiliwa kwa kipindi hicho ni wanafunzi 515 ikiwa pungufu ya wanafunzi 88 kati ya waliopangwa. 
 
Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanafunzi waliopo katika shule ya Sekondari Marumba hadi kufikia tarehe 28/10/2019 ni 345 ikiwa wavulana 208 na wasichana 137 kukiwa na upungufu wa wanafunzi 170.  
 
Akitoa ufafanuzi huo Mkurugenzi Mtendaji Halmasahuri ya Tunduru Gasper Balyomi amesema hii ni wazi kuwa idadi ya wanafunzi 350 wa sekondari ya Marumba walioripotiwa hawajulikani walipo hazina ukweli wowote kufuatia takwimu zilizotolewa na kubaini kuwa:- 
 
1.Kwa kipindi cha miaka minne mfululizo jumla ya wanafunzi 20 walihama kwenda katika shule nyingine. 
2.Wanafunzi 15 waliacha masomo baada ya kupata ujauzito
3.Wanafunzi 63 waliacha masomo kutokana na sababu mbalimbali
4.Wanafunzi 72 waliopewa nafasi ya kurudia masomo baada ya kufeli  kidato cha pili  baadhi yao wazazi waliamua kuwapeleka katika vyuo vya Ufundi stadi kama  (VETA) na shule binafsi. 
 
Hivyo kufanya jumla ya wanafunzi 170 kwa kipindi cha miaka minne ndio hawapo shuleni tofauti na taarifa ilivyoonesha jumla ya wanafunzi 350 wa shule hiyo wameacha masomo.
Aidha kuhusu suala la utoro wa reja reja Halmshauri inaendelea kushirikiana na wazazi pamoja walezi wa wanafunzi katika kuahikisha utoro mashuleni unadhibitiwa. 

Imetolewa na 
Kitengo cha Habari na Mawasiliano 
Halmashauri ya Tunduru

Muungano wa Tigo na Zantel unavyokusudia kuboresha soko la mawasiliano nchini

$
0
0
Sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi imekua kwa kiasi kikubwa sana katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Katika kipindi hiki cha ukuaji huu makampuni ya simu yametanua wigo wa huduma na matumizi ya simu za mkononi imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku kwa mamilioni ya Watanzania tofauti na zamani ambapo simu ilikuwa kama anasa na ni wachache tu waliweza kuwa nazo. Maendeleo haya yanazidi kukua siku hadi siku kutokana na kuongezeka kwa ubunifu katika teknolojia. 

Simu ya mkononi sasa imebadilika na kuwa si tu kifaa cha kupiga, kupokea na kutuma meseji baina ya watumiaji lakini pia imeleta mapinduzi katika namna tunavyoweka akiba ya fedha, kulipana, kulipa bili mbalimbali na kuendesha maisha yetu ya kila siku.  
 
Mfano wa namna ambavyo simu za mkononi zimebadili maisha yetu ni kampuni ya Tigo Tanzania. Mfumo wa Tigo Pesa wa kutuma na kupokea pesa unatupa nafasi ya kutumiana na kupokea pesa bila haja ya kwenda na kupanga foleni benki.

Vivyo hivyo wenye maduka na biashara mbalimbali nao wametengenezewa mfumo wa Tigo Pesa Merchant ambao unawapa uwezo wa kupokea malipo kutoka wateja wote wa Tigo Pesa ambao kwa sasa ni zaidi ya watu milioni 16.   

Tigo Tanzania pia ni moja ya makampuni yanayoongoza kwa kutoa huduma ya 4G ambayo ni teknolojia yenye ina kasi zaidi katika mawasiliano nchini.

 Huduma hii inakupa uhakika wa kutazama vitu kama videos mtandaoni bila wasiwasi wa kukwama kwama au hata kufanya mikutano kwa njia ya video (conferencing)

Hata hivyo katika siku za karibuni umekuwepo wasiwasi kwamba sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi imejaa watoa huduma ambao wengi hawana tija na wasiolipa soko afya katika kuhudumia wateja.

Hali hii inaelezwa kuleta changamoto kwa ubunifu na utoaji huduma wenye tija na viwango bora kwa wateja. 

Katika sekta nyingi za uchumi uwepo wa watoa huduma wengi huwa ni faida kwa mteja. Bahati mbaya ukweli huu haupo kwenye sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi. 

Utafiti unaonyesha kuwa kupunguza idadi ya watoa huduma katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi huwezesha makampuni machache yalipo sokoni kuongeza faida ambayo huwawezesha kuwekeza zaidi katika mitambo na teknolojia yenye kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake. 

Katika soko la Tanzania, siku za karibuni zimekuwepo hatua mbalimbali za kibiashara kupunguza watoa huduma ili kuongeza uwekezaji kwenye teknolojia na ubora wa huduma kwa wateja.

Makampuni mawili ya Tigo Tanzania na Zantel yamekuwa na mjadala kuungana. 

Hatua hii ya Tigo Tanzania na Zantel kuungana ni habari njema sana kwa wateja wa Zantel. Maana yake ni kwamba sasa wateja hao wa Zantel wataweza kufurahia huduma zote ambazo sasa wateja wa Tigo Tanzania wanazipata.

Muungano huo pia utasaidia sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini kuendelea kuwa bunifu na kutoa huduma bora kwa mamilioni ya wateja wake nchi nzima.

AfDB kuipatia Tanzania zaidi ya shilingi Tirioni 1 kujenga uwanja wa ndege msalato

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Abidjan, Ivory Coast.
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamia Dodoma na kuahidi kuidhinisha kiasi cha dola za kimarekani milioni 455 sawa na zaidi ya shilingi za Kitanzania trilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato sambamba na ujenzi wa barabara za mzunguko Jijini  humo.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina ameyasema hayo katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Abijdan Nchini Ivory Coast wakati wa Mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na kuongeza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kipindi chake cha Uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) lakini pia kwa Tanzania.

Amesema Benki hiyo tayari imeshaidhinisha kiasi cha dola za marekani milioni 180 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko jijini  Dodoma na kwamba kiasi kingine cha dola za marekani milioni 275 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato kinatarajiwa kuidhinishwa na mapema mwezi Novemba 2019.

Dkt. Adesina ameongeza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ina imani na mageuzi ya kiuchumi yanayotekelezwa chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za kijamii ikiwemo elimu bila malipo,afya na maji pamoja na mapambano dhidi ya rushwa na kuleta uwajibikaji katika taaisisi za uma na kwamba iko tayari kuunga jitihada hizo za serikali kwa kuwekeza katika sekta ya miundombinu.

Aidha Dkt. Adesina ameelezea nia yake ya kutaka kushudia bara la Afrika likipiga hatua kubwa za kimaendeleo sasa na kwa haraka na sio kusubiri baadae na kwamba katika kipindi chake cha uongozi katika Benki ya Maendeleo ya Afrika atapambana kuhakikisha azma hiyo inatekelezeka.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ushirikiano inayoutoa kwa Tanzania hususani katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambayo kimsingi yalikuwa ni maono ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere kwa nia ya kuiwezesha Tanzania kujitegemea kiuchumi na hatimae Bara zima la Afrika.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa tayari Benki ya Maendeleo ya Afrika iko tayari kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa yaani Standard Gauge Railway ya kipande cha kutoka Isaka hadi Kigali nchini Rwanda na kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mara baada ya kukamilika mchakato wa utoaji wa fedha hizo ambapo mazungumzo ya awali kuhusu ufadhili huo yameanza.

Pia Prof. Kabudi amemtaka Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Akinwumi Adesina kuimarisha ofisi za kanda za benki hiyo ili ziweze kutoa huduma zote za kibenki ili kusogeza huduma karibu na wanufaika wa benki hiyo sambamba na kuunga mkono miradi yote ya kimkakati inayounganisha nchi na nchi katika bara la Afrika ili kuboresha nakurahisisha huduma ya usafiri katika Bara la Afrika na hivyo kuwezesha biashara miongoni mwa nchi za Kiafrika na kujiletea maendeleo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi yuko Abijdan Nchini Ivory Coast kushiriki mkutano wa siku mbili wa dharura wa Mawaziri wa fedha uliondaliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB).

Saratani Ya Matiti Yaweza Kushika Namba Moja

$
0
0
Na. Catherine Sungura, WAMJW-DSM
Endapo hatua zisipochukuliwa za  saratani ya matiti inaweza kushika namba moja kwa kuwa na idadi  kubwa ya wagonjwa  nchini.
 
Hayo yanesemwa na Mkurugenzi wa huduma za Kinga ya Saratani  katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dkt. Crispian Kahesa  alipozungumza na waandishi wa habari  kuhusu mwezi wa uhamasishaji , uelimishaji na uchunguzi wa saratani ambao huadhimishwa kila mwezi oktoba kila mwaka.
 
“Idadi ya saratani ya matiti  inaonekana kuongezeka nchini ambapo hivi sasa wanawake wenye umri  kuanzia miaka 20 na kuendelea nao wanagundulika  kuugua ugonjwa huu”. Alisema Dkt. Kahesa.
 
Alisema kuwa endapo hatua zisipochukuliwa  saratani hiyo itazidi kuwa tishio zaidi na kwamba  idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika  hospitalini hapo wanatoka katika maeneo ya mjini ambapo mkoa wa Dar es salaam unaonekana kuongoza.
 
“Tathimini  ya miaka 10 iliyopita saratani hii ilikua inashika nafasi ya tano ,hivi sasa ni ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa,zamani tulikua tunawaona wagonjwa kuanzia miaka 55 ukashuka hadi miaka 50 na sasa tunaona hadi wenye umri wa miaka 20”.
 
Dkt. Kahesa alisema kuwa kwa mwaka huu pekee wameweza kuona wanawake 1443 ambapo kati ya 342 wamekutwa na uvimbe 170 walikuwa na dalili za awali za saratani.
 
Kwa upande wa saratani kwa wanaume Dkt. Kahesa alisema kuwa saratani hiyo huathiri asilimia moja kwa wanaume hata hivyo kwa upande wao ni hatari  zaidi na endapo isipogundulika huweza kuathiri mapafu yao kwa haraka.
 
“Saratani hii huathiri wanawake zaidi  kuliko wanaume kwa asilimia 99 na wanaume ni asilimia 1 tu,ambapo dalili kwa wanaume  ni tofauti  kidogo na wanawake,hivyo kwa mwanaume ni rahisi kugundua kuliko mwanamke kwa kuwa kifua chake kina mafuta mengi.
 
Aliongeza kuwa kati ya wanawake 170 waliofanyiwa vipimo  zaidi ya 68 waligundulika na vivimbe ambavyo ni ugonjwa wa saratani.
 
Hapa nchini saratani ya shingo ya kizazi inaongoza ikifuatiwa  na saratani ya matiti,saratani  ya njia ya chakula,saratani ya tezi dume na saratani  nyingine ni zile zinazoathiri  mfumo wa kinga.

Harmonize, Ali Kiba Wamjibu Diamond Kuhusu Tamasha lake la Wasafi Festival......." UNIKOME, Unaniibia Afu Unanisaidia?"

$
0
0
Muda mfupi baada ya msanii,  Diamond Platnumz kuwaalika Harmonize na Ali Kiba katika tamasha la Wasafi, wawili hao wameibuka na kumjibu.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Ali Kiba ameandika; “Usiniletee mambo ya darasa la Pili unaniiibia penseli alafu unanisaidia kutafuta .(UNIKOME) Mwanaume huwa anaongeaga mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema @diamondplatnumz”

Leo Jumatano Oktoba 30, 2019 Diamond wakati akizungumzia tamasha hilo litakalofanyika Novemba 9, 2019  jijini Dar es Salaam alisema ana imani Harmonize atashiriki na kwamba amepeleka mwaliko kwa uongozi wa Ali Kiba, ili msanii huyo naye ashiriki tamasha hilo.

"Wenzetu Nigeria ndio maana wanaendelea kwenye muziki kwani kunapokuwa na matamasha kama haya wanaweka tofauti zao pembeni, kumkuta jukwaa moja Wizkid na Davido ambao walikuwa na bifu kwao ni jambo la kawaida.”

“Kwa nini tung’ang’anie bifu hata sehemu ambayo ni ya kutengeneza pesa na kutuleta Watanzania pamoja,” amesema Diamond katika mkutano wake huo na waandishi wa habari.


Harmonize kwa upande wake alipoulizwa alijibu;  “achana na hayo mambo ya Diamond, tuongee mambo mengine.”

Kilichoamuliwa Leo Ndani ya Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi October 31

Watu Waliokutwa na tausi wa Ikulu wahukumiwa kulipa Milioni 6

$
0
0
Watu watatu wanaodaiwa kukutwa na ndege aina ya tausi wa Ikulu wamehukumiwa kulipa fidia zaidi ya Sh6.8 milioni baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya uhujumu uchumi kwa kujihusisha na nyara za Serikali bila kibali.

Kadhalika mahakama hiyo imetaifishwa ndege hao kuwa mali ya serikali. Pia imewaachia huru kwa masharti ya kutokutenda kosa ndani ya miezi sita.

Hukumu hiyo ilisomwa jana na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salumu Ally, baada ya washtakiwa kumwandikia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) barua ya kukiri makosa yao.

“Mahakama hii inawaamuru washtakiwa kulipa fidia ya Sh. 6,890,000, ndege hao wanataifishwa kuwa mali ya serikali na inawaachia huru kwa masharti kwamba wasitende kosa la jinai ndani ya miezi sita,” alisema Hakimu Ally wakati akisoma hukumu hiyo.

Awali, washtakiwa walidaiwa kujihusisha na genge la uhalifu, kukutwa na nyara za serikali ikiwamo ndege aina ya tausi watatu wa Ikulu ya Tanzania.

Washtakiwa hao ni David Graha, Mohammed Hatibu na Mohammed Mahamoud, wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Vick Mwaikambo.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kuwa shtaka la kwanza, kati ya Juni Mosi, 2015 na Oktoba 14, mwaka huu waliratibu mipango ya uhalifu kwa kujihusisha na biashara ya ndege hao wenye thamani ya Dola za Marekani 1,500 (sawa na Sh. 3,444,150).

Nchimbi alidai katika shtaka la pili, washtakiwa walikutwa na ndege watatu aina ya tausi wenye thamani hiyo ya fedha.


Wankyo alidai katika shtaka la tatu, Oktoba 14, mwaka huu eneo la Mikocheni, mshtakiwa wa tatu Mahamoud alikutwa na tausi hao.
 
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images