Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Uteuzi Mpya Uliofanywa na Rais Magufuli Leo


Mahakama Yataka uthibitisho wa afya ya Tundu Lissu

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema  wadhamini wa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu wanatakiwa kutoa uthibitisho wa maendeleo ya afya ya Lissu pindi shauri hilo linapoitishwa tena mahakamani hapo.

Lissu na wenzake watatu kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwemo kuandika taarifa zenye maudhui ya uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Hayo yamebainishwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kuuliza maendeleo ya Lissu ndipo mdhamini wake, Robert Katula alidai kuwa mshtakiwa huyo bado anaumwa.

Kutokana na kauli hiyo, Wakili wa Serikali, Estazia Wilson ameieleza mahakama kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa hivyo hawawezi kuendelea na shauri hilo hivyo wataendelea kumsubiri Lissu hadi afya yake itakapoimarika.

Hakimu Simba alisema shauri hilo litakapokuja  mahakamani hapo mdhamini wa Lissu anatakiwa kuja na  uthibitisho wa maendeleo ya afya yake.

“Mdhamini wa Lissu utatuletea uthibitisho wa afya ya Lissu ili tuweze kuweka kwenye rekodi zetu,”alisema Simba.

Baada ya kusema hayo, Hakimu Simba ameahirisha shauri hilo hadi Novemba 21 2019 itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Mbali na Lissu washtakiwa wengine ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Inadaiwa kuwa Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’

Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Viongozi Wa AALCO Na Naibu Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa China - Ikulu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali.

Viongozi wa AALCO waliokutana na Rais Magufuli ni Rais wa AALCO, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Waziri wa Sheria na Katiba, Tanzania), Makamu wa Rais wa AALCO Prof. Mohamad Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina), Katibu Mkuu wa AALCO Prof. Kennedy Gastorn (Tanzania) na Naibu Makatibu Wakuu wa AALCO watatu ambao ni Yukihiro Takeya (Japan), Wang Liyu (China) na Dr. Ali Garshasbi (Iran).

Rais Magufuli amewashukuru na kuwakaribisha wajumbe wa AALCO nchini Tanzania na amewahakikishia kuwa Serikali inatambua kazi inayofanywa na taasisi hiyo tangu ijiunge nayo mwaka 1965 na kuwa mwanachama kamili kuanzia mwaka 1973.

Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa AALCO kutekeleza malengo ya taasisi hiyo kama alivyoelezwa na viongozi hao, na ametoa wito wa kuendelea kuzitetea nchi wanachama hasa zinazowekewa vikwazo mbalimbali.

Ametolea mfano wa Zimbabwe ambayo imewekewa vikwazo kwa miaka mingi hali inayosababisha wananchi wa Zimbabwe kuteseka.

Rais wa AALCO Balozi Mahiga na Katibu Mkuu Prof. Kennedy Gastorn wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kupata fursa ya kukutana nae na wameahidi kuwa AALCO itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa maslahi ya Asia na Afrika.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba Mhe. Amon Mpanju.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amemuomba Yezhou kufikisha shukrani zake kwa Rais wa China na Mwenyekiti wa CPC Mhe. Xi Jinping kwa kutoa tuzo kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuiwezesha China kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Rais Magufuli amemhakikishia kuwa Sera za Tanzania kuhusu China hazijabadilika na amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika jitihada mbalimbali za maendeleo.

Mazungumzo hayo yamehudhriwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bashiru Ally Kakurwa na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke.

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Tangazo la Nafasi 54 za Kazi Serikalini | The National Institute for Medical Research (NIMR)

$
0
0
Jobs Opportunities at NIMR Tanzania The National Institute for Medical Research (NIMR) is a parastatal Organization, established by the Parliamentary Act (NIMR Act Cap 59 R.E.2002) under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children. The Institute is mandated to carry out, control, coordinate, register, monitor, evaluate and promote health research in Tanzania.
 
In order to fulfill its mandate, the Institute is now looking for qualified, competent and highly motivated Public Servants with check numbers who wish to transfer to NIMR to fill various positions located in Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Tanga, Tabora, Dodoma, Tukuyu, Amani-Muheza and Ngongongare-Arusha, as provided below:

1. POSITION:   Artisan III (1)
QUALIFICATION:Holder of Form IV Examination Certificate and Trade Test Grade II or equivalent from recognized Institution.
SALARY SCALE: PGSS 1.1
DUTY STATION: Dar es Salaam
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

2.POSITION:   Research Assistant (10)
QUALIFICATION: Fresh graduates with a minimum of an Upper Second Class Honours degree in natural, social or engineering sciences. For unclassified degrees such as MD and BVM, fresh graduates with an overall minimum of B.

SALARY SCALE: PRSS 1.1
DUTY STATION: Arusha/Mwanza/ Mbeya/ Tabora/ Tukuyu/Mwanza/ Amani- Muheza/ Tanga/Dodoma
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

3.POSITION:   Research Scientist II (10)
QUALIFICATION: Holders of a Master’s in natural, social or engineering sciences who attained a minimum of an Upper Second Class Honours degree at Undergraduate level.

SALARY SCALE: PRSS 2.1
DUTY STATION: Arusha/Mwanza/ Mbeya/ Tabora/ Tukuyu/Mwanza/ Amani- Muheza/ Tanga/Dodoma
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

4.POSITION:   Personal Secretary III (2)
QUALIFICATION: Holder of Form IV/VI secondary certificate with principal passes in English and Kiswahili or credit pass in English and Kiswahili plus 100/120 w.p.m. Shorthand in English or Kiswahili and 50 w.p.m. typing, tabulation and manuscript stg III, secretarial duties and office procedure stg II and should have completed Advanced Computer course from a recognized institution.

SALARY SCALE: PGSS 3.1
DUTY STATION: Tabora/DSM
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

5.POSITION:
   Driver III (3)
QUALIFICATION:Holder of Form IV National Examination Certificate with Class C valid driving license. Must have a clean record in driving for at least three years. Holder of Trade Test Grade III (motor vehicle mechanics) will be considered first.

SALARY SCALE: POSS 2.1
DUTY STATION: Tabora/Mwanza/DSM
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

6.POSITION: Data Entry Clerk I (2)
QUALIFICATION: Holder of Form IV Examination Certificate plus possession of certificate of computer course (with a bias in computer operations) from a recognized Institution.

SALARY SCALE: PGSS 1.1
DUTY STATION: Mwanza/Mbeya
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

7.POSITION:   Senior Human Resource Officer I (2)
QUALIFICATION:Holders of Master’s degree in Public/ Business administration/Personnel management or equivalent qualification with post qualification of at least management or equivalent qualification with post qualification of at least seven years in a senior position at a reputable public Institution. Lawson knowledge is an added advantage.

SALARY SCALE: PGSS 9.1
DUTY STATION: Dodoma/Amani-Muheza
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

8.POSITION:   Principal Research Scientist II (8)
QUALIFICATION:Holders of PhD in natural, social or engineering sciences who attained a minimum of an Upper Second Class Honours degree at undergraduate level. A working experience of at least three years in research work after PhD.

SALARY SCALE: PRSS 6.1
DUTY STATION: Arusha/Mwanza/ Mbeya/Tabora/ Tukuyu/Mwanza/ Amani- Muheza/ Dodoma
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

9.POSITION:   Assistant Accountant III (3)
QUALIFICATION:Holder of ATEC II, Ordinary Diploma with working experience of four years in that grade.

SALARY SCALE: PGSS 4.1
DUTY STATION: Tukuyu/Mwanza/ Amani – Muheza
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

10.POSITION:   Attendant II (7)
QUALIFICATION: Holder of Form IV National Examination Certificate and must be physically fit with at least two years of working experience.

SALARY SCALE: POSS 1.1
DUTY STATION:Tukuyu/Tanga/Amani/DSM/Mwanza
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

11.POSITION:   Clinical Officer II (1)
QUALIFICATION: Holder of Form IV/VI National Examination Certificate with a Diploma in Clinical Officers Course from a recognized Institution with at least four years working experience in a reputable organization.

SALARY SCALE: PMGSS 5.1
DUTY STATION:  Mwanza
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

12.POSITION:   Health Laboratory Assistant III (2)
QUALIFICATION: Holder of Form IV/VI secondary education with at least two Principal pass in science subjects or credit pass in any three science subjects and has successfully passed Medical Laboratory Science Certificate.

SALARY SCALE: PMOSS 1.1
DUTY STATION:  Mwanza
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

13.POSITION:   Health Laboratory Scientist II (3)
QUALIFICATION:Holder of first degree in Laboratory Sciences or Fellow of Medical Laboratory Sciences or its equivalent with at least four years working experience in a reputable organization.

SALARY SCALE: PGMSS 6.1
DUTY STATION: Arusha/Mwanza

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

==>Kutuma Maombi ya Nafasi Hizo za Kazi na Taarifa Zaidi <<INGIA  HAPA>> 

Nafasi Mpya za Kazi Benki Ya CRDB | Deadline ni 28th, October 2019

$
0
0
Benki ya CRDB Wametangaza Nafasi mbalimbali za Kazi kama zilivyoorodheshwa hapo chini | Deadline ni 28th, October 2019  
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

1 Senior Manager; Corporate Social Investment 

2 Corporate Social Investment Business Analyst 

3 Senior Specialist; Corporate Communication & PR

4 Manager; Strategic Partnership

5 Senior Specialist; Financial Literacy

6 Specialist; Grant and Communications 

 ==>>Pia zipo nafasi mbalimbali za kazi kama vile; Afisa Mtendaji (Simiyu), Walimu, UBER TANZANIA,  AIRTEL, JUMIA, NOKIA TANZANIA,UMOJA WA MATAIFA

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Bonyeza hapo chini kujua zaidi

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/jobs

Nafasi Nyingine Mpya ya Kazi Serikalini | Senior Corporate Communications Officer II- UCSAF

$
0
0
 Employer: Universal Communications Service Access Fund - UCSAF
Date Published: 2019-10-23
Application Deadline: 2019-11-05
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:
i.To manage Corporate branding and image of the Fund;
ii.To manage discrepancies between the company's desired identity and brand features;
iii.To develop Strategic Corporate Communications Plans that leverage multiple traditional and innovative elements to create a powerful, impactful program;
iv.To promote the Fund’s brand and engage executives and customers in relevant industry dialogues;
v.To mobilize internal and external support to meet the Fund’s organizational objectives;
vi.To manage communications with all stakeholders of the Fund; relationships with investors, business persons in ICT sector, media, internal and external audiences etc.;
vii.To assist in managing Corporate Social Responsibility (CSR) activities of the Fund;
viii.To position the Fund strategically as a key player in its core business and maintain a good understanding of the Fund’s core business;
ix.To manage relationships with the media, organize press briefings, write and disseminate press releases to the media through different channels; and
x.To carry out any other duties as assigned from time to time by supervisor.

QUALIFICATION AND EXPERIENCE:
Holder of University Bachelor Degree either in Journalism, Public Relations, Mass Communication or equivalent from a recognized University or Institute with minimum of six (6) working experience in related field.

REMUNERATION: Salary Scale USCAF SCALE 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

 ==>>Pia zipo nafasi mbalimbali za kazi Toka CRDB,EWURA,TIGO, COCA-COLA,VODACOM,NIMR

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Bonyeza hapo chini kujua zaidi

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/jobs  

Putin: Afrika Ni Muhimu Kwa Maendeleo Ya Uchumi Wa Dunia

$
0
0
RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amefungua Kongamano la Biashara baina ya Urusi na Afrika (Russia Business Forum) ambapo amesema Bara la Afrika ni muhimu katika maendeleo ya uchumi wa dunia na ni kivutio kikubwa kwa wafanyabiashara wa Urusi.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 23, 2019) wakati akihutubia mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Olympic Park katika mji wa Sochi nchini Urusi. Rais Putin amesema takwimu zilizotolewa na watalaamu wa masuala ya uchumi zinaonyesha kwamba pato la Afrika (GDP) litafikia dola trilioni 29 ifikapo 2050.

Amesema biashara kati ya Urusi na Afrika imeongezeka mara dufu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kufikia dola za Marekani bilioni 20 na kwamba nchi yake inaunga mkono wazo la kuanzishwa eneo huru la biashara katika bara la Afrika ukiwa ni mkakati wa Umoja wa Afrika (AU) na kwamba itatoa ushirikiano ili kufanikisha wazo hilo.

Kadhalika, Rais Putin ameongeza kuwa nchi yake inatekeleza kwa vitendo mpango kuzifutia madeni nchi za Afrika na hadi sasa imeshafuta madeni ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 20.

Amesema utoaji wa mafunzo ya taaluma mbalimbali umekuwa ni utamaduni wa ushirikiano kati ya Urusi na Afrika. “Hadi katikati ya miaka ya 80 nchi yake imejenga taasisi zipatazo 100 za mafunzo mbalimbali Barani Afrika na watu 500,000 wampata mafunzo katika taasisi hizo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameshiriki katika mkutano huo akimwakilisha Rais John Pombe Magufuli. Pamoja naye idadi kubwa ya Wakuu wa Nchi na Serikali katika Bara la Afrika wamehudhuria mkutano huo.

Miongozi mwa viongozi hao ni Rais Yoweli Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais wa Misri na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Abdel Fattah al Sissi, Rais wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa, Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na viongozi wengine kutoka Bara la Afrika.

Kesho (Alhamisi, Oktobba 24, 2019) Waziri Mkuu anatarajia kushiriki katika mkutano baina ya Urusi na Wakuu wa nchi na Serikali wa Bara la Afrika.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Maswali 15 Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kwenye Usaili ( Interviews ) na Namna ya Kuyajibu

$
0
0
Usail wa ajira (interviews) husababisha hofu na msongo wa mawazo kwa vijana wengi kabla au baada ya kutoka chumba cha usaili.

Tatizo hilo hutokana na hofu inayojenga wakati wa kujibu maswali unayoulizwa  na watu ambao wamekuzunguka wakati wa kufanyiwa usaili.

Njia moja ya kuzuia hii kutokea ni kufuatilia mfumo wa kujibu maswali.

Ifuatayo ni orodha yetu ya maswali 15 yanayoulizwa mara kwa mara kwenye interviews( Usaili) na namna ya kuyajibu;

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

1.Jitambulishe(Wewe ni Nani?)
Mara nyingi hili ni swali ambalo mtahiniwa huulizwa mara tu aingiapo kwenye chumba cha usaili. Kwa bahati mbaya watahiniwa wengi hudhani kuwa waajiri hutamani kujua majina yao. Hapana, majina yako wanayafahamu na pengine hata taarifa za ziada. Katika swali hili waajiri uhitaji kujua sifa zako zihusianazo na ajira zitakazo dhihirisha kuwa wewe ni mtu sahihi.

Mfano mtu anaweza kujibu hivi, “Jina langu ni Mti Mkavu, ni Mhitimu wa Shahada ya Masoko ya Chuo Kikuu Dodoma. Ni mtu makini, mbunifu, mchapa kazi na ninayependa watu. Pamoja na hayo ninao ujuzi usio na shaka kwenye masuala ya mawasiliano. Uwezo wangu unadhihirishwa na mrejesho ambao huwa na upata kwa kila mtu ninaye fanya naye kazi”.

Katika swali hili ni muhimu kujua kuwa halihitaji wewe kuzungumzia mambo yasiyo husiana na kazi na ajira. Kwenu mpo wa ngapi,jina la mama yako, mkoa unaotoka, kabila, kazi ya baba au mama yako havihitajiki katika taarifa unazotakiwa. 


2.Kwanini upewe ajira kwetu? | au unaweza ukaulizwa Kwa nini unahisi wewe ni mtu sahihi kwa kazi hii na siyo mwingine?

Kumbuka kuwa usaili wa kazi unahusisha ushindani hivyo swali hili linataka uoneshe utofauti ulionao. Katika kujibu swali hili zingatia mahitaji ya kazi husika kujenga hoja kwani hata kama una utofauti wa aina gani kama hautasaidia katika kufikia  malengo ya taasisi bado itakuwa ni kazi bure.

Mfano, “ Siyo kwamba mimi ni mchapakazi na mbobezi katika uhasibu pekee lakini pia ni mtu ambaye ninaweza kufanya shughuli zangu bila kusimamiwa. Mimi ni mtu wa matokeo hivyo kwa kila ambacho hufanya hulenga kutimiza malengo kwa wakati na kufikia viwango stahiki. 


"Ubora wangu unathibitishwa na tuzo kadhaa nilizowahi kupata ikiwemo mfanyakazi bora wa mwezi mara nne nilipokuwa nikifanya kazi na na Magogo Media. Hii inathibitisha kuwa mkinipa fursa hii hamtakuwa mnajaribu bali mtakuwa mnafanya maamuzi sahihi”.

3.Unajua nini kuhusu sisi?
Siku zote maandalizi ya usaili yanaenda sambamba na kutafuta taarifa sahihi za taasisi husika. Hivyo ni vyema kuhakikisha kuwa taarifa unazotoa hapa ni sahihi na muhimu katika kudhirisha kuwa ulishafanya utafiti wa kutosha kuhusu taasisi husika.

Mfano, “ Benki yenu ilianzishwa mwaka 1987 ina maono ya kuwa benki bora kuliko zote nchini kwa kutoa huduma za kifedha zinazo aminika na kufikia maeneo mengi nchini. Kwa sasa benki yenu ina matawi 700 na ATMs 500 huku ikiwa na mpango wa kufungua matawi mengine Kigoma hivi karibuni. 


Endapo mtanipa fursa ya kufanya kazi na nyinyi nitahakikisha natumia vyema uwezo wangu katika masuala ya masoko ili kuongeza wateja na kuhaikisha huduma bora mnayotoa inafahamika kwa watu wengi.”

4. Ni vitu gani unavyojivunia?
Katika swali hili waajiri huhitaji kujua mambo kadhaa ambayo unayaona kama mtaji mkubwa katika utendaji kazi. Ni vyema kukumbuka kuwa mambo utakayo yataja hapa ni yale yenye umuhimu katika kuongeza ufanisi au ubora katika kazi husika kwani kila kazi inamahitaji yake ya tofauti na kazi nyingine.

Kwa mfano, “mambo makuu mawili ninayojivunia ni ujuzi na uwezo katika huduma kwa wateja na kujisimamia katika majukumu yangu. Kila ninapowahudumia wateja huwa napokea mrejesho chanya juu ya namna wanavyoridhishwa na huduma yangu hivyo kutamani kuhudumiwa nami tena.


Hii hunifanya nijione kuwa mtu muhimu sana katika taasisi yoyote ninayofanya nayo kazi. Pia, uwezo wangu katika kufanya shughuli bila kusimamiwa au chini ya usimamizi mdogo unanifanya niwe mtu wa kuaminiwa na kutegemewa katika kufanya shughuli zangu.Haya ni baadhi ya mambo mengi yanayonifanya mimi kuwa mtu wa tofauti. Nina amini hamtaacha fursa ya kufanya kazi nami”
 

5.Udhaifu wako ni upi?
Hili ni moja ya maswali ambayo watainiwa wengi huyachukia na kuyaona kama yana lengo la kuwatafutia sababu za kuwanyima kazi. Wengine kwa lengo la kuonesha ukamilifu huthubu kusema kuwa hawana udhaifu wowote-usithubutu kusema hivyo. Kila mtu ana udhaifu wake kwani hakuna aliye mkamilifu.

Suala la msingi ni kujua namna ya kujibu suali hili. Mambo ya kuzingatia ni pamoja na kuchagua udhaifu ambao hauta athiri utendaji wako na pili hakikisha udhaifu huo unahusiana na ujuzi na sio tabia. 


Ujuzi ni rahisi kuutafuata lakini kubadilisha tabia ni ngumu zaidi hivyo usiseme kuwa wewe ni mvivu,mdokozi, na mengineyo ya kitabia. Na unapotaja udhaifu wowote kumbuka kuonesha jitihada ambazo umeshazifanya ili kudhibiti udhaifu huo.

Kwa mfano, kwa kazi ya uhasibu mtu anaweza sema, “Udhaifu nilio nao ni masuala ya ‘graphic designing’ niligundua hili nilipohitaji kuandaa tangazo kwa ajili ya ofisi niliyokuwa nikifanya nayo kazi. Hata hivyo, nimeanza kujifunza mwenyewe kupitia mtandao wa internet na naona napata mabadiliko chanya kila leo”.

Kwa jibu hili ni dhahiri kabisa graphic designing siyo mahitaji muhimu ya kazi ya uhasibu hivyo haita athiti utendaji wa kazi.


6. Kwa nini uliacha kazi yako ya mwanzo?
Hapa unahitajikua makini sana, kumbuka na epuka kuzungumza vibaya kuhusu muajiri yeyote kabla au sasa au uwezo wa muajiri. 


Hapa unaweza ukawajibu tu kwamba;" Kwa sababu ya kuboresha na kuongeza ujuzi, pia natafuta fursa bora zaidi."

7.Unatarajia kupata nini kutokana na kufanya kazi hapa? au unaweza ukaulizwa | Baada ya miaka mitatu wewe mwenyewe utakua wapi?
Ongelea unachotumaini kutimiza ila kuwa mkweli. Pia usiongee kwa ujumla. Chagua kitu maalum ambalo ni muhimu kwa kampuni alafu ilenge. Ila, uwe wazi kwa kusema itachukua muda kujifunza zaidi kuhusu kampuni ili kufanikiwa zaidi.

Kwa mfano; “Nikiwa mwalimu wa kiingereza, lengo langu ni kuongeza asilimia ya wanafunzi wanaofaulu mtihani wa taifa kuwa 85% ya darasa yangu. Najua itachukua muda kujua vizuri changamoto za wanafunzi ila, naamini nitafanikiwa”


Ni vizuri kusema kwamba unatumaini kuona uwajibikaji zaidi  katika kampuni hiyo na kuongeza thamani katika kampuni kwa mchango wako. 

8.Kwanini umekaa muda mrefu bila kupata ajira?

Wajibu kwamba; "Nilikuwa najiendeleza katika taaluma yangu "


9. Eleza namna unavyoweza kujisimamia mwenyewe
Wajibu kwamba: Nitakuwa nafanya kazi niliyopewa nikishirkiana na wasimamizi wangu na viongozi juu ya namna ya kumaliza kazi kabla ya muda uliopangwa.


10. Kitu gani kinakukera miongoni mwa wafanyakazi wenzako?

Wajibu kwamba; "Naamini katika kufanya kazi kwa pamoja. Hata kama nikikerwa na kitu chochote, huwa najaribu kuepuka isipokuwa kama ni kitu cha binafsi."

11.Unategemea kufanya kazi kwa muda gani kama ukipewa ajira?

Wajibu:Kwa muda mrefu kama nitaendelea kuongeza kitu katika taaluma yangu.

12:Je, mwenyewe unajiona kufanikiwa?

Wajibu: Ndio, ukiachana na uwezo wa taaluma yangu, nadhani nimepata watu sahihi wa kufanya nao kazi.

13. Uwezo wako ni upi katika kazi?
Wajibu: Mimi huwa naelewa na kufundishika kwa haraka na ni mchapakazi wa kweli.

14,Unapenda nafasi au cheo gani katika timu unayofanya nayo kazi?
Wajibu: Haijalishi hadi nitakapojifunza kitu kipya kwa kila mradi au kazi.

15.Je, unaswali lolote kwetu? 

Mwishoni wa interview, ni kawaida kwa mwajiri kuuliza kama una maswali kwao. Ukipewa nafasi hii, usiulizie mshaara na faida zingine. Badala yake, uliza:
  1.     Maadili ya kampuni
  2.     Aina ya uongozi
  3.     Wafanyakazi wenzako
  4.     Chochote ambacho hukuelewa kuhusu kazi hiyo.
  5.     Watakupa jibu baada ya muda gani?
==>>USIFANYE HAYA MAKOSA KATIKA SWALI HILO:
- Je, kuna fursa ya kukua / kupandishwa ngazi?
- Nitapata siku ngapi za likizo?

- waajiliwa wanafaidika vipi na kampuni hii. 

==>Tiba bora ya msongo wa interview ni kujiandaa
Ingawa interview inaweza ikakupa misongo mingi, ukijiandaa vizuri Utashangazwa na mafanikio yako.

Interview ni nafasi yako ya mwisho kumvutia mwajiri, na vidokezo vilivyoelezwa hapo juu vitakusaidia na hilo.

Kumbuka, hamna haja ya kuwa na wasiwasi ukiwa umejiandaa. 


Nakutakia Mafanikio mema kwenye Interview
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

👉Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya kujibu vizuri maswali ya Interview, anza kutafuta kazi unayoitaka kwa kubofya hapo chini. 


Hilo ni Jukwaa Maalumu la Ajira zote za Serikali, Makampuni Binafsi n.k. Kuna Nafasi za Kazi zaidi ya 7000 kwa ajili yako.

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/jobs 


▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi October 24

Serikali Yashtukia Kusuasua Kwa Uendeshaji Kiwanda Cha Tanga Fresh.

$
0
0
Na. Edward Kondela
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeshtukia kusuasua kwa uendeshaji wa kiwanda cha Tanga Fresh hali iliyolazimu kuundwa tume kufanya uchunguzi wa namna kiwanda kinavyofanya kazi ikiwemo kuchunguza mtambo unaotumika kusindika maziwa ya muda mrefu ambao unadaiwa umekuwa ukiongeza gharama ya uendeshaji wa kiwanda hicho.

Akizungumza jana (21.10.2019) katika kiwanda cha Tanga Fresh mjini Tanga, kwenye kikao kilichohusisha menejimenti ya kiwanda pamoja na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) kinachomiliki asilimia 43 ya kiwanda hicho.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amefafanua kuwa serikali itahakikisha inachukua hatua kunusuru kiwanda kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alipotembelea kiwanda hicho mwaka 2017 na kuahidiwa na menejimenti kusindika maziwa lita laki moja kwa siku ambapo katika ziara hiyo Rais Magufuli aliwasaidia kupata hati iliyokuwa imekwama kwa miaka mingi, kuondoa changamoto ya wanahisa juu ya hisa zao Tume ya Ushindani (FCC) hali iliyopelekea kiwanda  kuanza kujitanua na kuongeza uzalishaji wa maziwa ya muda mrefu (UHT) ingawa kiwanda kiliamua kuchukua mkopo Benki ya Biashara (NMB), unaoonekana kuwalemea na kutofanya vizuri sawa na ahadi kwa Rais Magufuli.

“Kwanza serikali imebaini manunuzi ya mtambo wa kusindika maziwa ya muda mrefu kuwa ni mtambo uliyokwishatumika na umenunuliwa kwa zaidi ya Shilingi Bilioni Sita, pia riba ya mkopo kuwa ni kubwa na kuwa mzigo, hivyo nimeagiza iundwe tume ambayo tayari Mkuu wa Mkoa wa Tanga ameiunda kuanzia leo kufanya uchunguzi wa mtambo ulionunuliwa ikiwemo fedha ya kununulia mtambo huo na utaratibu uliotumika kununulia mtambo.” Amesema Mhe. Ulega

Aidha Mhe. Ulega ameitaka bodi ya wakurugenzi wa kiwanda pamoja na wamiliki wakae pamoja na Benki ya Kilimo (TADB) kuitaka benki hiyo kununua deni hilo ili kutoa nafuu kwa kiwanda na kuondoa mzigo kwa wafugaji na kuinua kipato chao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigella amesema tayari timu ya wataalamu wakiwemo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) imeshaundwa ili kubaini hali ya mtambo wa kusindika maziwa. 

Bw. Shigella amefafanua kuwa serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayebainika kukihujumu Kiwanda cha Tanga Fresh ikiwemo kununua mtambo wa kusindika maziwa usio na tija kwa kiwanda hicho.

Nao baadhi ya wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) wamepongeza hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na uongozi wa Mkoa wa Tanga kutafuta suluhu ya namna ya kuboresha Kiwanda cha Tanga Fresh ili kiweze kuongeza uzalishaji na kuwanufaisha wafugaji ambao wamekuwa wakiuza maziwa katika kiwanda hicho pamoja na kutaka kiwanda hicho kiongeze bei ya kununua maziwa kutoka kwa wafugaji hao ambao hawaridhiki na bei ya Shilingi 700 kwa lita moja.

Kikao baina ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, uongozi wa mkoa wa Tanga, menejimenti ya kiwanda cha Tanga Fresh, bodi na wamiliki wa kiwanda kinatarajiwa kuendelea hii leo (22.10.2019) ili kutafuta suluhu ya kunusuru kiwanda hicho baada ya kupata hasara kwa miaka mitatu mfululizo.

Mwisho.

Uamuzi wa Mahakama Kuhusu Sheria ya mtoto kuolewa chini ya miaka 18

$
0
0
Mahakama ya Rufani Tanzania imeitaka Serikali ya Tanzania kubadilisha vifungu vya Sheria ya Ndoa inayoruhusu Mtoto wa Kike kuolewa chini ya miaka 18 ili kuweka usawa baina ya Mtoto wa Kike na Kiume.

Uamuzi huo umesomwa jana na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Eddie Fussi ambapo alisema Mahakama ya Rufani inakubaliana na hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa Julai 8, 2016.

Msajili Fussi akisoma uamuzi huo ulioandikwa na Jopo la Majaji watatu ambao ni Augustine Mwarija , Winfrida Korosso na Dk Mary Lavira amesema sheria hiyo inakiuka Katiba na haiweki usawa baina ya mtoto wa Kiume na Wakike.

Katika uamuzi huo, amesema kuwa mahakama ya rufaa inaona watoto wote ni sawa bila kuangalia mtoto wa Kiume ama Wakike.

“Hauwezi kusema ndoa itampa ulinzi mtoto wa Kike wakati huko ndio kwenye manyanyaso, anaweza kupata mimba za utotoni. Kama mtoto hawezi kupiga kura na hawezi kuingia katika mkataba wowote, kwanini aingie kwenye mkataba wa ndoa na aolewe,”

Amesema kuwa Mahakama ya Rufani inakubaliana na Mahakama Kuu ya kutaka kubadilishwa kwa kipengele cha 13 cha Katiba ambacho kinasema (Mtoto wa Kiume awe na 18 ili aweze kuoa na mtoto wa kike anaweza kuolewa chini ya miaka 18).

Pia Kifungu cha 17 (Kinatoa namna ambayo mzazi ama mlezi anaweza kutoa ridhaa ya mtoto kuolewa), vifungu ambavyo vinakiuka Katiba na havina mashiko.

“Serikali ifate maelezo ya Mahakama Kuu ya kubadilisha sheria hizo,” amesema.

Julai 8, 2016 Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Jopo la majaji watatu wakiongozwa na Shaban Lila ilibatilisha vifungu cha Sheria ya Ndoa kinachoruhusu ndoa za utotoni.

Kutokana na uamuzi huo, Serikali ya Tanzania ilikata rufaa ambapo miongoni mwa sababu zao ni kwamba wanalinda watoto dhidi ya ngono na kupata watoto nje ya ndoa.

Kesi ya sheria ya Ndoa za Utotoni ilifunguliwa na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Msichana Initiative, linalojihusisha na utetezi wa haki ya mtoto wa kike ya kusoma, Rebeca Gyumi.

DC Mjema Amjibu RC Paul Makonda

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema pamoja na afisa utamaduni wa Wilaya Cloude Mpelembwa wameeleza kuwa hawajakataza watu wasifanye ibada katikati ya wiki.

Hayo yamesemwa  na mkuu wa wilaya hiyo, baada ya mkuu wa Mkoa  wa Dar Paul Makonda kutengua kauli ya awali ya mkuu wa wilaya ya Ilala ya kuwataka wananchi kuto fanya ibada katikati ya wiki.

Mjema amesema kwamba watu wamemtafasiri vibaya kuwa amekataza  ibada ila amepinga wale wanao anzisha makanisa yasiyo rasmi.

“Wale ambao wamejenga tu turubai na wameweka maspika hao lazima watuambia wamesha sajiliwa na nimemuagiza afisa utamaduni aende akawaangalie kama wamesajiliwa,” amesema  Mjema.

“Nataka niliweke sawa kabisa mimi ni muumini mzuri wa kumuamini Mungu siwezi kuzuia watu wasiende kuabudu tumesema kuna watu wanaanzisha makanisa yasiyo stahili na ukiingia ndani ya makanisa hayo unakuta watu wa tano au sita wanao sali jumatatu hadi jumatatu. Kazi wanafanya lini,” amesema Mjema.

Naye afisa utamaduni wa manispaa  hiyo  Mpelembwa, amesema  mkuu wa wilaya hakuwa na kosa lolote bali alitoa ushauri kuwa matumizi ya vyombo vya mziki visiwe kero kwa wananchi wengine na waumini wanatakiwa wafanye kazi za kujiletea kipato.

“Siku za ibada za msingi kabisa ni Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, lakini Jumatatu mpaka Ijumaa watu wanaruhusiwa kufanya ibada katika maeneo ya ibada na ushauri ulitolewa kwamba wazingatie katika matumizi ya vyombo vya muziki," amesema Mpelembwa.

Wanafunzi 8 waliochoma mabweni shule ya sekondari Kiwanja wafukuzwa

$
0
0
Wanafunzi nane wa Shule ya Sekondari Kiwanja, wilayani Chunya, wamefukuzwa shule kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kuchoma mabweni ya shule hiyo pamoja na kukutwa na simu na vitu vingine ambavyo haviruhusiwi shuleni.

Uamuzi huo umetangazwa jana  shuleni hapo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, alipoenda kuangalia maendeo ya ukarabati wa mabweni hayo ambapo amesema uamuzi huo umefanywa na Bodi ya Shule hiyo kabla haijavunjwa.

Chalamila amesema wanafunzi saba kati ya waliofukuzwa wanakabiliwa na kesi ya kuchoma mabweni ya shule mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu na kuisababisha serikali hasara kubwa. Na mwanafunzi mmoja amefukuzwa kosa la kukutwa na simu pamoja  na kondomu kwenye begi lake wakati akirejea shuleni.

“Hao wote wanaokabiliwa na kesi wamefukuzwa, lakini wanaunganishwa na huyo ambaye alirejea tena shuleni akiwa na simu kwenye begi lake pamoja na kondomu, inaonyesha hii shule mnabakana sana, sasa ole wenu tuje tuwakamate” amesema Chalamila.

Aidha, Chalamila amesema kwa wanafunzi ambao bado hawajakamilisha malipo yao hawataruhusiwa kuingia darasani mpaka Novemba 1, mwaka huu ambapo watatakiwa kupeleka risiti za malipo na barua ya kukiri kosa na kueleza sababu ya kwanini wamechelewa. Na endapo watakiuka agizo hilo Bodi ya Shule itatakiwa ikae na kufanya maamuzi mengine dhidi yao ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule.

Hata hivyo, amewapa wiki moja wanafunzi ambao bado hawajakamilisha malipo ya fedha za kukarabati mabweni yaliyoteketea kwa moto kuhakikisha wanakamilisha ili waendelee na masomo.

Mkuu wa Shule hiyo, Elly Mnyarape amewataja wanafunzi waliofukuzwa shule kuwa ni Loren Msechu, Barnaba Minga, Samwel Ibrahim na Osward Msomba kidato cha sita, James Kunambi na Baraka Kasisike kidato cha nne.

Na kijana aliyekutwa na simu pamoja na kondomu kwenye begi lake baada ya kurejea kuwa ni Peter Kabimilo wa kidato cha sita ambaye amekimbia na hajulikani alipo.

Jafo Aziagiza Halmashauri Zote Nchini Kufungua Akaunti Maalum Ya Fedha Za Wanawake, Vijana Na Walemavu

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jafo ametao mwezi mmoja kwa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinafungua akaunti maalum ya Benki kwa ajili ya fedha za maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo jana wakati akifunga kongamano la wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma nakuwataka wataalam hao kuhakikisha wanakwenda kusimamia zoezi hilo na kukamilisha katika kwa kipindi cha mwezi mmoja.

‘’Natoa maagizo ifikapo Novemba, 30 kila Halmashauri Nchini iwe imefungua akaunti maalum ya Benki kwa ajili fedha ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kuwa fedha zikitolewa katika mfumo wa sasa zinakuwa kama zinaelea’’. Alisitsiiza Waziri Jaffo.

Aidha Waziri Jafo aliongeza kuwa fedha hizi zinapotelewa bila akaunti hiyo inakuwa vigumu kwa serikali kuzifanyia tathimini hivyo kuwaimiza wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii katika Halmashauri zao kuhakikisha wanatekeleza agizo hilo ili malengo na matumizi ya fedha hizo yaweze kufanyiwa tathimini.

Pamoja na kutoa agizo hilo Waziri Jafo pia ameongeza kuwa ili jamii iweze kuleta mabadiliko yanayotakiwa suala la kutumia wataalam wa maendeleo ya jamii halikwepiki kwa sasa wakati jamii inataka mabadiliko ya haraka kuelekea Tanzania ya viwanda.

Wataalam hawa ni chachu ya mabadiliko na katika mashirika makubwa duniani wataalam wa maendeleo ya jamii wamekuwa wakitumiwa sana ili kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali na wamekuwa msaada mkubwa kitaifa na kimataifa.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katika hotuba yake kwa Waziri huyo aliongeza kuwa kongomano hilo lilikuwa na mjadala mkubwa kuhusu kuhamasisha jamii kujiletea maendeleo  kwa kutumia istilahi zilizoko katika jamii akitolea mfano wa istilahi maalufu kwa mikoa ya ya kati ijulikanayo kama Msalagambo.

Aidha Dkt. Jingu aliongeza kuwa matokeo ya kongamano hilo pia nikuwafanya wataalam hao wajione kuwa wao ni chachu ya maendeleo katika kuhamasisha wananchi kuwa na ari ya kujiletea maendeleo.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka TAMISEMI aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara yake katika Kongomano hilo Bw.John Miayo Cheo aliwataka wataam wa maendeleo ya jamii kutumia taaluma yao kuhamasisha wananchi kugombea nafasi za uongozi ili waweze kuwa viongozi wa kufuatia uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa.

Wataalamu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wamekutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wao wa mwaka kwa lengo la kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku nne

Waziri Jafo Azitaka Mamlaka Za Serikali Za Mitaa Kuwatumia Ipasavyo Wataalam Sekta Ya Maendeleo Ya Jamii.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo ameagiza Wizara yake kuhakikisha wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii wanapewa jukumu la kusimamia kazi  ya  Bima ya Afya ya Jamii (CHF) Iliyoboreshwa katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri kwa kuwa ndio wenye utaalam wa kuhamasisha jamii.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa kufunga Kongamano la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii lililofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu nakuwataka wataalam hao kutumia taaluma yao iposavyo kufanikisha zoezi hilo.

Aidha Waziri Jafo aliongeza kuwa kazi hiyo imekuwa ikitekelezwa na wataalam wa sekta ya Afya ambao kitaaluma wana fani ya tiba na madawa lakini linapokuja suala la uhamasishaji wa jamii kuhamasika kushiriki masuala ya maendeleo ni wataalam wa maendeleo ya jamii waliobobea katika fani hiyo.

“Katika wafanyakazi ambao wamekuwa hawapewi kipaumbele na kudhalauliwa katika maeneo yao ya kazi ni wataalam wa maendeleo ya jamii lakini sasa wakati umefika kuwapatia vitendea kazi na kuwatumia katika shughuli zote za maendeleo ya Taifa”. Aliongeza Waziri Jaffo.

Aidha Waziri Jafo aliongeza kuwa kwa kipindi kirefu wataalam hawa wamekuwa hawatumiki ipasavyo na badala yake wamekuwa wakitumiwa wakati wa dharula au katika kazi za zimamoto wakati ukiangalia watumishi wengi wa serikali wataalam hawa ni moja ya kada yenye wasomi wengi.

Kufuatia ari hiyo waziri Jafo ameagiza mamlaka zilizochini ya Serikali za mitaa Nchini kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ya wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii kwa kuwapatia vitendea kazi ikiwemo kuhakikisha wanapatiwa magari ili waweze kufuatilia kazi zao vizuri tofauti na sasa ambapo mazingira yao ya kazi yana hali duni.

Waziri Jafo pia amewataka wataalam hao wa maendeleo ya jamii kujiamini katika utendaji kazi wao na kuhakikisha wanasimamia misimamo katika vikao vya mbalimbali vya maamuzi ikiwemo CMT ili waweze kukubalika na kuaminika kama ilivyo kada nyingine katika maeneo yao ya kazi.

Waziri huyo amewaagiza watendaji kazi wote serikalini kufanya kazi kwa bidii ili hata mtumishi akienda likizo wanaobaki ofisini waone umuhimu wake lakini kama mtumishi akiama au kwenda likizo na watu wasione upungufu wowote ujue mtumishi huyo hatoshi katika eneo hilo.

Wakati huohuo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu katika salamu zake kwa waziri huyo alisema kuwa kongamano la wataalam wa maendeleo wa jamii limekuwa na mada ambazo kimsingi zitawaletea mabadiliko katika utendaji kazi wao ikiwemo mada ya kuamsha ari ya wananchi kuoresha makazi yao.

Aidha Dkt Jingu amesema kongamano hilo limekuja na maadhimio na mapendekezo yanayoangazia namna bora ya utendaji kazi wao lakini kutokana na kongamano hilo wataalam hawa wamejiwekea malengo yanayopimika kwa mstakabali wa taaluma yao.

Wataalamu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wanakutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wao wa mwaka kwa lengo la kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku nne.

MWISHO.

Matumizi Ya Tehama Yameimarisha Usalama Wa Taarifa Na Huduma Za Serikali

$
0
0
Na Ismail Ngayonga,MAELEZO
SERA ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2003, pamoja na mambo mengine inasisitiza juu ya Serikali kutumia fursa za TEHAMA katika utendaji kazi wa kila siku na utoaji huduma kwa wananchi.

Katika kutekeleza sera hiyo, mwaka 2004 Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR-MUU) ilianza kuchukua hatua mbalimbali kuongeza matumizi ya TEHAMA katika kuimarisha mifumo ya utoaji habari na huduma kwa wananchi.

Baadhi ya hatua hizo ni pamoja na kuanza utekelezaji wa dhana ya Serikali Mtandao iliyokuwa sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Mabadiliko katika Utumishi wa Umma (Public Service Reform Programu – PSRP).

Programu hiyo ililenga kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na uboreshaji wa utoaji huduma kwa umma. Pamoja na mambo mengine, Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ziliwezeshwa kuwa na mifumo imara ya Menejimenti ya Habari.

Aidha, Serikali iliziwezesha taasisi za umma kuwa na Tovuti zake ambapo hadi kufika mwaka 2010 takribani Taasisi zote za Serikali zilikuwa na Tovuti, ambapo kwa sasa matumizi ya TEHAMA yameongezeka kwa kasi Serikalini na zimeongeza uwazi, ufanisi, uwajibikaji na tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika anasema Serikali imeendelea kusimamia matumizi ya mifumo na miundombinu ya TEHAMA Serikalini ili kuongeza ufanisi na usalama wa taarifa za Serikali.

Anaongeza kuwa mifumo na miundombinu hiyo ni pamoja na Vituo Vikuu vya Kuhifadhi Mifumo  na Taarifa za Serikali kwa kuongeza Taasisi mpya 13 hivyo kufanya jumla ya taasisi zilizohifadhi mifumo na taarifa zao kufikia 43, Mfumo wa barua pepe Serikalini (GMS) kwa kuongeza taasisi mpya 39 na kufanya jumla ya taasisi zilizounganishwa kufikia 398.

Anaitaja mifumo na miundombinu mingine ni  Mfumo wa Ofisi Mtandao (e-office) kwa kuongeza taasisi  mpya  15  na  kufanya jumla ya taasisi zilizounganishwa kufikia 48, Mfumo wa kutoa huduma kwa Umma kupitia simu za Mkononi (Government Mobile Platform (GMP) kwa kuongeza taasisi mpya 24 na kufanya jumla ya taasisi zilizounganishwa kufikia 146.

Kwa mujibu wa Mkuchika anasema Serikali ilitoa mafunzo ya utekelezaji wa Serikali Mtandao kwa kwa Viongozi, Wasimamizi wa TEHAMA na watumiaji wa huduma za Serikali Mtandao kwa Taasisi za Umma 98 ili kuongeza uelewa na uwezo wa Taasisi hizo katika kutumia TEHAMA, kuongeza ufanisi wa kiutendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Waziri Mkuchika anasema Serikali pia ilitoa ushauri wa kitaalam kwenye maeneo ya Serikali Mtandao kwa Taasisi za Umma 23 ili kuhakikisha kwamba uwekezaji unaofanywa na Serikali kwenye TEHAMA unatoa matokeo yaliyokusudiwa.

‘‘Msaada wa kiufundi umetolewa kwa Taasisi za Umma 252 kupitia Mfumo wa Kutoa Msaada na Huduma kwa Wateja (Helpdesk System) unaopatikana saa ishirini na nne (24/7)’’ anasema Waziri Mkuchika.

Akifafanua zaidi Waziri Mkuchika anasema Mifumo mikubwa ya TEHAMA imetengenezwa kwa Taasisi za Umma kwa lengo la kuboresha utendaji kazi, kuboresha utoaji huduma kwa umma, kurahisisha ukusanyaji wa mapato na kuondoa mianya ya rushwa.

Anaitaja baadhi ya mifumo iliyotengenezwa ni pamoja na Mfumo wa Tiketi za Kieletroniki kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Mfumo wa kusajili wahandisi kwa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Mfumo wa kufanya usajili wa wataalam wa ununuzi na ugavi kwa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

‘’Wataalam wa Wakala ya Serikali Mtandao 11 wamewezeshwa kupata  mafunzo yanayotolewa na Bodi mbalimbali za Kitaalam kwenye maeneo ya usalama mtandao, miundombinu na utengenezaji wa Mifumo na Vile vile watumishi 7 wamewezeshwa kupata mafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya Stashahada, Uzamili na Uzamivu’’ anasema Waziri Mkuchika.

Matumizi ya TEHAMA yameisaidia Serikali kuongeza uwazi, ufanisi, uwajibikaji na tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi hususani katika zama hizi ambazo  taarifa na huduma za Serikali zimekuwa zikitolewa kwa njia ya nyaraka kupitia muundo wa karatasi.

PICHA: Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Akisalimiana Na Rais Wa Urusi Vladimir Putin

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimaiana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin katika hafla ya kuwakaribisha Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya  Afrika  wanaoshiriki katika Mkutano baina ya Urusi na Afrika unaofanyika  Sochi nchini Urusi, Oktoba 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

VIDEO | Rosa Ree Ft. Fik Fameica – Acha Ungese

$
0
0
VIDEO | Rosa Ree Ft. Fik Fameica – Acha Ungese

Wateja wa TECNO sasa kunufaika na ujio wa toleo jipya la TECNO Camon 12, Camon 12 air na Camon 12 pro

$
0
0
Wateja wa TECNO sasa kunufaika na ujio wa toleo jipya la TECNO Camon 12, Camon 12 air na Camon 12 pro pamoja na kauli mbiu mpya ya TECNO EXPECT MORE.

Kauli mbiu ya TECNO EXPECT MORE inathibitisha juu ya ujio wa matoleo mapya kuwa na ubora zaidi kama ilivyo kwa toleo jipya la TECNO Camon 12 lakin vile vile ujio wa TECNO Camon 12 unaashiria mapinduzi ya mapinduzi katika mfumo wa kidigital kupita kamera yake yenye 16MP AI Max Rear Triple Camera.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi, afisa wa mahusiano wa TECNO Mobile Tanzania Bwana Eric Mkomoye alisema kwamba, “mageuzi ya kiteknolojia kutoka analojia kwenda digitali yanawezekana kama sifa zote zinazoitajika zinapatikana kiganjani mwako kama vile kamera nzuri, batteri yenye nguvu, uwezo mkubwa wa kuhifadhi data na muonekano mzuri wa kipekee”,
 
Bwana Mkomoye, aliorodhesha sifa za TECNO Camon 12 kama zifuatavyo; “16MP+2MP+8MP Rear camera with quad flash, 16MP AI Clear Selfie, GB 64+GB 4,4000mAh batteri, 6.52" Crystal Dot Notch Screen, 4G na Android 9 Pie”,
 
Vile vile aligusia kuhusiana na kauli mbiu mpya ya TECNO EXPECT MORE na ofa inayopatikana katika camon 12 kwa kusema ni muda mrefu sasa wadau wa TECNO wameshuhudia mengi ikiwamo simu zetu zenye kubeba sifa za hali ya juu katika bei Rafiki na sasa tumeona ni muda wakutegemea mapinduzi yenye ubora zaidi ya awali na kuhusiana na ofa TECNO imewapa nafasi watumiaji wote wa TECNO camon series kubadili kwa TECNO camon 12 kwa kiasi cha shilling 203,463 za kitanzania. https://www.tecno-mobile.com/pre-order/tz/camon12series-activity?uid=359#/
 
Wakati wa uzinduzi mmoja wa mawakala wa TECNO, Bw.Abuyi alituelezea uzoefu wake wakufanya kazi na TECNO kuanzia ilipoanzaishwa nchini Tanzania, alieleza zaidi kuhusu furaha yake kuiona TECNO kupiga hatua kubwa pia imesaidia wafanyabiashara kufanikiwa katika soko.
 
Uzinduzi huu uliudhuriwa na wadau kutoka sekta mbalimbali mfano, masoko,mauzo na teknolojia. Kutoka upande wa masoko na mauzo alikuepo mkurugenzi mtendaji wa Airtel Bw.George Mathen pamoja na Afisa Masoko wa Airtel Bw. Amit Chandiramani, Mkurugenzi mtawala wa TIGO Bw.Simon akiwa na Afisa Masoko Bw.Tariq na kutoka Vodacom alikuwepo Mkurugenzi mtawala Bw.Hashim Hendi na Mragahabishi ambaye pia ni mpiga picha Bw.Osse Greca Sinare.
 
Tofauti na Uzinduzi ,shughuli nyingine kama burudani kutoka kwa wasanii na droo ya kubahatisha vilifanyika ambapo wageni waalikwa walipata nafasi kujishinda toleo jipya la simu aina ya TECNO Camon 12 papo kwa hapo.
 
TECNO inajivunia kutengeneza na kusambaza simu janja zenye ubora na matumizi Rafiki kwa mazingira husika. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti hii https://www.tecno-mobile.com
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images