Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wizara Ya Kilimo Yaja Na Mkakati Wa Kuzalisha Miche Milioni 20 Ya Kahawa

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kilimanjaro
Moja ya changamoto katika kuimarisha ubora wa Kahawa ni uzalishaji mdogo ya Miche ya Kahawa huku mahitaji yakiwa ni makubwa kwa wakulima.

Wizara ya Kilimo imekusudia kuzalisha mbegu mpya ambazo ni bora za kahawa kwa lengo kubwa la kubadilisha mikahawa ya zamani ipatayo milioni 240 kwa kutumia aina mpya za kahawa.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 21 Octoba 2019 wakati wa uzinduzi wa vitabu vya kanuni bora na mitaala ya ufundishaji katika zao la Kahawa katika Ofisi za Taasisi ya utafiti wa Kahawa TACRI Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa uzalishaji wa idadi ya miche milioni saba (7) kwa mwaka ni kidogo, ambapo itatuchukua takribani Miaka 35 kubadili aina hizi za zamani hivyo aliahidi kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo itahakikisha kunakuwa na mapinduzi ya Kilimo cha kahawa nchini.

Katika kuifikia dhamira ya kubadili mikahawa ya zamani serikali kupitia wizara ya kilimo imejipanga kuanza kuzalisha Miche milioni 20 ya kahawa mpya ili kuongeza tija na uzalishaji wa kahawa.

Amesema kuwa sekta ndogo ya kahawa ina umuhimu mkubwa kwenye uchumi wa taifa na huchangia takribani asilimia 24 kwa mwaka ya mapato ya mauzo ya bidhaa za kilimo nje ya nchi, ambapo ni wastani wa asilimia 4 ya pato la taifa.

Hata hivyo, pamoja na mchango huo wa sekta ndogo ya kahawa uzalishaji bado ni mdogo sana, ambapo kwa mwaka wastani wa tani 50,000 huzalishwa.

Aliongeza kuwa hali hiyo inasababishwa na tija ndogo ambapo mpaka sasa mti mmoja wa kahawa unatoa gramu 250 ikilinganishwa na wastani wa gramu 1,000 inayotakiwa kuvunwa kwa mti.

Moja ya changamoto inayosababisha tija kuwa chini katika sekta ndogo ya kahawa ni ukosefu wa elimu ya kanuni bora ya kilimo cha kahawa kwa wakulima ambapo amewataka maafisa kilimo kote nchini kuanza kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa mikahawa mipya.

Alisema ili kuhakisha kuwa mkulima anapata tija kubwa na kuongeza kipato kutokana na kilimo cha kahawa, ni muhimu kupata elimu ya uzalishaji wa kahawa kwa kuzingatia matumizi sahihi ya kanuni bora za kilimo cha kahawa.

Waziri Hasunga ameipongeza TaCRI kwa kuandaa vitabu vilivyozinduliwa kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kanuni bora za utunzaji wa kahawa aina ya Arabika na Robusta pamoja na mitaala ya mafunzo ambavyo vitatumika kwa Maafisa Ugani, Wakulima na Wananchi wote wenye nia ya kujifunza mbinu bora za kilimo cha kahawa chenye  tija.

Mhe Hasunga amesema kuwa Vitabu hivyo vyenye picha na maelezo ya kutosha vimelenga kuwapa wakulima wa kahawa utaalamu wa kukuza zao la kahawa katika lugha rahisi ambapo lengo la vitabu hivyo ni kuhakisha kuwa kaya za wakulima wa kahawa zipatazo 420,000 nchini; wanakuwa na rejea ya haraka na rahisi wakati wote wawapo shambani, mahali ambapo hawana wataalamu; na pale ambapo kutakuwa na mtaalamu vitakuwa vichocheo vya mazungumzo ili kuweza kujua zaidi au kupata ufafanuzi wa kitaalamu wa masuala ya kilimo cha kahawa.


Ofisa Takukuru atiwa mbaroni kwa madai ya kumuua Mkewe kwa Risasi

$
0
0
Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Tunduru, James Paulo (27), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuua kwa kumpiga risasi mke wake.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya kitendo hicho usiku wa kuamkia Oktoba 21, mwaka huu, baada ya kutokea ugomvi kati yao.

Kamanda Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba chanzo cha kifo hicho ni ugomvi uliosababishwa na tukio la wivu wa kimpenzi.

Kamanda alimtaja mtu aliyeuawa kuwa ni Beatha Kufuru (25), ambaye alikuwa muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru.

Kamanda Marwa ambaye alikuwa akizungumzia tukio hilo akiwa njiani kwenda Tunduru ili kujiridhisha na hali halisi, alisema mtuhumiwa huyo alimpiga risasi tatu kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo.

Alisema polisi wanaendelea na uchuguzi wa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria.

Makonda atengua kauli ya DC wa Ilala....."Huwezi Kunipangia Muda wa Kusali"

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ametengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, iliyokuwa inazuia watu kuabudu katikati ya juma kwa madai ya kuwa hawezi kuwapangia watu masaa na siku za kumuabudu Mungu wao wanayemuamini.

Kauli ya kutengua agizo hilo ameitoa leo Oktoba 22, 2019, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake na kuwataka viongozi mkoani humo kuwa na kiasi hasa linapokuja suala la imani za watu na kwamba yeye anazihitaji ibada hizo katika mkoa wake.

''Upande wa imani Serikali haina dini, Natengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, watu wendelee kwa imani zao bila kuathiri sheria za nchi, viongozi tunapaswa kuwa makini tunapoingia kwenyeatika mambo ya dini, mambo ya dini ni mambo imani, mimi mwenyewe hapa ni mlokole hunipangii muda wa kusali'' amesema Makonda.

Aidha Makonda amewataka Wakuu wa Wilaya wote mkoani kwake, kuhakikisha wanakutana na viongozi waliochini yao ili kujadili njia na namna yakuleta ufumbuzi katika masuala ambayo hayako sawa, badala ya kutoa maagizo ambayo yataathiri imani za watu, kwani suala la ibada linahitaji moyo na utayari wa mtu binafsi.

Kura za maoni CCM zafutwa maeneo yenye malalamiko, vurugu

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, amesema chama hicho kumeamuru kufutwa kwa kura ya maoni maeneo yote ambayo yalikuwa na ukiukwaji wa kanuni, kisha kurudiwa upya.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Dk. Bashiru alisema kura hizo zitarudiwa bila kujali kanuni kwa kuwa zilikiukwa katika maeneo yote yanayolalamikiwa.

Alisema wote waliokuwa wamechukua fomu sasa watapata fursa ya kuchujwa kupitia kura za wanachama na si kamati za uongozi.

Dk. Bashiru alisema kutokana na hitilafu hizo, katika maeneo yote ambayo uongozi wa chama umeorodhesha na unaendelea kuorodhesha hitilafu, upigaji kura utarudiwa tena bila kufuata utaratibu wa mchujo, kama ilivyokuwa awali.

Alisema kwa sasa wale wote waliokuwa wamechukua fomu awali watapigiwa kura na mchujo wao utafanywa kwa kura za wanachama, bila kujali idadi ya waliokuwa wamechukua fomu.

“Na kwa sasa tumeamua kufanya hivi si kwa nia ya kukiuka kanuni na taratibu, bali kwa kuwa hakuna muda wa kutosha kuanza mchakato huo upya.

“Wakati wote tumekuwa tukisisitiza utii wa katiba, kanuni na taratibu za chama. Tumekuwa tukisisitiza tusipuuze maelekezo ya chama na Serikali,” alisema.

Dk. Bashiru alifafanua kuwa ni katika utaratibu huo, uongozi umeamua kuongeza siku mbili zaidi katika mchakato wa ndani ya chama, kutoka Oktoba 29 hadi Oktoba 31 ili kukamilisha marudio hayo.

“Kwa kuwa utaratibu wa wagombea wa vyama kuchukua fomu kule serikalini unaanza Oktoba 29 hadi Novemba 4, ninaamini tutawahi kukamilisha na wagombea wetu watachukua fomu kwa wakati,” alisema.

Alisema yapo maeneo ambayo hayakuzingatia kanuni za chama katika kuteua, yapo ambayo hapakuwa na maelewano katika uteuzi na yapo ambayo hayakufuata utaratibu wa uteuzi.

Askari polisi mbaroni kwa tuhuma za Rushwa

$
0
0
Na Silvia Mchuruza. Kagera.
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa  (TAKUKURU) mkoani Kagera inamshikilia  askali wa jeshi la wananchi Tanzania mwenye cheo cha Koplo(Corporal) aitwaye Nyambita Makayaga Magoma kwa kuomba rushwa.

Akizungumza na vyombo vya habari mkuu wa Takukuru mkoa John Joseph amesema kuwa askali huyo anashikiliwa kwa kosa la kuomba rushwa kwa mkazi mmoja wa wilaya ya Biharamulo kijiji cha Nemba Tsh. 3,000,000 kwa kosa la kuingiza ng’ombe katika hifadhi ya taifa(Biharamulo forest reserve.

Pamoja na hayo uchunguzi wa Takukuru ulibaini kuwa licha ya askali huyo kuomba kiasi hicho cha fedha Askali huyo alishikiliwa  mifugo hiyo mpaka  alipopatiwa jumla ya Tsh.800,000  na kisha kumwachia mwananchi huyo ambaye alilazimika kutoa taarifa hizo Takukuru.

Aidha ameongeza kuwa taasisi hiyo pia inamshikilia Koplo  (Coplo) Nassoro Maulidy Mirambo kutoka kituo cha Runazi kwa kushilikiana na Bw. Asaph Manya Manya ambaye ni mwajiriwa katika Harmashauli ya wilaya ya Biharamulo idara ya misitu ambapo walishirikiana kumuomba rushwa mfanyabiashara  wa mkaa mara baada ya kumkamata akiwa na maguni  50 ya mkaa. 

Vilevile alisema kuwa uchunguzi wa Takukuru ulibaini kwamba fedha hizo zilipokelewa na Bw.Nassor Maulidy Mirambo Agoust 23 mwaka huu  kwa mikupuo miwili ambapo alipokea kwanza shilingi 250,000 kisha baadae akapokea kiasi cha Tsh.148,000 na baadae mfanyabiashara huyo aliweza kurudishiwa mkaa wake.

Sambamba na hayo mkuu wa takukuru mkoa alimalizia kwa kutoa lai kwa watumishi wa umma kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya rushwa vinginevyo watalipia kwa matendo yao wanayoyafanya.

Serikali Yashtukia Kusuasua Kwa Uendeshaji Kiwanda Cha Tanga Fresh.

$
0
0
Na. Edward Kondela
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeshtukia kusuasua kwa uendeshaji wa kiwanda cha Tanga Fresh hali iliyolazimu kuundwa tume kufanya uchunguzi wa namna kiwanda kinavyofanya kazi ikiwemo kuchunguza mtambo unaotumika kusindika maziwa ya muda mrefu ambao unadaiwa umekuwa ukiongeza gharama ya uendeshaji wa kiwanda hicho.

Akizungumza jana (21.10.2019) katika kiwanda cha Tanga Fresh mjini Tanga, kwenye kikao kilichohusisha menejimenti ya kiwanda pamoja na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) kinachomiliki asilimia 43 ya kiwanda hicho.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amefafanua kuwa serikali itahakikisha inachukua hatua kunusuru kiwanda kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alipotembelea kiwanda hicho mwaka 2017 na kuahidiwa na menejimenti kusindika maziwa lita laki moja kwa siku ambapo katika ziara hiyo Rais Magufuli aliwasaidia kupata hati iliyokuwa imekwama kwa miaka mingi, kuondoa changamoto ya wanahisa juu ya hisa zao Tume ya Ushindani (FCC) hali iliyopelekea kiwanda  kuanza kujitanua na kuongeza uzalishaji wa maziwa ya muda mrefu (UHT) ingawa kiwanda kiliamua kuchukua mkopo Benki ya Biashara (NMB), unaoonekana kuwalemea na kutofanya vizuri sawa na ahadi kwa Rais Magufuli.

“Kwanza serikali imebaini manunuzi ya mtambo wa kusindika maziwa ya muda mrefu kuwa ni mtambo uliyokwishatumika na umenunuliwa kwa zaidi ya Shilingi Bilioni Sita, pia riba ya mkopo kuwa ni kubwa na kuwa mzigo, hivyo nimeagiza iundwe tume ambayo tayari Mkuu wa Mkoa wa Tanga ameiunda kuanzia leo kufanya uchunguzi wa mtambo ulionunuliwa ikiwemo fedha ya kununulia mtambo huo na utaratibu uliotumika kununulia mtambo.” Amesema Mhe. Ulega

Aidha Mhe. Ulega ameitaka bodi ya wakurugenzi wa kiwanda pamoja na wamiliki wakae pamoja na Benki ya Kilimo (TADB) kuitaka benki hiyo kununua deni hilo ili kutoa nafuu kwa kiwanda na kuondoa mzigo kwa wafugaji na kuinua kipato chao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigella amesema tayari timu ya wataalamu wakiwemo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) imeshaundwa ili kubaini hali ya mtambo wa kusindika maziwa. 

Bw. Shigella amefafanua kuwa serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayebainika kukihujumu Kiwanda cha Tanga Fresh ikiwemo kununua mtambo wa kusindika maziwa usio na tija kwa kiwanda hicho.

Nao baadhi ya wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) wamepongeza hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na uongozi wa Mkoa wa Tanga kutafuta suluhu ya namna ya kuboresha Kiwanda cha Tanga Fresh ili kiweze kuongeza uzalishaji na kuwanufaisha wafugaji ambao wamekuwa wakiuza maziwa katika kiwanda hicho pamoja na kutaka kiwanda hicho kiongeze bei ya kununua maziwa kutoka kwa wafugaji hao ambao hawaridhiki na bei ya Shilingi 700 kwa lita moja.

Kikao baina ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, uongozi wa mkoa wa Tanga, menejimenti ya kiwanda cha Tanga Fresh, bodi na wamiliki wa kiwanda kinatarajiwa kuendelea hii leo (22.10.2019) ili kutafuta suluhu ya kunusuru kiwanda hicho baada ya kupata hasara kwa miaka mitatu mfululizo.

Mwisho.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano October 23

Taarifa ya UTEUZI wa Kamati Maalum ya Kusimamia Haki na Kazi za Wasanii Nchini


Tanzania Yasaini Mkataba wa Mabilioni Ya Pesa Kupeleka Huduma ya Internet Burundi

$
0
0
Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tanzania TTCL imesaini makubaliano na kampuni ya BBS ya Burundi kuhusu kutoa huduma za mtandao wa Internet.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya TTCL Bw. Waziri Kindamba amesema, Makubaliano hayo yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 6 yatatekelezwa nchini Burundi kwa miaka 10 ijayo. 

Amesema TTCL itatoa huduma za ngazi ya juu kwa Burundi kwa kupitia vituo vyake vya Kabanga na Manyovu, Mkoa wa Kigoma.

Bw. Kindamba amesema utoaji wa huduma za Internet utarahisisha na kuboresha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Rwanda yazindua bandari kavu yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 35

$
0
0
Rais Paul Kagame wa Rwanda amezindua bandari kavu ya ugavi mjini Kigali, ikayotaifanya Rwanda iwe kitovu cha usafirishaji wa mizigo cha kanda hiyo.

Bandari hiyo yenye ukubwa wa mita elfu 2.5 za mraba, pia itatumiwa na kituo cha uvumbuzi wa Yiwu cha Jukwaa la biashara ya kielektroniki ya kimataifa la Alibaba (eWTP).

Kampuni kubwa zaidi ya China ya biashara ya kielektroniki ya Alibaba na kampuni ya uendeshaji wa bandari ya Dubai Ports World, zinalenga kujenga ghala hilo kuwa ghala kuu la bidhaa za China katika eneo la Afrika Mashariki na kuvumbua mfumo mpya wa kuingiza na kuuza bidhaa nje.

Habari zinasema, bandari hiyo inayogharimu dola za kimarekani milioni 35 ina yadi ya vyombo vya usafirishaji yenye ukubwa wa mita elfu 12 za mraba, na kituo cha ghala chenye ukubwa wa mita elfu 19.6 za mraba. 

Uwezo wake wa kuhifadhi mizigo utafikia tani laki 6.4 kwa mwaka.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ashindwa kuunda baraza la mawaziri

$
0
0
Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu ametangaza kushindwa kuunda baraza la mawaziri, na kurejesha mamlaka ya kufanya hivyo kwa rais Reuven Rivlin wa nchi hiyo. 

Amesema amefanya juhudi kujaribu kuunda serikali ya muungano yenye uwakilishi mkubwa, lakini ameshindwa kumshawishi kiongozi wa Chama cha Blue and White Bw. Benny Gantz kufanya mazungumzo naye. 

Taarifa iliyotolewa na ikulu ya nchi hiyo inasema rais Rivlin anapanga kumkabidhi Bw. Gantz jukumu la kuunda baraza la mawaziri, na atakuwa na muda wa siku 28 kufanya hivyo.

Waalimu Watoro Na Wachelewaji Kuchukuliwa Hatua

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amefanya ziara ya kushtukiza katika baadhi ya shule za Msingi na Sekondari na kisha kumuagiza Afisa Elimu Mkoa kuwachukulia hatua za kinidhamu waalimu wote ambao wanachelewa au kutohudhuria shuleni.

Brig. Jen.  Mwangela ametoa agizo hilo mapema jana mara baada ya kutembelea shule za sekondari za Myovizi na Simbega pamoja na Shule ya Msingi Iyula za Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi na kubaini utoro na uchelewaji wa waalimu mara baada ya kukagua madaftari ya mahudhurio.

“Mahudhurio ya waalimu sio mazuri, waalimu hawafiki wote katika shule zao na wengine huchelewa sana, pia vitabu vya mahudhurio havijafungwa ifikapo saa moja na nusu na saa moja na dakika 45 kama inavyotakiwa ili kuwabana wachelewaji.”, amesema Brig. Jen.  Mwangela.

Brig. Jen.  Mwangela amesema Afisa Elimu Mkoa anapaswa kusimamia mahudhurio ya waalimu kwakuwa msingi wa taifa unajengwa shuleni na msingi huo hauta imarika endapo waalimu watakosa nidhamu katika kuwahi na kuhudhuria shuleni.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Myovizi Tabu Mtafya amesema amekuwa akitoa onyo kwa waalimu ambao wanachelewa hivyo agizo la Mkuu wa Mkoa ataendelea kulitekeleza.

“Baada ya Mkuu wetu wa Mkoa kukagua kitabu cha Mahudhurio ameniagiza niendelee kusimamia mahudhurio ya waalimu, nami nitawaita waalimu wote wa shule yangu niwakumbushe juu ya kuwahi na kutimiza wajibu wao.”, amesema Mtafya.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo amekiri kuwepo kwa mapungufu ya waalimu kutohudhuria au kuchelewa shuleni na hivyo wamejipanga katika Wilaya ya hiyo kusimamia mahudhurio ya waalimu na kwachukulia hatua za kinidhamu waalimu watoro na wachelewaji.

Chuo kikuu cha Dar es Salaam Kuanza Kutoa Mitihani Ya Kiswahili Ya Kimataifa Kuanzia Januari,2020

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika jitihada za kukuza na kuieneza lugha ya Kiswahili,Chuo kikuu cha Dar es Salaam mapema mwezi January mwaka 2020 kinatarajia kuanza kutoa mitihani ya kimataifa ya ujuzi wa lugha hiyo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari hii jana Jijini Dodoma,Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo amesema kuwa katika awamu hii wameona mafanikio makubwa katika kuiendeleza
lugha ya Kiswahili kwani sasa imekuwa moja kati ya lugha rasmi za Jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika yaani SADC

Dkt.Akwilapo ameongeza kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitakuwa ndio Chuo kikuu cha kwanza Duniani kutunga mitihani hiyo,kusimamia udahiri na usahihishaji wake na kutoa cheti cha kimataifa kinachoonesha kiwango cha ujuzi wa mtahiniwa ambapo pia ametabainisha walengwa wa mitihani hiyo

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtanzania kutoka Taasisi ya Confucius,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Mgoda Mutembei yeye amesema kuwa kuna wananfunzi wengi wanaosoma lugha ya Kiswahili nje ya nchi na wangependa kutambulkika kuwa wamesoma lugha hiyo kwa kuwa na cheti
maalumu hivyo Chuo kikuu cha Dar es Salaam kitakuwa ni suluhisho katika suala hilo.

Dkt.Akwilapo pia ameuhakikishia umma kuwa tayari kuna makubaliano baina ya walimu wa Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na walimu wanaofundisha kiswahili katika vyuo vya nje kuhusiana na mitihani hiyo

Waziri Ummy Awataka Wataalam Wa Maendeleo Ya Jamii Kuacha Kupoteza Muda Wao Kutumiana Katuni Kwenye Makundi Ya Whatsapp

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa afya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh Ummy mwalimu amewataka wataalamu wa  Maendeleo ya Jamii kuongeza kasi ya kuhamasisha jamii ili itumie teknolojia zitakazowasaidia kubadilisha maisha yao  na kupata muda zaidi wa kufanya shughuli za maendeleo .

Waziri ummy ameyasema hayo jana  jijini Dodoma wakati akifungua kongamano na mkutano mkuu wa sekta ya maendeleo ya jamii wa mwaka 2019, pamoja na  kuzindua mwongozo wa majukumu ya wataalamu wa maendeleo ya jamii na chama cha watalaamu wa maendeleo ya jamii huku pia akiwataka kuacha kutumiana katuni kwenye makundi ya Mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na Whatsaap.

Aidha, Waziri ummy ameongeza kuwa ni wajibu wa wataalamu wa maendeleo ya jamii kuwafikia wanachi katika kupata    maendeleo  licha ya kuwa ziko changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabili ambapo amewataka  kutokujiweka nyuma katika utendaji wao wa kazi kila siku na kuwasisitizia kuwa wabunifu.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Maendeleo ya jamii kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia ,wazee na watoto Patrick Golwike amesema kongamano hilo limefanyika kwa nia ya  kuwakutanisha watunga sera na watekelezaji ili kutathmini utekelezaji wa malengo ambayo wamejipangia.

Nae Rais wa Chama cha wataalamu wa maendeleo ya jamii, Wambura Sunday amesema chimbuko la chama hicho ambacho waziri ummy amezindua ni chimbuko la matokeo ya mkutano mkuu wa watalaamu wa maendeleo ya jamii uliofanyika November 2017 katika ukumbi wa nyerere katika chuo cha mipango ya maendeleo vijijini, jijini hapa.

Hatahivyo, Waziri ummy amesema serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa  na wataalamu  wa maendeleo ya jamii hapa nchini  kwani juhudi  zao zimekuwa na manufaa na jamii imeendelea kutambua wajibu wao wa kushiriki  katika maendeleo  .

RCC Kagera Yaazimia Kila Mwananchi Kulima Hekali Moja Ya Mazao Ya chakula Na Moja Ya Biashara Kuondoa Udumavu.

$
0
0
Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera
Wadau mbalimbali mkoani Kagera kwa kushirikiana na serikali pamoja na wananchi wametakiwa kulipa kipaumbeli swala la lishe bora mkoani hapa hili kupunguza na hatimaye kuondoa tatizo la lishe duni linalokabili makundi mbalimbali hususani watoto.
 
Hayo yameazimiwa katika kikao cha kamati  ya ushauri ya mkoa (Rcc) mkoani Kagera kilicho fanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkoa  mnamo tarehe 21/10/2019 nakukutanisha wajumbe zaidi 50 wakiwemo wakuu wa wilaya zinazounda mkoa wa kagera,wenyeviti wa halmashauri ,wajumbe wakamati ya ulinzi na usalama pamoja nawadau mbalimbali kutoka katika mashirika ya serikali na yasiyo ya kiserikali chini ya mkuu wa mkoa kagera Brigedia Marco Gaguti
 
Ili kufikia azimio hilo wajumbe wa kikao hicho wameazimia kuwa kila mwananchi anaye ishi katika mazingira ya kilimo lazima alime kiasi cha hekali moja ya mazao ya chakula pamoja na hekali moja ya mazao ya biashara ili kufikia malengo nakuondoa udumavu

Aidha akizungumzia soko la kahawa katibu tawala wa mkoa wa kagera Faustine Kamzola katika kikao  hicho  amesema wananchi wamkoa wa Kagera wanatakiwa kuwa wa kwanza kutumia zao hilo mara baada yakuwa limeongezewa thamani ikiwa ni baada ya kutoka kiwandani nakusema kuwa nchi za Ethiopia,Uganda na nchi kama Brazil niwazalishaji wa Kahawa kwa kiwango kikubwa lakini pia ni watumiaji wakahawa kwa wingi ukilinganisha na mkoa wa Kagera na nchi kwa ujumla.
 
“Minadhani mkoa wa Kagera ili kukuza soko la biashara ya zao letu la kahawa lazima tuwe wakwanza kutumia mavuno yetu kwsababu hata nchi za Ethiopia Uganda na Brazil ambazo zimefanikiwa katika soko la kahawa wanatumia kiwango kikubwa tofauti nasisi kagera”
 
Baada ya kuwasilishwa kwa taarifa mbalimbali ndani ya kikao hicho mmoja wa wajumbe kutoka shirika la Kadetfu ambaye nimkurugenzi wa shirika hilo Dokta Peradius Mchuruza amewaomba wajumbe kuazimia kuundwa kwa tume ya watu maalumu (tasiki force) itakayochunguza maendeleo ya maazimio yaliyowekwa katika wiki ya uwekezaji mkoani Kagera 
 
Katika upande wataaluma wajumbe wote wakikao wamepongeza ufaulu katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu baada ya kushika nafasi ya 4 kitaifa kutoka nafasi ya 5 mwaka 2018 mbali napongezi hizobado mkoa unaupungufu wa walimu mbali nakusema kuwa namaeneo mengine yana changamoto za ukosefu wa wataalamu

The List Of Batch I Loan Allocation For SUA First Year (Fresher) Students 2019-2020

$
0
0
The List Of Batch I Loan Allocation For SUA  First  Year (Fresher) Students 2019-2020
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
 
Chuo Kikuu Cha Sokoine kimetoa majina ya Wanafunzi Waliopewa Mkopo na Bodi ya Mikopo Pamoja na Kiasi cha Fedha/Mkopo waliopatiwa

Aidha, Chuo hicho kimetangaza  Nafasi za Ufadhili (Scholarships kwa wanafunzi wa PHD)


==>>Kuona namna ya kupata Ufadhili/ Scholarships  <<Ingia Hapa>>

Nafasi za Kazi Coca-Cola Kwanza (Tanzania) | Resident Account Developer

$
0
0
Job Title: Resident Account Developer
Function: Marketing & Sales
Company: Coca-Cola Kwanza (Tanzania)
Job Type : Permanent
Location - Country Tanzania
Location - Province Not Applicable
Location - Town / City Mbeya

Coca-Cola Kwanza Ltd has an exciting opportunity in Sales and Marketing department. We are looking for a talented individual with relevant skills and experience in Sales and Marketing for a Resident Account Developer position to be based in Mbeya. The successful candidate will directly report to the respective Area Sales Manager.

Key Duties & Responsibilities
The incumbent will be responsible in identifying and implementing new business opportunities, optimize customer services, manage and maintain company assets, execute outlets as per the company strategies, execute market survey and formulate account plans.

The incumbent should have at least a Degree or diploma in Sales and Marketing. Two years practical relevant experience preferably with FMCG, computer literate, flexible team player and team builder, assertive and persuasive , and demonstrate high integrity.

Deadline:  26th October, 2019

CLICK HERE TO APPLY

Waziri Mkuu: Usafiri Wa Reli Kuimarishwa Katika Majiji Yote Nchini

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Russian Railways, Bw. Alexander Misharin na kumweleza kuwa Tanzania inahitaji sana kuimarisha usafiri wa ndani wa reli hasa katika Majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Tanga.

Amesema kampuni hiyo yenye uwezo mkubwa wa kujenga reli mpya, kukarabati reli, kutengeneza injini za treni na mabehewa pamoja na ukarabati wake inahitajika sana nchini ili kufanikisha mpango wa Serikali wa kuimarisha reli za zamani za TAZARA, Reli ya Kati na kufugua reli ya Kaskazini inayounganisha mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Waziri Mkuu alizungumza na Mkurugenzi huo jana (Oktoba 22, 2019) kwenye hoteli ya Marriot iliyopo Sochi nchini Urusi, ambapo alitumia fursa hiyo kuikaribisha kampuni ya Russian Railways kuwekeza nchini hususani katika sekta ya ujenzi, ufundi na mafunzo ikishirikiana na makampuni ya Watanzania.

Waziri Mkuu yuko nchini Urusi kuhudhuria mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa ya Afrika na Urusi (Russia-Africa Summit), unaotarajiwa kuanza leo Oktoba 23 hadi 24, 2019 katika jiji la Sochi. Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli.

“Katika kipindi hiki ambacho Tanzania inajenga reli ya kiwango cha kimataifa ya SGR pamoja na kufufua reli ya Kaskazini, inaikaribisha Kampuni ya Russian Railways kwa mikono miwili ije ifanye mazungumzo rasmi na Wizara husika. Pia Serikali inao mkakati wa kujenga reli mpya katika ukanda wa Kusini kutoka Mtwara hadi Ruvuma ili kuiunganisha bandari ya Mtwara na mikoa ya Kusini pamoja na nchi jirani za Malawi na Zambia.”

Alisema Tanzania kwa sasa inahitaji sana kuimarisha usafiri wa ndani wa reli hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Tanga hivyo endapo mazungumzo kati ya Wizara husika na kampuni hiyo yataonekana kuwa na tija na yana maslahi kwa Watanzania, kampuniyo itapewa fursa ya kuwekeza nchini.

Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wafanyabiashara wa Tanzania, wito wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuwataka watumie fursa lukuki zilizopo nchini kuanzisha makapuni ya pamoja na makampuni ya nje ili kuunganisha nguvu kwa kuendesha kwa pamoja makampuni yatakayoanzishwa.

Alisema utaratibu wa makampuni ya Tanzania kuanzisha makampuni ya pamoja na makampuni ya nje utawapa Watanzania fursa ya kujipatia kipato pia wataweza kulinda maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Kapuni ya Russia Railways, Bw. Misharin alimuhakikishia Waziri Mkuu kuwa kampuni yake iko tayari kushirikiana na wafanyabiashara wa Kitanzania katika kuanzisha makapuni ya pamoja ili kuipatia Tanzania tekinolojia ya masuala ya reli na kubadilisha ujuzi.

Awali, Waziri Mkuu alizungumza na Wakurugenzi wa Kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP, Bw. Alexsey Punkov na Bw. Ignat Dydyshkoa ambaye alisema  kuwa kampuni yake  inakusudia kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya kilimo kwa kuleta nchini mashine mbalimbali  kama vile matrekta na mitambo ya ujenzi wa barabara.

Viongozi wote  wa makampuni ya Urusi waliozungumza na Waziri Mkuu waliahidi  kuja Tanzania mwaka huu ili kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji na kufanya mazungumzo yenye lengo la kushirikiana na wafanyabiashara wa Kitanzania katika uwekezaji wao wanaokusudia kuufanya nchini.

Mheshimiwa Majaliwa pia alizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Zarubezhnefe, Bw. Sergey Kundryashov ambaye pia alionyesha nia ya kutaka kuwekeza nchini Tanzania.

Katika safari hiyo Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Mumwi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), James Matarajio.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Wauzaji wa Mbao Mafinga Iringa, Tanzania | Mzigo Unatumwa Popote Ulipo

TRA: Atakayefichua Wakwepa Kodi Atalipwa Asilimia 3 Ya Kodi Itakayokombolewa

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Diana Masalla amesema kuwa, mwananchi yeyote atakayefichua wakwepa kodi na TRA ikafuatilia na hatimaye kodi hiyo ikagundulika ni kweli ilikuwa imekwepwa na ikakusanywa, mwananchi aliyetoa taarifa hizo za ukwepaji kodi atalipwa asimilia 3 ya kodi iliyokusanywa lakini haitazidi shilingi milioni 20.
 
Masalla ameyasema hayo wakati wa Jukwaa la Biashara na Uchumi lililofanyika katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu ambalo lengo lake ni kujadili fursa, changamoto na kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji wilayani humo na kuzitafutia ufumbuzi.
 
“Natoa wito kwa wananchi na washiriki wa jukwaa hili kuhakikisha mnawafichua wakwepa kodi wote kwa sababu watu hao wanaiibia Serikali yetu mapato na wanarudisha nyumba jitihada za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi wake,” Amesema Masalla.
 
Aidha, Masalla amewahimiza wafanyabiashara na wawekezaji walioshiriki jukwaa hilo kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa pindi wanapokuwa wamefunga biashara kutokana na sababu mbalimbali ili kuepuka kuendelea kutozwa kodi au kuonekana wamekaidi kulipa kodi.
 
“Ni muhimu kutoa taarifa TRA pale ambapo mfanyabiashara amefunga biashara yake lakini pale anapofungua ni muhimu pia kuitaarifu TRA ili kuepuka kuendelea kutozwa kodi unapofunga biashara na pia kuanza kutozwa kodi sahihi pale unapofungua biashara,” amesisitiza Masalla.
 
Naye, Mwenyekiti wa wafanyabiashara Wilaya ya Busega David Mateko amempongeza Meneja wa TRA Mkoa wa Simuyu kwa kutoa elimu ya kodi kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara mkoani humo pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa kuwahamasisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari na hatimaye kuifanya Wilaya ya Busega kuwa wilaya ya pili kati ya wilaya 5 za mkoani Simiyu kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali yanayosimamiwa na TRA.
 
“Nampongeza Meneja wa TRA katika Mkoa wetu wa Simiyu kwa kuwatembelea wafanyabiashara na kuwapatia elimu ya kodi na pia nachukua fursa hii kumpongeza Mkuu wetu wa Wilaya Mheshimiwa Tano Mwera kwa kutuhamasisha kulipa kodi kwa wakati na sasa wilaya yetu imekuwa ya pili hapa mkoani kwa ukusanyaji Mapato yanayosimamiwa na TRA,” alibainisha Mateko.
 
Jukwaa hili la biashara na uchumi wilayani Busega limewakutanisha wafanyabiashara na wawekazaji zaidi ya 200 ambapo taasisi mbalimbali za Serikali zimealikwa kutoa mada ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Mwisho.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images