Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Muuguzi anayedaiwa kumbaka binti aliyekuwa akimuuguza mama yake asimamishwa kazi

$
0
0
Baraza la Ukunga na Uuguzi Tanzania (TNMC) limeisimamisha kwa miezi mitatu leseni ya Muuguzi aliyemchoma sindano ya usingizi na kisha kumbaka kuanzia saa nne usiku hadi saa nane msichana mwenye umri wa miaka 16

Damian Mgaya(41) aliyetoroka anadaiwa kumfanyia hivyo msichana huyo aliyekuwa akimuuguza mama yake katika hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora

Inaelezwa kuwa mara baada ya kumaliza kumbaka binti huyo aliamua kumtupa eneo la kufulia nguo kwenye nyasi akiwa hajitambui na kummwagia maji mwili mzima

Inaelezwa kuwa mnamo mwaka 2017, Damiani akiwa katika kituo cha Afya cha Igurubi, aliwahi kufanya tukio kama hilo, ambapo alipelekwa Polisi na kisha Mahakamani na aliachiwa huru na kurejeshwa kazini mwaka 2018

Taarifa hiyo imetolewa na Msajili wa Baraza hilo, Agnes Mtawa na kusema kuwa baada ya mtumishi huyo kurejeshwa kazini, alihamishwa kutoka kituo cha Afya cha Igurubi na kupelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Igunga

Kufuatia mtiririko wa matukio hayo, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, (TNMC) limeamua kumchukulia hatua ya kusimamisha leseni yake ya kutoa huduma za ukunga na uuguzi popote nchini Tanzania kwa muda wa miezi mitatu

TMA yatoa angalizo la Mvua Kubwa Kanda ya Ziwa, Tanga na Kigoma

$
0
0
Mvua kubwa inatarajiwa kunyesha kwenye baadhi ya maeneo ya Kagera, Geita, Mwanza, Kigoma, Tanga, visiwa vya Unguja na Pemba.

Hayo yalibainika Dar es Salaam jana Oktoba 18,2019 baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kutoa utabiri wa kifurushi cha siku tano.

Utabiri huo umetoa angalizo la mvua kubwa kwenye mikoa hiyo kwa siku mbili kuanzia Oktoba 19 hadi 20 mwaka huu na kubainisha kuwepo kwa kiwango cha joto chini ya nyuzi joto 11 mkoani Njombe na nyuzi joto 15 mkoani Mbeya.

TMA pia imeeleza kwamba Mkoa wa Tabora unatabiriwa kuwa na kiwango cha juu zaidi cha joto cha nyuzi joto 33.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, athari zinazoweza kukitoleza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Aidha imewataka wananchi na mamlaka za kiserikali kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kutokea.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Ahojiwa TAKUKURU Kwa Ubadhirifu wa Milioni 300

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - Takukuru Mkoa wa Tanga inamhoji aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Kazimbaya Makwega kwa tuhuma za ubadhirifu wa Shilingi 300 milioni za upimaji wa viwanja katika shamba la Mnazi wilayani Lushoto.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Christopher Mariba jana alisema Makwega alihamishiwa Halmashauri ya Wilaya Mbozi kabla kutenguliwa na Rais John Magufuli.

Alisema zipo fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya upimaji wa viwanja na mkataba ulikuwa wa Sh300 milioni ambapo mtuhumiwa kwa kutumia nafasi yake anatuhumiwa kubadilisha baadhi ya vipengele.

Alivitaja vipengele vinavyodaiwa kubadilishwa mkurugenzi huyo ni vile vilivyoitaka Kampuni ya Geoplan (EA) ya jijini Dar es Salaam kuweka kiasi cha gharama kwa ajili ya tahadhari ikiwa itachelewa kukamilisha kazi ile gharama itakatwa.

Kamanda huyo wa Takukuru alisema mkataba huo wa upimaji ulitakiwa uanze Juni  28 mwaka 2013 hadi Agosti 28, 2018 kitu ambacho hakikufanyika hadi Desemba 3, 2018 ambapo muda ulikuwa  kinyume na taratibu za mkataba na hata fedha za dharura zilizotakiwa kukatwa kama kipengele cha 44 kinavyoonyesha hazikukatwa.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mbeya Lakamata Silaha Mbili Aina Ya Short Gun.

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekamata silaha mbili aina ya Short Gun zikiwa na risasi mbili ambazo zilikuwa kwenye mtutu wa kila silaha ambazo zilikuwa zimefichwa kwenye mfuko wa plastiki.

Kufuatia msako mkali uliofanyika Oktoba 17, 2019 saa 17:00 jioni huko maeneo ya Pambogo, mtaa wa Isengo, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jiji la Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilikamata silaha hizo ambazo zimetengenezwa kienyeji na baada ya kuzikagua zilibainika kutokuwa na namba za usajili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ametoa  rai kwa wananchi kutoa taarifa za mtu/watu au kikundi cha watu ambacho wanakitilia mashaka katika maeneo yao ili ufuatiliaji ufanyike. 

Aidha ametoa rai kwa mtu yeyote anayemiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha silaha hiyo mara moja kituo cha Polisi

Waziri Mkuu: Viwanda 4,000 vimejengwa chini ya Serikali ya awamu ya tano | Sasa Vinachangia Pato la Taifa kwa asilimia 8.05 na kutoa ajira 306,180

$
0
0
Waziri  Mkuu  Kassim Majaliwa amesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa na hivyo kufanya sekta hiyo kuchangia Pato la Taifa kwa asilimia 8.05 na kutoa ajira 306,180 mwaka 2018.

Akizungumza kwa niaba ya Rais John Magufuli jana Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa tuzo za Rais kwa wazalishaji bora wa viwandani (PMAYA)  mwaka  2018 alisema  kutokana na sekta hiyo kuwa na mchango mkubwa, Serikali itavipa kipaumbele viwanda vinavyotumia malighafi za ndani zaidi.

Tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) ilishirikisha makampuni 61 ambapo mshindi wa jumla ilikuwa ni kampuni ya Hanspaul iliyoko mkoani Arusha.

“Sekta ya viwanda imeendelea kuongeza pato la taifa na mwaka 2018 imeongezeka kwa asilimia 8.05  tofauti na mwaka  2017ambayo ilikuwa asilimia 7.67, Aidha, katika kipindi cha mwaka 2018 Sekta ya viwanda ilichangia asilimia 18.1 ya mauzo yote ya nje, ikilinganishwa na asilimia 15 mwaka 2017 pia, takwimu zinaonyesha kwamba katika mwaka 2018 Sekta ya viwanda imetoa ajira rasmi 306,180 ikilinganishwa na ajira 280,899 mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 9.

“Mkakati wetu wa kuendeleza viwanda nchini kipaumbele kimewekwa katika viwanda ambavyo vinatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini, tunahitaji kupunguza uuzaji wa mazao yetu ya kilimo, misitu, madini na maliasili nje ya nchi yetu yakiwa ghafi, hali kadhalika tunalenga kutumia rasilimali zilizopo nchini kuzalisha  bidhaa ambazo  hivi sasa tunaziagiza kutoka nje.

“Shabaha yetu ni kutosheleza mahitaji ya ndani ya bidhaa za viwandani, na kuwa na ziada tutakayouza nje  ya nchi ili kupata fedha za kigeni, kukuza ajira na kuongeza kipato cha Watanzania kwa ujumla,yote haya yatawezekana kama tutatengeneza miundombinu kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa bora,”alisema Majaliwa.

Alisema ili kufikia lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati inayoongozwa na uchumi wa viwanda Serikali haina budi kuhahakikisha ukuaji wa uchumi unafikia asilimia 12 kwa mwaka.

Muhas Wametangaza Nafasi Mpya Za Udhamini Wa Masomo (Scholarships) Kwa Vijana Wa Kitanzania.

$
0
0
Habari Njema | Muhimbili University of Health and Allied Sciences(MUHAS) Wametangaza Nafasi Mpya Za Udhamini Wa Masomo (Scholarships) Kwa Vijana Wa Kitanzania..
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

👉Uwe na GPA Ya 3.5 na kuendelea
👉Ambatanisha CV yako,Vyeti vyako vya Elimu wakati wa kutuma maombi
👉Mwisho wa Kutuma Maombi : 30th October, 2019.
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  

 Bonyeza Hapo Chini Kujua Zaidi
👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/scholarship/

Mifuko Ya Uwezeshaji Kiuchumi Yatakiwa Kuwawezesha Wananchi Mitaji Waanzishe Viwanda

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga ametoa wito kwa Mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kuangalia jinsi ya kuwezesha wananchi wengi zaidi kupata mitaji ya kuanzisha viwanda, ili uchumi wa nchi ukue na kupunguza changamoto zinazokabili jamii.

Kiswaga ameyasema wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika uzinduzi wa Maonesho ya tatu ya  mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

“Sote tunafahamu kwamba Tanzania inalenga kufikia uchumi wa katika ifikapo mwaka 2025 na viwanda ni nyenzo itakayowezesha nchi kufika huko; viwanda vina mchango mkubwa sana katika kukuza uchumi wa nchi  kwa kuwa vinanufaisha jamii kwa kutoa ajira, kulipa kodi, kununua malighafi kutoka kwa wakulima na mengine mengi,” alisema Kiswaga.

Aidha, Kiswaga alitoa wito kwa wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa na maeneo mbalimbali nchini kufika katika maonesho haya kupata maelezo kutoka kwa wawakilishi wa mifuko /programu za uwezeshaji za Serikali, kuonesha bidhaa, kunua bidhaa za wajasiriamali na kupata uelewa wa masuala ya uwezeshaji wananchi.

Naye Afisa Maendeleo ya Biashara wa Taasisi ya kusaidia sekta binafsi na Kilimo,  (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo amesema wameandaa mpango mkakati wa miaka mitano ambapo wanatarajia kutoa ajira 700,000 ambao unatarajia kuzifikia familia zaidi ya 200,000.

Kaimu Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Bi.Esther Mmbaga kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), amesema malengo ya maonesho haya ni pamoja na kukuza uelewa wa wananchi  kuhusu uwepo, majukumu na vigezo katika kutoa huduma za mikopo na programu za uwezeshaji.

Bi. Mmbaga ameongeza kuwa malengo mengine ni kuhamasisha wananchi ili waweze kunufaika na fursa zilizopo katika mifuko na programu za uwezeshaji na kuhamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza katika miradi yenye tija.

Maonesho ya tatu ya  mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, yenye Kauli Mbiu “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Uchumi wa Viwanda”ambayo yanaendelea katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi yanatarajiwa kufungwa rasmi Oktoba 20, 2019 .

MWISHO

Nafasi 61 za Kazi Shirika la Hifadhi ya Taifa TANAPA | Elimu ni Kuanzia Cheti/Diploma/Degree | Mwisho Tarehe 30 Mwezi Huu

$
0
0
 Nafasi 61  za Kazi TANAPA
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Shirika la Hifadhi ya Taifa (Tanapa) limetangaza Nafasi 61 za kazi kwa Watanzania.

==>Elimu ni kuanzia Cheti, Dilpoma au Degree.

==>Nafasi Zilizotangazwa ni kama ifuatavyo;
👉 Conservation Assistant I
I - Accounts (Nafasi 2)
👉 Conservation Assistant II - Procurement (Nafasi 6)
👉 Conservation Assistant II -  Records Management (Nafasi 1)
👉 Conservation Assistant II - Wildlife Management - Ecology (Nafasi 1) 
👉 Conservation Officer II - Accountant (Nafasi 3) 
👉 Conservation Officer II - Accounts (Nafasi 14)  
👉Conservation Officer II - Corporate Communication (Nafasi 2)   
👉 Conservation Officer II -Geographical Information Systems (Nafasi 1) 
👉 Conservation Officer II - Human Resource And Administration (Nafasi 1)      
👉 Conservation Officer II - Procurement And Supplies (Nafasi 9) 
👉 Conservation Officer II - Wildlife Management - Law Enforcement (Nafasi 3)
👉 Conservation Officer II - Wildlife Management - Tourism (Nafasi 1) 
👉 Conservation Ranger III - Accounts (Nafasi 5)  
👉 Conservation Ranger III - Artisan (Nafasi 3)  
👉 Conservation Ranger III - Records Management (Nafasi 1)  
👉 Conservation Ranger III - Supplies (Nafasi 5)   
👉 Conservation Ranger III - Wildlife Management - Tourism (Nafasi 3)    
 ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
 
 ==>>Pia zipo nafasi mbalimbali za kazi kama vile; Afisa Mtendaji (Simiyu), Walimu, UBER TANZANIA,  AIRTEL, JUMIA, NOKIA TANZANIA,UMOJA WA MATAIFA

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Bonyeza hapo chini kujua zaidi

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/jobs

Serikali Yatoa Ufafanuzi Madai Ya Komputa Kuibiwa Ofisi ya DPP

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amekanusha kuwa hakuna kompyuta za Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) zilizoibiwa kama ilivyoripotiwa, bali vimeibiwa vipande viwili vya kompyuta za Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Dk. Mahiga amesema nyaraka zote zilizoko kwenye Ofisi ya DPP, Biswalo Mganga,  na taarifa muhimu za wahujumu uchumi hazijaguswa, ziko salama.

"Vyombo vya habari mmetoa taarifa, kwa mfano gazeti la leo limesema, nyaraka muhimu zinazohusiana na watuhumiwa walioko mahakamani zimeibiwa na zimesababisha kesi hizo kuathiriwa," amesema bila kutaja gazeti hilo

"Ukweli ni kwamba, ofisi ambayo ilivunjwa na baadhi za kompyuta, si zote bali ni vipande tu. Ofisi ya Mkurugenzi mkuu wa mashitaka ya serikali haikuguswa, nyaraka zote zipo, taarifa zote zipo na kazi yake inaendelea," amesema Waziri Mahiga

Ameendelea kusema sasa Jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza uhalifu huo.

Serikali Yasaini Mkataba wa Ununuzi wa Ndege Mpya ya Bombardier Q400

$
0
0
Serikali ya Tanzania imesaini mkataba na kampuni ya kutengeneza ndege kutoka Canada kwa ajili ya ununuzi wa ndege mpya aina ya Bombardier Q400, inayotarajiwa kufika nchini June 2020, yenye uwezo wa kubeba abiria 78.
 
Mkataba huo umesainiwa leo Jumamosi Oktoba 19, 2019 lengo likiwa ni kuimarisha na kuboresha utoaji huduma za usafiri wa anga nchini kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Mtendaji mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali, Dk Benjamin Ndimila amesema ndege hiyo itakua na uwezo wa kutua hata kwenye viwanja vya vumbi.

Uteuzi Mpya Uliofanywa na Rais Magufuli Jioni Hii

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili October 20

Waziri Mkuu Ataka Mikoa Iliyobakia Itekeleze Agizo Lake Kuhusu Uwekezaji

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka mikoa ambayo bado haijatekeleza agizo lake la kuandaa makongamano ya uwekezaji ihakikishe inafanya hivyo mara moja.

Ametoa agizo hilo jana mchana (Jumamosi, Oktoba 19, 2019) wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji kwa mkoa wa Pwani katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

“Nitumie fursa hii kuwapongeza viongozi wa mkoa wa Pwani kwa kutekeleza agizo nililolitoa Juni 18, 2018 wakati wa kongamano la tatu la uwezeshaji wananchi kiuchumi la kuhakikisha mikoa yote inaandaa kongamano la uwekezaji na inakuwa na mwongozo wa uwekezaji wa mkoa. Mikoa ambayo haijatekeleza agizo hilo, ifanye hivyo mara moja,” amesema.

Waziri Mkuu amesema mkoa huo umeweza kubaini fursa zilizopo katika mkoa wa Pwani na kuzitangaza kupitia mwongozo wa uwekezaji ambao pia ameuzindua leo.

Amesema kaulimbiu ya kongamano hilo isemayo: ‘‘Ijenge Tanzania, wekeza Pwani mahali sahihi kwa uwekezaji (Build Tanzania, Invest in Pwani, the Best Place for Investment)” ina maana kuwa, licha ya mkoa wa Pwani kubainisha na kutangaza fursa za uwekezaji na biashara zilizopo, unajipambanua vizuri na kuonyesha kuwa ni kwa namna gani umejiandaa na umetengeneza mazingira bora yanayovutia wawekezaji wa ndani na nje.

“Ili kudhihirisha dhamira ya dhati ya kukuza uchumi kupitia viwanda, nimeelezwa kuwa mkoa umetenga hekta 53,016 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ambavyo vitatumia rasilmali zilizopo ndani ya mkoa na maeneo mengine ya nchi kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wanachi,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wahakikishe wanasimamia miundombinu inayoelekea kwenye viwanda vilivyopo kwenye maeneo yao.

"Kila mmoja ahakikishe maji, umeme na barabara vinafika kila eneo ambalo mwekezaji anataka kujenga kiwanda. Nitumie fursa hii kuwaomba mlete mabadiliko chanya yanayotokana na maboresho yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano."

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Bibi Angella Kairuki alisema kwamba Serikali imeanza kutekeleza mapendekezo ya mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (Blueprint for Improving Business Environment Regulatory Licensing in Tanzania) kwa kuondoa tozo 163 zilizokuwa zikilalamikiwa na wawekezaji.

“Pia tumetenganisha majukumu ya TBS ya TFDA ambayo sasa ni TMDA. TBS itashughulika na vyakula na TMDA itashughulika na dawa na vifaatiba. Vilevile, tumeondoa ada za usajili sehemu za kazi ambazo zamani ilikuwa ni sh. 28,000 na sasa hivi zinatolewa bure,” alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikillo aliwataka watu wote wanaotaka kuwekeza nchini waufikirie kwanza mkoa wa Pwani kwa sasabu uko kimkakati na una fursa nyingi ikiwemo hali nzuri ya usalama na kwa maana hiyo mitaji yao italindwa.

“Mkoa wetu uko kwenye eneo la kimkakati la kuwezesha biashara kwa kuwa uko karibu na bandari ya Dar es Salaam na uwanja wa ndege; uko karibu na soko kubwa ambalo ni Dar es Salaam; unapitiwa na reli zote kwenda mikoani na nchi jirani; unapitiwa na barabara kuu itokayo Dar es Salaam na pia una bandari kavu ya Kwala.”

Mbali ya hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa alisema faida nyingine ambayo mkoa huo unayo ni uwepo wa miundombinu ya maji, umeme na nishati ya gesi asilia ambayo imeanza kutumiwa na baadhi ya viwanda kama Goodwill na Lodhia Steel.

Naye Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi ya Kijamii (ESRF) ambayo ilisimamia uandaaji wa mwongozo wa uwekezaji kwa mkoa wa Pwani, alisema taasisi yao inasaidia kuandaa na kuchambua fursa zilizopo kwenye mikoa mbalimbali. “Hadi sasa tumekwishaisadia mikoa 17 kuandaa miongozo ya uwekezaji na kwa sasa mikoa 12 imeshakamilisha na mikoa mitano iko kwenye hatua mbalimbali,” alisema.

Akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela ambao ni wadhamini wakuu, Afisa Mkuu wa Biashara, Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts alisema benki hiyo imeendelea kugusa sekta zote za uchumi na hivyo kuongeza tija kwenye mnyororo mzima wa uzalishaji.

Alisema huduma zao zimelenga kuongeza tija na ufanisi katika sekta ya viwanda nchini ikiwemo utoaji wa mikopo ya biashara kwa ajili ya kuongeza mikopo ya uendeshaji (working capita loans) na mikopo ya uwekezaji (investment loans).

“Benki yetu inatoa mikopo ya biashara na uwekezaji katika maeneo mbalimbali ambapo mikopo ya kilimo ni shilingi bilioni 357, uzalishaji wa viwanda (shilingi bilioni 214), biashara (shilingi bilioni 347), mahoteli (shilingi bilioni 87) na sekta ya madini (shilingi bilioni 91),” alisema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Dkt. Mwakyembe Aipongeza Taifa Stars

Makamu Wa Rais Kufungua Mkutano Wa mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO)

$
0
0
Eric Msuya – MAELEZO
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan anatalajia kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa 58 wa mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) utako anza  Jumatatu tarehe 21 hadi 25 Oktoba jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amesema Mkutano huo utaudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Nchi 48 za Wanachama wa Shirika hilo pamoja na Masharika mbalimbali ya Kitaifa. 

“Mkutano huu utakaoanza Jumatatu unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali toka Nchi Wanachama, Wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa, Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao hapa Nchini na Viongozi Waandamizi wa Serikali kutoka Nchi Wanachama” Amesema Mhe. Mahiga 

Mkutano huo utaofanyika kwa siku tano, utajadili masuala mbalimbali ya kisheria za Kimataifa ikiwa pamoja na Changamoto za kisheria zinazoyakabili Mataifa Wanachama na Kuangalia namna bora ya kushughulikia changamoto hizo ili kuwa na Dunia yenye Amani, Usalama na Utulivu kwa ajili ya Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii. 

Sambamba na hilo maswala mengi yatako jadiliwa katika mkutano huo ni, Sheria ya Kimataifa ya Bahari, Mitandao na Biashara na Uwekezaji, Kuvunjwa kwa Sheria ya Kimataifa Nchini Palestina, Utatuzi wa Migogoro kwa njia ya Amani, Matumizi ya Sheria za Nchi nje ya Nchi na Tume ya Sheria ya Kimataifa. 

Tanzania ilijiunga na The Asian – African Legal Consultative Organisation (AALCO) mwaka 1973 chini ya Uongozi wa Rais Hayati Baba wa Taifa  Mwl. Julius Kambarage Nyerere, huku Tanzania ikiwa ni mara yake ya tatu kuwa wenyeji wa kushiriki katika mkutano huu wa Shirika la Mashauriano ya kisheria kwa nchi za Asia na Afrika 

“Kwa mara nyingine tena, Tanzania tunakuwa wenyeji kwa mara ya tatu katika mkutano huu … Nchi yetu ina miaka 46 toka tujiunge na chama hichi, mafaniko ni mengi na maslahi ni makubwa na mapana tunayoendelea kuyapata katika chama hiki” Amesema Mhe. Mahiga 

Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika ( The Asian-African Legal Consultative Organisation – AALCO kilianzishwa  mwaka 1956 ikiwa ni matokeo ya Mkutano wa Kihistoria wa Bangung, Indonesia tarehe 18-24 April 1995 (Bandung Conference).

Tanesco Yakusanya Bilioni 46 Kwa Wiki

$
0
0
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa sasa linakusanya shilingi bilioni 46 kwa wiki hali inayofanya Shirika hilo kuendelea kujitegemea baada ya kuacha kupokea ruzuku kutoka serikalini ili kujiendesha.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani tarehe 18 Oktoba, 2019 wakati wa kikao chake na wafanyakazi wa TANESCO wa Kanda ya kaskazini kilichofanyika jijini Tanga na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Nishati, Raphael Nombo na viongozi kutoka TANESCO Makao Makuu.

” Niwapongeze TANESCO kwa kuendelea kujiendesha kwani hampokei tena ruzuku kutoka Serikalini na sasa mnakusanya shilingi Bilioni 46 kwa wiki tofauti na miaka miaka miwili iliyopita mlipokuwa mkikusanya bilioni Sita hadi Tisa kwa wiki, mnao uwezo, endeleeni.”alisema Dkt Kalemani

Kuhusu mkakati wa kuongeza mapato ya Shirika alisema kuwa, kunzia mwaka huu wa fedha, Kila Ofisi ya Mkoa ya TANESCO itapewa malengo ya makusanyo na atakayefikia malengo hayo atapewa motisha, ila atakayeshindwa atachukuliwa hatua.

Kuhusu ongezeko la wateja waliounganishwa na umeme, Dkt Kalemani ameliagiza Shirika hilo kufanya kazi kama makampuni ya simu kwa kufuata wateja kule waliko ili idadi ya wateja hao iongezeke na hivyo mapato ya Shirika kuongezeka.

Katika hatua nyingine, Dkt Kalemani alisema kuwa, kuanzia sasa miradi yote ya TANESCO inayotekelezwa kwa fedha za ndani itasimamiwa na wataalam wa ndani ya nchi ukiwemo mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (MW 2115).

” Niwapongeze TANESCO kwa kusimamia mradi huu mkubwa wa Julius Nyerere, zamani tulikuwa tukisimamiwa lakini sasa tunawasimamia wakandarasi na hii inaokoa fedha za Serikali ambazo zingetumika kutafuta wasimamizi wa miradi kutoka nje ya nchi kuja kusimamia miradi yetu.” alisema Waziri wa Nishati

Kuhusu suala la umeme vijijini, Dkt. Kalemani alisema kuwa bei ya umeme vijijini ni shilingi 27,000 bila kujali umbali aliopo mteja hivyo kila mtumishi ahakikishe hilo linatekelezeka.

Aidha, aliagiza wataalam wa TANESCO kuacha mara moja lugha  lugha ya “hakuna vifaa” ambayo mara kadhaa imekuwa ikitumika wakati wateja wanapotaka kuunganishiwa umeme na kueleza kuwa vifaa vya umeme kama vile nguzo, mita, transfoma na nyaya vinazalishwa ndani ya nchi na kupatikana kwa urahisi hivyo lugha za visingizio zisiwepo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Raphael Nombo alizungumza na wafanyakazi hao kuhusu masuala ya muundo wa TANESCO, mikataba  ya wafanyakazi na suala la mishahara.

TANESCO, Kanda ya Kaskazini inajumuisha mikoa minne ambayo ni Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara.

Naibu Waziri Wa Maliasili Na Utalii, Mhe.kanyasu Awataka Wazazi Watimize Wajibu Wao

$
0
0
Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewakumbusha Wazazi wenye watoto waliowapeleka kusoma katika shule binafsi wahakikishe wanawatimizia mahitaji yao ya muhimu katika kipindi chao chote cha masomo ili waweze kufaulu mitihani yao ya mwisho.

 Badala ya kuja na  zawadi nyingi siku ya mahafali ajili ya kuwapongeza wanapohitimu  ilhali wanafunzi hao walikuwa wakirudishwa nyumbani kila wakati wakachukue ada ya shule.

Ametoa kauli hiyo jana wakati wa mahafali ya kidato cha nne kwa wanafunzi  60 yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Rocks Hill iliyopo katika wilaya ya Ilemela  jijini Mwanza.

Amesema wazazi lazima wawekeze kwa watoto wao ili waweze kusoma katika mazingira ya kutokuwa na hofu ya kurudishwa nyumbani kwa sababu wazazi wao  hawajawalipia ada ya shule.

"Ukiamua kumsomesha mtoto lazima ukubali kwamba elimu haijawahi kuwa bure, hivyo ni jukumu la kila   mzazi kukidhi mahitaji ya mwanae likiwemo suala la  kumlipia ada kwa wakati." alisisitiza Kanyasu

Amesema ni vyema wazazi hao kutambua dhamana waliyonayo katika kuwandaa watoto wao kielimu badala ya kusubili hadi watoto  warudishwe nyumbani.

Mhe.Kanyasu amesema kitendo hicho cha wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa ajili ya ada kimekuwa kikiwarudisha nyuma kimasomo kwa vile wamekuwa wakikosa baadhi ya vipindi.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka wazazi kuendelea kuwalea watoto wao katika maadili mema ili wasiweze kuharibikiwaa mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Kwa upande wake Meneja wa Shule hiyo, Meshak Mpalanga amesema katika kipindi chao chote cha masomo wamelelewa kimaadili hali itakayowasaidia kupambana zaidi katika kuyamudu maisha

Akizungumzia jinsi walivyoandaliwa kwa ajili ya mtihani wao wa mwisho, Amesema anatarajia idadi kubwa ya wanafunzi watafaulu na kujiunga na kidato cha tano.

NayevMwanafunzi bora katika masomo yote aliyetajwa katika mahafali hayo, Diana Titus amesema wamejianda vyema na wapo tayari kwa ajili ya mtihani wao wa mwisho.

" Tunawashuru walimu wote kwa kutulea na kutufundisha, tunaamini sote tutafanya vizuri mitihani yetu.alisisitiza Mwanafunzi huyo

Live: Rais Magufuli Akiwaapisha Viongozi Aliowateua

$
0
0
Live: Rais Magufuli Akiwaapisha Viongozi Aliowateua

Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Magufuli Urusi

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumapili, Oktoba 20, 2019) kwenda Urusi kuhudhuria mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi (Russia-Africa Summit), utakaofanyika jijini Sochi, Urusi, Oktoba 23 – 24, 2019.

Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.

Mkutano huo utakaoendeshwa chini ya uenyekiti wa pamoja (Co-chaired) wa Rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin, na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), unalenga kurejesha na kuimarisha uhusiano baina ya mataifa ya Afrika na Urusi ambao uliyumba baada ya kusambaratika kwa “Union of Soviet Socialist Republic” (USSR) mwaka 1991.

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali utafanyika katika sehemu mbili, ambazo ni Kongamano la Biashara (Russia Business Forum) linalotarajiwa kufanyika Oktoba 23, na Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Urusi na Afrika uliopangwa kufanyika Oktoba 24, 2019.

Waziri Mkuu atashiriki kwenye mikutano yote miwili.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

PICHA: Rais Magufuli Awaapisha Viongozi Mbalimbali Ikulu Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Bazi Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerald Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshugulikia Elimu katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ali Sakila Bujiku kuwa Balozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali walioapishwa kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali walioapishwa kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakisaini Hati ya kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustine Mahiga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru wapili kutoka (kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli wa kwanza (kushoto), pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakwanza (kulia) mara baada ya uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa sambusa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images