Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Naibu Waziri Mabula Aagiza Wakala Huduma Za Misitu Kupima Shamba La Miti La Rubya Ukerewe

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM UKEREWE
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha inalipima na kupatiwa hati shamba lake la Miti la Rubya lenye ukubwa wa hekta 1,926.3 lililopo kijiji cha Bugula tarafa ya Ilangala kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana wakati alipokwenda kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakati akiwa katika ziara yake ya siku moja katika kisiwa cha Ukerewe kufuatilia utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika hamashauri za mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Alisema, kinachohitajika sasa kwa Wakala wa Huduma za Misitu ni kuhakikisha shamba hilo la Miti la Rubya linapimwa na kupatiwa hati itakayoonesha mipaka halisi ya shamba hilo ili kuepuka migogoro ya ardhi.

‘’Miji inakuwa kuwa na wananchi bado wanahitaji maeneo bila kuwa na hati inaoonesha mipaka ya shamba kunaweza kuleta migogoro na tuelewe hati inalinda mipaka ya shamba lisivamiwe   na wananchi’’ alisema Dokt Mabula

Pamoja na kuagiza kupimwa hilo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliagiza pia eneo la shamba kuwa Mpango Kina utakaonesha kila matumizi ya sehemu ya ardhi ya shamba hilo kwa kuwa katika eneo hilo mbali na shamba la misitu lakini kuna makazi ya watu.

Kwa upande wake Meneja wa Shamba la Miti la Rubya wilayani Ukerewe Festo Chaula alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba an Maendeleo ya Makazi kuwa, Shamba la Miti la Rubya ni miongoni mwa mashamba 23 yanayomilikwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania lililoanzishwa mwaka 1951 kwa Tangazo la Serikali Namba 230.

Alisema, pamoja na shamba hilo la Rubya pia Wakala inalo eneo lingine lilipandwa miti kwa ubia na halmashauri ya wilaya ya Ukerewe lenye ukubwa wa hekta 1,152 ambapo miti iliyopandwa eneo hilo ni ya Misindano.

Kwa mujibu wa Chaula, katika kuboresha makazi ya watumishi wa wakala wa Huduma za Misitu TFS katika mwaka huu wa fedha 2019/2020 TFS imetenga zaidi ya milioni 383.8 kwa ajii ya ujenzi wa nyumba tatu, tenki la kuhifadhia maji, ukarabati wa nyumba mbili na ujenzi wa uzio wa bustani ya miti ambapo ujenzi wa nyumba tatu ulianza Agosti mwaka huu.

Katika Hatua Nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka halmashauri ya wilaya ya Ukerewe kufanya zoezi la upimaji maeneo katika halmashauri hiyo kama operesheni maalum ili kuondoa migogoro ya ardhi sambamba na kuondoa ujenzi holela.

Akizungumza na Madiwani pamoja na Watumishi wa Sekta ya Ardhi katika halmashauri hiyo, Dkt Mabula alisema tayari halmashauri hiyo inavyo vifaa vya upimaji inachotakiwa kwa sasa katika kuharakisha zoezi hilo ni kuwasiliana na Ofisi ya Ardhi Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kupatiwa Wapimaji.

Hata hivyo, Dkt Mabula alishangazwa na halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kutokuwa na kijiji chenye mpango wa matumizi bora ya ardhi wakati asilimia kumi ya kisiwa hicho ni ardhi ya nchi kavu. Halmashauri kerewe ina jumla ya vijiji 73 ambapo Naibu Waziri aliwataka Madiwani wa Halmashauri ya Ukerewe kuhakikisha inapanga mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji vyake ili kuainisha matumizi mbalimbali ya vijiji hivyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe George Nyamaha alieleza kuwa halmashauri yake imekuwa na chanagmoto kubwa ya upungufu wa wataalamu wa sekta ya rdhi jambo alilolieleza kuwa linasababisha idara hiyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Kijana Aliyeishi kwa kupumulia mashine afariki dunia

$
0
0
Hamad Awadh, aliyeishi kwa kutegemea mashine ya kumsaidia kupumua amefariki dunia jana jioni Oktoba 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Mke wa Awadh aitwaye Catherine Kulekana amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema, hali ya mumewe ilianza kubadilika usiku wa kuamkia jana akawa chini ya uangalizi wa madaktari hospitalini hapo. Ilipofika asubuhi hali yake haikurejea kawaida na saa 10 jioni alifariki.

Juni 10, 2019 Mloganzila ilimpa msaada wa mashine hiyo ya kumsaidia kupumua yenye thamani ya Sh4 milioni kutokana na matatizo yake ya afya ambayo yalimlazimu kutumia mashine ya Oksjeni muda wote ili aweze kupumua. Awadh alifikishwa Mloganzila Julai 9, 2018 na kuruhusiwa Juni 9, 2019 baada ya afya yake kuimarika.

Licha ya kutakiwa kurejea hospitali kila baada ya muda alishindwa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwa na usafiri wa kutoka nyumbani kwake Kipawa hadi katika hospitali hiyo umbali wa zaidi ya kilomita 10.

Wadau na taasisi mbalimbali walijitokeza kumsaidia ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) lililomfungia umeme katika nyumba aliyokuwa akiishi na kumpatia Sh10 milioni za matibabu. Awadh aliomba msaada Tanesco kutokana na mashine ya kumsaidia kupumua kutumia umeme mwingi.
 
Pia, Hospitali ya Mloganzila ilitoa gari la wagonjwa kwa ajili ya kumpeleka Awadh katika hospitali hiyo kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake, mara ya mwisho hali yake ilibadilika na kulazwa hadi umauti ulipomkuta.

Urusi yafanya majaribio ya makombora ya kisasa ya nyuklia karibu na Marekani

$
0
0
Rais Vladimir Putin wa Russia ameshuhudia majarbio ya makombora matano ya kisasa ya nyuklia katika eneo la Bahari ya Arctic nchini humo ambalo linapakana na Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa, makombora hayo ya nyuklia yamefanyiwa majaribio katika mazoezi makubwa ya kijeshi ambayo yamefanyika katika eneo zima la Arctic kaskazini mwa nchi hiyo.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema makombora ya kuvuka mabara yaliyofanyiwa majaribio ni pamoja na RS-24, RSM-50 na Sineva.

Mazoezi ya kijeshi ya Russia yanayofanyika katika eneo la Arctic yanajumuisha wanajeshi 12,000, nyambizi tano za nyuklia, ndege 105 za kivita na magari 213 ya kurusha makombora.

Mazoezi hayo yaliyopewa jina ya Grom-19 au Radi 19 yalikamilika Alhamisi kwa mafanikio. 

Wakati akitazama mazoezi hayo kwa njia ya video akiwa mjini Moscow, Rais Putin, akiwa ameandamana na Waziri  wa Ulinzi Sergei Shoigu amesema majeshi ya Russia yalikuwa yanafanya mazoezi kuhusu vita vya nyuklia na vita vya kawaida. 

Mazoezi hayo yamekuja baada ya ya Rais Trump wa Marekani kutangaza kuwa meli za kivita za nchi yake zitaimarisha harakati katika Bahari ya Arctic.

Credit:Parstoday

Jinsi Ya Kuandika CV Nzuri Ambayo Itamvutia Mwajiri na Kukufanya Upate KAZI Kirahisi

$
0
0
WATU wengi nchini wamekosa ajira  kwa sababu ya makosa wanayoyafanya wakati wa kuandika CV zao.

Kumbuka,  makampuni  karibia yote yanayotangaza nafasi za kazi hupokea wastani wa maombi 200-500 ya kazi kwa tangazo moja la kazi. 

Hivyo, CV yako lazima ikae vizuri ili kumshawishi mwajiri. Utaratibu wa kuomba kazi unaweza ukawa tofauti kati ya makampuni na mashirika, ila yote yatahitaji uwatumie CV.

CV ni nini?
CV ni maelezo ya ujumla kwa kiundani ya historia yako ya kazi na shule. Kawaida, inatumika kwenye maombi ya kazi ya nafasi za kati, za juu na za utafiti.

Mambo yafuatayo yatasaidia kuifanya CV yako iwe bora na hivyo, kukusaidia kupata interview za kazi.

👉Soma na kuelewa maelezo ya kazi
Una ujuzi gani? Mwajiri anatafuta mfanyakazi wa aina gani? Maswali haya ni muhimu kujua kama utaiweza hiyo kazi au la. Pia, ni vizuri kujua nini hasa ni muhimu kwa muajiri na kufanya maombi yako yaendane zaidi na mahitaji ya mwajiri.

Kwa mfano, kama kazi inaweka umuhimu kwenye ujuzi wa kutumia mitandao ya kijamii kwa matangazo, hakikisha CV yako ina kazi zote zilizohitaji matumizi ya mitandao ya kijamii.

👉Andika maneno muhimu yaliyotumika kwenye maelezo ya kazi, uyatumie kwenye CV
Usichukue sentensi nzima kutoka kwenye maelezo ya kazi na ukaitumia vile vile kwenye CV yako. Ila, tumia lugha na baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye CV.

👉Fanya utafiti juu ya kampuni iliyotangaza kazi
Pamoja na kuchambua maelezo ya kazi, ni muhimu kufanya utafiti juu ya kampuni yenyewe. Kama wana tovuti au wapo kwenye mitandao ya kijamii, jaribu kujua ni kazi gani na sekta ipi wanayohusika nayo. 

Pia, ikiwezekana jaribu kuwajua wafanyakazi/meneja wa kampuni hiyo. Hii itakusaidia kujua maadili na muelekeo wa kampuni. Hii itakusaidia kuweka maombi yako ya kazi yaendane na kampuni hiyo.

👉Orodhesha ujuzi wako wakufanya kazi
Hapa, usiweke kazi zote ulizozifanya maishani mwako ila, weka zile ambazo zilikuongezea ujuzi utakayo kusaidia kufanya kazi unayoomba.

==>Format/Staili inayotumika zaidi kwenye kuandika CV:
   1. Lengo la CV na ujuzi wako
    2.Ujuzi wako wa kazi
   3. Mafanikio maalum
   4. Elimu
   5. Ujuzi muhimu binafsi

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Angalizo:
  1.  Tumia maandishi ya kawaida ya Times New Roman
  2.  Tumia size 9 – 12 ya herufi
  3.   Hakikisha unatumia staili moja ya kuandaa CV kote
  4.   CV isiwe zaidi ya ukursasa 2
  5.   Usitumie sentensi ndefu
  6.  Hakikisha CV yako inasomeka kiurahisi na inawasilisha   mafanikio yako kwa uwazi.
  7.  Anza na kazi yako ya sasa hivi au ya hivi karibuni alafu rudi nyuma.
   ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 
   ==>.Hakikisha Yafuatayo:
1.Ukiwa unaandika jina la kampuni uliyo fanya kazi, andika jina la kampuni kikamilifu. 
2.Eleza kwa ufupi kampuni yao inahusika na nini. 
3.Tatu, weka muda uliyofanyakazi hapo (mwezi na mwaka).  
4.Baada ya hapo, orodhesha kazi na majukumu yako kwenye hiyo kampuni.
5.Usidanganye

👉Maandalizi ya Mwisho

1.Pitia kila kitu kwa mara ya mwisho
 -Print CV yako alafu ipitie. Hii huwa inasaidia kuona makosa yako.

2.Mpe Rafiki  yako apitie CV
-Muombe rafiki yako apitie CV yako. Macho manne ni bora zaidi ya mawili!

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

Hatua ya kwanza kwenye kupata kazi unayotaka ni kutuma maombi. Tunatumaini kwamba maelezo yaliyoelezwa humu yatakusaidia kuandaa CV bora kwa ajili ya mwajiri.

👉Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya kuandika CV nzuri, anza kutafuta kazi unayoitaka kwa kubofya hapo chini.

AU 

Waziri Mkuu Aeleza Jinsi Ya Kufikia Nchi Ya Kipato Cha Kati

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ili Tanzania ifikie lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati inayoongozwa na uchumi wa viwanda, haina budi kuhakikisha kuwa inatimiza vigezo kadhaa, kikiwamo cha ukuaji wa uchumi kwa kiwango cha asilimia 12 kwa mwaka.

Amesema vigezo vingine ni mchango wa viwanda katika Pato la Taifa usiopungua asilimia 15; utoaji ajira rasmi na za moja kwa moja uongezeke na kufikia asilimia 40 ya ajira zote; na sekta ya viwanda iweze kuiingizia nchi mapato ya fedha za kigeni zaidi ya asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni.

Alitoa kauli hiyo jana usiku (Alhamisi Oktoba 17, 2019) wakati akizungumza na wageni na washiriki waliohudhuria hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa mwaka 2018 iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli alisema: “Ili kufikia vigezo hivyo na kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta ya viwanda, ni lazima tujizatiti na kuimarisha ushirikiano wa karibu baina ya sekta ya umma na sekta binafsi,” huku akiwasihi washiriki katika hafla hiyo waitumie fursa hiyo kutafakari mbinu mpya za kufikia vigezo hivyo muhimu vya kuijenga Tanzania mpya ya viwanda.

“Kila mmoja wetu anatambua umuhimu wa sekta ya viwanda katika kukuza uchumi wa nchi yoyote duniani. Viwanda ndivyo vimekuwa chimbuko la maendeleo ya haraka ya nchi mbalimbali duniani na mhimili mkuu wa kutegemewa katika kuondoa umasikini kwa kutoa ajira nyingi na za uhakika kwa wananchi. Maendeleo ya sayasi na teknolojia yanategemea sana sekta ya viwanda.”

“Takwimu pia, zinaonesha kwamba katika mwaka 2018, sekta ya viwanda imetoa ajira rasmi 306,180 ikilinganishwa na ajira 280,899 za mwaka 2017; sawa na ongezeko la asilimia tisa. Tutaendelea kuchukua hatua zinazostahiki ili kuwezesha sekta hii ikue kwa haraka na kutoa mchango mkubwa zaidi katika Pato la Taifa na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi na kuondoa umaskini wa wananchi wetu,” alisema Waziri Mkuu.

Aliema kutokana na jitihada kubwa zinazoendelea kufanywa na Serikali za kujenga uchumi wa viwanda, jumla ya viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa katika mikoa mbalimbali. “Viwanda vilivyojengwa vinazalisha bidhaa za ujenzi (saruji, nondo, vigae, mabomba, marumaru, n.k); pamoja na viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ikiwemo nafaka, matunda, mafuta ya kupikia na bidhaa za ngozi,” alisema.

Alisema viwanda vingi vimeanzishwa nchini na ni faraja kuona wawekezaji wa ndani nao wanaendelea kufungua viwanda vipya pamoja kuongeza uwekezaji wao. “Moja ya viwanda vinavyohamasishwa ni vile vinavyochochea uzalishaji wa ajira kwa wingi. Ujenzi wa viwanda vipya nchini, katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano, umechangia kupatikana kwa ajira mpya 482,601 nchi nzima,” alisema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wenye viwanda na washiriki wa hafla hiyo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Innocent Bashungwa alisema wizara yake kwa kushirikiana na sekta binafsi itaendelea kuondoa kero zinazokwamisha ufanisi na ukuaji wa sekta ya viwanda zikiwemo kero kubwa zinazolalamikiwa na sekta hiyo.

Alizitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni ucheleweshaji wa malipo ya madai ya kodi za ongezeko la thamani (VAT) na asilimia 15 ya ziada inayolipwa na waagizaji wa sukari ya viwandani; ushindani usio na uwiano na bidhaa za bei nafuu kutoka nje ya nchi kama vile nondo, mabomba ya plastiki, nguo na mavazi, bidhaa za ngozi na marumaru.

“Pia tutaangalia upya uwepo wa utitiri wa tozo na ada za juu zinazotozwa na taasisi mbalimbali za Serikali, ongezeko la kodi ya kuagiza mali ghafi kutoka nje ya nchini, na kucheleweshwa upatikanaji wa vibali vya kufanya kazi kwa wataalam wa kigeni wasiopatikana hapa nchini (expetriates employees),” alisema.

Kuhusu usajili wa makampuni, Waziri Bashungwa alisema Wizara hiyo kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imekamilisha kuweka mifumo ya kusajili majina ya biashara kwa njia ya mtandao. “Mifumo hiyo inawawezesha wafanyabiashara kusajili jina la biashara, uandikishwaji wa makampuni, usajili wa alama za biashara na usajili wa viwanda mahali popote walipo kupitia tovuti ya wakala (www.brela.go.tz).”

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Bw. Subhash Patel, alisema CTI inaunga mkono azma ya Rais Magufuli ya kuleta viwanda nchini. “Hakuna nchi itakuwa imefanikiwa duniani bila kuwekeza kwenye viwanda,” alisema.

Akielezea uwepo wa fursa za biashara kwa wawekezaji wa Kitanzania, Bw. Patel alisema Tanzania ina majirani ambao hawana bandari na hiyo ni fursa tosha ya kuwekeza na kuendeleza biashara kwenye nchi jirani.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Nafasi Mpya za Kazi SIMIYU (Halmashauri Ya Wilaya Bariadi.) | Mtendaji wa Kijiji Daraja la Tatu

$
0
0
Nafasi Mpya za Kazi SIMIYU (Halmashauri Ya Wilaya Bariadi.) | Mtendaji wa Kijiji Daraja la Tatu
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
👉Wanahitajita Watendaji Daraja la Tatu
👉  Elimu ni Kuanzia Kidato cha nne, sita na Cheti 
👉  Mwisho wa Kutuma Maombi : 30th October, 2019.
👉Mshahara ni TGS B/1

 ==>>Pia zipo nafasi mbalimbali za kazi UBER TANZANIA, VODACOM, AIRTEL, JUMIA, NOKIA TANZANIA,UMOJA WA MATAIFA

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Bonyeza hapo chini kujua zaidi

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/jobs

Wanafunzi 39 wa darasa la nne Geita Wanusurika Kufa kwa RADI

$
0
0
Wanafunzi 39 wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Ihumilo kata ya Nkome Wilayani Geita wamenusurika kufa kwa radi wakati wakiwa darasani baada ya kupoteza fahamu kisha  kukukimbizwa katika Hospital ya Wilaya Nzera na wengine Zahanati ya Nkome kwa matibabu.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Oktoba 18, 2019 na  mganga mkuu wa mkoa wa Geita,  Josephat Simeo inaeleza kuwa wanafunzi 24 wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Nzera na 15 wamepatiwa matibabu katika zahanati ya Nkome.

Dk Simeo amesema radi hiyo imesababisha watoto kupata mshtuko na kuzimia lakini baada ya kupatiwa huduma ya kwanza wanaendelea vizuri na tayari wanafunzi 36 wameruhusiwa kutoka hospitali.

Benki Ya Dunia Kuijaza Zanzibar Dola Za Marekani Milioni 150 Kukuza Utalii Na Ustawishaji Miji Zanzibar.

$
0
0
Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington DC
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajia kupata dola za Marekani Milioni 150 kutoka Benki ya Dunia-WB zitakazotumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya kukuza Utalii na kustawisha miji katika visiwa hivyo.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Khamis Omar alisema Jijini Washington DC kuwa Benki ya Dunia imekuwa mshirika mzuri wa maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokana na misaada mbalimbali wanayoitoa katika kutekeleza miradi yao ya maendeleo.

Bw. Omar alisema Benki hiyo imesaidia kufadhili ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara zinazoingia mijini, Uwanja wa Ndege wa Zanzibar pamoja  na bandari.

Aidha, alisema Benki hiyo imesaidia zaidi katika ujenzi wa Uwanja wa ndege, kwa kujenga sehemu ya maegesho ya ndege, njia ya kutua na kurukia ndege na njia ambazo ndege zinapita kabla ya kuingia kwenye sehemu ya kurukia (runway).

“Pia Benki hii imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya Elimu Visiwani Zanzibar ukiwemo mradi wa kukuza matokeo na kuongeza ufaulu wa  wanafunzi katika shule za Zanzibar” alisema Bw. Omar

Alieleza kuwa kwa sasa wanatekeleza mradi mkubwa wa ustawishaji wa huduma za mijini ambao unafadhaliwa na Benki ya Dunia, na mradi huo utasaidia kuboresha huduma muhimu katika Miji ya Zanzabar ikiwa ni pamoja na kuongeza vivutio vya utalii.

“Mradi huu umekamilika katika awamu ya kwanza,na awamu ya pili itatekelezwa baada ya Benki hiyo kuridhia na kutoa idhini ya utekelezaji wa mradi huo ambapo idhini hiyo  inatarajiwa kutolewa mwezi Aprili, 2020” alisisitiza Bw. Omar 

Katibu Mkuu -Wizara ya Fedha na Mipango ameishukuru Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa kwa ushikiano mzuri wanaouonyesha katika kusukuma maendeleo ya Visiwani Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla.             

Awali Waziri wa Fedha na Mipango, wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Mohamed Abdiwawa alisema lengo la kushiriki katika Mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia-WB na Shirika la Fedha la Kimataifa -IMF ni kujadiliana na vyombo hivyo vya fedha duniani kuhusu miradi inayotekelezwa kwa sasa na kuangalia mustakabali wa utekelezaji wa miradi ambayo inategemewa kutekelezwa kwa siku zijazo.

Mwisho



Maombi ya Freeman Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA Yakataliwa

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali maombi ya upande wa utetezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo mwenyekiti wake Freeman Mbowe juu ya kuanza kwa mashahidi wao kujitetea na badala yake wataanza kujitetea washtakiwa wenyewe.

Baada ya kutolewa uamuzi huo wakili wa utetezi, Peter Kibatala aliomba muda wa wiki tatu kwa ajili ya wateja wake kujiandaa kutoa utetezi huku akisema aliyekuwa tayari ni shahidi hivyo anaomba wateja wake wapewe muda wa kujiandaa.

Upande wa serikali ukiongozwa na Wakili Faraja Nchimbi umepinga muda huo ukisema hakuna sababu ya mahakama kuwapa muda huo hivyo hakimu kutokana na kuibuka kwa hoja hizo ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 21 mwaka huu atakapotoa uamuzi wa lini wataanza kujitetea.

Washtakiwa hao wanaanza kutoa utetezi wao baada ya mashahidi  nane wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao na Mahakama kuwaona washtakiwa hao wana kesi ya kujibu wajitetee.

Wanaokabiliwa katika kesi hiyo,  mbali Mbowe ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar-Salum Mwalimu, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji.

Wengine ni wabunge; John Heche (Tarime Vijijini), Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Esther Matiko (Tarime Mjini).

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendajia jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam

Muhas Wametangaza Nafasi Mpya Za Udhamini Wa Masomo (Scholarships) Kwa Vijana Wa Kitanzania.

$
0
0
Habari Njema | Muhimbili University of Health and Allied Sciences(MUHAS) Wametangaza Nafasi Mpya Za Udhamini Wa Masomo (Scholarships) Kwa Vijana Wa Kitanzania..
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

👉Uwe na GPA Ya 3.5 na kuendelea
👉Ambatanisha CV yako,Vyeti vyako vya Elimu wakati wa kutuma maombi
👉Mwisho wa Kutuma Maombi : 30th October, 2019.
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬  

 Bonyeza Hapo Chini Kujua Zaidi
👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/scholarship/

Zaidi ya watu Milioni 16 wajiandikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2019

$
0
0
Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI
 WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo amesema hadi sasa uandikishaji wa orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa umefikia watu milioni 16.9  kati ya malengo  yaliyowekwa ya watu milioni 22. 9 sawa na asilimia 74.

Mhe Jafo amesema hayo jana wakati wa kutoa tathimini ya uandikishaji wa Wapiga kura katika Orodha ya Daftari la wapiga kura katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika katika Ofisi za TAMISEMI Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amesema kumekuwa na hamasa kubwa kwenye uandikishaji baada ya viongozi mbalimbali hususani Wakuu wa Mikoa na wilaya kuingia mitaani kuhamasisha wananchi.

Mhe Jafo anafafanua kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa kuandikisha wapigakura kwa asilimia 89. Wakati hali bado tete kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo mpaka juzi  ikiwa ni siku ya kwanza tangu kuongezwa muda wa kuandikisha imeadikisha kwa asilimia 37 tu.

Amesema mpaka sasa wapiga kura 16,906,545  wameandikishwa ikiwa ni sawa na asilimia 74 huku Dar es Salaam iliyoandikisha kwa asilimia 89 ikiwa kinara ikifuatiwa na Pwani iliyoandikisha kwa asilimia 86, Tanga kwa asilimia 81, Mtwara kwa asilimia 80 na Lindi kwa asilimia 77.

Mhe. Jafo anaendelea kusema kuwa kwa upande wa Mikoa hakuna Mkoa ulioandikisha chini ya asilimia 50, hata hivyo Mkoa ulioandikisha chini zaidi ni Kigoma iliyoandikisha kwa asilimia 57, Kilimanjaro kwa asilimia 58, Arusha na Shinyanga kila mmoja ukiandikisha kwa asilimia 66.

Akifafanua kuhusu Halmashauri zilizofanya vibaya amesema hali ni mbaya kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambayo imeanikisha kwa asilimia 37 na kufuatiwa na Halmashauri ya Moshi na Korogwe ambazo  kila mmoja imeandikisha kwa asilimia 51.

Awali akitoa tathimini ya uandikishaji wa siku saba za mwanzo zilizoishia Oktoba 14,  Mhe. Jafo amebainisha  wapigakura walioandikishwa walikuwa milioni 15.5 ambao ni sawa na asilimia 68 ya lengo la kuandikisha wapigakura milioni 22.9 huku Mkoa wa Pwani uliongoza kwa kuandikisha kwa wastani wa asilimia 80, ikifuatiwa na Dar es Salaam kwa asilimia 77, Tanga ikiandikisha kwa asilimi 76, Mtwara na Lindi kila mmoja kwa asilimia 75.

Pia Kilimanajro ilishika mkia kwa kuandikisha wastani wa asilimia 48, ikifuatiwa na Kigoma kwa asilimia 53 Arusha kwa asilimia 59.

Wakati huohuo Mhe. Jafo amesema anawashangaa  wanasiasa wanaobeza kuwa uchaguzi na uandikishaji wa mwaka huu ni wa kusuasua na kuwataka kuacha upotoshaji na kujikita kwenye takwimu za ukweli ambapo uandikishaji ulikuwa mkubwa ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2014.

Amefafanua kuwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita, Watanzania zaidi ya milioni 11.49 (11,491,661) ikiwa ni asilimia 62 ya makadilio ya kuandikisha watu 18,587,742 walijiandikisha katika uchaguzi uliofanyika Desemba 14 mwaka 2014

Aidha, Mhe.Jafo amesisitiza kuwa watumishi wa umma hawalazimishwi kujiandikisha na kuwa hakuna hatua au adhabu yeyote  itakachochukuliwa kwa asiyejiandikisha na kuwa kinachofanyika ni kuhamasisha ili kuhakikisha demokrasia inachukua mkondo wake.

“ Kanuni za uchaguzi ziko wazi, hakuna mtu analazimishwa ila kinachotakiwa kufanyika ni watu kuhamasishwa. Tumeona sehemu zingine kuna maandamano ya pikipiki au magari ya kuhamasisha na hili jambo jema kwa nchi yetu, kujiandikisha kunampa fursa mtu ya kwenda kuchagua kiongozi, ukikosa fursa hiyo unaweza baadaye kulalamika umechangua kiongozi ambaye haleti maendeleo” Amesisitiza Mhe. Jafo

Akizungumzia kuhusu “clip za  video” zinazotembea kuwa asiojiandikisha atakosa fursa zingine za maendeleo,  amesisitiza kuwa kanuni  ziko wazi, suala la kujiandikisha na kupiga kura ni hiyari na  mambo haya siyo maelekezo ya Ofisi ya TAMISEMI, watu wanatakiwa kuambiwa faida za kujiandikisha na kupiga kura kwa mustakabali wa maendeleo  ya Taifa.

Hata hivyo, Mhe. Jafo amefafanua kuhusu taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya  watumishi wa Jiji la Dodoma kulazimishwa kujiandikisha  na kusema kuwa lengo lilikuwa ni kuwahamaisha watumishi kwasababu wao wanafanya kazi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo ni vyema wakawa mstari wa mbele kujiandikisha ili kuwahamasisha wengine kujiandikisha.


Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Mawaziri Wa Sekta Za Mazingira, Maliasili Na Utalii Nchi Za SADC

$
0
0
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Mkutano huo utafanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuanzia tarehe  21 hadi 25 Oktoba, 2019.

Madhumuni ya mkutano huu ni pamoja na kuangalia mwenendo wa hali ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi; kubainisha utekelezaji wa mikakati ya hifadhi na usimamizi wa mazingira; kupitia Mkakati wa SADC wa Uchumi wa Bahari (SADC Strategy on Blue Economy); na kutathmini maendeleo katika sekta za misitu, wanyamapori na utalii.

Mkutano wa Mawaziri wa sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii utatanguliwa na mikutano ya wataalam wa sekta ya wanyamapori utakaofanyika tarehe 18 hadi19 Oktoba, 2019. Aidha, Mkutano  wa Makatibu Wakuu wa sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii utafanyika tarehe 21 hadi 24 Oktoba, 2019. Mikutano hii miwili itajadili na kuandaa mapendekezo yatakayowasilishwa katika kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 25 Oktoba, 2019 kwa maamuzi na maelekezo.

Mkutano wa Mawaziri  unatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ijumaa Oktoba 25, 2019, ukumbi wa AICC, Arusha. Aidha Mkutano wa Makatibu Wakuu unatarajiwa kufunguliwa na Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii, Oktoba 21, 2019 katika ukumbi wa AICC, Arusha.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 wanachama wa SADC wanaotekeleza Mkakati wa SADC kuhusu Usimamizi wa Sheria na Vita Dhidi ya Ujangili wa Wanyamapori (SADC Law Enforcement and Anti-poaching). Maeneo mengine yanahusu Programu za uhifadhi yaliyovuka mpaka wa nchi moja hadi nyingine kwenye maeneo ya misitu, uvuvi, mazingira na mabadiliko ya tabianchi; utalii; ukuzaji viumbe maji na Mkakati wa Ubora wa Afya wa wanyama wa majini (SADC Transfontiers Conservation Areas; forestry; fisheries; environment and climate change; tourism;  regional Aqua-culture strategy and action plan; and SADC Aquatic Animal Health Strategy) pamoja na Programu ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi (Environment and Climate change Program).

Ili kufanikisha mkutano huu sekta ya habari ni muhimu kuhabarisha umma kuhusu masuala yote muhimu yatakayojadiliwa hususan yanayohusu maendeleo ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa nchi wanachama. Serikali inatoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na Mikoa ya jirani kuchangamkia fursa za kibiashara kutokana na kuwepo kwa wageni hao.

Mkutano wa Mawaziri wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii ni muendelezo wa mikutano itakayofanyika nchini katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Tanzania ni Mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

Mapema mwezi Agosti mwaka huu, Serikali ya Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikabidhiwa na kupokea rasmi jukumu la  uenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ni moja kati ya jumuiya za  kikanda katika bara la Afrika. Jumuiya hii iliundwa kwa dhumuni la kuimarisha ushirikiano katika nyanja za uchumi,  ulinzi , siasa na usalama.  Jumuiya hii inaundwa na  nchi wanachama 16 ambazo ni: Angola, Botswana, Comoros, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.

Imetolewa na:

Constantine Kanyasu
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
16 Oktoba, 2019

Wadau Wa Uchaguzi Wakutana Jijini Dodoma Katika Maandalizi Ya Uboreshaji Daftari La Kudumu La Wapiga Kura.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi na wadau mbalimbali wa Uchaguzi wamekutana jijini Dodoma kujadili juu ya uboreshaji wa Daftari lakudumu la wapiga kura ambapo imeeleza uboreshaji katika awamu hii utafanyika kwa kutumia teknolijia ya kieletroniki ya Biometriki (BVR) kama ilivyokuwa mwaka  2015..

Akiongea katika  mkutano huo wa wadau wa uchaguzi mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi,Jaji Semistocles Kaijage  amesema Teknolojia hiyo itachukua taarifa za mtu za kibaiolojia na kuzihifadhi katika kanzidata kwaajili ya utambuzi ,na ndio iliyotumika kuandikisha wapigakura mwaka 2015.

Pia amesema , uboreshaji wa safari hii hautohusisha wapiga kura wote waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga mwaka 2015 bali litahusisha wapiga  kura wapya ambao wametimiza umri wa miaka 18 na wale ambao watatimiza umri wa miaka 18 siku ya uchagauzi mkuu wa mwaka ujao 2020.

Kwa upande wake Mkurugenzi  wa uchaguzi Wilson Charles amesema kwa mujibu wa kifungu cha 10  cha sheria ya taifa ya uchaguzi sura  ya 343 na kifungu cha 15 cha sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa sura ya 292 inasema ili mtu aweze kuandikishwa kuwa mpiga kura anapaswa kuwa raia wa Tanzania.

Pia amebainisha ili mtu aweze kuandikishwa lazima awe na umri wa miaka 18 au zaidi au atatimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya uchaguzi.

Hata hivyo amesema kuwa mtu anaweza kukosa sifa za kuandikishwa kama amethibitisha kuwa ana ugonjwa wa akili ,amehukumiwa adhabu ya kifo,anatumikia kifungo cha zaidi ya miezi sita ,amezuiliwa kujiandikisha kuwa mpiga kura na sheria za uchaguzi au sheria nyingine kwa makosa yanayohusiana na uchaguzi au hatakuwa ametimiza umri wa kupiga kura ifikapo siku ya uchaguzi.

Katika hatua nyingine amesema uzoefu inaonyesha kuwa katika chaguzi ndogo vyama vimekuwa havipeleki malalamiko yao kwenye kamati za maadili na badala yake vimekuwa vikipeleka malalamiko yao kupitia vyombo vya habari hali ambayo hupelekea malalamiko yao kutofanyiwa kazi na kamati za maadili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mara baada kukamilika kwa zoezi la kuapisha viongozi hao Kamishna wa Tume ya taifa ya uchaguzi Asina Omary amesema zoezi hilo ni la kisheria hivyo ni lazima taratibu zote za kisheria zifuatwe ili kulifanikisha   huku akizungumzia umuhimu wa uboreshaji wa Daftari hilo la wapiga kura.

Mkurugenzi wa idara ya usimamizi Tume ya taifa ya uchaguzi Anseem Mwampoma amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi wanaowataka.

Ikumbukwe kuwa,Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekamilisha uboreshaji wa Daftari awamu ya Kwanza katika mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Manyara,Simiyu,Mara,Mwanza,Geita,Shinyanga,Kagera  na Kigoma .

Hivyo kwa sasa zoezi hilo linaendelea katika mkoa ya Tabora,Katavi na Rukwa  na litaendelea mikoa mingine ikiwemo Dodoma.
Mwisho

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi October 19

Waziri Biteko Atatua Mgogoro Wa Wachimbaji Misungwi

$
0
0
Na Tito Mselem Mwanza,
Waziri wa Madini Doto Biteko ametatua mgogoro ulio dumu kwa muda mrefu na kuruhusu wachimbaji waendelee na shughuli za uchimbaji katika Machimbo ya wachimbaji wadogo ya Shilalo Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.

Mgogoro huo ulisababisha shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu kusitishwa kutokana na sababu za kimaslahi katika madura 38 kati ya 57 yaliyoko kwenye Machimbo hayo.

Shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zilisitishwa Oktoba 7 mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwa muda usiojulikana kutokana na mgogoro wa umiliki wa eneo yalipo mashimo hayo ili kuweka utaratibu wa usimamizi wa mapato.

Akizungumza na wachimbaji wadogo katika mkutano wa hadhara Waziri Biteko aliwataka waache fitina, majungu na makundi huku akiwataka kufanya kazi na kushirikiana kwa pamoja kwani lengo la Serikali ni kuwafanya wanufaike na uchumi wa madini.

“Rais Dkt. John Pombe Magufuli alituteuwa tufanye kazi kubwa mbili katika sekta ya madini, tuwapatie wachimbaji wadogo maeneo ya kuchimba ili mshiriki kuinua uchumi wa nchi na tuhakikishe mnalipa kodi za Serikali ili fedha hizo zisaidie kuboresha maeneo mbalimbali kwa maslahi ya wananchi wote ikiwemo afya na elimu”.

“Lazima mfanye shughuli zenu kwa usalama lakini mtakapokuwa na migogoro hicho ni kiashiria cha uvunjifu wa amani, Serikali hatuwezi kuruhusu watu wake wakaumizana ndiyo maana Mkuu wa Mkoa alichukua jukumu la kusitisha shughuli za uchimbaji kwa muda, tumeshirikiana tumetatua mgogoro huo hivyo ninawasisitiza wachimbaji wote muachane na siasa zisizo na maana badala yake mfanye kazi na mlipe kodi ya serikali,” alisema Biteko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliwataka wachimbaji na wamiliki wa eneo hilo kuweka utaratibu wa usimamizi wa mapato ili kila mtu apate haki yake anayostahili na anufaike kutokana na mapato yanayopatikana katika machimbo hayo.

Aidha, Mmiliki wa eneo hilo Wilbert Kukwanja, alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mongella kwa kuwakutanisha na Waziri Biteko na kumaliza mgogoro huo kwa sababu kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji katika machimbo hayo kuliwaathiri kiuchumi ambapo aliahidi kulinda amani katika eneo hilo na kutoruhusu migogoro kutokea tena.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga aliwataka wachimbaji katika eneo hilo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia usalama wao kwanza pamoja na kuepuka migogoro ambayo itawaletea hasara wao na familia zao endapo serikali itasitisha shughuli za uchimbaji huku akiwasisitiza kulipa kodi za serikali kila wanapozalisha.

Baadhi ya wachimbaji katika eneo hilo akiwemo Ally Bushiri na Maige Gaude, walimshukuru Rais Magufuli kwa  kuteuwa viongozi wachapa kazi kama Biteko ambae ametatua mgogoro huo kwani walikuwa wamekwishakata tamaa walidhani tatizo hilo litadumu kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi.

Dokta Msonde:kufuta Mtihani Mmoja Wa Shule Ya Msingi Ni Kupata Hasara Ya Upotevu Wa Tsh.bilioni 100.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Imeelezwa kuwa kufuta  matokeo ya Mtihani mmoja wa shule ya msingi ni Sawa na  kupata hasara  ya Upotevu wa Bilioni 100  . 
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dkt Charles Msonde  amebainisha hayo jijini Dodoma katika kikao kilichokutanisha Maafisa wa Baraza la Mitihani Tanzania pamoja na Chama Cha Walimu Tanzania[CWT]Wenye lengo la kujadili na kutathimin namna bora ya kuendelea kudhibiti ufujaji wa mitihani hapa nchini.
 
Dkt.Msonde amesema Mwalimu ni afisa muhimu  katika udhibiti ufujaji mitihani lakini anapojihusisha na wizi wa mitihani hiyo  ni kujidhalilisha taaluma yake hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwa mnyenyekevu na  mwadilifu kwa maslahi ya nchi yake katika kuhakikisha ufujaji wa mitihani haitokei ili kuweza heshima na hadhi ya mitihani kwani hukumika gharama kubwa katika uandaaji wa mitihani.
 
Aidha, Dkt Msonde amesema wamekwisha kuhakiki jumla ya watumishi laki tano na kumi na mbili na mia saba sabini  na saba ambapo watumishi elfu kumi na tano na mia nne kumi na moja wamebainika wameghushi vyeti.
 
Katika hatua nyingine Dkt.Msonde amesema Baraza la Mitihani Tanzania ndio Baraza pekee linaloongoza barani Afrika kwa utendaji kazi mzuri ambao hudhibiti wa ufujaji wa mitihani upo kiwango cha juu ndio maana nchi mbalimbali barani Afrika huja kujifunza nchini Tanzania namna baraza hilo linavyofanya kazi.
 
Hivyo,Dokta.Msonde ametumia fursa kukipongeza chama cha Walimu Tanzania CWT,pamoja na wadau wa elimu kwa ujumla wakiwemo walimu kwa kuendelea kuwa wanyenyekevu na kuonesha uzalendo mzuri katika kudhibiti ufujaji wa mitihani.
 
Kwa upande  wa  Rais wa Chama cha walimu Tanzania Mwalimu Leah Ulaya Pamoja na katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania CWT  Komred Mwalimu Deus Seif   Wamesema ni   vyema serikali ikaangalia  vyema suala la kupandisha vyeo pamoja na madaraja kwani  walio wengi wamekuwa wakipandishwa huku mshahara ukiwa palepale.

Kwa upande wao,walimu waliobahatika kuhudhuria katika kikao hicho wamesema semina na mafunzo mbalimbali waliyoyapata yatawasaidia  kuendelea kuwa na nidhamu,uzalendo katika taaluma zao.



Waziri Jafo:Watanzania Milioni 19.7 Wamejiandikisha Kupiga Kura Serikali Za Mitaa

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri  Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa  [TAMISEMI] Mhe,Seleman Jafo amesema hadi kufikia Tarehe 17,Oktoba,2019,Jumla ya Wapiga Kura 19,681 ,259 wamejiandikisha katika daftari la Orodha ya wapiga kura kwa mwaka 2019.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma,Waziri Jafo amesema kati yao,wanaume ni 9,529,992 na wanawake ni 10,151,267 ambapo ni sawa na asilimia 86 ya lengo la kuandikisha wapiga kura ,22,916,412.
 
Waziri Jafo amebainisha kuwa uandikishaji wa mwaka huu umekuwa na mafanikio makubwa  ikilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2014 ambapo serikali ilikadiria  kuandikisha  watu 18,787,820 na waliojitokeza kujiandikisha  ni 11,882,086 sawa na asilimia 63% ya makadirio.
 
Mafanikio ya mwaka 2019 yametokana na hamasa kubwa iliyofanywa na viongozi wa kitaifa,viongozi wa OR-TAMISEMI ngazi ya makao makuu Wizara,hadi ngazi za chini za vitongoji na vijiji pamoja  vyombo vya habari.
 
Aidha,Waziri Jafo ameitaja Mikoa   mitano iliyofanya vizuri  zaidi katika suala la uandikishaji kuwa ni;-wa  kwanza DSM  malengo ilikuwa ni kuandikisha watu 2,673,873 na uandikishaji halisi ni 2,898,535 sawa na asilimia 108%,wa pili ni mkoa wa Pwani  malengo ilikuwa  594,247 uandikishaji halisi 568,627 sawa na  asilimia 96%,mkoa wa tatu ni Mwanza malengo ilikuwa 1,404,078 uandikishaji halisi  ni 1,340,177 sawa na asilimia 95%.
 
Mkoa wa  nne ni Tanga  ulikuwa na Malengo ya kuandikisha watu 1,087,921 na umevuka lengo na kuandikisha watu 983,104 sawa na asilimia  90%   na mkoa wa Tano ni Singida malengo ni watu 679,427 na umevuka lengo na kuandikisha watu 610,344 sawa na asilimia 90%.
 
Waziri Jafo ameainisha halmashauri tano zilizofanya vizuri zaidi kuwa ni :-ya kwanza ni halmashauri ya Mlele DC Malengo ni 17,848 uandikishaji  ni 27,196 sawa na asilimia 152%,ya pili ni Ngorongoro DC Malengo ni 75,145 uandikishaji ni 96,622 sawa na asilimia 129%,ya tatu ni Kibiti DC  Malengo ni 47,887 uandikishaji  ni 60,539 sawa na asilimia 126%,ya nne ni halmashauri ya Temeke MC malengo ni 718,883 uandikishaji ni 879 ,619  sawa na asilimia 122% nay a Tano ni Monduli DC Malengo 75,173 uandikishaji ni 91,363 sawa na asilimia 122%.
 
Hata hivyo,Waziri Jafo amezitaja halmashauri tano zilizofanya vizuri  kwa kuandikisha  idadi kubwa ya wapiga kura kuwa ni :-ya kwanza ni Temeke MC lengo  ilikuwa 718,883 uandikishaji  ni 879,619 sawa na asilimia122%,ya pili ni Ilala MC  Lengo 741,703 uandikishaji ni 820,600 sawa na asilimia 111%, la tatu ni jiji la Mwanza lengo ni 214,985 uandikishaji 224,901 sawa na asilimia 105% ,nne ni Ubungo MC  Lengo 525,600 uandikishaji 542,728 sawa na asilimia 103% nay a tano ni Kinondoni MC Lengo 592,279  uandikishaji ni  569,872 sawa na asilimia 96%.
 
Pia,Waziri Jafo ametaja mikoa yote 26 kwa ujumla   Tanzania Bara ilivyoshiriki katika zoezi hilo la uandikishaji kuwa ni DSM  lengo 2,673,873 uandikishaji 2,898,535 sawa na asilimia 108%,Pwani lengo 594,247 uandikishaji 568,627 sawa na asilimia 96%,Mwanza lengo  1,404,078 uandikishaji 1,340,177 sawa na asilimia 95%,Tanga lengo 1,087,921 uandikishaji  983,104 sawa na asilimia 90%,Singida Lengo 679,427 uandikishaji 610,344  sawa na asilimia 90%.
 
Mikoa mingine ni Morogoro lengo 1,201,916 uandikishaji 1,075,379 sawa na asilimia 89%,Mbeya  lengo 939,011 uandikishaji 776,811 sawa na asilimia 83%,Ruvuma lengo 737,937 uandikishaji 651,257 sawa na asilimia 88%,Katavi lengo 276,452 uandikishaji 243,163 sawa na asilimia 88% na Mtwara lengo 700,543 uandikishaji 604,670 sawa na asilimia 86%.
 
Kwa Dodoma lengo ni 1,053,799 uandikishaji 893,890 sawa na asilimia 85%,Rukwa lengo 485,254 uandikishaji  410,760 sawa na asilimia 85%,Arusha lengo 931,612 uandikishaji  787,232  sawa na asilimia 85%,Lindi lengo 474,150 uandikishaji 396,832 sawa na asilimia 84%,Iringa  lengo  518,409 uandikishaji 433,259 sawa na asilimia 84%.
 
Mara lengo 842,680 uandikishaji 673,065 sawa na asilimia 80%,Kilimanjaro lengo 936,041 uandikishaji 741,130  sawa na asilimia 79%,Geita lengo ni 839,280 uandikishaji 664,100 sawa na asilimia 79%,Manyara  lengo 720,742 uandikishaji 565,827 sawa na asilimia 79%,Tabora lengo 1,124,660 uandikishaji 879,664 sawa na asilimia 78%,Songwe lengo 515,798 uandikishaji  402,840 sawa na asilimia 78%,Kagera  lengo ni 1,231,631 uandikishaji 961,520 sawa na asilimia 78%.
 
Na kwenye mkoa wa Shinyanga lengo 766,725 uandikishaji 583,928 sawa na asilimia 76%,Simiyu lengo 749,819 uandikishaji 568,342 sawa na asilimia 76%,Njombe lengo 387,529 uandikishaji 290,791  sawa na asilimia 75%,na Kigoma  lengo ni 1,042,880 uandikishaji  676,012 sawa na asilimia 65% hivyo Jumla ya malengo ilikuwa ni 22,916,412   na jumla ya watu waliojiandikisha ni 19,681,259 sawa na asilimia 86%.
 
Licha ya hivyo Waziri Jafo amesema uandikishaji wa wapiga kura ulikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali ya mvua,wananchi kuchanganya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura  linalofanywa na tume ya taifa ya uchaguzi [NEC]na uandikishaji wa daftari la orodha ya wapiga kura  pamoja na umbali kwa baadhi ya vituo vya kujiandikisha.
 
Ikumbukwe kuwa,zoezi la uandikishaji  wa orodha ya wapiga kura lilianza tarehe 8,oktoba ,2019 mpaka tarehe 17,oktoba,2019  huku uchaguzi wa Serikali za mitaa ukitarajia kuanza Novemba 24,2019.

Nafasi Mpya ya Kazi VODACOM Tanzania .....Wanataka Network Director Mwenye Degree ya Telecommunication

$
0
0
Nafasi Mpya ya Kazi VODACOM Tanzania .....Wanataka Network Director 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
👉 Awe na Degree ya Telecommunication au Electrical
👉  Tangazo limetolewa jana: 19th October, 2019.

 ==>>Pia zipo nafasi mbalimbali za kazi kama vile; Afisa Mtendaji (Simiyu), Walimu, UBER TANZANIA,  AIRTEL, JUMIA, NOKIA TANZANIA,UMOJA WA MATAIFA

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Bonyeza hapo chini kujua zaidi

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Wasiooa na kuolewa kucharazwa bakora Mbeya

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kuwa hivi sasa wanatumia bakora katika kila jambo hata kwa watu ambao wanakaa tu nyumbani wakati wamefikisha umri wa kuoa na kuolewa.

Chalamila amesema kuwa bakora ndiyo njia pekee ambayo inasaidia katika kunyoosha mambo.

"Maana siku hizi tumeanza kutumia viboko kwenye kila jambo hata tukikuta umekaa pale nyumbani uolewi ni bakora tu kwamba nenda katafute mume, tunakuona umekaa pale nyumbani huoi ni bakora tu wewe nenda katafute mke.," amesema Chalamila na kuongeza kuwa

"Kuna umri ambao unatosha lazima uchangamshwe kwa hiyo viboko vinasaidia," amesema 

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa huo, alitawala kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuonekana anawachapa bakora baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiwanja, iliyopo Chunya mkoani Mbeya, baada ya kuteketeza kwa moto mabweni yao.

Atiwa Mbaroni kwa Tuhuma za Kumkatakata na Kumuua Mdogo wake

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma, linamshikilia Mohamed Luambano (70) mkazi wa Mtelamwai wilayani Namtumbo kwa tuhuma za kumkata na kitu chenye ncha kali kichwani na kiganja cha mkono wa kulia mdogo wake, Abeid Luambano (65) na hatimaye kufariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, alisema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 2:00 usiku katika kitongoji cha Doroba kilichoko katika kijiji cha Mtelemwai.

Alisema inadaiwa siku ya tukio, Abeid alikutwa akiwa ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali na pia kukatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiofahamika.

Maigwa alisema Abeid kabla ya kuuawa, alivamiwa ghafla na watu wasiojulikana nyumbani kwake na kisha kutolewa nje ya nyumba yake na kuanza kupigwa na kitu chenye ncha kali hadi kupoteza maisha.

Kutokana na tukio hilo, alisema Luambano ambaye ni kaka wa marehemu, amekamatwa kwa mahojiano zaidi kutokana na madai kwamba siku za karibuni kumekuwapo na kutoelewana kati ya ndugu hao.

Alisema ugomvu huo ulisababishwa na Abeid kuchomewa nyumba yake aliyokuwa akiishi akimtuhumu kaka yake na mtoto wake aliyetajwa kwa jina la Msajiri kuwa walikuwa wakimfanyia vitu vibaya.

Mtoto huyo wa Luambano amekimbia na kutokomea kusikojulikana baada ya tukio hilo la mauaji. Kamanda maigwa alisema juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images