Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tembelea Ivigo Herbal Clinic: Kituo Cha Tiba Asili Na Tiba Mbadala Kwa Magonjwa Ya Binadamu

0
0
IVIGO HERBAL CLINIC ni Kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa Magonjwa ya Binadamu ikiwemo Kisukari, presha, Nguvu za Kiume, Vidonda vya Tumbo, Tambazi, MATATIZO ya Uzazi, BAWASIRI, Muwasho sehemu za siri, Miguu kuvimba, UVIMBE Tumboni, Tezi Dume, SHINGO ya KIZAZI kwa Akinamama ,Meno bila  kung'oa, Maumivu ya Mgongo na kiuno , Kuborsha Maumbile ya Kiume pamoja na MATATIZO Mbalimabali ya Kimaisha.

Kwa Huduma zetu Tembelea Vituo vyetu ulichokaribu nacho. MBEYA tupo barabara ya ISANGA kabla hujafika Darajani simu 0744687649, Mbarali KITUO KIPO IGAWA STAND YA BARABARA KUU YA KWENDA MBEYA SIMU 0767007704, DODOMA KITUO KIPO CHANG'OMBE STAND simu  0746906010 na Makao Makuu NJOMBE simu 0767944041.Nyote Mnakaribishwa IVIGO HERBAL CLINIC kwa Tiba  Bora

Mifuko ya Pamoja yamuenzi Mwl. Nyerere kwa kuchochea maendeleo

0
0
Na Mwandishi Wetu
OKTOBA 14, mwaka huu, Tanzania imeadhimisha miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Nyerere.
 
Katika uhaki wake, Mwalimu Nyerere alikuwa na sifa ya utu, mpenda maendeleo, hakupenda kuona watu wakinyanyaswa, wakionewa au kupuuzwa kwa sababu za unyonge wao.
 
Mwalimu Nyerere alichukia rushwa, ufisadi, wizi na aina zote, kujenga misingi imara ya kulifanya Taifa lijitegemea, kutumi rasilimali zilizopo ili kujiletea maendeleo ya kweli.
 
Pia Mwalimu Nyerere alipenda kuona taasisi zilizoanzishwa na serikali zikiwakomboa Watanzania katika nyanja mbalimbali ili waweze kukuza mitaji, kipato chao na kulipa kodi stahiki.
 
Miongoni mwa taasisi iliyobeba maono ya Mwalimu Nyerere na kuyafanyia kazi kwa vitendo ni UTT AMIS.
 
Taasisi hiyo ipo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango iliyopewa dhamana ya usimamizi wa mali kupitia Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja. 
 
Utajiri siyo fedha ambazo mtu anakusanya bali ni fedha zinazowekwa na kufanya kazi. Tamaduni zetu zimeifanya jamii kubwa kuhifadhi fedha ndani katika vyungu, magodoro, vibubu.
 
Uwekaji akiba na uwekezaji ni dhana mbili tofauti. Uwekaji akiba ni mzuri lakini bila kuziwekeza ni bure. 
 
Ili uwe muwekaji akiba mzuri, unapaswa kuwa na nidhamu ya kujizoesha muda mrefu. 
 
Awali UTT AMIS ilipewa dhamana ya usimamizi wa mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi. Hivi sasa taasisi hiyo imeongeza mfuko mwingine wa Hati Fungani.
 
Nchini Tanzania unaweza kuwekeza fedha zako katika masoko ya fedha, mitaji. Hatua hiyo inahusisha akaunti za muda maalum na zisizo za muda maalum katika benki za biashara.
 
Pia hati fungani za Serikali za muda mfupi, mrefu, kampuni na hisa zilizoorodhosgwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ambazo zina nafasi kubwa ya kurejesha gawio zuri. 
 
Uwekezaji unaofanywa na taasisi hiyo kupitia mifuko ambayo wanaisimamia ni fursa mbadala inayowezasha watu, vikundi, taasisi, kampuni kuwekeza pesa zao kwa Meneja wa UTT.
 
Meneja huzichukua fedha hizo, kuziwekeza kwenye masoko ya fedha, mitaji kulingana na waraka wa makubaliano.
 
Faida inayopatikana hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji uliofanyika kwenye mfuko husika. 
 
Mfuko wa Umoja, ulioanzishwa Mei 16, 2005 ukilenga kutimiza mahitaji tofauti ya wawekezaji. Awali bei ya kipande ilikuwa sh. 70, kwa sasa sh. 590.2060.
 
Sifa zilizopo katika mfuko huo ni vipande kuuzwa kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga). kiwango cha chini cha kujiunga ni vipande 10 tu.
 
Malipo ya mauzo hutozwa asilimia moja ya thamani halisi, pia ni rahisi kujiunga, kutoka ambapo manunuzi na mauzo hufanyika kila siku ya kazi. 
 
Mfuko wa Watoto una lengo la kuwasaidia watoto katika maendeleo yao nchini. Awali bei ya kipande ilikuwa sh. 100, mfuko ulianzishwa Oktoba 1, 2008. 
 
Sifa za mfuko huo ni uwekezaji kwa ajili ya mtoto mwenye umri chini ya miaka 18. Kiwango cha chini cha uwekezaji sh. 10,000, unaruhusiwa kuwekeza kidogo kidogo kwa sh. 5,000.
Sifa nyingine ni vipande kuuzwa kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga), mfuko hutoa mipango ya aina mbili, kwanza malipo ya ada, pili mpango wa kukuza mtaji.
 
Malipo ya ada na mauzo ya vipande yanaruhusiwa pale mtoto anapofikisha miaka 12. Mfuko huo ni miongoni mwa mifuko  inayotatua changamoto za kielimu hasa katika ulipaji ada kwa wanafunzi, kutoa mtaji baada ya ukomo wa shule kufikia. 
 
Pia mfuko una mipango miwili mikubwa, mpango wa ada za shule na mtaji kwa mwanao. Ili mzazi aweze kuchangia kupitia mfuko huo, anapaswa kuweka sh. 10,000 kima cha chini na hakuna ukomo kwenye kiwango cha juu. 
 
Mfuko ulianzishwa mwaka 2008. Kiwango cha chini cha kipande kilianzia sh. 100, hivi sasa sh. 346.3151.
 
Mfuko wa Jikimu una lengo la kukidhi mahitaji ya wawekezaji wanaohitaji uhakika wa mapato ya mara kwa mara, ulianzishwa  Novemba 3, 2008 ukiwa na sifa za mipango ya uwekezaji, kiwango cha uwekezaji, mpango wa gawio robo mwaka.
 
Kiwango cha chini cha uwekezaji sh. milioni 2, mpango wa gawio wa mwaka (kiwango cha chini cha uwekezaji sh. milioni moja), tatu mpango wa mwaka wa kukua (sh. 5,000).Vipande vinauzwa kwa thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga). 
 
Mfuko wa Ukwasi unaotoa nafasi ya uwekezaji mbadala kwa wawekezaji wakubwa au taasisi ambao wangependa kuwekeza fedha zao za ziada kwa kipindi kifupi ama cha kati huku wakikuza mtaji wao. 
 
Ulianzishwa Aprili 30, 2013, bei ya kipande ikiwa sh. 100.00, hivi sasa imepanda sh. 126.3239.
 
Sifa za mfuko huo ni rahisi mwekezaji kupata fedha zake za mauzo ya vipande ndani ya siku tatu za kazi baada ya maombi ya kuuza vipande kupokelewa Makao Makuu ya UTT AMIS.
 
Mfuko huo hauna ada ya kujitoa wala kujiunga, una unafuu wa gharama za uwekezaji, unafaa kwa wawekezaji mmoja mmoja au taasisi, kiwago cha chini cha kuwekeza sh. 5,000,000.00.
 
Kuongeza uwekezaji wako sh. 1,000,000.00, pia unaruhusu uhamishaji vipande kutoka kwa mwekezaji mmoja kwenda mwingine, kuruhuusu uhamishaji vipande kwenda kwenye mifuko mingine, kuviuza kwa thamani halisi.
 
Mfuko wa Wekeza Maisha unamwezesha mwekezaji kupata faida pacha (mapato mazuri pamoja na mafao ya bima). 
 
Mfuko huo ulianzishwa Mei 16,2007, wawekezaji kati ya miaka 18 na 55 ndio wanaoruhusiwa kujiunga. Unatoa mipango ya aina mbili, kuchangia uwekezaji awamu ya kwanza, mkupuo mmoja.
 
Vipande vinauzwa kwa thamani halisi, hakuna gharama za kujiunga. Kujiunga ni sh. 8,340.00 tu kwa mwezi. Bei ya kipande kwa sasa sh. 416.4499.
 
Mafao ya bima yanayopatikana ni bima ya maisha, ulemavu wa kudumu na bima ya ajali. 
 
Mfuko unamwezesha mwekezaji kuwekeza kwa mpangilio, kuchangia kwa mwezi, mara mbili kwa mwaka, mara moja kwa mwaka ambapo faida za uwekezaji katika Mifukoya Uwekezaji wa Pamoja ni kukuza mtaji kwa kutoa faida nzuri ukilinganisha na mifuko mingine kwenye masoko ya fedha.
 
Faida nyingine ni kutawanya hatari za uwekezaji, mwekezaji hupunguza athari za uwekezaji kwa kuwekeza katika uwekezaji auai, wawekezaji kufaidika na unafuu wa gharama za uwekezaji.
 
Pia wawekezaji wanaweza kufuatilia maendeleo ya masoko ya fedha kwa kufuatilia maendeleo ya mifuko.
 
Mfuko mpya Hati Fungani unaojulikana kama ‘Bond Fund’ ni kati ya mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS ulioanzishwa kwa malengo maalum.
 
Kuanzishwa kwa Mfuko wa Hati Fungani kumetokana na mahitaji ya wawekezaji na uchambuzi wa bidhaa za kifedha zilizoko kwenye soko la mitaji kwa sasa. 
 
Mfuko utawawezesha wawekezaji wadogo na wa kati kuzifikia fursa za uwekezaji ambazo kwa hali ya kawaida ni wawekezaji wachache na wakubwa ndio wanaozifikia. 
 
Pia utawekeza kwenye hati fungani zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa kwa asilimia 90 na asilimia 10 itakuwa kwenye uwekezaji wenye ukwasi mkubwa.
 
Lengo ni kuwawezesha wawekezaji wanaohitaji kuchukua fedha kutokana na uwekezaji wao katika mfuko wafanye hivyo. 
 
Mfuko umeundwa ili kumwezesha kila mwekezaji kuchagua kama anapenda kukuza mtaji au kupokea gawio kwa mwezi, kila miezi sita kutokana na mahitaji yake ya kifedha. 
 
Akiuzungumzia mfuko huo, Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga, alisema umelenga  kuondoa changamoto ambazo wawekezaji wanakutana nazo.
 
Anasema soko la fedha lina bidhaa nyingi zilizobuniwa ili kukidhi mahitaji tofauti ya watumiaji. 
 
Baadhi ya bidhaa hizo zinaeleweka kirahisi hata namna ya kuzifikia na kuwekeza lakijni wakati mwingine hazitoi faida shindani kwa wawekezaji. 
 
Anasema baadhi ya wawekezaji hasa wadogo ni vigumu kuwekeza kwenye baadhi ya bidhaa katika soko la fedha. Mfuko wa Hati Fungani umeratibiwa ili kuondoa changamoto hizo. 
 
Mwekezaji anapata faida sawa na wawekezaji wakubwa, akihitaji fedha anauza baadhi ya umiliki wake kwenye mfuko kwa utaratibu rahisi bila kupoteza faida aliyoipata.
 
Pia mfuko huo unawafaa wawekezaji wakubwa kwa sababu ya faida shindani, gharama ndogo za kuwekeza, ukwasi wa kutosha, usalama wa mtaji, hatari ndogo za uwekezaji.
 
Mfuko unatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza, kushiriki katika masoko ya mitaji, kufaidika na uwekezaji huo. 
 
Kwa mantiki hiyo, mfuko umeandaliwa ili kutoa fursa kwa wawekezaji wa kipato cha chini, kati na kipato cha juu ambao ni watu binafsi, kampuni, taasisi na vikundi rasmi wanaweza kushiriki katika uwekezaji kwenye mfuko huo. 
 
Mbaga anasema, mfuko una mipango miwili ya uwekezaji ili kukidhi matakwa tofauti ya wawekezaji. 
 
Kuna mpango wa kukuza mtaji, gawio kila mwezi na gawio kila miezi sita, mpango wa kukuza mtaji.
 
Gawio la mara kwa mara halitatolewa kwa wawekezaji badala yake faida iliyopatikana itarudishwa kwenye uwekezaji wa awali kwa kununua vipande vitakavyonunuliwa kwa bei ya wakati huo. 
 
Mpango huo utawafaa wawekezaji wanaohitaji kuweka akiba kwa malengo maalum mfano kujenga nyumba au wafanyakazi wenye kipato kama wangependa kuwa na fedha ya akiba.
 
Wawekezaji katika mpango huo wanaweza kuuza kiasi chochote cha uwekezaji wakiwa wamekidhi vigezo vinavyohusu uuzwaji wa vipande.  
 
Wawekezaji wanaohitaji kuchukua faida kila mwezi kama  wastaafu wanaopata fedha zao za mkupuo, kuwekeza kwenye mfuko, wanashauriwa kuchagua kupokea gawio kila mwezi ili wapate kipato cha kuishi bila kupoteza fedha walizopata. 
 
Mbaga anasema wawekezaji wengine wanaopata fedha nyingi mara moja mfano wachimba madini, wanaweza kuchagua gawio kila mwezi ili wafanye shughuli zao bila kuathiri mtaji wao.
 
Pia wawekezaji watakaojiunga na mpango huo wanaweza kuuza vipande kidogo au vyote ili mradi wawe wamekidhi vigezo vya mfuko vinavyohusu uuzwaji vipande. 
 
Mpango wa gawio kila miezi sita, Mbaga alisema hutegemea na mahitaji ya fedha ya mwekezaji na anavyochagua kwenye fomu ya maombi ya kuwekeza kwenye mfuko. 
 
Kwa wawekezaji ambao wanahitaji kuchukua faida kila miezi sita mfano wafanyakazi wanaohitaji kuweka kiasi cha fedha ili faida inayopatikana itumike kulipa ada kusomesha watoto, wanaweza kuchagua kupokea gawio kila miezi sita. 
 
Pia kuna wawekezaji wanaopata fedha nyingi mara moja kama wakulima wa mazao mbalimbali ya msimu, wanaweza kuchagua kupata gawio kila miezi sita.
 
Wawekezaji watakaojiunga na mpango huo wanaweza kuuza vipande kidogo au vipande vyote ili mradi wawe wamekidhi vigezo vya mfuko.
MWISHO.

Nchi Wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu Zajadili Halia ya Amani, Usalama

0
0
Na Mwandishi wetu, Brazzaville
Nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu wakutana jijini Brazzaville na kujadili hali ya amani na usalama katika maeneo yaliyokubwa na ugonjwa wa ebola.

Wanachama hao walikutana na pamoja na wataalamu wa afya kutoka nchi hizo kuanzia tarehe 11 hadi 14 Oktoba 2019, jijini Brazzaville Jamhuri ya Kongo

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianao wa Jamhuri ya Kongo, Mhe. Jean Claude Gakosso ambapo alisema kuwa mkutano huo uliitishwa kwa ajili ya kujadili masuala makuu mawili ikiwemo hali ya ugonjwa wa ebola katika ukanda wa maziwa makuu pamoja na hali ya usalama katika maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa wa ebola.

Kuhusu hali ya ugonjwa wa ebola, ilielezwa kwamba nchi ya DRC ndiyo iliyoathirika zaidi na ugonjwa huo. Ikielezwa kwamba zaidi ya watu 3000 wameathirka na ugonjwa huo na kati yao zaidi ya 2000 wamepoteza maisha ambapo maeneo yaliyoathika zaidi ni yale ya mashariki mwa DRC ambayo ni Kivu Kaskazini, Ituri na Kivu Kusini.

“Juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya DRC hadi sasa kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na wadau wengine katika kupambana na ugonjwa huo ni kutoa chanjo ya kinga ya ugonjwa huo na elimu kwa wananchi wa maeneo yaliyoathirika na ugionjwa huo” alisema Waziri Gakosso

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya kutoka ukanda wa maziwa makuu, imeelezwa kuwa hali ya maambukizi kwa sasa imepungua katika maeneo hayo.

Aidha, pamoja na jitihada hizo za serikali ya DRC kwa kushirikiana na wadau wengine katika mapambano hayo kumekuwa na changamoto ya usalama kutokana na kuendelea kuwepo kwa makundi ya waasi katika maeneo hayo ambayo yamekwamisha jitihada hizo

Katika hatua nyingine, mkutano wa waratibu wa kitaifa kutoka nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu kutoka nchi zote 12 walikutana na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo, michango ya wanachama,  suala la ajira, hali ya ulinzi na usalama katika nchi wanachama wa pamoja na suala la watu wasio na utaifa

Mikutano hiyo miwili imetangulia mkutano mkuu wa mawaziri wa mambo ya Nje kutoka nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu utakao fanyika leo, Brazzaville ambapo ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro

Nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu ni pamoja na Angola, Burundi, Jamhuri ya Kati, Demokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudani Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.

Rais Magufuli Ambana Mkurugenzi Nachingwea....Ataja Sababu za Kutumia magari ziara yake mkoani Lindi

0
0
Rais  Magufuli amewabana Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea (DC) Rukia Muwango na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bakari B Bakari baada ya wananchi kulalamikia ucheleweshwaji wa miradi ya maendeleo.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Oktoba 16, 2019 wakati Rais akihutubia wananchi katika wilaya ya Nachingwea ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa wa Lindi.

Baada ya hotuba za viongozi mbalimbali, Rais alimuomba Mwenyekiti wa CCM, Mzee Hashim Mkanjauka aeleze matatizo yote yanayowakabili wakazi wa Nachingwea.

Mkanjauka alianza kuelezea miradi ya maendeleo iliyokwama hali iliyowafanya wananchi waibuke kwa shangwe na hivyo kumfanya Rais atake kujua Zaidi kero hizo.

“Viongozi wetu siyo wakweli, miradi wilaya ya Nachingwea vijijini haitekelezeki, stendi ya wajasiriamali hakuna, soko halina kitu mkandarasi waliyempa hajamaliza, redio imenunuliwa na kufungwa kwa fedha za wananchi zaidi ya Sh100 milioni lakini haifanyi kazi. Maji yamekuja na mwenge yameondoka na mwenge Nachingwea ni wilaya kongwe,” amesema Mzee Mkanjauka.

Baada ya maelezo hayo Rais alimuita Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo akimtaka atoe majibu ya kwanini miradi hiyo inasuasua na mingine imesimama kabisa.

“Sh200 milioni ilijenga sehemu ya kupumzikia wasafiri , mabanda 12 ya biashara sisi tulikuta imefungwa tuliwekeza kwa kuweka mabanda kwa mapato ya ndani ya Sh81 milioni, kujenga mabanda 26 kumalizia choo na kuanza kwa kuwa ni kubwa maeneo tuliyotenga kwa ajili ya wajasiriamali itabidi tuyapimie wameshapimiwa na wanaohitaji miundombinu ni mama lishe.”

Majibu hayo yalizalisha maswali zaidi kwamba ni kiasi gani hasa kilichotumika kwa upande wa soko pekee, Mkurugenzi huyo alijibu kuwa ni Sh71 milioni.

Baadaye Rais aliamua kushuka katika gari na kutembea mita kadhaa eneo la soko ili kujiridhisha kama kweli ujenzi unaendana na thamani ya fedha inayotajwa.

Baada ya kufika katika soko hilo na kuona hali halisi, alitaka kujua Sh71 milioni namna zilivyotumika lakini Mkurugenzi alionekana kujikanyaga namna alivyokuwa anajibu.

“Nawashukuru ndugu zangu wa Nachingwea kwa kuwa wakweli, ukweli humweka mtu huru, Tsh milioni 71 zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa soko lakini mambo yanasuasua. Hayo mengine niachieni mimi nitafanya maamuzi.

“Tunahitaji watendaji wakali, huyu mkurugenzi wenu ameniuzi sana, anasema alikua anafanya kazi Marekani, sijui alikua anaokota makopo?

“Nafahamu shida mnayopitia barabara, ndiyo maana nimekuja na usafiri wa gari, ningeweza kuja na ‘helikopta’ lakini nimeamua kutumia barabara ili niyapate maumivu mnayoyapitia. Nataka niwahakikishie kuwa hii barabara ya kilometa 45 ya Nachingwea tutaijenga katika kiwango cha lami.

“Hii barabara tutaijenga kwa kiwango cha lami, kutoka Nachingwea – Ruangwa na Nanganga – Masasi, tumezoea kuona barabara za lami ni za mkoa kwa mkoa lakini sasa tunaanza kuunganisha hadi wilaya. Mliojenga pembezoni mwa barabara mjiandae kuhama bila fidia

Wafanyabiashara Manyara Wakunwa Na Utendaji Wa Rais Magufuli-waahidi Kulipa Kodi Kwa Hiari

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Manyara
WAFANYABIASHARA mkoani Manyara, wameahidi kuendelea kulipa kodi kwa hiari baada kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Wafanyabiashara hao wamemweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji aliyekutana nao Mjini Babati ili kujadili fursa na changamoto zinazoikabili sekta binafsi pamoja na kuwaelimisha namna Serikali ilivyofuta kodi lukuki kwa lengo la kuwawezesha kufanyabiashara zao kwa tija Zaidi.

Pamoja na ahadi hiyo ya kulipa kodi kwa hiari, wafanyabiashara hao wamemwomba Dkt. Ashatu Kijaji awasaidie kufikisha kilio chao kwa Serikali ili idadi kubwa ya taasisi za Serikali zinazowabana kulipa kodi zipunguzwe, ama kodi zinazodaiwa ziunganishwe ili kumwondolea mfanyabiashara adha ya kudhibitiwa na Mamlaka nyingi.

Baadhi ya Mamlaka zilizotajwa ni pamoja na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Wakala wa Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) na nyingine nyingi ambazo wamesema mbali na kuwatoza kodi kubwa lakini wamekuwa wakipata usumbufu wa aina mbalimbai.

Akijibu hoja mbalimbali za wafanyabiashara hao, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amewapongeza wafanyabishara hao kwa kulipa kodi ambayo imeiwezesha Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya.

“Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, mwezi Septemba, tumekusanya Zaidi ya shilingi trilioni 1.76 kiasi ambacho hakijawahi kutokea tangu nchi ipate uhuru” alisema Dkt. Kijaji

Alisema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya ufanyajibiashara ambapo mpaka sasa imeondoa Zaidi ya kodi 50 zilizokuwa zikiwakwaza wafanyabiashara lengo likiwa ni kuwawezesha kufanyabishara yao kwa ufanisi zaidi ili waendelee kulipa kodi

“Tumepunguza kodi nyingi sana!, Mwaka uliopita wa fedha (2018/2019) tulipunguza kodi 108 na mwaka huu wa fedha (2019/2020 tumepunguza kodi na tozo 54 kwa makusudi, Dkt, John Pombe Magufuli ameamua kuwawezesha watanzania, kila mmoja kwenye eneo lake la kazi afyanye kazi vizuri” alisisitiza

Aidha, Dkt. Kijaji aliwataka wafanyabiashara waliopata msamaha wa riba kwenye kodi mbalimbali walizokuwa wanadaiwa, walipe madeni yao kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na kwamba hakutakuwa na muda mwingine utakao ongezwa.

Aliwataarifu wafanyabiashara hao kwamba Serikali imesitisha kwa muda utoaji fedha kwenye miradi mikubwa ya kimkakati iliyopangwa kutekelezwa na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI yenye lengo la kuziwezesha Halmashauri kujitegemea kimapato hadi pale mfumo madhubuti wa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo utakapo wekwa.

Dkt. Kijaji alitoa kauli hiyo baada ya kupokea maombi kutoka kwa Mbunge wa Babati Mjini Mhe. Pauline Gekul, aliyeomba shilingi bilioni 5.5 kutoka Serikalini kwa ajili ya kujenga kituo cha mabasi ili kuboresha mazingira ya biashara na utoaji huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake Naibu Kamishna Operesheni ya Kodi Bw. Simon Kingu, alisema TRA iko tayari kushirikiana na wafanyabishara na kuhakikisha wanatatua kero zao ili walipekodi kwa hiari kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Alisema juhudi kubwa inayofanywa na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifikisha nchi katika uchumi wa kati wa viwanda unategemea mchango mkubwa wa wafanyabiashara katika kulipa kodi stahiki.

Mwisho

Mahakama ya Rufaa Yatengua Hukumu na Amri ya Mahakama Kuu kuzuia Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi Mkuu

0
0
Mahakama ya Rufani Tanzania imetengua uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyobatilisha sheria inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu.

Kutokana na hatua hiyo, kuanzia sasa Wakurugenzi wapo huru kusimamia uchaguzi.

Uamuzi wa Mahakama ya Rufani, umetolewa na Msajili Elizabeth Mkwizu baada ya Serikali kukata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu juu ubatilisho wa sheria hiyo.

Katika uamuzi uliosomwa na Msajili wa Mahakama, Mkwizu amesema kuwa miongoni mwa hoja ni kwamba;

Wakurugenzi hawawi wasimamizi wa Uchaguzi moja kwa moja kwa kuteuliwa kwao bali kuna mchakato wa kisheria wanapitia ikiwemo kula kiapo, kutunza siri na kukana uanachama wa Chama walichokuwa nacho kabla ya uteuzi.

Mei 13, 2019 Serikali ilitangaza kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mei 10, 2019 uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo ilibatilisha sheria inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Atuganile Ngwala katika kesi ya msingi namba 6 ya mwaka 2018 iliyofunguliwa na mtoto wa marehemu Chacha Wangwe ambaye ni Bob Chacha Wangwe.

Katika kesi hiyo ya Kikatiba, Jaji Ngwala alibatilisha vifungu viwili vya Katiba cha 7 (1) ambapo kinaeleza kuwa ‘Kila Mkurugenzi wa Jiji na Halmashauri wanakuwa wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu’

Pia alibatilisha Kifungu cha 7 (3) kinachoeleza kuwa Tume inaweza kumchagua mtu yoyote kuwa msimamizi wa Uchaguzi wakati katiba inasema huwezi kuwa Mwanasiasa na ukawa msimamizi wa uchaguzi bali inatakiwa achaguliwe mtu huru.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi October 17

Msema Mkuu wa Serikali Awatoa Hofu Watanzania....."Serikali haidaiwi na haijawahi kukopa Standard Charterd ya Hong Kong."

0
0
Mahakama  ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID), imeiamuru Tanzania kulipa Dola za Marekani milioni 185 pamoja na riba kwa madai ya uharibifu ilioufanya kwenye Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) kuhusu mzozo wa akaunti ya IPTL Escrow.

Hata hivyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas jana kupitia ukurasa wake wa Twitter, alitoa ufafanuzi wa hukumu hiyo na kusema kuwa deni hilo siyo la serikali bali ni la Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Katika maelezo yake Dk. Abbas alisema kuwa serikali itahakikisha wanasimamia utawala wa sheria ili IPTL ilipe deni lao.

"Nimekuwa nikiulizwa kuhusu kesi zilizoamuliwa za Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) dhidi ya Tanesco na sasa serikali. Msingi wa kesi zote mdaiwa si serikali wala Tanesco, ni deni la Benki dhidi ya IPTL walilorithi miaka mingi kutoka wakopeshaji wa Malaysia."

"Kwa muktadha huo na kisheria serikali na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ziliunganishwa tu kama kanuni za kisheria zinavyomruhusu mdai kuwaunganisha wahusika wengine kwenye kesi ili kuhakikisha au kupata uhakika kuwa analipwa madai yake," alifafanua.

Dk. Abbas aliwatoa wasiwasi Watanzania kuwa serikali haidaiwi na haijawahi kukopa Standard Charterd ya Hong Kong.

"Ila kama Baraza la Usuluhishi lilivyoamua, tutahakikisha tunasimamia utawala wa sheria kwa kuona IPTL wanalipa deni lao," alisema.

Hukumu ya kesi hiyo ilifanyika Oktoba 11, mwaka huu na jopo lililosikiliza shauri hilo liliundwa na David Unterhalter kutoka nchini Afrika Kusini, aliyeteuliwa na mlalamikaji na Kamal Hossain kutoka nchini Bangladeshi aliyeteuliwa na mlalamikiwa.

Julai 11, mwaka 2016 Unterhalter aliteuliwa baada ya kujiuzulu kwa Stanley Burnton kutoka Uingereza.Wawakilishi wa mlalamikaji walikuwa ni Herbert Freehills kutoka Uingereza na wa mlalamikiwa ni kampuni ya uwakili ya Crax Low Partners na Rweyongeza and Company Advocates za jijini Dar es Salaam.

Mwaka jana pia, mahakama hiyo ya ICSID iliikataa rufani ya Tanesco ya kupinga hukumu ya kuilipa Benki ya Standard Chartered Dola za Marekani milioni 148.4 sawa na Sh. bilioni 336.

Katika kesi hiyo, Rais wa ICSID, Claus von Wobeser alitupilia mbali hoja za Tanesco za kuitaka mahakama hiyo kutengua uamuzi wa awali ulioipa ushindi benki hiyo ya Hong Kong, nchini China.

Fedha hizo ni madai ya malipo ya umeme baina ya Tanesco na IPTL iliyopewa zabuni ya kufua umeme wa dharura kuanzia Mei 26, mwaka 1995 huku ikidaiwa na benki hiyo.


Asilimia 25 Ya Mazao Yanayozalishwa Duniani Yanaathiriwa Na Sumukuvu

0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Singida
Kwa miaka ya hivi karibuni kumejitokeza changamoto ya chakula salama (Safe food) kutokana na uwepo wa tatizo la sumukuvu katika mazao ya chakula, hususani mahindi na karanga ambayo huchangia upatikanaji wa lishe bora na ni chakula muhimu kwa Watanzania walio wengi.

Taarifa zinaonesha kuwa tatizo la sumukuvu ni kubwa kwani inakadiriwa kuwa asilimia 25 ya mazao yote yanayozalishwa duniani yanaathiriwa na sumukuvu. sumukuvu ina athari kubwa za kiafya na huchangia karibu asilimia 30 ya saratani ya ini, kuharibu mfumo wa kinga na kupelekea udumavu kwa watoto.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameasema hayo jana tarehe 16 Octoba 2019 wakati akifunga Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani mwaka 2019 ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Bombadier Mkoani Singida.

Amesema kuwa athari hizi haziishii tu kwa binadamu, bali hata mifugo nayo huathiriwa na tatizo hili, hivyo kupelekea mtu kula sumu hizi kupitia mazao ya wanyama kama vile maziwa, mayai, samaki na nyama kutoka kwa wanyama waliolishwa vyakula vyenye sumukuvu kwa kiwango kikubwa.

Mazao hayo pia yana umuhimu mkubwa katika kupata lishe bora, hivyo ametoa mwito kwa wafugaji wote nchini kuchukua tahadhari dhidi ya sumukuvu katika sekta ya mifugo ili kutekeleza kaulimbiu ya maadhimisho haya kwa vitendo.

Kadhalika amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufi kupitia wizara ya kilimo hivi karibuni ilizindua mkakati maalumu wa kupambana na sumukuvu nchini hivyo wananchi wanapaswa kuunga mkono juhudi hizo za serikali.

Amesema kuwa Madhara ya Sumukuvu si tu huchangia upotevu wa nguvukazi na kudumaza akili za watoto bali pia hupunguza tija na kipato kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. "Kama tunavyokumbuka mwaka 2016, watu 68 katika Halmashauri za Bahi, Chemba, Kiteto na Kondoa waliugua baada ya kula chakula chenye kiwango kikubwa cha sumukuvu na watu 19 kufariki dunia kutokana na tatizo hilo" Alikaririwa Mhe Hasunga

Amesema kuwa ili kupata lishe bora na ulimwengu usio na njaa, serikali haina budi kushughulikia changamoto hizi kwa ujumla wake ili kuendana na kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya chakula Duniani mwaka 2019 isemayo Lishe bora kwa ulimwengu usio na njaa, kwani ina maana kubwa sana katika kuhakikisha si tu tunazalisha chakula cha kutosheleza mahitaji lakini tunahitaji chakula kilicho salama ili kuboresha lishe na afya za wananchi wetu

"Kama tunavyokumbuka mnamo mwezi Machi  mwaka 2019, nilizindua Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu  Nchini (TANIPAC) ambao una lengo la kupunguza sumukuvu (aflatoxin) katika mazao ya mahindi na karanga. Hivyo, naamini mafanikio ya mradi huu yatachangia sana katika kuimarisha lishe na kuongeza upatikanaji wa chakula bora na salama hapa nchini. Nirudie kuagiza tena watendaji wa Wizara kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi huu ikiwemo elimu kwa wananchi ili kuepuka madhara ya sumukuvu, na hivyo kuimarisha lishe kwa watu wa rika zote" Alisema Mhe Hasunga

Maadhimisho hayo ambayo yamefikia kilele leo ni ya 39 tangu yalipo adhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1981. Maadhimisho hayo hufanyika tarehe 16 ya mwezi Oktoba kila mwaka ambapo Tanzania na nchi zingine Wanachama wa Umoja wa Mataifa,  huadhimisha Siku ya Chakula Duniani. 

Aidha, amesema lengo mahsusi la maadhimisho hayo ni kuamsha ari ya uzalishaji wa mazao ya chakula hususani yaliyoongezewa virutubishi na kutoa hamasa ya kuongeza tija kwenye uzalishaji ili kujihakikishia usalama wa chakula na lishe kuanzia ngazi ya Kaya hadi Taifa, kuhamasisha watu hususani waishio Vijijini na wale walio katika matabaka ya mazingira magumu kushiriki katika kufanya maamuzi sahihi juu ya ulaji bora, pamoja na kupanua wigo wa usambazaji wa teknolojia ili kuongeza tija ya uzalishaji lengo likiwa kupambana na Adui Njaa, Lishe duni (Utapiamlo) na Umaskini.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa mwito kwa wananchi wote hasa wakulima, wafugaji na wavuvi kufuata kanuni bora za ulaji, kuzalisha vyakula vyenye virutubishi, ufugaji bora na uvuvi ili kusaidia kuboresha afya na kupunguza matatizo ya lishe nchini.

Amewataka Wataalamu wa sekta ya kilimo kutafuta namna bora ya kuhakikisha Tanzania inaondokana na tatizo la lishe duni kwa kaya kwani Tanzania inazalisha chakula kwa wingi na cha kutosha. "Nchi yetu haina njaa na tutaendelea kusimamia uzalishaji kwa kutoa kipaumbele kwa upatikanaji wa pembejeo na viuatilifu vyenye bei nafuu na kuhakikisha masoko ya mazao ya wakulima yanapatikana"

Mhe Hasunga ametumia fursa hiyo pia kuwakumbusha wakulima kujipanga vyema na maandalizi ya msimu ujao wa kilimo kwani katika maeneo mengi ya nchi tayari mvua zimeanza kunyesha. Amesema wananchi wanapaswa kutumia mvua hizo za mwanzo kupanda mazao kwa kutumia kanuni bora za kilimo ili kuwezesha tija kupatikana.

Waziri Hasunga amesema kwa uoande wa Maafisa Ugani wa Kata na Vijiji wanalo jukumu la msingi kutoa elimu na ushauri wa kanuni bora za kilimo kwa wakulima na wafugaji nchini.

MWISHO

Waziri Mkuu Akagua Ujenzi Wa Hospitali Ya Wilaya Ya Ruangwa....Akemea Ujenzi Mbovu Wa Kuta, Aagiza Zibomolewe Na Kurekebishwa

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi na kusema kwamba hajaridhishwa na baadhi ya majengo.

Amemwagiza Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Tengamaso Wilson abomoe kuta zenye hitilafu na kurekebisha kasoro zilizopo kwenye majengo hayo ikiwemo kutonyooka kwa kuta za majengo hayo.

Alitoa agizo hilo jana (Jumatano, Oktoba 16, 2019) wakati akikagua majengo ya hospitali hiyo, na kumweleza mhandisi huyo kwamba kuta zimepishana unene kwa sababu hakusimamia kazi yako ipasavyo. “Ukuta huu ni mbovu kwa sababu hukuwasimamia vizuri mafundi wako. Kuna mahali juu unaona ukuta ni mdogo na huku chini ni mnene.”

Majengo ambayo Waziri Mkuu aliyakagua na kuonesha kutoridhishwa nayo ni ya utawala, wagonjwa wa nje (OPD) na maabara. Majengo mengine yanayojengwa ni jengo la wazazi, la X-ray, la utoaji dawa na la kufulia nguo.

Alipouliza ni kwa nini kumetokea tofauti baina ya kuta hizo, Waziri Mkuu alijibiwa kwamba tatizo ni upigaji wa lipu. “Mhandisi wa Wilaya simamia hili, kagonge upya kuta za jengo hili na lile. Hatuwezi kuwa na jengo la Serikali la aina hii. Tukitoa fedha ya Serikali ni lazima mjiridhishe kama kilichojengwa ndicho sahihi.”

“Tunahitaji majengo yote yawe smart, hata ujenzi wake nao uwe smart. Usikubali kutoa certificate kama kazi haijakamilika. Kama kuna kazi haujaridhika nayo, usikubali certificate itoke. Zile sentimeta 30 ni lazima zirekebishwe la sivyo, itaonekana huku uliweka matofali mengi kuliko upande ule,” alisisitiza.

Akiwa hospitalini hapo, Waziri Mkuu alielezwa kwamba katika awamu ya kwanza, Serikali imetoa sh. bilioni 1.5 na kuelekeza yajengwe majengo saba ya kipaumbele ambayo ni jengo la wazazi, la wagonjwa wa nje (OPD), maabara, la X-ray, la utoaji dawa, la kufulia nguo na la utawala.

Ujenzi wa hospitali hiyo unafanyika kwa kutumia njia ya manunuzi inayoitwa ‘Force Account’ ambapo Halmashauri inanunua vifaa vya ujenzi na kuajiri mafundi wa kujenga majengo yaliyoelekezwa wakisimamiwa na wataalam wa halmashauri na kamati mbalimbali.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemwagiza mweka hazina wa Halmashauri hiyo, Bw. Frank Chonya ajiridhishe na kazi za ujenzi zinazofanyika kabla hajaamua kutoa fedha za malipo.

“Mweka hazina, wakati wote ukiambiwa kuwa certificate imeletwa ni lazima uende ukakague mradi na kama haujaridhika, sema wazi kwamba hujaridhika na kazi iliyofanywa,” alisema Waziri Mkuu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bw. Andrea Chezue alisema kiasi chote kilichotolewa na Serikali cha sh. bilioni 1.5 kimeshatumika, na kwamba Halmashauri illitumia zaidi ya sh. milioni 100 ili kusafisha eneo na kulipa fidia ili wapate eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 56.

“Mchango wa Halmashauri ya Wilaya kwenye ujenzi wa hospitali hii, mpaka sasa ni kwamba tumelipa sh. milioni 88.266 zikiwa ni fidia ya eneo la ujenzi na sh. milioni 14.418 zimetumika kusafishia eneo lote,” alisema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Simbachawene Aagiza Waliokiuka Maagizo Ya Serikali Wafutiwe Vibali Vya Kuingiza Na Kusafirisha Vyuma Chakavu.

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. George Simbachawene ameagiza kufutwa kwa vibali vya wafanyabiashara wote wanaosafirsha vyuma chakavu ambao hawakufuata maelekezo na maagizo ya Serikali.
 
Amesema hayo jijini Dodoma wakati wa mkutano wa kupokea ripoti ya kamati aliyoiunda kwa ajili ya uchunguzi wa makontena ya bidhaa za chuma chakavu yaliyokua yamekamatwa  kwa uchunguzi katika bandari ya jiji la Dar Es Salaam. Ninaagiza wafanyabiashara wote waliokiuka maagizo na maelekezo ya Serikali wafutiwe vibali vyao.
 
Waziri Simbachawene ameipongeza kamati hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya na amepokea mapendekezo yote yaliyopendekezwa na kamati hiyo. “Nawapongeza sana mmefanya kazi kubwa na mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati nimeyapokea na ninaagiza NEMC kama msimamizi mkuu kusimamia jambo hili’ alisema Waziri
 
Aliongeza kuwa Wafanyabiashara wa vyuma chakavu siyo wakweli mana wengi wanasafirisha bidhaa zingine tofauti na vyuma chakavu huku wakisingizia kuwa wamebeba vyuma chakavu wakati siyo kweli.  Vitu mbalimbali vinasafirishwa kama vile mifuniko ya chemba, injini za vifaa vya moto, mita za maji, vipande vya bomba na vingine ni vipya kabisa na haviko kwenye kundi la vyuma chakavu.
 
Akiongea wakati wa kumkaribisha Mh. Waziri, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la usimamizi wa hifadhi ya mazingira (NEMC)  Dkt Gwamaka Mafwenga alisema kuwa ziko Kampuni sita ambazo makontena yao yalikamatwa Bandarini  na yalikua yakifanyiwa uchunguzi. Makampuni hayo ni J. M Kambi and General Services(makontena 88), JBR Group of Companies(makontena 35), Villa Plast L.td(makontena 3) , Three Star Metal Group(makontena 12) na Steel Com Ltd(makontena 2).
 
  Waziri Simbachawene alifanya ukaguzi katika bandari ya Dar Es salaam na kuagiza makontena yote ya Kampuni tajwa hapo juu yaliyokua yamebeba shehena ya vyuma chakavu kuzuiliwa kusafirisha bidhaa hizo na kufanyike uchunguzi wa haraka sana juu ya makontena hayo.



Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Kufungua Maonyesho Ya Pili Ya Viwanda Mkoani Pwani

0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MAKAMU wa Rais wa Jamhur ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua maonyesho ya viwanda ambayo yanafanyika kwa mara ya pili mkoani Pwani, octoba 17  mwaka huu.
 
Katika maonyesho hayo ,wenye viwanda 206 wamejitokeza kushiriki .
 
Maonyesho hayo yataambatana na kongamano la uwekezaji litakalofanyika octoba 19 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Wazir Mkuu Kassim Majaliwa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu suala hilo, mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema, waratibu wa maonyesho hayo watakuwa ni wabobezi wa masuala ya maonyesho kama hayo kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) pamoja na mamlaka ya maendeleo ya viwanda (TANTRADE) .
 
Alieleza, malengo ya matukio hayo ni kuonyesha kwamba mkoa wa Pwani ,umedhamiria kuwa ukanda wa viwanda,wenye viwanda kupata masoko ya uhakika,kupanua wigo wa soko la ndani ya mkoa kufikia kimataifa na ,kuvutia wawekezaji wapya.
 
Aidha Ndikilo alifafanua lengo la kongamano hilo ,kuwa ni kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo kupitia sekta mbalimbali ikiwemo utalii,uchumi,kijamii,kilimo,uvuvi na viwanda.
 
“Kufanyika kwa kongamano hili italeta picha halisi ya fursa zote zilizopo mkoani Pwani,na kuonyesha namna mkoa ulivyopiga hatua katika sekta ya viwanda,uwekezaji na fursa za miradi mikubwa ikiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa uzalishaji umeme megawatts 2,100 STIGO ,huko Rufiji”alibainisha Ndikilo.
 
Hata hivyo,mkuu huyo wa mkoa alisema wenye viwanda maonyesho ya mwaka jana walikuwa 166 mwaka huu wanatarajia  wameongezeka 206.
 
Nae Januarius Maganga wa TSN alisema ,wanakwenda kuratibu maonyesho hayo ikiwa ni maonyesho ya kumi .
 
Maonyesho hayo pia yatafungwa octoba 23 mwaka huu na Wazir Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda

Zaidi ya watu Milioni 16 wajiandikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2019

0
0
Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI
 WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo amesema hadi sasa uandikishaji wa orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa umefikia watu milioni 16.9  kati ya malengo  yaliyowekwa ya watu milioni 22. 9 sawa na asilimia 74.

Mhe Jafo amesema hayo jana wakati wa kutoa tathimini ya uandikishaji wa Wapiga kura katika Orodha ya Daftari la wapiga kura katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika katika Ofisi za TAMISEMI Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amesema kumekuwa na hamasa kubwa kwenye uandikishaji baada ya viongozi mbalimbali hususani Wakuu wa Mikoa na wilaya kuingia mitaani kuhamasisha wananchi.

Mhe Jafo anafafanua kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa kuandikisha wapigakura kwa asilimia 89. Wakati hali bado tete kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo mpaka juzi  ikiwa ni siku ya kwanza tangu kuongezwa muda wa kuandikisha imeadikisha kwa asilimia 37 tu.

Amesema mpaka sasa wapiga kura 16,906,545  wameandikishwa ikiwa ni sawa na asilimia 74 huku Dar es Salaam iliyoandikisha kwa asilimia 89 ikiwa kinara ikifuatiwa na Pwani iliyoandikisha kwa asilimia 86, Tanga kwa asilimia 81, Mtwara kwa asilimia 80 na Lindi kwa asilimia 77.

Mhe. Jafo anaendelea kusema kuwa kwa upande wa Mikoa hakuna Mkoa ulioandikisha chini ya asilimia 50, hata hivyo Mkoa ulioandikisha chini zaidi ni Kigoma iliyoandikisha kwa asilimia 57, Kilimanjaro kwa asilimia 58, Arusha na Shinyanga kila mmoja ukiandikisha kwa asilimia 66.

Akifafanua kuhusu Halmashauri zilizofanya vibaya amesema hali ni mbaya kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambayo imeanikisha kwa asilimia 37 na kufuatiwa na Halmashauri ya Moshi na Korogwe ambazo  kila mmoja imeandikisha kwa asilimia 51.

Awali akitoa tathimini ya uandikishaji wa siku saba za mwanzo zilizoishia Oktoba 14,  Mhe. Jafo amebainisha  wapigakura walioandikishwa walikuwa milioni 15.5 ambao ni sawa na asilimia 68 ya lengo la kuandikisha wapigakura milioni 22.9 huku Mkoa wa Pwani uliongoza kwa kuandikisha kwa wastani wa asilimia 80, ikifuatiwa na Dar es Salaam kwa asilimia 77, Tanga ikiandikisha kwa asilimi 76, Mtwara na Lindi kila mmoja kwa asilimia 75.

Pia Kilimanajro ilishika mkia kwa kuandikisha wastani wa asilimia 48, ikifuatiwa na Kigoma kwa asilimia 53 Arusha kwa asilimia 59.

Wakati huohuo Mhe. Jafo amesema anawashangaa  wanasiasa wanaobeza kuwa uchaguzi na uandikishaji wa mwaka huu ni wa kusuasua na kuwataka kuacha upotoshaji na kujikita kwenye takwimu za ukweli ambapo uandikishaji ulikuwa mkubwa ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2014.

Amefafanua kuwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita, Watanzania zaidi ya milioni 11.49 (11,491,661) ikiwa ni asilimia 62 ya makadilio ya kuandikisha watu 18,587,742 walijiandikisha katika uchaguzi uliofanyika Desemba 14 mwaka 2014

Aidha, Mhe.Jafo amesisitiza kuwa watumishi wa umma hawalazimishwi kujiandikisha na kuwa hakuna hatua au adhabu yeyote  itakachochukuliwa kwa asiyejiandikisha na kuwa kinachofanyika ni kuhamasisha ili kuhakikisha demokrasia inachukua mkondo wake.

“ Kanuni za uchaguzi ziko wazi, hakuna mtu analazimishwa ila kinachotakiwa kufanyika ni watu kuhamasishwa. Tumeona sehemu zingine kuna maandamano ya pikipiki au magari ya kuhamasisha na hili jambo jema kwa nchi yetu, kujiandikisha kunampa fursa mtu ya kwenda kuchagua kiongozi, ukikosa fursa hiyo unaweza baadaye kulalamika umechangua kiongozi ambaye haleti maendeleo” Amesisitiza Mhe. Jafo

Akizungumzia kuhusu “clip za  video” zinazotembea kuwa asiojiandikisha atakosa fursa zingine za maendeleo,  amesisitiza kuwa kanuni  ziko wazi, suala la kujiandikisha na kupiga kura ni hiyari na  mambo haya siyo maelekezo ya Ofisi ya TAMISEMI, watu wanatakiwa kuambiwa faida za kujiandikisha na kupiga kura kwa mustakabali wa maendeleo  ya Taifa.

Hata hivyo, Mhe. Jafo amefafanua kuhusu taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya  watumishi wa Jiji la Dodoma kulazimishwa kujiandikisha  na kusema kuwa lengo lilikuwa ni kuwahamaisha watumishi kwasababu wao wanafanya kazi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo ni vyema wakawa mstari wa mbele kujiandikisha ili kuwahamasisha wengine kujiandikisha.


Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Mawaziri Wa Sekta Za Mazingira, Maliasili Na Utalii Nchi Za SADC

0
0
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Mkutano huo utafanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuanzia tarehe  21 hadi 25 Oktoba, 2019.

Madhumuni ya mkutano huu ni pamoja na kuangalia mwenendo wa hali ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi; kubainisha utekelezaji wa mikakati ya hifadhi na usimamizi wa mazingira; kupitia Mkakati wa SADC wa Uchumi wa Bahari (SADC Strategy on Blue Economy); na kutathmini maendeleo katika sekta za misitu, wanyamapori na utalii.

Mkutano wa Mawaziri wa sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii utatanguliwa na mikutano ya wataalam wa sekta ya wanyamapori utakaofanyika tarehe 18 hadi19 Oktoba, 2019. Aidha, Mkutano  wa Makatibu Wakuu wa sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii utafanyika tarehe 21 hadi 24 Oktoba, 2019. Mikutano hii miwili itajadili na kuandaa mapendekezo yatakayowasilishwa katika kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 25 Oktoba, 2019 kwa maamuzi na maelekezo.

Mkutano wa Mawaziri  unatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ijumaa Oktoba 25, 2019, ukumbi wa AICC, Arusha. Aidha Mkutano wa Makatibu Wakuu unatarajiwa kufunguliwa na Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii, Oktoba 21, 2019 katika ukumbi wa AICC, Arusha.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 wanachama wa SADC wanaotekeleza Mkakati wa SADC kuhusu Usimamizi wa Sheria na Vita Dhidi ya Ujangili wa Wanyamapori (SADC Law Enforcement and Anti-poaching). Maeneo mengine yanahusu Programu za uhifadhi yaliyovuka mpaka wa nchi moja hadi nyingine kwenye maeneo ya misitu, uvuvi, mazingira na mabadiliko ya tabianchi; utalii; ukuzaji viumbe maji na Mkakati wa Ubora wa Afya wa wanyama wa majini (SADC Transfontiers Conservation Areas; forestry; fisheries; environment and climate change; tourism;  regional Aqua-culture strategy and action plan; and SADC Aquatic Animal Health Strategy) pamoja na Programu ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi (Environment and Climate change Program).

Ili kufanikisha mkutano huu sekta ya habari ni muhimu kuhabarisha umma kuhusu masuala yote muhimu yatakayojadiliwa hususan yanayohusu maendeleo ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa nchi wanachama. Serikali inatoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na Mikoa ya jirani kuchangamkia fursa za kibiashara kutokana na kuwepo kwa wageni hao.

Mkutano wa Mawaziri wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii ni muendelezo wa mikutano itakayofanyika nchini katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Tanzania ni Mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

Mapema mwezi Agosti mwaka huu, Serikali ya Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikabidhiwa na kupokea rasmi jukumu la  uenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ni moja kati ya jumuiya za  kikanda katika bara la Afrika. Jumuiya hii iliundwa kwa dhumuni la kuimarisha ushirikiano katika nyanja za uchumi,  ulinzi , siasa na usalama.  Jumuiya hii inaundwa na  nchi wanachama 16 ambazo ni: Angola, Botswana, Comoros, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.

Imetolewa na:

Constantine Kanyasu
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
16 Oktoba, 2019

Wadau Wa Uchaguzi Wakutana Jijini Dodoma Katika Maandalizi Ya Uboreshaji Daftari La Kudumu La Wapiga Kura.

0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi na wadau mbalimbali wa Uchaguzi wamekutana jijini Dodoma kujadili juu ya uboreshaji wa Daftari lakudumu la wapiga kura ambapo imeeleza uboreshaji katika awamu hii utafanyika kwa kutumia teknolijia ya kieletroniki ya Biometriki (BVR) kama ilivyokuwa mwaka  2015..

Akiongea katika  mkutano huo wa wadau wa uchaguzi mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi,Jaji Semistocles Kaijage  amesema Teknolojia hiyo itachukua taarifa za mtu za kibaiolojia na kuzihifadhi katika kanzidata kwaajili ya utambuzi ,na ndio iliyotumika kuandikisha wapigakura mwaka 2015.

Pia amesema , uboreshaji wa safari hii hautohusisha wapiga kura wote waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga mwaka 2015 bali litahusisha wapiga  kura wapya ambao wametimiza umri wa miaka 18 na wale ambao watatimiza umri wa miaka 18 siku ya uchagauzi mkuu wa mwaka ujao 2020.

Kwa upande wake Mkurugenzi  wa uchaguzi Wilson Charles amesema kwa mujibu wa kifungu cha 10  cha sheria ya taifa ya uchaguzi sura  ya 343 na kifungu cha 15 cha sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa sura ya 292 inasema ili mtu aweze kuandikishwa kuwa mpiga kura anapaswa kuwa raia wa Tanzania.

Pia amebainisha ili mtu aweze kuandikishwa lazima awe na umri wa miaka 18 au zaidi au atatimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya uchaguzi.

Hata hivyo amesema kuwa mtu anaweza kukosa sifa za kuandikishwa kama amethibitisha kuwa ana ugonjwa wa akili ,amehukumiwa adhabu ya kifo,anatumikia kifungo cha zaidi ya miezi sita ,amezuiliwa kujiandikisha kuwa mpiga kura na sheria za uchaguzi au sheria nyingine kwa makosa yanayohusiana na uchaguzi au hatakuwa ametimiza umri wa kupiga kura ifikapo siku ya uchaguzi.

Katika hatua nyingine amesema uzoefu inaonyesha kuwa katika chaguzi ndogo vyama vimekuwa havipeleki malalamiko yao kwenye kamati za maadili na badala yake vimekuwa vikipeleka malalamiko yao kupitia vyombo vya habari hali ambayo hupelekea malalamiko yao kutofanyiwa kazi na kamati za maadili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mara baada kukamilika kwa zoezi la kuapisha viongozi hao Kamishna wa Tume ya taifa ya uchaguzi Asina Omary amesema zoezi hilo ni la kisheria hivyo ni lazima taratibu zote za kisheria zifuatwe ili kulifanikisha   huku akizungumzia umuhimu wa uboreshaji wa Daftari hilo la wapiga kura.

Mkurugenzi wa idara ya usimamizi Tume ya taifa ya uchaguzi Anseem Mwampoma amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi wanaowataka.

Ikumbukwe kuwa,Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekamilisha uboreshaji wa Daftari awamu ya Kwanza katika mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Manyara,Simiyu,Mara,Mwanza,Geita,Shinyanga,Kagera  na Kigoma .

Hivyo kwa sasa zoezi hilo linaendelea katika mkoa ya Tabora,Katavi na Rukwa  na litaendelea mikoa mingine ikiwemo Dodoma.
Mwisho

As Roma yawa timu ya kwanza ya Ulaya kufungua Twitter ya Kiswahili

0
0
Timu ya soka ya 'As Roma' ya nchini Italia imekuwa klabu kubwa ya kwanza barani Ulaya kuanzisha ukurasa wake katika mtandao wa Twitter kwa lugha ya Kiswahili.

Ukurasa wa klabu hiyo mashuhuri nchini Italia na barani Ulaya ambayo ilianzishwa mwaka 1927 utakuwa ukiandika habari zake kwa lugha adhimu ya Kiswahili.

Ukurasa huo wa lugha ya Kiswahili ulizinduliwa rasmi jana, na inaaminika lengo kuu la 'As Roma' ni kuwafikia mamilion ya watu wanatumia lugha ya Kiswahili katika eneo la Afrika Mashariki na maeneo mengine duniani.

Baada ya kuzinduliwa ukurasa huo, wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili katika maeneo mbalimbali wameonekana wakipongeza hatua hiyo na kuanza kutoa maoni yao katika ukurasa huo. 

Msimamizii wa ukurasa huo ameandika haya baada ya kuzinduliwa ukurasa huu: Ahsante kwa upendo na ushirikiano ambao mmetuonyesha tangu tumezindua ukurasa huu rasmi. Ni dhahir kwamba, kwa pamoja tutaendelea kushirikiana na kufurahia pamoja hapa hapa kwa lugha ya Kiswahili.
Itakumbukwa kuwa katika mkutano wake mwezi uliopita huko jijini Dar es Salaam Tanzania Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ilipitisha pendekezo kuwa Kiswahili kianze kutumika kama lugha ya nne katika jumuiya hiyo.

Dawa Komesha Ya Maumbile Madogo , Nguvu Za Kiume Na Magonjwa Mengineyo

0
0
*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*📌SUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
📍Kuishiwa kwa nguvu za kiume 📌/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*📞+255788468114*

Rais Magufuli Amfuta Kazi Kamanda wa TAKUKURU Mtwara

0
0
Rais Magufuli amemtumbua Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Mtwara, Stephen Mafi pa kutokana na kukosekana kwake katika mkutano wa hadhara alioufanya katika Kijiji cha Chukuku kilichopo Masasi mkoani humo.

Akiwa Chukuku, wananchi walimueleza Rais kuhusu madai yao dhidi ya fedha wanazowadai vingozi wa chama cha msingi Amcos baada ya viongozi hao kutoweka na fedha hizo.

Baada ya kupata malalamiko hayo, Rais Magufuli alimuita Kamanda wa Polisi wa mkoa ambaye alieleza kuwa wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa.

Jibu hilo lilionekana kutomfurahisha Rais Magufuli ndipo alipotoa siku tano kwa kamanda huyo kuhakikisha viongozi hao wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia.

“RPC nakupa ndani ya siku tano waliokula fedha za wananchi wa hapa wakamatwe na wapelekwe mahakamani, mshirikiane na Takukuru, kamanda wa Takukuru mkoa yuko wapi,” aliuliza Rais Magufuli bila kupata majibu

Kufuatia ukimya huo aliomba simu yake kutoka kwa wasaidizi wake ambapo alipewa na kumpigia Brigedia Jenerali Mbungo na kumuelekeza kumuondoa kamanda huyo wa mkoa na kumtaka ampeleke mtu mwingine kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.


“Brigedia Jenerali, nipo hapa Masasai, nimemuita Kamanda wako wa TAKUKURU hapa hayupo, nimemfuta kazi hapahapa. Sasa nakuagiza leo hii uteue Kamanda mwingine, aje hapa asaidizane na RPC kuwakamata hao wezi na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.

“Hatuwezi tukavumilia huu ujinga na siwezi kukubali wananchi wangu wakanyanyasika. nataka utekeleze mara moja,” alisema Magufuli wakati akitoa maelekezo hayo kwa Brigedia Jen. Mbungo kupitia njia ya simu ya mkononi.

Tiba Bora Ya Nguvu Za Kiume, Kisukari , Mvuto Wa Mapenzi Nk

0
0
Je wewe ni mwathilika wa punyeto? 
Je umesumbuliwa na matatizo ya KISUKARI, PRESHA, TUMBO KUUNGULUMA NA KUJAA GESI, NGIRI, MAUMIVU YA MGONGO NA KIUNO, MIGUU KUWAKA MOTO AMA KUFA GANZI, KINYESI KUWA KIGUMU AMA KUWA KAMA CHAMBUZI   mpaka ikapelekea upotevu ama upungufu wa nguvu za kiume na maumbie kuwa madogoa kama ya mtoto mdogo?

MIHINI    nidawa ya kiasili iliyotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu (1) huimarisha misuli  uliolegea wakati wa tendo la ndoa
2.huchelewesha kufika kileleni takiribani dk 20-45 kwa tendooja na kukufanya uwe na ham ya kurudia tendo zaidi ya maratatu (3) bila ham kuisha wara kuhisi kuchoka
3.huzalisha viini vya uzazi ilo vitoke kwa speedi inayotakiqa wakati wa tendo (manii)

YOLINA   hurefusha  maumbire madogo  na kuwa makubwa ; dawa hii niyamitishamba hainamadhara kwa mtumiaji

PATA DAWA YA KUTIBU MATATIZO YA , Kisukari, pumu, presha, miguu kuwaka moto, na kufa ganzi, vidonda vya tumbo, tumbo kuunguluma na kujaa gesi, maumivu ya mgongo na kiuno, kuondoa makovu, mabaka, na chunusi mwilini, 

Je umeachwa na mume, mke, mchumba, mpenzi,? Sululisho kwa DR KITINGA

 NAPATIKANA DAR ES  SALAAM
KAMA HUNA UWEZO WA KUFIKA OFISINI HUDUMA HII INAKUFIKIA POPOTE ULIPO
call +255 758 840 958
Watsap +255 653 182 109

Tangazo Muhimu Toka Sekretarieti Ya Ajira

0
0
TANGAZO MUHIMU TOKA SEKRETARIETI YA AJIRA
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Katibu wa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwaatarifu waombaji kazi wa kada za “Geologist” II na “Engineer” II (Mineral Processing)  zilizotangazwa kwa niaba ya Tume ya Madini Tanzania (TMC) kuwa kada ya “Geologist” II itafanya usaili wa Mchujo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE) mnamo tarehe 18/10/2019 saa 3:00 Asubuhi katika Ukumbi wa LECTURE THEATRE C na tarehe ya usaili wa Mahojiano  ni tarehe 21/10/2019 saa 1:00 Asubuhi Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma jengo la Utumishi Kivukoni.

 Aidha kada ya “Engineer” II (Mineral Processing) haitakuwa na usaili wa Mchujo na usaili wa Mahojiano utafanyika tarehe 21/10/2019 saa 1:00 Asubuhi Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma jengo la Utumishi Kivukoni.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
15/10/2019

 👉Bonyeza hapo chini  kuendelea kupata matangazo mbalimbali ya Ajira,Nafasai za Kazi

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/jobs
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images