Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Barabara ya Segera - Mkomazi yafunguliwa baada ya Mafuriko Kupungua

$
0
0
Barabara ya Segera - Mkomazi ambayo ilikuwa imefungwa tangu jana kutokana na barabara hiyo kujaa maji eneo la Mandera, imefunguliwa leo baada ya maji kupungua na Tanroads kuifanyia marekebisho.


Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Kimetangaza Nafasi 62 za Ufadhili ( Scholarships) kwa Undergraduate na Post Graduate.....Mwisho ni mwezi wa 11

$
0
0

UDSM YATANGAZA FURSA 62 ZA UDHAMINI
( SCHOLARSHIPS)

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬
Chuo kikuu cha Dar es Salaam Kimetangaza Fursa Za Udhamini Wa Masomo(Scholarships) 62 Kwa Mwaka wa masomo 2019/2020.

👉 Nafasi 52 ni kwa Undergraduate

👉 Nafasi 10 ni kwa Post Graduate  (at the Master’s Level)
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

Deadline: November 03,2019

Bonyeza Hapo Chini Kujua Zaidi

👇👇👇👇👇👇👇👇

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne October 15

JPM Anamuenzi Nyerere Kwa Vitendo-RC Mtaka

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema serikali ya awamu ya tano chini ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe inamuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo hususani katika kuendeleza kazi nzuri alizozifanya.

Mtaka ameyasema hayo Oktoba 14, 2019 katika Kongamano la Kitaifa la Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere lililofanyika Oktoba 14, 2019 Mjini Bariadi, likiwashirikisha viongozi wa Serikali, wananchi na baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu, UVCCM Simiyu, UVCCM kutoka mikoa mbalimbali nchini na ngazi ya Taifa(makao makuu).

“Mwalimu amepewa heshima ya kuenziwa ninyi  kizazi hiki mnashuhudia kwa macho, wapo watu wanasimuliwa tu kuwa ile barabara inaitwa ‘Nyerere road’, lakini hamkuwepo; leo mnajua kwamba hifadhi fulani inaitwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, mnasikia Mradi mkubwa wa kufua umeme wa maji wa  J.K. Nyerere,  Mhe.Rais amemheshimisha Mwalimu kwa vitendo,” alisema Mtaka

“Mwalimu aliamini katika Watanzania kufanya shughuli za kiuchumi  ikiwemo kilimo,  ufugaji na uvuvi  na akataka waongeze thamani katika shughuli hizo; ndiyo maana Mhe Rais ameanza kufufua viwanda vya nguo, viwanda vya korosho, viwanda vya kahawa na mengine aliyoyaacha Mwalimu, “ aliongeza Mtaka.

Aidha, Mtaka amemzungumzia Mwalimu Nyerere kuwa alikuwa kiongozi wa karne mwenye utu, maono na msimamo ambaye alijua wapi anapotoka na anapotakiwa kwenda kama kiongozi na aliyewaheshimisha Watanzania.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa Vijana wa UVCCM  kuwaeleza ukweli na kuwashauri viongozi vijana ndani ya Serikali kufanya kazi zao kwa kuzingatia misingi ya uongozi na kuepukana na tabia ya kuweka urasimu wa kufikika na watu , ili viongozi hao watekeleze vema wajibu wao wa kuwatumikia wananchi na kumsaidia Mhe. Rais Magufuli katika majukumu aliyowapa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo amewataka vijana kumuenzi Hayati  Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere kwa kufanya kazi kwa bidii, ili wajiletee maendeleo kwa kuwa Mwalimu aliamini kuwa kazi ni kipimo cha uhai.

Naye Kaimu Katibu Idara ya Mahusiano ya Kimataifa na Vyuo Vikuu, Bi Asha Feruz amesema kwa kuwa vijana wengi wamezaliwa wakati Hayati Baba wa Taifa,Mwl. Julius K. Nyerere akiwa amefariki ni vema vijana hao wakasoma  vitabu, ili wajue historia ya mwalimu na waasisi wengine wa Taifa la Tanzania.

Mmoja wa Wajukuu wa Mwalimu Nyerere Chifu Edward Magige amesema pamoja na Watanzania kuendelea kukumbuka na kuenzi mambo mazuri yaliyofanywa na Hayati Mwalimu Nyerere ni vema pia wakaukumbuka mchango wa Mama Maria Nyerere katika kazi zilizofanywa na mwalimu.

Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe. Njalu Silanga ametoa wito kwa Vijana hapa nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura, ili waweze kuitumia vema haki yao kuchagua viongozi bora ikiwa ni namna mojawapo ya kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuchagua viongozi watakaosimamia misingi ya uongozi aliyoiweka.

MWISHO

Lusinde: Kijana Mdogo,una miaka 22,huna kazi ya uhakika,huna mshahara lakini una mademu wanne ,wewe ni tatizo

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mbunge wa jimbo  la Mtera mkoani Dodoma Livingstone Lusinde amewataka vijana kote nchini kujitathimini na kuachana na masuala ya anasa ikiwa ni pamoja na Umalaya na badala yake wawajibike katika kazi za kuwaletea maendeleo. 

Mhe.Lusinde amesema hayo jijini Dodoma akiwa mgeni Rasmi katika kongamano la  Vijana Mkoa wa Dodoma lililolenga kujadili mchango wa  Baba wa Taifa Mwl.Julus  Kambarage Nyerere ikiwa  taifa la Tanzania likifanya kumbukizi ya Miaka 20 tangu afariki dunia  mwaka 1999. 

Mbunge huyo amesema vijana wa siku hizi wamekuwa wakifanya masuala ya Umalaya na ukahaba na mambo mengine ya anasa wakiwa wadogo na kushinda baa badala ya kuwajibika katika kazi hivyo wanapaswa kubadilika. 

“Kijana Mdogo,una miaka 22,huna kazi ya uhakika,huna mshahara lakini una mademu wanne ,wewe ni tatizo,shida ni wewe,piga hela zote ulizotoa Guest na chipsi ni mtaji.Wewe ni tatizo kubwa,huwa ninaangalia sana mitaala ya elimu,wakati mwingine watoto tunawafundisha ujinga.Alisema. 

Mhe.Lusinde amesema kuna baadhi ya mambo vijana wanatakiwa kujitathimin na kufanya mambo makubwa na kwa kasi na kuacha kupoteza muda kupoteza fedha kwa kujiunga internet na kuchati kwenye Magroup ya Whatsaap yasiyokuwa na tija kwani ni kupoteza muda na badala yake watumie miundombinu iliyoachwa na   Mwalimu Nyerere katika kuwaletea Maendeleo. 

“Lazima kuna baadhi ya vitu unapaswa kugundua na kung’amua,lazima miundombinu tuifanyie kazi katika kutuletea maendeleo,kuna mambo mengine yanahitaji haraka,mtu anakwambia polepole ndio mwendo na wewe unakubali.huna shughuli,huna mshahara lakini una simu tatu unachati group hili hadi lile,wewe ni Poyoyo.Amesema. 

Hata hivyo,Mhe.Lusinde amewaasa  Vijana kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kupambana na rushwa kwani rushwa hunyonya haki ya mtu. 

Aidha,Mhe.Lusinde amewataka vijana kujiandaa mapema pindi wanapotaka kufanya maendeleo na akatolea mfano mwanafunzi anayefaulu vizuri mtihani ni Yule aliyejiandaa mapema katika  na kudai kuwa ng’ombe hanenepi siku ya mnada. 

Kwa upande wake katibu wa  Vijana mkoa wa Dodoma Joel Makwaia  amesema Mwl.Nyerere alikuwa kiongozi Mzalendo wa Taifa na alijitolea kwa hali na mali ili kuhakikisha taifa linasonga mbele.

Serikali Kulipa Mil 315.1 Za Wakulima Wa Muzia Amcos

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Rukwa
Serikali imetangaza dhamira yake ya kuwalipa wakulima 156 wa mahindi jumla ya Shilingi 315,118,510 kutokana na kuzulumiwa na mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Ndg Linus Kalandamwazye.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ametoa kauli hiyo tarehe 13 Octoba 2019 wakati akizungumza na wanachama wa Muzia Amcos Wilayani Kalambo wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Rukwa.

Malipo hayo yatawahusu wakulima wa Tarafa ya Mwimbi yenye kata nne ambazo ni Mambwe Kenya, Ulumi, Mkombo na Mwazye kutokana na kupima mahindi yao zaidi ya Tani 622.679 kwenye Chama cha Muzia Amcos kilichopewa uwakala na serikali wa kununua mazao kwa wakulima tarehe 8 Agosti 2017 kwa makubaliano ya kulipwa ndani ya wiki tatu kutoka tarehe ya kupimwa lakini hawakulipwa mpaka sasa.

“Kesi ikiwa mahakamani serikali haiwezi kuingilia badala yake wakati tunaendelea na kesi hiyo ninaziagiza taasisi zangu tatu kuchanga fedha kwa ajili ya kuwalipa wakulima hao” Alikaririwa Mhe Hasunga

Alisema wanaotakiwa kuchanga fedha hizo kwanza ni Wizara ya Kilimo kwa kushindwa kulishughulikia jambo hilo kwa wakati ili wakulima hao waweze kulipwa fedha zao.

Ameiagiza pia Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuchanga fedha hizo kwani wao ndio wasimamizi wa Vyama vya Ushirika lakini kwa kipindi chote wameshindwa kushughulikia changamoto hiyo ya wakulima.

Kadhalika, Mhe Hasunga Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula kuchangia fedha hizo.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli haina dhamira ya kuwadunisha na kuwafedhehesha wananchi badala yake imejipambanua kuwanufaisha wakulima katika kilimo.

Alisema kuwa serikali imeamua kuwalipa fedha hizo wakulima ili kuendelea na uzalishaji bora wa mazao ya kilimo lakini kesi itakapomalizika serikali itazidai fedha hizo.

Mhe Hasunga amemuagiza Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Rukwa kupanga vizuri madai ya wakulima hao huku akisisitiza kutoingizwa majina mapya (Majina Hewa) yasiyohusika na madai ya fedha hizo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe Joachim Wangabo amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kwa kukubali kulivalia njuga jambo hilo kwa kuwalipa fedha hizo wakulima kwani kufanya hivyo kutarahisisha wakulima hao kuendelea na uzalishaji wa mazao katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020.

Amesema kuwa maamuzi hayo ya wizara kuamua kuwalipa wakulima huku taratibu zingine za kisheria ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua Mwenyekiti huyo zikiwa zinaendelea zimeibua ari na nguvu mpya katika kilimo.

Awali, akisoma taarifa ya malalamiko ya kutapeliwa fedha hizo katibu wa chama cha MUZIA AMCOS Ndg Geofrey Mbati amesema kuwa pamoja na kupeleka malalamiko katika maeneo mengi lakini ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano wa karibu katika kipindi chote cha kutafuta muarobaini wa malipo ya wakulima.

Alisema kuwa miongoni mwa maoni ya wakulima ilikuwa ni ombi la kupatiwa fedha hizo kwa ajili ya kuwanusuru kutokana na kadhia hiyo ya muda mrefu iliyopelekea kushindwa kulipa ada za wanafunzi shuleni, kushindwa kuwekeza tena kwenye kilimo pamoja na kushindwa kumudu gharama za maisha hali iliyopelekea kuishi maisha ya kifukara.

MWISHO

Waziri Biteko Akutana Na Wawekezaji Kujadili Changamoto Za Makaa Ya Mawe

$
0
0
Na Tito Mselem, Mwanza
Waziri wa Madini Doto Biteko amewatoa wasiwasi Wawekezaji wa Viwanda vinavyotumia Makaa ya Mawe na kuieleza Kampuni inayochimba Makaa ya Mawe ya TANCOAL kuwa hairuhusiwi kuongeza bei kiholela badala yake inatakiwa kuuza kulingana na bei elekezi iliyopangwa na serikali.

Kauli hiyo ilitolewa Septemba 15, 2019 na Waziri Biteko baada ya kukutana na wawekezaji wa Viwanda vya Saruji na Vigae kujadili changamoto za Makaa ya Mawe katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza.

Katika Kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Biteko, kilihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa huduma za Leseni wa Tume ya Madini Mhandisi, Yahaya Samamba, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza Fredy Mahobe, Afisa Kodi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Venance Kasiki pamoja na wawekezaji wa viwanda vya Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company pamoja na Lake Cement Ltd.

Kampuni hizo tatu za Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company pamoja na Lake Cement Ltd. zinatumia kiasi kikubwa cha Makaa ya Mawe kwa matumizi ya kuyeyushia Mawe kwa ajili ya uzalishaji wa saruji na vigae ambapo zaidi ya nyuzi joto 2000 zinatakiwa ili kuyeyusha Mawe hayo ziliomba kukutana na Waziri wa Madini ili kueleza changamoto zao.

Hatua hiyo ilikuja kutokana na wanunuzi wakubwa wa makaa yam awe nchini kuwa na mvutano wa bei ya Makaa ya Mawe kati yao na mzalishaji wa Makaa hayo kampuni ya TANCOAL anayozalisha Mawe hayo katika eneo la Kitai Mkoani Ruvuma katika Mgodi wa Ngaka.

Mvutano huo ulianza mara baada Serikali kupitia Tume ya Madini Kuitaka Kampuni ya TANCOAL Kulipa deni lake la kiasi cha shilingi Bilioni 23.9 ambazo zilitokana na malimbikizo ya kutolipa mrabaha wa mauzo na usafirishaji wa Makaa hayo pamoja na adhabu ya asilimia 50 kuanzia Septemba 2011 mpaka Juni 2019.

Aidha, Waziri Biteko amezitaka kampuni hizo kuendelea na uzalishaji wa Saruji na Vigae bila kuhofia kupandishiwa bei kwa maana bei hazitapanda kiholela, ameeleza kuwa, Makaa ya Mawe kote nchi yatauzwa kulingana na bei iliyo elekezwa na serikali.

Imeonekana kwamba, deni la kampuni ya TANCOAL kuwa kubwa, kampuni hiyo imeonesha nia ya kupandisha bei kwanye Makaa ya Mawe ili kufidia deni wanalodaiwa na Serikali.

Kwa upande wake, Mdhibiti wa Fedha wa Tanga Cement, Issac Lupokela alimweleza Waziri Biteko kuwa, kitendo cha kupandishiwa bei na kampuni ya TANCOAL ni kama wanawaadhibu kutokana na ukweli kwamba hakuna mbadala wa kununua kwa wingi sehemu ingine makaa hayo baada ya serikali kusitisha uingizwaji wa Makaa ya Mawe nchini.

“Kipindi cha Nyuma tulikuwa tunanunua Makaa ya Mawe kutoka Afrika ya Kusini kwa kuwa Makaa yaliyokuwa yanazalishwa nchini hayakuwa na kiwango cha kutosha hivyo baada ya serikali kusitisha uingizwaji wa Makaa ya Mawe nchini, tulilazimika kushirikiana na kampuni ya TANCOAL ili kutoa elimu ya namna bora ya uzalishaji wa Makaa hayo, leo tunashangaa wameamua kutupandishia bei,” alisema Lupokela. 

LIVE: Rais Magufuli katua Jimboni kwa Nape Nnauye

$
0
0
LIVE: Rais Magufuli katua Jimboni kwa Nape Nnauye

CHADEMA watoa Kauli kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hawatasusia uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Novemba 24 mwaka huu na amewataka viongozi, wanachama na Watanzania kuhamasishana kujiandikisha.

Amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi ambapo ameeleza  uchaguzi huo ndio unawaleta viongozi wanaokwenda kutatua changamoto za wananchi hivyo kuacha serikali ifanye uamuzi ni kosa.

“Tunapaswa kuweka kando tofauti zetu, twendeni kwa wingi tukajiandikishe ili tushiriki kwenye uchaguzi huu muhimu,” amesema Mbowe

Ameendelea kwa kusema wananchi kusuasua kwenda kujiandikisha ni matokeo ya kile alichodai kuwa ni serikali  kuweka msisitizo katika kuwazuia watu wa upinzani kufanya mikutano ya kisiasa.

“Ni makosa makubwa na aibu kususia. Kwa muda wa siku tatu zilizoongozwa, viongozi wote wa kada zote, wahamasishane watoke kwa wingi kwenda kujiandikisha, hatuna sababu za kususia kwani tutakuwa tumesusia maisha yetu,” amesisitiza Mbowe

“Tunakwenda kushiriki uchaguzi huu na tutashinda, hatutakuwa woga na haya ni mapambano ya kisiasa, tutatumia nguvu za umma kuhakikisha tunashinda uchaguzi huu.”

Madson Property Limited Inakuletea Mkopo Wa Viwanja Usio Na Riba Wala Dhamana

$
0
0
MADSON PROPERTY LIMITED
inakuletea Mkopo wa Viwanja usio na riba wala dhamana
✅Maeneo yapo GOBA, BOKO, BAGAMOYO, KIBAHA NA VIGWAZA.

📌Goba kinzudi- 35,000
📌Goba njia nne- 38,000
📌Goba mpakani- 32,000
📌Goba Kulangwa-30,000
✅ BOKO viwanja vipo karibu na St Joseph University- 32,000
✅KIBAHA- 11,000
✅BAGAMOYO-13,000
✅ Vigwaza-mashamba 2M kwa hekari moja.
 
NB: Bei hizo ni kwa sqm moja na Viwanja vyetu vimepimwa na Hati zipo tayari.
 
Karibuni ofisi zetu zipo Mwenge Tower Opposite na Mlimani city

Contact: 0718 65 71 89

Breaking News: NECTA yatangaza matokeo ya Darasa la Saba 2019. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 3.78

$
0
0
Matokeo ya darasa la saba 2019, yametangazwa. NECTA imeeleza ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78. Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369. Pia Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwemo udanganyifu.

Dk. Msonde amesema mwanafunzi aliyeongoza Kitaifa ni Grace Manga kutoka Shule ya Msingi Graiyaki Mara, akifuatiwa na Francis Gwagi kutoka Shule ya Msingi Paradise ya Geita.

Amesema kuwa aliyeshika nafasi ya tatu ni Loi  Kitundu kutoka Shule ya Msingi Mbezi ya Dar  es Salaam, na Victor Godfrey kutoka Graiyaki ameshika nafasi ya nne.

"Katika ufaulu wa masomo, somo la Kiswahili, Kiingereza na Sayansi katika mtihani huo ufaulu wake umepanda na somo la Hisabati umeshuka,"

Wanafunzi 10 Bora Kitaifa | Shule Kumi Bora Kitaifa | Mikoa 10 Bora Kitaifa Matokeo Darasa la Saba 2019

$
0
0
Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ambako mikoa ya kanda ya ziwa imeonekana kuongoza .

Katika matokeo hayo yaliotangazwa leo Jumanne Oktoba 15, 2019 nafasi ya kwanza hadi ya 10 katika orodha ya wavulana waliofanya vizuri zimeshikwa na wanafunzi kutoka katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Kutangaza Watakaopata Mikopo Kesho Kutwa Alhamisi

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema itatangaza orodha ya kwanza ya majina ya wanafunzi walioomba na kupangiwa mikopo Alhamisi, Oktoba 17 mwaka huu.

Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa kazi ya uchambuzi wa maombi ya mikopo yapatayo 55,444 ya wanafunzi ambao wamepata udahili katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake jijini Dar es salaam leo (Jumatatu, Oktoba 14, 2019), Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema wanafunzi watakaopangiwa mikopo wataweza kupata taarifa zao kupitia akaunti zao kwenye mtandao wa taasisi hiyo.

Pamoja na kutangaza orodha hiyo, Badru amesema HESLB pia imeamua kutoa fursa kwa waombaji 4,794 ambao bado hadi sasa hawajakamilisha maombi yao kukamilisha kwa kuambatisha nyaraka muhimu mtandaoni.

Kuhusu malengo ya mwaka huu wa masomo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB amesema Serikali imetenga TZS 450 bilioni ambazo zitawanufaisha jumla ya wanafunzi 128,285. Kati yao, wanafunzi zaidi ya 45,000 watakuwa ni wa mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ni wanufaika wa mikopo wanaoendelea na masomo. Bajeti ya mwaka wa masomo 2018/2019 ilikuwa TZS 427.5 bilioni na iliwanufaisha jumla ya wanafunzi 123,329.

Tanzania Inatarajia Kupata Dola Za Marekani Milioni 500 Kwa Ajili Ya Mradi Wa Elimu

$
0
0
Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington Dc
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amefanya mazungumzo na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayewakilisha nchi za Afrika Bi. Anne Namara Kabagambe, Mjini Washington DC, Marekani.

Mazungumzo hayo yalilenga katika kubadilishana uzoefu juu ya utekelezaji wa Sera mbalimbali za fedha na namna uchumi wa Dunia unavyoendeshwa.

Katika mazungumzo hayo baadhi ya miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa(SGR), ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha umeme la mto Rufiji, mradi wa elimu,na miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), ilijadiliwa. 

Dr. Mpango alieleza dhamira ya Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuinua kiwango cha elimu, kwa kutafuta fedha zaidi na mikopo ya masharti nafuu ambayo itaelekezwa kwenye elimu.

‘’Katika Mradi wa Elimu unaotarajiwa kuwasilishwa Benki ya Dunia mwezi Novemba, 2019, tunatarajia kupata dola za Marekani milioni 500, na nimemuomba Bi. Anne Namara Kabagambe azidi kusisitiza ili Taifa liweze kupatafedha hizi kwa wakati, na tunaamini kwamba fedha hizo zitaidhinishwa na Benki ya Dunia kama tunavyotarajia.”Alisisitiza Dkt Mpango.

Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango alisema pamoja na miradi ya Elimu, Sekta  ya nishati ya umeme pia ni muhimu katika kuinua uchumi wa nchi kwa sababu ukipatikana umeme wa kutosha utasaidia kwa vitendo agenda ya uchumi wa viwanda kwa kuongeza thamani ya mazao na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii nchini.

Aliiomba Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa zisaidie kwenye miradi ya mikubwa inayotekelezwa na Serikali hasa katika sekta ya umeme na miundombinu.

Aidha Dkt. Mpango alieleza kuwa hivi karibunii Benki ya Dunia iliipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 450 kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF, awamu ya tatu.

“Hivyo kupitia miradi miwili ya Elimu na TASAF, Tanzania inatarajia kupata dola za Marekani milioni 950”. Aliongeza Dkt. Mpango

Kwa upande wa Benki ya Dunia Bi. Anne Namara Kabagambe alielezea kufurahishwa na utekelezaji wa miradi inayofanyika Tanzania kwani alipata fursa ya kuona miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na miradi inayotekelezwa na TASAF, na kuelezea kuwa ni miradi ya mfano na kwa nafasi yake ataendelea kuitangaza miradi hiyo ili Tanzania iweze kupata fedha zaidi ya kutekeleza miradi hiyo.

Dkt. Mpango anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Dunia IMF ambapo amesema mikutano hiyo ni muhimu kwa kuwa nchi itapata fursa ya kuweza kujadiliana na Taasisi hizi za IMF na WB kuhusu  miradi wanayofadhili.

Aidha, kupitia mikutano hiyo vipaumbele vya nchi vitaelezwa na kupitia changamoto zilizopo kwa sasa, kutetea maslahi mapana ya Tanzania katika utekelezaji wa programu za maendeleo na mabadiliko ya kimfumo katika uendeshaji wa uchumi kutegemeana na mwenendo wa Dunia unavyokwenda,

 Alisisitiza kuwa nchi inapata uzoefu wa nchi nyingine wanavyotekeleza na kusimamia program zao na wao pia kuweza kuzieleza nchi nyingine namna ambavyo Tanzania inatekeleza programu mbalimbali za kimaendeleo.

Mwisho

Dawa Komesha Ya Maumbile Madogo , Nguvu Za Kiume Na Magonjwa Mengineyo

$
0
0
*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*📌SUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
📍Kuishiwa kwa nguvu za kiume 📌/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*📞+255788468114*

Waziri Jafo Aongeza Siku Tatu Uandikishaji Daftari La Orodha Wapiga Kura Serikali Za Mitaa

$
0
0
Na Oscar Job, Kisarawe
Waziri  wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameongeza siku tatu kwa wananchi kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 Mwaka huu.
 
Akizungumza kabla ya kujiandikisha Kijijini kwake Kimani,Kisarawe mkoani Pwani , Waziri Jafo alisema kuongezwa kwa siku tatu hizo kumetokana na sababu mbalimbali ambazo kimsingi zimesababisha wananchi kuikosa fursa hiyo.
 
Alisema kimsingi siku za uandikishaji huo zilizoongezwa kutoka leo hadi Oktoba 17, kumesabishwa na tatizo la mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali na hivyo kuleta shida kwa wananchi wengi kujiandikisha.
 
Aliitaja sababu nyingine kuwa ni pamoja na uwepo wa zoezi la wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, hali iliyoleta dhana  kwa baadhi ya wananchi kuwa kitambulisho cha mpiga kura kitawawezesha kupiga kura katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa.
 
“Kutokana na sababu hizo na kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 na matangazo ya Serikali Na 371,372,373 na 374 ya Mwaka 2019 Waziri mwenye dhamana na Serikali za mitaa ana mamlaka ya kutoa miongozo mbalimbali kuhusu uchaguzi wa  Serikali za Mitaa”  alisema Jafo
 
Alisema kutokana na kanuni hizo na changamoto zilizojitokeza Wizara yake imeona vyema kuongeza siku hizo tatu ili kuwapa nafasi wananchi kujiandikisha na hivyo kutumia fursa yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowataka.
 
Aidha alisema tangu kuanza kwa Oktoba 8 hadi Octoba 12 Mwaka huu wananchi zaidi ya Milioni 11 walikuwa tayari wamejiandikisha nchi nzima kushiriki uchaguzi huo huku akilitaja zoezi hilo kuwa lenye mafanikio makubwa ikilinganishwa na kipindi kingine chote.
 
Alisema kufuatia mabadiliko, ratiba ya uandikishaji wa orodha ya wapiga kura na matukio yanayohusu uandikishanji yatakuwa na mabadiliko fulani fulani ikiwemo kubandikwa kwa orodha ya wapiga kura litakalofanyika kuanzia Oktoba 18, utoaji wa pingamizi kuhusu uandikishaji wapiga kura litakalofanyika Oktoba 14 hadi 24.
 
Mabadiliko mengine ni pamoja na uamuzi kuhusu pingamizi litalofanyika kuanzia Oktoba 24 hadi 25,marekebisho ya orodha ya wapiga kura kuanziaa Oktoba 25 hadi 25 pamoja na ukataji wa rufaa dhidi ya uamuzi wa pingamizi utakaofanyika Oktoba 24 hadi 26 sambamba na ukataji wa rufaa utakaofanyika Oktoba 24 hadi 29 Mwaka huu.
 
Aidha alisema matukio mengine yote zikiwemo kampeni za wagombea zitaendelea kubaki kama kawaida huku akiwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuwa na sifa ya kupiga kura katika uchaguzi huo.

Ongeza Nguvu Za Kiume, Maumbire Madogo Pamoja Na Tiba Mbalimbali

$
0
0
MASISA 3 POWER nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoazaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wara kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-40

SUPER MONGERA  Hurefusha na kunenepesha maumbile madogo yaliosinyaa. Matatizi haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguluma na kujaa gesi,ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia ninadawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

Ni DR CHIPUPA  pekee mwenye uwezo wa kumrudisha mume , mke ,mchumb.

Kwa nini uhangaike na matatizo ya uzazi;   ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,

 wasiliana na DR. CHIPUPA 

Call+255 0620510598

watsap +255 0758840958

Huduma hii inakufikia popote ulipo

Tembelea Ivigo Herbal Clinic: Kituo Cha Tiba Asili Na Tiba Mbadala Kwa Magonjwa Ya Binadamu

$
0
0
IVIGO HERBAL CLINIC ni Kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa Magonjwa ya Binadamu ikiwemo Kisukari, presha, Nguvu za Kiume, Vidonda vya Tumbo, Tambazi, MATATIZO ya Uzazi, BAWASIRI, Muwasho sehemu za siri, Miguu kuvimba, UVIMBE Tumboni, Tezi Dume, SHINGO ya KIZAZI kwa Akinamama ,Meno bila  kung'oa, Maumivu ya Mgongo na kiuno , Kuborsha Maumbile ya Kiume pamoja na MATATIZO Mbalimabali ya Kimaisha.

Kwa Huduma zetu Tembelea Vituo vyetu ulichokaribu nacho. MBEYA tupo barabara ya ISANGA kabla hujafika Darajani simu 0744687649, Mbarali KITUO KIPO IGAWA STAND YA BARABARA KUU YA KWENDA MBEYA SIMU 0767007704, DODOMA KITUO KIPO CHANG'OMBE STAND simu  0746906010 na Makao Makuu NJOMBE simu 0767944041.Nyote Mnakaribishwa IVIGO HERBAL CLINIC kwa Tiba  Bora

Maonesho Ya Mifuko Ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kufunguliwa Rasmi Oktoba 16 Simiyu

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  yanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho  Oktoba 16, 2019 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Mjini Bariadi Mkoani hapa, ambapo washiriki kutoka taasisi za Umma na binafsi zaidi ya 100, mifuko ya uwezeshaji zaidi ya 40 na vikundi vya kijamii (VICOBA) wanatarajiwa kushiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 15, 2019 Mjini Bariadi Afisa Uhusiano Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), Bw. Edward Kessy  ambao ndiyo waandaaji amesema maonesho haya ni fursa kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa kujifunza huduma za mifuko ya uwezeshaji, taasisi za fedha na programu mbalimbali.

“Maonesho haya yameanza Oktoba 14, 2019 na yatafunguliwa rasmi Oktoba 16, 2019 na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na yatahitimishwa tarehe 20 Oktoba, 2019 na Mhe. Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, nitoe wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili waje wajionee huduma mbalimbali za mifuko, taasisi na vikundi vya kijamii,” alisema Kessy.

Afisa Biashara wa Taasisi ya Private Agricultural Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao kujua huduma zao, huku akibainisha kuwa Taasisi hiyo kupitia mpango mkakati wa miaka mitano ulioanza mwaka 2018 inatarajia kuzifikia familia 235,000 kwa kudhamini mikopo kiasi cha shilingi bilioni 210.6 .

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Posta Tanzania tawi la Bariadi, Bw. Shadrack Daudi amesema benki hiyo kwa kushirikiana na NEEC na PASS imetoa mikopo ya vikundi mbalimbali vya kijamii, vikundi rasmi na visivyo rasmi, wafanyabiashara, hivyo ni vema wananchi wafike kwa wingi kujionea fursa hizo ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Naye mnufaika wa mikopo ya mifuko ya uwezeshaji, Bw. Emmanuel Nyambi Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi kutoka Kahama, ametoa wito kwa wananchi kufika katika maonesho hayo ili waweze kuona fursa za upatikanaji wa mikopo kupitia mifuko, programu na taasisi mbalimbali za kifedha huku akieleza kuwa hakuna urasimu katika utoaji wa mikopo.

“Natoa wito kwa wajasiriamali wadogo au vyama mbalimbali, wafike kwenye maonesho haya waje wajifunze namna ya kupata mikopo ya kuendeshea shughuli za kiuchumi, niwahakikishie hakuna urasimu kwenye mikopo, tunaipata kwa wakati na Benki Kuu inadhamini kikubwa ni kuwa waaminifu kurejesha mikopo,” alisema Nyambi.

Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii  mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu: “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Tanzania ya Viwanda”.

MWISHO

Waziri Lugola Afanya Mazungumzo Na Balozi Wa Ethiopia Nchini, Jijini Dodoma Leo

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA, Dodoma.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.

Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Lugola, jijini Dodoma, leo, ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia.

Waziri Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini.

“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.

Kwa upande wake Balozi Sanbe, alimshukuru Waziri Lugola kwa mazungumzo waliyoyafanya na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Ethiopia na Tanzania.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images