Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Jeshi la Polisi Iringa laonya watakaovuruga Maonyesho ya Utalii Kusini

$
0
0
Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi
JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa limewaonya wananchi wa Mkoa huo kuchukua tahadhari wanapotumia barabara hususani kipindi hiki cha Maonyesho ya Utalii Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi, ACP Juma Bwire alisema wakazi wengi wamekuwa wakitumia bararabara bila kufuata tahadhari hali inayoweza kusababisha kugongwa na magari.
 
” Niwape tahadhari Wananchi pindi wanapotumia barabara ikiwemo kuvuka wasivuke huku wakichat au kuongea na simu, kutakuwa na misafara ya magari hivyo wawe makini” alisema

Alisema Jeshi la Polisi limejipanga kudumisha Ulinzi kipindi chote cha maonyesho hayo huku akitoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto na nyumba za kulala wageni kudumisha Ulinzi kwenye maeneo yao, kwani mara nyingi kumekuwa na matukio ya upororaji wa kompyuta na mali.
 
Maonyesho ya Utalii Kusini yanatarajiwa kufunguliwa Septemba 20 na Rais wa Zanzibar na Serikali ya Mapinduzi Do. Ali Muhamed Shein kwenye viwanja wa Kihesa Kilolo.

Trump kupokea ushauri wa kijeshi juu ya kuiadhibu Iran

$
0
0
Wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon inatarajiwa hii leo kumkabidhi rais wa nchi hiyo Donald Trump, mikakati kadhaa ya kijeshi anayoweza kuitumia kujibu mashambulizi dhidi ya miundombinu ya mafuta ya Saudi Arabia, ambayo utawala wa Trump unaituhumu Iran kuyafanya. Iran imekanusha shutuma hizo. 

Maafisa wa kijeshi watakutana na Rais Trump katika Ikulu ya White House, na kumpa orodha ya vituo vinavyoweza kulengwa ndani ya Iran, na wakati huo huo kumtahadharisha kiongozi huyo kuwa mashambulizi dhidi ya Iran yanaweza kusababisha vita kamili. 

Afisa ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema huo ni mkutano wa kwanza unaoweza kuchukua uamuzi juu ya namna ya kulipiza kisasi kwa mashambulizi dhidi ya mmoja wa washirika muhimu wa Marekani, Saudi Arabia. 

Hata hivyo, uamuzi wowote wa kujibu mashambulizi hayo, utategemea ushahidi utakaotolewa kuthibitisha kwamba ndege zisizo na rubani pamoja na makombora vilivyoipiga miundombiu ya mafuta zilitokea Iran.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi September 21

Viwanja vinauzwa Bunju na Mapinga (Baobab sec).....Malipo ya Awamu

$
0
0
Kwa Mapinga vipo viwanja vya sqm 300 bei tsh 3.5 milion, sqm 400 kwa tsh 4.5 milion, sqm 600 kwa tsh 7.5 milion, sqm 1000 kwa tsh 12 milion, sqm 1600 kwa tsh 20 milion, sqm 2000 kwa tsh 26 milion na sqm 2400 kwa tsh 31 milion.
Viwanja hivi viko umbali wa km 2 kutoka main road (Dar to Bagamoyo Road)

Kwa Bunju vipo viwanja vya sqm 600 kwa tsh 25 milion na sqm 1750 kwa tsh 51 milion.

Biashara hii haina dalali/udalali
Mpigie mhusika kwa 0758603077 au whatsap 0757489709

Msimu Ujao Korosho Kununuliwa Kwa Kujisajili Kupitia Mfumo Wa ATMIS

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Serikali imetangaza ununuzi wa korosho wa msimu mpya   unaohusisha teknolojia ya wanunuzi kujisajili kwenye Bodi ya Korosho kupitia mfumo wa Wizara ya Kilimo wa kusimamia Biashara za Kilimo (Agricultural Trade Management Informataion System – ATMIS).

Imeeleza pia kuhusu deni la korosho msimu uliopita  inalodaiwa na wakulima wakubwa kuwa shilingi bilioni 50, ambalo linaendelea kulipwa kila siku kulingana na shehena ya korosho zinazonunuliwa na wanunuzi. 

Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  Tarehe 20 Septemba 2019 Jijini Dar es Salaam.

“Msimu wa 2019/2020 mfumo wa ununuzi wa korosho utakuwa kwa njia ya mnada wa wazi kwa kutumia jukwaa la Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) ambapo hakutakuwa na matumizi ya masanduku ya mnada,”alisema Waziri.

Amesema kuwa wanunuzi watakaosajiliwa na kukidhi vigezo watatakiwa kulipa Kinga ya Dhamana (Bid Security) kutegemeana na kiasi cha korosho mnunuzi anachotaka kununua kupitia kwenye akaunti ya usuluhishi inayomilikiwa na Soko la Bidhaa.

“Mfumo huu utaruhusu wanunuzi mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali duniani kushiriki katika mnada. Wanunuzi wa nje ya nchi wataweza kushiriki katika mnada moja kwa moja na hawatalazimika kufungua makampuni hapa nchini,” alisema Waziri.

Amesema badala yake wanunuzi hao watadhaminiwa na benki za malipo (Settlement Bank) zinazotambuliwa na Soko la Bidhaa (TMX) hivyo kuongeza ushindani katika minada.

“Benki za malipo zitawajibika kutoa uhakikisho wa uwepo wa fedha kwa ajili ya malipo ya korosho kwa mujibu wa taratibu za soko,”alisema.

Akizungumzi kuhusu wanunuzi wa ndani na nje ya nchi alisema wataruhusiwa kununua korosho  ghafi kwa mafungu (stakes) kati ya tani 50 mpaka tani 500 kulingana na mahitaji.

“Korosho hizo katika mafungu (stake) zitapangwa kulingana na vigezo vya ubora na daraja.  Kiwango cha korosho kitakachouzwa katika kila kikao (mnada) kitatokana na taarifa zilizopo katika katalogi ya mauzo,” alisema.

“Mnunuzi atalazimika kununua kiasi chote cha korosho kilichopo katika fungu katika kikao kimoja  ili kuwezesha utoaji wa korosho katika ghala kwa kutumia utaratibu wa korosho za kwanza kuingia ndizo za kwanza kutoka (first in, first Out- FIFO),”alifafanua Waziri.

Alisema Wanunuzi wenye leseni watapewa msimbo (code) maalumu watakazozitumia kuingia kwenye mfumo na kushiriki katika minada. Mnunuzi atakaeshinda katika mnada atawajibika kulipia korosho alizoshinda ndani ya siku tatu (3) baada ya mauzo kufanyika.

Malipo yote yatafanyika kupitia benki za malipo (Settlement Bank) zinazotambuliwa na Soko la Bidhaa. Soko la bidhaa litawalipa wadau wote kwa mujibu wa sheria ndani ya siku mbili tangu mnunuzi kukamilisha malipo husika.

Waziri alieleza  kuwa utaratibu huu utaondoa ulazima wa wanunuzi kusafiri kutoka eneo moja kwenda lingine ili kushiriki minada ya korosho.

“Minada ya mauzo ya korosho itafanyika siku mbili kwa wiki katika maghala yote kulingana na upatikani wa korosho, minada itakuwa siku ya Jumanne na Alhamisi,” alisema.

Waziri Hasunga amesema lengo la utaratibu huu mpya ni kupanua wigo wa soko ambao wanaamini utaongeza chachu ya ushindani na kuwezesha bei nzuri zaidi kupatikana kulingana na mwenendo katika soko la dunia.

Kupitia jukwaa la Soko la Bidhaa kutakuwa na wigo mpana kwa wanunuzi, kutakuwa na uwazi wa bei za korosho na wakulima watalipwa haraka zaidi na kwa wakati.

Alisema lengo la Serikali ni kuona wakulima wote wanalipwa fedha zao moja kwa moja  kwenye akaunti zao binafsi katika Benki zilizopo katika maeneo yao ya uzalishaji.

“Msimu wa ununuzi wa korosho Mwaka 2019/2020 kwa sasa umefunguliwa rasmi. Katika msimu wa 2019/2020 tunategemea kuzalisha tani 300,000 za korosho ghafi kutoka tani 224,000 zilizozalishwa 2018/2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 34%,” alisema Waziri.

Alibaiisha kuwa Wizara ina mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji ikiwa ni pamoja na Kuhamasisha matumizi sahihi ya viutilifu bora na  kuhakikisha upatikanaji wa viuatilifu hivyo kwa wakati na kwa bei nafuu pamoja na kutoa mafunzo kwa wakulima.

Waziri alisema  kuwa  matumizi sahihi ya viuatilifu yataongeza tija miongoni mwa wakulima kutoka wastani wa kilo 10 kwa mti kwa mwaka hadi kufikia kilo 35 kwa mti kwa mwaka.

Alisema Wizara yake kupitia Bodi ya korosho imeongeza maeneo mapya yanayolima korosho kutoka mikoa mitano ya awali ambayo ni Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga na kufikia mikoa 17.

“Mikoa mingine inayolima korosho kwa sasa ni Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Katavi, Morogoro, Songwe,Kigoma, Njombe na Shinyanga,”alisema. 

Katika musimu wa mwaka 2018/2019 serikali iliamua kununua korosho zote toka kwa wakulima kutokana na kuyumba au kushuka kwa bei ya korosho katika soko la minada.

“Hatua hii ilikuwa ni ya dharura iliyochukuliwa ili kulinda maslahi ya mkulima, kuanza mkakati wa kubangua korosho zote hapa nchini, kufufua viwanda vya kubangua korosho vilivyopo na kuongeza ajira kwa watanzani,”alisema.

 Lengo la Serikali ya Tanzania chini ya Rais John Magufuli ni kuhakikisha kuwa wakulima wananufaika na mazao yao na kupata bei nzuri kulingana na mwenendo wa soko.

Bei ya korosho ghafi katika Mwaka 2018/2019 iliyotolewa na wanunuzi ilikuwa ndogo sana, ikilinganishwa na bei ya Msimu wa 2017/2018.

Utekelezaji wa maamuzi na maagizo hayo ulifanywa kwa ushirikiano mkubwa kati ya wizara ya kilimo, viwanda na biashara, wizara ya  Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, TAMISEMi, na wizara ya mipango na Fedha.

MWISHO

Waziri Mpina Atengua Uteuzi Wa Kaimu Mtendaji Mkuu Wa Wakala Wa Vyuo Vya Mafunzo Ya Mifugo(Lita)

Lowassa Ammwagia SIFA Rais Magufuli....Kasema Utendaji Wake Umeifanya Nchi Ishike Adabu

$
0
0
Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Lowassa amepongeza utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli ambapo amesema kampeni yakutumbua watu ambao ni wazembe imesaidia nchi kushika adabu na mambo yanakwenda kwa utaratibu

Lowassa ameyasema hayo jana  katika mahafali ya shule ya msingi ya Meyers mjini Arusha.

"Rais  Magufuli anastahili pongezi anafanya kazi nzuri sana, tunaona mawaziri wanafanya kazi nzuri , Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) yupo kule wengine huku, nchi imewaka moto kila sehemu.” Amesema Lowassa

Kwa mujibu wa Lowassa, kazi za Rais Magufuli, zinatakiwa kupakwa ‘poda’ kwa kuhusisha uboreshaji wa elimu ambayo itawapa ujuzi wahitimu kujiajiri. 

"Kuna vijana wengi wanamaliza masomo kutokana na mpango wa elimu bure sasa tujitahidi elimu hii iwasaidie vijana kupata ujuzi na ubunifu ili kuweza kujiajiri."Ameongeza Lowassa.

Lowassa aliyejiunga ndani ya Chadema tarehe 28 Julai 2015 na kupitishwa kuwa mgombea urais wa chama hicho akiungwa mkono na vyama rafiki vya Ukawa, alishindwa kuhimili mikikimikiki ya upinzani na kuamua kurejea ndani ya chama tawala CCM tarehe mosi Machi mwaka huu.

Video: Rostam Ft. Nay wa Mitego - KIJIWE NONGWA

$
0
0
Video:  Rostam Ft. Nay wa Mitego - KIJIWE NONGWA

Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi La Polisi Mkoani Mbeya

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Kelvin Manyusi (32) fundi umeme, mkazi wa Teku Jijini Mbeya akiwa na sare za Jeshi la Polisi ambazo ni TT 2 kitengo cha FFU, koti la mvua rangi nyeusi pamoja na mkanda wa filimbi ambavyo ni mali za Jeshi la Polisi Tanzania.

Mtuhumiwa alikamatwa Septemba 20, 2019 saa 15:30 alasiri katika msako uliofanyika huko Mtaa wa Ngosi, Kata ya Mwakibete, Tarafa ya Iyunga, Jiji la Mbeya.

Pia mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa na vifaa vya kuvunjia ambavyo ni panga, bisibisi pamoja na tindo. Aidha mtuhumiwa baada ya kupekuliwa nyumbani kwake alikutwa na mali mbalimbali zidhaniwazo kuwa za wizi ambazo ni

1.“TV” 2 aina ya “Samsung” nchi 32, “Aborder” nchi 32,
2.“System Case” mbili aina ya “Dell na Hp”,
3.“Keyboard” 1 aina ya “Hp”,
4.“Receiver” tatu za vinga’muzi vya “Dstv”, Azam na “Startime”,
5.Speaker” mbili za “Seapiano” na “Topsonise”,
6.Simu za Mkononi 9 kati yake “Smartphone” tatu na sita za kawaida 6,
“External” 4,
7.Kamera moja aina ya “Ricoh”,
8.“Remote control” 14,
9.“Switch ya Internet” 1,
10.“Dryer” mbili moja ya mkono ndogo na kubwa,
11.Jiko la umeme 1,
12.Amplifier na Equalizer 1 aina ya metal,
13.Twitter 7,
14.mouse 1,
15.Rasta bunda 7 za kusukia nywele bandia,
16.Uzi bunda mbili za kushonea,
17.Mashine ya Blenda nyeupe ,
18.Saa 3,
19.Deki 1 aina ya LG,
20.Mitungi 2 ya Gesi aina ya Oryx,
21.Jiko la Gesi 1 la plate mbili

Upelelezi unaendelea.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WATATU KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NYARAKA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wanawake watatu kwa tuhuma za kughushi nyaraka mbalimbali kwa lengo la kupata mkopo katika Benki ya Posta Tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya.

Watuhumiwa wamekamatwa Septemba 19, 2019 saa 16:00 jioni huko Benki ya Posta iliyopo maeneo ya Mwanjelwa Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa watuhumiwa wameghushi majina yao halisi kwa lengo la kupata mkopo kwa njia ya udanganyifu na kukwepa kuonekana kuwa wanadaiwa na taasisi nyingine za fedha.

Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
    1.FARIDA YESSAYA @ TUMPALE [23] Mfanyabiashara na Mkazi wa Uyole ambaye ametengeneza nyaraka zake kwa kutumia jina la mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aitwaye CAREN ZABRON @ BANDARI.
    2.ASHA HARZINA @ NAMWENE [29] Mfanyabiashara na Mkazi wa Uyole ambaye ametengeneza nyaraka zake kwa kutumia jina la mama yake mzazi ambaye ni marehemu aitwaye ZAITUNI ABIANI @ BAKILI.
    3.REBECCA YESSAYA @ MSIGALA [47] Mfanyabiashara na Mkazi wa Uyole ambaye ni Mwenyekiti wa Kikundi na alithibitisha majina hayo huku akijua sio majina yao halisi waliyotumia kuchukua mkopo katika taasisi ya fedha – FINCA.

Watuhumiwa kwa pamoja waliomba mkopo wa shilingi milioni mbili na laki tano [2,500,000] na walitegemea kupewa mkopo huo tarehe 19.09.2019 ila kabla ya kupewa fedha hizo Jeshi la Polisi liliweza kubaini kuwa watuhumiwa wametumia majina yasiyo yao ili kukwepa kurejesha fedha hizo. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa Mahakamani.

KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

Mnamo tarehe 21.09.2019 majira ya saa 00:15 usiku wa kuamkia leo huko nyumba ya kulala wageni iitwayo Gaga iliyopo Mtaa na Kata ya Bagamoyo, Tarafa  ya Tukuyu Mjini, Wilaya ya Rungwe na Mkoa Mbeya. Polisi walimkamata BONNY BONNY BANDA [35] raia na mkazi wa Nchni Malawi akiwa ameingia Nchini bila kibali. Upelelezi unaendelea.

KUPATIKANA NA BHANGI NA POMBE MOSHI.

Mnamo tarehe 19.09.2019 majira ya saa 01:50 usiku huko Kijiji cha Izumbwe kilichopo Kata ya Igale, Tarafa ya Usongwe, Wilaya Mbeya Vijijini, Mkoa Mbeya.  Askari Polisi walimkamata AHAZI ISSA @ MAPOGELO [31] Mkazi wa Izumbwe akiwa na bhangi kilo 2 na gramu 220 pamoja na Pombe Moshi ujazo wa lita moja [01] ndani ya nyumba yake. Mtuhumiwa ni mtumiaji na muuzaji wa bhangi na Pombe Moshi. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa Mahakamani.

Waziri wa Kilimo Aiagiza TFRA Kuhakikisha Mbolea Inapatikana Kwa Bei Nafuu

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imeiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mbolea inapatikana kwa wakati na bei nafuu.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo  tarehe 18 Septemba 2019 wakati akifunga mkutano mkuu wa Wakala wa usambazaji wa mbolea Tanzania (TADCOs) katika ukumbi wa Polisi Jamii Jijini Dodoma.

Mhe Hasunga amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti uwepo wa pembejeo feki nchini.

Alisema Kwa upande wa mbolea, tayari Wizara ya Kilimo imetoa mafunzo na kuwapitisha Wakaguzi 50 wa mbolea ambao wanaenda kuongeza nguvu kwa kufanya kazi nchi nzima za kudhibiti ubora wa mbolea.

Mhe Hasunga alisema kuwa kwa upande wa Viuatilifu, ameiagiza Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa Viuatilifu ukanda wa Kitropiki (TPRI) kuhakikisha wanafanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini na kuondoa viuatilifu feki vyote sokoni.

Aidha, tayari Wizara imeridhia na kuwapitisha Wakaguzi (Inspectors) 45 wa kukagua viuatilifu ambao nao wanaenda kuongeza nguvu nchi nzima kuhakikisha tatizo la viuatilifu feki linamalizika.

Kadhalika Mhe Hasunga amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kudhibiti na kuondokana na changamoto ya uwepo wa pembejeo ambazo hazikidhi viwango.

Katika mkutano huo Mhe hasunga ameupongeza uongozi wa TADCOs kwa mwanzo mzuri wa kiuongozi hususani kuwasomea wananchama wao mapato na matumizi hukuakitoa rai kwa Viongozi wote, kuhakikisha wanaendesha chama hicho kwa ufanisi mkubwa, uwazi na uwajibikaji kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za ushirika nchini.

Aliongeza kuwa ana matarajio kwamba, kuanzishwa kwa chama hicho cha Ushirika kutapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zilizokuwepo na kusaidia kuwanufaisha wakulima kwa kuagiza na kusambaza  pembejeo zenye ubora, kwa wakati na bei nafuu.

“Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwakomboa wakulima nchini kwa kuhakikisha wanazalisha mazao yao kwa tija ili waweze kuinua hali zao za maisha na kuchangia uchumi wa nchi.  Ni ukweli usiopingika kuwa azima hii hawezi kufikiwa kama wakulima hawatapata pembejeo zenye ubora, kwa wakati na kwa bei nafuu” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

“Dhamana mliyonayo  ni kubwa sana, hivyo ni matarajio yangu kuwa mtatimiza jukumu lenu kuu la kuhakikisha mnasimamia usambazaji wa pembejeo za kilimo wakulima wa Tanzania walio wanyonge kwa uaminifu na uweledi mkubwa.”

Aliwataka (TADCOs) kufuata Sheria, kanuni na taratibu zote zinazohusu uendeshaji wa biashara ya pembejeo nchini na kuzingatia kanuni za ushirika.  Aidha, kushirikiana na Taasisi zote zinazodhibiti na kusimamia tasnia ya pembejeo na ushirika nchini kama vile TFRA, TPRI, ASA, TOSCI, TCDC na TFC ili waweze kuwasaidia wakulima kupata pembejeo zenye ubora.

Ili kupunguza gharama na kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo sahihi, kwa wakati na bei nafuu, Mhe Hasunga aliwaagiza Viongozi wenu wa TADCOs kusimamia vilivyo zoezi la uagizaji wa pembejeo kwa pamoja, moja kwa moja kutoka viwandani na si kwa wauzaji wa kati. 

MWISHO

Video: Rostam Ft. Nay wa Mitego - KIJIWE NONGWA

$
0
0
Video:  Rostam Ft. Nay wa Mitego - KIJIWE NONGWA

Waziri Lugola Kutatua Kero Za Wamiliki, Waendesha Vyombo Vya Moto Kupitia Bonanza Kubwa La Vijana Mkoani Dodoma Kesho

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Bonanza kubwa la Vijana litakalofanyika Chang’ombe jijini Dodoma, kesho.

Bonanza hilo, pia litashirikisha wananchi mbalimbali wakiwemo wamiliki na waendesha vyombo vya moto kutoka Wilaya zote za Mkoa huo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, jijini Dodoma leo, Waziri Lugola alisema amealikwa na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kuwa mgeni rasmi ambao ndio waratibu wa Bonanza hilo.

Lugola alisema amepewa taarifa na uongozi wa UVCCM Mkoa, kuwa wamejipanga vizuri na pia Bonanza hilo litaambatana na michezo mbalimbali na burudani kutoka kwa wasanii wa miondoko ya kizazi kipya.

“Kupitia mkutano huo wa Dodoma, nitalenga kuwahabarisha vijana wote na wananchi kwa ujumla hapa nchini, kuhusu mafanikio ya Serikali katika kuwasaidia vijana kupambana na umaskini, na kutatua tatizo la ajira pasipo kunyanyaswa kwa kujua au kwakutokujua kwa vyombo vya ulinzi na usalama hususani jeshi la polisi, pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali,” alisema Lugola.

Alisema vijana ni nguzo ya taifa, hivyo Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na inawathamini katika mazingira yao ya kujipatia kipato ikilenga kuwapa nafasi mbalimbali ili waweze kupata mafanikio zaidi.

“Mwezi uliopita nilikutana na wamiliki na waendesha bodaboda na bajaj zaidi ya 2000 mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro, nilitoa mwarobaini wa kero zao, ambazo nyingi zaidi zilihusu Manispaa ya Moshi kutowatendea vema katika maeneo mbalimbali ya maegesho ya vyombo vyao vya moto, pamoja na kero nyingine zilizowahusu baadhi ya askari wangu wa kikosi cha usalama barabarani ambapo vijana hao waliwalalamikia,” alisema Lugola.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, Billy Chidagwa alisema Bonanza hilo litaacha historia katika mkoa huo kutokana na maandalizi yao waliyoyafanya katika kufanikisha vijana mkoani humo wanakutana pamoja na kero zao kutatuliwa.

Chidagwa alisema vijana mbalimbali watakuwepo katika tukio hilo, hasa wanaotumia vyombo vya moto mbalimbali vikiwemo Bajaj, Bodaboda na waendesha daladala kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma.

“Tumejipanga vizuri kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mbunge wa Vijana, Mbunge wetu wa Jimbo, viongozi wa chama, tunaamnini uwepo wao kutakuwa na tija kufanikisha tukio hili ambalo maandalizi yake ni ya muda mrefu, na tayari yamekamilika,” alisema Chidagwa.

Alisema Bonanza hilo litaambatana na michezo mbalimbali, ambapo kwa upande wa mpira wa miguu, timu ya bodaboda itacheza na timu ya Askari Polisi mkoani Dodoma.

“Vijana njooni kwa wingi kesho jumapili tarehe 22 mwezi huu wa tisa pale Chang’ombe ili tufurahi kwa pamoja na kumsikiliza mgeni wetu rasmi, ambaye ni Waziri Lugola atakapotatua kero zetu na kutuonyeshea njia ya mafanikio zaidi katika Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli,” alisema Chidagwa.

Waziri Lugola ambaye alikuwa mkoani Arusha kikazi, amewasili leo jijini Dodoma kwa ajili ya kufanikisha tukio hilo muhimu kwa maendeleo ya vijana.

Marekani kupeleka vikosi zaidi vya kijeshi nchini Saudi Arabia baada ya shambulizi dhidi ya kiwanda cha mafuta

$
0
0
Rais Donald Trump ameidhinisha hatua ya kupeleka vikosi zaidi vya kijeshi Saudi Arabia kusaidia vikosi vya ulinzi vya angani nchini humo. Hii ni baada ya shambulizi lililoharibu viwanda vikuu vya mafuta nchini humo.
 
Waziri wa ulinzi wa Marekani Mark Esper amethibitisha hatua hiyo ya kupelekwa kwa vikosi hivyo zaidi vya kijeshi nchini Saudi Arabia jana Ijumaa. 

Idadi kamili ya maafisa wa kijeshi na vifaa vitakavyotumiwa bado haijabainika lakini itakuwa sehemu ya "uhamishaji wa wastani'' katika eneo hilo. 

Hii ni kulingana na jenerali wa jeshi la wanamaji Joseph Dunford, ambaye ni mwenyekiti wa kundi shirikishi la wakuu wa kijeshi.

"Kwa kujibu ombi la taifa hilo la kifalme, rais ameidhinisha kupelekwa kwa vikosi vya kijeshi vya Marekani ambavyo vitatekeleza jukumu la ulinzi  na kuangazia zaidi ulinzi wa angani na makombora," Esper aliwaambia wanahabari.

Tangazo hilo linajiri baada ya shambulizi la Sepetmba 14 dhidi ya muundo msingi mkuu wa mafuta nchini Saudi Arabia ambalo lilitatiza nusu ya usambazaji wa bidhaa ya mafuta nchini humo. 

Waasi wa kihouthi nchini Yemen wamedai kuhusika katika shambulizi hilo lakini Marekani na Saudi Arabia zinashuku kuwa Iran ndio iliyohusika. Iran inayoungwa mkono na kundi hilo la kihouthi, imekanusha madai hayo.

Dkt. Ashatu Kijaji Kutatua Changamoto Ya Maji Kijiji Cha Mwongolo Kondoa Vijijini

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Kondoa
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini mkoani Dodoma Dkt. Ashatu Kijaji ameahidi kumaliza kero ya maji inayo wakabili wakazi wa Kijiji cha Mwongolo mkoani humo.

Ametoa ahadi hiyo alipokutana na wananchi wa kijiji hicho ambao walimweleza kuhusu changamoto yao ya muda mrefu ya kukosa huduma ya maji safi na salama pamoja na changamoto nyingine za ukosefu wa miundombinu mingine inayoweza kuchochea kasi yao ya maendeleo.

Wananchi hao walisema kero kubwa inayo waumiza ni upatikanaji wa maji katika kijiji hicho ambapo wanawake wamekuwa wakilazimika kwenda umbali mrefu kuchota maji jambo ambalo limewafanya kuchoka na kuhatarisha usalama wa maisha yao.

Dkt. Kijaji alisema kuwa amekuwa akichimba visima katika vijiji mbalimbali wilayani humo ambapo hadi sasa jumla ya visima 65 vimeshakamilika na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

"Leo nimekamilisha kisima cha 65 Shule ya Msingi Kalamba niliposoma ndani ya miaka minne ya uongozi wangu, hapa Mwongolo ni nyumbani na kwa mapenzi niliyonayo kwa ndugu zangu wa Mwongolo, mhandisi akimaliza kuchimba kisima cha kijiji cha Mwaisanga atakuja Mwolongo katika kipindi cha mwezi huu au wa kumi kisima kitakuwa kimechimbwa" alisisitiza Dkt. Kijaji.”

Aidha ameahidi kufuatilia visima 14 vilichoahidiwa kuchimbwa kwenye sehemu ya machinjio ya kijiji hicho na Wizara ya Maji kupitia Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa, (DDCA), ili nao waweze kupata maji kwa ajili ya shughuli zao za kila siku.

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ni sikivu hivyo itaendelea kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama vile Sekta ya elimu, huduma za afya, nishati, maji, miundombinu ili ziweze kuwafikia wananchi wote nchini kwa urahisi zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwolongo Bw. Miraji Ramadhani, amemshukuru Dkt. Ashatu Kijaji kwa kutenga muda wa kwenda kutembelea kijiji hicho na kutatua baadhi ya kero zilizokuwa vinawasumbua muda mrefu.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameahidi hadi kufikia 2020 vijiji vyote 84 vya Jimbo lake la Kondoa Vijijini vitakua vimepata huduma ya maji kwa njia ya visima vya maji ili kumaliza kabisa kero ya maji Jimboni humo.

Mwisho.

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
Dalili:mwili kuchoka,maumivu ya mgongo na kiuno,kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu

Misuli  kulegea na kusinyaa hata kushindwa kufika kileleni miguu kuuma na kuwaka moto:

TIBA YAKE:

TULLO4 MIX.Ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizi hayo, inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kukufanya urudie tendo la ndoa zaidi mara tatu bila kuchoka au kukinai.

NTINJE3 PUMP.Ni dawa inayoongeza maumbile na kukupa umbile la kudumu.Itumie tiba hii kuokoa ndoa yako na kuokoa kukimbiwa na umpendae.
GASELA: Ni dawa mvuto kumvuta umpendae na kumrudisha alie mbali .

NTOBO: Inatibu KISUKARI:siku7 na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenyetatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari.

mpigie DR LIZENGO .OFISI IPO MBAGALA SABASABA.SIMU 0655283534/0621737576

Balozi Iddi: Taasisi Ziboreshe Mifumo Ya Kukusanya Mapato Ya Serikali

$
0
0
Na Farida Ramadhani, WFM, Dar es Salaam
Taasisi za Serikali zinazotumia mifumo ya kielektroniki zametakiwa kuhakikisha zinaanzisha mfumo wa kuziwezesha kuona taarifa za kila taasisi pindi watakapo huisha mifumo hiyo.

Agizo hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea banda la Serikali Na. 26 la mifumo ya kielektroniki ya kukusanya maduhuli ya Serikali (GePG), Mfumo wa Usimamizi wa Makosa Barabarani (TMS) na Mfumo wa Taarifa za Mali zilizopote (Los Report System) katika Mkutano wa Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wa Sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa.

Balozi Iddi ambaye alifunga mkutano huo, alisema kitendo cha taasisi kuweza kuona taarifa kutoka taasisi nyingine kutarahisisha kazi na kuongeza ufanisi wa Serikali katika kuhudumia wananchi.

“Kama GePG inarahisisha malipo kwa taasisi zote ni vema kukawa na mfumo wa kuziwezesha taasisi hizo hasa zinazotegemeana kuweza kushirikishana taarifa, kama mtu akienda TRA kuhuisha leseni na anadaiwa na Trafiki basi mfumo uoneshe kuwa anadaiwa moja kwa moja”, alisema.

Aidha Balozi Iddi alipongeza mifumo ya GePG, TMS na ule wa taarifa za mali zilopotea na kusema kuwa mifumo hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na imeanzishwa wakati muafaka.

Alisema kuwepo kwa mifumo hii kunaiwezesha Serikali kupata mapato ya kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumzia mfumo wa GePG Mkuu wa Uendeshaji wa Mfumo huo, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Basil Baligumya, alisema mfumo umeunganisha taasisi zote za Serikali ambapo kila malipo ya taasisi hizo hupitia katika mfumo huo.

Alisema  mfumo huo umeongeza makusanyo  ya Serikali, umedhibiti fedha za umma, umeongeza uwazi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, pamoja na kuongeza usahihi wa taarifa za mapato.

Naye Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Dkt. Gabriel Mukungu alisema kuwa mfumo wa TMS unasaidia kudhibiti makosa ya barabarani kwa kuwakamata wahalifu wote wa makosa hayo kwa kuwa mfumo huo unawezesha kuona watu wote wanaodaiwa tozo za makosa barabarani.

Mwisho.

Serikali yaagiza Halmashauri zote za mkoa wa Shinynaga kujenga maeneo ya Maegesho ya malori ya mizigo kabla ya octoba 25 mwaka huu.

$
0
0
NA SALVATORY NTANDU
Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Shinyanga wametakiwa kujenga maaeneo ya maegesho ya malori ya mizigo na mafuta ambayo yemekuwa yakiengeshwa katika maeneo yasiyorasimi(makazi ya watu) hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa wananchi kabla ya octoba  25 mwaka huu

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack kwenye kikao cha robo ya pili ya bodi ya barabara mkoa wa shinyanga, na kusema kuwa kumekuwa na tabia ya uegeshaji holela wa malori ya  katika makazi ya watu huku mengine yakiwa na kemikali hatari kama vile gesi na mafuta.

Amesema serikali haiwezi kukubali hali hiyo huku wenye mamlaka ya kusimamia na kupanga maeneo ya miji na wilaya wakiwa hawatimizi wajibu wao na kuendelea kuruhusu uegeshaji holela wa malori hayo ambao ni hatari kwa maisha  kwa uslama wa wananchi wa mkoa huo.

Amefafanua kuwa utengaji wa maeneo ya malori ya mizingo kwenye halmashauri za mkoa wa shinyanga kutaongeza mapato  kutokana na malori hayo na pia itawawezesha wamiliki wa malori hao kutoibiwa vifaa vyao vya magari katika vituo hivyo kwani  katika maeneo hayo kutakuwa na ulinzi wa kutosha.

Michael Matomora ni mkurugenzi wa Halamshauri ya Ushetu na Godfrey Mwangulumbi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga wamesema katika bajeti ya mwaka 2018/19 hawakutenga bajeti kwaajili ya kutenga maeneo hayo lakini kwa mwaka huu wa fedha watahakikisha agizo hilo linatekelezwa harasa.

Naye Kaimu Meneja wa TANROAD mkoa wa Shinyanga Mhandisi, Mibara Ndilimbi amesema kwa sasa Wakala  huo unaendelea kujenga eneo la maengesho la Kagonjwa Isaka ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi sambamba na kuboresha eneo la Maegesho la Mjini Kahama.

Ongeza Nguvu Za Kiume, Maumbire Madogo Pamoja Na Tiba Mbalimbali

$
0
0
MASISA 3 POWER nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoazaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wara kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-40

SUPER MONGERA  Hurefusha na kunenepesha maumbile madogo yaliosinyaa. Matatizi haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguluma na kujaa gesi,ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia ninadawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

Ni DR CHIPUPA  pekee mwenye uwezo wa kumrudisha mume , mke ,mchumb.

Kwa nini uhangaike na matatizo ya uzazi;   ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,

 wasiliana na DR. CHIPUPA 

Call+255 0673878343

watsap +255 0620510598

Huduma hii inakufikia popote ulipo

Waiomba Wizara ya Afya kuweka mkazo ukatili wa Kijinsi kwa watu wenye Ulemavu

$
0
0
Shirikisho la Vyama vya Walemavu (SHIVYAWATA) limeiomba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jmaii, Jinsia, Wazee na Watoto kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa umma juu ya kupambana na manyanyaso na vitendo ya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu nchini.

Ombi hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Taifa Bi. Ummy Hamisi Nderiananga wakati wa kikao kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo kinachoshughulikia watu wenye ulemavu.

Bi. Ummy ameongeza kuwa kama Wizara ilivyoweka nguvu kwenye masuala ya jinsia hasa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto basi pia waongeze nguvu katika kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya walemavu katika jamii.

“Vitendo vya ukatili dhidi ya walemavu wawe watoto au wanawake hata wanaume pia vinatendeka katika familia zatu ila havipigiwi kelele za kutosha” alisema Bi. Ummy.

Bi. Ummy amesisitiza Wizara kupitia Mpango Mkakati wa Taifa wa kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ili uweze kuwezesha kuingiza masuala ya watu wenye ulemavu ili kuondokana na vitendo vya kikatili vinavyowapata watu wenye ulemavu nchini.

Akifafanua kuhusu Wizara kutilia Mkazo suala la Ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mwajuma Magwiza amesema kuwa Wizara inalenga kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya makundi yote ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu nchini.

Bi. Mwajuma ameongeza kuwa Wizara imejikita katika Kampeni mbalimbali za kupambana na vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto likiwemo kundi la watu wenye elemavu kwa kutoa elimu kwa jamii ya kupambana na vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amesema kuwa kikao hicho kimeisaidia Wizara kupata namna bora ya kuyafikia makundi ya watu wenye ulemavu kabla ya kuandaa miongozi na Mikakati mbalimbali ya Wizara ili katika utekelezaji wake isiache kundi la watu wenye ulemavu na makundi mengine maalum.

Bw. Golwike ameongeza kuwa Wizara itashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha watu wenye ulemavu katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira wezeshi kwa watu wenye ulemavu katika kapata fursa sawa kama makundi mengine katika jamii hasa katika utoaji wa mikopo na elimu ya ujasirimali.

Naye Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha watu wenye Ulemavu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Philbert Kawemama amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inafuatilia utekelezaji wa Sheria namba 9 ya mwaka 2010 na Kanuni zake ili kuhakikisha kila Wizara na Taasisi zake zinazingatia masuala ya watu wenye ulemavu katika kuhakikisha wanapata mazingira stahiki katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ameongeza kuwa pia Ofisi ya Waziri Mkuu inafuatilia uwezeshwaji wa kundi la watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha wanapata fursa sawa za kimaendeleo na kusaidia kundi hilo kuondokana na vitendo vya unyanyapaa na vitendo vya kikatili dhidi yao.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la ADD International, Bw. Isack Idama amesema kuwa Wizara ina dhamana kubwa kwa maendeleo ya watoto na wao kama wadau wa masuala ya watu wenye ulemavu hasa watoto wangependa kuona kwa jinsi gani masuala ya watoto wenye ulemavu yanashughulikiwa.

Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo kinachoshughulikia watu wenye ulemavu kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania wanatembela Wizara na Taasisi za Serikali katika kufuatilia na kuona kwa jinsi gani masuala ya watu wenye ulemavu yatekelezwa.

Waziri Mkuu: Wakulima Msiuze Pamba Chini Ya Sh. 1,200

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa zao la pamba nchini wasikubali kuuza pamba yao chini ya bei elekezi ya sh. 1,200.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewashauri wafanyabiashara wa zao hilo waungane na kuanzisha viwanda vya kutengeneza nyuzi na nguo ili kuongeza thamani kabla ya kuuza pamoja na kuwahakikishia wakulima soko.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Septemba 21, 2019) wakati akizungumza na viongozi na wananchama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Chato  (CCU) pamoja na wananchi kwenye kiwanda cha kuchambua pamba cha Chato kinachomilikiwa na CCU mkoani Geita.

Amesema wakulima waendelee kuwa na subira kwa sababu wanunuzi hao wamepewa fedha za kutosha kununua pamba yote kwa bei ya 1,200 na si vinginevyo.

“Hata mkiwa na shida msikubali kuuza pamba yenu chini ya sh. 1,200 kwa kuwa haitachukua muda mrefu mtakuwa mmeshapata fedha zenu. Tuna taarifa kuwa kuna wanunuzi wamepata fedha na wanawatumia watu kwenda kuwalaghai wakulima kwa kutaka kununua kwa bei ya sh. 800, msikubali na mkiwaona mtupe taarifa.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema viwanda vya nyuzi na vya nguo vikijengwa nchini vitakuwa na uhakika wa soko kwani hivi sasa Tanzania  haina viwanda vya kutosha vya nguo. Amesema Serikali ipo tayari kuwaunga mkono Watanzania wote au mwekezaji yeyote atakayekuwa tayari kuanzisha viwanda vya aina hiyo kwa sababu mahitaji ni makubwa.

“Tuna shule zaidi ya 18,000 Tanzania na wanafunzi wote wanavaa sare zinatokanazo na pamba, tukisema majora ya sare yasukwe humu humu ndani na kisha kusambazwa mikoa yote bado nguo za watu wanaovaa mitaani. Watapata faida tu.”

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wote wa vyama vya ushirika katika maeneo yanayolima pamba kuwaelimisha wakulima kuhusu umuhimu wa kuzalisha pamba safi ili walinde heshima ya pamba ya Tanzania ambayo duniani inasifika kuwa ni dhahabu nyeupe.

Awali, Meneja wa CCU, Charles Nyasi alimwambia Waziri Mkuu kuwa makampuni ya METEL, KCCL na FRESHO yamejitokeza kununua pamba kupitia AMCOS na tayari kilo 9,611,860 zimenunuliwa  kati ya kilo 11, 140,529 zilizokusanywa.

Alisema kampuni ya FRESHO imenunua kilo 4, 869, 960, KCCL imenunua kilo 3, 025,051 na METEL imenunua kilo 1,716, 420.

Pia Meneja huyo aliiomba Serikali  isaidie kuwalipia deni la sh. 696,854,475.20 ili kumaliza tatizo la madai ya watumishi na wadai wengine. Pia aliiomba Serikali isaidie kuilipia CCU deni la sh. 102, 942,300.00 la ardhi waliyotumia kujengwa kiwanda chao.

Akijibu maombi hayo Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haiwezi kulipa deni hilo hadi itakapopewa maelezo ya kina ni nani aliyesabaisha deni, mazingira yaliyosababisha deni hilo.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images