Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Jeshi la Polisi Iringa laonya watakaovuruga Maonyesho ya Utalii Kusini

$
0
0
Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi
JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa limewaonya wananchi wa Mkoa huo kuchukua tahadhari wanapotumia barabara hususani kipindi hiki cha Maonyesho ya Utalii Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi, ACP Juma Bwire alisema wakazi wengi wamekuwa wakitumia bararabara bila kufuata tahadhari hali inayoweza kusababisha kugongwa na magari.
 
” Niwape tahadhari Wananchi pindi wanapotumia barabara ikiwemo kuvuka wasivuke huku wakichat au kuongea na simu, kutakuwa na misafara ya magari hivyo wawe makini” alisema

Alisema Jeshi la Polisi limejipanga kudumisha Ulinzi kipindi chote cha maonyesho hayo huku akitoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto na nyumba za kulala wageni kudumisha Ulinzi kwenye maeneo yao, kwani mara nyingi kumekuwa na matukio ya upororaji wa kompyuta na mali.
 
Maonyesho ya Utalii Kusini yanatarajiwa kufunguliwa Septemba 20 na Rais wa Zanzibar na Serikali ya Mapinduzi Do. Ali Muhamed Shein kwenye viwanja wa Kihesa Kilolo.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo,Pamoja Na Magonjwa Sugu

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  call 0759 208 637

watsap  0620510598

Aliekuwa Rais wa Simba Evans Aveva na Godfrey Nyange maarufu Kaburu Waondolewa mashitaka ya utakatishaji fedha.....Mahakama Yasema Dhamana Yao Iko Wazi

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa dhamana aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Godfrey Nyange maarufu Kaburu baada ya kuondolewa mashitaka ya utakatishaji fedha.

Dhamana hiyo ni kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh.Mil 30, ambapo hatua hiyo inatokana na washitakiwa hao kukutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka 8 isipokuwa mawili ya utakatishaji fedha.

Hata hivyo washitakiwa hao wameshindwa kutimiza masharti ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 20, 2019 kwa ajili ya washitakiwa hao kuanza kujitetea akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zachariah Hans Pope.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema jukumu la kuthibitisha shitaka kwa washitakiwa ni la upande wa mashitaka, pia kwa kosa moja moja na sio kwa kutegemeana.

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
Dalili:mwili kuchoka,maumivu ya mgongo na kiuno,kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu

Misuli  kulegea na kusinyaa hata kushindwa kufika kileleni miguu kuuma na kuwaka moto:

TIBA YAKE:

TULLO4 MIX.Ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizi hayo, inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kukufanya urudie tendo la ndoa zaidi mara tatu bila kuchoka au kukinai.

NTINJE3 PUMP.Ni dawa inayoongeza maumbile na kukupa umbile la kudumu.Itumie tiba hii kuokoa ndoa yako na kuokoa kukimbiwa na umpendae.
GASELA: Ni dawa mvuto kumvuta umpendae na kumrudisha alie mbali .

NTOBO: Inatibu KISUKARI:siku7 na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenyetatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari.

mpigie DR LIZENGO .OFISI IPO MBAGALA SABASABA.SIMU 0655283534/0621737576

Tegesha Yawaumiza Kichwa Wathamini Fidia Nyamongo

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM NYAMONGO
Zoezi la uthamini kulipa fidia kwa wananchi wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara kupisha upanuzi wa Mgodi wa Dhahabu North Mara kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Maji Taka limekumbwa na changamoto kufuatia baadhi ya wananchi kujenga nyumba ama kuongeza sehemu za nyumba zao maarufu kama ‘Tegesha’ ili kujipatia faida kupitia thamani ya fidia.

Wathamni katika zoezi hilo walibaini tofauti kubwa katika uthamini walioufanya awali na pale walipoenda kwa mara ya pili kwa ajili ya uhakiki ambapo ilibainika baadhi ya vyumba katika nyumba zilizofanyiwa uthamini kuwa wazi baada ya waliokuwa wakiishi kuondoka baada ya kuthaminiwa.

Imeelezwa kuwa lengo wananchi wanaofanya ujanja wa ‘Tegesha’ ni kujipatia posho ya makazi ambayo kwa kawaida hutolewa kama fidia kwa wamiliki kulingana na idadi ya vyumba kwenye nyumba ya mmiliki.

Kwa mujibu wa Wathamini wa zoezi hilo, mbali na wamiliki walioathirika na zoezi hilo kulipwa gharama nyingine kama vile nyumba na mazao pia hulipwa posho ya makazi kwa kipindi cha miezi 36 lengo kumuwezesha mpangaji kupata mahali pa kuishi kabla ya kuanza zoezi la kuondolewa.

Mwandishi wa Gazeti hili alishuhudi moja ya nyumba iliyopo kitongoji cha Kigonga A katika kijiji cha Matongo ikiwa na vyumba ishirini na moja wakati nyumba hiyo ilistahili kuwa na vyumba vitatu na baadhi ya vyumba havina hata madirisha.

Mthamni Mkuu wa Serikali Evaline Mugasha ambaye alitembelea baadhi ya nyumba hizo kukagua maendeleo ya kazi ya uthamini katika eneo hilo aliweka wazi kuwa Ofisi yake inafanya kazi kwa kufuata sheria ya Uthamini na hatua kali zitachukuliwa kwa mtu atakayeonekana kufanya udanganyifu kwa kwa lengo la kujipatia kipato.

Kwa mujibu wa Mugasha, zoezi la uthamini katika eneo la Nyamongo linalohusisha vitongoji vitatu katika kijiji cha Matongo limekuwa likifanyika kwa uwazi na kushirikisha pande zote wakati wa kuorodhesha mali na kufafanua kuwa hata mwananchi asiyeridhika na uthamini katika eneo lake hupewa fomu maalum ya kujaza lengo likiwa kutoa haki.

‘’Tumeona watu walihamisha magodoro, vitanda na mizigo mingine lengo ni kupata posho ya makazi ili kujipatia faida na cha kushangaza baadhi ya wapangaji hawajui hata choo cha nyumba wanayoishi kilipo, ofisi yangu haitavumilia vitendo hivyo kila mtu atalipwa anachostahili’’ alisema Mugasha.

Mthamini kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Lazaro Magumba alieleza kuwa wakati zoezi la uthamini kumekuwa na changamoto hasa wakati wa kukagua mali za wananchi kutokana na baadhi yao kuwa na dhana ya kujipatia utajiri kupitia mradi huo ambapo hufanya maendelezo ya kuegesha maarufu kama ‘tegesha’ ili kulipwa fedha nyingi.

‘’ Wananchi wanajenga nyumba zilizopangana na hakuna hata nafasi na wakati wa uthamni usiku kucha watu wanahamisha vyombo, magodoro na wengine hata wanyama ili ionekane ni makazi halali’’ alisema Lazaro.

Alisema wanachokifanya wao ni kukagua kwa awamu kwa lengo la kujiridhisha kama kweli walionekana wakati wa uthamini kama ni wakazi halali ama walienda kutegesha.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Matongo wilayani Tarime mkoa wa Mara ambao hawakupenda majina yao yawekwe wazi kutokana na sababu za kiusalama walikiri kuwepo mchezo huo wa Tegesha lakini walidai hufanywa na watu wasio wakazi wa muda mrefu katika kijiji hicho bali walienda kwa lengo la kujipatia faida kupitia zoezi hilo.

Kwa mujibu wa wakazi hao, baadhi ya wananchi kutoka nje ya kijiji hicho walinunua nyumba ama maeneo kwa wenyeji na kuongeza vyumba na kuwakodisha watu kuishi ili kuvizia zoezi la uthamini wa fidia wapate faida.

Kwa muda mrefu wananchi wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoa wa mara hasa wale wanaoishi vitongoji vinavozunguka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara wamekuwa wakilalamikia uchafuzi wa mazingira hasa maji yanayovuja kutoka Mgodi huo kuwa yana sumu inayoathiri afya zao jambo lililomlazimu Rais John Pombe Magufuli wakati wa ziara yake katika eneo hilo kuagiza kufanyika utafiti ili kubaini ukweli huo.

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Waziri Mkuu Amsimamisha Kazi Mhandisi Morogoro ....Amwagiza Mkuu Wa Mkoa Aungalie Vizuri Mkoa Wake

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Ujenzi wa wilaya ya Morogoro, Brown Undule baada ya kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo,  ikiwemo usimamizi mbovu wa ujenzi wa kituo cha afya Mkuyuni.

Amemsimamisha kazi Mhandisi huyo leo (Jumatano, Septemba 18, 2019) baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Amesema hajaridhishwa na aina ya milango iliyotumika.

“Milango yote katika jengo hili ing’olewe leo leo, huwezi kuweka milango ya hovyo namna hii yaani mtu wa nje anamuona aliyeko ndani, nimesitisha kuendelea kukagua jengo. Yeye na usomi wake ameridhishwa na milango ya hovyo kama hii.”

Waziri Mkuu amesema aina ya milango iliyowekwa katika kituo hicho cha afya haiwezi kutumika hata kwenye nyumba ya mtu binafsi, lakini kutokana na uangalizi mbovu kutoka kwa watendaji walikubali kuweka milango hiyo mibovu.

Amesema Serikali imeamua kujenga vituo vya afya vitano kwenye wilaya hiyo ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi na kuwapunguzia kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya, hivyo amewataka watendaji wasimamie ipasavyo miradi hiyo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi, hivyo amewataka wananchi hao waendelee kuwa na imani na Serikali yao.

Baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya, Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa hospitali ya wilaya, ambako nako ameagiza kuong’olewa kwa mbao zote zilizotumika kwa ajili ya kupaulia jengo la mama na mtoto la hospitali hiyo kwa kuwa hazina viwango. “Fundi usiendelee na kazi hii ya upauaji kwa sababu mbao unazotumia hazikidhi viwango.”

Kwa upande wake, fundi anayejenga jengo hilo la mama na mtoto, Johnson Ishengoma amesema changamoto kubwa anayoipata katika ujenzi huo ni ucheleweshwaji wa vifaa pamoja na kulazimishwa kutumia vifaa vilivyo chini ya kiwango.

Fundi huyo ametolea mfano suala la mbao za kupaulia kuwa aliomba mbao za urefu wa futi 20 lakini aliletewa mbao zenye urefu wa futi 12 na kulazimishwa azitumie hivyo hivyo. “Mhandisi wa wilaya Brown Undule na mtu wa manunuzi Grace ndio wanaoniletea vifaa hivi. Baadhi ya vifaa huwa navikataa kutokana na kutokuwa na ubora.”

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe kuuangalia vizuri mkoa wake na kuhakikisha anauchunga vizuri kwa sababu umekithiri kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

“Wakati nikiendelea na ziara mkoani hapa, nimepata taarifa kwamba zaidi ya sh.milioni tisa zimetumika kwa ajili ya kilipana posho katika Halmashauri ya mji Ifakara . Posho hizo ni kwa ajili ya ziara ya Waziri Mkuu na imetoka kwa mtendaji wa kata ya Viwanja 60, hili jambo halikubaliki. Nakukabidhi risiti zote na uwachukulie hatua wote waliohusika. Mkoa wa Morogoro ni shida”

Wakingumzia kuhusu utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano na ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, wakazi wa Tarafa ya Mkuyuni wameipongeza Serikali kwa namna inavyowajali wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma.

Mmoja wa wananchi hao, Uwesu Mwichumu (71) mkazi wa  kijiji cha Kibungo  ameipongeza Serikali kwa usimamizi wa miradi na hatua inazochukua kwa baadhi ya watendaji wanaojihusisha na wizi wa fedha za umma.

Amesema Serikali inajitahidi kuwaletea miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao tatizo lililopo ni kwa watendaji wa chini. “Watendaji wengi huku chini wanashindwa kutekeleza majuku yao ipasavyo, wanashirikiana na wazabuni kuiibia Serikali.”

Mkazi mwingine wa Tarafa hiyo, Hanifa Shaban amesema anaishukuru Serikali kwa kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya na zahanati. Amesema awali walikuwa wanakwenda zahanati na kuandikiwa vyeti bila ya kupewa dawa , hivyo walilazimika kwenda kununua kwenye maduka ya dawa jambo ambalo kwa sasa halipo.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
Dalili:mwili kuchoka,maumivu ya mgongo na kiuno,kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu

Misuli  kulegea na kusinyaa hata kushindwa kufika kileleni miguu kuuma na kuwaka moto:

TIBA YAKE:

TULLO4 MIX.Ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizi hayo, inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kukufanya urudie tendo la ndoa zaidi mara tatu bila kuchoka au kukinai.

NTINJE3 PUMP.Ni dawa inayoongeza maumbile na kukupa umbile la kudumu.Itumie tiba hii kuokoa ndoa yako na kuokoa kukimbiwa na umpendae.
GASELA: Ni dawa mvuto kumvuta umpendae na kumrudisha alie mbali .

NTOBO: Inatibu KISUKARI:siku7 na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenyetatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari.

mpigie DR LIZENGO .OFISI IPO MBAGALA SABASABA.SIMU 0655283534/0621737576

Ofisi Ya Makamu Wa Rais Yatoa Elimu Ya Udhibiti Wa Kemikali Zinazoharibu Tabaka La Ozoni Kwa Maofisa Forodha.

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Faraja Ngerageza amesema kuwa  Matokeo ya kuharibika kwa Tabaka la Ozoni ni kuruhusu mionzi zaidi ya urujuani (UV-B) kufikia uso wa ardhi hivyo kutishia afya ya viumbe hai katika ikolojia mbalimbali.  Ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam wakati akifungua  warsha ya mafunzo kwa Maafisa forodha na Wasimamizi wa sheria Nchini kuhusu udhibiti wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni.

Aliongeza kuwa, Wanasayansi duniani wamethibitisha kuongezeka kwa magonjwa ya kansa ya ngozi, uharibifu wa macho kama vile "mtoto wa jicho" unaosababisha upofu, upungufu wa  uwezo wa mwili kujikinga na maradhi na kujikunja kwa ngozi hivyo mtu aweza kuonekana mzee kuliko umri wake. Pia watoto wako katika hatari zaidi ya kupata madhara haya. Madhara mengine ni pamoja na kuharibu fiziolojia ya mimea na michakato ya ukuaji wake na kusababisha mabadiliko katika muundo wa spishi, hivyo kusababisha mabadiliko ya bioanuwai katika ikolojia mbalimbali


Aidha katika kuhakikisha kuwa jukumu hili chini ya Sheria ya Mazingira linatekelezwa na kusimamiwa ipasavyo Ofisi ya Makamu wa Rais  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Maafisa forodha imekuwa ikijitahidi kujenga uwezo wa Taasisi mbalimbali katika kusimamia Kanuni za Udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la Ozoni za mwaka 2007 pamoja na kutoa vifaa katika mipaka yetu vinayowezesha kutambua gesi  hizi zinapoingizwa nchini. 

Ofisi ya Makamu wa Rais imekua na utaratibu wamara kwa mara  kuandaa warsha ya mafuzo kwa Maafisa Forodha na Wasimamizi wa sheria Nchini kote kuhusu udhibiti wa kemikali  ambazo zinzingizwa Nchini zinazoharibu tabaka la ozoni.   Warsha hiyo imehudhuriwa na Maafisa forodha wa mipaka yote Nchini kutoka katika Taasisi mbalimbali za Serikali.

Waziri Mkuu Amsimamisha Kazi Mhandisi Morogoro ....Amwagiza Mkuu Wa Mkoa Aungalie Vizuri Mkoa Wake

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Ujenzi wa wilaya ya Morogoro, Brown Undule baada ya kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo,  ikiwemo usimamizi mbovu wa ujenzi wa kituo cha afya Mkuyuni.

Amemsimamisha kazi Mhandisi huyo leo (Jumatano, Septemba 18, 2019) baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Amesema hajaridhishwa na aina ya milango iliyotumika.

“Milango yote katika jengo hili ing’olewe leo leo, huwezi kuweka milango ya hovyo namna hii yaani mtu wa nje anamuona aliyeko ndani, nimesitisha kuendelea kukagua jengo. Yeye na usomi wake ameridhishwa na milango ya hovyo kama hii.”

Waziri Mkuu amesema aina ya milango iliyowekwa katika kituo hicho cha afya haiwezi kutumika hata kwenye nyumba ya mtu binafsi, lakini kutokana na uangalizi mbovu kutoka kwa watendaji walikubali kuweka milango hiyo mibovu.

Amesema Serikali imeamua kujenga vituo vya afya vitano kwenye wilaya hiyo ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi na kuwapunguzia kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya, hivyo amewataka watendaji wasimamie ipasavyo miradi hiyo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi, hivyo amewataka wananchi hao waendelee kuwa na imani na Serikali yao.

Baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya, Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa hospitali ya wilaya, ambako nako ameagiza kuong’olewa kwa mbao zote zilizotumika kwa ajili ya kupaulia jengo la mama na mtoto la hospitali hiyo kwa kuwa hazina viwango. “Fundi usiendelee na kazi hii ya upauaji kwa sababu mbao unazotumia hazikidhi viwango.”

Kwa upande wake, fundi anayejenga jengo hilo la mama na mtoto, Johnson Ishengoma amesema changamoto kubwa anayoipata katika ujenzi huo ni ucheleweshwaji wa vifaa pamoja na kulazimishwa kutumia vifaa vilivyo chini ya kiwango.

Fundi huyo ametolea mfano suala la mbao za kupaulia kuwa aliomba mbao za urefu wa futi 20 lakini aliletewa mbao zenye urefu wa futi 12 na kulazimishwa azitumie hivyo hivyo. “Mhandisi wa wilaya Brown Undule na mtu wa manunuzi Grace ndio wanaoniletea vifaa hivi. Baadhi ya vifaa huwa navikataa kutokana na kutokuwa na ubora.”

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe kuuangalia vizuri mkoa wake na kuhakikisha anauchunga vizuri kwa sababu umekithiri kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

“Wakati nikiendelea na ziara mkoani hapa, nimepata taarifa kwamba zaidi ya sh.milioni tisa zimetumika kwa ajili ya kilipana posho katika Halmashauri ya mji Ifakara . Posho hizo ni kwa ajili ya ziara ya Waziri Mkuu na imetoka kwa mtendaji wa kata ya Viwanja 60, hili jambo halikubaliki. Nakukabidhi risiti zote na uwachukulie hatua wote waliohusika. Mkoa wa Morogoro ni shida”

Wakingumzia kuhusu utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano na ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, wakazi wa Tarafa ya Mkuyuni wameipongeza Serikali kwa namna inavyowajali wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma.

Mmoja wa wananchi hao, Uwesu Mwichumu (71) mkazi wa  kijiji cha Kibungo  ameipongeza Serikali kwa usimamizi wa miradi na hatua inazochukua kwa baadhi ya watendaji wanaojihusisha na wizi wa fedha za umma.

Amesema Serikali inajitahidi kuwaletea miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao tatizo lililopo ni kwa watendaji wa chini. “Watendaji wengi huku chini wanashindwa kutekeleza majuku yao ipasavyo, wanashirikiana na wazabuni kuiibia Serikali.”

Mkazi mwingine wa Tarafa hiyo, Hanifa Shaban amesema anaishukuru Serikali kwa kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya na zahanati. Amesema awali walikuwa wanakwenda zahanati na kuandikiwa vyeti bila ya kupewa dawa , hivyo walilazimika kwenda kununua kwenye maduka ya dawa jambo ambalo kwa sasa halipo.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa September 20

Biteko - Lazima dhahabu ya mgodi wa serikali iuzwe hapa nchini

$
0
0
Na Issa Mtuwa – Biharamulo Kagera. 
Waziri wa Madini Doto Biteko ameagiza mgodi wa dhahabu wa Mistamigold unaomilikiwa na Shirika la madini la Taifa STAMICO kuanzia Mwezi Desemba 2019 dhahabu inayozalishwa mgodini hapo iuzwe kwenye masoko ya dhahabu ya hapa nchini hususani kwenye soko la Biharamulo. 

Biteko amesema hayo  tarehe 19/09/2019 alipotembelea mgodi huo uliopo wilaya ya Biharamulo. Amesema aiwezekani serikali ihimize dhahabu yote iuzwe kwenye masoko ya ndani wakati mgodi wa serikali dhahabu yake inazwa Ususwi. 

“Naagia kuanzia Desemba mwaka huu, dhahabu yote inayo zalishwa katika mgodi huu iuzwe kwenye masoko ya ndani, mara baada ya mkataba wenu kuisha mwezi Novemba. Kwa kufanya hivyo gharama isiyo ya lazima mtaiepuka.” amesema Biteko. 

Wakati huo huo Biteko amemuagiza Afisa Madini Mkazi mkoa wa Kagera Mhandisi Lucas Mlekwa kuzifuta leseni 159 ambazo haziendelezwi ili zigawiwe kwa wanaohitaji kuendeleza leseni hizo na serikali ipate mapato yake. 

Awali, akitoa taarifa ya madini mkoa wa Kagera Mhandisi Mlekwa pamoja na mambo mengine alimwambia Waziri kuwa kuna changamoto nyingi kwenye mkoa wake pamoja na nyingine ni uwepo wa leseni nyingi zisizo endelezwa.  

Ameongeza kuwa kila anapo jaribu kufanya mawasiliano na wamiliki wa leseni hizo ili waendeleze hawapatikani.  

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa mgodi wa STAMIGOLD  Mhandisi Gray Shamika amemueleza Waziri jinsi mgodi unavyo endeshwa na kwa sasa wanajiendesha wenyewe kwa kugharamia gharama zote ikiwemo kulipa mishara ya watumishi na kulipa wazabuni. Amesema taarifa za kijiolojia zinaonyesha kuwa mgodi bado utaendelea kuishi pamoja na uwepo wa  changamoto mbalimbali zikiwemo za madeni. 

Akitoa taarifa yake kwa Waziri Mhandisi Shamika amesema, kwa sasa Mgodi upo kwenye utaratibu kuanzisha mradi wa kuchenjua Visusu (Tailings) mradi utakao upa uhai wa mgodi hadi miaka 7-10 ijayo. Kuhusu kupunguza gharama za uzalishaji Shamika amesema mgodi umepunguza gharama za uzalishaji kutoka 1800 hadi 940 kwa wakia (Ounce) moja. 

Kufuatia taarifa hiyo, Waziri Biteko ameupongeza uongozi na wafanyakazi wote kwa hatua hiyo na kuwaomba kuendela kupunguza gharama hiyo angalau kufikia 800 kwa wakia.  

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Brigadia Jenerali Silvester Ghuliko amesema wako teyari kutekeleza maagizo ya Waziri na walisha anza kujipanga kutekeleza maagizo hayo hususani kuanza kuuza dhahabu katika soko la ndani mara baada ya mkataba wa kuuza dhahabu nje kumalizika mwezi Novemba mwaka huu.  

Akimkaribisha Waziri wa Madini, Katibu Tawala wa Wilaya ya Biharamumo ambae ni Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Agness Alex amemwambia waziri hali halisi ya sekta ya madini wilayani humo pamoja na changamoto mbalimbali ikiwemo deni la Halmashauri yake kwa mgodi huo.  

Kufuatia hoja hiyo ya deni la Halmashauri, Biteko amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Biharamulo Ionde Ng’ahala kutuma timu ya wahasibu wake kwenda STAMIGOLD kukaa na uongozi kupitia deni hilo na kuhakiki na kukubaliana namna ya kulipa deni hilo. 

Waziri Mkuu : Sadc Tuweke Sera Na Viwango Vya Aina Moja Kurahisisha Usafirishaji Wa Bidhaa Naukuzaji Biashara

$
0
0
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuwa kuwa na mipango, sera, viwango na mifumo ya pamoja ya kisheria itakayorahisha utoaji wa huduma za usafirishaji wa bidhaa na kukuza biashara ndani ya Ukanda huo.

Akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya hiyo wanaosimamia sekta za Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa jana Alhamisi (Septemba 19, 2019) Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka Mawaziri hao kutumia mkutano kuandaa mapendekezo ya suluhisho la changamoto ya nnjia bora za kuimarisha mtandao wa biashara ndani ya sadc.

Majaliwa alisema Tanzania kwa upande wake imekuwa mstari wa mbele katika nja wanachama wa SADC katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji ikiwemo kuboresha bandari ya Dar es Salaam ambayo kwa sasa imekuwa ikihudumia  Nchi mbalimbali za Jumuiya ya SADC ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Kongo, Malawi na Zambia pamoja na Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aliongeza kuwa Tanzania pia imeendelea na ujenzi na reli ya kisasa inayojengwa katika Ukanda wa kati pamoja na ujenzi wa reli ya Tazara inayonganisha Tanzania na  Zambia, na kutaja juhudi hizo ni moja ya mikakati ya Tanzania ya kuhakikisha inaimarisha mtandao wa biashara ndani ya Jumuiya hiyo.

“Katika Ukanda wa reli ya Tazara kwa sasa tumeweza kuongeza kiwango cha usafirishaji kutoka tani 88,000 mwaka 2014/2015 hadi kufikia tani 220,000 mwaka 2017/2018 pamoja pia na kujenga Meli 2 za mizigo katika Ziwa Nyasa zenye uwezo wa kubeba tani 200” alisema Majaliwa

Akizungumzia kuhusu Maendeleo ya Sekta ya Tehama katika Ukanda wa SADC, Majaliwa alisema Nchi hizo hazina budi kufikia malengo yaliyowekwa katika Mkutano Windohoek Nchini Namibia mwaka 2018 wa kuhakikisha kuwa kunawepo na Intaneti yenye kasi kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kibiashara na utoaji huduma kwa wananchi ifikapo mwaka 2023.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya  Shirika la Mawasiliano  Duniani (ITU) zinaonesha kuwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasliano katika Nchi za SADC imekuwa na kufikia asiliami 22.3 ikilinganisha na kiwango cha dunia ambacho ni asilimia 51, na hivyo kuwa katika kiwango cha juu ikilinganishwa na kiwango kilichowepo katika miaka ya 2000.

Akifafanua zaidi Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka Mawaziri hao kuweka mkazo katika kujadili kiwango cha matumizi na umuhimu wa kuunganisha Intaneti ili kuweza kuongeza kasi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa Jumuiya hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alisema kutokana na Nchi za SADC kuwa na changamoto zinazoshabihiana katika masuala ya hali ya hewa, Tehama, Uchukuzi na Habari, Mkutano wa Mawaziri hao umepanga kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kuimarisha ustawi wa wananchi wake.

Aidha aliongeza kuwa Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri wa Nchi 8 za Jumuiya hiyo ikiwemo Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji, Zambia, Afrika Kusini, Lesotho, Zimbambwe, Tanzania ambapo Mawaziri hao katika Mkutano wao wa siku mbili wanatarajia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo maazimio yaliyopitishwa katika Mkutano Mkuu wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya hiyo uliofanyika Agosti 17-18 mwaka huu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma wa SADC, Rosemary Mokoena alisema Mkutano huo wa Mawaziri unatarajia kujadili masuala mbalimbali ambayo ni muhimu katika utekelezaji wa Mipango Mkakati mbalimbali iliyopangwa kutekelezwa na jumuiya hiyo katika kuimarisha mifumo ya biashara na huduma mbalimbali ndani ya SADC.

MWISHO

Waziri wa Kilimo Aiagiza TFRA Kuhakikisha Mbolea Inapatikana Kwa Bei Nafuu

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imeiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mbolea inapatikana kwa wakati na bei nafuu.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo  tarehe 18 Septemba 2019 wakati akifunga mkutano mkuu wa Wakala wa usambazaji wa mbolea Tanzania (TADCOs) katika ukumbi wa Polisi Jamii Jijini Dodoma.

Mhe Hasunga amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti uwepo wa pembejeo feki nchini.

Alisema Kwa upande wa mbolea, tayari Wizara ya Kilimo imetoa mafunzo na kuwapitisha Wakaguzi 50 wa mbolea ambao wanaenda kuongeza nguvu kwa kufanya kazi nchi nzima za kudhibiti ubora wa mbolea.

Mhe Hasunga alisema kuwa kwa upande wa Viuatilifu, ameiagiza Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa Viuatilifu ukanda wa Kitropiki (TPRI) kuhakikisha wanafanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini na kuondoa viuatilifu feki vyote sokoni.

Aidha, tayari Wizara imeridhia na kuwapitisha Wakaguzi (Inspectors) 45 wa kukagua viuatilifu ambao nao wanaenda kuongeza nguvu nchi nzima kuhakikisha tatizo la viuatilifu feki linamalizika.

Kadhalika Mhe Hasunga amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kudhibiti na kuondokana na changamoto ya uwepo wa pembejeo ambazo hazikidhi viwango.

Katika mkutano huo Mhe hasunga ameupongeza uongozi wa TADCOs kwa mwanzo mzuri wa kiuongozi hususani kuwasomea wananchama wao mapato na matumizi hukuakitoa rai kwa Viongozi wote, kuhakikisha wanaendesha chama hicho kwa ufanisi mkubwa, uwazi na uwajibikaji kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za ushirika nchini.

Aliongeza kuwa ana matarajio kwamba, kuanzishwa kwa chama hicho cha Ushirika kutapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zilizokuwepo na kusaidia kuwanufaisha wakulima kwa kuagiza na kusambaza  pembejeo zenye ubora, kwa wakati na bei nafuu.

“Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwakomboa wakulima nchini kwa kuhakikisha wanazalisha mazao yao kwa tija ili waweze kuinua hali zao za maisha na kuchangia uchumi wa nchi.  Ni ukweli usiopingika kuwa azima hii hawezi kufikiwa kama wakulima hawatapata pembejeo zenye ubora, kwa wakati na kwa bei nafuu” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

“Dhamana mliyonayo  ni kubwa sana, hivyo ni matarajio yangu kuwa mtatimiza jukumu lenu kuu la kuhakikisha mnasimamia usambazaji wa pembejeo za kilimo wakulima wa Tanzania walio wanyonge kwa uaminifu na uweledi mkubwa.”

Aliwataka (TADCOs) kufuata Sheria, kanuni na taratibu zote zinazohusu uendeshaji wa biashara ya pembejeo nchini na kuzingatia kanuni za ushirika.  Aidha, kushirikiana na Taasisi zote zinazodhibiti na kusimamia tasnia ya pembejeo na ushirika nchini kama vile TFRA, TPRI, ASA, TOSCI, TCDC na TFC ili waweze kuwasaidia wakulima kupata pembejeo zenye ubora.

Ili kupunguza gharama na kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo sahihi, kwa wakati na bei nafuu, Mhe Hasunga aliwaagiza Viongozi wenu wa TADCOs kusimamia vilivyo zoezi la uagizaji wa pembejeo kwa pamoja, moja kwa moja kutoka viwandani na si kwa wauzaji wa kati. 

MWISHO

Iran yaonya dhidi ya shambulio dhidi ya nchi yake

$
0
0
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran amesema shambulio lolote dhidi ya nchi yake, kufuatia hujuma dhidi ya miundombinu ya mafuta ya Saudi Arabia litasababisha vita kamili na kuongeza mvutano katika Guba ya uajemi.

Tamko hilo la waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammed Javad Zarif, limewakilisha onyo kali la Iran katika kipindi kirefu cha kiangazi, kilichogubikwa na mashambulio na matukio kadhaa ya kukanganya kufuatia kuporomoka kwa makubaliano yake ya nyuklia na mataifa yalio na nguvu duniani baada ya rais Donald Trump kuiondoa Marekani katika makubaliano hayo.

Tamko lake hilo pia linaangaliwa kama jibu kwa Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo ambaye siku moja iliyopita alipokuwa akielekea Saudi Arabia aliyataja mashambulio hayo kama "tukio la vita.”

Alipoulizwa na shirika la habari la CNN ipi athari ya shambulio la Marekani na Saudi Arabia kwa taifa lake, Zarif alisema anatoa taarifa muhimu kwamba Iran isingelipenda kuingia katika majibizano ya kijeshi lakini pia akasema hawatofumba macho kulilinda taifa la Jamhuri ya Iran.

Ameongeza kuwa vikwazo vyovyote vilivyowekwa na Marekani kwa taifa lake baada ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia, inabidi viondolewe kabla ya kufanyika majadiliano ya aina yoyote, huku akisema Marekani imefanya kila iwezalo lakini bado haijaifikisha Iran kuinyenyekea kwa kuipigia goti.

Rais wa zamani waTunisia Zine Abidine ben Ali afariki dunia uhamishoni Saudi Arabia

$
0
0
Rais wa zamani wa Tunisia, Zine Abidine ben Ali aliyeitawala nchi hiyo kwa zaidi ya miongo miwili amefariki dunia uhamishoni nchini Saudi Arabia.

 Habari hizo zimetangazwa na wakili wake. Zein Alabidini ben Ali aling'olewa madarakani kufuatia vuguvugu la wapenda demokrasia nchini humo la mwaka 2011.

Rais wa shirikisho la vyama vya wafanya kazi Tanzania TUCTA Azungumzia Ongezeko Kubwa la Wafanyakazi Kuomba Kustaafu Kwa Hiari

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Rais wa shirikisho la vyama vya wafanya kazi Tanzania TUCTA ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania TALGWU bw.Tumaini Nyamhokya,amesema ni haki ya mfanyakazi kustaafu kwa hiari hivyo shirikisho halina tamko kwa wafanya kazi kutokana na habari zilizoenea mitandaoni kuwa watumishi wengi wameanza kuomba kustaafu kwa kuhofia KIKOKOTOO.

Rais wa TUCTA ameyasema hayo mkoani Njombe wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania TALGWU mkoa wa Njombe ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili ukiambatana na uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.

“Nimeulizwa na waandishi wa habari wengi kwamba watumishi wanastaafu kwa hiari wanakuwa na hofu,kustaafu kwa hiari kupo kwa mujibu wa sheria,mtu akiona atumie kustaafu kwa hiari ili apate fedha afanye mambo yake mengine hilo ni jambo jingine,na kama kuna mtu ameamua kustaafu kwa hiari ili asifike kule ambako kuna sintofahamu kwamba kuna KIKOKOTOO gani kitafuatia hiyo pia ni haki yake kwa mujibu wa sheria”alisema Nyamhokya

Nyamhokya ameongeza kuwa shirikisho hilo halina tamko la kuwaondoa hofu wafanyakazi.

“Kwa hiyo sisi hatuna tamko lolote la kuwaambia wafanyakazi,hatuna tamko lolote la kuwaondoa hofu,hofu ilikuwepo kubwa sana wakati kikokotoo kimebadilika na kikaja  kikokotoo ambacho kiukweli tunakiita kikokotoo kandamizi katika masalahi ya wafanyakazi hasa wale ambao wamekuwa wamestaafu sasa tumerejeshewa kiu na tumepewa muda wa miaka mitano tuweze kusimamia na kuandaa kwa hiyo timu zipo na zinaendelea kufanya kazi kuhakikisha tunaandaa kikokotoo ambacho kitakuwa rafiki kwa pande zote Mbili”aliongeza Nyamhokya

Katika hatua nyingine Nyamhokya amesema bado kuna badhi ya viongozi wa serikali na wanasiasa ambao wamekuwa wakifanya kazi za kimihemko na kuwaumiza watendaji hali ambayo inasababisha kuvunjika moyo kiutendaji.

“Sehemu kubwa viongozi wanakwenda vizuri lakini kuna baadhi ya wanasiasa ambao ni wateule wa mheshimiwa Rais, sisi kama viongozi wa vyama tunaona hawatendi vyema,baadhi tumeona wana hulka ya kuchukua hatua zinaonekana kuwa za kinidhamu kwenye majukwaa,utaona wanatamka simtaki mtumishi huyu mkoani kwangu,au wanasema kuanzia sasa wewe sio mkuu wa idara kiukweli inaumiza sana”alisema Nyamhokya

Serikali Yaonya Mifugo Kutoka Nje Ya Nchi Kuingizwa Nchini Kwa Ajili Ya Malisho

$
0
0
Serikali imewaonya wafugaji wanaoishi katika mipaka ya Tanzania na nchi jirani kutoingiza mifugo ya raia wa nchi za jirani hapa nchini kwa ajili ya malisho na kuiweka katika vitalu walivyopewa kwenye ranchi za taifa na kutoa taarifa za uongo kuwa mifugo hiyo ni yao kwa kuwa atakayebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema hayo katika Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo ambapo amebaini baadhi ya wafugaji wamekuwa wakikiuka sheria za nchi kwa kuchukua mifugo ya wafugaji wengine kutoka katika nchi za jirani na kuiweka kwenye ranchi hizo kwa ajili ya malisho ilhali wafugaji wengi nchini bado wanahitaji maeneo ya kulishia mifugo yao.

“Kwanza hairuhusiwi ng’ombe kutoka nje ya mipaka yetu kuingia nchini kuvuna majani na malisho ya hapa ndani ya nchi yetu kwa sababu sisi wenyewe tuna migogoro ya wakulima na wafugaji wetu ambayo hatujaimaliza na moja ya mikakati ni kuamua kutoa vitalu ili wafugaji wa Tanzania waweze kulisha mifugo yao atakayebainika kutofuata sheria za nchi atachukuliwa hatua za kisheria.” Amsesma Mhe. Ulega

Aidha Mhe. Ulega amesema mikakati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni kuhakikisha Tanzania inaondokana na vikwazo vyovyote vilivyopo katika baadhi ya nchi kutonunua nyama kutoka hapa nchini kutokana na sababu zisizo sahihi kuwa mifugo ya Tanzania ina maradhi.

Kwa upande wake Meneja wa Ranchi ya Missenyi Bw. Oscar Mengele amesema ng’ombe waliopo katika ranchi hiyo wana afya njema na wamekuwa wakipatiwa dawa na kinga dhidi ya maradhi mbalimbali hivyo kuwa katika hadhi ya soko la kimataifa na kuwaasa wananchi kutangaza vyema nje ya nchi bidhaa zitokazo hapa nchini.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiwa katika Ranchi ya Missenyi Mkoani Kagera katika ziara yake ya kikazi mkoani humo amepata fursa ya kuzungumza na wawekezaji waliopatiwa vitalu vilivyopo katika Ranchi ya Missenyi na kumuagiza Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Ugani na Mafunzo kutoka katika wizara hiyo Dkt. Angello Mwilawa kuratibu zoezi la elimu ya ufugaji bora kwa wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi zote zilizopo hapa nchini pamoja na kutafuta teknolojia ya kisasa yenye gharama nafuu kwa ajili ya kuogeshea mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali ambayo wawekezaji hao wanaweza kununua.

Mwisho.
Imetolewa: Kitengo cha Mawasiliano serikalini
     Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Serikali yaagiza Halmashauri zote za mkoa wa Shinynaga kujenga maeneo ya Maegesho ya malori ya mizigo kabla ya octoba 25 mwaka huu.

$
0
0
NA SALVATORY NTANDU
Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Shinyanga wametakiwa kujenga maaeneo ya maegesho ya malori ya mizigo na mafuta ambayo yemekuwa yakiengeshwa katika maeneo yasiyorasimi(makazi ya watu) hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa wananchi kabla ya octoba  25 mwaka huu

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack kwenye kikao cha robo ya pili ya bodi ya barabara mkoa wa shinyanga, na kusema kuwa kumekuwa na tabia ya uegeshaji holela wa malori ya  katika makazi ya watu huku mengine yakiwa na kemikali hatari kama vile gesi na mafuta.

Amesema serikali haiwezi kukubali hali hiyo huku wenye mamlaka ya kusimamia na kupanga maeneo ya miji na wilaya wakiwa hawatimizi wajibu wao na kuendelea kuruhusu uegeshaji holela wa malori hayo ambao ni hatari kwa maisha  kwa uslama wa wananchi wa mkoa huo.

Amefafanua kuwa utengaji wa maeneo ya malori ya mizingo kwenye halmashauri za mkoa wa shinyanga kutaongeza mapato  kutokana na malori hayo na pia itawawezesha wamiliki wa malori hao kutoibiwa vifaa vyao vya magari katika vituo hivyo kwani  katika maeneo hayo kutakuwa na ulinzi wa kutosha.

Michael Matomora ni mkurugenzi wa Halamshauri ya Ushetu na Godfrey Mwangulumbi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga wamesema katika bajeti ya mwaka 2018/19 hawakutenga bajeti kwaajili ya kutenga maeneo hayo lakini kwa mwaka huu wa fedha watahakikisha agizo hilo linatekelezwa harasa.

Naye Kaimu Meneja wa TANROAD mkoa wa Shinyanga Mhandisi, Mibara Ndilimbi amesema kwa sasa Wakala  huo unaendelea kujenga eneo la maengesho la Kagonjwa Isaka ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi sambamba na kuboresha eneo la Maegesho la Mjini Kahama.

Ujenzi Wa Mahandaki Yatakayopitisha Reli Ya Kisasa – Sgr Katika Milima Ya Kilosa Wazidi Kunoga

$
0
0
Maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha awamu ya pili Morogoro -Makutopora Singida wazidi kunoga umefikia zaidi ya 15% , ujenzi huu unaambatana na ujenzi wa Mahandaki 4 yatakayokuwa na jumla ya urefu wa Kilomita 2.6

Maendeleo ya ujenzi wa mahandaki washika kasi katika Milima ya Kilosa ambapo zaidi ya Mita 470 kati ya Mita 1030 zimechorongwa katika handaki namba 2, ujenzi wa handaki hilo umefika 45% hivi karibuni Septemba 2019.

Mpaka sasa wataalamu wanaendelea na hatua za ujenzi wa handaki hilo ambazo ni kuchoronga na kuimarisha kuta za handaki kwa kufunga nondo (reinforcement work) na kuweka zege kali (shotcrete application) ambapo hivi sasa kazi kubwa inayofanyika ni kuchimba Mita tatu kwenda chini ndani ya handaki ili kukamilisha urefu wa Mita 9.6 za handaki katika Kazi ya Uchorongaji wa Mahandaki iliyozinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Atashasta Nditiye mapema Julai 22, 2019.

Sambamba na kazi kuanza rasmi baada ya maandalizi ya uchorongaji kukamilika katika eneo ambalo handaki namba 2 linajengwa. Katika hatua nyingine wahandisi wanaendelea na maandalizi ya uchorongaji wa handaki namba 1 litakalokuwa na urefu wa Mita 424, mahandaki haya yote yataunganishwa na Madaraja marefu ili kuepusha athari za mto Mkondoa ambao umekuwa ukiathiri miundombinu ya reli za zamani mara kwa mara.

Kukamilika kwa ujenzi wa Handaki namba mbili kati ya mahandaki 4 yanayojengwa eneo la Kilosa kutalifanya Hanadaki hilo kuwa la kwanza kwa urefu hapa Tanzania. Ujenzi wa Mahandaki katika eneo la Kilosa unatokana na Jiografia ya eneo lenye milima mingi na uwepo wa mto Mkondoa.

Usanifu huu wa ujenzi wa reli ya kisasa -SGR unaondelea nchini, kutokana na changamoto za kijiografia utakua chachu wa kuilinda miundombinu ya reli ili isipate madhara hasa katika kipindi cha mvua kali.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images