Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Simbachawene Aagiza Taasisi Ziandae Mazoezi Ya Upandaji Miti Zinapofanya Hafla Mbalimbali

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. George Simbachawene ameagiza taasisi ziwe zinaandaa utaratibu wa upandaji miti wakati wa matukio au sherehe mbalimbali hatua itakayohakikisha utunzaji wa mazingira unafanyika kwa ufanisi.

Pia amezitaka taasisi za umma, binafsi na za dini kuhakikisha zinaandaa vitalu vya miche ya miti na kugawa kwa wananchi waende kupanda akisema kuwa utaratibu huo utasaidia katika kuhakikisha kunakuwa na ongezeko la miti nchini.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Pwaga wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe Mkoani Dodoma, Mhe. Simbachawene alisema wastani wa ukataji miti kwa mwaka ni 496,000 ambao unatokana na shughuli za kibinadamu, hali inayochangia uharibifu wa mazingira na kwa hali hiyo jukumu la kupanda miti ni la kila mtu.

“Nitafurahi kuona kiongozi yeyote anapofanya ziara mahali popote anaandaliwa utaratibu wa kupanda miti halafu ndio ahutubie mkutano na kwa kufanya hivyo tutaweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zinazotokana na kukosekana kwa miti na hapa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 inasema kila mtu ni taasisi ya mazingira hivyo ni lazima apande mti,” alisisitiza Waziri.

Kwa hali hiyo Mhe. Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe alitahadharisha kuwa matumizi ya mkaa kwa kiasi kikubwa yanachangia upotevu wa misitu yetu kwani unahusisha ukataji wa miti ya asili ambayo huleta mvua na uaoto wa asili.

Aidha, katika ziara hiyo Kijijini hapo pamoja na mambo mengine mara baada ya kuwasili Waziri huyo aliongoza zoezi la upandaji miti kwenye eneo la Kituo kipya cha Afya cha Pwaga kwa pamoja na viongozi mbalimbali Wilayani humo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Paul Sweya.

Waziri huyo alibainisha kuwa shughuli za kibinadamu ni nyingi na harakati za kutafuta maisha zinazosababisha akate miti kwa wingi zimeongezeka na hivyo kumfanya aharibu mazingira kwa kukata miti hivyo ni lazima sasa tulinde misitu yetu kwani ndio uhai wetu.
 
Kutokana na hilo aliwataka wananchi kuacha mara moja kuvichezea vyanzo vya maji huku na kutaka uwekwe msukumo zaidi kwa wananchi kuhusu suala zima la utunzaji mazingira na kuwa elimu itolewe kuanza ngazi ya shule za msingi ili wanafunzi wapate uelewa.

“Miti ni muhimu sana kwani kusaidia kupunguza mabadiliko ya tabianchi tena wataalamu wanasema ni vizuri kupanda miti ya asili kwani ina uwezo mkubwa wa kunyonya hewa ya kaboni ambayo ikiungana inatengeneza gesi joto ambayo inasababisha tabaka la ozone linalosababisha joto kubwa duniani,” aliasa Mhe.Waziri.


Naibu Waziri Ulega Atoa Miezi Mitatu Kuondolewa Changamoto Za Soko La Nyama Nje Ya Nchi

0
0
Serikali imesema itahakikisha katika kipindi cha miezi mitatu ijayo changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi kwenye soko la nyama nje ya nchi zinatatuliwa ili kuhakikisha wafugaji wananufaika kupitia mifugo yao kupitia soko la nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema hayo katika Ranchi ya Kikulula iliyopo Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera wakati akizungumza na wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi hiyo, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo, ambapo amesema baadhi ya masoko nje ya nchi hushindwa kununua nyama kutoka Tanzania kwa madai yasiyo sahihi kuwa mifugo iliyopo nchini ina maradhi.

Akizungumza na wawekezaji takriban 33 waliopewa vitalu katika ranchi ya Kikulula iliyopo Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera, Naibu Waziri Ulega amesema katika kipindi cha miezi mitatu ijayo ni lazima vikwazo vilivyopo katika soko la nyama nje ya nchi viwe vimetatuliwa kwa wawekezaji kwenye vitalu kuwa na mipango maalum ya ufugaji ili wakaguzi kutoka nje ya nchi wakija kukagua ubora wa mifugo nchini wapate taarifa sahihi itakayowezesha mifugo na nyama itokanayo na mifugo hiyo ipate soko nje ya nchi kwa kuwa na afya bora.

Aidha Waziri Ulega amesema Ranchi ya Kikulula lazima iendelezwe na kuwa ya mfano kwa kuwekewa mikakati mbalimbali ili iweze kuwa na tija kwa mfugaji na taifa kwa ujumla pamoja na kuwataka wawekezaji kuendeleza vitalu vyao kwa kuweka miundombinu imara bila kuwa na hofu ya uwepo wa mkataba wa muda mfupi wa mwaka mmoja.

Nao baadhi ya wawekezaji katika Ranchi ya Kikukula wameiomba serikali kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo ya ufinyu wa maeneo ya mifugo yao huku wakiipongeza kwa namna inavyoboresha sekta ya mifugo nchini.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) Prof. Phillemon Wambura akijibu hoja hizo amewataka wawekezaji kuhakikisha wanapata vitalu kwa misingi ya kisheria.

Awali Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega mara baada ya kuwasili mjini Bukoba alipata nafasi ya kukutana na mkuu wa mkoa huo brigedia jenerali Marco Gaguti ambapo ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufanya utafiti namna wafanyabiashara wanavyoweza kunufaika na mabaki ya samaki yakiwemo mabondo.

Naibu Waziri Ulega yupo Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo katika siku ya kwanza ametembelea ranchi za Kikulula na Mabale pamoja na kuzungumza na wawekezaji katika ranchi hizo na kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Katanda kilichopo Kata ya Kihanga, Wilayani Karagwe.

 Mwisho.

Imetolewa: Kitengo cha Mawasiliano serikalini
     Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Waziri Mkuu: Tutatekeleza Ahadi Zote Zilizotolewa Na Rais

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ahadi zote zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli ikiwemo ujenzi wa barabara ya Mikumi-Ifakara kwa kiwango cha lami zitatekelezwa, hivyo amewataka wananchi waendelee kuiamini Serikali yao.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumanne, Septemba 17, 2019) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa Mji wa Ifakara pamoja na wilaya ya Kilosa alipokuwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

“Kila alichokiahidi Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli nitakisimamia kuhakikisha kinatekelezwa, hivyo wananchi endeleeni kuiamini Serikali yenu. Serikali yenu ipo makini na ina dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo kama Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2015-2020 inavyoelekeza.”

Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli iko makini na inaendelea kuchapa kazi kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwenye maeneo mbalimbali nchini yakiwemo na mkoa wa Morogoro.

Pia, Waziri Mkuu alisema kila mtumishi wa umma anatakiwa ahakikishe anafanya kazi kwa bidii ili kuiwezesha Serikali kutimiza lengo lake la kuboresha maendeleo ya wananchi kwenye maeneo mbalimbali nchini hususani ya vijijini.

Waziri Mkuu alisema iwapo watumishi wa umma watatimiza majukumu yao ipasavyo changamoto nyingi zinazowakabili wananchi kama upatikanaji wa maji zitakuwa historia kwa kuwa Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Alisema watumishi wa umma wanapaswa kuwa na nidhamu ya fedha za Serikali zinazopelekwa katika maeneo kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ikiwemo ya afya, elimu na maji. “ Sina mzaha na watakaotafuna fedha hizo.”

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Yakanusha Kuhusu Taarifa Ya Sarafu Ya Shilingi 3,000

0
0
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kukanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kwamba mwezi Julai 2019 ilitoa sarafu ya kumbukumbu ya visiwa vya Dokdo yenye thamani ya shilingi 3000. 

Benki Kuu inapenda kuufahamisha umma kuwa taarifa hizo si za kweli na kwamba sarafu hiyo siyo mali ya Benki Kuu ya Tanzania na haijatolewa na Benki Kuu kwa njia yoyote ile na wala Benki Kuu haijawahi kuingia mkataba na kampuni yoyote kutoa sarafu hiyo.

Wimbo Mpya wa Aslay – Naenjoy

0
0
Wimbo Mpya wa  Aslay – Naenjoy

VIDEO : Mbosso Ft. Reekado Banks – Shilingi

0
0
 VIDEO : Mbosso Ft. Reekado Banks – Shilingi

IGP Sirro afanya mabadiliko kwa RPC Wanne

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amefanya mabadiliko ya kikazi kwa Makamanda wakuu wa Mikoa minne hapa nchini.
 
Taarifa iliyotolewa  Septemba 17 na Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime, imeeleza kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida katika uboreshaji wa utendaji wa kazi kwa jeshi hilo.

Mabadiliko hayo yamemhusisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa aliyehamishiwa Makao Makuu na nafasi yake imejazwa na Hamis Issah aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro.

Makamanda wengine ni pamoja na Saidi Hamdani aliyekuwa Njombe, ambaye amehamishiwa Kilimanjaro na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Geita, Daniel Sillah anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe.

Makusanyo Ya Mapato Yameleta Mageuzi Ya Huduma Za Afya Tamisemi

0
0
Na Ismail Ngayonga,MAELEZO
UKUSANYAJI wa mapato ni moja ya vipaumbele muhimu vya Serikali ya Awamu ya Tano katika  kujenga uwezo wa ndani wa kujitegemea na kupunguza kwa kadri inavyowezekana utegemezi kutoka kwa Wadau wa Maendeleo.

Aidha, azma ya Serikali ya kuifanya Tanzania nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, haiwezi kufikiwa endapo Serikali haitokuwa na uwezo wa kifedha wa kugharamia shughuli mbali mbali za maendeleo.

Takwimu zilizopo zinaonesha tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani mwaka 2015, kumekuwepo na ongezeko la makusanyo kwa mwezi kutoka Tsh Bilioni 800 hadi kufikia Tsh Trilioni 1.3 kwa mwezi kutokana na mwitikio chanya wa wananchi wa kulipa kodi na usimamizi makini katika ukusanyaji mapato.

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inatekeleza Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 unaozingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano Awamu ya Pili wa Mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 na Agenda ya Dunia ya Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Mwaka 2030.

Katika Mwaka wa Fedha 2018/2019, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Tume ya Utumishi wa Walimu, Mikoa na Halmashauri iliidhinishiwa jumla ya Tsh Trilioni 6.58 kwa ajili ya Mishahara, Matumizi Mengineyo na Miradi ya Maendeleo, ambapo Kati ya fedha hizo, Tsh trilioni 4.13 ni Mishahara, Tsh Bilioni 649.3 ni Matumizi Mengineyo na Tsh trilioni 1.80 ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi, kwa mwaka 2019/2020, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo anasema katika mwaka 2018/19, Halmashauri Halmashauri ziliidhinishiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 735.6 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya ndani.

Waziri Jafo anasema  hadi kufikia Februari, 2019, Halmashauri zilikuwa zimekusanya jumla ya Tsh Bilioni 392.90 sawa na asilimia 53 ya makadirio, ambacho ni sawa na ongezeko la Tsh Bilioni 111.6 ikilinganishwa na kiasi cha Tsh Bilioni 281.3 zilizokusanywa hadi Februari, 2018.

“Ongezeko la makusanyo limechangiwa na kuimarishwa kwa usimamizi na udhibiti, elimu na hamasa kwa walipa kodi na matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato pamoja na mkakati uliowekwa na Ofisi ya Rais- TAMISEMI wa kuzishindanisha Halmashauri kila robo mwaka” anasema Waziri Jafo.

Kwa mujibu wa Waziri Jafo anasema kutokana na mageuzi hayo ya ukusanyaji mapato Ofisi ya Rais TAMISEMI imeendelea kutekeleza vyema mpango wa utoaji huduma bora za afya na kuharakisha Maendeleo ya wananchi kwa kuwa na Hospitali kila Wilaya, Kituo cha Afya kila Kata na Zahanati kila Kijiji.

Akizungumzia kuhusu Mpango wa Maboresho ya Huduma za Afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Waziri Jafo anasema katika Mwaka wa Fedha 2018/2019, ziliidhinishwa jumla ya shilingi bilioni 100.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali 67 za Halmashauri.

Anaongeza kuwa Hadi Februari 2019, fedha zote zilikuwa zimepokelewa kwenye Halmashauri na ujenzi unaendelea kwa kutumia utaratibu wa “Force Account” kwa kuzingatia Kanuni ya 167 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma za mwaka 2013 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016.

Kuhusu hospitali za Halmashauri, Waziri Jafo anasema ujenzi unahusisha majengo saba ambayo yamejengwa kwa kutumia shilingi bilioni 1.5 kwa kila Halmashauri zilizowekwa kwa kila Halmashauri. Majengo hayo ni ya Utawala, majengo ya nje, stoo ya madawa, maabara, jengo la mionzi, jengo la kufulia na jengo la wazazi.

Akifafanua zaidi Waziri Jafo anasema katika mwaka wa fedha 2018/2019, Ofisi ya Rais, TAMISEMI imeendelea na ujenzi, ukarabati na ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma afya 352 ikihusisha ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto, nyumba moja ya mtumishi, jengo la wagonjwa wa nje na chumba cha kuhifadhia maiti.

“Serikali imeendelea kutoa fedha nyingi kwa kutumia utaratibu wa “Force Account” ambapo gharama zimepungua kutoka Shilingi bilioni 2.5 hadi Tsh Milioni 400 au 500 kwa kila Kituo cha Afya na Serikali pia metoa jumla ya Shilingi bilioni 41.6 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba sambamba na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa usingizi zaidi ya 200 kwa ajili ya kuimarisha huduma na upasuaji kwenye vituo vya afya” anasema Waziri Jafo.

Waziri Jafo anasema katika kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana, Ofisi ya Rais, TAMISEMI imeratibu uanzishwaji wa Mfumo wa Mshitiri katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara ikiwa ni utekelezaji wa Awamu ya Nne ya Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya na kuviwezesha vituo vya kutolea huduma ya afya kupata mahitaji ya vifaa, vifaa tiba, dawa na vitendanishi kutoka kwa wauzaji binafsi walioteuliwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

lengo la Serikali kuhakikisha kwamba Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaendelea kutumia fursa za kimapato zilizopo katika maeneo yao na hivyo kutoa huduma bora zaidi na zenye uhakika kwa wananchi.

Ni jukumu la Mamlaka za Serikali za Mitaa kubuni na kuandaa kwa umakini na utaalamu miradi ambayo inatarajiwa kuongeza uwezo wa Halmashauri kimapato ili kuweza kujitegemea na kuboresha utoaji wa huduma bora na zenye uhakika kwa wananchi.

MWISHO

Mwakyembe Aomboleza Kifo cha Mwanahabari Godfrey Dilunga

Tatizo la Upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo

0
0
Upungufu wa nguvu za kiume na maumbile  madogo huchangiwa na upungufu wa Vichocheo vya hormones  za getrogeni.

Wanaume wengi kwa sasa wamekuwa na upungufu wa nguvu za kiume na kuwa na maumbile  madogo  kutokana na kupungukiwa na virutubisho mwilini na kusababisha ndoa nyingi kuvunjika au ugomvi usio isha ndani ya nyumba 

Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume sio geni na  tiba sahihi ya kukutibia tatizo lako utaipa  NTUZU HEBRISTI CLINIC iliyopo mbagara zakhemu inatoa uduma bora zaidi tofauti na ulizowai kutumia 

MTINJETINJE; ni dawa ya kisukari ambayo  hutibu kisukari na kuifanya iwe normal 6-8 

MAJINJAS ;hii ni dawa ya nguvu za kiume ambayo hutibu matizo yafatayo. 1 kushindwa kurudia tendo 
2 kuwahi kufika kabla mwenzi wako hajafika
 3  maumbile ya kiume kulegea na kusinyaa 
4 maumbile madogo na kuingia ndani hasa kwa wale wanaojichua.

KWA USHAURI NA TIBA FIKA OFISINI MBAGALA ZAKHEMU KARIBU NA BENKI YA KCB utaona bango letu kanda ya ziwa yupo wakala wetu MWANZA mpigie DOKTA AGU SIMU   whatsAp 0783185060. 0620113431

Simbachawene Aagiza Wanaoharibu Vyanzo Vya Maji Wachukuliwe Hatua

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. George Simbachawene ameagiza wanaoharibu vyanzo vya maji katika maeneo yenye miinuko waondolewe mara moja na kuchukuliwa hatua kali za sheria.
 
Mhe. Simbachawene ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Chogola na Makosea wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe ambapo alikemea tabia ya baadhi ya watu kukata miti kwenye maeneo yenye miinuko hali inayosababisha uharibu wa vyanzo vya maji.
 
Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo aliagiza watendaji wa kata na vijiji kuweka alama za mipaka kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji yenye umbali wa urefu wa mita 500 kila upande ili kuhakikisha wananchi hawavivamii.
 
"Tunapokata miti ya asili tunafanya maisha yetu kuwa magumu na vyanzo vya maji vinategemea uhifadhi wa misitu ya asili, inashangaza watu wanafyeka miti hadi kwenye milima kitakachotokea mvua ikinyesha kwa kasi ule udondo unaporomoka na kusababisha mmomonyoko wa udongo mtakuta kijiji chote kinasombwa," alitahadharisha.
 
Pamoja na hayo Simbachawene alibainisha kuwa changamoto ya mabadiliko ya tabianchi imesababisha mabadiliko ya misimu na hivyo kuleta athari kwa wanadamu kushindwa kuendesha shughuli za kilimo.
 
Aliongeza kuwa hali hii imechangia kubadilisha misimu na ndio maana wananchi wanalalamuka kukosa mvua za kutosha kuweza kufanya shughuli za kilimo.
 
Akiendelea kutoa elimu kwa wananchi Waziri Simbachawene alisema kitendo cha kukata miti kinaharibu ikolojia ya wanyama na mimea hali inayosababisha kukosekana kwa mvua na hivyo mabadiliko ya tabianchi.
 
"Tarehe 23 ya mwezi huu (Septemba), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa marais wote kujadili namna nchi hizi zimezalisha hewa ya ukaa ambayo tunaita kaboni kutokana na shughuli zetu wenyewe.
 
"Hewa ya ukaa imeongezeka na kutengeneza joto gesi ambalo linatoboa anga la dunia ambayo ni 'ozoni layer' hali husababisha misimu kubadilika na hivyo ndo maana tunakabiliwa na changamoto ya mabadliko ya tabia nchi," alisema waziri huyo.

Ofisi Ya Makamu Wa Rais Yatoa Elimu Ya Udhibiti Wa Kemikali Zinazoharibu Tabaka La Ozoni Kwa Maofisa Forodha.

0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Faraja Ngerageza amesema kuwa  Matokeo ya kuharibika kwa Tabaka la Ozoni ni kuruhusu mionzi zaidi ya urujuani (UV-B) kufikia uso wa ardhi hivyo kutishia afya ya viumbe hai katika ikolojia mbalimbali.  Ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam wakati akifungua  warsha ya mafunzo kwa Maafisa forodha na Wasimamizi wa sheria Nchini kuhusu udhibiti wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni.

Aliongeza kuwa, Wanasayansi duniani wamethibitisha kuongezeka kwa magonjwa ya kansa ya ngozi, uharibifu wa macho kama vile "mtoto wa jicho" unaosababisha upofu, upungufu wa  uwezo wa mwili kujikinga na maradhi na kujikunja kwa ngozi hivyo mtu aweza kuonekana mzee kuliko umri wake. Pia watoto wako katika hatari zaidi ya kupata madhara haya. Madhara mengine ni pamoja na kuharibu fiziolojia ya mimea na michakato ya ukuaji wake na kusababisha mabadiliko katika muundo wa spishi, hivyo kusababisha mabadiliko ya bioanuwai katika ikolojia mbalimbali


Aidha katika kuhakikisha kuwa jukumu hili chini ya Sheria ya Mazingira linatekelezwa na kusimamiwa ipasavyo Ofisi ya Makamu wa Rais  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Maafisa forodha imekuwa ikijitahidi kujenga uwezo wa Taasisi mbalimbali katika kusimamia Kanuni za Udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la Ozoni za mwaka 2007 pamoja na kutoa vifaa katika mipaka yetu vinayowezesha kutambua gesi  hizi zinapoingizwa nchini. 

Ofisi ya Makamu wa Rais imekua na utaratibu wamara kwa mara  kuandaa warsha ya mafuzo kwa Maafisa Forodha na Wasimamizi wa sheria Nchini kote kuhusu udhibiti wa kemikali  ambazo zinzingizwa Nchini zinazoharibu tabaka la ozoni.   Warsha hiyo imehudhuriwa na Maafisa forodha wa mipaka yote Nchini kutoka katika Taasisi mbalimbali za Serikali.

Waziri Mkuu Amsimamisha Kazi Mhandisi Morogoro ....Amwagiza Mkuu Wa Mkoa Aungalie Vizuri Mkoa Wake

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Ujenzi wa wilaya ya Morogoro, Brown Undule baada ya kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo,  ikiwemo usimamizi mbovu wa ujenzi wa kituo cha afya Mkuyuni.

Amemsimamisha kazi Mhandisi huyo leo (Jumatano, Septemba 18, 2019) baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Amesema hajaridhishwa na aina ya milango iliyotumika.

“Milango yote katika jengo hili ing’olewe leo leo, huwezi kuweka milango ya hovyo namna hii yaani mtu wa nje anamuona aliyeko ndani, nimesitisha kuendelea kukagua jengo. Yeye na usomi wake ameridhishwa na milango ya hovyo kama hii.”

Waziri Mkuu amesema aina ya milango iliyowekwa katika kituo hicho cha afya haiwezi kutumika hata kwenye nyumba ya mtu binafsi, lakini kutokana na uangalizi mbovu kutoka kwa watendaji walikubali kuweka milango hiyo mibovu.

Amesema Serikali imeamua kujenga vituo vya afya vitano kwenye wilaya hiyo ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi na kuwapunguzia kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya, hivyo amewataka watendaji wasimamie ipasavyo miradi hiyo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi, hivyo amewataka wananchi hao waendelee kuwa na imani na Serikali yao.

Baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya, Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa hospitali ya wilaya, ambako nako ameagiza kuong’olewa kwa mbao zote zilizotumika kwa ajili ya kupaulia jengo la mama na mtoto la hospitali hiyo kwa kuwa hazina viwango. “Fundi usiendelee na kazi hii ya upauaji kwa sababu mbao unazotumia hazikidhi viwango.”

Kwa upande wake, fundi anayejenga jengo hilo la mama na mtoto, Johnson Ishengoma amesema changamoto kubwa anayoipata katika ujenzi huo ni ucheleweshwaji wa vifaa pamoja na kulazimishwa kutumia vifaa vilivyo chini ya kiwango.

Fundi huyo ametolea mfano suala la mbao za kupaulia kuwa aliomba mbao za urefu wa futi 20 lakini aliletewa mbao zenye urefu wa futi 12 na kulazimishwa azitumie hivyo hivyo. “Mhandisi wa wilaya Brown Undule na mtu wa manunuzi Grace ndio wanaoniletea vifaa hivi. Baadhi ya vifaa huwa navikataa kutokana na kutokuwa na ubora.”

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe kuuangalia vizuri mkoa wake na kuhakikisha anauchunga vizuri kwa sababu umekithiri kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

“Wakati nikiendelea na ziara mkoani hapa, nimepata taarifa kwamba zaidi ya sh.milioni tisa zimetumika kwa ajili ya kilipana posho katika Halmashauri ya mji Ifakara . Posho hizo ni kwa ajili ya ziara ya Waziri Mkuu na imetoka kwa mtendaji wa kata ya Viwanja 60, hili jambo halikubaliki. Nakukabidhi risiti zote na uwachukulie hatua wote waliohusika. Mkoa wa Morogoro ni shida”

Wakingumzia kuhusu utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano na ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, wakazi wa Tarafa ya Mkuyuni wameipongeza Serikali kwa namna inavyowajali wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma.

Mmoja wa wananchi hao, Uwesu Mwichumu (71) mkazi wa  kijiji cha Kibungo  ameipongeza Serikali kwa usimamizi wa miradi na hatua inazochukua kwa baadhi ya watendaji wanaojihusisha na wizi wa fedha za umma.

Amesema Serikali inajitahidi kuwaletea miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao tatizo lililopo ni kwa watendaji wa chini. “Watendaji wengi huku chini wanashindwa kutekeleza majuku yao ipasavyo, wanashirikiana na wazabuni kuiibia Serikali.”

Mkazi mwingine wa Tarafa hiyo, Hanifa Shaban amesema anaishukuru Serikali kwa kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya na zahanati. Amesema awali walikuwa wanakwenda zahanati na kuandikiwa vyeti bila ya kupewa dawa , hivyo walilazimika kwenda kununua kwenye maduka ya dawa jambo ambalo kwa sasa halipo.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Shule ya Sekondari Old Tanga inateketea kwa moto

0
0
Shule ya Sekondari Old Tanga inateketea kwa moto ulioanza leo mchana Jumatano Sept. 18, 2019.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe amesema chanzo cha moto huo ulioteketeza chumba cha mikutano na cha kuhifadhi vifaa bado hakijafahamika.

Kikosi cha Zimamoto tayari kiko eneo la tukio  kuuzima moto huo.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo,Pamoja Na Magonjwa Sugu

0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  call 0759 208 637

watsap  0620510598

Jeshi La Polisi Mkoani Dodoma Lawakamata Watuhumiwa 45 Kwa Kujihusisha Na Biashara Ya Mafuta Aina Ya Petrol Katika Makazi Ya Watu

0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limefanya msako mkali katika Wilaya zote mkoani hapa na kufanikiwa kukamata Watuhumiwa 45 kwa kosa la kufanya biashara ya mafuta ya petrol na diesel  katika makazi yao bila leseni ambacho ni kinyume cha sheria.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Sept.18,2019,Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP.Gilles Muroto amesema mafuta yaliyokuwa yakiuzwa ni aina ya Petrol lita 2118 na Diesel lita 2327.

SACP.Muroto amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo tofautitofauti mkoani Dodoma ambapo walikuwa wakijihusisha na biashara hiyo bila vibali na katika mazingira hatarishi  kwani huhifadhi na kuuza katika maeneo ya makazi na kuhatarisha maisha.

Kamanda Muroto ameainisha kuwa,katika Wilaya ya Mpwapwa wamekamatwa watu 7 waliokuwa wakiuza Petrol lita 70 pamoja na diesel lita 404,ambao ni Happiness Mtikwa [44] mkulima na mkazi wa Pwaga,Elizabeth Kululinda [20]mkulima mkazi wa wa Kimagai,Isaack Mtikwa  [27]mfanyabiashara mkazi wa Pwaga,Richard Mchigani miaka [18] mkulima na mkazi wa Mwanakianga.

Wengine ni Michael Almasi [32],mkazi wa Godegode,Justin Letema [27]mkulima mkazi wa Kimagai,Ernei  Fundi [28] na Mwingine ni Masta Kudeli[28]mkulima mfanyabiashara na mkazi wa Mang’angu.

Katika Wilaya ya Chemba kamanda Muroto amesema jeshi hilo limekamata watuhumiwa 5  waliokuwa wakiuza Mafuta ya Petrol lita 248, ambao ni Inbrahim Rajab [30],Rashid Ally Bakari [35],Fatuma Yusuph Mohamed [49],Juma Rajab[34] na Zubeda Ramadhan[30] wote wafanyabiashara na wakazi wa kijiji cha Hamai.

Wilaya ya  Bahi amekamatwa mtuhumiwa mmoja Saul Lesaka miaka 21 mkazi wa kijiji cha Ibihwa alikiwa anafanya biashara ya mafuta ya petrol lita 640  katika makazi yao kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Katika Wilaya ya Kongwa wamekamatwa watuhumiwa 8 wakiwa wanauza lita 80 ya petrol na diesel lita 730  ambao ni Samahani Chilingo [34]mkulima na mkazi wa Mbande,Festo Sailowa  [22] mkazi wa Mbande,Emmanuel Jonas [27]mkulima na mkazi wa Mbande,Abdul Hamis [26]mkulima na Mkazi wa Kibaigwa ,Mushi Mushi [36]mkulima na mkazi wa Kibaigwa,Hatibu  Omary Madudu  [34]  mkulima na Mkazi wa Banyibanyi na Shadrack Stephano[39] mkulima na Mkazi wa Banyibanyi.

Wilaya ya Chamwino wamekamatwa watuhumiwa 13  wakiwa wanauza mafuta petrol lita 587 na diesel lita 887   katika makazi yao ambao ni Stephano Kefa[29]mkulima na Mkazi wa kijiji cha Wilunze,Mateso Nzubesi [33] mkulima na mkazi wa kijiji cha Chalinze,Philemon Amos [32]mkazi wa kijiji cha Manchali,Ally Mohammed [35]mkazi wa Wilunze,Aman Msanga [42]mkazi wa Chinangali,Greyson Hotai [21]mkazi wa Maduma,Atanas Chigoji[22]mkazi wa kijiji cha Chamwino,

Wengine ni Issa Shamte [23]mkazi wa Kijiji cha Chamwino,Emmanuel Yared [22]mkazi wa Chamwino,Richard John [31]mkazi wa Chinangali,Peason Makasi [36]mkazi wa Chinangali,Musa Malogo [27]mkazi wa kijiji cha Msanga  na Issa Msemo mkulima na Mkazi wa Msanga.

Katika Wilaya ya Kondoa wamekamatwa watuhumiwa 2 waliokuwa wakijihusisha na biashara ya mafuta katika makazi ya watu ambao ni Fami Juma Omary [22]mkazi wa Haubi na Aziz Hatibu [33] mkazi wa Pahi.

Wilaya ya Dodoma Waliokamatwa na Jeshi la polisi ni 7 wakiwa wanauza mafuta ya Petrol lita 45 katika makazi yao  ambao ni Luka Lulambo[23]mkazi wa Chang’ombe,Khalid Hussein [42]mkazi wa Chang’ombe,Amina Seiph[37]mkazi wa Ndachi,Khalifa Ramadhan[45]mkazi wa Chang’ombe,Seiph Omary [44]mkazi wa Ndachi,Alshabih Issa[42]mkazi wa Itega na Daudi Kamwela [30]mkazi wa Chinangali.

Aidha Kamanda Muroto amesema Jeshi hilo limefanikiwa kukamkamata Happy Gidion [42] mkazi wa Kizota akiwa na Pombe haramu ya Moshi lita 8 na Misokoto 20 ya dawa za kulevya aina ya  banghi  kavu iliyosokotwa yenye ujazo wa nusu kilo.

Sanjari na hayo, jeshi la Polisi mkoani Dodoma limemkamata Emmanuel Jackson[35] mkazi wa Nkuhungu  akiwa na seti moja ya kompyuta  aina ya dell ambayo ni mali ya wizi  akihifadhi na kumiliki pasipo na nyaraka  za uthibitisho katika umiliki wake kinyume cha sheria.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limekamata Noti bandia zenye thamani ya zaidi ya Tsh.Milioni moja .

Waziri wa Kilimo: Tutachukua Hatua Dhidi Ya Wala Rushwa Katika Wizara Ya Kilimo

0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imesema kuwa inaendelea kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watumishi wanaobainika endelea kubainika wakijihusisha na vitendio ovu vya rushwa.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 17 Septemba 2019 wakati akifungua kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea.

Alisema kuwa serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipambanua kukabiliana na wala rushwa hivyo yeyote anayebainika hakutakuwa na huruma badala yake atapelekwa mahakamani.

“Wenyeviti na Wakurugenzi msipoisaidia serikali kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaotoa au kupokea rushwa maana yake na ninyi ni sehemu yaw ala rushwa na kama sio sehemu lazima tuchukue hatua”

“Nimeyasema haya hadharani sina lengo la kumtishia mtu yeyote katika hili badala yake nimelisema ili hatua zichukuliwe” Alisisitiza Mhe Hasunga
Ni lazima kukumbuka kuwa wajibu mkubwa wa watumishi ni kuhakikisha kuwa dira inafikiwa kwa mujibu wa mkakati uliowekwa.

Mhe Hasunga amesema kuwa wizara ya Kilimo itapimwa katika ammbo makubwa matano, ambayo ni kuongeza uzalishaji wa chakula na tija katika kilimo ili kuimarisha usalama wa chakula na lishe.

Jambo la pili ni kwa namna gani wizara imewezesha upatikanaji wa fedha za kigeni jambo huku jambo la tatu ikiwa ni kupimwa kuwa kilimo kinakuwa kwa asilimia ngapi na kinachangia kiasi gani kwenye pato la Taifa.

Jambo la nne alilolitaja Mhe Hasunga ni kuhusu upatikanaji wa malighafi sahihi kwa ajili ya viwanda nchini, huku jambo la tano ikiwa ni kipimo cha idadi ya ajira zitakazokuwa zinapatikana kwenye sekta ya kilimo, huku jambo la sita ikiwa ni namna ushirika utakavyokuwa umeimarika pamoja na usimamizi madhubuti wa ardhi kwa ajili ya kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji.

Mhe Hasunga alisema kuwa endapo maeneo hayo matano yatafanyiwa kazi ipasavyo ni wazi kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kabisa kukibadilisha kilimo kuwa cha kibiashara na sio cha kujikimu.

Alisema kuwa maendeleo ya Sekta ya Kilimo na Tasnia ya Ushirika nchini itaimarika baada ya kuzinduliwa mfumo rasmi wa mauzo ya mazao ya kilimo kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).

TMX ina lengo la kuongeza ufanisi katika juhudi za Serikali za kurasimisha mifumo ya masoko ambayo imekuwa na changamoto kwa muda mrefu; kwa kuwaunganisha Wauzaji na Wanunuzi wa bidhaa, kuleta ushindani kwenye bei, kupunguza gharama za uendeshaji biashara na kuweka uwazi.

Amesema kuwa mbali na soko la bidhaa pia kuzinduliwa kwa Mfumo wa Kielektoniki wa usajili wa wakulima na mfumo wa kielekroniki wa Kusimamia Biashara (Agricultural Trade Management Information System – ATMIS) utaimarisha makusanyo ya maduhuli na tozo kwa kuhakikisha huduma zote za utoaji vibali, leseni na vyeti unafanyika kielektroniki na pia kudhibiti udanganyifu katika hati na nyaraka za huduma hizo.

MWISHO

Wanajeshi 128,000 kutoka mataifa nane kushiriki katika mafunzo makubwa ya kijeshi Urusi

0
0
Takribani wanajeshi 128,000 kutoka mataifa nane ya mashariki watashiriki katika mafunzo makubwa ya kijeshi nchini Urusi na mataifa ya Asia ya kati.

Mafunzo hayo yalianza siku ya Jumatatu nchini Urusi, Kazakhstan na Tajikistan na yanatarajiwa kukamilika siku ya Jumamosi.

Mazoezi hayo huandaliwa na Urusi kila mwaka, ingawa mwaka huu imeshirikisha China, India, Pakistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Uzbekistan.

Inaripotiwa kuwa zaidi ya vitengo 20,000 vya silaha za kijeshi, ndege 600 na meli za vita 15 zitashiriki katika zoezi hilo.

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

0
0
Dalili:mwili kuchoka,maumivu ya mgongo na kiuno,kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu

Misuli  kulegea na kusinyaa hata kushindwa kufika kileleni miguu kuuma na kuwaka moto:

TIBA YAKE:

TULLO4 MIX.Ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizi hayo, inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kukufanya urudie tendo la ndoa zaidi mara tatu bila kuchoka au kukinai.

NTINJE3 PUMP.Ni dawa inayoongeza maumbile na kukupa umbile la kudumu.Itumie tiba hii kuokoa ndoa yako na kuokoa kukimbiwa na umpendae.
GASELA: Ni dawa mvuto kumvuta umpendae na kumrudisha alie mbali .

NTOBO: Inatibu KISUKARI:siku7 na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenyetatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari.

mpigie DR LIZENGO .OFISI IPO MBAGALA SABASABA.SIMU 0655283534/0621737576

Mohamed Dewji ‘Mo’ Alazimika kuomba Msamaha Tukio la Kutekwa na Watu Wasiojulikana

0
0
Mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ ameibua mjadala mtandaoni baada ya kuweka ujumbe uliowaibua wachangiaji kukumbushia tukio la kutekwa kwake.

Septemba 17, 2019 , Mo aliweka ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter akisema, “Kuna maisha ya mtandaoni na maisha halisi.”
 
Ujumbe huo umejadiliwa kwa mitizamo tofauti huku wengine wakikumbushia alivyotekwa na watu wasiojulikana jinsi watu walivyotumia mitandao hiyo kupaza sauti zao.

Mmoja wa watu hao ni mwanaharakati Maria Sarungi Tsehai alieandika “Bring Back Mo ilikuwa maisha ya mtandaoni au maisha halisi? Tutaelewana Tu”

MO Dewji baada ya kuona hivyo akaamua kuomba msamaha “Nisamehe sana dada yangu. Naona umeichukulia tweet yangu out of context. Narudia kuwashukuru wote ambao mliniombea ne kunisemea”.

Msanii Lady Jay Dee akichangia ujumbe huo amesema, “Nadhani (Mo) alimaanisha watu wanaoishi maisha ya uongo kuonyesha vitu ambavyo hawana katika maisha yao halisi. Hasa watu wengi maarufu wana hizo sana. Hata kupigia picha juice ambayo sio yako na kui post nayo ni maisha ya mtandaoni"

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images