Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Polisi Pwani Yakamata Madumu 859 Ya Mafuta Ya Kula Yasiolipiwa Ushuru Takriban Mil.50

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
JESHI la polisi mkoani Pwani, limekamata madumu 859 ya mafuta ya kula yanayodaiwa kutolipiwa ushuru ,yenye thamani takriban milioni 50 ,huko Chemchem kata ya Magomeni ,Bagamoyo.

Akithibitisha kuhusu tukio hilo, kamanda wa polisi mkoani hapo,Wankyo Nyigesa alisema ,madumu hayo yalikuwa yakisafirishwa na Christopher Emmanuel (32).

Alieleza kuwa, Christopher aliyasafirisha madumu hayo kupitia gari yake namba T.621 BCG aina ya fuso baada ya kukwepa kulipa ushuru kwenye moja ya bandari bubu Bagamoyo.

“Tunachunguza risiti zake za malipo kwani pia zina TIN namba tofauti,tunamshikilia mtu huyu pamoja na aliyeshirikiana nae kutoa Hassan Saidi mpemba huyu mkazi wa Bagamoyo.”

Wankyo alisema, huo ni usafirishaji haramu na kulitia hasara Taifa kwa kukwepa kulipa ushuru ama kodi,hivyo aliwaasa wananchi kuacha biashara za magendo.

Kamanda huyo alifafanua, wafanyabiashara wanapaswa kulipa ushuru kwa maendeleo ya Taifa na sio kutaka faida kwa njia za mkato.

Alibainisha hawatawaachia nafasi wakwepa ushuru na kudhibiti mianya ya kukwepa ushuru kwenye bandari zote bubu kwakuwa zinafahamika.

Tatizo la Upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo

$
0
0
Upungufu wa nguvu za kiume na maumbile  madogo huchangiwa na upungufu wa Vichocheo vya hormones  za getrogeni.

Wanaume wengi kwa sasa wamekuwa na upungufu wa nguvu za kiume na kuwa na maumbile  madogo  kutokana na kupungukiwa na virutubisho mwilini na kusababisha ndoa nyingi kuvunjika au ugomvi usio isha ndani ya nyumba 

Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume sio geni na  tiba sahihi ya kukutibia tatizo lako utaipa  NTUZU HEBRISTI CLINIC iliyopo mbagara zakhemu inatoa uduma bora zaidi tofauti na ulizowai kutumia 

MTINJETINJE; ni dawa ya kisukari ambayo  hutibu kisukari na kuifanya iwe normal 6-8 

MAJINJAS ;hii ni dawa ya nguvu za kiume ambayo hutibu matizo yafatayo. 1 kushindwa kurudia tendo 
2 kuwahi kufika kabla mwenzi wako hajafika
 3  maumbile ya kiume kulegea na kusinyaa 
4 maumbile madogo na kuingia ndani hasa kwa wale wanaojichua.

KWA USHAURI NA TIBA FIKA OFISINI MBAGALA ZAKHEMU KARIBU NA BENKI YA KCB utaona bango letu kanda ya ziwa yupo wakala wetu MWANZA mpigie DOKTA AGU SIMU   whatsAp 0783185060. 0620113431

Askofu Mkuu Jimbo la DSM Ruwa’ichi atolewa ICU.....Apelekwa Wodi ya Kawaida

$
0
0
Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Ruwa’ichi, hali yake imeendelea kuimarika na sasa amehamishiwa katika wodi ya kawaida kutoka katika chumba cha ICU.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Septemba 16, 2019 katika taarifa ya kitengo cha uhusiano cha taasisi ya Mifupa(Moi) iliyosainiwa na Patrick Mvungi.

“Jopo la wataalam saba wanaomhudumia Ruwai’chi limeamua kumhamisha baada ya kujiridhisha na maendeleo ya afya yake.”

“Limefanya uamuzi huo leo asubuhi baada ya kufanya tathmini ya vipimo pamoja na taarifa mbalimbali za maendeleo yake tangu alipopokelewa Moi na kufanyiwa upasuaji Septemba 9, 2019,” inaeleza taarifa hiyo.

Serikali Kuendelea Kujumuisha Masuala Ya Watu Wenye Ulemavu Katika Mipago Na Bajeti Ngazi Ya Wizara

$
0
0
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) imewahakikishia watu wenye ulemavu nchini kupitia Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kuwa itaendelea kujumuisha masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti kwa ngazi ya Wizara ili kuweza kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata huduma bora  na stahiki.

Akiongea wakati wa kikao kazi  kuhusu ushawishi na utetezi pamoja na ujumuishwaji wa  masuala  ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti  ngazi ya wizara,  kilicho washirikisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu wa Ofisi hiyo, Filbert Kawemwamwa amebainisha kuwa lengo la kikao hicho  ni kuibua mikakati ya ujumuishaji, usimamizi na utekelezaji wa masuala watu wenye ulemavu nchini.

“Katika kuhakikisha kuwa mipango na bajeti ngazi ya wizara zinajumuisha masuala ya watu wenye ulemavu tutaendelea kukutana na wizara nyingine saba za kisekta ili kuweza kuhakikisha mipango ya maendeleo yao inaweza kuwafikia watu wenye ulemavu hasa walio vijijini, kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma ya  Watu wenye Ulemavu ya Mwaka 20014” amesistiza Kawemwamwa

Awali akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Ummy Ndeliyanaga, ameshukuru kwa jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano, inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli katika kuboresha huduma za msingi za watu wenye Ulemavu nchini, hata hivyo amebainisha kuwa wanazo hoja za msukumo kumi ambazo anaamini utekelezaji wake ukikamilika zitaboresha huduma  na maendeleo kwa watu wenye ulemavu nchini.

“Tayari serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu imeshaunda madawati ya watu wenye ulemavu katika wizara na taasisi zake tunaomba majukumu ya maofisa hao yapitiwe upya, pia uanzishwaji wa mchakato wa uundwaji wa mfuko wa Kitaifa wa watu wenye Ulemavu, masuala mengine ni kuanzishwa kwa rejista  ya watu wenye ulemavu, kupitia sheria ya watu wenye ulemavu, Makakati wa ufukiwaji wa 3% ya watu wenye ulemavu kwenye kila taasisi inayo ajiri watu kuanzia 20”  amesema Ndeliyanaga

Ameongeza kuwa wanaomba serikali isisimamie ukamilishwaji wa mchakato wa uandaaji wa taarifa ya utekelezaji wa mkataba wa umoja wa mataifa  wa haki za watu wenye Ulemavu, pamoja na kuwaelekeza waajiri wote kuandaa na kuwasilisha taarifa ya mwaka ya hali ya ajira  kwa watu wenye ulemavu katika taasisi zao, pia ukamilshawaji wa mwongozo wa viwango vya ufikikaji wa miundo mbinu, Mipango ya Kisekta pamoja na Baraza la ushauri la watu wenye ulemavu kuhakikisha  linafanya kazi kikamilifu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Programu, Shirika la Kimataifa la ADD, Rose Tesha, amefafanua kuwa shirika hilo limeamua kuunga juhudi za serikali za kuwahudumua watu wenye Ulemavu kwa kuwezesha SHIVYAWATA kukutana na wizara za kisekta ili kuweza kuhakikisha kuwa wanaweza kuzitetea vizuri fursa na haki za watu wenye ulemavu hapa nchini.

Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) iliundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tangazo  kwenye gazeti la Serikali Na.144 la mwezi Aprili, 2016. Pamoja na majukumu mengine Ofisi hiyo inajukumu la kusimamia utekelezaji wa sera, sheria, AMiongozo, Kanuni na Viwango vya Ubora katika utoaji wa huduma za watu wenye ulemavu nchini.

MWISHO.

 

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao.

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari.

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume.

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18.

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

Pia tunadawa za Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto.
 
DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 AU  0762293390 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Rais Magufuli Azindua Rada Mbili Za Usafiri Wa Anga.

$
0
0
Na Dianarose  Shirima-Maelezo.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amezindua RADA za usafiri wa Anga katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICA) na uwanja wa ndege Kilimanjaro(KIA) ikiwa ni mwendelezo wa mradi uliokuwa umeanzishwa na serikali ya awamu ya tano kufuatia kuhamasisha safari za ndege na kuendeleza shirika la ndege la Tanzania(ATCL) uzinduzi huo umefanyika jijini Dar Es Salaam katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA). 

 Akizungumza na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo, Dkt. Magufuli amewapongeza wakandarasi toka Ufaransa waliopewa mradi huo na kuukamilisha mapema kama alivyohimisa hapo awali. 

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic  Clavier, amesema Ufaransa inaunga mkono katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania kupitia viwanda na kusema kuwa Ufaransa ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuleta maendeleo na kufikia uchumi wa kati kwa maslahi mapana ya taifa la Tanzania. Balozi pia akampongeza Rais Dkt. Magufuli pamoja na watanzania kwa jinsi walivyoungana kwa pamoja ili kuleta maendeleo nchini kwa kasi. 

Katika uzinduzi huo, Dkt. Magufuli amewakaribisha nchi za Afrika na Ulaya kupitisha ndege zao katika anga la Tanzania kwa kuwathibitishia usalama katika anga la Tanzania na kuwataka wasiogope wao wapite katika anga la Tanzania na wataongozwa vizuri, Rais Magufuli amesema kuwa licha ya kuanzisha safari Mumbai, India serikali imelenga kuanzisha na nchi zingine pia duniani, ikiwemo China na London na kusisitiza kuwa zingine zitafuata. 

Aidha, Rais Magufuli amewataka watanzania kutokukata tamaa pale zinapotokea changamoto katika harakati za kuleta maendeleo,  akasema kuwa hata ndege  iliyokamatwa huko Afrika Kusini ni moja ya changamoto katika maendeleo, hivyo watanzania wanatakiwa kuwa na umoja hata pale changamoto zinapotokea bila kuangalia tofauti zao za kisiasa kwani maendeleo ya Tanzania hayana chama bali yatafaidisha kila mmoja hata wajukuu wa kizazi kilichopo sasa. 

Rais Magufuli amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari, kutokana na uchapakazi mahiri aliouonesha katika nafasi hiyo, pia akasema kwa mwaka wa fedha uliopita, Mamlaka hiyo ilikusanya mapato ya Billioni 71 kutoka Billion 40  na kwamba mwaka ujao wa fedha wanatarajia kukusanya kiasi cha shilingi Billioni 82. 

Trump Athibitisha Kifo Cha Mtoto wa Osama Bin Laden

$
0
0
Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kwamba Hamza Bin Laden mwana wa mwanzilishi wa kundi la Al Qaeda Osama Bin Laden aliuawa katika operesheni ya Marekani.

Mwezi uliopita vyombo vya habari vya Marekani vilinukuu duru za kijasusi ambazo ziliripoti kwamba aliuawa katika shambulio la angani.

Alitajwa na Marekani kuwa gaidi miaka miwili iliopita. Alionekana kuwa mrithi wa moja wa moja wa babake.

Akidaiwa kuwa na umri wa miaka 30 alikuwa ametoa wito wa mashambulizi dhidi ya Marekani na mataifa mengine.

''Hamza Bin Laden kiongozi mkuu wa al-Qaeda na mwana wa Osama bin Laden aliuawa katika shambulio la operesheni ya Marekani dhidi ya ugaidi nchini Afghanistan / Pakistan''.Trump alizungumza katika taarifa fupi iliotolewa na Ikulu ya Whitehouse.

Taarifa hiyo haikutoa mda wa operesheni hiyo.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo,Pamoja Na Magonjwa Sugu

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  call 0759 208 637

watsap  0620510598

Rais John Magufuli aahidi kutekeleza miradi ya maji Singida Mashariki....Kasema Jimbo Lilikiwa Limetelekezwa na Tundu Lissu

$
0
0
Rais  Magufuli amempongeza mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu akisema jimbo hilo lilikuwa limetelekezwa na Tundu Lissu.

Akizungumza leo Jumatatu Septemba 16, 2019 katika hafla ya uzinduzi wa rada za kuongoza ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Rais Magufuli amewapongeza wajumbe wa kamati ya Bunge ya Miundombinu pamoja na mbunge huyo wa Singida Mashariki, aliyemtaka akawatetee wananchi bila kujali vyama.

 “Nimefurahi kumuona hapa kwenye Kamati ya Miundombinu mbunge wa CUF , lakini pia na mheshimiwa Mtaturu wa lililokuwa jimbo lililokuwa limetelekezwa na Tundu Lissu.

"Saa nyengine majimbo yanakosa uwakilishi...Kama ulivyoagiza mheshimiwa Spika (Job Ndugai) kwamba tushughulikie tatizo la maji katika jimbo lile…kama tulivyoshughulikia jimbo la Dar es Salaam…ninakuahidi kwamba serikali yangu itashughulikia, ili yale yaliyokuwa yamechelewa yaanze kufika haraka haraka," amesema Magufuli.

Mtaturu amechaguliwa hivi karibuni kuwa mbunge wa Singida Mashariki kuchukua nafasi ya Lissu ambaye Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alitangaza kuwa amepoteza sifa za kuwa mwakilishi wa wananchi  wa jimbo hilo.

Reli Ya SGR Kuinua Pato La Taifa Kupitia Sekta Ya Mifugo Nchini

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na ufufuaji wa reli ya zamani ni mkombozi mkubwa kwa wafugaji na wafanyabiara ya mifugo katika kupunguza gharama ya kufikia masoko na namna ya kufikia masoko hayo.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, wakati alipotembelea ujenzi wa reli ya SGR pamoja na eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya bandari kavu ambapo pia kuna eneo maalum lilmetengwa kwa ajili ya kushushia na kupakia mifugo katika shamba la kupumzishia mifugo la serikali lililopo katika Kata ya Kwala, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani Mhe. Ulega alisema ujenzi huo unapaswa kuendelea kuzingatia sekta ya mifugo kadri kazi inavyoendelea kufanyika.

“Reli ya zamani ilikuwa na miundombinu yote inayohusisha mifugo na reli yetu ya kisasa SGR iendelee kuhusisha mifugo na ufufuaji wa reli ya zamani uende sambamba na kujua kwamba malighafi yetu watanzania ni mifugo yetu.” Alisema Mhe. Ulega

Mhe. Ulega amesema ujenzi wa reli hiyo ya kisasa mara utakapokamilika na kuanza kufanya kazi, pato la taifa litakuwa kupitia sekta ya mifugo kwa kuwa mifugo itakuwa inasafirishwa kwa haraka ambapo reli ya mizigo itakuwa na mwendokasi wa Kilometa 120 kwa saa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, aliyeambatana na Naibu Waziri Ulega amemuarifu kuwa wizara yake imepata mkopo wa bei nafuu wa Dola za Marekani Milioni 300 kwa ajili ya kufufua reli ya zamani hivyo wizara itahakikisha wakulima na wafugaji wanatumia ipasavyo reli ya kisasa (SGR) pamoja na reli ya zamani.

Mhe. Nditiye amemuomba Naibu Waziri Ulega kufikisha wataalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika eneo la bandari kavu lililopo Kata ya kwala wilayani Bagamoyo, ambalo limetengwa maaalum kwa ajili ya mifugo ili wataalam hao watoe muongozo wa michoro ya namna eneo hilo linavyopaswa kuwa ili kuwezesha mifugo hiyo kuwa katika mazingira inayostahili.

Aidha Mhe. Niditiye amemshukuru Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kwa kuwa na mawazo mazuri ya namna reli hiyo ya kisasa inavyopaswa pia kuwa mkombozi kwa wafugaji kwa kuhakikisha miundombinu yote inayohusu mifugo katika usafirishaji inazingatiwa.

Naye Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Bw. Maghembe Makoye ameishukuru serikali kwa ujenzi ya reli ya kisasa kwa kuwa mifugo itakuwa inasafirishwa kwa muda mfupi na kufika katika eneo husika ikiwa na afya njema.

Aidha Bw. Makoye amefafanua kuwa uwepo wa miundombinu ya kupakia na kushushia mifugo iendelee kuzingatiwa katika ujenzi huo kwa kuwa kwa wafugaji mifugo ni uchumi kwao na taifa kwa ujumla.

Mwisho.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne September 17

Rais Magufuli atengua uteuzi wa DC na DED Malinyi Mkoani Morogoro.

$
0
0
Rais Magufuli  ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi  mkoani Morogoro, Majura Mateko Kasika na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mussa Mnyeti.

Waziri Mkuu Awasimamisha Kazi Watumishi Wanane Ulanga.....Aagiza wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma za ubadhilifu wa sh bilioni tatu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi wanane  wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kuagiza wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma za ubadhilifu wa zaidi ya sh. bilioni tatu za mapato ya ndani.

Amesema watumishi wa umma wanawajibu wa kufanya kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu. “Nawasihi nyote muache kufanya kazi kwa mazoea, mbadilike na kuenenda sawa na matakwa na maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano na anayejiona hatoshi ajiondoe.”

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi hao leo (Jumatatu, Septemba 16, 2019) wakati akizungumza na watumishi na madiwani  wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo uliopo mjini Mahenge.

Watumishi hao kuwa ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Yusuph Semguruka ambaye kwa sasa amehamishiwa TAMISEMI, Rajabu Siriwa (mwekahazina), Stanley Nyange, Jonson Mwenyembole, Isack Mwansokope, Said Majaliwa, Charles Steven na Hezron Lopa.

Pia, Waziri Mkuu ametumia kikao hicho kumrejesha kazini na kumpandisha kuwa mkuu wa Idara ya Ukaguzi wa Ndani, Agustine Mwaria ambaye awali alikuwa akikaimu nafasi na kuibua ubadhilifu huo. Baada ya kuibua ubadhilifu huyo mtumishi huyo alisimamishwa kazi.

Waziri Mkuu amewataka watumishi hao wazingatie sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi pamoja na kujiepusha na vitendo vya wizi kwa sababu wanaoathirika baada ya wao kuchukuliwa hatua za kisheria ni wenza wao na watoto.

Awali,Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto wa ubadhilifu wa fedha za umma hali inayosababisha kuwepo kwa mpasuko kati ya watumishi na Baraza na Madiwani. Alisema watumishi wanaotekeleza majukumu yao ipasavyo wanaandamwa.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Wanafunzi Waruhusiwa Kujisomea Wakiwa Gerezani Kufuatia Tuhuma Zinazo Wakabili Za Kushiriki Katika Mahuaji Ya Mwanafunzi Mwenzao.

$
0
0
Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Wanafunzi wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya mwanafunzi Muddy Muswadiku aliyekuwa anasoma katika shule ya sekondari Katoro Islamic Seminary ya Mkoani Kagera wameruhusiwa kuendele kujisomea wakiwa gerezani wakiwa wanajiandaa na mtiahani wa kidato cha nne utakao fanyika  mnamo Novemba 4,mwaka huu nchini.

Ruhusa hiyo imetolewa na mahakama ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera baada ya mmoja wa watuhumiwa wa kesi hiyo  Majaliwa Abdu (mwalimu) kuwasilisha maombi ya kuwaruhusu wanafunzi hao kusomea gerezani huku wakijiandaa na mtihani, wakati kesi hiyo ilipotajwa kwa mara ya pili mahakamani hapo.

Kufuatia ombi hilo, Wakili wa Serikali mkoani Kagera, Haruna Shomari amesema watuhumiwa hao watapatiwa hati hiyo ya mashtaka   na pia vitu kama madaftari, vitabu na kalamu wanaruhusiwa kuwa navyo gerezani.

Katika kesi hiyo pia idadi ya watuhumiwa wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya mwanafunzi huyo aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Katoro Islamic ya mkoani Kagera, imeongezeka baada ya wanafunzi wengine wawili kuongezwa katika shitaka hilo.

Wanafunzi waliongezwa ni Sharifu Amri (19) na Fahadi Abdulazizi Kamaga (20) na kusababisha idadi ya watuhumiwa kufikia wanafunzi sita, mwalimu mmoja na mlinzi mmoja wa shule hiyo.
 
Kesi hiyo ya mauji namba 18/2019 inayosikilizwa na Hakimu Frola Kaijage, imetajwa kwa mara ya pili Jana katika Mahakama ya Wilaya ya Bukoba, mkoani Kagera.
 
Watuhumiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni wanafunzi Husama Ramadhan (17), Sharifu Huled (19), Abdalah Juma (19) na Hussein Mussa (20), Majaliwa Abud (35) mwalimu na Badru Issa Tibagililwa (27) mlinzi.
 
Kesi hiyo imehairishwa hadi Septemba 30 mwaka huu ambapo pia itatajwa tena kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza shitaka hilo.
 
Wakili Shomari amesema upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuwa wanafunzi walioongezwa, nao wamebainika walishiriki kumpiga Mudy (marehemu).
 
“Katika upelelezi tunaoendelea kuifanya tulibaini kuwa pia wanafunzi hao wawili walioongezwa nao walishiriki kumpiga marehemu (Mudy) wakati huo huo bado upelelezi unaendelea,” alisema Shomari.

Mauji hayo yalitokea Aprili 14 mwaka katika shule ya sekondari ya Katoro Islamic iliyoko katika Halmashauri ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera.
 
Watuhumiwa wamerudishwa rumande hadi kesi itakapo tajwa tena





Rais Magufuli azuia ukusaji Ushuru machinjio ya Vingunguti.....Atoa Maagizo MAZITO Kwa Uongozi wa Mkoa wa Dar, Ilala na NHC

$
0
0
 Rais John Magufuli ameuagiza uongozi wa Hamashauri ya Ilala kutochangisha fedha katika machinjio ya Vingunguti hadi pale watakapokamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa.

Rais Magufuli amesema hayo, alipofanya ziara ya kushtukiza na kuwataka viongozi wa Halmashauri hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na watendaji wengine kuangalia namna ya kukamilisha kazi hiyo ili kuwaondolea adha wafanyabiashara wa maeneo hayo.

Amesema, kuanzia sasa mkurugenzi wa Halmashauri na watendaji wengine ni marufuku kukusanya ushuru wa aina yoyote sambamba na kuwataka kufanyia kazi maagizo yake usiku na mchana.

Uamuzi huo umepokelewa kwa shangwe na wafanyabiashara wa eneo hilo la machinjioni ambalo linadaiwa kukusanya takribani milioni 100 kwa mwezi baada ya kupita akitokea kwenye uzinduzi wa Rada na kiwanda cha mabomba ya plastiki kilichopo maeneo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam

Dereva taksi kesi ya Mo Dewji aendelea kusota....Watuhumiwa Wengine bado Wanasakwa

$
0
0
Upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili dereva taksi mkazi wa Tegeta, Mousa Twaleb (46) ya uhujumu uchumi ikiwamo kusaidia kutendeka uhalifu, kutakatisha Sh. milioni nane na kumteka Mohamed Dewji maarufu kama ‘Mo’ umedai kuwa bado unaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wanne kwa ajili yakuwaunganisha katika kesi hiyo.

Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, na kwamba bado upande wa Jamhuri unaendelea na juhudi za kuwatafuta watuhumiwa wengine.

Alidai kuwa upande wa Jamhuri unaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Hakimu alisema kesi hiyo itatajwa tena Septemba 30, mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu.

Rais Magufuli: Wasimamizi Wa Miradi Ya Serikali Tumieni Vifaa Vya Viwanda Vya Ndani

$
0
0
Na Paschal Dotto-MAELEZO
RAIS Dkt. John Magufuli amewataka watendaji wanaosimamia miradi ya Serikali kutumia vifaa vinavyozalishwa na viwanda vya ndani ili kuinua sekta ya viwanda na kuongeza ajira kwa watanzania  wanaofanya kazi katika viwanda hivyo.

Akizungumza katika uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza mabomba ya plastiki cha Pipe Industirial Co.Ltd jana (Septemba 16, 2019) Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kuwa Serikali inatekeleza miradi mingi mkubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji na sekta ya umwagiliaji ambayo yote hiyo inatumia mabomba ya kusafarisha maji.

“Miradi yote inayotekelezwa na Serikali inahitaji matumizi ya mabomba kwa asilimia 100, kwa hiyo ni lazima tutumie mabomba yanayotengenezwa nchini, sijasema tusiagize pengine lakini lazima tuwe wazalendo ili kuinua sekta yetu ya viwanda kwa kulinda viwanda vyetu vya vinavyozalisha bidhaa mbalimbali hapa nchini” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema kuwa viwanda vinavyojengwa nchini vitakuwa na faida nyinyi kwa wananchi na kwa Serikali kwa ujumla ikiwemo, upatikanaji wa ajira, ambapo Serikali itakusanya kodi ambazo zitatumika katika ujenzi wa barabara, ununuzi wa Ndege, ununuzi wa madawa, pamoja na uuzaji wa bidhaa zinazoenda nje zitakazoifanya Serikali kupata fedha za kigeni.

AIdha Rais Magufuli alisema katika kuhakikisha sekta ya Viwanda imekua, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufufua viwanda vuilivyokufa, kuondoa  urasmu katika taasisi zinazohusika na viwanda kama TBS, TFDA, NEMC, OSHA na Taasisi zinginezo ili kuwawezesha wawekezaji kuja kuwekeza kwa wingi nchini.

“Serikali imefanya yote hayo kwenye Taasisi husika, lakini pia imeweza kupunguza utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara na kwa wenye viwanda, kwa mwaka huu wa fedha tumefuta tozo zipatazo 54 ambazo zingekuwa zinakwamisha juhudi za Serikali za kuwa na viwanda vya kutosha”, Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema kuwa kiwanda cha Pipe Industirial Co.Ltd Jijini Dar es Salaam ni kiwanda ambacho kinatumia teknolojia ya kisasa kuzalisha mabomba ambapo uwekezaji wake umetumia Bilioni 120 kwa wawekezaji kujenga kiwanda hicho.

“Nimefurahi kusikia kwamba wakati wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda hiki watu wapatao 215 wamepata ajira, ambapo awamu ya pili itakapokamilika kiwanda hiki kitaweza kuzalisha mabomba ya kusafirisha gesi, mafuta na nyaya za umeme na kitaajili watu wapatao 500 hii ni hatua kubwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati wenye viwanda”, Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli, alisema kuwa Sekta ya viwanda ni Sekta muhimu kwa nchi yoyote duniani, kwani Takwimu za Shirika la Biashara Duniani (WTO) zinaeleza kuwa asilimia 70 ya biashara ya kimataifa kwa mwaka 2018 bidhaa za viwandani zilichukua nafasi kubwa na kuwa na thamani ya dola za kimarekani Trilioni 12.41 ikifuatiwa na bidhaa ya mafuta asilimia 15, bidhaa za kilimo asilimia 10 na bidhaa nyinginezo asilimia 5 na thamani yake ni dola trilioni 5.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, alisema kuwa Serikali kupitia Wizara hiyo inalenga kuwasaidia wafanyabiashara kuzalisha kwa kulenga masoko yote ndani na nje ya nchi ili kuinua sekta hiyo muhimu nchini.

“Kiu ya Serikali ya Awamu ya Tano, ni kuona Tanzania hatuzalishi tu kwa soko la ndani, bali tunazalisha kwa ajili ya masoko ambayo Tanzania ni mwanachama wa jumuiya mbalimbali, kwa hiyo uzalishaji katika viwanda vyetu ni vizuri ukalenga masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika(SADC) na Soko la Pamoja la Nchi Huru za Afrika (AU)”, Waziri Bashungwa.

TANCOAL Yatakiwa Kulipa Deni La Dola Milioni 10.4

$
0
0
Na Greyson Mwase, Dodoma
Tume ya Madini imeitaka kampuni ya kuzalisha makaa ya mawe nchini ya TANCOAL kulipa deni la Dola za Marekani 10,408,798 ambalo ni  kwa kipindi cha Septemba, 2011 hadi Juni, 2019 na kuacha kupotosha umma wa watanzania.

Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 16 Septemba, 2019 jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kufuatia taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikichapishwa na kampuni ya TANCOAL kupitia tovuti ya www.miningreview.com tarehe 03 Septemba, 2019 na kusambazwa kwenye mitandao mingine ya kijamii.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, Dkt. Venance Mwase, Mkurugenzi wa Huduma za Tume, William Mtinya, Meneja wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Gift Kilimwomeshi, Meneja wa Leseni, Mhandisi Ramadhani Lwamo na Kaimu Meneja wa Utafiti na Sera, Andendekisye Mbije.

Profesa Manya alifafanua kuwa, kampuni ya TANCOAL kupitia taarifa yake ilidai kuwa, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeanza kuitoza TANCOAL tozo ya mrabaha kwenye gharama za usafirishaji wa makaa ya mawe kutoka mgodini hadi kwa mtumiaji wa mwisho wa ndani na nje ya nchi.

 Aliongeza kuwa, kampuni ya TANCOAL ilidai kulazimishwa kuuza makaa ya mawe kwa wateja wenye leseni za biashara ya madini hali itakayoongeza gharama za makaa ya mawe.

Profesa Manya alisema kuwa TANCOAL imekuwa ikilipa tozo ya mrabaha kwa kuzingatia thamani ya madini yakiwa yadi ya Kitai bila kujumuisha gharama za usafirishaji kwenda kwa wateja jambo ni kinyume na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.

“Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kifungu cha 87 (6) kinaelekeza namna ya kukokotoa mrabaha kwa kuzingatia thamani ya madini sokoni (kwa mtumiaji wa mwisho) ambayo inajumuisha gharama za usafirishaji hadi kwa mteja (Gross Value). Utaratibu huu wa malipo umekuwa ukifuatwa na kampuni nyingine zote zinazochimba ama kuuza makaa ya mawe isipokuwa TANCOAL,” alisema Profesa Manya.

Aliongeza kuwa, pamoja na kuelimishwa mara kwa mara juu ya namna ya kukokotoa malipo ya mrabaha kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, TANCOAL imekuwa ikikaidi kulipa mrabaha kwa kuzingatia msingi huo.

Alisema kuwa, utaratibu ambao kampuni ya TANCOAL inautumia kwa kuwauzia wateja wa makaa ya mawe katika yadi ya Kitai badala ya kusafirisha wenyewe au kutumia wafanyabiashara wa madini walioidhinishwa (Mineral Brokers or Dealers) unakwenda kinyume cha Sheria. Kifungu cha 18 (1) cha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kinakataza mtu au kampuni yeyote isipokuwa mmiliki halali wa leseni ya madini au mfanyakazi wa wamiliki wa leseni hizo: kumiliki, kusafirisha au kuuza madini bila kuwa na kibali cha kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Alifafanua kuwa, kutokana na Kampuni ya TANCOAL kulalamikia Madai ya Mrabaha inayotakiwa kulipa Serikalini, iliundwa Timu maalum kwa ajili ya kuhakiki deni la mrabaha unaojumuisha usafirishaji wa makaa ya mawe kwa kwa kipindi cha Septemba, 2011 hadi Juni, 2014 ambayo yalikuwa hayajalipwa pamoja na kufanya upembuzi wa madai ya mrabaha ambao TANCOAL inatakiwa kulipa Serikalini kwa kipindi cha Septemba 2011 hadi Juni, 2019.

Alisema kuwa katika upembuzi na uchambuzi wa takwimu za mauzo na usafirishaji wa makaa ya mawe uliofanyika, imebainika kuwa TANCOAL inatakiwa kulipa USD 1,103,594 ikijumuisha na adhabu ya asilimia 50 kwa kipindi cha Septemba 2011 hadi Juni 2014. TANCOAL inapaswa kulipa USD 9,305,205 ikijumuisha na adhabu ya asilimia 50 kwa kipindi cha Julai 2014 hadi Juni 2019. Jumla ya malipo ni USD 10,408,798 kwa kipindi cha Septemba, 2011 hadi Juni, 2019.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akizungumza katika mkutano huo aliitaka kampuni ya TANCOAL kutopandisha bei ya makaa ya mawe kwa wateja na badala yake kuuza kulingana na bei elekezi zinazotolewa na Tume ya Madini kila mwezi.

Waziri Mkuu Aagiza Gari La Wagonjwa Lipelekwe Ifakara

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupeleka gari la kubebea wangonjwa katika kituo cha Afya cha Kibaoni kilichopo Halmashauri ya Mji wa Ifakara ili kuwapunguzia wananchi gharama ya kukodi gari kwa sh. 800,000 pale wagonjwa wao wanapopata rufaa.

Wananchi wa Mji wa Ifakara wameiomba  Serikali iwasaidie kuwapatia gari la wagonjwa kwani kitua chao hakina gari na wagonjwa wao wanapopata rufaa ya kwenda hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro wanalazimika kukodi gari kutoka hospitali ya Mtakatifu Francis kwa gharama ya sh. 800,000 ambazo baadhi yao wanashindwa kuzimudi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Septemba 17, 2019) wakati akizungumza na wananchi wa Mji wa Ifakara katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa kituo cha mabasi cha mji huo. Amesema iwapo fedha za makusanyo ya mapato ya ndani  katika halmashauri husika zingekuwa zinatumika vizuri kusingekuwa na changamoto  kama hizo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi, hivyo amewataka wananchi hao kuendelea kuwa na imani na Serikali yao. “Nitampigia simu Waziri Ummy (Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) katika mgao ujao alete gari la wagonjwa hapa.”

Pia, Waziri Mkuu ameielekeza Ofisi ya Rais-TAMISEMI ihakikishe katika mgawo wa ujenzi wa hospitali za wilaya, Halmashauri ya Mji wa Ifakara ipewe kipaumbele kwa sababu eneo hilo ni kubwa na lina watu wengi lakini hakuna hospitali ya wilaya hivyo kusababisha msongamano mkubwa katika kituo cha Afya cha Kibaoni.

“Nimetembelea mwenyewe kituo cha Afya cha Kibaoni na nimeshuhudia msongamano wa wagonjwa, mgao wa pili wa ujenzi wa hospitali za wilaya Mji wa Ifakara lazima upewe kipaumbele. Suala la huduma za afya ni suala nyeti, hivyo ujenzi wa hospitali hiyo ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.”

Awali, Mganga Mfawidhi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Dkt. Happyness Ndosi alisema kituo cha Afya cha Kibaoni kinapokea na kuwahudumia wagonjwa wa  nje 225 hadi 250 kwa siku na wagonjwa wanaolazwa ni kati ya 50 hadi 80 kwa siku. Wakinamama wanaojifungulia kituoni hapo ni 400 kwa mwezi.

Akizungumzia kuhusu changamoto zinazikabili kituo hicho amesema kina upungufu wa watumishi 92, kwani kina jumla ya watumishi 83 huku mahitaji yakiwa ni watumishi 175,  ukosefu wa gari la wagonjwa na pia hakina gari lolote la kutolea huduma zikiwemo za chanjo, na usambazaji, uchakavu kwa baadhi ya majengo kama la wagonjwa wa n je.

Pia, kituo kinakabiliwa na ukosefu wa jengo la kutunzia watoto njiti, watoto wachanga na wale wanaohitaji uangalizi maalumu baada ya kuzaliwa (neonatal unit), ufinyu wa chumba cha kujifungulia pamoja na ukosefu wa mashine ya kutolea dawa za usingizi (anesthesia machine).

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali haitokuwa na msamaha  na watendaji wa halmashauri watakaobainika kutafuna fedha za makusanyo ya mapato ya ndani pamoja na fedha zinazotolewa kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao.

“Fedha za mapato ya ndani hazitumiki vizuri watu wanadukua mifumo, wanapaswa watambue kwamba Serikali ipo makini wakati wote. Watumishi wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo vya ubadhilifu hatua kali za kinidhami zitachukuliwa dhidi yao. Watumishi wa umma mnatakiwa kutekeleza majukumu yenu kwa weledi.”

Waziri Mkuu amesema watumishi wa umma wanatakiwa kujiepusha na  migogoro kwa kuwa ni kunyume na taratibu za kiutumishi. “Haiwezekani viongozi wakagombania zabuni zitokanazo na fedha za kodi za wananchi, kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Serikali itasimamia zabuni zote.”

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Makonda: Ni Njaa tu, Vinginevyo Ningeandika Barua ya Kujiuzulu

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amekiri kudhalilishwa na watendaji wake wa chini hii ni baada ya Rais Magufuli kuonesha kutoridhishwa na utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati, ikiwemo machinjio ya Vingunguti na ufukwe wa Coco.

Makonda ameyabainisha hayo leo Septemba 17, 2019 katika hafla ya utoaji udhamini kwa Wanafunzi wa kike 100, wanaosoma masomo ya Sayansi kutoka katika familia zenye kipato cha chini, kwa madai ya kwamba amedhalilika mbele ya Mkuu wa nchi hali iliyomnyima raha hadi kutamani kuacha kazi.

''Jana ilikuwa aibu, jana nimedhalilika mimi, watendaji wangu jana mmenivua nguo na aibu ile imenifanya hata sijalala, usingizi sijapata kabisa mpaka nikawa najiuliza nakosea wapi? sababu tunakaa vikao vingi vya kutoa maelekezo mengi dhidi ya miradi ya maendeleo katika mkoa wetu'' amesema Rc Makonda.

Makonda amedai kuwa, njaa ndiyo inamfanya aendelee kushikilia nafasi hiyo.

''Yaani kwa sababu njaa tu ni kali, kama sio njaa kali leo ilipaswa mimi niwe nimeandika barua ya kuacha kazi, sasa ukiwaza kuacha kazi njaa hii, huko kwenu kwenyewe ulikotoka, kijijini kwetu Koromije hata majirani nishawasahau'' amesema Makonda.

Kufuatia hali hiyo Makonda ameunda kamati maalumu ya kusimamia utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika mkoa huo, itakayohusisha TAKUKURU ili kuhakikisha aibu kama hiyo haijirudii tena.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Magufuli, kutembelea machinjio ya Vinguguti na kubaini ucheleweshwaji wa ujenzi wa machinjio hayo na kumuagiza Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, kuacha maneno na badala yake wahakikishe miradi inamalizika kwa wakati.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images