Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao.

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari.

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume.

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18.

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

Pia tunadawa za Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto.
 
DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 AU  0762293390 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo,Pamoja Na Magonjwa Sugu

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  call 0759 208 637

watsap  0620510598

Rais Magufuli kufungua mkutano wa wakuu wa polisi kutoka nchi 14 Arusha

$
0
0
Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kufungua mkutano mkuu wa 21 wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa nchi za Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu mjini Arusha kaskazini mwa nchi hiyo.

Mkutano huo utashirikkisha wajumbe ambao ni ma Inspekta Jenerali wa Polisi kutoka nchi 14 za Burundi, Comorro, Djibouti, Congo Brazzaville, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ethiopia na Rwanda. Nyingine ni Ushelisheli, Sudan Kusini, Uganda, Eritrea, Sudan na mwenyeji Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, David Misime amesema kuwa, maandalizi ya mkutano huuo yamekamilika na kwamba, walianza kupokea wageni hapo jana.

Misime amesema pia kuwa, kabla ya kufanyika ufunguzi wa mkutano huo, kutakuwa na vikao vya wakuu wa vitengo vya Interpol vitakavyofanyika kuanzia kesho Jumapili tarehe 15 hadi tarehe 17 mwezi huu, kisha kufuatiwa na mkutano wa wakurugenzi wa upelelezi wa makossa ya jinai na kikao cha wajumbe wa kamati ndogo.
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania amesema pia kutakuwa na kikao cha kamati ndogo ya wataalamu wa sheria, vikao vya wajumbe wa kamati ya dawati la masuala ya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kikao cha wajumbe wa masuala ya kukkabiliana na ugaidi nchini.

Kwa mujibu wa Misime kaulimbiu ya mkutano huo ni "Kuimarisha Ushirikiano na Ubunifu Katika Kupambana na Uhalifu Unaovuka Mipaka" ambapo lengo hasa ni kuongeza ushirikkiano katika kukabiliana na makosa yanayovuka mpaka na kuwekka mikakati ya pamoja katika maazimio ya kukabiliana na uhalifu wa aina hiyo.

Mamlaka Za Maji Nchini Zapewa Maagizo

$
0
0
Mamlaka za maji zinazotumia bei za kukadiria (flat rates) kote nchini zimepewa miezi mitatu kuhakikisha zinawafungia dira za maji wateja wao wote ili kila mteja alipe gharama ya maji kwa kiasi alichotumia.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (Mb) alitoa agizo hilo Septemba 14, 2019 alipokuwa akizindua mradi wa maji wa Kijiji cha Shilima Kata ya Kikubiji, Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.

Waziri Mbarawa alisema Serikali imetenga Bilioni moja kusaidia mamlaka za maji ambazo hukadiria matumizi ya maji wateja wake badala ya kutumia dira ya maji ili kuepuka kumbebesha mteja mzigo usiyo kuwa wake.

Waziri Mbarawa vilevile ameziagiza mamlaka za maji za mikoa kuhakikisha zinadhibiti upotevu wa maji kwani maji mengi yanapotea kabla ya kufika kwa wananchi sambamba na kuongeza mtandao wa maji ili kuwaunganisha wananchi wengi zaidi.

Akizungumzia mradi wa maji wa Shilima, Profesa Mbarawa alisema ujenzi wake ni utekelezaji wa Sera ya Maji pamoja na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inayoelekeza kuwapatia  huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 85 wakazi wote waishio vijijini ifikapo mwaka 2020.

Aliongeza kuwa uzinduzi wa mradi huo ni awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa maji katika Vijiji vya Shilima, Mhande na Izizimba.

Alibainisha kwamba mradi wa maji wa Shilima ulianza kutekelezwa mwaka 2013 na ulitakiwa kukamilika katika kipindi cha miezi sita. Hata hivyo, kutokana na udhaifu wa Mkandarasi aliyekuwa anautekeleza pamoja na usimamizi mbovu haukuweza kukamilika kwa wakati.

Waziri Mbarawa aliwapongeza wote walioshiriki kwenye ujenzi wa mradi kwa namna mbalimbali na kwa ushirikiano waliotoa kwa kipindi chote cha ujenzi wake hadi unakamilika kwa wakati kama alivyokuwa ameelekeza.

Akizungumzia ujenzi wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa ujenzi, Mhandisi Anthony Sanga alisema walizingatia agizo la Waziri Mbarawa na kwamba mradi huo ulikamilka tarehe 25 Agosti, 2019 kabla ya muda uliyokuwa umeelekezwa.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Boaz Matundalo alisema kuwa Kijiji cha Shilima kina wakazi wapatao 7,526 ambapo mradi huu wenye magati 35 una uwezo wa kuhudumia wakazi 8.750 ikiwa ni wastani wa watu 250 kwa kila gati.

Waziri Mbarawa tarehe 3 Julai, 2019 akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Kwimba alitoa ahadi ya kukamilisha mradi huo kwa kutumia wataalamu wa ndani kwa kuhakikisha wananchi wa Kijiji cha Shilima wanapata maji katika kipindi cha miezi miwili, yaani hadi kufikia tarehe 3 Septemba, 2019, ahadi ambayo hata hivyo ilikamilika tarehe 25 Agosti, 2019 siku tisa kabla ya tarehe ya makubaliano.
 

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu September 16

Waziri Mkuu: Tatizo La Barabara Ifakara Mlimba Kuwa Historia

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya barabara ya kutoka Ifakara hadi Mlimba iliyokuwa inawakabili wananchi wa maeneo hayo kwa muda mrefu imepatiwa ufumbuzi baada ya Serikali kupanga kuijenga kwa kiwango cha lami.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha miundombinu ya barabara nchini ikiwemo barabara ya kutoka Ifakara hadi Mlimba yenye urefu wa km. 126.5.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Matangini, Mlimba wilayani Kilombero.

“Serikali imedhamiria kuimarisha barabara katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Ifakara-Mlimba kwa kiwango cha lami lengo likiwa ni kurahisisha usafiri pamoja na kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.”

Alisema Serikali inatambua umuhimu wa barabara hiyo kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya wananchi na kwamba itajengwa kwa kiwango cha lami, hivyo aliwataka wananchi hao waendelee kuiamini Serikali yao.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Morogoro, Jackson Mpankuli ahakikishe amepeleka walimu katika shule ya msingi  Matangini na Mwangazaambazo zinakabiliwa na upungufu wa walimu.

Waziri Mkuu alisema hadi Sepetemba 30 mwaka huu kiongozi huyo awe ameshawahashimia walimu katika shule husika. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Suzan Kiwanga kulalamikia upungufu wa walimu hao.

Mbunge huyo alisema katika jimbo kuna tatizo kubwa la upungufu wa walimu hali inayosababisha baadhi ya wazazi kukodi walimu kwa ajili ya kuwafundisha watoto wao, hivyo Waziri Mkuu aliagiza walimu wahamishiwe katika shule ndani ya wiki mbili.

Akizungumza na wananchi katika eneo la Mchombe alipokuwa njiani kuelekea Mlimba, Waziri Mkuu aliwataka wazazi, walezi na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro kuhakikisha wanadhibiti ongezeko la mimba kwa watoto wa shule.

“Lazima kuwalinda watoto wa kike ili wasipate mimba kwani watashindwa kuendelee na masomo, hivyo watashindwa kutimiza ndoto zao. Viongozi simamieni utekelezaji wa sheria kwa kuwachukulia hatua wote waliowapa mimba wanafunzi.”

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mbunge wa jimbo la Kilombero, Lijualikali na Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga waliiomba Serikali iwasaidie ujenzi wa barabara za kutoka Ifakara hadi Mlimba na barabara ya Ifakara hadi Kidatu ambayo ujenzi wake unasuasua.

Pia Suzan alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu kwa barabara ya Ifakara-Mlimba na baadae kuwekwa lami kwa awamu na kusema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ikiahidi kitu inatekeleza

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro ambapo anatarajiwa kutembelea Halmashauri za wilaya ya Ulanga na Malinyi kukagua miradi ya maendeleo ukiwemo mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na kuzungumza na wananchi pamoja na watumishi.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Rais Magufuli :serikali Kuendeleza Mahusiano Mazuri Kati Yao Na Madhehebu Ya Dini Nchini

$
0
0
Rais wa Dkt John Magufuli amesema kwamba serikali ina kila sababu ya kuendeleza mahusiano mzuri kati yao na madhehabu ya dini nchini kwa sababu kazi wanayoifanya haina mbadala wake kwenye jamii.

Hayo aliyasema jana kwenye hotuba yake iliyotolewa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipomwakilisha kwenye Jubilee ya miaka 25 Uaskofu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga Anthony Banzi.

Jubilee hiyo ilikwenda sambamba na ibada iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Kadinali Mstaafu Policapy Pengo, Maaskofu, Mapadre, Masista na watawa,Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa na Mkewe wakiwemo pia viongozi wa serikali wa sasa na wastaafu

Alisema kwamba anaamini kwa pamoja wanaweza kujenga na kuendelea kuimarisha amani na umoja uliopo hapa nchini kwa wakishirikiana na  kuongeza kasi ya watawezesha watanzania kupata maendeleo.

“Baba Askofu sisi kama serikali tutatimiza wajibu wetu kutengeneza mazingira mazuri kwa madhehebu ya dini kutekeleza wajibu wake kwani uhuru wa kuabubdu uliopo nchini unaheshimuwa na kutekelezwa kwa vitendo.

Aidha alisema pia wataendelea kushirikiana na kusaidia na madhehebu ya dini kwenye upande wa shughuli zenu za huduma za kiuchumi na kijamii wanazofanya watafanya hivyo kwa kutambua mchango wao muhimu unaotolewa na huduma hizo kwa maendeleo ya nchi na ustawi wa watu wake.

“Maombi yangu kwamba msiwaruhudu watu waovu kutumia fursa hiyo muhimu…tunapopata taarifa za kutumika kinyume hatutasumbuka sana wakati wote viongozi wa dini na serikali wana jukumu la ulezi na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani umoja upendo na mshikamano.

Waziri Ummy alisema kwamba licha ya utofauti za dini, kabila rangi au vyama Rais Dkt Magufuli anasema tofauti hizo hatuna budi kuishi nazo na wasiziache zikawa nyufa za uhasama ambao sio zitaligawa taifa bali linaweza kulimonyony’oa hata kanisa.

Aidha alisema kwamba matumaini ya waumini wa Jimbo Katiloki la Tanga na wananchi ni kwako Mhashamu Banzi na sio ya kiroho peke yake hivyo atambue kwamba wanayomatarajio chini ya uongozi wake kanisa katoliki linaweza kuendelea kutoa huduma huduma za kijamii kama walivyfanya huko nyuma.

“Wana tanga wanayo matumaini makubwa kwa sababu wanathamin i na kutambua manufaa makubwa yanayofanya kwenye harakati za kujilete maendeleo kutokana na kazi kubwa mnayoifanya kuwapa maendeleo kutokana na kazi kubwa”Alisema

Waziri Ummy alisema kwamba Rais Magufuli ataendelea kutambua na kuthamani mchango wa viongozi wa dini nchini hususani kwenye suala la kuliombea Taifa ili liendelea kuwa na amani na utulivu uliopo ili kuwawezesha wananchi kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo.
Hata hivyo alisema kwamba Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuunga mkono juhudu za makanisa na viongozi wa dini kwenye kujenga amani ya nchi na kuleta ustawi wa Taifa ikiwemo kujenga masikilizano endelevu kati ya taasisi za dini na serikali.

“Niwaambie ndugu zangu maaskofu kwamba Rais Dkt Magufuli anasema ataendeleza ushirkiano uliopo kati ya serikali na Kanisa Katoliki pia kuunga mkono shughuli za kanisa kwenye kutoa huduma za jamii hususani elimu,afya na nyengine”Alisema.

Awali akitoa salamu za kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ,Balozi wa Papa nchini Askofu Mkuu Marek Solczriski alisema kuwa mchango wa askofu Banzi ni mkubwa kwa kanisa na uhudumu wake wa kazi za kanisa umekuwa ni kichocheo cha maendeleo .

“Nakuombea katika kipindi hiki cha kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 kiwe sababu za Baraka kwako na jimbo zima la Tanga na Mungu aendelee kukulinda na kukuongoza”alisema Mwakilishi huyo.

MWISHO

Waziri wa Ujenzi Mhandisi Isack Kamwelwe Azikaribisha Nchi Wanachama wa SADC kutumia bandari ya Dar es Salaam

$
0
0
Na Paschal Dotto-MAELEZO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amezikaribisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) kutumia bandari ya Dar es Salaam mara baada ya ukarabati wake hasa gati namba sufuri kuanza kupokea mizigo.

Akizungmza Jijini Dar es Salaam alipotembelea kuona meli kubwa ya Mizigo ya Magari ya kampuni ya Meli ya Mv Grand Duke iliyotua bandarini hapo jana, Waziri Kamwelwe alifurahishwa kuona meli hiyo kubwa nyenye urefu wa mita 200 na uwezo wa kubeba magari 6,000 ambapo imetua ikiwa na magari 1,347 imedhihirisha uwezo wa bandari hiyo kwamba iko tayari kupokea mizigo mikubwa.

“Tuko hapa kuwahabarisha Watanzania, na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC), kwamba ukarabati wa Bandari ya Dar es Salaam unaenda vizuri ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa gati namba moja, mbili na hili gati namba sifuri liko mwishoni na limeanza kupokea meli kubwa za Mizigo kama mnavyoona hapo, hiyo ni meli ya mizigo ya magari yenye uwezo mkubwa sana”, Waziri Kamwelwe.

Malengo ya Serikali ni kufanya ukarabati wamagati nane ambapo mpaka sasa gati
namba moja na gati namba mbili yako kwenye matumizi mara baada ya kukamilika
na sasa meli zinaendelea kutoa huduma kama kawaida, gati namba sifuri ambalo ni maalum kwa meli za mizigo ya magari linaendelea na ukarabati lakini asilimia
kubwa liko vizuri.

Waziri Kamwelwe alisema kuwa mara baada ya gati hilo kukamilika Tanzania
itakuwa na uwezo mkubwa wa kupokea mizigo ya magari laki 6 kwa mwaka, lakini
pia bandari hiyo inabeba tani milioni 17 kwa mwaka huku malengo ya Serikali ikiwa ni kufikia tani milioni 25 ifikapo mwaka 2021.

“Malengo yetu ni kufikia tani milioni 25 kwa mwaka tofauti na tani za sasa milioni
17, kwa hiyo Nchi Wanachama wa SADC, bandari hii sasa inafanya kazi vizuri, kwa
hiyo majirani zetu kutoka SADC, DRC, Malawi, Zambia na nchi zingine za ukanda
huu wa Kusini mwa Afrika wanakaribishwa sana kutumia bandari ya Dar es Salaam” Alisisitiza Waziri Kamwelwe.

Waziri Kamwelwe alisema Serikali itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na wafanyabiashara kutoka Nchi Wananchama wa SADC ili maeneo ambayo yana changamoto ziweze kutatuliwa haraka.

“Serikali imewekeza fedha nyingi katika ukarabati huo, kwa hiyo itahakikisha kuwa inaipa bandari hii mizigo ya kutosha na hasa kutoka kwa Nchi Wanachama wa SADC, ili kuwawezesha kupata huduma rahisi za usafirishaji” alisema Kamwelwe.

kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko, alisema kuwa gati jipya namba sufuri limeanza kufanya kazi kwa kupokea meli kubwa ya Mv Grand Duke ambayo imetua jana na mzigo wa magari 1347.

“ Hili gati ni Jipya ni kati ya magati nane ambayo yanajengwa, lenyewe limejengwa kwa zege kama mnavyoona, lina uwezo wa kubeba magari 10,000 kwa wakati mmoja kutoka uwezo wa kubeba magari 2,500 ambao tulikuwa nao hapo mwanzo, lakini pia lina urefu wa mita 320 kwa hiyo ni gati kubwa na hii meli ina urafu wa mita 200 kwa hiyo kuna mita 120 zimebakia kwenye gati hili”, Alisema Mhandisi Kakoko.

Gati hilo ambalo ni la kisasa Zaidi litakuwa na taa ambazo zitawezesha kufanyika kazi usiku na mchana hapo bandarini, na makabidhiano ya gati hilo yatafanyika kesho ambapo Mkandarasi ataikabidhi Mamlaka ya Bandari (TPA).

Aidha, Mhandisi Kakoko alisema kuwa meli ya Abiria ziwa nyasa imeingia kwenye majaribio ya mwezi mmoja ambapo mwezi ujao inatarajiwa kukabidhiwa kwa Mamlaka hiyo ili kuanza kuhudumia wananchi wa maeneo hayo.

Naibu Waziri Kanyasu Awafunda Wazazi Wenye Watoto Waliohitimu Darasa La Saba

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Geita mjini, Mhe.Constantine Kanyasu amewahimiza wazazi wenye watoto waliomaliza darasa la saba mwezi huu nchini  wahakikishe wanawalinda watoto hao wasijiingize katika makundi yasiyofaa.

Akizungumza kwenye mahafali ya saba ya wanafunzi 69 waliomaliza darasa la saba katika shule ya msingi ya Waja Springs ya mkoani Geita,Mhe.Kanyasu amewataka wazazi wawe mstari wa mbele katika malezi bora ya watoto wao

.Aidha, Mhe.Kanyasu amewataka pia wahitimu hao wakawe mfano bora katika jamii kwa kuwa kuwasaidia wazazi wao kwa kufanya kazi za majumbani badala ya kuacha kazi zote zifanywe na Wafanyakazi wa ndani

Katika hatua nyingine, Mhe. Kanyasu ameipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa na  kuufanya mkoa wa Geita kuwa miongoni mwa  mkoa inayokuwepo kwenye tano bora kitaifa.

Pia, Mhe.Kanyasu amewataka wanafunzi hao watumie muda mwingi kujisomea vitabu vya hadithi badala ya kutumia muda mwingi kuangalia Televisheni hasa vipindi visivyofaa

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameuhakikishia Uongozi wa shule hiyo kutafuta ufumbuzi wa tatizo la barabara iinayoelekea katika shule hiyo pamoja tatizo maji machafu wakati mvua ikinyesha .

Kwa upande wake Meneja wa Shule hiyo, Mhandisi.Chacha Wambura amewaasa wazazi kujiepusha kuwapatia simu watoto wao ili wasiweze kuingia katika vishawishi katika kipindi hili kifupi walichohitimu masomo yao.

" Wazazi jiepusheni kuwapa simu zenu hawa watoto, hii mitandao ya kijamii inawapelekea watoto kuanza kuangalia mambo yasiyofaa " alisisitiza Wambura.

Aidha, Amewataka Wahitimu hao waache kuzitumia simu za wazazi wao pindi wakiwa majumbani badala yake wasome vitabu kama walivyokuwa wakifundishwa shuleni

Naye, Janeth Ndibalema ambaye ni mzazi wa mhitimu wa darasa la saba, Amesema malezi ya watoto kwa sasa yamekuwa na changamoto nyingi kutokana na wazazi kuacha jukumu la malezi kwa Wasichana wa kazi  hali  inatopelekea watoto wengi kuharibikiwa.

Kufuatia hali hiyo, Ndibalema ametoa wito kwa wazazi kutenga muda kukaa na watoto wao badala ya kujikita kwenye majukumu ya kazi ili kuwasaidia watoto wao kujiepusha kufanya mambo yasiyofaa yatakayowafanya wasiweze kuendelea na shule.

LIVE: Rais Magufuli Anazindua Rada Mbili Za Kuongozea Ndege

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli anazindua Rada mbili (2) za kuongozea ndege za Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanajaro (KIA). Hafla inayofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam .

Marekani Yasema iko tayari kujibu mashambulizi yaliyofanywa Saudi Arabia

$
0
0
Rais Donald Trump amesema Marekani iko tayari kujibu mashambulizi yaliyofanywa katika miundo mbinu ya mafuta ya Saudi Arabia, mashambulizi ambayo Marekani imeoinyoshea kidole cha lawama Iran.

Mashambulizi hayo yamesababisha kuongezeka kwa kiwango kikubwa kwa bei ya mafuta duniani.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais huyo wa Marekani kudokeza kuwa Marekani huenda ikajibu kijeshi mashambulizi hayo yaliyofanywa na ndege isiyo na rubani ambayo yamepunguza uzalishaji mafuta wa Saudi Arabia kwa nusu na kuifanya nchi hiyo ya kifalme pamoja na Marekani kusema kuwa huenda wakaamrisha kutumika kwa hifadhi zao za mafuta iwapo kutakuwa na upungufu.

Katika ujumbe alioutoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Trump ameandika na hapa nanukuu "Usambazaji mafuta wa Saudi Arabia umeshambuliwa. Kuna sababu ya kuamini kwamba tunamjua mhusika, tuko tayari kabisa kulipiza kwa kutegemea na thibitisho lakini tunasubiri Saudi Arabia iseme inayeamini ndiye mhusika wa shambulizi hili," mwisho wa kunukuu.

Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran wamedai kuhusika na mashambulizi hayo katika visima viwili vya mafuta vinavyomilikiwa na kampuni kubwa ya mafuta ya Saudi Arabia, Aramco.

Lakini Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameinyoshea kidole cha lawama Iran akisema hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa mashambulizi hayo yalitokea Yemen.

Iran imeghadhabishwa na kauli hiyo ya Pompeo na msemaji wa wizara ya mambo ya nje Abbas Mousavi amesema madai hayo yasiyo na mwelekeo hayana maana.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman amesema nchi hiyo iko tayari kujibu mashambulizi hayo aliyoyataja kuwa ya kigaidi. 

-DW

Ahukumiwa Kifungo cha miaka 60 kwa kuvutisha bangi watoto na kuwalawiti

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara, imemuhukumu Nyamasheki Malima (41), kifungo cha miaka 60 jela, kwa kumkuta na hatia ya kuwavutisha bangi watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 11 na 13 wa familia moja, kisha kuwalawiti.


Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Hakimu Jacob Ndira amesema kuwa Malima alitenda makosa hayo kati ya Septemba 2017 na Septemba 2018, baadaye alikamatwa na kufikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka yanayomkabili, lakini alikana kufanya kitendo hicho.

Awali, Baba wa watoto hao, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kubaini hali hiyo kwa mtoto mmoja wapo akiwa katika hali isiyo ya kawaida, baada ya kumfanyia uchunguzi na kuwahoji ndipo walimtaja mtuhumiwa ambaye alikuwa anawafanyia vitendo hivyo.

Hakimu Ndira, amesema mahakama ilisikiliza maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili na kuridhika bila ya kuacha shaka yeyote huku mshtakiwa akijitetea mwenyewe.

Kwa mujibu wa majibu ya vipimo yaliyotolewa na daktari aliyewafanyia vipimo watoto hao, unaonesha kuwa sehemu za haja kubwa zilikuwa zinaingiliwa kila wakati baada ya kuwavutisha bangi watoto hao ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi.

Kutokana na maelezo ya kina ya kitabibu ya daktari, hakimu Ndira amesema mahakama imejiridhisha watoto walileweshwa bangi na kulawitiwa.

Hakimu alipo muuliza mshtakiwa kama ana chochote cha kujitetea kwanini mahakama impunguzie adhabu, yeye alidai hana nguvu za kiume hivyo asingeweza kufanya kitendo hicho na kuiomba mahakama imsamehe.

Baada ya utetezi wake Hakimu Ndira alimwambia mtuhumiwa hana namna ya kupunguziwa adhabu, hivyo atakwenda jela miaka 60 kutokana na makosa mawili ya kuwavutisha bangi na kulawiti watoto.

Rais Magufuli Alipongeza Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL)

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa sababu ya ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kumatwa nchini Afrika Kusini ni wivu, kutokana na shirika hilo kuanza kuimarika na kuteka masoko mbalimbli ndani na nje ya Afrika.

Rais ameyasema hayo leo asubuhi alipokuwa akizindua kituo cha mfumo wa rada ya kuongozea ndege katika kituo cha Dar es Salaam, ambayo ni moja ya rada mpya nne zitakazofungwa nchini na kuwezesha kuona na kuongoza ndege katika anga lote la Tanzania.

“Ukiona hadi watu wanakamata ndege zetu basi ujue shirika letu linafanya kazi vizuri,” alisema Rais Magufuli

Amesema kuwa licha ya kukamatwa kwa ndege hiyo (ambayo tayari imeshaachiliwa) ataendelea kuchapaka kazi, huku akitolea mfano kutoka kwenye mashairi ya wimbo wa kundi la Sauti Sol la Kenya, wimbo unaoitwa Extravaganza ambao mashairi hayo yanasema, wakifunika, tunafua, wakianika, tunaanua, wakitufungia milango, wanatukuta ndani.

Rais ametoa pongezi kwa ATCL kwa namna ambavyo limekuwa likikua huku akieleza kwamba wakati lilipoanza safari zake lilikuwa likimiliki asilimia tatu pekee ya soko la ndani, lakini sasa linamiliki asilimia 75. Ameongeza kuwa, tayari shirika hilo limeanza safari za kimataifa, na karibuni litaanza kwenda China, hivyo ni lazima washindani wake waone wivu.

Akizungumzia rada iliyopaswa kununua kipindi cha nyuma, Rais ameonesha kukerwa kwamba fedha za Watanzania zilitafunwa na watu wachache na rada hiyo iliyokuwa inunuliwe nchini Uingereza haikusimikwa tena, hivyo mabilioni ya fedha yakawa yamepotea. Amesema aliwashangaa waliohusika kwenye sakata hilo kutokujiuzulu, angali wale wa upande wa Uingereza walijiuzulu.

Baada ya mifumo mipya ya rada za kuongozea ndege kukamilika kusimikwa, Tanzania itaweza kuona na kuongoza angala lote la nchi, tofauti na awali ambapo ilikuwa inaweza kuongoza asilimia 25 pekee ya anga lote.

Kuwa na uwezo wa kuongoza anga lote kutaongeza mapato ya serikali, kutaongeza kasi ya ndege kuweza kuruka na kutua katika viwanja vya Tanzania, hatua itakayoongeza abiria, lakini pia hatua hiyo ni kukidhi vigezo vya kimataifa.

Serikali Yachukizwa Na Mgongano Wa DC, DED Malinyi ....Waziri Mkuu Aelekeza Weledi Wao Kiutendaji Uchunguzwe

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amechukizwa na mgongano uliopo kati ya Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Majura Kasika na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Mussa Mnyeti, hivyo kumuelekeza Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kwenda kuchunguza weledi wa utendaji kazi  wao.

“Ni aibu Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli amewateua vijana wawe viongozi lakini leo hadi wananchi wa kawaida wanajua mgongano wenu maofisini. Ni aibu Mkuu wa Wilaya ya Mkurugenzi mnagombana tena wakati mwingine mnagombania miradi, mmesahau kutekeleza majukumu yenu.”

Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo leo (Jumatatu, Septemba 16, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Malinyi pamoja na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Toboa, akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Amesema Serikali imewapa nafasi hiyo ili wakasimamie maendeleo ya wananchi na inapeleka fedha kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya jamii kama kuimarisha huduma za afya, elimu, maji na miundombinu ya barabara lakini wao wanagombania miradi na mingine wanaichakachua.

Waziri Mkuu amesema mbali na CAG na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kwenda kuchunguza utendaji wa viongozi hao, pia ameuelekeza uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakakague miradi ya ujenzi inayotekelezwa kwenye wilaya hiyo kama ubora wake unalingana na thamani halisi.” Baada ya kupata majibu ya uchunguzi na kubaini kiini cha tatizo ndani ya wilaya hii hatua zitachukuliwa.”

Awali, Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Dkt. Haji Mponda alimweleza Waziri Mkuu kwamba kwenye wilaya hiyo kuna matatizo ya mahusiano kati ya Serikali na Halmashauri jambo linalosababisha kukwama kwa shughuli za maendeleo.

Mbunge huyo alisema kutoelewana kwa viongozi wa wilaya hiyo Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kumesababisha mgawanyo mkubwa kuanzia katika Baraza la Madiwani hadi kwa wananchi mitaani, hivvyo alimuomba Waziri Mkuu awasaidie katika. Kilipatia ufumbuzi suala hilo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu  amesema kuwepo kwa mabango mengi kwenye mikutano ya hadhara  ya viongozi wakuu kunadhihirisha wazi kwamba watendaji wa Halmashauri hawawatembelei  wananchi katika maeneo yao na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

“Watendaji hamuendi kuwatembelea wananchi na kusikiliza matatizo yao, haiwezekana wawe wanawasubiri viongozi wa juu na kuwasilisha kero zao kwa njia ya mabango, sasa jipangeni haya mabango yote mtakuja kuyajibu kwa sababu katika mabango yao hakuna hoja hata moja inayomuhusu Waziri Mkuu zote ni za ngazi ya halmashauri.”

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa kiwango kinachostahili.

Mapemaalipowasili wilayani Malinyi, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi linalojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa kwa gharama ya sh. bilioni 3.9. Ujenzi huo ulianza 29/11/ 2017 na utakamilika 29/09/ 2019.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
Dalili:mwili kuchoka,maumivu ya mgongo na kiuno,kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu

Misuli  kulegea na kusinyaa hata kushindwa kufika kileleni miguu kuuma na kuwaka moto:

TIBA YAKE:

TULLO4 MIX.Ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizi hayo, inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kukufanya urudie tendo la ndoa zaidi mara tatu bila kuchoka au kukinai.

NTINJE3 PUMP.Ni dawa inayoongeza maumbile na kukupa umbile la kudumu.Itumie tiba hii kuokoa ndoa yako na kuokoa kukimbiwa na umpendae.
GASELA: Ni dawa mvuto kumvuta umpendae na kumrudisha alie mbali .

NTOBO: Inatibu KISUKARI:siku7 na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenyetatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari.

mpigie DR LIZENGO .OFISI IPO MBAGALA SABASABA.SIMU 0655283534/0621737576

LIVE: Rais Magufuli Anazindua Kiwanda Cha Kutengeneza Mabomba Ya Plastiki

$
0
0
LIVE:  Rais Magufuli Anazindua  Kiwanda Cha Kutengeneza Mabomba Ya Plastiki

Ofisi Ya Makamu Wa Rais Yaadhimisha Siku Ya Tabaka La Ozoni Duniani Kwa Kutoa Mafunzo Kwa Mafundi Mchundo Wanaoshughulikia Majokofu Na Viyoyozi.

$
0
0
Utafiti wa kisayansi katika tabaka la ozoni katika karne ya ishirini ulithibitisha kumong’onyoka kwa  tabaka hilo kutokana na kulundikana angani kwa kemikali aina ya chloroflourocarbons (CFCs), halons, methyl choroform, methyl bromide, carbon tertrachoridena nyinginezo. 

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Chuo cha VETA– Chang’ombe Bi Vaileth Mfumbwa wakati wa warsha ya mafunzo kwa Mafundi mchundo wanaoshughulikia majokofu na viyoyozi  ikiwa ni maadhimisho ya siku ya tabaka la ozoni Duniani  iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, iliyofanyika katika Chuo cha VETA-Chang’ombe jijini Dar Es Salaam.
 
Aliongeza kuwa Kemikali hizi hutumika katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya kuzimia moto, ushafishaji chuma, utengenezaji wa magodoro, madawa na manukato ya kupulizia, ufukizaji wa udongo katika vitalu vya tumbaku na mashamba ya maua na ufukizaji wa mazao katika maghala kabla ya kusafirishwa nje ya nchi. Matumizi ya kemikali hizi yapo kwa wingi katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea, kama Tanzania.
 
Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bi Kemilembe Mutasa  alisema kuwa , Kitaifa maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni yanafanyika jijini Dar es Salaam ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira kwa kushirikiana na Wakufunzi wa Chuo cha Ufundi Dar es salaam wamepanga kutoa mafunzo kwa vitendo kwa mafundi mchundo wanaohudumia majokofu na viyoyozi kuhusu njia bora za kuhudumia vifaa hivyo; kutoa elimu jinsi ya kutumia vitambuzi vya gesi; na kubadilisha tekinolojia zinazotumia kemikali haribifu kwa tabaka la Ozoni kwa kemikali mbadala. 
 
“Katika maadhimisho haya, tunakumbushwa kuwa katika Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Monteral uliofanyika nchini Rwanda mwaka 2016, nchi wanachama zilikubaliana kupunguza uzalishaji na utumiaji wa  kemikali jamii ya Hydrofluorocarbons (HFCs) ambazo pia hujulikana kama R-143a kwa jina la biashara  na kukubaliana kuzuia ongezeko la joto la dunia kwa nyuzi joto 0.5 (0.5 degrees Celsius)” alisema Bi. Mutasa 
 
Warsha hiyo ya mafunzo ya siku moja imekua chachu kwa Mafundi Mchundo wanaoshughulikia majokofu na viyoyozi kwa kufundishwa njia mbalimbali za kiutaalamu za kutumia wanapokua katika shughuli zao za kila siku.  Mafunzo hayo yalitolewa na Wakufunzi wa Chuo cha Ufundi-VETA Chang’ombe jijini Dar Es Salaam.

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao.

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari.

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume.

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18.

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

Pia tunadawa za Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto.
 
DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 AU  0762293390 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo,Pamoja Na Magonjwa Sugu

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  call 0759 208 637

watsap  0620510598

Wizara Ya Kilimo Yafanya Maaandalizi Ya Sera Mpya Ya Kilimo

$
0
0
Waziri wa Kilimo Japheti Hassunga leo  amekutana na Menejimenti ya wizara,wakuu wa Taasisi na  Wenyeviti wa Bodi za Mazao  zilizopo chini  ya Wizara.  

Lengo la mkutano huu wa siku mbili unaofanyika  katika ukumbi wa wizara Jijini Dodoma  ni kujadili maandalizi ya sera mpya ya kilimo ya mwaka 2019 na kuondoa mapungufu yaliopo katika sera ya mwaka 2013. 

Akiongea katika kikao kazi hicho Waziri  Hasunga ameeleza umuhimu wa kuwa na sera mpya ya kilimo ni kufanya kilimo kuwa na tija na cha kibiashara ,hivyo kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo 

“Tunataka sera mpya ya kilimo ilenge kukifanya kilimo kuwa shughuli kuu ya kiuchumi itakayochangia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira” alisisitiza Waziri Hasunga. 

 Waziri Hasunga amebainisha kwamba sera mpya  inatakiwa kukamilika  kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kutoa fursa kwa Bunge kutunga sheria na kanuni za kilimo. 

Aidha katika mkutano huu wizara ya kilimo itajadili na kupitia taarifa ya utekelezaji wa shughuli kwa mwaka 2018/2019 na kuweka mkakati madhubuti wa utekelezaji mipango utendaji kazi ya wizara kwa mwaka 2019/2020. 

Kikao hicho kinahudhuriwa na Manaibu Waziri Hussein Bashe na Omary Mgumba,Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu Prof.Siza Tumbo. 

Mwisho.
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo-DODOMA
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>