Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mbalawa Alipongeza Shirika La Maendeleo La Ujeruman Kwa Kufanikisha Mradi Wa Maji Ulioshindikana Takribani Miaka 7.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
SERIKALI imesema kuwa imejipanga kukarabati miradi yote ya maji iliyotelekezwa kwa kipindi kirefu ili kupunguza adha ya uhaba wa maji kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa jana Septemba 11,2019  jijini Dodoma  na Waziri wa Maji Prof.Makame Mbalawa wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Nghong'onha Katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji Katika kata hiyo .

Waziri Mbalawa amesema makandarasi wa ovyo wamekuwa wakikwamisha juhudi za serikali Katika maendeleo na kusababisha hasara hivyo  kuwataka kujitathimini upya.

"Serikali haitomfumbia macho mkandarasi yeyote anayegeuza miradi ya maji Kama kitega uchumi chake,lazima kila mtu akae kwenye mstari kuhakikisha anafanya maendeleo kwa moyo mmoja,"amesema.

WaziriProf.Mbalawa amesema Mradi wa maji Katika kata hiyo ulianza tangu  mwaka 2013  ambapo umechukua miaka 7 kukamilika kwake huku akilipongeza Shirika la Maendeleo la Ujeruman [ GIZ ]Kwa kufanikisha mradi huo.

"Huu ni uzembe mkubwa ,Mradi wa maji unachukua miaka mingi tunaweza kuufananisha na umri wa mtoto ambapo mwaka 2013 angezaliwa mwaka angeanza darasa la kwanza,"alisema na kuongeza,

"Katika Mradi huu kulifanyika uzembe wa hali ya juu na uhuni kwani Mradi huu ulitakiwa kukamilika kwa kipindi Cha miezi sita tu tangu kuanza kwake,"alisisitiza Mbalawa.

Kutokana na hayo amewataka watendaji wote wa wizara ya maji kuhakikisha wanakuwa makini kushughulikia miradi ya huduma za kijamii ili kuhakikisha inaondoa kero kwa wananchi.

Mwakilishi wa Shirika la maendeleo la Ujerumani (GIZ)Vera Rosender alisema Mradi huo Hadi kukamilika ,umegharimu jumla ya shilingi milioni 350 huku akiongeza kuwa Serikali ya Ujerumani kwa kuona umuhimu wa maendeleo iliamua kusaidia kuwapatia maji wakazi hao ambao tangu kipindi Cha Uhuru hawajawahi kuwa na maji ya uhakika.

Kwa upande wake mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira (DUWASA)Mhandisi David Palangyo aliishukuru serikali ya Ujerumani kujitolea kushirikiana nao kutatua kero ya maji kwa wakazi wa Kata ya Nghong'onha .

Mhandisi huyo amesema wao Kama wadau wa maji watahakikisha wanakuwa karibu na wakazi hao kuhakikisha wanalinda miundombinu ya maji huku wakijipanga kuanzisha kamati ya maji ya kata hiyo itakayosimamia mapato kwa uzalendo.

"Hakuna asiyefahamu shida nliokuwa mkiipata,na Sasa mmepata maji moiyoyatamani kwa kipindi kirefu tafadhalini ndugu zangu tushirikiane kwa pamoja kuyaenzi kwani maji ni uhai,"alisema.

Pia amefafanua kuwa  kabla ya Mradi huo kukamilika wananchi walikuwa wakitumia maji yasiyo salama na kwamba walinunua ndoo moja ya maji kwa shilingi miatano ambapo kwa Sasa Lita 20 ya maji itauzwa kwa shilingi 25.

Naye Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma ,ambaye pia ni Mkuu wa  wilaya Patrobas Katambi aliwataka wananchi wa Nghong'onha kuitunza miundombinu ya maji na kuepuka kuihujumu.

"Tunafahamu Kuna watu hawapendi maendeleo nataka kuwaambia kila mtu awe mlinzi wa mwenzie ,hakikisheni pia mnalinda mazingira ya vyanzo vya maji ili kiendelea kufurahia  huduma hiyo,"amesema.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma  Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi ,vijana na Ajira,Mhe.Anthony Mavunde amesema kukamilika kwa mradi huo itakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo ambapo amebainisha kuwa alikuwa halali usiku na mchana kutafuta mwarobaini wa kutatua kero ya maji.
“Wakati nasaka kura hapa nilisema yasipokuja maji Nghong’ona  mpaka kufikia mwaka 2020 msinipigie kura,Moyo wangu ulikuwa unadunda sasa inakaribia 2020 na Maji bado,nililuwa silali napita hapa na pale kuhakikisha tatizo la uhaba wa maji linatatuliwa,lakini sasa imekuwa historia tujivunie tatizo hili ni la muda mrefu .amesema.

Kwa upande wao Baadhi ya Wananchi wa kata hiyo wamesema uzinduzi wa Mradi huo wa maji utawasaidia kuepukana na kero kubwa ya adha ya maji ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo ambapo awali ndoo moja walikuwa wananunua kwa Tsh.300 hadi 400 lakini sasa watakuwa wananunua kwa Tsh.25 tu kwa ndoo katika mradi huo hali ambayo itapunguza ukali wa Maisha.

 Jumla ya wakazi  10500 wa Kata ya Nghong'onha wanatarajiwa kunufaika na Mradi huo.

Hakimu Kortini kwa Tuhuma za Rushwa

$
0
0
Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kinondoni, jana Jumatano, Septemba 11, 2019, iliwafikisha mahakamani watuhumiwa watatu wa rushwa akiwemo Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo jijini Dar es Salaam, baada ya kukamilika kwa uchunguzi dhidi yao.

Takukuru imesema watuhumiwa hao ni Omary Mohammed Abdallah (40) aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni jijini Dar, ambaye ni mkazi wa Kijitonyama kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kiasi Tsh 703,000, Joseph Balongo (37) mfanyabiashara na mkazi wa Kibamba kwa kosa la kupokea rushwa ya Tsh 498,000 kinyume na sheria.
 

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007.

“Ilidaiwa kuwa mnamo Februari 12, 2017, Abdalah alimtaka mtoa taarifa ampe kiasi cha Sh. milioni moja ili aweze kumsadia kwenye kesi ya mirathi iliyokuwa mbele yake kinyume na utaratibu,” alisema.

Vile vile, alisema mlalamikaji alitoa taarifa Takukuru Wilaya ya Kinondoni, Machi mosi, 2017, uchunguzi ulifanyika na kubaini kuwa tuhuma hizo ni za kweli na shauri hilo kuanza upya.

“Uchunguzi dhidi ya tuhuma zote mbili umekamilika na watuhumiwa wamefikishwa katika Mahakama ya Kinondoni kujibu tuhuma zinazowakabili,” alibainisha.

Katika hatua nyingine, Takukuru imemfikisha mahakamani Katibu wa Kamati ya Upimaji wa viwanja katika Mtaa wa Nyakasangwe, Nerbert Malevu (33) kwa kuomba rushwa ya Sh. milioni 2.5 na kupokea Sh. 500,000.

Ilidaiwa kuwa mnamo Agosti 14, mwaka huu, mtuhumiwa huyo alimtaka mtoa taarifa ampatie fedha hizo ili aweze kumpatia sehemu ya kiwanja ambacho kilikuwa cha mtoa taarifa kabla ya upimaji na kwa madai kuwa sehemu ya kiwanja hicho kiligaiwa mtu mwingine baada ya upimaji.

“Mlalamikaji alitoa taarifa Takukuru na Agosti 16, mwaka huu uchunguzi ulifanyika, tuliandaa mtego wa rushwa na kumkamata mtuhumiwa Agosti 20, majira ya saa 10 eneo la Mwenge Lukani Pub, baada ya kupokea Sh. 500,000,” alisema Mnjagira.

Alisema, Takukuru mkoani humo imetoa wito kwa watumishi wa umma na sekta binafsi wanaodhani hawawezi kutoa huduma bila ya kuomba na kupokea rushwa, kwamba waache tabia hiyo kwa kuwa ni kosa la jinai.

Wanawake Wanne na Mwanaume Mmoja Wahukumia Jela Miezi 6 Kwa Kufanya Biashara ya Ukahaba

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Wanawake 4 na Mwanaume mmoja anaedaiwa kuwa ni mteja wao wamehukumiwa kifungo cha miezi 6 na Mahakama ya Mwanzo Makole, Dodoma na adhabu ya viboko 3 wakati wa kuingia, kwa kujihusisha na biashara ya ukahaba kufuatia msako wa kuwakamata Wanawake wanaodaiwa kuwa ni makahaba Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dodoma  kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto  aliwataja waliokamatwa na kuhukumiwa kifungo hicho bila  faini na mmoja aliyehukumiwa miezi mitatu baada ya kukiri kosa, kuwa ni Erica George (24), Lucy Saibati (28), Joyce Ndekwa (30),Hawa Said (28), na Grolia Michael (29).

Kamanda Muroto alisema, Septemba 8, mwaka huu katika Mtaa wa Uhindini, Kata ya Viwandani, watu hao walikamatwa kwa kosa la kufanya ukahaba kinyume na kifungu cha sheria namba 176 (a), f na g cha kanuni ya adhabu ya sura ya 16.
 
Aidha, kamanda muroto amesema  mnamo tarehe 8/9/2019 katika kituo cha polisi kati Dodoma kundi kubwa la waendesha pikipiki (Bodaboda) zaidi ya 70 walivamia kituo  cha polisi  wilaya ya Dodoma na kufanya fujo wakitaka kumtoa mtuhumiwa aliye kuwa mahabusu Bwana Brazil Mjungu aliyekamatwa baada ya kusababisha ajali ya gari kumgonga mwendesha pikipiki ili wamuadhibu kwa kujichulia sheria mkononi.

Watu 20 wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kufunguliwa mashtaka.
 
Katika hatua nyingine Kamanda muroto amesema wanaendelea na msako wa bodaboda wanao tumia pikipiki  za uhalifu, kwani jumla ya pikipiki 19 zimekamatwa zikidhaniwa kuwa niza uwizi na zinazotumika kufanya uhalifu.
 
Hata hivyo, Muroto amesema kuwa wanaendelea na misako katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma lengo likiwa ni kuwahakikisha kuwa raia wema hawabugudhiwi na wahalifu na wanafanya shughuli zao katika hali ya utulivu.
 
Ikumbukwe kuwa jeshi la polisi  liliwakamata na  kuwafikisha
mahakamani wanawake 15 wanaojiuza ambapo walihukumia kifungo cha miezi sita kila moja huku wanaume wanne waliosadikiwa kuwa ni wateja wao wakiachiwa baada ya kukosekana kwa ushahidi.
 
Hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limetoa onyo kwa wale wote watakao vunja sheria kwa makusudi kwani watakao kamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao .

Zuio La Kuendelea Na Masomo Kwa Wanafunzi Wajawazito Lasaidia Kupunguza Matukio Ya Mimba Shuleni

$
0
0
Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Zuio la kuendelea na masomo kwa wanafunzi wanaobebeshwa ujauzito wakiwa shuleni linatajwa kusaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza matukio ya mimba kwa wanafunzi katika meneo mengi Nchini.

Naibu Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Mh.   William  Ole Nasha ameyabainisha hayo  Bungeni Jijin Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Mh. Aida Joesph Kenan aliehoji juu ya matamko na makatazo ya wanafunzi wajawazito kurudi shuleni yamesaidia kwa kias gani.

Amesema pamoja na matamko hayo pia Serikali imeweka mpango wa kupunguza changamoto kwa watoto wa kike ikiwemo kujenga mabweni na hosteli katika maeneo ambayo wanafunzi wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.

Mh. Ole Nasha ameongeza kuwa serikali kwa kushirikiana na wananchi katika Halmashauri zao wanaendesha zoezi la ujenzi wa mabweni ili kuwaepusha wanafunzi hao kutembea umbali mrefu na lengo la kuwapeleka katika vyuo vya ufundi wanafunzi wanaobebeshwa ujauzito ili kuwasaidia kujiepusha na unyanyapaa ambao unaweza kujitokeza.

Aidha Mh. Ole Nasha ametoa wito kwa wazazi na walezi Nchini kushirikiana na Serikali katika kutokomeza matukio ya kubebeshwa mimba wanafunzi na inapotokea hivyo wahusika wafikishwe katika vyombo vya dola huku pia akitumia fursa hiyo kuwatakia mtihani mwema wanafunzi wote wa shule za msingi Nchini ambao leo wameanza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi.

Mwaka 2017 Rais Dr. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Chalinze mkoani Pwani alitangaza chini ya utawala wake hakuna mwanafunzi majamzito atakaeruhusiwa kurudi shuleni kuendelea na masomo na mwanaume aliehusika kumbebesha mimba mwanafunzi atafungwa miaka 30 jela

Freeman Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA Wakutwa na Kesi ya Kujibu

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewakuta na kesi ya kujibu viongozi 9 wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) akiwemo Mwnyekiti wa CHADEMA, Freeman  Mbowe

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi Septemba 12, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao.

Washtakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kufanya maandamano bila kibali, kushawishi wananchi kuichukia Serikali na uchochezi, matukio yanayodaiwa kufanyika Februari 16 mwaka 2018 wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

Rais Magufuli Amteua Kamishna Diwani Athumani Kuwa Mkurugenzi Mkuu Wa Idara Ya Usalama Wa Taifa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athumani Msuya Kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (DGIS) Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 12, 2019
PICHA NA IKULU

Majeruhi watatu ajali ya lori la mafuta Morogoro waruhusiwa kutoka Muhimbili

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imethibitisha kuwa, majeruhi watatu kati ya 11 wa ajali ya moto Morogoro waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo, wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya afya zao kuimarika.

Akizungumza leo Septemba 12, Dkt Edwin Mrema  ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Upasuaji amesema kuwa, kabla ya kuwaruhusu  hospitali hiyo imewapa huduma za kisaikolojia kwa kuwa tatizo la moto lilikuwa limewathiri kwa kiasi kikubwa.

“Majeruhi walikuwa wamebaki 11 hivyo sasa wamebaki wanane kati ya 47 waliofikishwa Muhimbili Agosti 11, ambapo majeruhi 36 walipoteza maisha. Tunaendelea kuwatibu majeruhi na kuwatafuta wanasaikolojia."  Amesema Dk Mrema.

Akizungumzia mgonjwa ambaye hadi sasa yuko kitengo cha uangalizi wa karibu (ICU), amesema kwa kuwa alikuwa ameungua zaidi miguuni, iliwalazimu kutoa viungo ambavyo vilionekana kupoteza uhai na amehifadhiwa katika chumba maalumu cha uangalizi ili kuzuia maambukizi kwa majeraha yake.

Aidha wakati mgonjwa mmoja bado yupo ICU, wengine wapo wodi ya kawaida wakiendelea na matibabu na hali zao zinaimarika.

Tukio la ajali ya moto Mkoani Morogoro, lilitokea Agosti 10, baada ya lori la mafuta kupinduka na kupelekea mlipuko wa moto

Wakazi 60 kutoka Kakola na Bugarama Halmashauri ya Msalala kunufaika na huduma za matibabu bure mwaka mzima baada kupatiwa kadi za CHF.

$
0
0
NA SALVATORY NTANDU
Baraza la Madiwani la halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga limewafukuza kazi watumishi 46 waliojipatia kazi kwa njia ya udanganyifu kwa kughushi vyeti vya taaluma na kuisababishia serikali hasara.

Uamuzi huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Mibako Mabubu kwenye kikao cha kawaida cha kufunga mwaka wa fedha wa 2018/19 kilichofanyika jana katika makao makuu ya halmashauri hiyo.

Amesema watumishi hao walibainika katika zoezi la uhakiki watumishi hewa ambalo lilifanyika nchi nzima mwanzoni mwa mwaka 2014 na idara zilizobainika kuwa na watumishi wengini ni idara ya afya na Maji.

Amefafanua kuwa watumishi hao walighushi vyeti na kujipatia ajira hizo kinyume na sheria za Utumishi wa Umma na kuisababishia serikali hasara huku wajijua wazimkuwa ni kosa.

Mibako amesema baada ya kuchukua hatua hizo baraza liliandikia wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kuhusu suala hilo ambapo hatua za haraka zilichukuliwa na tayari imeshaanza kuleta watumishi katika idara hizo.

Baraza la Madiwani Msalala mkoani Shinynga la wafukuza kazi watumishi wa umma 46 waliobainika kughushi vyeti vya taaluma

$
0
0
NA SALVATORY NTANDU
Baraza la Madiwani la halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga limewafukuza kazi watumishi 46 waliojipatia kazi kwa njia ya udanganyifu kwa kughushi vyeti vya taaluma na kuisababishia serikali hasara.

Uamuzi huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Mibako Mabubu kwenye kikao cha kawaida cha kufunga mwaka wa fedha wa 2018/19 kilichofanyika jana katika makao makuu ya halmashauri hiyo.

Amesema watumishi hao walibainika katika zoezi la uhakiki watumishi hewa ambalo lilifanyika nchi nzima mwanzoni mwa mwaka 2014 na idara zilizobainika kuwa na watumishi wengini ni idara ya afya na Maji.

Amefafanua kuwa watumishi hao walighushi vyeti na kujipatia ajira hizo kinyume na sheria za Utumishi wa Umma na kuisababishia serikali hasara huku wajijua wazimkuwa ni kosa.

Mibako amesema baada ya kuchukua hatua hizo baraza liliandikia wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kuhusu suala hilo ambapo hatua za haraka zilichukuliwa na tayari imeshaanza kuleta watumishi katika idara hizo.

Wawekezaji Kutoka Nchi Jirani Sasa Wapishana Kuchangamkia Uwekezaji Kagera ....Ni Baada Ya Wiki Ya Uwekezaji Kuwaonesha Fursa

$
0
0
Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.
Juhudi za viongozi wa mkoa wa Kagera kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha uchumi wa nchi za Afrika Mashariki na Kati zilizoanzia katika Wiki ya Uwekezaji Kagera sasa zaanza kuzaa matunda ni baada ya kundi la wawekezaji kutoka nchi jirani ya Rwanda kuitikia wito wa kuwekeza mkoani humo.
 
Kundi la Wawekezaji kumi wanaomiliki mampuni mbalimbali ya biashara nchini Rwanda walioamua kuunda Kampuni moja ya uwekezaji mkoani Kagera katika Sekta ya ufugaji wa kisasa na kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama waliwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti ili kumweleza nia yao na kuwa wapo tayari kuwekeza katika ufugaji na kiwanda cha kusindika nyama.
 
Bw. William Kawamala kiongozi wa wawekezaji hao kumi kutoka nchini Rwanda alimweleza Mkuu wa Mkoa Gaguti kuwa wapo tayari kuwekeza katika sekta ya ufugaji  wa kisasa wa ng’ombe katika Kampuni za  Ranchi za Taifa (NARCO) baada ya kupata fursa hiyo katika Wiki ya Uwekezaji Kagera iliyofanyika tarehe 12 hadi 17 Agosti, 2019.
 
“Sisi baada ya kushiriki Wiki ya Uwekezaji Kagera tulivutiwa kuwekeza katika Sekta ya ufugaji, na tuliporudi kwetu nchini Rwanda tilikaa pamoja na kukubaliana tujiunge kwa pamoja wafanyabiashara kumi ili kuanza uwekezaji mara moja, ndiyo maana tupo hapa ili kuanza hatua za awali pia tumekuja kuona maeneo ya kufugia na kuweka kiwanda..”  Alifafanua Bw. Kawamala
 
Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwakaribisha wawekezaji hao na kusema kuwa mkoa upo tayari kuwapa ushirikiano,  hatua ya kwanza alimwelekeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NARCO Prof. Philemon Wambula pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Sekretarieti ya mkoa  kuwaonesha maeneo yaliyotengwa ili wakubaliane nayo na taratibu  za kusajili kampuni na kuanza uwekezaji zianze mara moja.
 
“Baada ya Wiki ya Uwekezaji mwitikio umekuwa mkubwa sana wa wawekezaji kuja kwetu kuchangamkia fursa zilizopo Kagera na sisi tumejipanga tunawapokea na kuwaelekeza taratibu za uwekezaji, lakini jukumu letu ni kuhakikisha fursa zote ambazo wawekezaji wameziona wanazitumia katika uwekezaji ili kukuza uchumi wa mkoa wetu.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti
 
Profesa Philemon Wambula Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni za Ranchi za Taifa (NARCO) alisema kuwa mkoa wa Kagera bado una fursa kubwa za uwekezaji katika sekta ya mifugo hasa katika viwanda vya kusindika nyama na maziwa pia uwekezaji katika malisho ya mifugo aidha, NARCO bado inayo maeneo makubwa ya kuwekeza.
 
Wawekezaji hao kumi walieleza kuwa baada ya kuona maeneo wanataka kuwekeza katika ufugaji wa kisasa wa ng’ombe, ujenzi wa kiwanda cha kuchinja na kusindika nyama kwa viwango vya kimataifa. “Kwasasa baadhi ya Hoteli kubwa nchini Rwanda zimeanza kuagiza nyama kutoka nchi za Ulaya wakati tukifuga kisasa hapa Kagera tunaweza kuilisha Rwanda.”  Walisisitiza Wawekezaji hao kutoka nchini Rwanda.
 
 Kwa  Msaada Wa Ofisi Ya Mkuu Wa MKoa Kagera.

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao.

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari.

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume.

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18.

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

Pia tunadawa za Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto.
 
DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 AU  0762293390 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Erick Kabendera Asema Bado ni Mgonjwa, Mahakama Yatoa Maelekezo

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera (39), ambaye hali yake ya kiafya bado ni tete, arudi mahakamani baada ya siku saba ili kupata taarifa ya matibabu.

Uamuzi huo ulitolewa leo saa tatu asubuhi wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa katika mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Mahakama ilimpa nafasi Kabendera kuelezea maumivu anayosikia ambapo akijieleza alidai hali ya kushindwa kupumua usiku bado inaendelea na siku nane zilizopita alisikia maumivu makali mguu wa kulia, maumivu makali katika mfupa ndani ya paja hali inayomfanya akose usingizi.


Kabendera amesema  kuwa madaktari wa Gereza la Segerea walimpima damu na kumchoma Sindano tatu kutokana na tatizo la  kushindwa kupumua.
 
Amedai kuwa madaktari hao hawana vifaa vya kuwasaidia kugundua tatizo alilonalo hivyo, wamemshauri kufanya mazoezi.

Alidai mguu wa kulia na mfupa wa paja wa mguu huo una maumivu makali

Huku akionekana kuwa na maumivu makali, alidai alionana na daktari Alhamis iliyopita na juzi (jana) alimuona lakini hakumfanyia vipimo kwa sababu walikuwa na wageni hivyo, aliahidi kuonana naye leo.

“Nipo Segerea na kuna utaratibu wa madaktari kufanya matibabu kwa wagonjwa kila siku,” alidai.

Hatua ya Kabendera kueleza hayo ni baada ya Wakili wake, Jebra Kambole kudai kuwa hali ya mshitakiwa huyo inazidi kutetereka kwa sababu anashindwa kutembea vizuri na kushindwa kupumua.

Kambole amedai bado Kabendera hajafanyiwa matibabu vizuri kujua tatizo linalomsumbua na kuomba mahakama ielekeze magereza wampeleke hospitali yoyote ya Serikali ikiwamo Muhimbili ili wapate ripoti ya ugonjwa unaomsumbua.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai amewasiliana na Mkuu wa Gereza na kumueleza kuwa Kabendera anapatiwa matibabu na madaktari wamekuwa wakimuangalia mara kwa mara.

Amedai magereza wana utaratibu wao endapo wataona ugonjwa unaomsumbua unahitaji rufaa, watampeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 18, mwaka huu 2019 na kumuelekeza Kabendera kuonana na daktari kisha itakapotajwa tarehe nyingine ataieleza mahakama kama amepata matibabu au la ili mahakama itoe maelekezo.

Waliokuwa Wafanyakazi Na Wateja Wa Benki Ya Fbme Kulipwa Amana

$
0
0
Na. Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma
SERIKALI imeeleza kuwa itawalipa waliokuwa wateja na wafanyakazi wa Benki ya FBME baada ya taratibu za kisheria na majadiliano na Cyprus yatakapo kamilika hivi punde.

Hayo yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu maswali ya Mhe. Jaku Ayoub, aliyetaka kujua Benki ya FBME ipo katika hali gani na ni lini italipa wateja amana zao.

Dkt. Kijaji alisema kuwa wateja wa Benki ya FBME waliokuwa na amana ya milioni 1.5 Serikali imewalipa kwa zaidi ya asilimia 83 ya wateja wote, asilimia 17 iliyobaki ni ya wateja ambao hawajajitokeza kuchukua amana hizo.

“Bodi ya Bima ya Amana (Deposit Insurance Board- DIB) ilianza zoezi la kulipa fidia kwa mujibu wa sheria kwa waliokuwa na amana katika benki hiyo kuanzia Novemba, 2017 na bado zoezi hilo linaendelea”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa hadi kufikia Septemba 9, 2019 jumla ya kiasi cha Sh. milioni 2,404.2 kimelipwa kwa wateja 3426 kama fidia ya bima ya amana, ambapo kiasi hicho ni sawa na asilimia 55.9 ya kiasi chote kilichotarajiwa kulipwa kama fidia ya bima ya amana kwa wateja wote 6,628 waliopo Tanzania na wateja waliopo nje ya nchi (Tanzania International Banking Depositors- TIB)

Aidha jumla ya Sh. milioni 2,401.2 zimelipwa, ikiwa ni asilimia 83.3 ya lengo la kulipa jumla ya Sh. milioni 2,882.6 kwa wateja waliopo Tanzania tu.

Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango, amempongeza Mwanasheria na Wakili Mkuu wa Serikali pamoja na Benki Kuu ya Tanzania kwa kuhakikisha amana za wateja FBME ambao wako ndani na nje ya nchi zinabaki salama na kuzipata baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Dkt. Kijaji aliongeza kuwa, Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 imeipa Benki Kuu ya Tanzania- BOT, mamlaka ya kutoa leseni, kutunga kanuni, kusimamia benki zote zinazochukua amana za wateja na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya benki zinazoendesha biashara bila kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.

 Kwa ujumla Benki Kuu imepewa mamlaka ya kusimamia na kudhibiti benki na taasisi za fedha ili kuhakikisha kuwa amana za wateja zinakuwa salama na pia kuna usalama, utulivu na uthabiti wa sekta ya fedha na uchumi.

Benki ya FBME Ltd ilifutiwa leseni ya kufanya biashara hapa Tanzania na Benki Kuu ya Tanzania Mei 8, 2017 kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara ya kutakatisha fedha nchini Marekani.

Benki  Kuu nchini Tanzania iliiteua Bodi ya Bima ya Amana- DIB kuwa mfilisi wa Benki ya FBME, hivyo kwa sasa  benki hiyo haiendeshi shughuli zozote za kibenki hapa nchini.

Mwisho.

Serikali Kuwezesha Wakala Wa Mbegu Za Kilimo (Asa) Kuongeza Uzalishaji Wa Mbegu Bora Na Kuimarisha Soko La Zao La Nazi

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Upatikanaji wa mbegu bora zikiwemo za mahindi ngano, maharage, mpunga, soya, alizeti, mtama, ufuta, viazi mviringo na mbegu za mazao ya bustani kwa msimu wa 2018/19 ulifikia tani 49,040 kati ya hizo tani 38,507 sawa na asilimia 78.6 zilizalishwa nchini na tani 8,361 sawa na asilimia 17 ziliagizwa nje ya nchi na tani 2,171 sawa na asilimia 4.4 ni bakaa ya msimu wa 2017/2018.


Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe ameyasema hayo leo tarehe 12 Septemba 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Kasulu Mjini Mhe Daniel Nsanzugwanko mkakati wa serikali katika kutatua uhaba mkubwa wa mbegu hasa za mahindi na maharage ambayo ni mazao ya chakula na namna ambavyo serikali itajikita katika uzalishaji wa mbegu.

Alisema kuwa Mikakati ya Serikali ya kuongeza uzalishaji wa mbegu ni pamoja na kuwezesha Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kuongeza uzalishaji wa mbegu bora katika mashamba ya Mwele, Dabaga, Mbozi, Msimba, Bugaga na Arusha; kutumia Taasisi za Utafiti wa Kilimo kuzalisha mbegu mama, msingi na zilizothibitishwa ubora na kukodisha maeneo katika mashamba ya ASA kwa kampuni binafsi za mbegu ili kuongeza uzalishaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali ikiwemo mahindi na maharage.

Aidha, mikakati mingine ni kuongeza eneo la umwagiliaji katika mashamba ya mbegu ya Msimba, Arusha, Dabaga na mashamba ya Vituo vya Utafiti kutoka hekta 200 hadi 600; kushirikisha taasisi za umma kama Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuzalisha mbegu bora pamoja na vikundi vya wakulima wadogo kuzalisha mbegu za Daraja la Kuazimiwa ubora.

Mhe Bashe alisema kuwa shamba la mbegu la Bugaga lililopo katika Wilaya ya Kasulu lina ukubwa wa hekta 200. Shamba hilo linamilikiwa na ASA na kwa sasa linatumika kuzalishia mbegu bora za mahindi, maharage na alizeti. Aidha, shamba hilo linatumika kuzalisha miche bora ya michikichi, miche ya matunda ya machungwa na maembe.

Pia serikali imeanza kuchimba kisima cha maji katika shamba hilo ili kuwezesha uzalishaji wa mbegu kwa kipiti chote cha mwaka. Vilevile, ASA imejenga kitalu nyumba cha kukuzia miche ya chikichi pamoja na kuandaa bustani ya kukuzia miche hiyo ya michikichi na miche ya matunda.

Aliongeza kuwa Mkakati wa Serikali ni kuongeza uzalishaji wa mbegu ambapo Serikali katika mwaka wa fedha 2019/20 imetenga takribani shilingi bilioni 13 kwa ajili ya utafiti wa mbegu kupitia Taasisi ya Utafiti wa Mbegu-TARI na uzalishaji wa mbegu kupitia Wakala wa Mbegu za Kilimo –ASA kwa ajili ya kuzalisha mbegu kwa njia ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji mara tatu hadi nne zaidi ya sasa. "Aidha, nitumie fursa hii kuzisihi halmashauri kutotumia maeneo yaliyotengwa kwa tafiti za kilimo kwa shughuli zingine ikiwemo kujenga stendi za mabasi" Alikaririwa Mhe Bashe

Kadhalika, Wizara ya Kilimo itaamua kuyaachia maeneo hayo kwa shughuli zingingine baada ya kujiridhisha kwamba maeneo hayo hayana tija kwa shughuli hizo za kilimo.

Naye Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali la mbunge wa viti maalum Zaynab kuhusu serikali kutafuta soko la zao la nazi alisema kuwa Soko la kudumu la zao la nazi lipo nchini kwa sababu kiasi cha nazi kinachozalishwa bado hakikidhi mahitaji ya soko la ndani ya nchi kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya zao hilo ikiwemo ulaji wa madafu na watumiaji wa nazi.

Aidha, mafuta mwali yanayotokana na nazi yanaendelea kupata umaarufu kutokana na uhitaji wake kuwa mkubwa ndani na nje ya nchi, ambayo lita moja inafika hadi Shilingi 40,000/=. Bidhaa kama fagio, mbao, kamba na samani zinazotokana na mti wa mnazi na uwezo wa zao hilo kutunza mazingira huongeza thamani ya zao la minazi.

Alisema kuwa Katika kuimarisha soko la zao la nazi nchini msimu wa mwaka 2018/2019 wakulima wapatao 74 katika mikoa ya Lindi na Mtwara wamefundishwa namna ya kukamua mafuta mwali.

Vilevile, kikundi cha wanachama 50 katika Wilaya ya Bagamoyo kimepewa mashine yenye uwezo wa kukamua lita 500 za mafuta mwali kwa mwaka. Aidha, Serikali inaendelea kuimarisha masoko ya mazao yote ya kilimo likiwemo zao la nazi kwa  kuwaunganisha wakulima na wanunuzi kupitia vyama vya ushirika, masoko ya moja kwa moja na viwanda vidogo  vya kuongeza thamani ya zao la nazi.

Mhe Mgumba amesema, Serikali inaendelea kutoa elimu kwa wazalishaji wa zao la nazi kuendelea kupanda mbegu bora zenye ukinzani dhidi ya magonjwa na zenye tija  kubwa. Tanzania ni nchi ya kumi duniani kwa uzalishaji wa nazi ikiongozwa na nchi ya Indonesia na kwa Afrika ni nchi ya kwanza ambapo huzalisha wastani wa tani 530,000 za nazi kwa mwaka ikifuatiwa na Ghana ambayo huzalisha wastani wa tani 366,183.

Aidha, Serikali inaendelea kuhamasisha kilimo cha minazi nchini ambapo imeanzisha shamba lenye ukubwa wa hekta 54 katika kituo kidogo cha utafiti cha Chambezi Wilaya ya Bagamoyo ili kuzalisha miche bora  ya minazi yenye ukinzani dhidi ya ugonjwa wa kunyong’onyea kwa minazi (Coconut Lethal Disease) na kuisambaza kwa wakulima kwa gharama nafuu.

Aliongeza kuwa Serikali inahamasisha kilimo cha minazi katika maeneo mapya ili kuongeza uzalishaji wa nazi nchini ambapo msimu wa 2018/2019 ilizalisha na kusambaza jumla ya mbegu 11,000 kwa wakulima katika mikoa ya Rukwa na Mwanza. Aidha, Serikali inafanya mazungumzo na Jumuiya ya Asia - Pasific Coconut Community (APCC) ambayo hutunza “germplasm” ya minazi kuwezesha upatikanaji wa mbegu bora za minazi zenye kuongeza tija kwa wakulima.

MWISHO

Waziri Mkuu: Tozeni Bili Za Maji Zisizowaumiza Wananchi

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maji ifuatilie utendaji wa Mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini na ihakikishe kwamba bili wanazotozwa wananchi zinakuwa na uhalisia na si kuwaumiza.

Ametoa agizo hilo baada ya kuibuka wimbi la malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu upandaji wa bili za maji ambao hauna uhalisia kwa sababu Serikali ndiyo inayotoa fedha za miradi hiyo nchini.”Serikali haitakubali wala haitoruhusu mwananchi anatozwa gharama kubwa za maji.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 12, 2019) Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbungewa Viti Maalumu, Mariam Kisangi, aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu suala hilo.

“Yako maeneo ambayo mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji kumejitokeza wimbi la mabadiliko ya kuhusu kupanda kwa bei za bili, mfano wilayani Maswa mkoani Simuyu bei imeongezeka kutoka sh. 5,000 hadi 28,000 kwa mwezi.”

“Bei hizo hazina uhalisia na hakuna sababu ya mamlaka kuzoza bei kubwa kiasi hicho na kuwafanya wananchi washindwe kumudu kulipia bili zao, wakati Serikali ndio imetoa fedha za kugharamamia uanzwishwaji wa miradi hiyo na haijadai kurudishiwa fedha hizo.”

Waziri Mkuu amesema Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) ifuatilie bei za bili wanazotozwa wananchi ili kujiridhishwa kwamba zinazingatia uwezo wa wananchi wengi kuzilipa hasa wale wa vijijini.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Kilimo na Maafisa Biashara kote nchini wasimamie katika masoko yote na wajirishe iwapo vipimo vinavyotumika ni sahihi kwani lumbesa haikubaliki.

Ametoa agizo hilo wakati akijibu swali la Mbungewa Jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi aliyetaka kupata kauli ya Serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa katika kudhibiti unyonyaji wanaofanyiwa wakulima kupitia ufungaji wa mazao unaozidi viwango.

Waziri Mkuu amesema wanunuzi wa mazao mbalimbali lazima wafuate sharia, kanuni na taratibu za manunuzi ya mazao husika. “Maafisa Kilimo wasimamie biashara hiyo na waendeshe operesheni kwenye maeneo ya masoko ili kujirishana vipimo vinavyotumika.”

Amesema ni muhimu zaidi kutumia mizani ambayo haina utata ili kuwawezesha wakulima kuweza kunufaika kutokana na kilimo na kwamba suala la waununuzi kutumia vipimo visivyosahihi kama lumbesa halikubaliki.

Akijibuswali la Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa aliyetaka kupata kauli ya Serikali kuhusu kuhusu suala la ununuzi wa zao la pamba, Waziri Mkuu amesema Serikali imelifanyia kazi suala hilo na tayari zaidi ya tani 200,000 zimeshanunuliwa ambayo ni sawa na asilimia 80.

Waziri Mkuu amewahakikishia wakulima wa zao la pamba kwamba pamba yote iliyosailia majumbani itanunuliwa.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao.

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari.

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume.

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18.

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

Pia tunadawa za Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto.
 
DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 AU  0762293390 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Spika Ndugai Awapongeza Nape Nnauye, January Makamba na William Ngeleja Kwa Kumuomba Msamaha Rais Magufuli

$
0
0
Spika wa Bunge Job Ndugai, amewapongeza wabunge watatu wa CCM, Mh. Nape Nnauye, January Makamba na William Ngeleja kwa kitendo cha kiungwana cha kumwomba msamaha Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
 
Mh. Job Ndugai amesema Bungeni, leo September 12, 2019, kuwa ni vyema viongozi wote wakafuata nyayo hizo kwa wale wote ambao wamekuwa wakiwakosea hata kama ni wadogo kwako kicheo, kwakuwa uungwana ni vitendo.

Amesema anashangaa kuona magazeti mengi yamekuwa yakishabikia, na kuwachora wabunge picha za ajabu ajabu pamoja na kuandika habari za kishabiki baadhi ya vingozi nchini.

Pia amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwasemehe wabunge hao kwakuwa ni jambo la kiungwana sana kufanya kama binadamu.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo,Pamoja Na Magonjwa Sugu

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  call 0759 208 637

watsap  0620510598

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao.

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari.

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume.

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18.

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

Pia tunadawa za Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto.
 
DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 AU  0762293390 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Chama Cha Mapinduzi CCM Chazindua Rasmi Gazeti La Uhuru Ya Kijani.....Bashiru Awataka Wenyeviti Wa Mashina Kutopanga Foleni Kwenye Ofisi Za Serikali.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
CHAMA cha Mapinduzi(CCM), kimewataka wenyeviti wa mashina na mabalozi kutopanga foleni wanapofika kwenye ofisi za  serikali.


Kauli hiyo aliitolewa leo  jijini hapa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Taifa, Dk. Bashiru Ally,  wakati wa  uzindua wa gazeti la ‘Uhuru ya kijani’ ambalo linalenga kujenga na kuimarisha chama hicho.

Alisema kuwa mabalozi hawana kizuizi hata kwenye kugombea wao hawaitwi na hawazuiliwi wanaweza kugombea hata urais.

“Mwenyekiti wa shina au balozi akipiga simu au kupiga hodi sehemu yeyote zilipo ofisi za viongozi wa serikali naomba asipange foleni,”alisema.

Aidha, Dk. Bashiru alieleza kuwa, wamepanga kuwapatia vitambulisho  viongozi hao kwa sababu ndio njia pekee ya kutambua mchango wao kwa kuwa, viongozi hao katika ngazi ya chini ya chama wamekuwa wakijitolea Zaidi kuliko wanachama wengine.

“Chama chetu kitaendelezwa kwa njia ya kujitolea na nitumie fursa hii wabunge wetu na wabunge wa baraza la wawakilishi mfanye  kazi kwa kujitolea ili kuimarisha chama chetu,”alisema.

Dk.Bashiru alisema kazi wanayoifanya ni kuwalinda wabunge dhidi ya  wanaowasumbua na watu wasiofuata taratibu hivyo nao wasaidie kuimarisha chama.

Akizungumzia mkakati wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) wa ‘Tanzania ya kijani’, Dk.Bashiru alisema mkakati huo umepokelewa vizuri na kuwataka usitumike kama makongamano ya kuonekana kwenye TV na mitandao ya kijamii ikiwemo ‘You tube’

“Sasa nataka vijana wabadilike kutoka kwenye hamasa waende kwenye kazi ya siasa ya kuimarisha chama ili shughuli ipimike, vinginevyo huu mkakati nitausimamisha nimeshaongea na katibu ni mkakati mzuri tusiposimamia unaweza kuzaa jambo ambalo hatujalitarajia,”alisema.

Alieleza kuwa vijana wawe na mvuto wa kukilinda chama na inapotokea mtu anakichokoza chama ahame chama aonekane ni jasiri na sio legelege.

Kuhusu gazeti hilo, Dk.Bashiru alisema litatumika kujenga na kuimarisha chama nayeye atakuwa na ukurasa wake ambao atakuwa anazungumzia kuhusu urithi.

Alisema katika ukurasa huo kutakuwa na mambo matano ikiwemo haki, tunu za taifa.

“Kuna mjadala kuhusu tunu za Taifa kulikuwa na mjadala hata kwenye Bunge la Katiba ambapo moja ya tunu ni lugha ya Kiswahili, na gazeti hili litatumika kukuza Kiswahili,”alisema.

Alisema kati ya mambo ambayo yamefanyika chini ya uongozi wa Spika Job Ndugai ambayo ni kubwa kuliko yote ni uamuzi wa kimapinduzi wa kulinda rasilimali kwa kutunga sheria ambayo inaonesha nchi imegoma kugeuzwa shamba la bibi.

Aidha alisema katika mikakati ya kisiasa ya kuimarisha uhai wa chama ipo minne ambapo ni pamoja na kukomaza demokrasia mashinani kupitia kwa wenyeviti wa mashina na mabalozi ili kukifanya kuwa karibu na wananchi na wanachama.

Awali, Spika wa Bunge Job Ndugai, alipongeza kuanzishwa kwa gazeti hilo na kudai kuwa kukosekana kwa habari kwenye matawi kumekuwa ni unyonge mkubwa.

“Gazeti lina habari za kuelimisha jambo hili ni jema nakuahidi sisi wabunge tutatoa kila aina ya ushirikiano, tutachukua nakala kwa idadi ya matawi, kata, na wilaya na limekuja wakati muafaka maana tunaelekea kwenye uchaguzi,”alisema.

Alisema chama kina nguvu kubwa ya kuvitumia vyombo vyake vya habari ili kukabiliana  na vitendo vya upotoshaji.

Mwisho.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images