Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo,Pamoja Na Magonjwa Sugu

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  call 0759 208 637

watsap  0620510598

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Bunge Lafanya Azimio La Kumpongeza Rais Magufuli Kwa Kuchaguliwa Kuwa Mwenyekiti SADC

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo Sept.3,2019 limefanya azimio la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli baada ya hivi Karibuni kupewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Bunge la Jumuiya Ya Madola  Afrika SADC.
 
Mwenyekiti  kamati ya Bunge ya Mambo ya nje  na Usalama  Mhe. Musa Azan Zungu amesema Waasisi wa Jumuiya ya maendeleo nchi wanachama wa Kusini Mwa Afrika wamefanya makubwa ikiwa ni pamoja na  kuunganisha nchi wanachama hivyo matamanio ya waasisi hao ikiwa ni pamoja na Rais wa awamu ya Kwanza Mwl.Julius Kambarage Nyerere na Aman Abeid Karume yanatimizwa na Rais Magufuli katika kusukuma mbele maendeleo .
 
Nao baadhi ya Wabunge wamesema kuchaguliwa kwa Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti  wa SADC itasaidia kuondoa kuritimba wa masoko katika  biashara  huku  pia wakisema kuwa Tanzania ni Kitovu cha Cha Ukombozi kwa nchi wanachama wa SADC katika kupigania Uhuru.
 
Akihitimisha katika Azimio hilo la Pongezi  bungeni jijini Dodoma Mhe.Zungu amesema ili Nchi wanachama wa SADC kujikomboa lazima kwanza kutafuta masoko ya ndani

Mamlaka Ya Hali Ya Hewa Tanzania Yatoa Mwelekeo Wa Msimu Wa Mvua Za Vuli Kwa Kipindi Cha Mwezi Oktoba Hadi Desemba 2019.

$
0
0
Dondoo muhimu za msimu wa mvua za Vuli kipindi cha Oktoba – Disemba, 2019 

Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kipindi cha Oktoba - Disemba 2019, ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na wanyamapori, maliasili na utalii, nishati na maji, mamlaka za miji, afya pamoja na menejimenti za maafa. 

Utabiri huu ni mahsusi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Nyanda za juu kaskazini mashariki, Pwani ya kaskazini, Ukanda wa Ziwa Viktoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma). Kwa muhtasari, mwelekeo huo na athari zake unaonesha kuwa:  
 
a) Mvua za msimu wa Vuli, 2019
i. Maeneo yanayozunguka ukanda wa Ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani.
ii. Maeneo mengine yaliyosalia (Pwani ya Kaskazini pamoja na Nyanda za juu kaskazini Mashariki), mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani.  
iii. Maeneo ya ukanda wa Ziwa Viktoria mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya pili ya mwezi Oktoba, 2019 isipokuwa maeneo machache ya mkoa wa Kagera ambapo vipindi vya mvua za nje ya msimu zilizoanza toka mwezi Agosti 2019, vinatarajiwa kuendelea na hivyo kuungana na kuanza kwa msimu wa mvua za Vuli. 

b) Athari zinazotarajiwa
i. Katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua nyingi matukio ya magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza, hali kadhalika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani magonjwa ya mlipuko pia yanaweza kujitokeza kutokana na uhaba wa maji safi na salama.  
ii. Upungufu wa malisho hususani katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani unaweza kujitokeza. Hali hiyo inaweza kusababisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
iii. Vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa kujitokeza hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani na chini ya wastani.

(I) MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA KIPINDI CHA OKTOBA – DISEMBA, 2019 
Kutokana na mifumo ya hali ya hewa ilivyo kwa sasa na jinsi inavyotarajiwa kuwa kwa kipindi cha Oktoba – Disemba, 2019 (kipengele II cha taarifa hii), mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya Nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na Pwani ya kaskazini. Aidha, maeneo ya ukanda wa Ziwa Viktoria pamoja na maeneo ya kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma (Kibondo) yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani. 
 
1. Mvua za msimu wa Vuli
Msimu wa mvua za Oktoba – Disemba (Vuli) ni mahususi katika maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini-mashariki, pwani ya Kaskazini pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.  

Katika msimu wa Vuli, 2019 maeneo mengi ya nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na pwani ya kaskazini yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani. Aidha, mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Viktoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. 

1.1 Kanda ya Ziwa Viktoria: (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga): 

Maeneo machache ya mkoa wa Kagera mvua za nje ya msimu zinaendelea toka mwezi Agosti na zinatarajiwa kusambaa katika maeneo mengine ya ziwa Viktoria hadi kufikia wiki ya pili ya mwezi Oktoba, Hivyo kuungana na msimu wa mvua za Vuli. 
 
Mvua hizo zinatarajiwa kuendelea kusambaa katika mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Simiyu na Shinyanga katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Oktoba. Kiwango cha mvua kinachotarajiwa katika msimu huu ni mvua za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya ukanda huo. Msimu wa mvua za Vuli katika maeneo haya unatarajiwa kuisha kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Januari, 2020. 
 
1.2 Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro):

Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza katika wiki ya pili ya mwezi Oktoba ingawa mtawanyiko wake unatarajiwa kuwa hafifu. Vipindi virefu vya ukavu na mvua chache pia vinatarajiwa katika maeneo mengi ya ukanda wa pwani ya kaskazini. Hata hivyo, mvua zinatarajiwa kunyesha katika kiwango cha wastani kuanzia wiki ya pili ya mwezi Novemba. Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuisha katika wiki ya nne ya mwezi Disemba.  
 
1.3 Nyanda za juu Kaskazini Mashariki: (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara): 

Mvua katika maeneo ya Nyanda za juu Kaskazini Mashariki zinatarajiwa kuanza katika wiki ya nne ya mwezi Oktoba na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Mvua hizi zinatarajiwa kuisha katika wiki ya nne ya mwezi Disemba 2019.
(II) MIFUMO YA HALI YA HEWA
Hali ya joto la bahari la juu ya wastani katika maeneo ya kati mwa bahari ya Hindi, kusini-magharibi pamoja na kaskazini magharibi (pwani ya Somalia) mwa Bahari ya Hindi inatarajiwa kuendelea katika kipindi chote cha Oktoba-Disemba 2019. 

Hali hiyo inatarajiwa kusababisha mtawanyiko wa upepo kutoka katika pwani ya Tanzania kuelekea katikati ya Bahari ya Hindi. Hivyo, kusababisha vipindi vya upungufu wa mvua katika maeneo ya pwani ya kaskazini pamoja na nyanda za juu kaskazini mashariki. 

Aidha, joto la juu ya wastani katika Bahari ya Hindi linatarajiwa kuongeza uwezekano wa matukio ya vimbunga katika maeneo ya kusini-magharibi mwa Bahari ya Hindi. 

Kwa upande mwingine, joto la chini ya wastani linatarajiwa kuendelea kusini-mashariki mwa Bahari ya Atlantiki (karibu na pwani ya Angola) na hivyo inatarajiwa kuwepo kwa msukumo wa   upepo wenye unyevunyevu kutoka katika misitu ya Kongo, na kusababisha mvua katika maeneo ya magharibi mwa nchi.

 Uwepo wa hali ya joto la wastani katika eneo la kati la kitropiki la Bahari ya Pasifiki unatarajiwa kuwa na mchango hafifu katika mwenendo wa mifumo ya mvua nchini kwa kipindi cha Oktoba-Disemba, 2019. 

(III) ATHARI NA USHAURI 
Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na Wanyamapori
Katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani, upungufu wa unyevunyevu ardhini unatarajiwa kujitokeza. Upungufu wa malisho na maji kwa ajili ya mifugo pia unatarajiwa hivyo kusababisha uwezekano wa migogoro kati ya wakulima na wafugaji.  
 
Wafugaji wanahamasishwa na kushauriwa kuvuna mifugo yao ikiwa bado katika hali nzuri. Wafugaji pia wanashauriwa kutunza mifugo yao kwa kuzingatia ushauri kutoka kwa maafisa ugani katika maeneo yao. 
 
Sekta ya uvuvi, katika maeneo hayo, inaweza kuathiriwa kutokana na upungufu wa maji katika mabwawa ya samaki na hivyo wafugaji wanashauriwa kuimarisha miundombinu ya ufugaji wa samaki na kuzingatia matumizi sahihi ya maji. 
 
Katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani, shughuli za kawaida za kilimo zinatarajiwa. Aidha, malisho na maji ya kutosha kwa ajili ya mifugo na wanyamapori vinatarajiwa.

Nishati, Maji na Madini 
Upatikanaji wa maji unatarajiwa kuimarika, hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani. Kina cha maji katika mabwawa na mito kinatarajiwa kuongezeka. 

Hata hivyo, athari katika miundombinu ya rasilimali maji inaweza kujitokeza. Shughuli za uchimbaji madini katika migodi midogomidogo zifanyike kwa kuzingatia tahadhari zinazotolewa kwani ongezeko la maji katika udongo linaweza kusababisha maporomoko ya ardhi. Aidha, maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki na pwani ya kaskazini, ambapo mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa, kina cha maji katika mabwawa kinatarajiwa kupungua, hivyo matumizi sahihi ya maji kwa ajili ya umwagiliaji, majumbani pamoja na kuendesha mitambo ya umeme yanashauriwa. 
 
Aidha, matumizi ya nishati mbadala za umeme yanashauriwa ili kuzuia upungufu unaoweza kujitokeza.

Mamlaka za Miji
Huduma za maji safi na maji taka zinaweza kuathirika, hususan katika vipindi vya mvua kubwa, hivyo, Mamlaka za miji pamoja na wananchi wanashauriwa kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa mifumo na njia za kupitisha maji zinafanyakazi katika kiwango cha kutosha ili kuepusha maji kutuama na kupelekea mafuriko na athari nyingine. 
 
Sekta ya Afya 
Katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua nyingi matukio ya magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza. Katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza mara kwa mara, kutokana na upungufu wa maji safi na salama. 

Aidha, matumizi ya maji yasiyo salama katika jamii yanaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko yanayohusiana  na maji. Hivyo, ushauri unatolewa kwa mamlaka husika na jamii kuchukua hatua stahiki kupunguza athari za kiafya zinazoweza kujitokeza.

Menejimenti za Maafa
Menejimenti za maafa zinashauriwa kuandaa mikakati ya kupunguza athari zinazoweza kujitokeza katika msimu wa mvua za Vuli 2019. Kuandaa mbinu za kukabiliana na mafuriko na vipindi vya ukavu, kama vile kuimarisha na kutenga rasilimali tayari kwa ajili ya kukabiliana na athari zinazoweza kijitokeza. Aidha, inashauriwa kuimarisha programu na njia za mawasiliano katika ngazi mbalimbali. 

Vyombo vya habari
Ushauri unatolewa kwa vyombo vya habari kufuatilia mara kwa mara na kusambaza taarifa sahihi za mwenendo wa hali ya hewa na mirejeo inayotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Wanahabari wanashauriwa kutafuta na kutumia maelezo ya wataalam wa sekta husika katika kuandaa na kufikisha taarifa za masuala mtambuka ya hali ya hewa kwa jamii.  
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inawashauri watumiaji wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na wakulima, wafugaji, Mamlaka za Wanyamapori, Mamlaka za Maji na Afya waendelee kutafuta, kupata na kufuata ushauri wa wataalamu katika sekta husika. 
 
Mwelekeo wa mvua uliotolewa hapa umezingatia zaidi kipindi cha msimu (miezi mitatu) na hali ya mvua katika maeneo makubwa. Hivyo, viashiria vinavyochangia mwenendo wa mifumo ya mvua na mabadiliko ya muda mfupi katika maeneo madogo utazingatiwa katika uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na mfupi. 

Watumiaji wa taarifa za utabiri huu wanashauriwa pia kufuatilia utabiri wa saa 24, siku 10 pamoja na mwezi kama unavyotolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania.

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa mirejesho ya mwelekeo wa mvua nchini kadri inavyohitajika.    

Kanuni bora za ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili)....Soma Hapa Uwe Tajiri

$
0
0
Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. 

Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi.

 Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. 

Muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.

Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku
Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
1.  Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.

2. Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe na kufukiwa.

3.  Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.

4.  Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.

5.  Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.

6.  Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.

7.Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.

Magonjwa na kinga kwa kuku wote

1.Ndui ya kuku
Huathiri sana vifaranga wanaokua na ujitokeza kwa wingi wakati wa mvua za muda mrefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na manyoya.

2.Mdondo/kideri
Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari katika magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.

3.Ukosefu wa vitamini A
Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.

4.Kosidiosisi
Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokua. Kuku hudhoofika, manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.

5.Viroboto, chawa na utitiri
Hawa ni wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga na kuatamia.

6.Minyoo
Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo.

Chakula cha ziada
1.Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.

2.Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai).

3.Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kama nyongeza ya protini.

4.Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.

5. Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.

6Mwagia maji hadi kila kilichomo kilowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chungu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuhi, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.

Utotoleshaji wa vifaranga
Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku.

Sifa za jogoo bora
1.  Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.

2.  Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi mueke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.

Sifa za tetea bora
Tetea bora ni yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.

Uhifadhi wa mayai
1.  Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.

2.  Tumia kasha lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.

3.  Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.

4.  Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.

5.  Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.

Kuatamiza mayai
1.  Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.

2.  Mayi 10 hadi 12 yanatosha kuatamia.

3.  Mayai ya kuatamiza yasizidi wiki 2 toka kutagwa.

4.  Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku wa kuyaatamia.

5.  Mayai ya kuatamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu na safi au kilichowekwa spiriti

Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja
1.  Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;

2.  Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.

3.  Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kisha wawekee kuku wote mayai yenye mbegu.

Matunzo ya vifaranga ili kuzuia vifo
Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifaranga wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;

Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine
1.  Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasiende mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.

Chanjo ya mdondo kideri/lufuo
Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.

Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia hadi wakifikisha wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi 3

Kinga dhidi ya kosidiosisi
Kinga ya kosidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.

1.  Wape dawa ya amprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya kosidiosisi.

2.  Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa katika maji au pumba

3.  Kama vifaranga wadogo wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvaa koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;

Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu

Hitimisho
1.  Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku ni visafi kuepusha magonjwa.

2.  Usichanganye kuku na bata katika banda moja

3.  Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.

4.  Kideri, kosidiosisi, ndui na upungufu wa vitamini A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.

5.  Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.

6.  Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri, fuata maelezo kuzuia vifo.

7.  Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.

8.  Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Gazi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume ,Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30 na kukusaidia kurudia   tendo la ndoa .

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara hata kama yupo mbali.

Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Wasiliana na mtaalam kwa; 0747100745

Tupo Mbagala

Mrithi wa Tundu Lissu kuapishwa kesho bungeni

$
0
0
Miraji Mtaturu (CCM), Mbunge mpya wa Singida Mashariki aliyekalia kiti hicho baada ya Tundu Lissu (Chadema) kutangazwa kuwa amekosa sifa za kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo, anatarajia kuapishwa kesho, Septemba 3, 2019 bungeni jijini Dodoma.

Ratiba ya Mkutano wa 16 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoanza kesho, iliyotolewa na Ofisi ya Bunge inaonesha kuwa pamoja na mambo mengine, Mtaturu atakula kiapo cha uaminifu mbele ya Spika.

Mtaturu alitangazwa kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo baada ya watu waliokuwa wamechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo kutoziwasilisha ndani ya muda uliokuwa umepangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Juni 28, 2019 Spika wa Bunge, Job Ndugai alitangaza kuwa jimbo la Singida Mashariki liko wazi na kwamba ameshamuandikia barua Mwenyekiti wa NEC na kumuelekeza kuitisha uchaguzi.

Spika Ndugai alisema amefikia uamuzi huo kwakuwa Lissu amevunja kanuni na sheria za Bunge kwa kutojaza fomu ya mali na madeni ya viongozi wa umma pamoja na kutohudhuria mikutano zaidi ya mitatu ya Bunge bila kutoa taarifa kwake (Spika).

Lissu ambaye alikuwa nchini Ubelgiji akipatiwa matibabu kufuatia tukio la kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana, Septemba 7, 2017 jijini Dodoma, amefungua kesi ya kupinga uamuzi wa Spika Ndugai. Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu.

Ni Nini Kinachosababisha Wanaume Wengi Kuishiwa Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanaume kuishiwa nguvu kiume na maumbile madogo.

Nini kinasababisha upungufu wa nguvu za kiume  (1) Msongo wa mawazo( 2) magonjwa ya sukari,presha,vidonda vya tumbo,kukosa choo,na tumbo kuunguruma( 3) kujichua kwa muda mrefu   (4) ngiri ,korodani kuvimba,

Tiba ya tatizo:
MAJINJAS;  ni dawa  yenye virutubisho na mchanganyiko wa wa mizizi tisa (9) dawa hii hutibu matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo -dawa hii itakupa uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu ( 2) kuwahi kufika kileleni dawa hii itakupa uwezo wa kuchelewa ( 3)  dawa hii hutibu tatizo la maumbile ya kiume kusinyaa hasa kwa wanaume  waliojichua kwa muda mrefu  

MTINJETINJE; ni dawa ya kisukari ambayo imechanganywa na mizizi na mbegu -dawa hii husaidia kurejesha kongosho kwenye hali yake ya kawaida.

Fika ofisini kwangu MBAGARA ZAKHEMU KARIBU NA BENK YA  KCB utaona bango limeandikwa NTUNZU HEBRISRI CLINIC na mwanza yupo wakala nipigie simu whasap  0783185060. 0620113431 DR AGU na utaletewa popote uduma  hii

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo,Pamoja Na Magonjwa Sugu

$
0
0
SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  call 0759 208 637

watsap  0620510598

Kanuni bora za ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili)....Soma Hapa Uwe Tajiri

$
0
0
Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. 

Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi.

 Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. 

Muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.

Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku
Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
1.  Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.

2. Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe na kufukiwa.

3.  Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.

4.  Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.

5.  Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.

6.  Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.

7.Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.

Magonjwa na kinga kwa kuku wote

1.Ndui ya kuku
Huathiri sana vifaranga wanaokua na ujitokeza kwa wingi wakati wa mvua za muda mrefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na manyoya.

2.Mdondo/kideri
Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari katika magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.

3.Ukosefu wa vitamini A
Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.

4.Kosidiosisi
Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokua. Kuku hudhoofika, manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.

5.Viroboto, chawa na utitiri
Hawa ni wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga na kuatamia.

6.Minyoo
Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo.

Chakula cha ziada
1.Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.

2.Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai).

3.Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kama nyongeza ya protini.

4.Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.

5. Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.

6Mwagia maji hadi kila kilichomo kilowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chungu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuhi, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.

Utotoleshaji wa vifaranga
Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku.

Sifa za jogoo bora
1.  Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.

2.  Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi mueke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.

Sifa za tetea bora
Tetea bora ni yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.

Uhifadhi wa mayai
1.  Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.

2.  Tumia kasha lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.

3.  Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.

4.  Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.

5.  Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.

Kuatamiza mayai
1.  Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.

2.  Mayi 10 hadi 12 yanatosha kuatamia.

3.  Mayai ya kuatamiza yasizidi wiki 2 toka kutagwa.

4.  Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku wa kuyaatamia.

5.  Mayai ya kuatamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu na safi au kilichowekwa spiriti

Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja
1.  Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;

2.  Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.

3.  Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kisha wawekee kuku wote mayai yenye mbegu.

Matunzo ya vifaranga ili kuzuia vifo
Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifaranga wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;

Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine
1.  Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasiende mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.

Chanjo ya mdondo kideri/lufuo
Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.

Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia hadi wakifikisha wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi 3

Kinga dhidi ya kosidiosisi
Kinga ya kosidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.

1.  Wape dawa ya amprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya kosidiosisi.

2.  Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa katika maji au pumba

3.  Kama vifaranga wadogo wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvaa koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;

Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu

Hitimisho
1.  Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku ni visafi kuepusha magonjwa.

2.  Usichanganye kuku na bata katika banda moja

3.  Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.

4.  Kideri, kosidiosisi, ndui na upungufu wa vitamini A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.

5.  Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.

6.  Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri, fuata maelezo kuzuia vifo.

7.  Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.

8.  Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano September 4

LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka Bundeni Dodoma

$
0
0
LIVE: Fuatilia kipindi cha maswali na majibu kutoka Bundeni Dodoma

LIVE: Rais Magufuli Anahutubia Mkutano Wa Wadau Wa Sekta Ya Ujenzi

$
0
0
LIVE: Rais Magufuli Anahutubia Mkutano Wa Wadau Wa Sekta Ya Ujenzi

Fursa Lukuki Kwa Watanzania Katika Kongamano La Biashara Kati Ya Tanzania, Uganda

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao Chato mkoani Geita mapema Julai 2019. PICHA NA IKULU.

Na Mwandishi Wetu.
MTANZANIA mwenzangu, najua unajua kuwa siku za karibuni nchi za Tanzania na Uganda zinatarajia kufanya Kongamano la kibiashara la pamoja ambalo litakuwa ni mara ya kwanza kufanyika nchini kwetu.

Kwa kukumbusha tu, kongamano hilo linatarajia kufanyika kuanzia Septemba 6 hadi Septemba 7 mwaka huu katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo baina ya Tanzania na Uganda linatarajia kuwashirikisha wafanyabiashara wa nchi hizo.

Kongamano hilo kwa namna moja au nyingine itakuwa fursa nzuri kwa wafanyabiashara wa nchi hizo kubadilisha uzoefu wa kibiashara na namna nzuri ya kuendelea kushirikiana kwa maslahi ya pande zote mbili.

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya utawala wa Rais mzalendo na mwenye upendo kwa nchi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mambo mengine ameweka msingi imara katika kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinapata soko kwenye nchi nyingine zikiwemo za Afrika Mashariki.

Kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda ambayo imekuwa ikihimizwa na Rais wetu imekuwa chachu kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa viwanda sambamba na utengenezaji wa bidhaa zenye ubora ambazo zinaweza kushindana kwenye soko la Dunia, Afrika na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kabla ya kuendelea kuzungumzia umuhimu wa kongamano hilo la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda naomba kutumia walau dakika moja ama mbili kutoa pongezi zangu za dhati kwa Rais Dk. Magufuli kwa namna ambavyo ameamua kufungua milango ya kuzikaribisha nchi mbalimbali kuja nchi kuwekeza.

Kwa upendo mkubwa kwa nchi yake, amehakikisha anaweka mkazo katika ujenzi wa miundombinu ya uwekezaji na kibiashara na matokeo yake muamko kwa watanzania katika kuwekeza na kufanyabishara umekuwa mkubwa na wenye tija. Hongera Rais wetu kwa kazi nzuri ambayo unaifanya kwa maendeleo ya nchi yetu.

Hata hivyo kupitia kongamano la biashara ambalo linahusisha nchi hizo mbili, ni wazi Tanzania itatumia nafasi hiyo kama fursa ya kutangaza bidhaa zake na wakati huo huo Uganda nayo itaonesha bidhaa zake.

Ni kongamano ambalo kwangu naliona limekuja wakati muafaka hasa kwa kuzingatia chini ya Rais Magufuli nchi yetu imekuwa na mazingira mazuri ya kibiashara. Ni wakati muafaka kwa nchi zote mbili kutumia maonesho hayo kujengeana ujuzi katika utengenezaji wa bidhaa bora na utafutaji masoko.

Pamoja na mambo mengine kupitia kongamano hilo la kibiashara itakuwa sehemu sahihi ya kuweka mbinu na mikakati itakayofanikisha kuongeza thamani kwa bidhaa zinazotokana na mazao.Sina shaka na hilo hata kidogo na ukweli kwa Tanzania imedhamiria kuongeza thamani kwa bidhaa za mazao.

Katika maisha ya kawaida najua unaweza kujiuliza hivi , je Tanzania tunauza nini zaidi kwa nchi ya Uganda? Jibu vyovyote lakini hili ambalo nitakueleza ni muhimu zaidi. Iko hivi mpaka sasa Tanzania inauza bidhaa za mazao na bidhaa za viwandani nchini Uganda.

Takwimu zilizopo zinaonesha kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita Tanzania imeweza kuuza bidhaa za mazao ya chakula na viwandani zenye thamani ya Sh. bilioni 300 kutoka Sh. bilioni 100. Hilo ni ongezeko mara mbili zaidi ya fedha zilizopatikana huko nyuma.

Ninaposema Rais Magufuli ameweka mazingira mazuri ya kibiashara naaminisha na takwimu zinaeleza wazi namna ambavyo nchi yetu ilivyoweka mazingira mazuri katika sekta ya biashara na viwanda.

Nikiri kwa namna ambavyo Tanzania unauza bidhaa zake nchini Uganda na kuingiza kiasi hicho cha fedha, kongamano litakalofanyika nchini litaongeza wigo zaidi wa kibiashara.

Hata hivyo kutokana na umuhimu wa kongamano hilo la kibiashara, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imejipanga vema kuhakikisha kongamano hilo linakuwa na tija na ushiriki wa Watanzania unakuwa mkubwa zaidi.

Nakumbuka wakati anazungumzia kongamano hilo Waziri wa Viwanda na Biashara Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amesema kongamano hilo litasaidia kuweka mazingira wezeshi ya kuongeza wigo wa kujenga viwanda zaidi nchini hasa vya usindikaji wa mazao ili kuongeza thamani ya mazao hayo.

Naomba nitoe rai kwa wafanyabishara na wawekezaji na wote wanaojihusisha na sekta ya biashara waliopo nchini Tanzania kuhakikisha wanashiriki kikamilifu na kwa vitendo katika kongamano hilo. Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imejikita katika msingi wa kufanya kazi kwa bidiii.

Hivyo kwa wafanyabiashara kupitia kongamano hilo wataendelea kunoa vichwa ili kujiimarisha zaidi kibiashara ana kiuwekezaji kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake kwa ujumla. Nihitimishe kwa kukumbusha tena kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda litafanyika Septemba 6 na Septemba 7 mwaka huu. Sote tushiriki bila kukosa.

Serikali Yadhamiria Kufuta Kesi Zote Zinazozikabili Kampuni Za Kilimo Ili Kuondoa Changamoto Ya Masoko Kwa Wakulima

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe.Husein Bashe amesema moja ya vikwazo vilivyokuwa vinasababisha  Sekta ya Kilimo kuendelea kuwa na Matatizo ni pamoja  na Migogoro na kesi za  muda mrefu dhidi ya Makampuni za Kilimo ambapo serikali imedhamiria   kufuta kesi zote zilizokuwa zinazikabili kampuni hizo ili ziweze kununua Mazao ya wakulima. .
 
Mhe.Bashe amesema ameyasema hayo Sept.3,2019 jijini Dodoma katika mkutano  uliokutanisha wizara ya Kilimo,Wizara ya Viwanda na biashara,Wizara ya Fedha pamoja na wadau wa kilimo hapa nchini.
 
Naibu Waziri Bashe amesema  kampuni za kilimo zilikuwa zikidaiwa zaidi ya Tsh.Trilioni 10  na Serikali hali ambayo ilikuwa inasababisha kushindwa kwenda kutoa huduma kwa wakulima hivyo serikali ina mkakati kabambe wa kufuta kesi na faini zote hizo ili ziweze kutoa huduma kwa wakulima.
 
Aidha,Mhe.Bashe amesema wamekubaliana na Mamlaka ya  Mapato Tanzania[TRA] kuwa ndani ya siku 90 Kuanzia leo Sept.4,2019 suala la madai  kwa kwa Kampuni 4  za kilimo  limekuwa limeisha ili kampuni hizo ziendelee kununua mazao kwa wakulima.
 
Pia Naibu Waziri  Bashe amesema kuna zaidi ya kilo Mil.12  za Tumbaku zipo mikononi mwa Wakulima na Kampuni za kilimo  chini ya Bodi ya Tumbaku Tanzania  zitakutana na wakulima kununua kilo hizo kuanzia Sept.12,2019  .

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku ,Tanzania Tobacco Board[TTB] Hassan Mwakasuvi    amesema ni vyema wakulima  kuheshimu mikataba huku akisema kuwa maazimio ya kikao hicho ni Faraja kwa wakulima katika msimu ujao wa kilimo. 
 
Naye  Mwenyekiti wa vyama vikuu vya wakulima wa Tumbaku Tanzania Emanuel Cherehani ameishukuru serikali kwa maamuzi hayo  huku akiomba kuanza kutekelezwa ndani ya Muda husika uliotajwa ili isiathiri zaidi wakulima huku akiwaomba wakulima kuendelea kutunza mazao yao ya tumbaku.
 
Aidha,Cherehani amesema hapo awali uzalishaji wa zao la tumbaku kwa mwaka 2015 ilikuwa milioni 120 lakini umeshuka mpaka milioni 41 jambo ambalo limeathiri kwa wakulima na Serikali kwa Ujumla.

Waziri Hasunga: Tutafanya Mabadiliko Makubwa Kwenye Sekta Ya Kilimo

$
0
0
Na Mathias Canal, Telaviv-Israel
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa serikali YA Tanzania imejipanga kuikabili sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kuona umuhimu wa kuwaandaa watanzania katika kubadilisha kilimo chao kutoka kwenye kilimo cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara.

Waziri Hasunga ameyasema hayo  tarehe 3 Septemba 2019 wakati akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima katika Ofisi za Ubalozi huo zilizopo katika mtaa wa 12, Abba Hillel Silver Jijini Tel Aviv nchini Israel.

Alisema kuwa katika ziara yake hiyo amejifunza namna ambavyo nchi ya Israel imepiga hatua ya ujuzi katika sekta ya kilimo hivyo kuona umuhimu wa serikali ya Tanzania kuwekeza katika skimu za umwagiliaji.

Alisema kuwa asilimia kubwa ya wakulima nchini Tanzania wanatumia majembe ya mkono katika kilimo jambo ambalo haliwezi kuongeza tija na uzalishaji. “Tunatumia majembe ya mkono mbaya zaidi kilimo chetu kinategemea msimu wa mvua, hivyo kilimo cha namna hiyo bado kinatuchelewesha, tuna wajibu wa kujifunza kwa wenzetu walioendelea” Alisema Mhe Hasunga

Alisema kwa kuanza serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa kilimo inaweza kujenga mabwawa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza uwezo wa kilimo cha umwagiliaji kitakachofanya kazi msimu mzima badala ya kilimo cha kutegemea mvua.

Mhe Hasunga alisema kuwa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kadhalika wizara ya Viwanda na Biashara zitafanya kazi kwa pamoja ili kuona namna ya kuzalisha kwa tija mazao ya kilimo na kutoa malighafi nyingi zitakazochangia katika kuinua na kuchagiza matakwa ya serikali ya kuwa na serikali ya viwanda.

Kuhusu masoko ya mazao yanayozalishwa nchini Tanzania Mhe Hasunga alisema kuwa serikali inaendelea na mkakati maalumu wa kuimarisha masoko kwani imeanzisha kitengo maalumu katika wizara ya kilimo kitakachokuwa na wajibu wa kushughulikia masoko ya mazao ya wakulima.

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga ameyaalika makampuni mbalimbali ya Israel yanayojishughulisha na kilimo kutembelea nchini Tanzania kwa ajili ya kujionea fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.

“Tanzania ni nchi yenye rutuba nzuri, eneo kubwa kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo, hivyo nayaalika makampuni yote yanayohusika na kilimo hususani yanayojishughulisha na utafiti, kutembelea Tanzania kwani ni nchi yenye eneo zuri na kubwa kwa ajili ya uwekezaji hususani katika sekta ya kiliumo” Alikaririwa Mhe Hasunga

Mhe Hasunga amesema kuwa Israel ni nchi yenye eneo dogo kwa ajili ya kilimo lakini wanazalisha chakula kinachotosheleza wananchi wake sambamba na kuuza mazao yao nje ya nchi jambo ambalo linaimarisha pato la serikali ya nchi hiyo na kipato cha mtu mmoja mmoja.

Vilevile, waziri Hasunga ameupongeza Ubalozi wa Tanzania nchini Israel unaoongozwa na Mhe Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima na watendaji wengine wote kwa kazi nzuri wanayoifanya ya uwakilishi wa Tanzania, Aidha Mhe Hasunga amemuomba Balozi huyo kutafuta fursa zaidi za makampuni ya kilimo na viwanda kwa ajili ya kuwekeza nchini Tanzania.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima amesema kuwa miongoni mwa mambo muhimu ya kuyafanyia kazi ni pamoja na kutafuta namna ya kuongeza idadi ya vijana wanaoshiriki katika mafunzo ya kilimo ya Agro Studies ili izidi kuongezeka maradufu.

Kadhalika, alisema kuwa ofisi yake inaendelea kufanya kazi kubwa kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini Tanzania kwani idadi kubwa ya watalii inaongeza pato la kigeni la nchi.

Balozi Masima alisema kuwa nchi ya Israel ina mafanikio makubwa kwenye sekta ya teknolojia hivyo ni wajibu wa Tanzania kutumia fursa hiyo muhimu katika elimu ya ujuzi wa teknolojia za kilimo hususani umwagiliaji.

MWISHO

Serikali Yasema Hakuna Ubaguzi Katika Utoaji Wa Mikopo Kwa Wanafunzi Elimu Ya Juu

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni ,Dodoma
BUNGE limeelezwa kuwa hakuna ubaguzi wowote katika utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwani hutolewa kwa wanafunzi watanzania wote wenye uhitaji na walioomba mikopo wa kuzingatia sheria taratibu na vigezo vilivyowekwa.
 
Hayo yamesemwa jana bungeni  na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  William Ole Nasha wakati alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti maalum (CCM) Halima Bulembo ambapo alisema kuwa ni vema waombaji wakazingatia maelekezo yanayotolewa na bodi wakati wa uombaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na kujaza taarifa zao kwa usahihi na kuambatanisha nyaraka zote muhimu.
 
Katika swali lake Mbunge Halima amesema kuwa  Je,ni kwanini mikopo ya wanafunzi wa chuo kikuu imekuwa ikitolewa kwa ubaguzi.
 
Akijibu swali hilo Mhe.Ole Nasha amesema kuwa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hotolewa kwa mujibu wa sheria ya bodi ya mikopo (sura 178) ambayo inabainisha  sifa za msingi.
 
Sifa hizo ni pamoja na awe mtanzania aliye dahiliwa katika masomo ya shahada katika taasisi inayotambuliwa na serikali,na asiwe na vyanzo vingine vinavyogaramia masomo yake,na kwa mwanafunzi anayeendelea na masomo awe amefaulu kuendelea na masomo katika mwaka unaofuata.
 
“Kwa mujibu wa sheria ya bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu,bodi inamamlaka  ya kuweka utaratibu wa kubaini wahitaji,hivyo bodi huandaa mwongozo unaoweka masharti kwa waombaji pamoja na maelekezo juu ya mambo muhimu ya kuzingatiwa kwa waombaji ambao yatima,wenye ulemavu au wenye wazazi wenye ulemavu,na wale ambao masomo yao ya sekondari au stashahada yalifadhiliwa na maelekezo hayo ni pamoja na kuambatanisha uthibitisho wa hali zao”amesisitiza

RC Makonda Akabidhi Muswaada Wa Mapendekezo Ya Sheria Ya Mirathi Wizarani Jijini Dodoma.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda  September 03 ametimiza ndoto za Wajane kwa kukabidhi Muswada wa Mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya Mirathi kwa Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwaajili ya Kufanyiwa maboresho na kufikishwa Bungeni.
 
Akikabidhi Muswada huo jana  Mjini Dodoma RC Makonda amesema ndani ya Muswada huo ameainisha mapendekezo ya kubadilishwa kwa Sheria kandamizi ambazo zimekuwa mwiba na Mateso kwa Wajane kwa muda wa miaka mingi.
 
Aidha RC Makonda amesema Miongoni mwa Sheria kandamizi anazopendekeza zifanyiwe mabadiliko ni Sheria ya Kiserikali ya Mirathi ya Mwaka 1865, Sheria ya Mirathi ya Kimila ya Mwaka 1963 na Sheria ya Mirathi ya Kidini ya Mwaka 1963 kwakuwa zimepitwa na Wakati na zimekuwa na Mapungufu mengi ya Kisheria.
 
RC Makonda amevitaja baadhi ya vipengele anavyopendekeza vifanyiwe maboresho ni pamoja na kipengele cha kumpa uhalali Mke wa marehemu kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, mjane kupewa haki ya kurithi na kusimamia mali za marehemu, Mjane kutoondolewa kwenye nyumba wala Mali kuhamishwa, Usawa wa watoto katika kumiliki mali za marehemu bila kujali jinsia pamoja haki ya mtoto wa nje ya Ndoa kurithi Mali.

Vifungu vingine ambavyo RC Makonda ameeleza kuwa ni kandambizi kwa Mjane ni pamoja na kipengele kinachoruhusu Mjane kurithiwa na kile kinachomnyima Mwanamke haki ya kurithi ardhi ya ukoo. 
 
Pamoja na hayo RC Makonda amesema chimbuko la muswada huo ni mapendekezo yaliyotokana na Kongamano la Wajane zaidi ya 5,181 alilohitisha mwezi April Ukumbi wa Mlimani City ambapo katika kongamano hilo alipokea Kero na Malalamiko yaliyomlazimu kuunda kamati iliyoshirikisha Wadau na Wataalamu mbalimbali kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia.
 
Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa alichokifanya RC Makonda kupigania haki za wajane ni Ushujaa wa hali ya Juu na ameweka historia ya Jambo ambalo halijawahi kufanyika ambapo amemuahidi kufanyia maboresho ya haraka na kuwasilisha Bungeni.

Vijiji 11 Njombe mjini vyakosa umeme

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amewataka wananchi wanaoishi ndani vijiji 11 halmashauri ya mji wa Njombe vilivyokosa umeme kuwa wavumilivu kwani serikali inategemea kufikisha umeme katika vijiji hivyo ndani ya miezi minne.

Waziri Kalemani wakati akiwasha umeme Kituo cha afya cha Ihalula kilichopo kata ya utalingolo halmashauri ya mji wa Njombe amesema,jimbo la Njombe mjini lina vijiji 44,vitongoji 29 huku vijiji 11 pekee vikikosa umeme.

“Hii ni Njombe mjini na sio Njombe vijijini kwa maana hiyo haikuwemo kwenye mpango wa umeme vijijini,lakini serikali imemsikiliza Mbunge wa hapa,umeme ulikuwa ni wa laki tatu na ishirini,ulikuwa ni wa laki moja na sabini na saba ila leo mnalipa elfu 27,na mbunge wa hapa ana vijiji 44 na vitongoji 29 katika vijiji 44 vijiji 11 vilivyobaki havijapelekewa umeme navyo vitapelekewa ndani ya miezi minne”alisema Kalemani

Mbunge wa jimbo la Njombe mjini Edward Frans Mwalongo amesema jimbo lake licha ya kutokuwepo kwenye mpango wa umeme wa rea lakini serikali imepeleka umeme huo huku akiomba vijiji vyote vilivyosalia vipatiwe umeme pamoja na kuwaangalia kwa ukaribu wazalishaji binafsi wa umeme  wa maporomoko ya maji.

“Lakini mh.waziri nikuombe sana wako wafuaji wa umeme binafsi.niwaombe kama wizara na kama tanesco,muwasimame wafanye kazi kwa mwendo unaolidhisha kwasababu wengine wamechukuwa mda mrefu sana kuzifanya hizo kazi bila mafanikio makubwa na wananchi wanahitaji umeme”alisema Mwalongo

Baadhi ya wakazi wa Ihalula wamesema kufika kwa umeme huo kutawasaidia kufungua miradi mbalimbali ya kiujasiriamali  kama viwanda vidogo vidogo vya kusindika nafaka na matunda.

Hata hivyo waziri Kalemani amefika na kuwasha umeme kijiji cha Itombololo kata ya Igima,Itowo kata ya Mdandu na kijiji cha Saja vilivyopo wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Latest Images