Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Majaliwa Azungumza Na Rais Wa AFRECO Nchini Japan....Wameahidi Kutoa Basi litakalotoa huduma za matibabu Dodoma na Mikoa Jirani

$
0
0
TAASISI ya Association of African Economy and Development in Japan (AFRECO) imeahidi kuipatia Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Chuo Kikuu cha Dodoma basi ambalo ni hospitali kamili litakalotoa huduma za matibabu kwa Manispaa ya Dodoma, Mikoa na Wilaya zinazoizunguka Mkoa wa Dodoma.

Basi hilo litakapowasili nchini kutoka Japan linatarajiwa kuwa ni mkombozi kwa wananchi waishio vijijini na katika maeneo ambayo hayana hospitali kwani kila litakakokwenda kutoa huduma litakuwa na madaktari waliobobea katika utaalamu wa tiba mbalimbali, vifaa tiba, maabara pamoja na dawa.

Hayo yamebainishwa leo (Jumapili, Septemba 1, 2019) na Rais wa   AFRECO, Bw. Tetsuro Yano katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa yaliyofanyika kwenye hoteli ya Yokohama Bay nchini Japan.

Bw. Yano amesema wameamua kuanza kutoa misaada na huduma zao nchini Tanzania baada ya kufurahishwa na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Ameongeza kuwa anaamini siku moja Tanzania itakuwa nchi ya mfano kwa Afrika Mashariki na Afrika yote kwa kutoa huduma bora za tiba kwani itakuwa na vituo vingi vya Afya na hospitali zenye uwezo wa kutibu magonjwa kama vile ya moyo na figo. Hata  hivyo tayari wagonjwa toka nchi jirani wameanza kuja kutibiwa nchini.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema mbali na kutoa basi ambalo litakuwa linatoa huduma za matibabu, pia taasisi hiyo ya AFRECO   itasaidia katika kupandisha hadhi hospitali ya Benjamin Mkapa ya Chuo Kikuu cha Dodoma kuwa Shule kamili ya tiba.

Amesema hospitali hiyo ya Benjamin Mkapa ya Chuo Kikuu cha Dodoma itapatiwa vifaa   mbalimbali vya tiba ambavyo vitaifanya hospitali hiyo kuwa ni shule bobezi   kwa utoaji wa tiba mbalimbali nchini Tanzania na Barani Afrika.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa wamekubaliana na AFRECO kuanzisha kitivo maalum cha Uhandisi wa Vifaa Tiba ambacho kitafundisha uhandisi wa vifaa tiba ili nchi yetu iwe na watalaamu wa  kukarabati vifaa tiba pindi vinapoharibika badala kuvipeleka nje ya nchi au kuagiza wahandisi na watalaamu kutoka nje ya nchi kuja kuvitengeneza.

“Hivi sasa yanafanyika makubaliano ya kuanzisha   kiwanda cha kutengeneza vifaa tiba na kwa kuanzia wataanza kutengeneza maji ya drip ambayo huongezwa kwa wagonjwa kwa maeelekezo ya madaktari na baadae watengeneza dawa mbalimbali.”

Naye,Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma,  Mipango, Utawala na Fedha, Profesa Donald Mpanduji amesema wametia saini hati ya makubaliano kati ya  AFRECO na Chuo Kikuu cha Dodoma ambayo yanalenga kuboresha hospitali ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

Awali, Dkt. Omary Ubuguyu kutoka Wizara ya Afya amesema maboresho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika huduma za tiba yameiwezesha Tanzania kupunguza wagonjwa wanaopelekwa nchi za nje kwa matibabu kutoka 800 hadi 42  ambalo ni punguzo la  asilimia inayotajwa kuwa 200.

Amesema hatua hiyo imeongeza nafasi kwa watalaamu wetu wa tiba kujifunza zaidi pamoja na kuwapunguzia wananchi gharama za kusafiri kwenda nje ya nchi kutafuta tiba na pia imeipunguzia Serikali gharama ya fedha za kigeni ambazo zingetumika kuwatibu wagonjwa nje ya nchi.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,        
JUMAPILI, SEPTEMBA 01, 2019.

Rais Magufuli Amualika Rais Yoweri Museveni katika Kongamano La Wafanyabiashara Tanzania Na Uganda

$
0
0
Rais Magufuli amemualika Rais Museveni wa Uganda katika ufunguzi wa mkutano mkubwa wa Wafanyabiashara kati ya Uganda na Tanzania  ambao utawashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 1000 ambao watapata nafasi ya kujadili namna ya kuongeza biashara mpya baina ya nchi hizi Mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akihamasisha  wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza Kwa wingi kushiriki katika kongamano hilo linalotaraji kufanyika Septemba 6,2019 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Bashungwa amesema kongamano hilo litafunguliwa na Rais Yoweri Museven wa Uganda, litahudhuriwa pia  na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli

Aidha Waziri Bashungwa ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao wengi wao ndio wamekuwa wakifanya biashara Moja kwa Moja na nchi za jirani hili waweze kupata mtandao mpya wa kibiashara.

Ametaja na kusema muungano wa kimtandao baina ya Tanzania na Uganda utafungua njia mpya ya Biashara hadi Sudan ya kusini ambao wamekuwa wakifanya biashara na Uganda kila uchwao.

Programu Ya Kitalu Nyumba Yawapa Hamasa Vijana Kushiriki Kwenye Sekta Ya Kilimo

$
0
0
Na; Mwandishi Wetu
Programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu nyumba (Green house) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imewapa hamasa vijana kushiriki kwa wingi kwenye sekta ya kilimo ikiwa ni chanzo cha kimoja wapo cha ajira nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Ziara yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba, Mkoani Iringa.

Waziri Mhagama alieleza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliamua kuanzisha programu hiyo kwa lengo la kuwawezesha vijana kushiriki kwa wingi kwenye masuala ya kilimo ili waweze kujiajiri wao wenyewe na kuajiri vijana wenzao kupitia teknolojia hiyo.

“Mradi huu unatekelezwa kwenye Halmashauri 185 nchini katika awamu hii ya kwanza ikiwa na lengo la kuwawezesha vijana kuwa na ujuzi pamoja na stadi za kilimo cha kisasa kupitia kitalu nyumba ambacho kina tija katika kuwapatia mazao bora na mengi yatokanayo kwenye eneo dogo,” alieleza Mhagama

Alieleza kuwa Serikali imeendelea kuwawezesha na kuwajengea uwezo vijana wa masuala ya ukuzaji ujuzi ili waweze kuongeza tija kwenye shughuli wanazozifanya na zitakazo wakwamua kiuchumi.

“Vijana wanaweza kupata ajira bora katika kilimo endapo watawekewa mazingira bora kama kuimarisha teknolojia na mbinu za kilimo,” alisema Mhagama.

Hata hivyo aliwasihii vijana kuhakikisha wanatunza vitalu nyumba hivyo kwa kuwa watanufaika navyo na vitawasaidia kufanilisha malengo yao sambamba na kuleta maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo.

Aidha alitoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakiksha wanawasilisha njia bora zaidi za kuwapata vijana stadi zitakazo wajengea uwezo kupata teknolojia za kisasa zitumikazo katika kilimo pamoja na kuwapatia mitaji ambayo itawawezesha kujenga vitalu nyumba vyao binafsi.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Venerose Mtenga alisema kuwa Ofisi hiyo inatekeleza programu mbalimbali zitakazo wawezesha vijana kupata ujuzi na stadi stahiki zitakazo wasaidia kuondokana na changamoto ya ajira.

Naye Mratibu wa Mradi huo katika Halmashauri ya Iringa Vijijini Bw. Daniel Mlay alisema kuwa jumla ya vitalu nyumba vinne vimejengwa na vijana 431 wameweza kunufaika na mafunzo hayo.

“Tutaendelea kuwahamasisha vijana washiriki kwa kikamilifu katika mradi huu kwa kuwa una manufaa mazuri kwao,” alisema Mlay  

Pia mmoja wa vijana walionufaika kupitia Mradi huo Bw. Ramadhani Haule alieleza kuwa mradi huo wa Kitalu Nyumba umewasaidia kupata elimu bora ya kilimo na umesaidia vijana kuondoka kwenye makundi ya wasiokua na ajira.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutuamini na kutupatia ujuzi huu, tunaahidi tutaendelea kushirikiana vijana wengi ili kujikwamua kiuchumi,” alisema

Katika ziara hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alitembelea Vitalu Nyumba vilivyopo katika eneo la Ihemi na Halmashauri ya Mafinga.

MWISHO

Usisumbuke Tena na Tatizo la Nguvu za Kiume....Soma hii

$
0
0
Super Mkunyati Mix; ni dawa bora ya mitishamba yenye uwezo wa kutibu na kumaliza matatizo yote ya ukosefu wa nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile:-
 
  -kuwai kufika kileleni ndani ya dakika chache tu.
 -Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa muda mrefu.
 -Kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu(punyeto) husababisha kuishiwa au kupungukiwa na nguvu za kiume.

Epuka matatizo haya kwa kutumia dawa bora ya asili ya Super Mkunyati Mix ni kiboko ya matatizo haya yanayowasumbua baadhi ya wanaume wengi.
 
Pia kuna dawa ya kutibu Presha,miguu kufa ganzi, tumbo kuuma chini ya kitovu, kisukari,ngiri, chango aina zote na nk, matatizo haya nayo uchangia matatizo haya ya ukosefu wa nguvu za kiume na kuwa na maumbile madogo na uume mfupi.
 
JABABILA;- ni dawa ya mvuto wa mapenzi ,mchumba, mke, mume aliyekuacha .
 
ITALIGULA;- ni dawa ya biashara  .

Ofisi zetu zinapatikana DAR ES SALAAM, SONGEA - BOMBAMBILI, SHINYANGA - KAHAMA MJINI. na pote pale ulipo utaipata huduma hii,kama huna nafasi utaletewa hulipo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na DR. MACHIMKENDA simu no, 0717 339 771AU 0763 172 670whatsApp 0621998653

Jeshi la Polisi Latoa Onyo Kwa Watakaofanya Vurugu Wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mtaa

$
0
0
Jeshi la Polisi nchini limewatahadharisha wale wote watakaoleta vurugu wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa  na kusema watachukuliwa hatua kali za kisheria

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime, ambaye amesema kuwa watu wakifuata sheria chaguzi zote nchini zitabaki kuwa na amani.

“Wale ambao wanahisi watatingisha kiberiti kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa, sisi tumejipanga vizuri kukabiliana nao kwa nguvu zote kwa jinsi ambayo tutazidi kupokea nguvu toka kwao au ubishani toka kwao” amesema Misime.

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Ni Nini Kinachosababisha Wanaume Wengi Kuishiwa Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanaume kuishiwa nguvu kiume na maumbile madogo.

Nini kinasababisha upungufu wa nguvu za kiume  (1) Msongo wa mawazo( 2) magonjwa ya sukari,presha,vidonda vya tumbo,kukosa choo,na tumbo kuunguruma( 3) kujichua kwa muda mrefu   (4) ngiri ,korodani kuvimba,

Tiba ya tatizo:
MAJINJAS;  ni dawa  yenye virutubisho na mchanganyiko wa wa mizizi tisa (9) dawa hii hutibu matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo -dawa hii itakupa uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu ( 2) kuwahi kufika kileleni dawa hii itakupa uwezo wa kuchelewa ( 3)  dawa hii hutibu tatizo la maumbile ya kiume kusinyaa hasa kwa wanaume  waliojichua kwa muda mrefu  

MTINJETINJE; ni dawa ya kisukari ambayo imechanganywa na mizizi na mbegu -dawa hii husaidia kurejesha kongosho kwenye hali yake ya kawaida.

Fika ofisini kwangu MBAGARA ZAKHEMU KARIBU NA BENK YA  KCB utaona bango limeandikwa NTUNZU HEBRISRI CLINIC na mwanza yupo wakala nipigie simu whasap  0783185060. 0620113431 DR AGU na utaletewa popote uduma  hii

Taarifa Kwa Umma: Kuhusu Mwenendo Wa Mlipuko Wa Ugonjwa Wa Ebola Ulioripotiwa Nchi Jirani Za Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo Na Uganda.


Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

$
0
0

Super nzoka  IKEMEKO   TRDITONAL clinic ;

Ni dawa ya Asili  iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 
 
Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji  ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 .
 
Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0789289945.Au whasap/0716343218 TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya mustang

Usisumbuke Tena na Tatizo la Nguvu za Kiume....Soma hii

$
0
0
Super Mkunyati Mix; ni dawa bora ya mitishamba yenye uwezo wa kutibu na kumaliza matatizo yote ya ukosefu wa nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile:-
 
  -kuwai kufika kileleni ndani ya dakika chache tu.
 -Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa muda mrefu.
 -Kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu(punyeto) husababisha kuishiwa au kupungukiwa na nguvu za kiume.

Epuka matatizo haya kwa kutumia dawa bora ya asili ya Super Mkunyati Mix ni kiboko ya matatizo haya yanayowasumbua baadhi ya wanaume wengi.
 
Pia kuna dawa ya kutibu Presha,miguu kufa ganzi, tumbo kuuma chini ya kitovu, kisukari,ngiri, chango aina zote na nk, matatizo haya nayo uchangia matatizo haya ya ukosefu wa nguvu za kiume na kuwa na maumbile madogo na uume mfupi.
 
JABABILA;- ni dawa ya mvuto wa mapenzi ,mchumba, mke, mume aliyekuacha .
 
ITALIGULA;- ni dawa ya biashara  .

Ofisi zetu zinapatikana DAR ES SALAAM, SONGEA - BOMBAMBILI, SHINYANGA - KAHAMA MJINI. na pote pale ulipo utaipata huduma hii,kama huna nafasi utaletewa hulipo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na DR. MACHIMKENDA simu no, 0717 339 771AU 0763 172 670whatsApp 0621998653

Miili ya waliofarikia ajalini Pwani Kupimwa DNA

$
0
0
Ndugu wa karibu wa watu waliofariki kwenye  ajali ya gari iliyotokea wilayani Kibiti mkoani Pwani wametakiwa kujitokeza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kesho Jumatatu Septemba 2, kwaajili ya zoezi la kufanya uchunguzi wa kulinganisha Vinasaba (DNA) ili waweze kupewa miili hiyo.

Miili ya watu hao wanne wakiwa watu wazima na mmoja mtoto ilifikishwa katika hospitali hiyo jana Jumamosi asubuhi kwa ajili ya kuhifadhiwa ikiwa haitambuliki kutokana na kuharibika.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Septemba 1,2019 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha imesema miili hiyo imeungua kupita kiasi na kusababisha utambuzi wake kuwa mgumu.

“Jana saa tano asubuhi tumepokea miili ya marehemu watano wa ajali ya gari iliyotokea huko Kibiti ambapo imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hivyo tunawaomba ndugu wa karibu wa marehemu waje kesho saa mbili asubuhi ili kuchukuliwa sampuli na Mkemia Mkuu wa Serikali ili kusaidia kufanya uchunguzi wa kulinganisha vinasaba kati ya ndugu na marehemu  ili waweze kupewa miili hiyo kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi kukamilika,” amesema.

Aligaesha amesema miili hiyo ambayo ni ya watu wazima wanne na mtoto mmoja imeungua sana hali iliyopelekea utambuzi wao kuwa mgumu lakini tayari wameshafanya uchunguzi na kuchukua sampuli kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali ili kufanya uchunguzi zaidi.

Taarifa Kwa Umma: Kuhusu Mwenendo Wa Mlipuko Wa Ugonjwa Wa Ebola Ulioripotiwa Nchi Jirani Za Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo Na Uganda.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Septemba 2

Basi la Mwendokasi lateketea kwa moto katika Kituo Kikuu cha Kimara Dar

$
0
0
Basi la Mwendokasi lililokuwa linatokea Mjini kuelekea Kimara Mwisho limeteketea kwa moto eneo la Kimara Mwisho Dar usiku wa kuamkia leo lakini  hakuna madhara yaliyojitokeza kwa Binadamu, 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Teopista Malya amesema bado chanzo cha ajali hakijajulikana hadi pale uchunguzi utakapofanyika.

Amesema basi hilo lilitoka Mjini likiwa na abiria na lilipofika eneo la Kimara Mwisho walifanikiwa kushuka kabla halijateketea kwa moto.

LIVE: Rais Magufuli Azungumza Na Watendaji Wa Kata Zote Tanzania Bara Ikulu Dar es Salaam

$
0
0
LIVE: Rais  Magufuli Azungumza Na Watendaji Wa Kata Zote Tanzania Bara  Ikulu Dar es Salaam

Mahakama kuamua leo kuhusu Hatima ya Mrithi wa Ubunge Jimbo la Tundu Lissu

$
0
0
Hatima ya kuapishwa kwa mbunge mteule wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (CCM), itajulikana leo baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuamua iwapo itatoa zuio la kuapishwa kwa mbunge huyo ama la.

Katika maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na kaka wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu, Alute Mungwai Lissu, pamoja na mambo mengine, ameiomba Mahakama hiyo itoe zuio la kuapishwa kwa mbunge huyo mpya na ruhusa ya kumshtaki Spika wa Bunge, Job Ndugai, kwa kumvua ubunge pasipo sababu za msingi.

Awali Mahakama hiyo ilitupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na upande wa Jamhuri uliotaka kesi hiyo isisikilizwe mahakamani hapo, kutokana na walichodai ni mapungufu ya kisheria ya maombi hayo, hivyo kutaka yasisikilizwe.

Jaji wa Mahakama Kuu, Sirilius Matupa, aliyatupa mapingamizi hayo baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kwa maelezo kwamba upande wa Jamhuri haukuwa na hoja za msingi za kuizuia kesi hiyo isisikilizwe mahakamani hapo, hivyo kukubaliana na hoja za Wakili wa Lissu, Peter Kibatala.

Ofisi Ya Makamu Wa Rais Yawapa Mafunzo Kamati Ya Bunge

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene amesema mchakato wa Mkataba Minataka kuhusu Zebaki unaenda hatua kwa hatua ili kuwaandaa watu kuweza kupokea mabadiliko.
 
Mhe. Simbachawene amesema hayo jana Septemba mosi, 2019 wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ya Mkataba wa Minamata kuhusu Zebaki na Uwajibikaji kisheria na fidia kwa madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya bioteknolojia iliyofanyika Jijini Dodoma.
 
Alisema Serikali iliridhia Mkataba wa Minamata ili kulinda afya ya binadamu na mazingira dhidi ya madhara yanayotokana na uchafuzi wa mazingira unaotokana na Zebaki. 
 
"Umoja wa Mataifa ulikaa na kuona kwa fundisho lililotokea Minamata huko Japan hivyo madhara hayo yasiendelee kutokea duniani pamoja na hayo lakini bado zebaki ina kazi ya kufanya unapotaka kuwatoa watu kutoka utamaduni mwingine mabadiliko yanakuwepo. 
 
"Pengine mnaweza kusema kwanini zebaki isipigwe marufuku mara moja mambo yanayobadilika yanafanywa polepole si kwa haraka na hatimaye watu wataelewa tu," alisema.
 
Awali aakiwasilisha mada hiyo, Mhandisi wa Viwanda kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo imeandaa semina hiyo Julius Enock alisema madhara yanayotokana na zebaki ni kuathiri mfumo wa neva za fahamu.
 
Katika kuathiri kwa mfumo huko inasababisha kusikia, kuongea, kuona, kumeng’enya, kumeza chakula, kutembea kuathiriwa pamoja na ukakamavu wa mwili. 
 
Aidha madhara mengine aliyotaja Enock ni kuathiri viungo muhimu vya mwili ambayo ni moyo, mapafu, ini, figo na hata mimba.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga Awatunuku Vyeti Wahitimu Wa Mafunzo Ya Agro Studies Mjini Jerusalem Nchini Israel

$
0
0
Na Mathias Canal, Jerusalem-Israel
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo Tarehe 2 Septemba 2019 ameshiriki mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika mjini Jerusalem nchini Israel na kuwatunuku vyeti vya kuhitimu wanafunzi 45 kutoka Tanzania.

Katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa ICC (Jerusalem International Conventional Center), Waziri Hasunga amewapongeza vijana hao kwa kuhitimu masomo yao hivyo amewaahidi kuwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuboresha mazingira wezeshi kwenye sekta ya kilimo hivyo wanayo nafasi nzuri kuutumia ujuzi walioupata kuboresha kilimo watakaporejea nchini Tanzania.

Mahafali hayo yatajumuisha vijana 1600 kutoka mataifa zaidi ya 12 ambapo kati ya hao vijana 45 ni watanzania, miongoni mwao wanawake wakiwa ni 9 na wanaume ni 36.

Waziri huyo wa kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepewa jumla ya nafasi 100 kwa ajili ya kupeleka vijana wa kitanzania kujifunza kilimo cha kisasa nchini Israel hivyo fursa hiyo ni muhimu kwani vijana hao wa Tanzania wamepata ujuzi wanachotakiwa kufanya  ni kutumia ujuzi huo kwa manufaa makubwa nchini mwao.

Akizungumza na mtandao wa WazoHuru  Blog mara baada ya kuwakabidhi vyeti wahitimu hao Mhe Hasunga amesema kuwa kupatikana kwa nafasi hizo 100 ni kutokana na ombi la Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa serikali ya Israel ili kuwawezesha vijana wengi wa kitanzania kujifunza mbinu na teknolojia za kilimo cha kisasa.

Kadhalika, Waziri Hasunga atakutana na kurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Agro Studies ambapo miongoni mwa mazungumzo muhimu itakuwa ni pamoja na kumuomba uwezekano wa kuongezewa nafasi zaidi ili vijana wengi wa kitanzania waende kujifunza mbinu mpya za kilimo nchini Israel.

Pia, Mhe Hasunga atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo nchini Israel kujadiliana nae maeneo mbalimbali na fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Katika mkutano mwingine, Mhe Hasunga atakutana na kufanya mazungumzo na wadau wawekezaji wakubwa wa sekta ya kilimo nchini Israel ili kuwaeleza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo tarehe 4 Septemba 2019 Mhe Hasunga atashiriki mapokezi ya vijana 100 ambao wapo nchini Israel kwa ajili ya kuanza mafunzo yao.

Leo tarehe 2 Septemba 2019 ni siku ya pili ya ziara ya kikazi ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga nchini Israel kati ya siku sita atakazokuwa nchini hapa.

MWISHO.

Rais Magufuli Atoa Maagizo Mazito Kwa Watendaji wa Kata Nchini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Watendaji Kata nchi nzima, kutembea kifua mbele na  kwa kujiamini kwa kuwa wao ni wawakilishi wake katika ngazi ya kata na hivyo amewataka wasimamie vema miradi ya Serikali ambayo inatekelezwa kwenye maeneo yao.

“Cheo cha ofisa mtendaji wa kata siyo kidogo, ninyi ni wawakilishi wangu ngazi ya kata. Tunapozungumza mafanikio ya Serikali ninyi ndiyo wasimamizi wa mwanzo katika mafanikio hayo.

“Kwa hiyo napenda kuwathibitishia ndugu zangu, tembeeni kifua mbele. Wala kamwe asitokee mtu kuwanyanyasa kule mlipo,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameyasema hayo  Ikulu, jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na watendaji hao wa kata, ambapo amewataka licha ya kusimamia miradi ya Serikali, pia kusimamia nidhamu ya watumishi wote wa umma wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, wanaoishi kwenye Kata zao.

"Nyinyi ndiyo wasimamizi wa Watumishi wa Umma kwenye Kata zenu, Mtumishi wa Umma aliyeko kwenye Kata yako, wewe ndiye msimamizi wake, kama kwenye Kata yako yuko RC, Waziri au DC usiogope kumwandikia mapendekezo kama anaenda kinyume na maadili ya kazi zake na ukimuona mkubwa sana nitumie nakala na mimi". amesema Rais Magufuli.

Kuhusu majukumu ya watendaji hao, Rais Magufuli amesema maofisa hao wana jukumu la kuhakikisha ulinzi na usalama wa kata zao.

Amewataka pia maofisa hao kuwa makini na utoaji wa vitambulisho vya Taifa kwa wageni.

Rais Magufuli amesema kikao hicho ni mwendelezo wa vikao mbalimbali anavyofanya na Watumishi wa Umma, Ikulu, ambapo lengo lake ni kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Watu zaidi ya 100 wauliwa Yemen na ndege za Suadi Arabia

$
0
0
Yemen bado imo katika mshtuko baada ya watu zaidi ya 100 kuuliwa kutokana na mashambulio yaliyofanywa na ndege za muungano unaoongozwa na Saudi Arabia. 

Mashambulio yaliyokuwa mabaya kabisa mnamo mwaka huu yalifanyika kwenye kituo cha mahabusu kinachosimamiwa na waasi wa Kihouthi. Watu wengine kadhaa walijeruhiwa katika hujuma hiyo ya majeshi ya nchi zinazoongozwa na Saudi Arabia. 

Mahabusu wapatao 170 walikuwamo kwenye kituo hicho kilichopo kwenye jimbo la Dhamar la kusini magharibi mwa Yemen. 

Shirika la misaada la Msalaba Mwekundu limesema watu 40 waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu lakini wengine wanahofiwa kuwa wamekufa. 

Mkuu wa shirika hilo nchini Yemen amesema idadi ya waliokufa inaweza kuwa kubwa zaidi. Nchi zilizofungamana kijeshi na Saudi Arabia katika vita vya nchini Yemen zimeshutumiwa vikali duniani kwa kufanya msahambulio ya ndege ambayo mara nyingine yamezilenga shule, hospitali na pia sherehe za harusi na kusababisha vifo vya maelfu ya raia. 

Tangu mwaka 2015, Mfungamano wa nchi hizo umekuwa unapambana na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images