Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Atoa wito kwa Mataifa ya Afrika kutafsiri vizuri dhana ya uhuru na kujiepusha na masalia ya fikra za kikoloni

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mataifa ya Afrika kutafsiri vizuri dhana ya uhuru na kujiepusha na masalia ya fikra za kikoloni za kuamini kuwa watawala wa zamani wa Mataifa ya Afrika ndio wenye uwezo wa kusaidia kusimamia na kuendeleza rasilimali zilipo katika Bara la Afrika.

Rais Magufuli ametoa wito huo jana Ikulu alipohutubia Mkutano wa 6 wa Jukwaa la Uongozi Afrika unaohudhuriwa na Marais Wastaafu Benjamin William Mkapa (Tanzania), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (Tanzania), Thabo Mbeki (Afrika Kusini), Hassan Mohamud (Somalia), Hery Rajaonarimampianina (Madagascar), Mabalozi, Wawakilishi wa Kimataifa na washiriki wa Jukwaa la Uongozi Afrika.

“Maana hasa ya kupigania uhuru ilikuwa ni kurejesha rasilimali na hasa maliasili zetu lakini pia kuwa na maamuzi kamili kuhusu namna ya kuzisimamia na kuzitumia kwa manufaa yetu ili kuleta ukombozi wa kiuchumi, na hii ndio maana pekee ya kulinda uhuru wa kisiasa” Rais Magufuli

Tusijidanganye watawala wetu wa zamani hawawezi kugeuka kwa usiku mmoja na kuwa wajomba zetu au wakombozi wetu kiuchumi, utegemezi huu ndio umeimarisha mizizi na misingi ya ukoloni mamboleo, ni lazima tuamke” Rais Magufuli.

Serikali Yafuta Miliki Ya Mashamba Ya MOA Mkinga

0
0
Na Munir Shemweta, WANMM MKINGA
Serikali imefuta miliki ya Mashamba matatu ya Mkomazi Plantantions maarufu MOA yaliyopo wilaya ya Mkinga mkoani Tanga kutokana na kukiuka masharti ya uendelezaji ikiwemo kutelekezwa bila kufanyiwa maendelezo yaliyokusudiwa  na kutolipiwa kodi ya pango la ardhi.

Uamuzi huo umetangazwa leo tarehe 30 Agosti 2019 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipozungumza na wananchi wa Mayomboni wilayani Mkinga mkoani Tanga alipokwenda kutatua mgogoro wa muda mrefu katika eneo hilo.

Mashamba yaliyofutiwa ni lenye hati Na 9780  na ukubwa wa ekari 14,688, shamba  Na 4268  ekari 804 na Shamba lenye Hati Na 9781  ekari 246 ambapo mashamba yote matatu yana ukubwa wa ekari 15,738.

Kufuatia uamuzi huo, jumla ya vijiji kumi vyenye kaya 3,236 zilizo na wakazi 16,450 zitanufaika na uamuzi wa serikali kutokana na wananchi wake kuvamia mashamba hayo na kufanya maendelezo ya kujenga makazi, shule pamoja na kuendesha shughuli za kilimo cha mazao ya kudumu na ya muda mfupi.

Vijiji vilivyonufaika ni uamuzi wa Serikali kufuta mashamba ya Mkomazi Plantations ni kijiji cha Kilulu-Dunga, Zingibari, Mwaboza, Mwakikoya, Mhandakini, Nkanyeni, Sigaya, Mayomboni, Ndumbani pamona na kijiji cha Moa

Akizugumza wakati wa kutangaza uamuzi huo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema uamuzi wa kufuta mashamba hayo matatu unafuatia maombi yaliyotumwa kwa Raisi John Pombe Magufuli ya kutaka kufutwa mashamba hayo kutokana na kutoendelezwa na wamiliki wake kwa muda mrefu.

Alisema, Rais ameridhia maombi hayo kwa kuwa serikali imekuwa ikisisitiza utekelezwaji wa sheria ya Ardhi Na 4 ya mwaka 1999 ikiwemo uendelezaji wa mashamba ambayo yamemilikishwa sehemu mbalimbali nchini.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliagiza kufanyika upimaji katika vijiji vyote kumi vilivyopo ndani ya shamba hilo sambamba na kuanishwa miapaka ya vijiji hivyo na kupatiwa hati ambapo alitaka wananchi wanaishi kwenye vijiji hivyo kutobughudhiwa.

Aidha, Waziri Lukuvi alitaka maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya uwekezaji katika shamba yaliyofutwa kuachwa kwa ajili ya shughuli hiyo ikiwemo muwekezaji wa Katani Azka International Tanzania mwenye ekari mia tano pamoja na maeneo ya viwanda kama kile cha kuzalisha chumvi na kusisitiza kuwa serikali inataka uwekezaji utakaotoa ajira kwa vijana na wakati huo kupata mapato kupitia kodi ya pango la ardhi.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameagiza kufanyika uhakiki wa mashamba mengine ya Kwa Mtili Estates Co Ltd yaliyopo Mkinga mkoani Tanga ambapo ekari 58 pekee ndizo zilizoombwa kufutwa kwa Rais kutokana na kutoendelezwa huku mmili wake ikidaiwa kumiliki ekari  2,841.

Hatua hiyo inafuatia Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili katika halmashauri ya wilaya ya Mkainga Obed Katonge kueleza kuwa, Kwa Mtili Estates Co Ltd inalo shamba la lenye ukubwa wa ekari 2,841 tofauti na inavyoonekana katika kumbukumbu za ofisi ya Msajili wa Hati Kanda ya Kaskazini ambazo ni 58.

Lukuvi aliagiza wataalamu wa ardhi kutoka Kanda ya Kaskazini kufanya uhakiki huo katika kipindi cha mwezi mmoja na kumpa taarifa ya uhakiki huo mwisho wa mwezi Septemba 2019 na kufafanua kuwa pale itakapothibitika kuna ujannja uliofanyika wa kumuongeza mmiliki wa shamba hilo hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika.

Mbunge wa Jimbo la Mkinga mkoani Tanga Dustan Kitandula aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kusikiliza kilio cha muda mrefu cha wananchi wanaoishi eneo la shamba lililofutwa la kutaka kurejeshewa ardhi yao waliyokuwa wakiutumia kwa shughuli mbalimbali.

Alisema, mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa mkinga na wamiliki wa mashamba ya Mkomazi Plantantions Co Ltd umekaa kwa muda mrefu na kuwafanya wananchi kuwa na ndoto isiyokuwa na majibu lakini uamuzi uliotolewa na Serikali umewafanya kuishi kwa furaha na amani .

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili 1 September

Rais Magufuli Na Mkewe Janeth Magufuli Washiriki Misa Takatifu Dominika Ya 22 Mwaka “C”

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 22 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Dkt. Alista Makubi, Septemba 01,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali  katika Misa Takatifu Dominika ya 22 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Dkt. Alista Makubi, Septemba 01,2019.

PICHA NA IKULU

Zabuni Ununuzi wa Treni 5 Za Umeme, Mabehewa na Vichwa Waiva

0
0
Na Mwandishi Wetu
Serikali imesema kuwa zabuni ya ununuzi wa treni 5 za umeme zilizokamilika za abiria utawezesha kuanza kwa huduma ya usafirishaji kati ya Jiji la Dar es Salaam na Morogoro na baadae Dodoma.
 
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jana  jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali hadi kufikia Agosti 2019. 
 
Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali imeanza zabuni hiyo ambayo itawezesha kununuliwa kwa  vichwa 22 vya Treni (vitano vya mafuta yaani Diesel Locomotive na 17 vya umeme yaani Electrical Locomotive), pamoja na mabehewa ya abiria 60 na 1430 ya mizigo.
 
“Treni tano (5) zilizokamilika (Electrical Multiple Unit) za abiria zenye mabehewa nane (8) kila moja na vichwa viwili kwa ajili ya uendeshaji wa treni za abiria kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na kisha Dodoma zitawezesha watanzania kuanza kutumia usafiri wa kisasa na wa gharama nafuu hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi.” Alisisitiza Dkt. Abbasi
 
Akifanua amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo katika kuimarisha miundombinu ikiwemo ya reli ndio maana imeweka mkazo katika ujenzi wa mradi huo wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR)
 
Kuanza kwa huduma ya usafirishaji kati ya Morogoro na Dar es Salaam na baadae Dodoma kunatajwa kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo hapa nchini.
 
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli imeweka mkazo katika kuimarisha miundombinu ili kukuza na kujenga uchumi jumuishi unaowawezesha wananchi kuondokana na umasikini kwa kujikwamua kiuchumi.

Kongamano La Wafanyabiashara Kati Ya Tanzania Na Uganda Kufanyika Jijini Dar Es Salaam

0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Innocent Bashungwa amesema Tanzania na Uganda zinatarajia kufanya Kongamano la Kibiashara la pamoja ikiwa ni mara ya Kwanza kufanyika nchini.

Bashungwa ameyasema hayo  jana mbele ya Waandishi wa Habari ambapo amesema Kongamani hilo linatarajia kufanyika Septemba 6, 2019 kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

“Kongamano hili la kibiashara baina ya Tanzania na Uganda ambalo litawashirikisha wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda litasaidia kuweka mazingira wezeshi ya kuongeza wigo wa kujenga viwanda zaidi nchini hasa vya usindikaji wa mazao ili kuongeza thamani ya mazao hayo”

Mpaka sasa Tanzania inauza bidhaa za mazao na bidhaa za viwandani nchini Uganda ambapo takwimu zinaonesha  kwa miaka miwili iliyopita Tanzania imeweza kuuza bidhaa za mazao ya chakula na viwandani zenye thamani ya shilingi Bilioni 300 kutoka Bilioni 100 ambalo ni ongezeko mara mbili ya fedha zilizopatikana huko nyuma.

Waziri Bashungwa amewakaribisha wafanyabiashara na wadau mbalimbali kujiandikisha ili kushiriki katika kongamano hilo ambalo litafungua fursa nyingi kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda, hivyo kuongeza fursa zaidi za kibiashara kati ya nchi hizo.

Halmashahuri Ya Wilaya Ya Bukoba Mkoani Kagera Yafanikiwa Kuvuka Malengo Ya Ukusanyaji Wa Mapato Kwa Mwaka Wa Fedha 2018/2019.

0
0
Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera
Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera imefikisha zaidi ya 97% za ukusanyaji wa mapato kwa mwaka mzima ambayo ni zaidi ya shillingi bilion moja na zaidi ya milioni mia tatu.
 
Hayo yamesemwa na Mwenyeki wa halmashahuri ya Wilaya ya Bukoba Mh Murshid Ngeze katika kikao cha halmashahuri hiyo chenye lengo la kufunga robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019.
 
Mh Ngeze amesema kuwa halmashahuri hiyo imepiga hatua  kubwa na kusema kuwa wakati wanaingia madarakani walikuwa wakikusanya zaidi  ya shilingi milioni mia sita kwa mwaka lakini mpaka sasa wamevuka malengo kwa 100% kwa miaka minne wakiwa kwenye uongozi.
 
Ameongeza kuwa mafanikio hayo yamekuja kutokana na kasi ya  Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuri ya usimamiaji mzuri wa rasirimali mbalimbali za nchi kitu kilichopelekea kila kiongozi kuwajibika kadri ya nafasi yake kuanzia ngazi ya juu mpaka ya chini kwa ajili ya maendeleo ya watanzania wote kwea ujumla.
 
Sanjali na hayo Mh Ngeze ambaye pia ni diwani wa kata ya Rukoma ameongeza kuwa wanafunzi wa kata hiyo wanaangaika kufata huduma ya elimu ambapo wanatembea takribani kilometa 38 jambo ambalo limepelekea kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ili kuweza kutatua changamoto hiyo.

Waziri Mwakyembe Atoa Agizo La Kuwasaka na Kuwakamata Washereheshaji Wa Harusi Wasio Kuwa Na Vitambulisho Mkoani Kagera.

0
0
Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera
Waziri  wa Habari sanaa utamaduni na michezo Dokta Harrison Mwakyembe ametoa agizo la kuwasaka  kubaini na kuwakamata washereheshaji wa  harusi maarufu kama mc mkoani Kagera ambao hawana vitambulisho vya kazi hiyo na kuwa atakayebainika atachukuliwa sheria kali ikiwemo harusi hiyo kusimama wakati huo.
 
 Waziri Mwakyembe  ametoa kauli hiyo August 30 Mwaka huu wakati akiwa mkoani Kagera katika mkutano na  wadau wa sekta ya habari utamaduni sanaa na michezo uliofanyika katika ukumbi wa mkoa uliopo Bukoba manispaa mkoani hapa.
 
Waziri Mwakyembe amesema kuwa tayari serikali imeishaweka utaratibu wa kila mfanya  biashara kuwa na kitambulisho na kudai kuwa utaratibu huo unajulikana  nchi nzima.
 
 Ametaja kuwa  kitendo cha  baadhi ya washereheshaji kunyonya jasho la ambao tayari wamelipia vitambulisho vya kuwatambua katika kazi hiyo ni kosa kisheria.
 
Waziri huyo Amesema ni jambo la kusikitisha na kutoa agizo la Wakaguzi kufanya  msako mkali ili kubaini washereheshaji ambao hawajasajiliwa na kuwa wakibainika watachukuliwa sheria kali ikiwemo harusi hiyo kusimamishwa wakati huo.  
 
Amesema  sambamba na kuwachukulia sheria kali watatozwa Faini itakayo ingizwa  katika mfuko wa wasanii ili kuinua tasnia ya utamaduni na sanaa.

Mjumbe Halmashauri kuu Taifa CCM aagiza wapinzani "Wapigwe Nondo" Kuhusu miradi na kazi zinazofanywa na Rais Magufuli

0
0

Na Amiri kilagalila-Njombe
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM taifa ndugu Musa mwakitinya amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi CCM nchini,kuwapa elimu ya kutosha wapinzani juu ya miradi na kazi zinazofanywa na Rais kupitia serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuliko kuendelea kuwaacha wakiichafua serikali na chama hicho.

Ameyasema hayo mkoani Njombe wakati akizindua Njombe ya kijani pamoja na mbio za balozi kwanza kwa vijana wa chama hicho UVCCM mkoa wa Njombe watakao kimbia mkoa mzima kueleza utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

“Tusipohubiri kazi alizofanya Mh.Rais hakuna watakaomsemea,sasa wale wengine huwa wanapita kuharibu na maneno machafu ya hovyo juu ya kazi zinazofanywa na Rais,tunahitaji kuwa wakalimani wengine hawawezi kuona wamejitia upofu,wamejitia uziwi hawaoni hizi kazi kama ujenzi wa mahospitali,kwa hiyo twendeni tuwachape vibao vya sera tuwaeleze mbona haya yanafanyika hamyaoni,na tukifanya hivi na uhakika moja kwa moja tutawazibua maskio yao na macho yao na wenyewe watayazungumza yale ambayo Rais amekuwa akiyafanya”alisema Mwakitinya

Aidha ameongeza kuwa;

“Tuna kazi kubwa ya kuelimisha watu,ukiona haelimiki mpige nondo zilizo nzito mpige hoja zilizo nzito,katika siasa tunazo lugha zetu ukizizungumza mwingine anaweza akateseka,lakini tukizungumza chama cha mapinduzi maneno haya kwa wapinzani inakuwa ni nongwa”aliongeza Mwakitinya

Kwa upande wake katibu wa umoja wa vijana UVCCM mkoa wa Njombe Amos Kusakula amesema tukio lililozinduliwa ni la umoja wa vijana kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwa lengo la kuwaeleza wananchi utekelezaji wa ilani ya chama cha mapainduzi kwa mwaka 2015-2020.

“Kampeni hii lengo lake ni kueneza mafanikio na utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa kutangaza miradi yote iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa mkoani Njombe na nchi kwa ujumla kwa kuwa wana CCM tunajua Rais amefanya nini sasa tuwakumbushe zaidi wanachama na wananchi wa kawaida”alisema kusakula

Baadhi ya wajumbe waliohudhulia katika mkutano huo wametoa baraka kwa vijana wao huku wakitoa wito kutumia lugha nyepesi kwa wananchi wanaokwenda kukutana vijijini.

Vijana 14 wa chama hicho mkoa wa Njombe wamekabidhiwa mabango yenye picha mbali mbali za miradi iliyotekelezwa na serikali ,picha ya Rais,bendera ya chama pamoja na bendera ya Rais kwa ajili ya kukimbia majimbo 6 ya uchaguzi mkoani humo ili kufikisha ujumbe huo.

PICHA: Muonekano wa Barabara ya Kyaka-Bugene

0
0
Picha zikionesha Sehemu mbalimbali za Barabara ya Kyaka-Bugene mkoani Kagera. Barabara hiyo yenye Urefu wa Kilometa 59.1 ni kichocheo kikubwa cha Uchumi katika Mikoa ya Kanda ya ziwa pia huunganisha nchi ya Tanzania na nchi jirani za Rwanda na Burundi.

Picha namba 1-2. Sehemu ya Barabara ya Kyaka-Bugene katika eneo la Kishoju Karagwe mkoani Kagera. PICHA NA IKULU

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Mamlaka Za Miji Zatakiwa Kutenga Maeneo Maalumu Kwa Ajili Ya Wafanya Biashara

0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amezitaka mamla za Miji zote nchini kuhakikisha zinatenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo ili kuepusha migogoro ya matumizi ya ardhi katika Miji yao.

Dkt. Mabula ameyasema hayo Wilayani Igunga Mkoani Tabora wakati akijibu maswali ya wananchi ambao waliwasilisha kero zao kwake, kwani kumekuwepo na migogoro baina ya wafanyabiashara wadogowadogo na baadhi ya mamla za Miji hii inatokana na Mamlaka hizo kutokutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara hao.

“ Lazima kila mamlaka ya Mji iweke utaratibu wa kuwatengea maeneo wafanyabiashara ili waweze kufanaya biashara zao katika maeneo maluumu na sio kuwafukuzafukuza, sasa mnawafukuza ili wakafanye biashara wapi wakati hamja watengea maeneo ya kufanya biashara zao” Amesema Dkt. Mabula.

Dkt. Mabula amesisitiza kuwa nilazima mamlaka za miji ziweke mipango maalumu ya miji yao kwa kutenga maeneo ya biashara ,maeneo makazi maeneo ya kufugia maeneo ya michezo maeneo ya umma na maeneo ya taasisi za dini ili kuepusha migogoro ya matumizi ya ardhi na kuepusha kero kwa wananchi kwa kuwahamisha hamisha mara kwa mara.

Akiwa Wilayani Igunga Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula alifanya mkutanao wa hadhara katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine na kusikiliza kero za migogoro ya ardhi ya wakazi wa Wilaya hiyo, ambapo wananchi walijitokeza na kumfikishia malalamiko yao ya muda mrefu yanayohusu matumizi ya ardhi .

Miongoni mwa wananchi hao ni Bw. Joseph Kamanga ambae ni fundi seremala anaejihusisha na uuzaji wa vitanda alimuwasilishia malalamiko yake kwa niaba ya vijana wanaojihusisha na uchongaji wa vitanda Naibu Waziri Mabula dhidi ya mamlaka ya Mji wa Igunga kushindwa kuwapatia maeneo maalumu kwa ajili ya biashara zao hali inayopelekea kufukuzwa kila wanapokuwa kwenye shughuri zao.

Ziara hiyo ya Dkt. Mabula ni muendelezo wa ziara zake za kila Wilaya kutatua migogoro ya ardhi na kuhamasisha ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali kupitia kodi ya pango la ardhi pamoja na kukagua masijara za ardhi.

Ni Nini Kinachosababisha Wanaume Wengi Kuishiwa Nguvu Za Kiume

0
0
Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanaume kuishiwa nguvu kiume na maumbile madogo.

Nini kinasababisha upungufu wa nguvu za kiume  (1) Msongo wa mawazo( 2) magonjwa ya sukari,presha,vidonda vya tumbo,kukosa choo,na tumbo kuunguruma( 3) kujichua kwa muda mrefu   (4) ngiri ,korodani kuvimba,

Tiba ya tatizo:
MAJINJAS;  ni dawa  yenye virutubisho na mchanganyiko wa wa mizizi tisa (9) dawa hii hutibu matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo -dawa hii itakupa uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu ( 2) kuwahi kufika kileleni dawa hii itakupa uwezo wa kuchelewa ( 3)  dawa hii hutibu tatizo la maumbile ya kiume kusinyaa hasa kwa wanaume  waliojichua kwa muda mrefu  

MTINJETINJE; ni dawa ya kisukari ambayo imechanganywa na mizizi na mbegu -dawa hii husaidia kurejesha kongosho kwenye hali yake ya kawaida.

Fika ofisini kwangu MBAGARA ZAKHEMU KARIBU NA BENK YA  KCB utaona bango limeandikwa NTUNZU HEBRISRI CLINIC na mwanza yupo wakala nipigie simu whasap  0783185060. 0620113431 DR AGU na utaletewa popote uduma  hii

Mahakimu Watakiwa Kutoahirisha Kesi Mara Kwa Mara

0
0
Lydia Churi-Mahakama Iringa
Mahakimu wametakiwa kusimamia uendeshaji wa mashauri na kuzuia maahirisho ya mara kwa mara ya kesi bila ya sababu za msingi kwa lengo la kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati Mahakamani.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema hayo wakati wa kikao cha majumuisho mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya siku tano katika mikoa ya Iringa na Njombe aliyoifanya kwa lengo la kukagua shughuli za Mahakama pamoja na kubainisha kwa wadau changamoto zilizoibuliwa wakati wa kikao cha Mahakama ya Rufani kilichomalizika leo mjini Iringa.

Jaji Mkuu amewata Mahakimu kutokubali kuahirisha mashauri kwa muda mrefu kwa ajili ya kuandaa maamuzi madogo yanayotokana na pingamizi ambazo nyingi hutumiwa vibaya kwa lengo la kuchelewesha mashauri.

“Maafisa wote wa Mahakama ni jukumu lenu pia kuzipa nguvu za kimahakama vifungu vya sheria zinazolinda haki ya Mwananchi aliye mahabusu kwa kuhakikisha hakuna mwananchi atashikiliwa bila kufikishwa mahakamani ndani ya siku zilizowekwa na sheria”, alisema.

Alitoa rai kwa Mahakimu kutokuwa wepesi kukubali hoja za waendesha mashitaka za kusema kuwa upelelezi bado unaendelea bila ya kufafanua ni kitu gani katika upelelezi bado kinatafutwa na ni kwa muda gani.

“Ni umakini wa Mahakama ndiyo utahakikisha kuwa shughuli za upelelezi haziwanyimi wananchi haki yao ya kikatiba ya kutochelewesha haki yao ya kusikilizwa kesi dhidi yao bila sababu za kimsingi,” alisisitiza Jaji Mkuu.

Akizungumzia dhamana, Jaji Mkuu amesema ni wajibu wa Mahakama kutoa dhamana kwa makosa yenye dhamana kwa kuwa Mahakama ni msimamizi wa haki ya kila mtu kuwa huru na kuishi kama mtu huru.

Alivitaja vigezo vya kutumiwa katika kutoa dhamana kuwa ni pamoja na vitambulisho vya Taifa, na vitambulisho vinavyokubalika. Aliongeza kuwa Mahakama pia ziwaruhusu washtakiwa kujidhamini wenyewe pale Hakimu anapojiridhisha na utambulisho wao kuwa watahudhuria mahakamani.

“Mashauri ambayo washtakiwa wamekosa dhamana yasikilizwe mfululizo, kwa yale makosa yasiyo na dhamana na yako ndani ya mamlaka ya Mahakama, matumizi ya sheria yatumike ili kuyaondosha”, alisema.

Katika kupunguza msongamano magerezani, Jaji Mkuu amesema Maafisa wa Mahakama hawana budi kutumia adhabu mbadala kwa makosa madogo madogo kwa kuzingatia sheria zilizopo.

Waziri Lugola Aagiza Bodaboda Zote Zisajiliwe Nchini..... Awataka Trafiki Kuacha Visingizio Ugumu Ukusanyaji Faini Barabarani

0
0
Na Felix Mwagara, Moshi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelitaka Jeshi la Polisi Kikosi Usalama Barabarani washirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuzisajili bodaboda na bajaj zote nchini ili ziweze kudhibitiwa katika ukusanyaji wa faini pamoja na matukio mbalimbali ya kiuhalifu zinapofanya makosa.

Lugola alisema ushirikiano kati ya viongozi au askari waliopo chini ya halmashauri nchini ipo ndani ya sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi Sura namba 322, hivyo Jeshi lake linapaswa kushirikiana na Polisi Wasaidizi waliopo chini ya halmashauri ya Miji, Wilaya, Manispaa na Jiji kwa mujibu wa sheria.

Waziri Lugola ameyasema hayo Mjini Moshi, leo, wakati alipokuwa anakagua vituo vya bodaboda na bajaj mjini humo ambapo mwezi uliopita alifanya mkutano na wamiliki na waendesha bodaboda na bajaj mkoani humo kwa lengo la kutatua migogoro mbalimbali waliokuwa wanailalamikia Manispaa ya Moshi kuwanyanyasa pamoja na kuwafukuza kuegesha kituo cha Sharif una Aghakan mjini humo ambapo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabara Mkoani humo aliwaelekeza wawepo katika eneo hilo.

“Askari wa usalama barabarani, muache visingizio kuwa ukamataji wa bodaboda ni mgumu hasa mnapowaandikia makosa walipe baada ya siku saba, mara usingizia bodaboda hazipo katika mfumo wa TRA kama magari, tukiziachia tuzipate wapi, nilishawaelekeza mshirikiane na viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijijini, Miji, Manispaa na Jiji kuanzisha kanzi data, kwenye mfumo wa kuwasajili waendesha bodaboda wote sehemu mbalimbali nchini, na taarifa za bodaboda hizo endapo zinafanya makosa inakua rahisi kuzikamata kwasababu zipo kwenye mfumo,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, lengo la usajili wa bodaboda huo, ni kutokana na kuepuka kuzikamata hovyo na kuziweka vituoni jambo ambalo analipinga kuepusha mlundikano wa boaboda vituoni na pia kuwasababishia bodaboda hao kuwaongezea umaskini zaidi.

“Naomba niendelee kurudia tena agizo hili, bodaboda zinazopaswa kuwepo vituo vya polisi ni za aina tatu, moja bodaboda zilizotumika katika matukio ya uhalifu, mbili zilizohusika katika ajali, na tatu bodaboda zilizookotwa, mbali na makundi hayo zinapaswa kulipwa faini,” alisema Lugola.
Pia Lugola aliwataka baadhi askari na wananchi kuacha tabia ya kuwatuhumu viongozi wanapowatetea waendesha bodaboda wanaambiwa kuwa wanasiasa ndiyo wanasababisha ajali kuongezeka.

Amesema kauli hiyo sio sahihi, kwani wanaosababisha ajali asilimia 76 kwa mujibu wa utafiti wa ajali zinazotokea barabarani zinasababishwa na makosa ya wanadamu na sio bajaj na bodaboda peke yao, na asilimia 24 za ajali zinatokea zinasababishwa na ubovu wa miundombinu.

“Kumekuwa na dhana potofu kwamba wanasiasa kama mimi tunasababisha ajali za bodaboda, kwasababu tunawatumia bodaboda kwa mgongo wa siasa, sasa nataka niwaambie, wanaosababisha ajali barabarani ni asilimia 76 ni makosa ya wanadamu ambao ni wanadamu watembea kwa miguu, waendesha baiskeli, wenye mikokoteni, wanafuga mifugo barabarani na madereva ndio wanasababisha ajali, na sio bodaboda wala bajaj peke yao,” alisema Lugola.

Lugola amesema hakuna mahali popote ambayo tumesema baodaboda wakifanya makosa wasikamatwe, tunachosema na kusimamia nikupunguza umaskini kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo inaelekeza Bodaboda na Bajaj wafanye biashara ili wapunguze umaskini.

  Aidha, Lugola amesema Serikali ya Magufuli inataka wananchi Watanzania wajiajiri hivyo sekta ya bodaboda lazima iheshimika kwakua nao wanatafuta ridhiki kama ilivyo kwa watanzania wengine.

Majeruhi wengine wa ajali ya moto Morogoro wafariki dunia

0
0
Majeruhi wengine wawili kati ya 13 waliokuwa wanatibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kutokana na ajali ya moto ya Mjini Morogoro, wamefariki Dunia na mpaka sasa jumla ya vifo imefikia 104.

Akizungumza leo Jumapili Septemba 1, 2019, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa MNH, Aminiel Aligaesha amesema Asha Ally Seleman (28) alifariki Jumatano iliyopita ya Agosti 28, 2019 na Avelina Pastory Aman (30) alifariki jana Jumamosi Agosti 31,2019.

Amesema majeruhi 11 ndio wamebaki hospitalini hapo kati ya 47 waliopokelewa tangu ajali hiyo ilipotokea ambapo 36 wamefariki.

Aligaesha amesema kati ya majeruhi 11 wanaoendelea kutibia MNH sita wapo wodi 22 ya Sewahaji na watano wako Chumba cha ungalizi maalum (ICU).

Lukuvi Ataka Wakuu wa Mikoa Kuharakisha Uanzishaji Ofisi Za Ardhi Za Mikoa

0
0
Na Munir Shemweta, WANMM TANGA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka Wakuu wa mikoa nchini kuhakikisha wanaharakisha uanzishwaji Ofisi za Ardhi za mikoa ili kusaidia upatikanaji huduma za ardhi katika mikoa hiyo.

Lukuvi alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mkoani Tanga wakati alipokagua ofisi zinazotarajiwa kuwa za ardhi katika mkoa huo ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa la kuanzisha ofisi za ardhi kila mkoa kwa ajili ya kusogeza huduma za ardhi kwa wananchi.

Katika Mkutano wa Wataalamu wa sekta ya ardhi uliofanyika hivi karibuni jijini Dodoma Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitangaza kuanzisha ofisi za ardhi katika kila mkoa ili kurahisisha huduma za sekta hiyo ambapo sasa zinapatikana katika Kanda tisa ikiwemo ile Maalum ya Morogoro.

Lukuvi alisema, uharakishwaji uanzishaji ofisi za ardhi katika mikoa utasaidia wananchi kupata huduma za ardhi katika mikoa yao tofauti za sasa ambapo hulazimu baadhi yao kutembea umbali mrefu kufuatilia nyaraka ofisi za kanda jambo aliloeleza linawakatisha tamaa.

Alimpongeza mkuu wa Tanga Martine Shighela kwa kuwa Mkuu wa mkoa wa kwanza kukubali na kupokea agizo la kuanzishwa ofisi hizo za ardhi mapema kwa lengo la kuhakikisha migogoro ya ardhi inaondolewa katika mkoa wake.

Alisema, pamoja na uwepo ofisi za Kanda ambazo baadhi yake zinahudumia zaidi ya mikoa miwili lakini kero kwa wananchi kuhusiana na masuala ya ardhi zinaendelea ndiyo maana Wizara yake imeona ianzishe ofisi za mikoa zitakazokuwa zikitoa huduma kama zile zinazotolewa katika kanda.

Alizitaja huduma hizo kuwa ni Upimaji, Uthamini, Mipango Miji, Usajili na Utoaji Hati za ardhi aliloueleza kuwa ulikuwa ukipatikana ofisi za kanda pekee jambo lililokuwa likiwalazimu wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo na kufafanua kuwa, uwepo ofisi za mikoa utaongeza ari ya wananchi kuchukua hati kutokana na ukaribu wa ofisi.

‘’Mtu atoke Korogwe afuate hati Moshi, trend ya kuchukua hati inapungua kutokana na umbali maana maeneo mengine mtu anavuka mikoa miwili kwenda kuifuata Hati na Kamishna aliyeko Moshi ni vigumu kusimamia mikoa iliyo mbali’’ alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, binafsi alitaka mikoa yote 26 kuanzisha ofisi za ardhi za mikoa kufikia Oktoba mwaka huu na Hati zitolewe katika mikoa hiyo jambo alilolieleza kuwa litapunguza kero na kuongeza wigo mpana wa makusanyao ya kodi ya pango la ardhi.

Lukuvi alibainisha kuwa, baada ya kuanzishwa ofisi za mikoa sasa ramani zote na historia ya masuala ya ardhi katika mikoa husika zitarudi katika ofisi hizo na Wakuu wa Mikoa hawatakosa msaada katika masuala ya ardhi kwa kuwa watalaamu wa ardhi watakuwa wakifanya kazi chini yao.

Kabla ya kukagua ofisi hizo Waziri Lukuvi alielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shighela kuwa, mkoa wake ulipokea kwa shauku kubwa uamuzi wa Serikali kuanzisha ofisi za ardhi katika mikoa na tayari umeshatenga ofisi hizo kwa ajili ya kuanza kazi ili kupunguza migogoro ya ardhi pamoja na kusogeza huduma karibu kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daud Mayeji alisema, uanzishwaji ofisi ya ardhi katika mkoa wa Tanga utausaidia sana mkoa huo kwa kuwa wamekuwa wakitumia muda mwingi kushughulika na masuala ya ardhi na hufanya zaidi ya safari 50 katika kipindi cha miezi mitatu kufuata huduma ya ardhi katika ofisi za kanda zilizoko Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Jiji la Tanga, uwepo wa ofisi za Ardhi za Mikoa itakuwa rahisi kwa jiji lake kushughulika na masuala mengine badala ya kujikita katika ardhi pekee suala alilolieleza lilikuwa likichukua muda mwingi.

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

0
0

Super nzoka  IKEMEKO   TRDITONAL clinic ;

Ni dawa ya Asili  iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 
 
Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji  ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 .
 
Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0789289945.Au whasap/0716343218 TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya mustang

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani Aagiza Msimamizi Wa REA Aondolewe

0
0
Na Zuena Msuya, Morogoro,
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, ameagiza Afisa aliyekuwa akisimimamia Mradi wa Umeme Vijijini (REA), Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Seif Abdallah, aondolewe kwenye nafasi hiyo kutokana na utendaji kazi usioridhisha.

Aidha Dkt. Kalemani ametoa siku 20, kwa Kampuni ya Ukandarasi ya State Grid inayotekeleza mradi huo kuwasha umeme katika vijiji vya Wilaya ya Ulanga la sivyo atakatwa asilimia kumi ya malipo yake kutokana na kazi hiyo.

Dkt.Kalemani alitoa kauli hiyo Agosti 31,2019, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa REA na kuwasha umeme katika Vijiji vya Makanga na Idunda wilayani Ulanga, mkoani Morogoro.

Waziri wa Nishati alifikia hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na usimamizi unaofanywa na mhandisi huyo kutoka Wakala wa Nishati Vijiji ( REA) pamoja na utekelezaji wa mradi usioridhisha.

“Huyu Mhandisi Seif Abdallah, utendaji wake wa kazi hauridhishi kabisa, hayupo katika maeneo ya kazi yanayotekelezwa mradi, anamuacha mkandarasi afanye kazi anavyojitakia yeye mwenyewe hakuna usimamizi wowote, ninamuagiza Mkurugenzi wa REA amuondoe huyu mhandisi hafai kuwa msimamizi”,alisisitiza Dkt.Kalemani.

Katika hatua nyingine, Dkt.Kalemani alitoa siku 20 kuanzia, Septemba 1 hadi 20, 2019 kwa kampuni ya ukarandari ya State Grid kuwasha umeme katika vitongoji vinne kabla ya kukamilisha Mradi wa REA awamu ya tatu, mzunguko wa kwanza unaotarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu nchini kote.

Alifafanua kuwa, utekelezaji wa Mradi wa REA awamu ya tatu umegawanyika katika mizunguko miwili ambayo ni mzunguko wa kwanza ulioanza kutekelezwa mwezi Juni, 2019 na utakamilika Desemba mwaka huu.

Aidha mzunguko wa pili wa REA awamu ya tatu unatarajiwa kuanza mwezi Januari na kukamilika mwezi Juni ,2020, hivyo alimtaka kila mkandarasi aliyepew kazi ya kutekeleza mradi huo ahakikishe anakamilisha mzunguko wa kwanza wa kazi yake kwa mujibu wa makubaliano ya mikataba na sheria.

Alisisitiza kuwa haridhishwi na hatua ya utekelezaji wa mradi huo katika Mkoa wa Morogoro ambao mpaka sasa umefikia asilimia 56 tu ya utekelezaji wake ambao hauendani na kasi ya utekelezaji wa mradi huo.

Sambamba na hilo alimtaka mkandarasi huyo,kuongeza nguvu kazi ya makundi ya vijana ili kuharakisha shughuli za utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza kama ilivyoelekezwa katika mkataba wa kazi hiyo.

“Sitakubali kukwamishwa na ninyi State Grid katika utekelezaji wa mradi huu kwa kuwa mnafanya kazi kwa kusuasua sana kasi yenu hairidhishi kabisa, na nyie ndiyo mko nyuma kabisa katika kasi ya kutekeleza mradi wa huu REA awamu ya tatu, mzunguko wa kwanza ikilinganishwa na wakandarasi wote wanaotekeleza miradi hii nchini, kama hamtatimiza makubaliano ya mkataba, tutawakata asilimia 10 ya malipo yenu”, alisema Dk.Kalemani.

Hata hivyo, Dkt.Kalemani alirejea kauli yake ya kuwataka wananchi kuwa wasinunue miundombinu ya umeme kama vile nguzo, pamoja Luku kwa kuwa vifaa hivyo vinatolewa bure kwa kila mwananchi aliyepitiwa mradi wa umeme vijijini.

Pia aliwataka wananchi kutumia umeme kwa faida kama vile kuongeza thamani ya mazao kwa kufanya usindikaji wa mazao yao ili kujiletea maendeleo zaidi.

Serikali imetenga shilingi Bilioni 42 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa REA awamu ya tatu, mzunguko wa kwanza kwa Mkoa wa Morogoro.

Vivutio vya Utalii vya Tanzania Kuanza Kuonekana Baidu Septemba Hii

0
0
Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Tanzania imeelekeza juhudi zake katika kuvutia watalii hasa wale kutoka nje ya nchi na ikilenga zaidi kuliteka soko la china lenye watu wengi duniani, ambapo kwa siku za karibuni Bodi ya utalii Tanzania ilifanya ziara kubwa ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika Miji ya Beijing, Shanghao, Chengdu, Guangzhuo, Hong Kong, Najing na Changsha.
 
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa Boti ya Utalii Tanzania (TTB) Jaji Thomas Mihayo, alisema kuwa matunda ya Ziara nchini China sasa yameanza kuonekana kwa kitendo cha kampuni ya Baidu kuja nchini kufanya mradi wa upigaji picha jongevu na mnato wa vivutio vya utalii Tanzania ili kuweza kuvitangaza katika mtandao huo wenye wafuasi zaidi ya milioni 700.
 
“Matunda ya ziara iliyofanyika katika Miji ya China yameanza kuonekana ambapo safari hii timu ya wataalam 11 kutoka katika kampuni kubwa za kimtandao nchini humo (Baidu) waliwasili nchini tarehe 22 Agosti ,2019 na kutembelea baadhi ya maeneno ya vivutio vya utalii hapa nchini kwa lengo la kupata picha jongevu na mnato ili kutangaza vivutio hivyo kwenye soko la utalii wa zaidi ya watu milioni 700 wanaoufuatilia mtandao huu wa Baidu”, Alisema Jaji Mihayo.
 
 China ni moja ya nchi duniani ambao wanatumia mtandao wao wa baidu, kwa hiyo ni dhahiri kuwa utengenezaji wa makala na picha mbalimbali walizopata kutoka katika vivutio hapa nchini vitaweza kuongeza watalii kutoka China kwani picha hizo zitaonekana kwa watumiaji zaidi ya milioni 700 wa mtandao huo.
 
 Aliongeza kuwa lengo la TTB ni kuiwezesha sekta ya utalii kupata watalii wengi kutoka China na kuongeza idadi ya watalii wa kigeni wanakuja kuitembelea Tanzania kutokana na kuona vivutio vitakawekwa  kwenye mradi huo wa Wander Planet kutoka katika  kampuni ya BAIDU, kuanzia Septemba 2019 na kuendelea.
 
Mihayo alisema kuwa kati ya nchi saba duniani Tanzania imeibuka kuwa nchi ya kwanza katika Mradi huo na ndiyo nchi pekee kutoka bara la Afrika na nchi zingine zinazolengwa na mradi huo ni kutoka mabara ya Amerika, Asia na Ulaya.
 
Wakiwa nchini wataalam hao wa mambo ya Picha jongevu na picha mnato walipata wasaa wa kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii nchini ikiwemo Mji wa kihistoria Bagamoyo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Makumbusho ya Oldvuai Gorge, Hifadhi ya Taifa Serengeti, ziwa Manyara, Mji wa Mwanza na Zanzibar. Na maeneo hayo yote yamechukuliwa picha ili kuweza kutangazwa katika mtandao huo mkubwa wenye wafuasi milioni 700 nchini China.
 
Aidha, Jaji Mihayo alisema kuwa lengo la ziara ya wataalam hao ni kupiga picha jongevu na mnato na kuandika taarifa za vivutio mbalimbali vya utalii katika maeneo waliyotembelea na kisha kuziweka kwenye mtandao wao, na wameahidi kutekeleza kama walivyolenga katika kutangaza utalii wa Tanzania nchini China ambapo baadhi ya taarifa za Shirika la Utalii Duniani(UNWTO) zinaeleza jinsi China ilivyo na soko kubwa la utalii Duniani.
 
“Takwimu za Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) zinaonesha kuwa China ni nchi ambayo ina soko kubwa la utalii duniani, mwaka 2018 wachina Milioni 130 walisafiri nje ya nchi huku Tanzania ikipokea watalii 32,773 idadi ambayo ni ndogo ukilinganisha na idadi ya watalii hao kutoka China kwenda nchi zingine, kwa hiyo juhudi hizi zinafanyika ili kuliteka soko la China kwenye sekta hii muhimu” Alisema Jaji Mihayo.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi alisema kuwa kampuni ya Baidu kutoka China imefanya vyema kuwaleta wataalam hao ili kutekeleza kazi ya kupiga picha jongevu na mnato na kuweza kutangaza utalii wa Tanzania nchini China kwenye soko la watu milioni 130 wanaotoka nje ya nchi kwenda kutalii sehemu mbalimbali Duniani.
 
“Tunaishukuru kampuni ya Baidu kutoka China kwa kuwaleta wageni hawa, kwani wameona na walichokiona kinatosha kabisa kwenda kukieleza nyumbani kwao China, Tanzania tuna vivutio vingi sana kwa hiyo picha na video zilizopigwa kwenye  vivutio ambavyo kila mtu duniani anatamani kuviona na kuitembelea Tanzania zitasaidia kuleta watalii wengi kutoka China ”, alisema Mdachi.
 
Naye kiongozi wa msafaro huo Bibi Jin Xiaping,  alisema kuwa  kampuni ya Baidu imefanya kitu muhimu kwa kuwaleta wataalam hao, kwani  wamekuja Tanzania ili kuona jinsi gani wataweza kutekeleza mradi huo(Wonder planet) kupiga picha jongevu na mnato na sasa wamefanya kazi yao, kwa hiyo kuanzia Septemba hii wataweza kuweka kwenye mtandao wao wa Baidu na kutangaza uzuri wa Tanzania kwenye soko la utalii China.
 
“Wataalam hawa 11 kila mmoja anazaidi ya wafuasi milioni mbili kwenye mitandao ya kijamii, kwa hiyo wamepiga picha jongevu, mnato na wataandika makala mbalimbali ili kuziweka kwenye mitandao yao na kuwezesha wafuasi wao kufahamu vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania”,Alisema Xiaping 
 
Mwisho
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images