Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

VIDEO: Rais Magufuli apokea hati za utambulisho wa balozi wa zimbabwe nchini tanzania

$
0
0
Balozi mteule wa Zimbabwe nchini Tanzania, Meja Jenerali Anselem Nhamo Sanyatwe, amekabidhi hati za utambulisho kwa Rais Magufuli leo Agosti 29 Ikulu Jijini Dar es Salaam

Waziri wa viwanda: Serikali imeondoa kodi kero 54 kwa wafanyabiashara

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema serikali imefuta kodi kero  54 kwa wafanyabiashara pamoja na kupunguza mamlaka za kutoa leseni za biashara .

Bashungwa ameyasema hayo mjini Makambako mkoani Njombe wakati akizungumza na wafanyabiashara kutoka mikoa zaidi ya 7 nchini waliokutana  mjini hapo kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya biashara na kuja na maazimio ya kuiomba serikali kupunguza utitili wa kodi,tozo na leseni kwa wafanyabiashara ili kunusuru sekta hiyo ambayo imetajwa kuwa katika hali mbaya kimaendeleo kwa sasa.

“Kuna kodi 54 zimeishaondolewa na ili nisiseme tu 54 mheshimiwa mwenyekiti wenu nimeisha mkabidhi hizo kodi kero 5”alisema Bashungwa

Awali wakizungumzia changamoto hizo wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka mikoa ya Tanga, Dar es salaamu,Mbeya,Songwe, Ruvuma, Iringa,Njombe na Katavi wamesema hali ya biashara nchini imezidi kuwa ngumu kwasababu kumekuwa na mrundikano wa tozo na ushuru kutoka mamlaka mbalimbali ikiwemo TRA,Halmashauri na nyinginezo hatua ambayo inawafanya watu wengi kufunga biashara zao.

Amani Mahellah,Sifael Msigala na Ismail Masoud ni baadhi ya wawakilishi walitoa maoni yao katika mkutano huo mkubwa wa wafanyabiashara nchini ambapo wamemuomba waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa kuhakikisha anakutana na wizara zote zinazomgusa mfanyabiashara katika majukumu yake ili kuzitafutia ufumbuzi changomoto hizo kwa ustawi wa sekta ya biashara na taifa kwa ujumla.

“Hizi taasisi zinazokusanya kodi za serikali zikutane kwa pamoja na wafanyabiashara ili kila mtu ajue kwa mfanya biashara yule anachukua shilingi ngapi”alisema Amani Mahellah mmoja wa wafanyabiashara

Akifafanua kiini cha kusuasua kwa sekta ya biashara nchini katibu mkuu wa jumuiya ya wafanyabiashara JWT Abdallah Mwinyi amesema kuwepo kwa urasimu mkubwa bandarini kunawafanya kutengeneza mianya ya rushwa huku  kamishna wa TRA nchini Edwin Mhede akimtaka kila mfanyabiashara kuviripoti vitendo vyote vya rushwa kwani vinaikosesha nchini Mapato.

“Forodha aangaliwe kwa makini nap engine sheria zibadilishwe kwenye udhaminishaji na uondoshaji mizigo bandalini” alisema Abdallah Mwinyi

Katika mkutano huo wizara nne zenye mahusiano ya karibu na wafanyabiashara zimealikwa ikiwemo ya viwanda na biashara ,tamisemi, fedha na uwekezaji.

Wizara Ya Uchukuzi Yaanza Kukusanya Maoni Ya Wadau Kujadili Rasimu 8 Za Kanuni Za Usafirishaji.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Wizara ya ujenzi , uchukuzi na mawasiliano imeanza kukusanya maoni kutoka kwa wadau wa usafirishaji  wa Ardhini nchini,  maoni yatakayosaidia kuboresha rasimu nane za kanuni  zilizoandaliwa na wizara hiyo zitakazo saidia kuondoa baadhi ya vikwazo vya usafiri wa Ardhini.
 
Akizungumza jijini Dodoma Agosti 28,2019   wakati akifungua kikao hicho kilichowahusisha wadau wa uasafirishaji pamoja na mamlaka ya uasafiri wa ardhini LATRA ,katibu mkuu wa  uchukuzi Dkta Leonard Chamriho amewataka wadau hao kuwa huru katika kutoa maoni yao yatakayosaidia kuleta matokeo chanya katika sekta ya usafirishaji wa Ardhini.

Mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti usafirishaji ardhini (LATRA) Gerald Ngewe amesema kuwa  maoni ya wadau ni muhimu katika urekebishaji wa sera na sheria katika sekta hiyo.
 
Hata,hivyo amezungumzia  kifungu cha kanuni ya 10 juu ya Masharti ,ambapo yanamtaka mtumiaji wa vyombo vya usafiri kutotumia vilevi,kuvaa sare safi,kutoruhusu watu kufanya biashara ndani ya basi ,kutozidisha abiria pamoja na kuzingatia ukomo wa mwendo kasi.
 
Nao baadhi ya Wadau wa Usafiri hapa nchini wamesema ni vyema LATRA ikajikita zaidi katika utoaji wa elimu kwa wadau.

Waganga Wakuu Wa Mikoa Watakiwa Kushirikiana Na Viongozi Wa Vijiji Kuhakikisha Kila Mwezi Wanaingiza Kaya Mpya 31 Katika CHF

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
NAIBU katibu mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya dokta DOROTHY GWAJIMA amewataka waganga wakuu wa mikoa kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji nchini kuhakikisha kila mwezi wanaingiza kaya mpya 31 za mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa(CHF).
 
Dokta GWAJIMA amesema hayo alipotembelea Zahanati ya kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino mkoani Dodoma kushuhudia namna ambavyo Zahanati hiyo imeweza kuandikisha idadi kubwa ya kaya katika mfumo huo.
 
Amesema zahanati hiyo ipo kijijini umbali wa km 90 lakini imeweza kuandikisha kaya 315 sawa na asilimia 63.
 
Azma ya serikali ni  kutengeneza mfumo wa bima ambao mwananchi atatambuliwa na pesa anayochangia itarudi kwenye kituo kama anavyoeleza meneja mradi wa HPSS Tuimarishe afya ALLY KEBBY.
 
Kwa upande wake mratibu wa CHF iliyoboreshwa mkoa FRANCIS LUTALALA amesema ili kupata mafanikio ni lazima uwepo ushirikiano baina ya viongozi.
 
Naye Muuguzi wa Zahanati hiyo SHIJA MAKEJA anaeleza siri kubwa ya mafanikio waliyoyapata kuwa  ni ushirikiano waliouweka baina yao na viongozi wa serikali ya kijiji.
 
Hadi kufikia agosti mwaka huu jumla ya kaya elfu 23,114 kati ya kaya laki 447,773 za mkoani hapa zimejiunga na CHF iliyoboreshwa huku uhamasishaji Zaidi ukiendelea kutolewa kwa kaya zote kuona umuhimu wa kujiunga na CHF iliyoboreshwa.

Ni Nini Kinachosababisha Wanaume Wengi Kuishiwa Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanaume kuishiwa nguvu kiume na maumbile madogo.

Nini kinasababisha upungufu wa nguvu za kiume  (1) Msongo wa mawazo( 2) magonjwa ya sukari,presha,vidonda vya tumbo,kukosa choo,na tumbo kuunguruma( 3) kujichua kwa muda mrefu   (4) ngiri ,korodani kuvimba,

Tiba ya tatizo:
MAJINJAS;  ni dawa  yenye virutubisho na mchanganyiko wa wa mizizi tisa (9) dawa hii hutibu matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo -dawa hii itakupa uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu ( 2) kuwahi kufika kileleni dawa hii itakupa uwezo wa kuchelewa ( 3)  dawa hii hutibu tatizo la maumbile ya kiume kusinyaa hasa kwa wanaume  waliojichua kwa muda mrefu  

MTINJETINJE; ni dawa ya kisukari ambayo imechanganywa na mizizi na mbegu -dawa hii husaidia kurejesha kongosho kwenye hali yake ya kawaida.

Fika ofisini kwangu MBAGARA ZAKHEMU KARIBU NA BENK YA  KCB utaona bango limeandikwa NTUNZU HEBRISRI CLINIC na mwanza yupo wakala nipigie simu whasap  0783185060. 0620113431 DR AGU na utaletewa popote uduma  hii

Kiwanda Cha Kuchakata Muhogo Mkuranga Kuondoa Tatizo La Ukosefu Wa Soko Kwa Wakulima

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
Muhogo uliokuwa ukiozea mshambani na kukosa soko la uhakika wilayani Mkuranga na maeneo mengine mkoani Pwani ,sasa unakwenda kupata soko la uhakika katika kiwanda cha kuchakata mhogo kilichopo Mkenge kata ya Veta wilayani hapo.
 
Inadaiwa kwamba ,uzalishaji wa muhogo mkoani humo ni tani 900,000 hadi milioni 1.2 hivyo kuna kila sababu uzalishaji ukaongezeka ili kunufaika na kiwanda hicho.
 
Akihimiza kilimo hicho ,mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo ambae anaendelea na ziara yake ya awali ya kuweka mawe ya msingi katika baadhi ya viwanda ,alisema soko la muhogo lilikuwa duni na wakulima walikuwa wakilima kwa wingi bila kupata faida.
 
“Kiwanda hiki kitatoa ajira,pia bei ya mhogo itakuwa yenye tija kwakuwa watatumia kupima kwa mzani, kwasasa bei haitabiliki ikiwa lumbesa 60,000 hadi 80,000 ,suzuki 300,000 ambapo kwa hali hiyo ni bei inayomlalia na kumnyonya mkulima huyu wa Mkuranga”alifafanua Ndikilo.
 
Hata hivyo alieleza ,moja ya malengo ya ziara yake ni kudhihirisha Pwani inakwenda kuwa ukanda wa viwanda pamoja na kuithibitishia Dunia kwamba Tanzania ni eneo linalovutia kwa viwanda.
 
Nae mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ,mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno alimuelekeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo na wataalamu wa kilimo waende vijijini kutoa elimu juu ya kilimo cha kisasa.
 
“Tumejifunza kupitia zao la korosho ,sasa mazao yote yaliyopata dawa ya kumkomboa mkulima yatolewe elimu kwa wakulima husika”alisisitiza Maneno.
 
Awali mhasibu wa kiwanda cha Tanzania Huafeng agriculture development Ltd,Leonard Jabee ,alieleza kiwanda kinamilikiwa na wachina ,kilianza ujenzi march 2019 na utakamilika mwishoni mwa mwaka huu,utagharimu bilioni 9.1.
 
Alielezea, wataanza kutengeneza vipande vya mhogo na kisafirisha China kisha kuzalisha wanga na kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 200 kwa siku kupitia Amcos za wakulima huku wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme.
 
Meneja wa Tanesco wilayani Mkuranga, Octavian Mmuni alisema , mwekezaji aliomba tariff II ,mkandarasi ameanza kazi ya kutandaza nyaya na nguzo lakini kazi haijakamilika.

Rais Magufuli Ahutubia Mkutano Wa Sita Wa Jukwaa La Uongozi Afrika Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja, alipowasili kuhutubia Mkutano wa sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Nigeria Jenerali Olusegun baada ya kuhutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi wastaafu katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Taasisi ya Uongozi baada ya kuhutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Somalia Mhe. Hassan Mohamed alipowasili kuhutubia Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019. Wanaofuatia kulia kwake ni Rais Mstaafu wa Nigeria Jenerali Olusegun Obasanjo, Rais Mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mhe. Thabo Mbeki na Mfanyabiashara mashuhuri wa Tanzania Bw. Ally Mufuruki

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na viongozi wastaafu kukiliza majadiliano wakati wa Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019.

Serikali Yasema Ina Nia Thabiti Kushirikiana Na Wadau Wa Tasnia Ya Nafaka Kukomesha Changamoto

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ina nia njema kabisa ya kuhakikisha kuwa inashirikiana na wadau wote katika kuhakikisha kuwa tasnia ya nafaka inaendelea na kuondoa changamoto zinazojitokeza.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 29 Agosti 2019 wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano JNICC Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa, Serikali peke yake, haiwezi kuziondoa changamoto hizo bila wafanyabiashara, wasindikaji na wasafirishaji kushirikiana na Serikali.

Katika mkutano huo waziri Hasunga amezitaja fursa zilizopo kwenye tasnia ya Nafaka kama ambazo ni pamoja na eneo linalofaa kwa kilimo ambalo linakadiriwa kuwa hekta milioni 44. Kati ya hizo, hekta milioni 29.4 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Eneo hilo, linafaa kwa kilimo cha mazao yote ya biashara na chakula, yakiwemo mazao ya nafaka kama mahindi, mtama, mpunga, ngano na mengineyo.

Fursa nyingine alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati, inajitahidi sana kufikisha umeme vijijini ambako ndiko nafaka zinapatikana. Hadi sasa asilimia 70 ya vijiji nchini, vimepatiwa umeme. Umeme huo unatakiwa utumike pia katika eneo la usindikaji. Hadi sasa, sehemu ndogo ya maghala kwenye usindikaji wa mpunga na mahindi kupitia mashine za kukoboa mpunga na mahindi.

Mhe Hasunga alisema kuwa Kuna baadhi ya maeneo, maghala mazuri yamejengwa  kwa usimamizi wa Serikali ili kuwa na uhifadhi mzuri wa nafaka. Mfano, maghala mengi yaliyojengwa wakati wa BRN bado hayajaweza kutumika ipasavyo.

Alisema Nchi yetu ina ikolojia tofauti tofauti, hali hii inasababisha baadhi ya maeneo kuwa na mvua za kutosha, na maeneo mengine kuwa na uhaba wa mvua. Maeneo yanayopata mvua za kutosha huzalisha chakula cha kutosha pamoja na ziada. Kwa maeneo ambayo yamezalisha ziada, wanayo fursa nzuri ya kupeleka ziada hiyo kwenye maeneo mengine ambayo hayazalishi vizuri.

“Vilevile, nchi yetu imezungukwa na nchi ambazo hazina fursa kubwa ya kilimo kama tuliyonayo. Miongoni mwa nchi hizo ni kama Uganda, Kenya, Congo, Sudan na nyinginezo. Hii ni fursa nyingine ya soko kwani tukizalisha vizuri, uhakika wa soko la nje, ni mkubwa pia” Alikaririwa Mhe Hasunga

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amezitaja mada zitakazojadiliwa katika mkutano huo kuwa ni pamoja na Fursa ya biashara ya mazao ya nafaka katika soko la Afrika na uwezo wa Tanzania kuzalisha nafaka na wafanyabiashara kushiriki kikamilifu, Upotevu wa mazao ya nafaka baada ya mavuno, mkakati wa Taifa wa kudhibiti na matokeo ya utafiti wa hali ya maghala yalivyo hapa nchini, Uongezaji thamani katika mazao na kuboresha mazingira ya biashara ya nafaka na Mfumo wa masoko na uzoefu.

Alisema kuwa mada hizo zitatoa nafasi pia ya kuelewa vizuri tasnia ya nafaka ili kuwa na maazimio ambayo yatajibu changamoto mbalimbali hususani ya upatikanaji wa taarifa na utumiaji vizuri wa fursa zilizopo katika tasnia hiyo.

“Nitoe rai kwa washiriki wote, tusikilize kwa makini, tuwe wawazi, na kwa uhuru tujadili mada hizo kwa mapana na marefu, ili baada ya siku mbili hizi, tutoke na maazimio yatakayojibu changamoto za tasnia hii ya Nafaka” Alisisitiza Mhe Hasunga

MWISHO

Ni Nini Kinachosababisha Wanaume Wengi Kuishiwa Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanaume kuishiwa nguvu kiume na maumbile madogo.

Nini kinasababisha upungufu wa nguvu za kiume  (1) Msongo wa mawazo( 2) magonjwa ya sukari,presha,vidonda vya tumbo,kukosa choo,na tumbo kuunguruma( 3) kujichua kwa muda mrefu   (4) ngiri ,korodani kuvimba,

Tiba ya tatizo:
MAJINJAS;  ni dawa  yenye virutubisho na mchanganyiko wa wa mizizi tisa (9) dawa hii hutibu matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo -dawa hii itakupa uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu ( 2) kuwahi kufika kileleni dawa hii itakupa uwezo wa kuchelewa ( 3)  dawa hii hutibu tatizo la maumbile ya kiume kusinyaa hasa kwa wanaume  waliojichua kwa muda mrefu  

MTINJETINJE; ni dawa ya kisukari ambayo imechanganywa na mizizi na mbegu -dawa hii husaidia kurejesha kongosho kwenye hali yake ya kawaida.

Fika ofisini kwangu MBAGARA ZAKHEMU KARIBU NA BENK YA  KCB utaona bango limeandikwa NTUNZU HEBRISRI CLINIC na mwanza yupo wakala nipigie simu whasap  0783185060. 0620113431 DR AGU na utaletewa popote uduma  hii

Simiyu Yaandaa Mkakati Maalum Wa Miaka Mitano Wa Mapinduzi Ya Kilimo Cha Pamba

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa  soko la pamba mkoa wa Simiyu umeandaa mkakati maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha zao hilo ili kujibu changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa Wadau wa Pamba uliofanyika uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,

Akifungua Mkutano huo Mtaka amesema upo umuhimu mkubwa kwa Mkoa wa Simiyu kuwa na kiwanda/viwanda vya kuongeza thamani ya zao la pamba ikiwemo viwanda vya nguo kama suluhisho la soko la pamba kwa wakulima.

“Kama hatutakuwa na viwanda vinavyoongeza thamani kwenye pamba,hata kama tukiongeza uzalishaji, itafika mahali tutatukanana tu, maana pamba itakuwa nyingi na hakuna mtu wa kukununua na wanaonunua wanajua hatuna kwa kuipeleka, kwa hiyo ni lazima tukubaliane na ndiyo maana tukasema tuje na mkakati huu unaoanza na mkulima kuanzia kwenye kulima” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema ili kuwasaidia wakulima katika upatikanaji wa mikopo ni vema benki zikaweka utaratibu rafiki wa kutoa mikopo kwa wakulima huku akitoa wito kwa Benki Kuu kupitia Kurugenzi ya Sera kuandika maandiko ya miradi ya mazao ya mikakati likiwemo pamba ambayo yatasaidia katika kuyaongezea thamani mazao hayo.

Akiwasilisha mkakati huo kwa wadau wa pamba mkoani Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi wa Mipango na Uratibu Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah amesema uongezaji thamani kwenye pamba mkoani Simiyu bado liko chini; ambapo kwa sasa kinachofanyika ni kutengenisha pamba nyuzi, mbegu na kuchuja mafuta, huku akibainisha kuwa matarajio ya mkoa ni kwenda kwenye hatua nyingine zaidi ya kuchambua pamba.

Pamoja na kuongeza thamani ya zao la pamba wadau wa pamba wametoa maoni mbalimbali katika kuboresha kilimo cha Pamba ili kiwe chenye tija na kubainisha kuwa “Ili tuweze kuboresha kilimo cha pamba ni lazima teknolojia zitakazokabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, wadudu na magonjwa” alisema Epifania Temu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) Ukiriguru

“Mbegu ndiyo msingi wa tija ya pamba inayopaswa kuzalishwa kwenye soko, hivyo kwenye eneo lililokubaliwa kuzalisha mbegu kama Meatu na Igunga ginners (wenye viwanda vya kuchambua pamba) watakaokununua pamba ya eneo wapewe jukumu la kuzalisha mbegu ili kuwa na mwendelezo wa mbegu bora” alisema Mkondo Cornelius Afisa Kilimo Mkuu, Wizara ya Kilimo.

Mkurugenzi wa Miradi kutoka Gatsby Africa, Samweli Kilua ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha kila mdau anatimiza wajibu wake katika kuhakikisha mkakati huo unatekelezwa kwa ufanisi katika kuboresha kilimo cha pamba.

Akifunga kikao Katibu Tawalawa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema mkakati wa mapinduzi ya kilimo cha pamba Mkoani Simiyu utatekelezwa kwa vitendo  na akazitaka  Taasisi za fedha, viongozi na wataalam wanaosimamia wakulima, vyama vya ushirika  na wadau wengine waanze mazungumzo ili mkakati huo utakapoanza kutekelezwa kuwe na uelewa wa pamoja kwa wadau wote.

Mkutano wa kuboresha mkakati maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha pamba ulijumuisha wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba ambao ni pamoja na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Simiyu, Watalaam wa kilimo kutoka Taasisi za Utafiti wa Kilimo, Wizara ya Kilimo, Halmashauri na Mkoa, Watendaji wa Taasisi za Fedha, viongozi  wa vyama vya msingi vya ushirika.

Taarifa muhimu kutoka Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam

$
0
0
Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam mnamo tarehe 25/08/2019 majira ya tatu na nusu usiku huko maeneo ya Pugu, lilifanikiwa kukamata silaha mbili aina ya Shortgun na bastola.


Katika ufuatiliaji alikamatwa mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la OMARY ATHUMANI @ DANGA MIAKA (39), mkazi wa mkuranga ambaye pia alikuwa anatafutwa kwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha, katika mahojiano ya kina mtuhumiwa alikiri kujihusisha na matukio mbalimba ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kuwa amewahi kufungwa miaka 30 na alitoka kwa rufaa na kujiunga na kundi lingine la ujambazi.

Mtuhumiwa huyo pia alieleza kuwa kuna wenzake watatu ambao anashirikiana nao pia wamepanga  wakavamie na kupora duka la M-pesa lililopo maeneo ya Pugu shuleni hivyo yuko tayari kuwapeleka Askari eneo la tukio, kikosi kazi wakiwa na mtuhumiwa waliweka mtego  na ilipofika muda huo eneo la Pugu washirika wake walijitokeza toka kwenye kichaka wanakoficha silaha  mara wakagundua kuwa wanafuatiliwa na askari  maeneo hayo ghafla majambazi hao walianza kurusha risasi kuelekea kwa Askari na mtuhumiwa alianza kupiga kelele na kujaribu kuwakimbia askari.

 Askari walijibu mapigo na walifanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu OMARI ATHUMANI, FULLSABA NA BABU SHOBO sehemu mbalimbali za miili yao na mmoja aitwaye DOGO SIDE alifanikiwa kukimbia kusikojulikana, majeruhi wote walikimbizwa hospitali ya taifa Mhimbili kwa matibabu lakini baada ya Daktari kuwapima alithibitisha kuwa wameshafariki dunia.

Baada ya upekuzi majambazi hao walipatikana na silaha mbili No. YA- 1547 aina ya SHORTGUN iliyo katwa kitako na mtutu, Ikiwa na risasi tatu, ganda moja la risasi na BASTOLA moja iliyo futwa namba ikiwa na risasi mbili  na maganda mawili(2) ya risasi.

Aidha silaha tajwa aina ya Shortgun ilibainika kuwa iliporwa tarehe 13.04/2019 saa nne na nusu usiku kesi ya unyang’anyi ilifunguliwa kituo cha Ukonga na silaha hiyo ilikuwa mali ya kampuni ya ulinzi iitwayo ALEMS SECURITY CO.LTD iliyopo njia panda Segerea Dsm na ilitumika kupora kiasi cha pesa Tsh 6,000,000/= huko MARKAZ Gongo la mboto kwa mfanyabiashara  aitwaye JUSTINE CHAULA, pamoja na simu 5 za aina mbalimbali.

Awali mtuhumiwa alikiri kuwa yeye na wenzake wamewahi kushtakiwa kwa makosa ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha zaidi ya kesi 6 ambazo zilikuwa mahakamani kabla ya kutoka kwa rufaa mwaka 2017.

Tukio lingine mwezi wa 6, 2019 walipora maduka ya M-pesa, Tigo pesa  maeneo ya mazizini Ukonga, mbezi juu wilaya ya ubungo  na walipora Tsh 800,000/= kwa mfanyabiashara wa mchanga, maeneo ya Machimbo wilaya ya Mkuranga. Pia polisi wilaya ya mkuranga ilifanya upekuzi nyumbani kwa marehemu OMARY ATHUMAN@DANGA na kufanikiwa kukamata risasi 7 za silaha aina ya Shorgun na jalada la shauri hili linapelelezwa.

Kikosi kazi kinaendelea na msako mkali ili kuhakikisha jambazi aliyetoroka kwenye eneo la tukio anakamatwa haraka na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Wananchi wazidi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuliweka jiji letu la Dar es salaam katika hali ya amani na utulivu ili raia wema waendelee kufanya kazi za kuinua kipato chao na taifa kwa ujumla.

Katika tukio la pili, Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa kumkamata jambazi mmoja aitwaye ELIA MATAYO KITULI (55) mkazi wa Kivule, wilaya ya Ilala jijini DSM aliyekuwa anatafutwa, Baada ya kukimbia kwenye tukio la ujambazi lililotokea tarehe  04/07/2019  ambapo majambazi wawili waliuwawa na kupatikana silaha mbili aina ya bastola huko Kitunda machimbo ambapo nilitoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Jambazi huyo alikamatwa akiwa na silaha moja aina ya Rifle yenye namba MK3-90893 ikiwa na risasi 3 ndani ya kasha(magazine) na vifaa mbalimbali vilivyoporwa maeneo mbalimbali kama ifuatavyo;
1. Ipad mbili aina ya Samsung na Apple
2. Smart phone nane(8) aina ya INFINX, Samsung, Nokia, Huawei, Techno na Iphone.
3. Saa moja ya mkononi aina ya Seiko 5 rangi ya dhahabu
4. Kisu kimoja
5. Digital camera moja aina ya Sony
6. Lap top moja aina ya Toshiba
7. Head phone moja na charger mbalimbali za simu

Mtuhumiwa aliendelea kuhojiwa kituo cha Polisi mara aliugua ghafla na kupelekwa hospitali ya taifa Muhimbili na baadaye alifariki dunia kwa maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.
 
Baadhi ya wahanga waliofanyiwa matukio ya uporaji wamefanikiwa kutambua vifaa vyao ambapo simu  2 aina ya Iphone na Samsung moja zilitambuliwa.

LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
29/08/2019

Usisumbuke Tena na Tatizo la Nguvu za Kiume....Soma hii

$
0
0
Super Mkunyati Mix; ni dawa bora ya mitishamba yenye uwezo wa kutibu na kumaliza matatizo yote ya ukosefu wa nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile:-
 
  -kuwai kufika kileleni ndani ya dakika chache tu.
 -Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa muda mrefu.
 -Kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu(punyeto) husababisha kuishiwa au kupungukiwa na nguvu za kiume.

Epuka matatizo haya kwa kutumia dawa bora ya asili ya Super Mkunyati Mix ni kiboko ya matatizo haya yanayowasumbua baadhi ya wanaume wengi.
 
Pia kuna dawa ya kutibu Presha,miguu kufa ganzi, tumbo kuuma chini ya kitovu, kisukari,ngiri, chango aina zote na nk, matatizo haya nayo uchangia matatizo haya ya ukosefu wa nguvu za kiume na kuwa na maumbile madogo na uume mfupi.
 
JABABILA;- ni dawa ya mvuto wa mapenzi ,mchumba, mke, mume aliyekuacha .
 
ITALIGULA;- ni dawa ya biashara  .

Ofisi zetu zinapatikana DAR ES SALAAM, SONGEA - BOMBAMBILI, SHINYANGA - KAHAMA MJINI. na pote pale ulipo utaipata huduma hii,kama huna nafasi utaletewa hulipo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na DR. MACHIMKENDA simu no, 0717 339 771AU 0763 172 670whatsApp 0621998653

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

Wizara Ya Afya Yaja Na Mfumo Wa Dharura Na Uokozi

$
0
0
Na Englibert Kayombo, WAMJW – Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara nchini TANROADS iko mbioni kuanzisha mfumo wa huduma za dharura na uokoaji katika barabara kuu nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa lengo namba tatu (AFYA BORA NA USTAWI) kati ya malengo 17 ya Malengo Endelevu ya Maendeleo  (SDG’s) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Kwenye ukumbi wa mikutano bungeni Jijini Dodoma.

Waziri Ummy Mwalimu amesema “mfumo huu una lengo la kusaidia kupambana na dharura au maafa pindi yanapotokea na kuweza kusaidia upatikanaji wa huduma kwa haraka na tutaanza na vituo 7 vya huduma za dharura katika barabara kuu toka Mkoa wa Dar Es Salaam mpaka Ruaha Mbuyuni Mkoa wa Iringa.

Amevitaja vituo vya huduma za dharura ambayo vitaanzishwa kuwa ni Kituo cha Afya Kimara (DSM), Hospitali ya Tumbi, Kituo cha Afya Chalinze (PWANI), Zahanati ya Fulwe (Mikese Morogoro), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Hospitali ya St. Kizito (Mikumi, Morogoro) pamoja na Zahanati ya Ruaha Mbuyuni Darajani (Iringa)

“Tumeweza kununua gari za kubebea wagonjwa (Ambulance) 12 ambazo tutazisamba katika vituo vya huduma za dharura” amesema Waziri Ummy na kuendelea  “bado tuna lengo la kuongeza magari matatu  ya uzimaji moto yenye uwezo wa kuinua na kukata vyuma ili kuwaokoa majeruhi na kuwapatia huduma eneo la tukio”

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa tayari watoa huduma 272 wamehitimu mafunzo ya huduma za dharura na uokoaji yaliyotolewa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi ambao kati yao, 1212 ni “basic provider” huku 160 ni watoa huduma ngazi ya Vijiji.

Akitoa maoni yake juu ya mfumo huo, Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Deo Ngalawa ameipongeza Wizara ya Afya kwa kuja na mfumo huo ambao utaokoa maisha ya watanzania wengi huku akitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuhakikisha kuwa mfumo huo unasambaa maeneo yote ya barabara kuu ili kusaidia upatikanaji wa huduma za uokozi kwa haraka zaidi.

Waziri Ummy amesema kuwa wameanza na eneo hilo kwanza kwakuwa limekuwa na athari za kutokea kwa ajali nyingi kulinganisha na maeneo mengine huku akisema kuwa huo ni mpango endelevu na wataendelea maeneo yote ya barabara kuu nchini huku akisema kuwa mfumo huo utazinduliwa mwishoni wa Mwaka 2019.

Waziri Lugola Afanya Mazungumzo Na Balozi Wa Canada Nchini.

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini, Pamela O’Donnel na kumuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.

Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Lugola, jijini Dar es Salaam, leo ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na ofisi ya Balozi huyo nchini.

Waziri Lugola alimuakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini.

“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.

Kwa upande wake Balozi Sara, alimshukuru Waziri Lugola kwa mazungumzo waliyoyafanya na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Canada na Tanzania.

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

$
0
0

Super nzoka  IKEMEKO   TRDITONAL clinic ;

Ni dawa ya Asili  iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 
 
Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji  ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 .
 
Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0789289945.Au whasap/0716343218 TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya mustang

RC Makonda Azindua Mpango Mkakati wa “PEKENYUA TUKUFUKUNYUE” Ili Kutokomeza wahamiaji haramu

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo August 29 amezindua Mpango Mkakati wa Kutokomeza Wahamihaji haramu Mkoa wa Dar es salaam alioubatiza jina la “PEKENYUA TUKUFUKUNYUE” na kuwaagiza Watendaji wa Mitaa kurejesha Daftari la Mkazi ili Kila Mkazi kuanzia ngazi ya Mtaa afahamike anapoishi na kazi anayofanya jambo litakalosaidia pia kuondoa uhalifu.

RC Makonda amesema mpango huo ni Mwarobaini tosha wa kupambana na Wageni wanaoishi Nchini kinyume na Sheria na utahusisha Watendaji wa Kata, Mitaa na Wananchi ambao watakuwa na jukumu la kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa mgeni au mtu wanaemtilia mashaka kwenye Makazi wanayoishi.

Aidha RC Makonda amesema uwepo wa Wahamihaji Haramu Nchini ni jambo la hatari kiusalama kwakuwa baadhi yao wanafanya uhalifu wa Wizi, Ubakaji, Uporaji, wanatumia rasilimali za nchi, wanatumia fursa ambazo zilipaswa kuwanufaisha wazawa ikiwemo Afya, Elimu na Ajira, kusababisha msogamano wa watu magerezani pamoja na kuwa Chanzo cha Migogo ikiwemo ya Ardhi.

Kutokana na hilo RC Makonda ameviagiza Vyombo Vyote vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Viongozi wa Kata na Mitaa kuhakikisha Mpango huo unafanikiwa kwa 100%.

Kwa upande wake Kamishina wa Uhamihaji Mkoa wa Dar es salaam amesema wamebaini idadi kubwa ya wahamihaji haramu wanatoka mataifa ya Burundi, DRC, Somalia na Ethiopia na wamekuwa wakipendelea kuishi Mkoa wa Dar es salaam kwakuwa umekuwa jiji lenye fursa nyingi za kibiashara.

Waziri Simbachwene Afungua Mkutano Wa 5 Wa Kisayansi Juu Ya Utunzaji Endelevu Wa Mazingira.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene ameziagiza Mamlaka zote za Serikali Nchini  kuanzia Mamlaka za Mikoa mpaka mamlaka za Vijiji kuweka utaratibu wa kutumia ardhi kwa ajili ya kuhifadhi misitu ili kuweza kutunza mazingira. 

Ameyasema hayo jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 5 wa Kisayansi juu ya utunzaji endelevu wa Mazingira ambapo alikua Mgeni Rasmi.
 
Amesema kuwa Elimu izidi kutolewa kwa Wananchi ili kuweza kupata uelewa zaidi juu ya maeneo ya uhifadhi wa misitu ambayo yametengwa.. 

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni Serengeti-Ngorongoro, Ziwa Manyara, East Usambara, Jozani Chwaka-Zanzibar na Gombe-Masito-Ugalla. 

Alisema kuwa maeneo hayo yametengwa kuwa maeneo ya hifadhi kwa sababu ya ikolojia na bayonuai iliyopo katika maeneo hayo. Kwa sasa maeneno hayo yanapata changamoto kwa kuvamiwa na shughuli za Binadamu hivyo kusababisha uharibifu katika maeneo hayo ya hifadhi.
 
Alisema kuwa ni vema kila  Mtanzania kujua umuhimu wa mazingira na hivyo kuweza kulinda na kuhifadhi maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi, na pale yalipoharibiwa basi parejelezwe kwani kwa kufanya hivyo ni kutunza mazingira.  
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George amefungua Mkutano huo wa 5 wa Kisayansi juu ya utunzaji endelevu wa Mazingira ambao umeandaliwa na Baraza la Usimamizi wa hifadhi ya Mazingira (NEMC) na umefanyika katika kumbi za Mikutano za AICC jijini Arusha.

Marufuku Kutoa Vitisho Kwa Watumishi Wa Serikali-mwenyekiti CCM Songwe

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Songwe Eliniko Mkola amewapiga marufuku viongozi wa Chama hicho Mkoani Songwe kutoa vitisho vya aina yoyote kwa Watumishi wa Serikali Mkoani hapa.

Mkola ametoa marufuku hiyo jana wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Songwe kilichoketi kupotea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Januari mpaka Juni 2019 ambapo taarifa hiyo ilipokelewa na kupitishwa.

“Liko tatizo la baadhi ya viongozi wa chama kusikiliza maneno na kutoyafanyia uchunguzi pia Wapo baadhi ya viongozi wa Chama hutishia viongozi wa Serikali, ni marufuku kwa vitendo hivyo kuanzia leo” amesisitiza Mkola.

Ameongeza kuwa taasisi zote zinafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo ni vema kujenga mazoea ya kuzisoma ili viongozi wa chama na wale wa serikai kila mmoja ajue mipaka yake ya utendaji kazi.

Mkola ametoa rai kwa viongozi wa chama na serikali kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuujenga Mkoa wa Songwe kwani wote wana nia moja ya kuhakikisha maendeleo yanapatikana Mkoani hapa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela amesema viongozi wa serikali waliopo hawana nia ya kuuharibu Mkoa wa Songwe hivyo viongozi wa chama wawatumie katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.

Brig. Jen. Mwangela ameongeza kuwa endapo viongozi wa chama wataona kuna mambo kwenye Mkoa au Halmashauri zao hayaendi vizuri wawasilishe masuala hayo kwa viongozi walioko Mkoani hapa ili yafanyiwe kazi na pia wajitahidi kuepuka misuguano isiyo ya lazima.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amesema Viongozi wa chama na Serikali wasioneane aibu kuelezana ukweli kuhusu mapungufu ya baadhi ya watendaji wa serikali kwani kufanya hivyo maendeleo ya Mkoa yatachelewa.

 

Ni Nini Kinachosababisha Wanaume Wengi Kuishiwa Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanaume kuishiwa nguvu kiume na maumbile madogo.

Nini kinasababisha upungufu wa nguvu za kiume  (1) Msongo wa mawazo( 2) magonjwa ya sukari,presha,vidonda vya tumbo,kukosa choo,na tumbo kuunguruma( 3) kujichua kwa muda mrefu   (4) ngiri ,korodani kuvimba,

Tiba ya tatizo:
MAJINJAS;  ni dawa  yenye virutubisho na mchanganyiko wa wa mizizi tisa (9) dawa hii hutibu matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo -dawa hii itakupa uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu ( 2) kuwahi kufika kileleni dawa hii itakupa uwezo wa kuchelewa ( 3)  dawa hii hutibu tatizo la maumbile ya kiume kusinyaa hasa kwa wanaume  waliojichua kwa muda mrefu  

MTINJETINJE; ni dawa ya kisukari ambayo imechanganywa na mizizi na mbegu -dawa hii husaidia kurejesha kongosho kwenye hali yake ya kawaida.

Fika ofisini kwangu MBAGARA ZAKHEMU KARIBU NA BENK YA  KCB utaona bango limeandikwa NTUNZU HEBRISRI CLINIC na mwanza yupo wakala nipigie simu whasap  0783185060. 0620113431 DR AGU na utaletewa popote uduma  hii
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images