Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Msemaji Mkuu wa Serikali Dr. Abbasi Aifunda TRC Misingi Minne Ya Kuutangaza Mradi Wa Reli SGR

$
0
0
Na.Paschal Dotto-MAELEZO
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi ametoa mafunzo kwa watumishi wa Shirika la Reli Tanzania TRC kuhusu umuhimu wa mawasiliano kimkakati katika miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali. 

Katika mafunzo hayo, Dkt.Abbasi amesema kuwa ili miradi mikubwa iweze kujulikana kwa wananchi, Taasisi husika zinapaswa kuzingatia misingi mikubwa minne katika kuandaa habari ili kuwahabarisha wananchi kuhusu miradi hiyo, akakumbusha; 

Katika kutekeleza ahadi zake kwa wananchi, Serikali ilitoa Fedha za utekelezaji wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) ambapo TRC inapaswa kutangaza mradi kwa wananchi, akasema, “kuna misingi minne ambayo inapaswa kutekelezwa ili kuwezesha mawasiliano ya kimkakati katika mradi huo ambao wananchi wanapaswa waujue”, Dkt.Abbasi.
Msemaji Mkuu huyo wa Serikali aliitaja misingi hiyo kuwa ni Maono katika kuwahabarisha wananchi (Pro-Active), akaeleza kuwa ili wananchi waweze kujua  kinachoendelea katika mradi wa ujenzi  wa reli ya kisasa (SGR),  TRC ambayo inakabidhiwa fedha nyingi za walipa kodi,haina budi kuonesha zinavyotumika. 

Msingi mwingine Dk. Abbasi ametaja kuwa ni  Ujumbe unaotolewa (Messaging) katika kutekeleza kufikisha ujumbe kwa wananchi, akasema,  TRC inapaswa kuwaeleza  wananchi kwa mahususi kuhusu mradi huo kuwa utakuwa na manufaa na faida gani kwa fedha zao. 

Akaongeza kuwa katika kuutangaza maradi huo, TRC wanapswa kuwa na mawasiliano baina ya wao na taasisi au wadau wao (Collaborations) ili hatimaye kubainisha kwa wananchi wayasemayo ili kuwezesha upatikanaji wa habari sahihi, hapa alisema wataalum katika kada mbalimbali kwenye Taasisi wanapaswa kushiriki kimkakati kutoa takwimu za kitaalamu kwa Afisa Habari ili aweze kuzinyambua kabla ya  kuzipeleka kwa wananchi au walengwa.  

Alitaja msingi mwingine ni kuweza kutanua wigo kwa kutumia Vyombo mbalimbali Kuhabarisha (Multi-Media) hii ni dhana ya kutumia njia nyingi za  habari, kuhabarisha wananchi  hasa mitandao ya kijamii,magazeti, radi na runinga, na kuwatumia wataalum wa kada ya Habari kwa kuandaa picha, Video na Graphics, kuandika habari na makala ili kurahisisha mtazamaji au msomaji kuelewa haraka kwa njia hizo na hivyo kuuelewa mradi wa SRG. 

“Taasisi za Serikali mnapaswa kuwekeza zaidi kwenye kitengo cha habari, ikiwemo kuwa na wataalamu mbalimbali katika kada hii, lakini mnatakiwa muwe hasa kwenye mitandao ya kijamii”  

Akaeleza kuwa nusu ya watu duniani wako kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa, na kwamba jitihada zinaendelea za kubadilisha Taasisi mbalimbali kutoka kutegemea gazeti la kesho badala ya pia kutumia mitandao ya kijamii ambako taarifa zinafika kwa haraka na kwa uhakika zaidi kwa watu wengi. 

Aidha, Dkt. Abbasi alitembelea ujenzi wa Stesheni mpya ya reli ya kisasa SGR ambapo alielezwa ujenzi wa reli unaendelea vizuri, na akawataka watanzania kuiunga mkono Serikali ili kutekeleza kwa pamoja ujenzi wa Reli hiyo na akasema,”reli hii itakuwa na manufaa kwa vizazi vya leo, kesho na vijavyo”. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu waTRC, Masanja Kadogosa alisema kuwa katika kutekeleza masuala ya kuwajuza wananchi kuhusu mradi huo, Idara ya Habari ni muhimu na amemshukuru Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO kuwatembelea na kuwapa darasa katika masuala ya mawasiliano kimkakati kwenye mradi wa SGR. 

“Siku zote tunasema huu ni mradi mkubwa sana ambao Serikali inautekeleza ndani ya nchi yetu, na wananchi hawa wakati wote wanahitaji kuhabarishwa manufaa ya mradi huu, kwa hiyo ujio wa Msemaji Mkuu wa Serikali kwetu sisi ni faraja ya kupata uzoefu mkubwa kwenye masuala ya Habari”, alisema Kadogosa. 

MWISHO

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya

$
0
0
KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili ZUNGU PAULO @ TINYA [45] na BARAKA LAZARO @ TIMOTHEO [40], wote wakazi wa Kijiji na Kata ya Lupa wakiwa na nyara za Serikali vipande vitatu [03] vya meno ya Tembo bila kibali.

Tukio hilo limetokea tarehe 19.08.2019 saa 20:00hrs katika Kijiji na Kata ya Lupa, Tarafa ya Kipembawe Wilaya ya Chunya. Thamani ya Nyara hizo bado kufahamika. Mbinu iliyotumika ni kuhifadhi pembe hizo kwenye mfuko wa Sandarusi na kutafuta wateja. Watuhumiwa hao ni wawindaji haramu. Taratibu za kisheria zinafanywa ili wafikishwe Mahakamani.

KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili IGELELE DANIEL [42] na NYIRENDA JOHN @ DAIMON [32], wote wakazi wa Kijiji cha Isangawana wakiwa na nyara za Serikali vipande kumi [10] vya meno ya Tembo bila kibali.

Tukio hilo limetokea tarehe 19.08.2019 saa 20:15hrs katika nyumba ya kulala wageni iitwayo UZUNGUNI chumba namba 113 iliyopo eneo la Sinjilili, Kata ya Itewe, Tarafa Kiwanja, Wilaya ya Chunya. Thamani ya Nyara hizo bado kufahamika. Watuhumiwa hao ni wawindaji haramu. Taratibu za kisheria zinafanywa ili wafikishwe Mahakamani.

AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA KUSABABISHA KIFO.
Jeshi la Polisi linamtafuta dereva mmoja ambaye alikimbia baada ya kutokea ajali na kusababisha kifo cha askari MT. 90399 CPL FRED GRAYSON @ MBALIZI [35] askari wa JWTZ Kikosi cha 44KJ – Mbalizi, mkazi wa Iwambi.

Tukio hilo limetokea tarehe 20.08.2019 saa 21:15hrs eneo la ZZK – Mbalizi, wilaya ya Mbeya Vijijini katika baraaaaaabara kuu ya Mbeya kwenda Tunduma. Katika tukio hilo marehemu alikuwa akiendesha gari ndogo T.219 CSU Nissan akitokea Songwe Airport kuelekea Mbalizi na kugongana uso kwa uso na gari kubwa T.838 APZ Scania Lori ambalo lilikuwa likitokea Mbeya mjini kueleka Tunduma hivyo kusababisha kifo chake papo hapo. Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo [marehemu] kujaribu kulipita gari linguine lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari. Jitihada za kumtafuta dereva ambaye alikimbia mara baada ya ajali zinaendelea. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali teule ya Ifisi.

OPERESHENI DHIDI YA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na operesheni na ukaguzi wa vyombo vya moto katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya vinavyokiuka sheria za usalama barabarani. Hivyo wamiliki wa Bajaji na madereva ni vyema wakafuata na kutii sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika. Zoezi hilo la ukaguzi na ukamataji wa vyombo vya moto kwa makosa mbalimbali ni endelevu katika mkoa wetu.

WITO:
Natoa wito kwa jamii kutoa taarifa katika mamlaka husika juu ya mtu/watu/kikundi au mtandao unaojihusisha na matukio ya ujangili ili hatua kali za kisheria dhidi yao zichukuliwe.
Imetolewa na :
[ ULRICH O. MATEI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Mpango Kazi Wa Uendelezaji Miji Kufanikisha Huduma Za Kijamii

$
0
0
Na. Josephine Majura, WFM, Dodoma
Serikali imezindua rasmi Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji Tanzania ili kuhakikisha nchi inakuwa na miji iliyopangwa na makazi yenye huduma zote za kijamii ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/17-2020/21.

Mpango huo umezinduliwa Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango kazi huo, Waziri Jafo alisema kuwa Serikali imejidhatiti kuandaa mipango miji madhubuti ambayo imezingatiwa katika miongozo ya kuandaa mipango ya taifa.

“Serikali inazindua rasmi Mpango huo ili kuleta mpangilio mzuri wa Miji wenye manufaa kwa Taifa na kufanya ukuaji wa miji kuwa mchakato wenye manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa nchi”, alisema Waziri Jafo.

Waziri Jafo alisema kuwa mpango huo umejikita katika maeneo manne ambayo ni matumizi ya lugha ya mpango kazi, suala la utawala na kanuni, mkakati wa fedha pamoja na kuchunguza njia za kukuza uchumi kwa kutambua njia ambazo zitachochea ukuaji wa uchumi katika viwango vya juu.

Alisema kuwa maeneo hayo manne ni muhimu kufanya ukuaji wa miji kuwa mchakato wenye manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa kuwa unatoa mapendekezo ya msingi kwa wakati ambayo ni muhimu kwa upangaji wa maendeleo ya miji nchini.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabula, alisema kuwa ukuaji wa miji ni suala pana ambalo linahitaji wadau wengi kuunganisha juhudi ili kuhakikisha ukuaji wa miji inayosimamiwa kikamilifu.

Dkt. Mabula amesema kuwa, wizara yake iko tayari kutoa ushirikiano katika kuleta pamoja jitihada za kila taasisi ili kuepuka jambo moja kufanywa na wadau zaidi ya mmoja, lengo likiwa kufanikisha malengo ya nchi iliyojiwekea. 

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adolph Ndunguru, aliwashukuru viongozi na wote waliohudhuria katika hafla hiyo muhimu kwa Taifa na kueleza kuwa mpango huo utasaidia kutatua changamoto za upangaji miji kwa maendeleo ya uchumi na Taifa kwa ujumla. 

Vilevile Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa kiuchumi na Kijamii, Dkt. Tausi Kida, amesema Mpango huo utasaidia katika uandaaji wa mipango ya kitaifa ya uendelezaji miji pamoja na uandaaji wa sera kwa kuwa uliotokana na utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii kwa kuwa uliofanywa kwa kufuata kanuni za kisayansi za ufanyaji tafiti.

MWISHO

Waziri Ummy Aipongeza WHO Kwa Kusaidia Kudhibiti Ebola Nchini Kongo

$
0
0
Na WAMJW- Brazzaville
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amelipongeza Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo kwa juhudi inazofanya kwa pamoja katika kudhibiti ugonjwa wa Ebola.

Waziri Ummy amesema hayo leo wakati akiwasilisha taarifa ya mkakati wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola katika mkutano wa 69 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaojumuisha Mawaziri wa Afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika unaoendelea jijini Brazzaville nchini Jamhuri ya Kongo.

Aidha, Waziri Ummy amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom kwa kutangaza Ebola kuwa janga la Kimataifa, na kuongeza kuwa Tanzania imefaidika na msaada wa WHO ambao umeiwezesha nchi kujenga uwezo wa utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo iwapo utaingia nchini.

Waziri Ummy amesema kumekua na uboreshaji wa mpango mkakati wa Ebola uliofanyika Mwezi Machi Mwaka 2019 ambao umelenga kuimarisha ufuatiliaji wa mgonjwa maeneo ya mipakani, kujenga uwezo wa watumishi wa afya kumtambua mgonjwa na kutoa matibabu, kununua vifaa vya kujikinga (PPE) na uratibu huu wa kukabiliana na Ebola umeshirikisha sekta mbalimbali zaidi ya Afya.

Pamoja na hayo, Waziri Ummy ametaja maeneo ambayo WHO isaidie ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza mpango mkakati wa kukabiliana na Ebola, kuimarisha ufuatiliaji katika ngazi ya jamii na kufanya mazoezi zaidi ya kupima utayari wa nchi.

Pia Waziri Ummy alitaka kujua chanjo ya ugonjwa Ebola inachukua muda gani kuanza kufanya kazi baada ya mtu kuchanjwa ambapo majibu yalitolewa kuwa chanjo hiyo inaanza kufanya kazi baada ya siku kumi huku muda wake wa kumkinga mtu ukiwa bado katika utafiti.

Vile vile Waziri Ummy alitaka kupata ufafanuzi kuwa chanjo hiyo ni kwa ajili ya aina gani ya virusi vya Ebola na ufafanuzi ulitolewa kuwa chanjo hiyo ni kwa ajili ya kirusi cha Zaire ambacho kwa sasa ndicho kinachosababisha mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

TBA Yadai Zaidi Ya Tsh.bilioni 1.5 Kwa Wapangaji Wake Dodoma

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) imewatolea uvivu wapangaji wake ambao wamekuwa sugu kwa kutolipa kodi ya pango kwa wakati hali iliyosababisha kuwatolea vitu vyao nje kutokana na kudai zaidi ya bil 1.5 huku wabunge wakitajwa kuhusika.
 
Pia wastaafu nao wametakiwa kuhama katika nyumba hizo kwani TBA wanaamini kuwa mtu akishastaafu anauwezo wa kuwa na nyumba yake mwenyewe.
 
Akizungumza  na waandishi wa habari Agosti 20,2019 jijini Dodoma  Kaimu Meneja Wakala wa Majengo Mkoa wa Dodoma Helman Tanguye  baada ya kufanya zoezi hilo alisema kuwa wadaiwa hao wamelimbikiza madeni yao kwa miaka 10 sasa.
 
Alisema kuwa TBA imekuwa ikidai fedha nyingi sana na hasa katika mkoa wa Dodoma kwa wafanyakazi wa serikali na taasisi mbalimbali za serikali ambazo wamezipangisha.
 
“Mpaka sasa tunadai zaidi ya bil 1.5 hivyo lengo kuu la TBA ni kuwaondoa wale watu walioshindwa kulipa kodi ya pango kwa wakati ili watu wanaohamia kutoka mikoa ya Dar es salaam na mingineyo nao waweza kupata nafasi”alisema Tanguye.
 
Akizungumzia zoezi zima walivyolianza alisema kuwa “tumelianza jana baada ya kufanya taratibu zote za kisheria na mikataba inavyosema kwahiyo tuliwapa notes ya siku 30 badaye tukaongeza Siku 14 lakini zilivyokwisha tulichukua vyombo ambavyo vinatambulika na mahakama ili tuweze kuwaondoa.
 
Alisema kampuni wanayoitumia katika zoezi zima la kuwatolea watu vitu vyao nje ni Yono Auction Mart ambayo wamekuwa wakiitumia mara kwa mara katika shughuli zao.
 
Wakati huo huo Tanguye alisema kuwa TBA ukiacha kazi yake yakujenga nyumba lakini pia inamiliki nyumba ambazo imewapangisha wananchi,taasisi,makampuni ,na wabunge lakini chakushangaza watu hao wamekuwa wakikaidi kulipa hata baada ya kupewa notes ya mwezi mmoja"
 
“Zoezi hili hapo awali lilifanyika jijini Dar es salaam  lakini kwa sasa limehamia jijini Dodoma ambapo litakuwa endelevu kwa mikoa yote nchini”alisema.
 
Pia wapangaji amabao hawajahuisha mikataba yao ya mwaka basi nao wanahusika kuondolewa kwani wanaonyesha kyuwa hawana nia ya kuishi katika nyumba hizo.
 
Kwa upande wake Kaimu Meneja Afisa miliki fredy mangala alisema kuwa mnamo juni 30 waliwasisitizia kuwa wametoa notes hivyo wanaodaiwa waende wakalipe lakini baada ya kuona wamekaidi agizo hilo wakaona bora kuchukua hatua hizo za kuwatolea vitu vyao nje.
 
“Wale wote wanaodaiwa na waliopata notes walipe madeni hayo kama inavyotakiwa hivyo zoezi hilo litakuwa endelevu kwani sheria inakataza kwa mtumishi wa umma kuwa na madeni.
 
Alisema kuwa fedha zaidi ya bil.1.5 ni nyingi sana kwani wangeweza kuzitumia ongeza nyumba nyingine eneo la Nzuguni ambapo wana eneo la hekali 630.
 
Mangala alisema kuwa wabunge nimiongoni mwa watu wanao daiwa hivyo wanachotakiwa ni kutekeleza majukumu yao kama mikataba inavyosema nakusema kuwa wao kama wakala wataendelea kutekeleza wajibu wao.
 
“Lakini endapo pia kuna mbunge atafikia kiwango cha kutolewa basi itabidi atolewa ingawa kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakijitokeza na kutuonesha ushirikiano”alisema.
 
Hata hivyo Malanga alisema kuwa mikataba hiyo inaelezea mtumishi akistaafu,akifariki au kuhamishwa mkoa mwingine inabidi kuachia nyumba ,hivyo katika zoezi hilo wanalolifanya pia wanaangalia watu hao.

Kilo za tumbaku milioni 2 na laki nne zilizolimwa nje ya mkataba kununuliwa haraka kabla ya kuanza kwa msimu wa kilimo.

$
0
0
NA SALVATORY NTANDU
Serikali imewahakikishia soko wakulima wa Wakulima wa zao la tumbaku  katika halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambao walizalisha kilo milioni 2 na laki nne nje ya mkataba ambazo mpaka sasa zilikuwa hazijanunuliwa.

Hayo yamebainisha  jana na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar balozi Seif Ali Idd, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi kangeme kata ya Ulowa ambao unalenga kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Amesema serikali kupitia wizara ya kilimo imeshatoa kibali kwa kampuni ya British American (BAT)kwaajili ya kununua tumbaku hiyo huku kampuni ya Alliance one nayo ikiwa tayari sokoni kwaajili ya kuanza ununuzi.

Amefafanua kuwa serikali ya awamu ya tano itaendelea kutatua kero za wananchi hususani wakulima watumbaku ambao hawajauza zao hilo ili kuwawezesha kujiandaa na msimu wa kilimo wa mwaka 2019.

Awali akimkaribisha Balozi Seif Ali Idd  mwenyekiti wa Chama cha mapindizi (CCM) mkoa wa shinyanga Mabala Mlolwa amesema kununuliwa kwa tumbaku hiyo kutaongeza mapato ya Halmashauri ya Ushetu ambayo inategemea kwa asilimia 80 kama mapato ya ndani.

Naye mkuu wa mkoa wa shinyanga Zainab Telack amesema atahakikisha wakulima wa tumbaku katika mkoa wake wanalima zao hilo kwa kuzingatia sheria za kilimo hicho ili kuleta tija kwao na kutunza mazingira.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika kahama KAKU Emanuel Charahani amesema kilo kilo milioni 7.9 za tumbaku zimeshanunuliwa na kampuni zinazonunua zao hilo kwa mwaka huu na aipongeza serikali kwa kutafuta mnunuzi wa tumbaku hiyo ambayo ili kuwawezesha kujiandaa na msimu mpya.

Asilimia 90 ya wakazi wa halmashauri ya ushetu ni wakulima wa tumbaku ambapo kutokana  bei ya tumbaku kuwa juu imesababisha hao kulima tumbaku hiyo kwa wingi na kwenda kinyume na mkataba na makampuni ya ununuzi wa zao hilo.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza

$
0
0
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawashikilia Watu Kumi Na Tatu (13) Kwa Tuhuma Za Kujihusisha Na Makosa Mbalimbali Ya Kiuhalifu Yaliyotendeka Katika Maeneo Mbalimbali Mkoani Mwanza.

Tukio La Kwanza
Kwamba Tarehe 20.08.19 10:00 Hrs Mtu Mmoja Aitwaye Samwel John @ Mtumwa, Miaka 26, Msukuma, Mkazi Wa Kijiji Cha Migombani - Luhama Wilayani Sengerema Aliuawa Kwa Kushambuliwa Sehemu Mbalimbali Za Mwili Wake Kwa Kutumia Fimbo Na Mawe Na Kundi La Wahalifu (Wananchi) Waliojichukulia Sheria Mkononi Wakati Alipokua Amehifadhiwa Katika Ofisi Ya Mwenyekiti Wa Serikali Ya Kijiji Cha Bulyahiru Akisubiri Kupelekwa Kituo Cha Polisi Baada Ya Kukamatwa Kwa Tuhuma Za Wizi Wa Mkungu Mmoja Wa Ndizi.

Hatua Hiyo Ya Mauaji Ilitokea Baada  Ya Mwenyekiti Wa Kijiji Hicho Kujaribu Kuwazuia Watu Hao Ambao Walianza Pia Kumshambulia Alipowasiliana Na   Polisi  Ili Wafike Kumchukua Na Polisi Walipofika  Walianza Kushambuliwa Na Hivyo Kulazimika Kumuoka Mwenyekiti Huyo Baada Ya Mtuhumiwa Kuwa Ameuawa.

Katika Kumuokoa Mwenyekiti  Huyo  Askari No D 9777 Sgt Juma Alijeruhiwa Kwa Jiwe Kichwani, Na Mwenyekiti Benjamini Kahitira Aliumia Kwenye Paji La Uso Na Watu Wawili Ambao Ni Dorica Majingo Alijeruhiwa Kwa Risasi Kwenye Paja La Mguu Wa Kulia Na Musa Mange Alijeruhiwa Kwenye Goti La Kushoto Kwa Risasi Baada Ya Kuwa Wanawashambulia Askari Polisi Kwa Mawe.  Majeruhi Walipelekwa Hospitali Ya Wilaya Sengerema Kwa Matibabu Na Hali Zao Zinaendelea Vizuri.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawashikilia Watu 11 Kuhusiana Na Tukio Hilo, Aidha Kazi Ya Kuwatafuta Watu Wengine Ambao Wamehusika Kwa Namna Moja Au Nyingine Bado Inaendelea.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linatoa Onyo Kwa Wananchi Wenye Tabia Ya Kujichukulia Sheria Mkononi  Waache Tabia Hiyo Kwani Ni Kosa La Jinai. Aidha,  Kwa Yeyote Atakayebainika Kujichukulia Sheria Mkononi Hatua Stahiki Za Kisheria Zitachukuliwa Dhidi Yake.

Tukio La Pili
Mtu Mmoja Aliyefahamika Kwa Jina Lafredrick S/o Chengula, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mngoni, Mkazi Wa Mbezi – Dar Es Salaam Anashikiliwa Na Jeshi La Polisi Kwa Tuhuma Za Kujipatia Fedha Kwa Njia Ya Udanganyifu (Utapeli) Kutoka Kwa Mfanyabiashara/muwekezaji   Wa Madini Aitwaye Mohamed Munnoo, Miaka 35, Raia Wa Mauritius Ambaye, Walimtapeli Dolla Elfu Sitini (Us$ 60,000) Sawa Na Tshs 138,000,000/=, Fedha Za Kitanzania, Kitendo Ambacho Ni Kosa La Jinai.

Tukio Hilo Lilitokea Tarehe 19.04.109, Baada Ya Mfanyabiashara Huyo Wa Madini Raia Wa Mauritius  Kukutana Na  Watu Hao  (Matapeli )  Waliojifanya Ni M,aafisa Wa Serikali Na Kumpeleka Kwenye Ofisi Mbalimbali Za Kuuza Madini Ya Dhahabu. Aidha Baada Ya Kupewa Taarifa Hizo Raia Huyo Wa Mauritius  Alielekezwa Kuweka Pesa  Kwenye Account Ya Mmoja Wao Katika  Equity Benki Tawi La Mwanza  Yenye Namba 3007211416820 Famm Amtl Co.ltd, Ili Aweze Kupatiwa Madini Ya Dhahabu Yenye Uzito Wa Kilogramu 7.

Hata Hivyo Baada Ya Matapeli Hao Kuingiziwa Kiasi Hicho Cha Fedha Walitoroka, Ufuatiliaji Uliwezesha Kuwakamata Watuhumiwa Wawili. Na Baadae Kiongozi Wao Nae Amekamatwa Akitokea Nchi Jirani.

Imetolewa Na:-
Muliro J. Muliro-acp
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza
21 Agosti 2019.

CCM,CHADEMA Njombe wazidi kutunishiana misuri

$
0
0
Na Amiri kilagalila-Njombe
Wakati vyama vya siasa vikiendelea kujiimarisha kabla ya kuanza uchaguzi wa serikali za mitaa mapema Novemba mwaka huu,Chama cha mapinduzi CCM pamoja na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Njombe vimeendelea kujitokeza na kutambiana hakuna atakayemshinda mwenzie katika chaguzi hizo hususani katika mitaa iliyopo Njombe mjini inayoongozwa na CHADEMA.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa Chadema mkoa wa Njombe Alatanga nyagawa amesema wanaamini wataendelea kushinda katika maeneo ya mijini ambako bado wanaongoza hadi sasa licha ya kuwapo kwa figisu kubwa za chama cha mapinduzi zinazofanyika katika kipindi cha uchaguzi.

 “Hapa mjini mshindani wetu sio CCM labda kizaliwe chama kingine,sisi tuna mtaji mkubwa hapa kwa asilimia kubwa wenzetu wameshachoka labda waende sehemu nyingine,sahizi tunachohangaika ni nani asimame kwa mazingira ya sasa kwasababu ushindani mkubwa upo ndani ya chama”alisema Nyagawa

Wakati chadema wakijinasibu kuendeleza ushindi katika maeneo yote ya mijini chama cha mapinduzi nacho kupitia katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto ngole anasema hakuna mtaa utakaokaliwa na upinzani katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.

“Tatizo Chadema ni chama cha fitina,na safari hii atakayefanya mzaha tunafukuza mchana kweupe na kushinda tutashinda CCM ya Magufuli ni ya tofauti”alisema Erasto Ngole

Diwani wa kata ya Njombe mjini kupitia Chadema Agrey Mtambo amesema ana imani vyama vyote vimejipanga kikamilifu na kutoa wagombea watakaowakilisha vyema vyama vyao huku akiwataka wananchi kujitokeza pindi uchaguzi utakapoanza ili waweze kuchagua viongozi watakao kuwa bora katika maeneo yao

Novemba 24 mwaka huu ni tarehe inayotajwa kuwa ya uchaguzi wa serikali za mitaa kuwachagua wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji ambapo watanzania wanahimizwa kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mpiga kura ili wapate fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka.

Daktari Bingwa Muhimbili aeleza sababu vifo vya majeruhi ajali ya moto kuongezeka

$
0
0
Daktari bingwa wa upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Laurian Rwanyuma amesema majeruhi wa ajali ya lori la mafuta iliyotokea eneo la Msamvu mkoani Morogoro wanaendelea kupoteza maisha kutoka na kuungua kwa asilimia 80 hadi 90.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Agosti 21, Dk. Rwanyuma amesema majeruhi wengi waliopelekwa hospitalini hapo, waliungua zaidi sehemu za ndani kama vile mfumo wa hewa na figo hivyo kusababisha kupumua kwa shida.

“Kutokana na ngozi zao kuungua kwa asilimia kubwa hali hiyo imesababisha mwili kukosa kinga na kupoteza maji mengi.

“Kwa kawaida wagonjwa walioungua kiasi hicho wana uwezekano mdogo wa kupona hata kama hospitali ina uwezo mkubwa wa vifaa na madawa,” amesema.

Hata hivyo, amesema wanaendelea kufanya juhudi za hali ya juu ili majeruhi waliobaki waweze kupona.

Hadi sasa watu 100 katika ajali hiyo ilitokea Agosti 10 mwaka huu katika eneo la Msamvu mjini Morogoro baada ya lori la mafuta kupinduka na kulipuka na kusababisha, wamefariki dunia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi August 22

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina AIVUNJA Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Maziwa Tanzani

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, ametangaza kuivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Maziwa Tanzania, kuanzia leo August 22, 2019 kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa kazi zao.

Kenya yashinda kura ya Afrika kutafuta kuwa mjumbe asiye wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

$
0
0
Kenya imeishinda Djibouti na kupata kura ya Umoja wa Afrika ambayo inatarajiwa kuongeza chachu ya kampeni ya nchi hiyo kuwa mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imesema, Kenya imepata kura 37 dhidi ya 13 za Djibouti wakati wa uchaguzi ulioandaliwa na Kamati ya Kudumu ya Wawakilishi ya Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Kenya inatarajiwa kuungana na Niger na Tunisia ambazo zilichaguliwa mwezi June kuwa wajumbe wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameupongeza Umoja wa Afrika kwa kuidhinisha nia ya Kenya ya kuwa na nafasi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuzitaka nchi nyingine wanachama wa Umoja huo kuunga mkono kenya kupata nafasi hiyo.

Korea Kaskazini yapuuza mazungumzo ya nyuklia na Marekani

$
0
0
Korea Kaskazini imesema haioni manufaa ya majadiliano hadi Marekani isitishe kile ilichokiita hatua za uhasama za kijeshi, wakati mjumbe wa Marekani akizuru Korea Kusini kwa jicho la kufufua mazungumzo ya nyuklia na Pyongyang. 

Mazungumzo kati ya Pyongyang na Washington yamekwama, tangu mkutano wa pili wa kilele kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mjini Hanoi Februari, ulipovunjika bila makubaliano. 

Wawili hao walikutana tena mwezi Juni katika ukanda wa amani kati ya Korea mbili na kukubaliana kuanzisha tena majadliano ya ngazi ya kikazi, lakini mazungumzo hayo bado kuanza. 

Wakati huohuo, Korea Kaskazini imefanya majaribio kadhaa ya makombora ya masafa mafupi katika wiki za karibuni, kupinga mazoezi ya  kijeshi ya kila mwaka kati ya Marekani na Korea Kusini, ambazo inaziona kama mazoezi ya kujiandaa na uvamizi. 

Stephen Biegum, mjumbe maalumu wa Marekani kwa ajili ya Korea Kaskazini, anaeongoza mazunguzo ya kikazi, aliwasili Seoul Jumanne jioni kwa ziara ya siku tatu, na alisema Washington itakuwa tayari kushiriki mazungumzo mara itakaposikia kutoka Pyongyang.

Waziri Jafo Atoa Maagizo Kwa Wakuu Wa Mikoa Na Makatibu Tawala Mikoa Kote Nchini Kusimamia Vyema Mpango Kazi Wa Taifa wa Uendelezaji Miji Tanzania.

$
0
0
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Seleman Jafo ametoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa,na Makatibu tawala wa Mikoa kote nchini kuhakikisha wanasimamia vyema mpango kazi wa Taifa wa uendelezaji wa Miji ili kuepuka ukuaji wa Makazi Holela.
 
Waziri Jafo ametoa Maagizo hayo jijini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Mpango kazi wa wa Taifa wa  Maendeleo ya Miji Tanzania .
 
Waziri Jafo amesema suala la mpango kazi wa Maendeleo ya Miji Tanzania itakuwa ajenda ya Kitalii na itakuwa na faida kubwa ikiwa ni pamoja na urahisi wa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na kupitikika kwa maeneo kwani amesema kuna baadhi ya Mitaa haipitikiki kutokana na Makazi holela  hali ambayo husababisha hata magari ya zimamoto kushindwa kutoa huduma vizuri.
 
“Unakuta nyumba zimekaa kiholela hata gari la zimamoto linashindwa kutoa huduma vizuri na hali ambayo inasababisha kuteketea kwa watu pamoja na mali,maeneo mengine ni ya kusikitisha sana hata kupitisha jeneza ni shida ,Bila shaka kuna Vijana wengine hapa wana Magari Mazuri lakini wanayaengesha nyumba ya ng’ambo kwa jirani  kisa hapapitiki”Alisema 
 
Hivyo Waziri Jafo amesema katika kuhakikisha mpango kazi wa Maendeleo ya Miji Tanzania unafanyika bila vikwazo vyovyote ameagiza Wakuu wa Mikoa na Makatibu tawala wa Mikoa kote nchini kusimamia vyema ili kuleta ufanisi Mzuri katika utekelezaji wake.
 
Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema  moja ya hatua ambayo Wizara imefanya ni pamoja na kupitia Sera ya Makazi  ya Taifa ya mwaka 2000 na kupanga  sera Mpya ya Nyumba lengo likiwa ni kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi pamoja na Kuboresha huduma za kijamii.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi [ESRF]Dkt.Tausi Kida amesema Mnamo Agosti ,2017 Serikali ya Tanzania iliungana na Taasisi hiyo kuanzisha Maabara ya ukuaji wa Miji Tanzania kwa lengo la kusaidia serikali katika uchambuzi mbalimbali wa ukuaji miji huku Naibu katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Adolf Ndunguru akishukuru ushiriki wa Taasisi hizo.

video: Harmonize Kaandika Barua ya Kuomba Kuvunja Mkataba na Kundi la Diamond la WCB

$
0
0
Meneja wa kundi la Wasafi,  Sallam amesema msanii Harmonize  kwa sasa ndani ya moyo wake hayuko WCB, isipokuwa tu yupo kimakaratasi na tayari ameshaandika barua ya komba  kuvunja mkataba na kundi hilo.

Akizungumza na Wasafi TV, Sallam amesema hata katika tamasha la Wasafi lililofanyika mjini Mwanza, Harmonize alitumia usafiri binafs na  kufanya baadhi ya mambo yaliyotoa tafsiri kuwa ameshajitenga na WCB.

“Hili jambo si sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi Festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuambatana na wasanii wenzake ambao wapo pamoja katika tamasha ni kwenda kinyume.

“Sisi katika tamasha letu hatupendi kutengeneza matabaka, tumeamua kuwa kitu kimoja, siyo kwamba Diamond, Rayvany hawakuwa na uwezo wa kutumia usafiri wao binafsi kama alivyofanya Harmonize” amesema Sallam na kuongeza;
 
“Harmonize ameshatuma barua ya maombi Wasafi kuvunja mkataba wake na yupo tayari kufuata sheria zote.

“Sisi tumependezwa na hatua yake kwa sababu labda kuna vitu ameona akivifanya atafika mbali.

==>>Msikilize Hapo Chini

Yoweri Museveni na Paul Kagame wasaini makubaliano kumaliza mgogoro baina yao

$
0
0
Marais  Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wamesaini makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda, kumaliza uhasama uliopo kati ya mataifa hayo jirani.

Walifikia makubaliano hayo katika mkutano huo wa pili mbele ya marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Angola na  Congo Brazzaville waliokuwa wapatanishi katika mgogoro huo.

Joto la kisiasa limekuwepo tangu mwanzoni mwa mwaka huu na limeathiri maisha ya watu kijamii na kiuchumi katika mataifa hayo jirani.

Maofisa nchini Rwanda wameishutumu Uganda kwa kuwafunga na kuwatesa kinyume cha sheria raia wake nchini Uganda, wakati Uganda nayo inaishutumu Rwanda kutekeleza ujasusi katika ardhi yake.

Taarifa ya TCU Kuhusu Waombaji Vyuo Vikuu 2019/2020 Waliochaguli Zaidi ya Chuo Kimoja

Ndikilo: Tanzania Ni Salama Kwa Uwekezaji,hususani Mkoani Pwani

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ,amesisitiza kwamba ,Tanzania hususan mkoani Pwani ni salama kwa uwekezaji na amekemea propaganda na uvumi unaoenezwa na baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa kuwa hakuna uwekezaji unaoendelezwa.

Aidha amewaasa ,wawekezaji na wenye viwanda kuhakikisha wanasajili namba za utambulisho ya mlipa kodi (TIN no) kwa meneja wa mamlaka ya mapato (TRA )mkoani hapo ili hali kuongeza pato la mkoa.

Ndikilo alitoa rai hiyo, wakati alipokwenda kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitano vilivyopo wilayani Mkuranga.

“Rais dkt.John Magufuli amekuwa akisisitiza uwekezaji na ujenzi wa viwanda kuelekea uchumi wa kati, sasa akitokea mtu kukwamisha jitihada hizo anakuwa halitakii mema Taifa, Pia mkoa wetu kupitia halmashauri umetenga maeneo hekta 22,937 kwa ajili ya uwekezaji ,nawaomba wawekezaji waje kuwekeza .”alifafanua Ndikilo.

Hata hivyo, mkuu huyo wa mkoa aliwataka wenye viwanda kujali mikataba,haki,maslahi ya wafanyakazi kwa kuzingatia sheria pamoja na kuwapa likizo na kuwawekea vitendea kazi .
Awali mkurugenzi wa kiwanda kinachozalisha matofali yenye ubora (Shaffa Ltd) kitongoji cha Kiguza, Suleiman Amour alibainisha ,ujenzi wa kiwanda umeanza 2018 kinatarajia kitakamilika mwaka 2019.

Amour alisema, lengo la mradi huo ni kuongeza wigo katika sekta ya ujenzi ,na ujenzi utagharimu sh.bilioni 15.3 hadi kukamilika ambapo itatoa ajira 200 mradi ukikamilika.

Kwa upande wake, msimamizi usafirishaji wa kiwanda cha super meals (Cool Blue) kilichopo Vianzi, Charles Malini alisema, ujenzi wa kiwanda umegharimu bilioni 2.7, kuna ajira 50 ,kinalisha maji ya kunywa ya chupa kwa matumizi ya majumbani na ofisini ambapo wanazalisha ujazo mbalimbali kuanzia nusu lita hadi lita 18.

Alitaja changamoto zinazowakabili ni kukosa umeme wa uhakika na miundombinu ya barabara isiyo rafiki .

Ndikilo alizungumzia tatizo la barabara na kuwaeleza ,ataangalia namna ya kuingiza hoja hiyo katika kikao cha barabara kijacho ili kiweze kutetea ipandishwe hadhi ihudumiwe na Tanroads.

Meneja wa shirika la umeme-TANESCO wilayani Mkuranga, Octavian Mmuni alisema tatizo la kukosekana umeme wa uhakika hutokana na maboresho yanayofanyika mara kwa mara.

Mmuni alieleza, kwa sasa shirika hilo limetenga sh.milioni 261 ili kusaidia kubadili nguzo na nyaya chakavu.

Viwanda vingine vilivyowekwa mawe ya msingi  katika wilaya hiyo ,ni kiwanda kinachozalisha zana za uvuvi Taxtrade T2 Ltd ,cha nyaya za umeme -Plug Ltd na kiwanda cha kutengeneza masufulia cha Maxima.

Serikali Kutumia Wataalam wa Ndani Kutekeleza Miradi ya Maji

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Serikali imedhamiria kutumia zaidi wataalam wake wa ndani katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa kazi walizopewa.

Amesema maamuzi hayo yamekuja baada ya wataalam hao kufanya kazi nzuri, zinazochukua muda mfupi kukamilika, zenye viwango na kwa gharama nafuu ukilinganisha na wakandarasi ambao kazi zao zimekuwa na changamoto mbalimbali zinazokwamisha juhudi za Serikali kumaliza tatizo la maji.

Naibu Waziri Aweso amesema kwa muda mrefu Serikali imekuwa na changamoto kubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini kutokana na ubabaishaji wa wakandarasi licha ya kutumia fedha nyingi kwa dhumuni la kufikisha huduma ya maji kwa kila mwananchi.

‘‘Tumekuwa na utaratibu wa kuwapa kazi Wataalam Washauri ya usimamizi wa ujenzi wa miradi kwa gharama kubwa, lakini wamekuwa wakishirikiana na wakandarasi kuihujumu Serikali kwa kutotimiza wajibu wao na kuingizia Serikali hasara kubwa’’, Naibu Waziri Aweso amefafanua.

‘‘Baada ya kugundua tatizo hilo tukaamua kutumia wataalam wa ndani waliopo kwenye mamlaka za maji, wahandisi wa mikoa na wilaya kwenye miradi mingi iliyokuwa imekwama au ujenzi wa miradi mipya kwa gharama ndogo na kupata mafanikio makubwa, Aweso ameeleza.

Akieleza kuwa baadhi miradi mingi iliyosimamiwa au kutekelezwa na wataalam wa ndani katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya na Kanda ya Ziwa imekuwa na mafanikio makubwa, jambo ambalo limeifanya Serikali kudhamiria kutumia zaidi wataalam hao na kuachana na wakandarasi wababaishaji kwa lengo la kupata matokeo mazuri.

Awali, Naibu Waziri Aweso alichukua hatua ya kumkamata Mkandarasi wa Kampuni ya Mbeso Construction Ltd kwa sababu ya kusuasua kwa ujenzi wa miradi ya maji ya Munge na Tella Mande iiliyopo katika Wilaya za Siha na Moshi, mkoani Kilimanjaro bila sababu za msingi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Aweso kukagua Mradi wa Maji wa Munge, wilayani Siha na kutoridhiswa na kasi ya mkandarasi na muda wa utekelezaji wake ukiwa umebaki mwezi mmoja na kazi ikiwa ni asilimia 25 hali akiwa hana madai yoyote ya fedha kwa Serikali.

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

$
0
0
Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa, Dalili zake Hizi Hapa..Makala
51 minutes ago

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.


Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.


Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.


Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.


Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Mpate mpenzi wako unayempenda na kumfunga mume,mke mpenzi asitoke kwa mwingine .

Kwa Ushauri na Msaada wa Wasaliana na  0714006521
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images